Mtayarishaji

Morning Star Radio

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Habari. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Habari. Onyesha machapisho yote

Jumanne, Agosti 09, 2016

Taarifa...UZINDUZI WA TRENI STESHENI PUGU DAR ES SALAAM.

 

Leo kampuni ya reli Tanzania TRL  kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo CHAMA CHA KUTETEA ABIRIA (Chakua), kwa pamoja tumezinduwa treni ya abiria itakayofanya safari zake kuanzia stesheni ya dsm kwenda pugu.

 

Katibu idara ya reli,, Godfrey Mali, kulia,, Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki, Wilson Sylvester na muheshimiwa waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa wakiwa kwenye uzinduzi wa treni ya abiria ya kwenda pugu leo.
 

 Katika Uzinduzi hua Chama Cha Kutetea Abiria (Chakua) iliwakilishwa na mkurugenzi wa kanda ya mashariki, Wilson na katibu idara ya reli, Godfrey Mali.



 Pongezi kwa Katibu mkuu idara ya reli, hiyo ni kazi nzuri sana.



 Ni safari  ambayo itaanza saa 10:45 alfajiri kwenda pugu tripu ya kwanza na tripu ya mwisho 4:20 asubuhi hiyo routi ya asubuhi.

Routi nyingine itaanza saa 09 :55 alasiri kuekea pugu mwisho wa routi za jioni ni saa 4:15 usiku. Nauli kwa mkubwa Tsh 400 mwanafunzi Tsh 100. Hizi zitakuwa nauli za majaribio mpaka hapo sumatra watakapotoa muongozo wa nauli.


Uzinduzi wa treni ya abiria ya kwenda Gongolamboto Pugu  tayari umezindiliwa na walielekea pugu  viongozi mbali mbali akiwemo waziri wa uchukuzi pia mea wa jiji halikadhalika   mkuu wa mkoa,, na viongozi wa shirika la reli Tanzania.


 Kama unavyoona kwenye Picha hapo Juu Mh.Makame Mbarawa akiwa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda.

 
 Kesho (Jumatano) Chakua itafanya mazungumzo na mkurugenzi mtendaji wa shirika la reli Tanzania TRL  ofisini kwake makao makuu ya reli tanzania kuanzia saa tisa kamili.


Jumatatu, Februari 24, 2014

Taarifa ya Wizara kuhusu ziara ya Waziri Membe nchini China



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atafanya ziara ya kikazi ya siku tano katika Jamhuri ya Watu wa China kuanzia tarehe 24 hadi 28 Februari, 2014. Ziara ya Mhe. Membe inakuja kufuatia mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi. 

Mhe. Membe anafanya ziara hiyo nchini China kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kirafiki uliopo kati ya Tanzania na China. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Membe atafuatana na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Ziara hii pia ni muendelezo wa maeneo ya utekelezaji baada ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping aliyoifanya hapa nchini tarehe 24 na 25 Machi, 2013 na baadaye ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda nchini China mwezi Oktoba, 2013.

Akiwa nchini China, Mhe. Membe atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mhe. Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China tarehe 25 Februari 2014. Siku hiyo hiyo Mhe. Membe atamtembelea Makamu wa Rais wa China, Mhe. Li Yuanchao kwa lengo la kumsalimia na baadaye atafanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Gao Hucheng.

Aidha, tarehe 26 Februari, 2014 Mhe. Membe atatembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Poly Technologies yaliyopo katika mji wa Shenzhen na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo kabla ya kutembelea Makao Makuu ya Kampuni ya China Merchant Holdings International ambako atapokea taarifa ya maandalizi ya kuanza kwa mradi wa Ujenzi wa Bandari katika eneo la Mbegani huko Bagamoyo.

Mhe. Membe pia atapata fursa ya kutembelea Kampuni ya HUAWEI ili kujionea shughuli mbalimbali. Kampuni ya HUAWEI ina Mkataba na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya hapa nchini kuhusu Elimu kwa Njia ya Mtandao (e-Education) kwa Shule za Sekondari.

Vile vile tarehe 27 Februari, 2014, Mhe. Membe atautembelea Mji maarufu wa biashara wa Guangzhou na kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi mjini hapo. Mhe. Membe atatoa taarifa kuhusu hali ya uchumi, siasa na masuala ya jamii yalivyo hapa nchini kwa sasa pamoja na kutoa taarifa ya maendeleo ya Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
Waziri Membe pia atatembelea Eneo la Viwanda la Huadu tarehe 28 Februari, 2014 kabla ya kurejea nchini tarehe 1 Machi, 2014.

IMETOLEWA NA: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM. 
24 FEBRUARI, 2014

Jumanne, Januari 28, 2014

RAIA WALAANI JARIBIO LA AL-SHABAAB KUHUSU INTERNET

Wasomali wanaperuzi intaneti katika mkahawa mjini Mogadishu. [Na Majid Ahmed/Sabahi]

Jaribio la al-Shabaab kupiga marufuku mkonga wa mawasiliano na huduma za mtandao wa intaneti limekumbana na hasira kali kutoka kwa raia wa Somalia na kuchochea onyo kali kutoka kwa serikali.
Katika taarifa iliyochapishwa siku ya tarehe 8 Januari kwenye mtandao wa Somalimemo, al-Shabaab ilitangaza kupiga marufuku intaneti wakiamuru kampuni za simu kuacha kutoa huduma ya intaneti ndani ya siku 15.

Taarifa hiyp pia ilionya kwamba kampuni na watu wasiofuata amri hiyo watachukuliwa kama maadui na kuadhibiwa chini ya sharia.
Al-Shabaab ilihalalisha tangazo lake la marufuku kwa kusema kwamba mashirika ya kijasusi wa Kimagharibi, hasa mashirika ya Marekani na Uingereza, yanatumia intaneti kukusanya taarifa dhidi ya mujahidina.

"Intaneti ya kwenye simu ni hatari kwa kila Muislamu kutumia huduma hiyo [kwani] inamruhusu adui kujua harakati za watu na kukusanya taarifa," lilisema tamko hilo.

"Intaneti ya kwenye simu ni hatari zaidi kwa usalama wa Waislamu wanaopigana na maadui waliokuja, kwa sababu inaongeza fursa ya majasusi [wao] kusambaza taarifa za kijasusi kuhusiana na mujahidina kwa mashirika ya kijasusi yaliyopo nchini," ilisema.

Taarifa hiyo ya al-Shabaab ilisema pia intaneti kwenye simu ya mkononi ilikuwa hatari kwa watoto na vijana ambao wanapata na kusambaza mambo yanayokwenda kinyume na misingi ya Uislamu. Kuendelea kutumia intaneti kwa vijana kutapelekea wawe na "tabia mbaya, ukosefu wa elimu na kupoteza wakati," ilisema taarifa hiyo.

Al-Shabaab iko kwenye shinikizo inayoongezeka

Al-Shabaab ina hofu kubwa na inayoongezeka juu ya huduma za kisasa, ambazo zimelipelekea kundi hilo kufanya uamuzi wa kiholela sana, alisema Abdi Aynte, mkurugenzi wa taasisi ya sera ya Heritage Institute for Policy Studies mjini Mogadishu.

"Wanaogopa kwamba simu zenye huduma ya intaneti zitatumika kuwasiliana na mashirika ya kijasusi ya kimataifa ambayo yanawawinda wapiganaji wa al-Shabaab, hasa ndege zisizo na rubani, ambazo zimepunguza kwa kiasi kikubwa pirika za viongozi wa al-Shabaab," aliiambia Sabahi.

Aynte alisema sababu nyengine ya uamuzi huo wa al-Shabaab ilikuwa ni kampeni yake ya kuwazuia wananchi kupata habari za kilimwengu.

Katika siku za karibuni, al-Shabaab imepiga marufuku upatikanaji wa taarifa muhimu kwenye maeneo inayoyadhibiti, kama vile marufuku yake dhidi ya kuangalia televisheni na unyanyasaji wake dhidi ya raia wanaotumia simu za kisasa.

"Wanataka kuwazuia watu kuishi kwenye ardhi wanazozikalia kuzungumzia ugumu wanaokabiliana nao na kuuwambia ulimwengu juu ya dhila ambayo [al-Shabaab] wanawasabishia," alisema Aynte. "Intaneti inawapa watu uhuru wa kupata habari na al-Shabaab iko dhidi ya uhuru."

Alisema inawezekana pia kwamba al-Shabaab inataka kuchopoa fedha kutoka kwenye kampuni za simu kwa mabadilishano ya kuondosha marufuku ya intaneti.

Aynte alisema hafikirii kuwa marufuku hiyo itatekelezwa kwenye maeneo yasiyo chini ya udhibiti wa al-Shabaab.

Mwezi Novemba, kampuni ya simu ya Liquid Telecommunications ilitangaza mkonga wake wa kwanza wa mawasiliano ndani ya Somalia. Mkonga huo unavuka mpaka wa Kenya na Somalia, na kisha kuunganisha na mtandao wa Hormuud Telekom, unaoongeza kasi ya intaneti katika eneo lote la kusini na kati ya Somalia.

Abdirahman Yusuf al-Adala, mkurugenzi wa idara ya vyombo vya habari katika Wizara ya Habari, Posta na Mawasiliano ya Simu, alisema kwamba jaribio la al-Shabaab kuzuia upatikanaji wa intaneti ya njia ya mkonga litashindwa kwa sababu serikali ilileta huduma hii nchini Somalia na itailinda. 

Hata hivyo, alisema kuwa vitisho vya al-Shabaab vingeweza kuathiri maisha ya watu wanaotumia intaneti jongevu na wanaoishi katika udhibiti wa wanamgambo. 

"Watu wanatumia intaneti kwa ajili ya biashara, elimu, kupata habari, na watayakosa hayo. Tatizo jengine ambalo litasababishwa na suala hili ukosefu wa ajira ambao watu wanaofanyakazi kama watoaji hduma za intaneti," al-Adala aliiambia Sabahi. "Makampuni yana chaguo la kupoteza biashara zao na kwa hivyo kukabiliana na kufilisika, au kudharau amri ya al-Shabaab na kugeuka kuwa lengo la mashambulizi holela ya al-Shabaab." 

Katika kujibu jaribio la al-Shabaab la kupiga marufuku intaneti, Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa alisema itachukua hatua za kupambana na mbinu mpya za al-Shabaab. 

"Wasomali, kama walivyo watu wengine popote pale, wanatuia intaneti kwa ajili ya elimu na kuifikia jamii ya kimataifa ili kupata habari za dunia. Hatutaruhusu wananchi wetu kunyimwa kupata intaneti na kutumia smartphones," Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa Abdikarim Hussein Guled alisema hapo tarehe 11 Januari.

"Serikali ya Somalia itafanya kazi na makampuni yote ya simu ili kuhakikisha uhuru wa kutoa intaneti kwa wananchi wetu, na serikali litafanya kila juhudi katika kulinda maslahi ya umma," alisema. 

Guled aliyaonya makampuni ya mawasiliano ya simu dhidi ya kufanya kazi na magaidi na alisema kwamba serikali ina dhamana ya kuwalinda wananchi wake. 

Makampuni ya mawasliano ya simu ambayo yanatoa huduma jongevu za intaneti hayajatoa kauli yoyote juu ya marufuku ya al-Shabaab na hayakujibu maombi ya Sabahi ya kutoa maoni.

Wananchi wapinga vikali marufuku ya intaneti ya al-Shabaab

Ahmed Mohamud, mwandishi wa habari mwenye umri wa miaka 27 anayefanya kazi na kituo cha redio chenye makao mjini Mogadishu, alisema kuwa alikuwa na matumaini kwamba upatikanaji wa intaneti nchini Somalia utaboreshwa kwa kuunganishwa na mkonga.

"Inanichukua muda mrefu kila mara ninapotaka kupata kitu kidogo chochote kile kutoka intaneti, lakini mkonga ni intaneti ya kasi kubwa sana ambayo inakuwezesha kupata kiasi kikubwa [cha data] kwa muda mdogo sana," aliiambia Sabahi.

Mohamud alisema kwamba njia pekee kwa watu wanaoishi katika maeneo yanayodhbitiwa na al-Shabaab kuwasiliana na dunia na kuwapa taarifa wengine ni kupitia intaneti jongevu. Lakini sasa, alisema, "watakuwa viziwi na vipofu." 

Abdi Ahmed Maalin, mkazi wa kitongoji cha Taleh cha Mogadishu mwenye umri wa miaka 27, alisema kuwa marufuku ya intaneti ya al-Shabaab itakuwa ni ushahidi zaidi kwamba kikundi hiki kiko kinyume na maendeleo na kuboresha maisha ya watu. 

Maalin anayo digirii ya kwanza katika sayansi ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Mogadishu na alikuwa akijitayarisha kujiandikisha na programu ya diplomasia ya kimataifa mtandaoni katika Chuo Kikuu cha Kampala.

"Uamuzi wa al-Shabaab inamaanisha kuwa hakuna elimu kwa ajili yangu," alisema. "Wanasema wanapambana dhidi ya adui, lakini ukweli ni kwamba wao ndio maadui." 

Maalin alisema kwamba matendo yanayoongezeka kwa matendo makali ya al-Shabaab yanatoa wito kwa umma kupambana kukishinda kikundi hiki. 

"Hapo awali tulijua kuwa waliwagawa watu katika makundi mawili: kikundi kinachoishi chini yao ambacho wanakinyanyasa na kikundi ambacho wamekipa jina la makafiri na wanakiuwa," alisema. "Kile wanachofanya sasa kuyafanya watu walio hai wawe wamekufa." 

"Je, tunawasubiri waidai kioa familia itoe mtu mmoja wamle? Hiki ni kikundi kidogo, kwa hivyo tukivamie mara ili tuweze kujikomboa wenyewe dhidi yao," Maalin alisema. "Hatuwezi kusubiri kwa hatua za kijeshi." 

CHANZO: http://sabahionline.com

Ijumaa, Januari 17, 2014

UDUKUZI

Rais Barack Obama





 Ufichuzi wa hivi karibuni uliochapishwa siku ya alhamisi unadai kuwa idara hiyo ya ujasusi ilidukua mamilioni ya ujumbe katika simu za watu za mkononi duniani kila siku.

Upelelezi huo wa simu zilizopigwa pamoja na mitandao umezua hisia kali kutoka kwa wanaharakati na makundi ya kijamii nchini marekani na washirika wake.

Hata hivyo vitengo vya ujasusi vimeonya kuwa uchunguzi zaidi wa mienendo yake huenda ukaathiri usalama wa marekani.

Rais Barrack Obama anajiandaa kutangaza ambavyo atarudisha imani katika idara ya ujasusi nchini humo kufuatia kufichuliwa kwa taarifa za idara hiyo na aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya kijasusi nchini humo Edward Snowden.

Chanzo: BBC


Alhamisi, Julai 19, 2012

Picha za Tukio la Tigo Ilivyokabidhi Fedha za TUCHANGE Kwa Hassan Majaar Trust




























HUU NI MPANGO WA MUDA MREFU ULIOUNDWA ILI KUBORESHA MAZINGIRA YA KUSOMA MASHULENI KWA KUGAWA MADAWATI KATIKA SHULE MBALIMBALI ZA WAHITAJI.

SHEREHE ZA MAKABIDHIANO ZILIHUDHURIWA NA MHESHIMIWA DK SHUKURU KAWAMBWA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI, WANACHAMA WA HMT, MWANDAMIZI MTENDAJI WA TIGO NA WAFANYAKAZI.

Picha zote kwa hisani ya: Prince Ema. Hebu tembelee H A P A