Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Februari 24, 2014

Je una mpango au tayari una mahusiano na mkubwa wako wa kazi (bosi)?



Nini kinafuata? 

Ukweli ni kuwa, mahusiano katika eneo la kazi si jambo geni. Mahusiano yanaathiri (zaidi kwa wasichana, na hasa warembo), walioelimika na wasioelimika, matajiri kwa maskini, kwenye makampuni madogo na makubwa sehemu zote. Kama umeingia au una mpango wa kuingia katika mahusiano hayo, fahamu kuwa unayafanya maisha yako ya kazini kuwa magumu na tata. 

Ni kweli pia kuwa si mara zote watu hutoka na kudhamiria kuwa na mahusiano kazini ila hujikuta tayari wamo.

Kabla hujaanza mahusiano na bosi wako, au katika hali yoyote ambayo umejikuta tayari una mahusiano hayo, tafiti na jiulize haya yafuatayo:-

1. Je, Kampuni unayofanya kazi ina sheria inayohusu mahusiano kazini? Kama ni ndiyo, jua kuwa unajiwekea mazingira magumu na kuhatarisha kazi yako. Hata kama mtu unayeingia naye kwenye mahusiano ni bosi wako, wewe ndiye utakayeondoka . Mtu mwenye cheo mara zote anabaki kwenye kampuni, kampuni haiwezi kuingia gharama ya kumpoteza bosi kwaajili ya mahusiano yako, ila wewe itabidi uondolewe kwakuwa gharama ya kumpata bosi ni kubwa kuliko kupata mtu kama wewe.

2. Je, Uliajiriwa kwa ujuzi wako na si vinginevyo, baada ya kuanza mahusiano mambo yanaanza kuwa tata kikazi. Bosi wako ni bosi wako tu, yeye ndiye anayeamua nani apandishwe cheo, kupata nyongeza za mishahara na mengine mengi. Hivyo mambo yataanza moto moto ila siku za usomi huanza kufifia na kinachobakia ni kutojisikia vizuri unapokuwa kazini. Hivyo uwe makini na maamuzi unayoyafanya hasa kuhusu mahusiano kazini.
3. Jua kuwa mahusiano hayo yatafika mwisho. Je, utajisikiaje kwenda ofisini ukiwa umeshaachana na bosi? Utendaji na ufanisi wa kazi utakuwaje? Hakuna ubishi kuwa utakuwa na maumivu makubwa, ingawaje wengi hujifanya hawajaumia.

Kama Bosi wako ameoa au kuolewa

1. Fahamu kuwa ni 10% tu ya mahusiano kazini ndiyo humea kwa muda mrefu; Mengi huvunjika.
2. Je, haya ni mahusiano yako ya kwanza? Fahamu kuwa watu wana vitu vingi vinavyoendelea kwenye maisha yao, tabia, hulka na mahusiano huwa tofauti. Kuwa makini kujua mtu anapitia nyakati gani.
Kama unaamua kuingia kwenye mahusiano

1. Kuwa makini, na tumia akili nyingi kutambua unamwambia nani hapo kazini. Hii inaweza kuhatarisha kazi na vyeo vyako unavyostahili kupandishwa kihalali uwapo kazini.
2. Kama umeoa au kuolewa, jua kuwa wewe ni mdanganyifu kwenye ndoa yako. Kuwa na mahusiano nje ya ndoa si suluhisho ya tatizo, bali kuwa jasiri kwa kujadili na mwenzi wako kutafuta njia ya kutatua kile kinachopungua kwenye ndoa yenu. Hiyo ndiyo namna ya kuonyesha upendo kwa mtu uliyeamua kuishi naye kwenye ndoa.
3. Tafuta ushauri kwa washauri wa masuala ya ndoa na mahusiano. 
Fikiria kwa makini na tafakari kabla maji hayajamwagika ukajutia. Bado unao uamuzi!

MKUTANO MUHIMU KWA WACHORA KATUNI KUHUSU MAPENDEKEZO YA WASANII KATIKA RASIMU YA KATIBA MPYA.











 


Ewe mchoraji katuni, mkongwe na chipukizi, tarehe 25.02.2014, Jumanne, saa 9.30 alasiri, Vijana Social Hall, Kinondoni, DSM, kutakuwa na mkutano wa kujadili mapendekezo ya wasanii kwenye Rasimu ya Katiba.

Taarifa ya hatua iliyofikiwa itawasilishwa na Mdau John Kitime. Usikose.

Sambaza ujumbe huu kwa wengine. 
Kwa taarifa zaidi 0713 262 902 (Nathan Mpangala)

Taarifa ya Wizara kuhusu ziara ya Waziri Membe nchini China



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atafanya ziara ya kikazi ya siku tano katika Jamhuri ya Watu wa China kuanzia tarehe 24 hadi 28 Februari, 2014. Ziara ya Mhe. Membe inakuja kufuatia mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi. 

Mhe. Membe anafanya ziara hiyo nchini China kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kirafiki uliopo kati ya Tanzania na China. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Membe atafuatana na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Ziara hii pia ni muendelezo wa maeneo ya utekelezaji baada ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping aliyoifanya hapa nchini tarehe 24 na 25 Machi, 2013 na baadaye ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda nchini China mwezi Oktoba, 2013.

Akiwa nchini China, Mhe. Membe atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mhe. Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China tarehe 25 Februari 2014. Siku hiyo hiyo Mhe. Membe atamtembelea Makamu wa Rais wa China, Mhe. Li Yuanchao kwa lengo la kumsalimia na baadaye atafanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Gao Hucheng.

Aidha, tarehe 26 Februari, 2014 Mhe. Membe atatembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Poly Technologies yaliyopo katika mji wa Shenzhen na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo kabla ya kutembelea Makao Makuu ya Kampuni ya China Merchant Holdings International ambako atapokea taarifa ya maandalizi ya kuanza kwa mradi wa Ujenzi wa Bandari katika eneo la Mbegani huko Bagamoyo.

Mhe. Membe pia atapata fursa ya kutembelea Kampuni ya HUAWEI ili kujionea shughuli mbalimbali. Kampuni ya HUAWEI ina Mkataba na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya hapa nchini kuhusu Elimu kwa Njia ya Mtandao (e-Education) kwa Shule za Sekondari.

Vile vile tarehe 27 Februari, 2014, Mhe. Membe atautembelea Mji maarufu wa biashara wa Guangzhou na kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi mjini hapo. Mhe. Membe atatoa taarifa kuhusu hali ya uchumi, siasa na masuala ya jamii yalivyo hapa nchini kwa sasa pamoja na kutoa taarifa ya maendeleo ya Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
Waziri Membe pia atatembelea Eneo la Viwanda la Huadu tarehe 28 Februari, 2014 kabla ya kurejea nchini tarehe 1 Machi, 2014.

IMETOLEWA NA: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM. 
24 FEBRUARI, 2014

Kwanini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?

Kipindi cha Familia...Bajeti katika familia

TUNGO ZETU. Matatizo katika mahusiano (Wanaume)

Kipindi cha familia kutoka Jamii Production...Kwanini wanandoa hutembea nje ya ndoa zao? (Pt II)

Kipindi cha familia kutoka Jamii Production...Kwanini wanandoa hutembea nje ya ndoa zao? (Pt I)

Majukumu ya Mama katika familia

Mahojiano na waTanzania Evans Mhando na Fatuma Matulanga wakiwa CHINA

Majukumu ya Baba katika familia

Ana kwa Ana na Astronaut Dr Donald Thomas

Mjadala kuhusu MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA kwa nchi yake

KWANINI WANANDOA HUTEMBEA NJE YA NDOA?

Karibu katika sehemu ya pili ya kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
 Katika kipindi hiki, tunaendeleza mjadala juu KWANINI WANANDOA HUTEMBEA NJE YA NDOA?  Wachangiaji studio walikuwa ni:
 

I

Mubelwa Bandio

Denzel Musumba

Elizabeth Cherehani
KARIBU UUNGANE NASI

Ijumaa, Februari 21, 2014

USEFUL SITE

Video>>
Youtube
Dailymotion
Hulu
Metacafe
Vimeo
Break.com
Movie>>
IMDb
Hulu Movie
MSN Movie
Yahoo! Movie
RottenTomatoes
Hollywood
Game>>
Yahoo! Game
IGN
Gamespot
Gamefaqs
Pogo
Zynga
Y8
News>>
Yahoo! News
CNN News
BBC News
Reddit
MSN News
Reuters News
TV>>
TV.com
Viki TV
Yahoo! TV
MSN TV
Hulu TV
IMDb TV
Sport>>
NBA
ESPN
Dailymail
MLB
Goal
Yahoo! Sport
Images>>
Flickr
imgur
Tinypic
Photobucket
Picasa
Twitpic
Music>>
SoundCloud
Beemp3
Grooveshark
MTV
Allmusic
Last.fm
Fun>>
Thebubble
9gag
Youtube Fun
Funny Videos
Yahoo! Fun
Comedy Central
Travel>>
Priceline
Expedia
Agoda
Booking
Travelocity
Tripadvisor
Social>>
Facebook
Twitter
Tumblr
Pinterest
Myspace
Badoo
Community>>
Craigslist
Digg
LiveJournal
deviantART
SoundCloud
Squidoo
Encyclopedia>>
Wikipedia
Wikia
Reference
About
Wikibooks
Wikiversity
Dictionary>>
Free Dictionary
Thesaurus
wordreference
Babylon
Wiktionary
Onelook
Blog>>
Blogspot
Blog Search
EzineArticles
Blogger
HubPages
Typepad
Technology>>
TechCrunch
Mashable
GSMArena
Engadget
W3C
W3schools
Storage>>
Mediafire
4shared
Filestube
Dropbox
Slideshare
Evernote
Download>>
CNET
Softonic
Torrentz
Brothersoft
Informer
Tucows
Money>>
Yahoo! Finance
DailyFinance
Dailymail Money
XE
CNN Money
eHow Money
Job>>
Linkedin
viadeo
eHow
indeed.com
Xing
Freelancer
Shopping>>
Amazon
Ebay
Nextag
Groupon
Bestbuy
Newegg
Health>>
Huffington Health
WHO
NIH
MSN Healthy Living
Menshealth
Foxnews Health
Food>>
Huffington Food
BBC Food
MSN Food
Foxnews Food
Guardian Food
eHow Food
Style>>
Huffington Fashion
MSN Style
Foxnews Style
Guardian Fashion
Reuters Style
eHow Style
Family>>
Huffington Family
MSN Family
Guardian Family
eHow Family
Washingtonpost Family
ikea

Jumatano, Februari 19, 2014

Fahamu nyenzo za usalama na faragha zinazotolewa kwako na Google


Ukiwa na Google, una zana mbalimbali zinazokusaidia kuwa salama na kuweka maelezo yako salama na faragha. Hapa kuna baadhi ya zana maarufu kabisa ambazo zinasaidia kufanya Google ikufanyie kazi nzuri zaidi.

Kuwa salama na faragha

Uthibitishaji wa hatua -2

Pindi tu unapounda nenosiri la Akaunti yako ya Google, tunakuhimiza uongeze safu ya ziada ya usalama kwa kuwezesha uthibitishaji wa hatua mbili. Uthibitishaji wa hatua mbili unakuhitaji kufikia simu yako, pamoja na jina lako la mtumiaji na nenosiri, unapoingia. Hii inamaanisha kuwa ikiwa mtu fulani ataiba au kudadisi nenosiri lako, mwingiaji kwenye akaunti bila idhini aliyepo bado hawezi kuingia kwenye akaunti yako kwa sababu hana simu yako. Sasa unaweza kujilinda kwa jambo ambalo unajua ( nenosiri lako) na jambo ulilo nalo (simu yako).

Hali fiche katika Chrome

Katika modi chini kwa chini, kurasa unazofungua na faili unazopakua hazirekodiwi katika historia ya kuvinjari au kupakua ya Chrome. Unaweza pia kutumia kipengele hiki katika Chrome ya Android – na Chrome ndio kivinjari chaguo-msingi kwa ajili ya bidhaa mpya za Android, kukuruhusu uvinjari mtandao kwenye simu yako au kompyuta ndogo kwa faragha. Fahamu jinsi ya kufikia modi chini kwa chini.

Google Talk

Google Talk, kipengele cha gumzo katika Gmail na bidhaa nyingine za Google, inakuruhusu kutokuhifadhi gumzo. Gumzo ambazo zimeondolewa kwenye rekodi hazihifadhiwi kwenye au historia ya gumzo za anwani ya Gmail. Unapoacha kupiga gumzo, ujumbe utaonekana kwako na katika anwani yako ukithibitisha kuwa gumzo zijazo hazitahifadhiwa, isipokuwa mmoja wenu abadilishe mipangilio.

Durara za Google+

Durara za Google+ hukusaidia kudhibiti marafiki zako na anwani. Kwa hivyo unaweza kuweka marafiki zako katika durara mmoja, familia yako katika nyingine na bosi katika durara akiwa peke yake - kama vile katika maisha halisi! Kisha unaweza kushiriki maudhui yanayolingana, kama vile chapisho za Google+, video za YouTube, au orodha za Eneo, na watu sahihi wakati wowote unapochagua.

Video za siri na zisizoorodheshwa kwenye YouTube

YouTube iliundwa ili watu washiriki mawazo na dunia nzima. Lakini wakati mwingine ungependelea kushiriki video na kundi dogo la marafiki au ujiwekee. Unaweza kufanya hivyo kwa kuchagua isiyoorodheshwa au ya faragha wakati unapakia video yako.

Angalia na udhibiti maelezo yako

Mipangilio ya Akaunti ya Google

Kwenye ukurasa wako wa mipangilio ya Akaunti, unaweza kuona huduma na maelezo yanayohusiana na Akaunti yako ya Google na ubadilishe mipangilio yako ya usalama na faragha.

Dashibodi ya Google

Dashibodi ya Google hukuonyesha kilichohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google. Kutoka kwa eneo moja la kati, unaweza kutazama na kusasisha kwa urahisi mipangilio yako ya huduma kama vile Blogger, Kalenda, Hati, Gmail, Google+ na zaidi.

Mimi kwenye Wavuti

Mimi katika Wavuti inaweza kukusaidia kuelewa na kudhibiti watu wanachokiona wanapokutafuta kwenye Google. Inakusaidia kuweka Tahadhari za Google ili uweze kufuatilia maelezo yanayokuhusu yakitokea mtandaoni, na inapendekeza otomatiki baadhi ya hoja za utafutaji unazoweza kutaka kufuatilia kwa umakini.

Shughuli ya Akaunti

Shughuli za Akaunti zinafanya iwe rahisi kwako kukagua jinsi unavyotumia huduma za Google wakati umeingia, na kuhakikisha ni wewe tu umekuwa ukiitumia akaunti yako. Ukifungua akaunti, utapata ufikiaji kwa ripoti ya kila mwezi penye utaona vitu kama idadi ya barua pepe zilizotumwa na kupokewa kutoka kwa akaunti yako, akaunti yako imefikiwa kutoka nchi zipi, na utafutaji wa Google unaoongoza kutoka akaunti yako.

Google Takeout

Google Takeout hukupa zana rahisi kutumia ya kupakua data yako binafsi, kama vile hati au picha, ili daima uweze kuwa na nakala au uweze kupakia maelezo yako kwa huduma nyingine.

Vidhibiti vya Historia ya Wavuti ya Google

Ikiwa umeingia kwenye Akaunti ya Google, Historia ya Wavuti inakusaidia kukupa matokeo na mapendekezo yanayohusiana zaidi. Ukichagua, unaweza kufuta maingizo, sitisha ukusanyaji au zima huduma hiyo kabisa. Unaweza kufanya vivyo hivyo na Historia ya YouTube.

Dhibiti wanachoona watangazaji na tovuti

Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo

Matangazo husaidia kulipia huduma nyingi za bila malipo mtandaoni ambazo unapenda na kutumia kila siku. Ukiwa na Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo ya Google, unaweza kuelewa jinsi matanagazo yanavyochaguliwa kwa ajili yako, dhibiti maelezo yanayotumika kuchagua matangazo, na zuia watangazaji maalum.

Chaguo la Kujiondoa kwenye Google Analytics

Google Analytics huzalisha takwimu kuhusu wageni katika tovuti, kama vile idadi ya maoni ya ukurasa au nyakati za kilele cha trafiki ili kusaidia wachapishaji wa tovuti kuboresha tovuti zao. Ikiwa hutaki data ya kivinjari chako ishirikiwe na wachapishaji unapotembelea wavuti zinazotumia Google Analytics, unaweza kusakinisha kuchagua kutoka.

Ijumaa, Februari 14, 2014

MPIGAJI MZURI WA PIANO


Eldar Nebolsin wa nchi ya Uzbekistani ni mpigaji wa piano mwenye kujulikana katika mataifa mengi. Alicheza piano katika vikundi vya wanamuziki huko Londres, Moscow, Saint Petersburg, New York, Paris, Roma, Sydney, Tokyo, na Vienna.

Eldar alikulia katika Muungano wa Kisovieti na hakuamini kwamba kuna Mungu. Lakini baadaye alikubali kwamba wanadamu waliumbwa na Muumbaji mwenye upendo.

KISA CHA AJABU...

Sikuzote nyumba yetu ilijaa vitabu ambavyo baba yangu alinunua katika mji wa Moscow. Kuna kitabu ambacho kilinivutia sana ni kitabu kilichokuwa na habari za Mungu. Biblia ilieleza kuhusu mwanzo wa mwanadamu na mambo ambayo yaliwapata Waisraeli.

Nilipohamia Hispania katika mwaka wa 1991 ili kujifunza muziki, nilibeba kitabu hicho na nikakisoma mara nyingi. Nilivumbua imani ambayo haitegemei tu namna mtu anavyojisikia moyoni lakini pia mambo yenye kupatana na akili na yenye nguvu ya kiroho.

Fundisho ambalo lilinivutia kabisa ni ahadi ya Biblia kwamba wanadamu wanaweza kuishi milele. Fundisho hilo lilikuwa lenye kueleweka bayana kabisa!

USHAURI WAKE...

Biblia ni kama muziki mzuri sana wa PIANO wenye mpangilio wa ajabu, na ina ujumbe wenye kuchochea kwa ajili ya wanadamu wote.

Jumatano, Februari 05, 2014

TANGAZO LA AJIRA




Wanatwafutwa ma-NURSE 10 wenye diploma na uzoefu wa kuanzia miaka 2 na kuendelea haijalishi umri, kabila wala dini. Awe na VYETI halisi pamoja na CV.

Awe tayari kufanya kazi mkoa wowote kati ya mikoa iliyopo Tanzania. Kuhusu mshahara si haba ni mnono ni kuanzia laki 5 hadi 8.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu: +255 713 40 32 78.

Upatapo taarifa hii share mara milioni au mjulishe na mwenzako.

Jumapili, Februari 02, 2014

SANAA NA MUZIKI WA INJILI

Mpendwa katika Bwana ni ombi langu kwa Mungu akubariki unaposoma somo hili ili uweze kufahamu mambo ambayo ulikuwa huyajuwi au kukumbuka yale ambayo unayajua lakini ulikuwa umeyasahau. Kipengele hiki kidogo cha somo hili nimekitoa katika makala ninayoandaa na hivyo, ni tamanio la moyo wangu kuwa litaeleweka vizuri kama somo lililokamilika kwa lengo hili na kwa wakati huu. Kama wewe ni mwanamuziki, mwimbaji au tu mdau wa muziki, basi naamini utapata jambo la kujifunza kwa kipindi hiki unaposoma.

Muziki, pasipo kujali unatumikaje, ki taaluma huwa uko katika eneo la Sanaa. Vitu vyote vyema vinatoka kwa Mungu(Yakobo1:17). Tunafahamu kuwa vitu vyote tulivyonavyo chanzo chake ni Mungu mwenyewe na vikitumika vyema, huonyesha sura fulani ya Mungu wetu. Hivyo mwana sayansi mkuu ni Mungu na mwana sanaa mkuu pia ni Mungu mwenyewe. Mungu kama mwana sanaa alipanga vitu vyote katika picha na kama mwana sayansi akatumia sayansi na sanaa kuviumba na kuviweka viwepo hata leo. Naamini kupitia sanaa ya Mungu, ndipo usemi maarufu wa Biblia, “Mungu akaona yakuwa ni vyema” ulirudiwa mara kwa mara katika kitabu cha Mwanzo.

Saana ina uwezo mkubwa sana kuunganisha vyema vitu visivyoonekana wala kusikika na kuvileta katika ulimwengu unaoonekana na kusikika. Mchoraji anaweza kuunganisha mistari na kuonyesha picha ya kitu fulani. Hivyo hivyo, mwana muziki au mwimbaji anaweza kuweka nota na milio tafauti tofauti na kutengeneza wimbo au muziki unaosikika vizuri.

Ni jambo la ajabu sana kuwa neno ‘Msanii’ limetumika vibaya sana katika sehemu hii ya dunia tunayoishi kufikia wasanii kuanza kuchukia kuitwa/kutambulishwa hivyo. Hata hivyo, ingekuwa ajabu pia kwa Ndovu kukataa kuitwa Ndovu kwa kukuta Fisi akiitwa Ndovu. Daktari hawezi kukataa kutambulishwa kama Daktari kama jina Daktari litatumika vibaya. Kwa nini Msanii akatae kuitwa hivyo kwa sababu jina hilo limetumika vibaya? Kwa hivyo, Msanii katika Kanisa lazima ajivunie kuwa Mungu amempa huduma ya kutumia Sanaa hiyo kumtumikia kama vile Injinia anavyoweza kujivunia kutumia taaluma yake ya ujenzi kwa ajili ya kujenga nyumba ya kuabudia Mungu. Mungu ameweka Sanaa ya Muziki ili utaalamu huo utumike kuleta sifa nyumbani mwake. Kwa maana hiyo, ni vyema wana muziki wakajitahidi kukuza taaluma hiyo kwa elimu ya kiroho na ya asili pia inayohusu muziki.

Ki ujumla, sanaa hutumia uwezo wa kuwaza na kufikiria na kutumia (imagination)
kwa upana sana, ambako huleta picha hiyo kuonekana au kusikika. Tofauti na taaluma nyingine, sanaa hutumia ubunifu(creativity) mwingi kwa sababu sheria na kanuni zake hazijabana sana tofauti na sayansi ambayo kanuni zake na mahesabu yake yako ya ki-vipimo zaidi. Hivyo, sanaa ina uwezo wa kubuni mambo mapya sana. Kwa mfano, muziki wa Jazz ulipobuniwa na watu weusi huko Marekani, watu walipinga uhalali wake huku wakisema kuwa kanuni za ki-muziki zimevunjwa. Lakini baada ya muda, muziki wa Jazz uliongezeka umaarufu wake na baadae ukakubalika kuwa muziki halali.

Muziki kama sanaa nyingine hutumia hisia nyingi ili kufikia walengwa.  Kwenye taasisi tatu za mtu, yaani roho, nafsi na mwili ambazo humfanya mwanadamu kuwa mwanadamu, nafsi hutumika kwa asilimia kubwa sana kufanya kazi ili kutengeneza na kuhudumu katika sanaa. Katika nafsi, kitengo cha hisia ndicho kinachofanya kazi kubwa ya ziada kufanya sanaa,(sisi hapa tukihusika na muziki.) Kwa hivyo tunapoenda kuongea muziki moja kwa moja, tunafahamu kuwa mambo mengi yanayowaathiri wana muziki na waimbaji, basi yanaathiri wana sanaa kwa ujumla wake.

Naamini kuwa wote tunakubaliana kuwa wanamuziki na waimbaji ni watu wa hisia nyingi. Ndivyo Mungu alivyowaweka duniani ili watumike kufariji, kufurahisha na kuonyesha huzuni ili kuhudumia jamii. Kwa sababu ya hisia nyingi zinazotumika katika muziki, wakati mwingine, ni rahisi kwa wanamuziki na waimbaji hawa kukosa mwelekeo, mizani na vipimo(balance), wingi au upungufu wa hisia unapotokea. Jinsi ya kujitunza ki-hisia, basi, huwa ni jambo la muhimu sana, jambo ambalo wengi wao hawajui, ili wasije wakafanyika kituko badala ya suluhisho katika jamii.

Kupitia hisia kuwa na sehemu kubwa ya mchango katika maisha ya mwanamuziki na mwimbaji, itaonekana jinsi ya kuvaa na staili zake za maisha kwa ujumla zilivyo tofauti sana na za watu wengine katika jamii. Hapa, hatuwezi kuwaambia wabadilike wasiwe hivyo, maana mara nyingi hicho huwa ni kitambulisho cha taaluma yao, ila wanahitaji tu kudumisha kiasi tu, ili wasipitilize, na pia wasifanye kwa kuiga.

Sasa, mtu yeyote anayetoa huduma katika jamii, lazima ajifundishe kurudisha katika maisha yake kile kinachotoka anapohudumia jamii ile. Kwa mfano, mwana riadha anahitaji ale chakula kizuri, apumzike, ajiweke vizuri ki saikolojia ili asihudumie jamii na baadae maisha yake yakaharibika. Anapofanya mazoezi na hatimae kushindana, anahitaji ajue ni chakula gani cha kutumia ili arudishe nguvu na kadhalika. Mtumishi wa kiroho, kama mchungaji anahitaji aombe na kuabudu Mungu, asome neno na kuwa na ushirika mzuri na pia kupumzika ili arudishe nguvu anazotumia katika huduma yake. Vile vile, mwanamuziki na mwimbaji wa nyimbo za injili  lazima ajue jinsi ya kurudisha nguvu anayotumia ikiwemo ya ki hisia ili aweze kuhudumu bila maisha yake mwenyewe kuharibika.

Huduma ya muziki na uimbaji ina shamrashamra nyingi, makelele mengi na kuhudumia mbele ya umati au watu wengi. Ni rahisi jambo hili likaingia vibaya katika akili ya mwimbaji au mwanamuziki huyo na kuanza kuishi katika ‘ulimwengu’ usiyo halisi. Ile kushangiliwa na muonekano wa kugusa umati au watu wengi unaweza ukaweka picha isio ya halisi katika maisha ya mtu huyo na akaanza kuishi maisha tu ya juu juu. Ikumbukwe kuwa mwanamuziki na mwimbaji wa nyimbo za Injili ni mwanadamu na hivyo ana mapito yake katika maisha. Tafakari sasa kuwa amekuwa na wakati mbaya katika maisha yake na sasa ana huzuni lakini hapo hapo anatakiwa kusimama mbele za watu na kuwafurahisha au kuwatia moyo. Anatakiwa hapo hapo atumie hisia yake kuwafurahisha watu wakati yeye mwenyewe ki-hisia yuko chini. Pasipo Mungu kuwa naye na kumsaidia katika huduma yake, hali hii inapotokea mara kwa mara, inaweza ikamchanganya ki-hisia.  

Kwa sababu ya umuhimu wa hisia katika maisha ya mwanadamu yeyote, hisia zinapochanganyikiwa, mwanadamu hujikuta katika ulimwengu usiyo halisi na  kuwa kituko katika jamii, huku yeye akiona kuwa yuko sawa.

Kwa nini Neno ‘Msanii’ limetumika vibaya?

Kwa nini neno Msanii limetumika kuonyesha utovu wa maadili? Ningependa (nikiwa na uchungu mwingi moyoni) kuangalia sababu ya jina Msanii kutumika kuonyesha sifa mbaya katika jamii. Hili linaniumiza kwa sababu na mimi nina taaluma ya sanaa. Imekuwa tabia ya watu wengi katika sehemu hii ya ulimwengu tunayoishi kutumia neno hili kuonyesha mtu tapeli, muongo asiyeeleweka na kadhalika.

Sifa ya sanaa ni kuonyesha picha ya kitu kilichopo au ambayo msanii anataka  kuitengeneza ili ionekana kama wazo katika jamii. Kwa mfano, msanii mwimbaji anaweza kutumia sanaa kukuonyesha mambo yaliyopo katika jamii. Anaweza kuimba wimbo wenye hadithi ya fulani hata kama sio picha halisi ya maisha yake. Anaweza kuimba wimbo kuwa anataka kuolewa na kupata watoto wengi hata kama ki halisi hataki hata mtoto mmoja. Mwimbaji anaweza kukupa picha ya maisha ukafikiri kuwa ndivyo alivyo, kumbe sivyo hivyo. Kupitia hili, Msanii ameonekana kama kuwa mwongo fulani hivi. Ameonekana kama mtu anayeweza kuichora picha yoyote  na kujionyesha mtu ambaye siye katika jamii.

Muziki umetumika kujibizana na hata kugombana na kutukanana, mwimbaji mmoja na mwingine. Mambo ambayo yameleta picha ya sanaa kutumika kuwa chombo cha (kumfagilia) kumsafishia jina msanii husika. Kwa sababu ya nguvu ya sanaa, wasanii wengi wameitumia kwa faida binafsi kujitengenezea nafasi katika jamii, badala ya kuihudumia jamii ile.

Kwa sababu hapa tunaangalia sanaa ya muziki katika nyumba ya Mungu, ni vyema tutoe tahadhari kuwa Muziki wa Mungu unatakiwa kumtukuza Yeye, kuhudumia kundi lake na kusaidia kuleta wengi katika kundi hilo. Muziki na vipawa vyote katika nyumba ya Mungu vinatakiwa kutumika kwa utukufu wa Mungu na hivyo sio kwa ubinafsi. Kwa sababu hiyo wana muziki katika nyumba ya Mungu wasiwe kama wa dunia ambao wanaimba nyimbo kuhamasisha jamii kuhusu jambo moja huku wao wakifanya kinyume. Mwanamuziki au muimbaji wa Mungu asiimbe kuwa yeye anapenda kuomba wakati sio kweli maana hapo ndipo atakapoonekana na watu kuwa ‘Msanii’ kwa kinyume cha matumizi ya jina hilo. Hili limeonekana kwa watu wengi wanaoimba nyimbo za injili na za kusifu na kuabudu kuwa wanachoimba na wanachofanya ni vitu viwili tofauti. Mungu asaidie ili neno hili linapotumika kinyume duniani, katika nyumba ya Mungu, Msanii awe ni chombo cha heshima cha kumtukuza Mungu na si vinginevyo.

Jambo lingine ambalo hufanya neno ‘Msanii’ kutumika vibaya ni kwa sababu ya kitu ambacho nimegusia awali kuwa, wengi wao huchanganyikiwa kwa kuzidiwa na msongamano wa hisia katika maisha yao na hivyo kuonekana kuishi maisha yasio halisi, na hivyo mtu yeyote anayeonekana kudhihirisha aina hii ya maisha hufananishwa na wasanii waliofanyika hivyo. Hivyo huonekana kama vile ndio maisha ya wasanii kuishi katika maisha ambayo sio ya kawaida na watu wengine, kwa kuvaa kwao labda na hali zingine ambazo huonekana maishani mwao. Wanamuziki na waimbaji wanaohudumu katika nyumba ya Mungu wanatakiwa kuonyesha mfano katika maisha yao ili waonekane kuwa ni wahudumu zaidi kuliko tu kuonekana kuwa ni waimbaji, kwani vipawa vyao vinatakiwa kudhihirisha tabia fulani ya Mungu.Njia ya kufuta dhana hii katika waimbaji na wanamuziki walio katika nyumba ya Mungu ni kushinda majaribu ambayo huwalenga na kuishi kwa Imani zaidi kuliko ki hisia, kwani, Biblia inasema tunaishi kwa Imani na sio kwa yale tunayoyaona na kuyahisi. Kwa hivyo wajenge nguvu ya kiroho katika maisha yao na waongozwe na Roho Mtakatifu.

Jambo jingine ni kuomba uongozi wa Mungu kwa Roho Mtakatifu ili nyimbo zao ziwe zinatokana na njaa na kiu ya Mungu na haki yake katika maisha yao, ili wasije wakaimba nyimbo ambazo wanawaelekeza watu wafanye yale ambayo wenyewe hawayafuati.

La mwisho, katika somo hili, ni kuomba kipawa chao kiambatane na neema iliyo juu ya maisha yao ili kipawa kisiwapeleke juu zaidi kuliko neema inayoweza kuwalinda katika kiwango  hicho. Pia waweze kuwa na afahamu wa kujua milango inayofunguka kwao, kama ni  Mungu aliyefungua au ni wanadamu maana mara nyingi hapo ndipo watu hupandishwa  na kujikuta mahali ambapo hakuna neema ya kumlinda mtu katika kiwango alichopandishwa. Hivyo wawe pia na ujasiri wa kufuata tu njia ambayo Mungu anatengeneza.

Muziki una nguvu yake wenyewe.Ni jambo la muhimu kujua kuwa Muziki kama Muziki una nguvu ya ajabu sana, ukiachilia mbali kuwa unaweza kuubeba upako. Kwa maana nyingine, muziki una uwezo ndani yake wa kujitegemea bila kujali ni nani anayeutumia. Muziki una nguvu kwa sababu ya asili ya ulivyoumbwa. Kama chombo cha mawasiliano, kuna uwezo ndani ya muziki ambao husaidia kuleta ujumbe katika jamii lengwa. Labda kwa sababu hii, ndio maana huduma ya muziki na uimbaji imebeba umuhimu mkubwa sana nyumbani mwa Mungu. Inawezekana umuhimu mkubwa ni ukubwa wa muziki wenyewe na sio tu kutokana na wana muziki na waimbaji wenyewe. Kwa sababu hii, watu walio katika huduma hii wanaweza kujibebea heshima kubwa bila kujua kuwa chombo chenyewe ndicho muhimu kuliko wenyewe.
Muziki ni chombo cha muhimu sana katika uumbaji wa Mungu kwa hiyo kinabeba nguvu nyingi sana na hivyo kinatumika kwa ajili ya kuleta mabadiliko makubwa sana katika uumbaji mwingine wa Mungu. Kipawa cha muziki, basi, kina uwezo wa kumuonyesha mwanamuziki na muimbaji katika hali fulani ambayo asipojiangalia, anaweza akajitafsiri katika hali ambayo sio halisi katika maisha yake. Anaweza kujisifu na kujiona yuko katika kiwango fulani cha ki-maisha ambacho sio halisi katika maisha yake, kumbe tu ni kwa sababu ya nguvu iliyo katika muziki wenyewe. Hata hivyo, nguvu ya muziki iko sana katika kugusa hisia za nafsi, na hivyo kutegemea nguvu ya kiroho kuleta mguso katika maisha ya kiroho. Katika muziki, maisha ya watu wanaohudumiwa, wanaweza kuguswa katika kiwango cha ki-hisia tu au, wakaguswa katika kiwango kingine, wakafikiwa katika maisha ya kiroho.

Sasa hapa ndipo tunapogundua umuhimu wa kipawa au talanta ya muziki kushukiwa na kipawa au karama ya kiroho. Wako wanamuziki wengi wa duniani kwa kujua hili wanatafuta nguvu za giza kwa kwenda kwa waganga/wachawi au hata kutafuta kuabudu mashetani ili wawe na mguso wa kiroho. Sisi tulio katika nyumba ya Mungu tunatafuta kwa Mungu uwezo na vipawa vya kiroho ili karama ishuke juu ya talanta na hivyo kugusa, sio tu nafsi na hisia zake bali roho ya mtu au maisha yake ya kiroho. Kipawa cha kimwili(talanta/kipaji) hakiwezi kugusa rohoni. Kipawa cha kiroho(karama) hugusa rohoni. Kwa hivyo vyote ni muhimu, ila tunajua kuwa vitu vya kimwili ni vya muda na vya kiroho ni vya kudumu.

Kuna mifano mingi katika Biblia ambayo inaonyesha talanta za ki-muziki ambazo zilishukiwa na karama za rohoni. Tunafahamu hadithi ya Daudi katika 1Samueli 16:23 “Ikawa ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa na, na ile roho mbaya ikamwacha.” Hapa kuna ufunuo mwingi sana. Kwanza, muziki ulimburudisha Sauli, kama vile tulivyoona hapo juu kuwa muziki una nguvu wenyewe na la pili, Sauli aliondokewa na roho mbaya, ambayo ni kipawa au karama ya kiroho ambayo ilifanya kazi hiyo. Pia kuna wazo hilo la ‘roho mbaya kutoka kwa Mungu’ ambapo watumishi wengi hutafsiri kuwa ni roho iliyoruhusiwa na sio kuwa ilitoka kwa Mungu wakisema kuwa Mungu hana roho mbaya. Wengine pia husema ni aina ya roho ya ghadhabu ambayo inatafsirika kuwa ni mbaya. Hata hivyo la muhimu kujua hapa ni kwamba ukombozi ulitokea kwa Sauli wakati Daudi alipopiga muziki.

Andiko jingine ni pale Nabii Elisha alipohitaji mwanamuziki katika 1Wafalme 3:14-15. “Elisha akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe. Ila, sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga mkono wa Bwana ukamjia juu yake. Akasema, Bwana asema hivi……..” Hapa, kuna hadithi ya nabii ambaye amekwazika kumuona adui ambaye alikuwa mfalme muovu. Lakini kwa ajili ya Yehoshefati, Elisha akaheshimu uwepo wake na akaomba mwanamuziki ambaye alipopiga muziki ule, upako ukaja juu ya Elisha na akatabiri. Hapa tunaona talanta/kipaji ya muziki ikishukiwa na karama ya unabii ambayo ilifanya kazi juu ya nabii Elisha. Kwanza nguvu ya muziki ilimuondolea Elisha kukwazika kwa kumfurahisha na pili, karama ya unabii ilichochewa na karama iliyokuwa juu ya mwanamuziki yule.

Na mwisho, kwa sasa katika mifano, tunaona katika 1Mambo ya Nyakati 25, mara kwa mara ikisemekana kuwa wana muziki waliochaguliwa na mfalme Daudi na viongozi wa kiserikali walipewa kazi ya kutabiri kupitia muziki, katika msari wa 2, “…..walioamriwa na Asafu aliyetabiri kwa amri ya mfalme” na mstari wa 3, “…..watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu Bwana.” Wana muziki na waimbaji wanatakiwa kuheshimu kuwa Mungu amewapa talanta za kumtumikia Yeye, lakini pia watafute karama za Roho Mtakatifu ili wanapogusa watu wa Mungu, basi iwe katika maisha yao yote kwa ujumla.

Ninaamini kuwa Mungu amekupa kitu chema cha kukusaidia ili uweze kutoa mchango wako katika huduma hii kwa ajili ya kuiboresha.

Jumamosi, Februari 01, 2014

MWANAHARAKATI WA USALAMA WA TAIFA - MWALIMU JULIUS K. NYERERE

Katika kumkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuzienzi kazi za kimapinduzi alizozifanya kwa maslahi ya taifa letu na watu wake, kila mtanzania mzalendo atakubaliana nami kwamba katika kipindi kifupi sana cha miongo miwili historia imetuonyesha kwamba mambo mengi aliyoyasimamia Mwalimu yalikuwa sahihi ingawa yametelekezwa.

Maandiko ya Mwalimu kuhusu Azimio la Arusha, siasa ya ujamaa na kujitegemea, elimu, afya, kilimo, viwanda, reli, bandari, ustawi wa maisha ya wananchi, utu, haki sawa kwa wote, nk na mafanikio yake yanauonyesha umahiri aliokuwa nao katika kubuni mikakati ya kulikomboa taifa, ingawa wapo vibaraka waliolishwa kasumba ya kibeberu, ambao wanazibeza kazi za Mwalimu kwani zinasuta dhamira zao juu ya ustawi Tanzania na watu wake.

Katika ulimwengu wa sasa tunashuhudia mataifa yanatikiswa na mengine yameangushwa na kumegwa vipande vipande na magaidi na majasusi ambao wamevunja ngome za ulinzi na usalama wa mataifa hayo. Mamilioni ya watu wasiokuwa na hatia wameuwawa. Duniani kote mapambano dhidi ya magaidi na majasusi yanaendelea kwa siri na wazi ili kulinda uhai wa watu na mali zao na ustawi wa mataifa. Hali hii si ngeni. Imekuwepo kwa miaka yote. Kwa Tanzania, Mwalimu Nyerere aliliweka mwanzo kabisa suala la usalama wa taifa ambao kimsingi ndio uhai wa Tanzania. Katika kumkumbuka Mwalimu nitaidurusu kazi aliyoifanya ya kuimarisha na kuulinda usalama wa taifa, pia nitatoa maoni yangu ya nini kifanyike katika juhudi za kuimarisha usalama wa nchi yetu katika ulimwengu huu wa kigaidi na kijasusi.

Historia inaonyesha kuwa Tanzania chini ya Mwalimu Nyerere ilianzisha sera ya kutetea na kusimamia haki watu duniani kote pamoja na kuongoza harakati za kupigania uhuru wa Afrika. Kwa kuwa harakati hizi zililenga kumkomboa mwafrika aliyenyonywa na kukandamizwa na mabeberu, mataifa makubwa yenye maslahi yake katika nchi za kiafrika yaligeuka kuwa hasimu mkubwa kwa Tanzania na yalitumia kila mbinu za kijasusi na kigaidi kutaka kulihujumu taifa letu na hata kuipindua serikali. Tanzania ya Nyerere ilikuwa macho na iliwadhibiti magaidi na majasusi kutoka kwa makaburu wa Afrika Kusini, serikali ya Ian Smith ya Rhodesia, serikali za kikoloni za Kireno wote hawa wakiungwa mkono na mataifa makubwa ya magharibi. Majasusi kutoka kwa Nduli Idd Amini nayo yalithibitiwa. Hali ya sasa ya ugaidi na ujasusi duniani na tishio lake kwa usalama wa Tanzania yetu inafanana na hali tuliyokumbana nayo wakati huo. Mbinu za magaidi na majasusi ni zilezile -- kujipenyeza kwa siri na kuujua udhaifu wa mfumo wa ulinzi na usalama na wapi pa kupiga kwa urahisi -- na malengo yao ni yaleyale -- kutia hofu, kuuwa watu na kuhujumu miundo mbinu ili kutimiza malengo yao ya kisiasa.

Nini kiliifanya Tanzania kuushinda ugaidi wa ujasusi? Jibu ni mfumo imara wa ulinzi na usalama ambao ulikuwa ni jukumu la kila mtanzania -- mfumo wa shina la nyumba kumikumi. Hapa neno shina lilimaanisha pia maofisi na maeneo yote ya kazi, starehe nk ili mradi upo mkusanyiko wa watu. Jukumu la usalama wa taifa halikuwa jukumu la vyombo vya usalama peke yake. Watu walilelewa hivyo na kuishi hivyo. Kila raia alikuwa ni askari katika kaliba yake. Mfumo huu imara aliounzisha Mwalimu Nyerere uliifanya Tanzania kuwa na ngome imara ya kuwadhibiti maadui wa ndani na nje na kudumu katika amani. Kila waliothubutu kuingia nchini kufanya ujasusi na ugaidi walikamatwa na kurejeshwa makwao. Kila mpango wa kijasusi na kigaidi ndani ya nchi ulijulikana na kudhibitiwa mapema. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, KIITIKADI (kijamaa), watanzania walitambua kuwa Tanzania ilikuwa na maadui wa ndani na nje na kwamba utayari wetu, mshikamo na ushirikiano wetu katika kuilinda nchi yetu ndiyo ilikuwa ni silaha yetu kubwa. “Moyo kabla silaha” yalikuwa ni maneno ya hamasa kutoka kwa Mwalimu. Idara ya Usalama wa Taifa ilitanda kila kona ya nchi si kwa maana ya maofisa kutoka “Idara ya Usalama Taifa” bali kila raia mwema, mzalendo, mwenye nia safi juu ya nchi yetu alikuwa ni mwanaidara. Kwa kujipanga sawasawa kimkakati tuliwashinda maadui. Tanzania ilibaki salama na hatimaye nchi za Angola, Namibia, Msumbiji, Zimbabwe na Afrika Kusini zilipata uhuru wake.

Tanzania ya sasa bado inao maadui wa ndani na nje na inakabiliwa na changamoto kubwa sana katika kukabiliana nao.. Lakini la kusikitisha ni kwamba suala la usalama wa taifa linaonekana kuwa ni suala la vyombo vya ulinzi na usalama tu. Haya ni matokeo ya kutelekezwa kwa mfumo wa usalama tuliokuwa nao baada ya kulitumbukiza taifa katika mfumo wa uliberali mamboleo. Tanzania ya katika mfumo mpya wa uliberali mamboleo ikasahau kwamba bado inao maadui wa ndani na nje. Tanzania ikacha milango na madirisha wazi na hata paa ikaezua. Mfano ni wahamiaji haramu wanaingia na kutoka Tanzania wapendavyo. Twiga na ukubwa wake anapitishwa uwanja wa ndege. Majengo marefu yamejengwa karibu sana na Ikulu jambo ambalo ni hatari sana kwa Usalama wa Taifa. Kisa? Eti wameweka mazingira mazuri ya uwekezaji. Ajabu sana! Tanzania ikawa kituo cha madawa ya kulevya. Ujangili na wizi wa kutumia silaha ukashamiri. Silaha za kivita zikatapakaa kila pembe ya nchi. Uhujumu uchumi ukawa ni njia kuu ya kujitajirisha. Tanzania ikaendeshwa na rushwa. Rushwa kidogo inawasahaulisha wenye dhamana athari za wahamiaji haramu (rejea hotuba ya Rais Kikwete akihitimisha ziara mkoani Kagera: youtube.com/watch?v=Pxsbyi82uxM) au madawa ya kulevya kwa taifa na vizazi vyetu. Matokeo yake tukaupa kisogo mfumo wetu mzuri na imara wa ulinzi na usalama wa taifa kuanzia shina la nyumba kumikumi, kwenda kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji au mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata, wilaya, mkoa hadi ngazi ya taifa.

Tukumbuke kwamba katika shina ndipo anakopatikana adui wa ndani na nje. Tunaanzia kidogo kwenye wilaya. Lakini nguvu zetu zote tumezielekeza kwenye ngazi ya taifa na mkoa. Kwamba kupitia kwenye kamati za ulinzi na usalama za taifa, mkoa na wilaya Tanzania iko salama. Kwa kweli tunajidanganya. Katika shina ndipo kila mmoja wetu anamfahamu jirani yake na nyendo zake na hata siri zake. Kupitia ufahamu huu taifa linaweza kumdhibiti yeyote yule kabla ya kuleta madhara uraiani au katika vyombo vya ulinzi na usalama. Hata kwenye nchi zenye teknolojia ya hali juu ambazo zimetandaza kamera kila kona na kufuatilia nyenendo za watu kwenye mitandao ya simu na intanet kama Marekani na Uingereza, mambo yakiwazidia huwa wanarudi kwenye mashina ili kukabiliana na hujuma za kigaidi na kijasusi. Nchi kama Cuba ambayo bado inautumia mfumo huu wa shina na imeweza kuwepo mpaka leo licha ya kuwa karibu sana hasimu wao mkubwa tena mwenye nguvu sana -- Marekani. Haiingii mtu Havana akafanya ugaidi na ujasusi. Ni ngumu sana tena sana. Wachina wana mfumo huu wa shina. Hapenyi mtu pale.

Nitumie fursa hii kusema kwamba katika kumuenzi Mwalimu basi turejeshe na tuimarishe mfumo huu wa usalama kuanzia kwenye shina. Kiitikadi (maana itikadi ndiyo inayozaa uzalendo) wananchi wahamasishwe na kushirikishwa zaidi katika usalama wa taifa katika mashina yote nchini na taarifa zao zisivujishwe kwani kufanya hivi ni kuhatarisha maisha yao hasa pale wanapotoa taarifa kuhusu watu wenye uwezo mkubwa kifedha. Mwaka 2010 nilikutana na mzee mmoja mkazi katika mojawapo ya vijiji vinavyozunguka jiji la Mwanza akaniambia kuwa kuna wakati aliitikia wito wa serikali wa kutoa taarifa polisi za wanaomiliki silaha za moto kinyume cha sheria lakini alipotoa taarifa hizo kesho yake wale aliowataja wakamwendea na kumtisha kweli. Hayo ndiyo matokeo ya mambo kuendeshwa kwa rushwa. Kwa hiyo tuwe na mtandao wa siri mpana na maalum wa upashanaji habari za kiusalama kuanzia ngazi ya shina ambao utaiwekea Tanzania ngome imara kwamba anapoingia muhamiaji haramu, gaidi, jasusi kwenye kaya au eneo fulani, shina linakuwa na taarifa hizo zinafikishwa kwenye vyombo husika haraka iwezekanavyo. Au raia mwema akishuku au kuwa na taarifa kwamba mtu fulani katika kaya, ofisi, au kundi fulani ana nyenendo za kutiliwa mashaka, basi habari zake zipelekwe kwenye vyombo husika mara moja na uchunguzi wa kina ufanyike haraka ili kuujua ukweli na kumdhibiti kabla hajafanya madhara. Tukifanya hivi tutaudhibiti vilivyo ugaidi na hujuma za jiasusi za aina yeyote. Tusisubiri CIA na FBI ambao kimsingi hawako kwa ajili ya maslahi ya Tanzania yetu.

Wapo wanaoweza kusema mfumo huo wa kuwa macho kuanzia kwenye shina unaifanya Tanzania itawaliwe kipolisi (police state) na kwamba unawaminya uhuru watu. Jibu kwa wasemao hivi ni kwamba hakuna kitu kinachoitwa UHURU-HURU. Uhuru usio na mipaka wala wajibu haupo. Uhuru wa watu kuachwa wakapanga mipango ya kigaidi na kijasusi ya kuhujumu nchi ni uhuru wa kuleta maangamizi. Kama taifa hatuwezi kukubali kuona watu wasio na hatia wanauwawa. Kwa hiyo, mfumo huu wa kiusalama katika mashina ni njia sahihi, nyepesi na ya uhakika ya kupata taarifa za magaidi na majasusi na kuwadhibiti. “Kinga ni bora kuliko tiba,” wahenga wetu walisema. Kwa mfumo huu tutawadhibiti wauza madawa ya kulevya. Tutawadhibiti majangili. Tutawakamata wakwepa kodi. Tutajua nani ni nani, yuko wapi, na afanya nini katika kulihujumu taifa na tutachukua hatua katika wakati muafaka kumdhibiti na kutokomeza uovu wake.  Na teknolojia simu za mkononi katika mfumo maalumu itatusaidia sana wananchi katika kufikisha taarifa kwa vyombo husika ili mradi tu siri za watoa taarifa hazivujishwi na vyombo husika. Pia tuangalie uwezekano kurejesha sheria ya kizuizini ili mradi iwepo haki, uadilifu, udhibiti na ulinganifu katika kuitumia ili isije kutumika kuwanyamazisha watu. Katika kumkumbuka Mwalimu tujadili kwa mapana na marefu na kujikumbusha historia ya nchi yetu na mafanikio yake na umuhimu wa mchango wa wananchi katika usalama wa taifa letu. Na wala asikudanganyeni mtu kuwa vita baridi ilikwisha. Bado ipo tena ni hatari zaidi. Kwa mfumo wa shina wa kuwashirikisha wananchi Tanzania itakuwa salama na amani yetu itadumu.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu udumishe uhuru na umoja wetu.

Ndugu yenu,
Amani Millanga.

Source: INGIA HAPA