Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Oktoba 20, 2016

HII NDIO NDEGE HATARI ZAIDI YA KIVITA DUNIANI



B-2 bomber ndio ndege hatari zaidi ya kivita kuwahi kutengenezwa duniani, ndege hii hujulikana sana kwa jina la (Popo) kwa sababu inafanana na popo kiumbo. Ilianza kutengenezwa kipindi cha vita baridi na utengenezaji wake ulitunzwa kwa siri kubwa ambayo haijawahi kuvuja hadi leo. (B-2) ni kifupi cha B-2 Spirit Steath Bomber. Wakati wa kutengenezwa kwake wafanyakazi na wahusika wa kiwanda kilichokuwa kinaitengeneza ndege hii walichunguzwa na kulishwa kiapo cha kutotoa siri , walikuwa wakilindwa na vyombo vya Usalama vya Marekani kwa hali ya futi

Thomas Cavanaugh mmoja ya waafanyakazi alikamatwa kwa kujaribu kutoa siri hii kwa Urusi na alihukumiwa kifungo cha maisha jela japo mwaka 2001 allitolewa kwa msamaha wa PAROLE.
Hadi sasa B-2 ndio ndege vita ghari zaidi kuwahi kutengenezwa duniani, ndege hii inamilikiwa na Jeshi la Anga la Marekani (United States Air Defence Forces /USAF), teknlojia hii na ndege hizi hazijawahi kuuzwa kwa nchi yoyote hata washirika wa Marekani NATO hawajawahi kuuziwa. Kwa sababu ya ughali wake na gharama kubwa za kuiendesha Jeshi la Marekani linasadikiwa kuwa na ndege hizi 20 tu ambazo zinalindwa na kuendeshwa kwenye kambi ya Jeshi la anga ya Whiteman huko Missouri. Ndege moja ya B-2 iligharimu Jumla ya Dollar Billioni 2.1 (kwa rate ya dollar ya mwaka 1997) kwa ajili ya kutengezwa hadi kukamilika.



B-2 bomber haionekani kwenye rada yoyote ile kwa sababu imetengenezewa mfumo wa kuvuruga mawimbi yoyote. Ndege hii ina mfumo wa kunasa na kutambua kila kilichopo ardhini ikiwa huko angani, ina mfumo wa Kushambulia wa Kieletroniki wa kisasa zaidi.

Ndege hii ina uwezo mkubwa wa kubeba silaha za kushambulia ikiwemo mabomu, Makombora, na pia ina uwezo wa kubeba makombora ya masafa marefu ya Nyuklia. Ina uwezo wa kutembea km 12,000 bila kujazwa mafuta. Inaweza beba silaha zenye uzito wa tani 18.

Dege hili hatari lina uwezo wa kupaa futi 50,000 juu sawa na mita 15,000.Ndege hii pia inafanya kazi katika mazingira oyote ya hali a hewa na pia usiku na mchana bila kupata matatizo yoyote. Ina uwezo wa kubeba Mabomu 16 ya tani 1.1 kila moja ya Nyuklia na na mabomu 8 ya kilo 230 kila moja ya GPS guided bombs. Ina uwezo wa kupenya katika anga yoyote duniani hata kama ina ulinzi wa kuzuia bila kuonekana, na lengo la kutengenezwa kwa ndege hii ilikuwa ni kuweza kupenya anga ya Urusi na kushambulia maeneo muhimu.



Dege hili lilianza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye sura ya dunia mwaka 1989 wakati wa vita ya Ghuba japo halikuhisika kwenye mashambulizi yoyote, tokea kuzinduliwa kwake ndege hii inasemekana imefanya mashambuzi nchini Kosovo mwaka 1999 na kwenye vita ya kumuondoa Sadam Hussein nchini Iraq 2003 na mwaka 2011 kwenye operesheni Odyssey dawn. Inatarajiwa kutumiwa na Marekani kama Korea Kaskazini itaendelea na majaribio yake ya Nyuklia .

Ninaomba msomaji atambue kuwa kuna aina nyingi za ndege za kivita kama Bombers, Jet Fighters, Intercepters , Carriers n.k ila hapa leo ninajadili BOMBERS, siku nyingine nitaandika kuhusu Jet fighters.Baadae yatafuata Maelezo ya Tupolev Tu-160 almaarufu kwa jina la Blackjack kifaa kutoka Urusi.

Jumatano, Septemba 07, 2016

SHUKRANI MUNGU KWA ZAWADI HII YA MAISHA KTK SIKU YANGU YA KUZALIWA





LEO TAREHE 7 SEPTEMBA NI MAPENZI YA MUNGU KUNIFIKISHA KATIKA TAREHE NA MWEZI NILIOZALIWA NA SASA NIMETIMIZIA MIAKA ZAIDI. NICHUKUE FURSA HII KUWAKUMBUKA KWA KUWASHUKURU WALIOTENDA YALIYOTENDEKA.

Si mnakumbuka mapitio ya udogoni, kucheza pamoja, kukaa pamoja katika shida na raha wakati mwingine kupigana pale tulipoudhiana, ila tulisameheana kwa vile tulifundishwa upendo. Mara zote tuliamini kwamba japo tulizaliwa katika hali ya umasikini ila hatutakufa masikini, kwa vile si lengo la Mungu watu wake wataabike katika dhiki.


Kwa watoto yatima wote na wale waishio katika mazingira magumu;


..Nawapenda sana na daima nakuwa na amani sana kuwaona mkitabasamu na kufurahi, bila kujali matatizo mliyonayo maishani. Sio lengo la Mungu mteseke kwa kuwakosa wazazi ama ndugu mliowapenda na kuwategemea kwa namna moja ama nyingine. Mungu si mwanadamu hata tuseme anakosea kufanya maamuzi..ishini mkimtegemea Mwenyezi Mungu, baba wa mbinguni ajuaye idadi ya nywele kichwani nina hakika ipo siku majonzi yenu yatageuka kuwa Furaha..hamtanung'unika tena..nawapenda sana!


Nichukue fursa ya awali kumshukuru Mungu baba wa mbinguni kwa kunifanya moja kati ya viumbe alivyoviumba chini ya jua ..ni kwa neema yake tu kuwepo kwangu hadi leo hii kwani sina haki kuliko wale wote waliotangulia umautini. Namshukuru zaidi kwa kunipa ufahamu wa kuelewa mambo..asante Mungu kwa kunijaalia karama nyingi mbalimbali..naomba uniwezeshe kuzitumia vizuri kwa wengine!




Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani..nawapenda sana na daima napenda kuona mnaishi maisha ya ujana, yenye kila aina ya furaha..narudia kusema nawapenda sana na kuna kitu nitafanya kwa ajili yenu! 


Shukrani za kipekee ziwafikie walimu wangu tangu shule ya msingi hadi wakufunzi wa chuo kwa juhudi kubwa walizofanya za kunifuta ujinga..hakika nisingakuwa nilipo kama si jitihada zenu! Mungu akujaalieni kheri popote mlipo!


Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisiposhukuru majirani na waumini wenzangu kwa kuwa mentor, influencer na watu mlioni-jengea hekima ya hali ya juu! Niwaombe radhi wale tuliocharuana kwa sababu moja ama nyingine pale tulipopishana!


Wapo pia ambao siwezi kuwaacha japo majina ni mengi ila kazi yao ilinifanya niwaone kuwa role model wangu katika vipindi vya radio walivyokuwa wanarusha kupitia SAUTI YA UJERUMA, BBC SWAHILI, SAUTI YA AMERIKA, RADIO TANZANIA DSM, KBC SWAHILI NA ENGLISH SERVICE na nyingine nyiiingi popote zilipo. 


Mungu awajaalie miaka 900 kama enzi za Adamu na Hawa bila kujali mapungufu mliyonayo! Nyote mmechangia kupata zawadi nzuri sana ya maisha tangu kuzaliwa, kukua kwangu hadi kufikia leo ninapotimiza umri huu nilionao.

MUNGU WEWE NI MUWEZA WA VYOTE HAKIKA UNATUPENDA SANA. 

p>

Jumanne, Septemba 06, 2016

JE UMESHASIKIA KUHUSU SMARTPHONE MPYA?



Kutana na TURING ya CADENZA, hakuna smartphone duniani kama hii. Smartphone Hii ni mama na baba yao wote na 12GB ya RAM na 2 Snapdragan 830 SoCs.


Fikiria smartphone iliyo na Snapdragon mbili 830 SoCs , 12GB ya RAM , kamera ya mbele ni 12MP, na 60MP kwa kamera ya nyuma

Ndiyo! Hizi ni specs ya smartphone ijayo kutoka nyumba ya Turing ambayo ni maarufu kwa ushahidi wa kudukua smartphones.


Wakati wazalishaji wengine wanajaribu kushinikiza ivuke mipaka ya RAM 6GB , Turing Cadenza itakuwa ni mara mbili hasa kwamba itakuwa na RAM ya 12GB.


Turing mpya super smartphone itatolewa mwaka 2017 na kuitwa Turing Simu Cadenza.

UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME:



01. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshitua.

02. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendae.

03. Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajika.

04. Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiri.

05. Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaume.

06. Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kesho tena.

07. Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maisha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maisha.

08. Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizwe.

09. Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushiba.

10. Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake.. baadae hugombana nae yakishamrudia mwenyewe kwa siku 2 tu.

Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamke kama kuna nyingine ziongezee katika comments hapo chini ili kupeana elimu na maarifa kuhusu saikolojia.

Alhamisi, Septemba 01, 2016

NAMNA YA KUTAMBUA TABIA YA MTU



Hakuna anayependa kusahihishwa, kugombana au kukemewa mbele za watu, hii ndiyo tabia ya watu wajeuri na walio na tabia za kitukutu. Mara nyingine hudhani wanapata sifa. Wako watu wa jinsi hii ambao hawawezi kukugombeza au (kukupa vidonge vyako) mkiwa wawili peke yenu, watangoja watu wengine wawepo ndiyo waanze kubwabwaja, cha kufanya jiepushe nao.

Kwa kule kukimbiwa na marafiki, na kuwa mpweke, huongeza tabia za kitukutu na kijeuri na hii huwafanya watu hawa kutambulika haraka na kiurahisi zaidi.


Zifuatazo ni alama zitakazokutambulisha mtu jeuri na mtukutu:


a) Alama za kimaneno

Mara kwa mara hupendelea kusema maneno haya vinywani mwao.
Nakwambia bora unge…"
Wewe sichochote, silolote…"
Nakwambia, lazima u..."
Fanya vile ninavyokuambia mimi…"
Nataka u..."
Wewe endelea tu tutaona..."


b) Alama za kimwili

Hupendelea kusimama wima
Huwa wenye pozi kavu, ngumu (still and rigid pause)
Hupenda kukunja mikono
Hupenda kupayuka au kupigia wengine kelele
Hupenda kuwanyooshea wengine vidole.
Hupenda kuwazodoa wengine na vidole (hawezi kukuelekeza hadi kidole chake kikusukume)
Hupenda kupiga au kugonga meza na viti akizungumza


2. Watu wapole, waliotayari kukubali kushuka (Submissive)

Hawa ni watu wanaopenda kujitoa sadaka kwa ajili ya manufaa ya wengine. Kwa hali hii ni rahisi watu hawa kujikuta wanatumiwa vibaya na watu wengine hasa wale wajeuri na watukutu tulio waangalia awali.


Mara nyingi watu walio wapole na wanaokubali kushuka hupenda kuwatia moyo wengine wawe kama wao. Katika vizazi vilivyopita, wanawake walitegemewa zaidi kuwa watu wa kundi hili. Ni mabadiliko ya maisha na ya jamii ya leo ambayo yamemfanya hata mwanamke kuwa mjeuri na mshindani tofauti na jamii za awali.

Kwa upande mwingine mfumo wa maisha wa vizazi vya nyuma ulimweka chini mwanamke na kuzuia maendeleo yake hasa katika kujiendelezea vipawa alivyonavyo kwa vigezo tu kwamba yeye ni wakukubali chochote na wakati wowote sasa tunayaona mabadiliko kwa kiasi fulani.


Mara kwa mara watu wapole, na waliotayari kushuka wamekuwa wenye hisia za kinyonge na kutengwa, wakijihisi kutokuwa salama wakati mwingi. Kujijali, kujipenda na kujithamini kwa watu hawa siyo kwa kudumu, bali kunakuwa na nyakati za kuyumbayumba kutokana na mazingira. Hawa siyo watu wenye ujasiri ndani yao wenyewe na hata katika vile wavifanyavyo.


Mara mtu wa kundi hili anapokutana na mtu mjeuri na mtukutu, hofu na ujasiri wake hupungua sana, na anaweza kukubali kupingwa hata kama alikuwa ana haki. Kwa sababu mara nyingi watu wa jinsi hii wanajua kuwa kwa upole wao watu wengi wamekuwa wakiwatumia na kuwachezea, hii imewafanya wawe ni watu wenye vihasira vya mara kwa mara.


Kwa sababu wameunganishwa na hisia zao zaidi, ni rahisi wao kuzielezea hisia zao kwa mtu mwingine, hata kama hisia zao ni za kujutia kile walicho kifanya wenyewe. Mara nyingi husikia amani kwa yale wanayofanya au kuyaamua.


Ingawa mara nyingine mambo huwaendela tofauti na walivyopanga, watu hawa hufahamu kuwa hawanabudi kukubali kosa au na kuwa tayari kujifunza kutokana na yale makosa.


Mambo yanapowaendea vema hupenda kujisifia na kujiona walio juu. Mara nyingine misimamo yao huwashawishi na kuwavutia wengine watazame kama wao, sio watu wanaopenda kuwatumia wengine vibaya (being manipulative) kama vile kuwasema au kuwasengenya wengine, hii huwafanya kuwa na wafuasi au washabiki wengi zaidi.


Kule kujiamini kwao na kuwa na ujasiri hupunguza sana msongo wa mawazo maishani mwao na hii huwasaidia kuelekeza nishati na nguvu zao zote katika kufikia malengo waliojiwekea.


Mara kwa mara sio watu wenye mabadiliko ya hisia (change of attitude) na hii hufanya mahusiano yao na wengine kuwa yasiyoyumba na mawasiliano baina yao na wengine huwa wazi, sio watu wakuficha wanachokiona, uwazi walionao kuwaweka huru.

Hujisikia vema hujipenda na kujithamini muda mwingi. Hujijengea hisia za usalama na imani kwa sababu ya mawasiliano bora walionayo na wale wanaowazunguka, hii pia husababishwa na wao kuelewa fika wajibu wao na wajibu wa wengine pia.


Ingawa wanaweza kuwa wabishi, lakini huheshimu misimamo ya wengine na kupenda ya kwao iheshimiwe pia na hii huwafanya kuwa na ushirika na wale wanaowazunguka. Mara nyingi ni wazuri katika kuwatia wengine moyo kujitahidi zaidi.


Alam za kuwatambua:

Alama za maneno

Nahisi……. Najisikia kuu……………"
Ningependa kuu…………"
Wewe unaonaje hapa/mawazo yako nini………….."
Unadhani njia gani bora kulishuhulikia hili ……….."
Nafikiri……….."
Hembu tu…………….."


Alama za kimwili

Hupenda kuwa wima ila wenye pozi laini (relaxed stance)
Huangalia kijasiri na kuangalia usoni (kukodoa macho).
Huwa na hisia za upole, kujitawala na kujimiliki wenyewe

Kwa vyovyote vile, mara zote unapokutana na mtu mwenye tabia yeyote kati ya hizi tatu kumbuka una haki ya kufanya yafuatayo;

Jifunze kuelezea hisia zako njema (usiogopoe au kuona aibu kwakuwa hutokuwa umejitendea haki)
Jifunze kuzielezea hisia zako mbaya au za hasira, kamwe usifunike. Mfano; "Sipendi kabisa unavyokula"
Jifunze kusema hapana, Mfano; "Hapana sitaweza kufika leo"

Toa wazo la kweli, usipake watu mafuta kwa mgongo wa chupa. Mfano; "Mimi siliafiki hilo jambo hata kidogo"
Kiri kuwa umekasirika, hasa pale ambapo haunabudi kukasirika.

Mfano: "Kweli umeniudhi sana baada ya kusema hayo maneno". Usitoe tabasamu la mamba tu, kutabasamu wakati ndani yako unahisi kuungua moto.


Credit: MziziMkavu

Jumanne, Agosti 09, 2016

Taarifa...UZINDUZI WA TRENI STESHENI PUGU DAR ES SALAAM.

 

Leo kampuni ya reli Tanzania TRL  kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo CHAMA CHA KUTETEA ABIRIA (Chakua), kwa pamoja tumezinduwa treni ya abiria itakayofanya safari zake kuanzia stesheni ya dsm kwenda pugu.

 

Katibu idara ya reli,, Godfrey Mali, kulia,, Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki, Wilson Sylvester na muheshimiwa waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa wakiwa kwenye uzinduzi wa treni ya abiria ya kwenda pugu leo.
 

 Katika Uzinduzi hua Chama Cha Kutetea Abiria (Chakua) iliwakilishwa na mkurugenzi wa kanda ya mashariki, Wilson na katibu idara ya reli, Godfrey Mali.



 Pongezi kwa Katibu mkuu idara ya reli, hiyo ni kazi nzuri sana.



 Ni safari  ambayo itaanza saa 10:45 alfajiri kwenda pugu tripu ya kwanza na tripu ya mwisho 4:20 asubuhi hiyo routi ya asubuhi.

Routi nyingine itaanza saa 09 :55 alasiri kuekea pugu mwisho wa routi za jioni ni saa 4:15 usiku. Nauli kwa mkubwa Tsh 400 mwanafunzi Tsh 100. Hizi zitakuwa nauli za majaribio mpaka hapo sumatra watakapotoa muongozo wa nauli.


Uzinduzi wa treni ya abiria ya kwenda Gongolamboto Pugu  tayari umezindiliwa na walielekea pugu  viongozi mbali mbali akiwemo waziri wa uchukuzi pia mea wa jiji halikadhalika   mkuu wa mkoa,, na viongozi wa shirika la reli Tanzania.


 Kama unavyoona kwenye Picha hapo Juu Mh.Makame Mbarawa akiwa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda.

 
 Kesho (Jumatano) Chakua itafanya mazungumzo na mkurugenzi mtendaji wa shirika la reli Tanzania TRL  ofisini kwake makao makuu ya reli tanzania kuanzia saa tisa kamili.


CARL GUGASIAN - The Friday Night Bank Robber.



Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17.

Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'! Muhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber)

Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'!

Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na FBI washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza kumzuia au kumkamata.

Mbinu, weledi na nidhamu aliyokuwa nayo na kutumia kutekeleza matukio yake yalikuwa ni siri na kitendawili mpaka pale alipokamatwa na kuamua kuwasimulia FBI ili kujaribu kuwashawishi kumpunguzia adhabu ya kifungo.. Na hii ni historia yake 'kwa kifupi' tu

ALIWEKA DHAMIRA AWE "MUHALIFU MWELEDI"

Akiwa na miaka 15 Carl alitekeleza tukio lake la kwanza la ujambazi ambapo alijaribu kuiba fedha katika candy store bila mafanikio na alipigwa risasi tumboni na kukamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa katika jela ya watoto ya Camp Hill kwa miezi 18.

Baada ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu mwenye weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio na hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo (majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha, ajue namna ya kujihami (self defense) na namna atakavyo toroka na fedha..

Baada ya kuweka dhamira hiyo Carl akachukua hatua ya kwanza na alichofanya ilikuwa ni kujiunga na Chuo kikuu cha Villanova ambapo alisomea Uhandisi wa umeme. Akiwa chuoni alitumia mwanya huo kujiunga na programu maalum ya jeshi la marekani kwa ajili ya kurecruit vijana walioko chuoni! Baada ya kumaliza Chuo akaenda kutumikia jeshi kwa muda mfupi kituo cha Fort Bragg na akiwa huko akapata mafunzo maalumu ya kijeshi (Special Forces and tactical weapons training)

Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi Carl akarudi Chuo kusoma masters degree ya System Analysis na alipomaliza masters degree akafanya mafunzo ya awali kwa ajili ya shahada ya uzamivu katika Statistics.

Pia mtaani alipokuwa anaishi alijiunga na kituo cha kufundisha mafunzo ya kujihami (karate and judo) ambapo alifanikiwa kupata mkanda mweusi (third degree black belt)

Baada ya kufanikiwa kufanya maandalizi yote hayo na kupata kila aina ya mafunzo na uzoefu aliyohitaji ili kuwa 'muhalifu wa daraja la kwanza' sasa ulikuwa ni wakati kwake kupita kila benki kukomba hela na kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakujapata kuwepo na itachukua miaka mingi kutokea muhalifu professional kama yeye Carl 'the Friday night bank robber'..

#1

MAANDALIZI KABLA YA TUKIO

Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio! Carl alikuwa anatumia had I miezi kadhaa katika kupanga utekelezaji wa tukio moja tu..

Kwanza kabisa Carl ali scout bank zilizopo katika miji midogo. Baada ya kupata orodha ya benki katika miji kadhaa midogo then Carl aliangalia kati ya bank hizo ni bank gani haziko katikati ya mji (kwa maana kwamba ziko pembezoni/nje ya mji). Kisha Carl aliichagua bank moja wapo kati ya hizo na bank ambayo inakuwa haiko karibu sana na makazi ya watu au iko karibu na msitu basi bank hiyo anaipa kioaumbele katika orodha yake..

Baada ya kuamua ni bank gani atafanya tukio, Carl alianza tafiti juu ya tukio lenyewe atakavyolitekeleza... Kwanza kabisa Carl alianza kwa kusoma mandhari yanayozunguka bank na interest yake kubwa inaelezwa kuwa alitafiti zaidi msitu ambao unakuwa karibia na bank.. Inaelezwa kuwa Carl angeutembelea msitu huo na kuukagua nukta baada ya nukta, haijalishi ni muda gani angetumia mpaka kumaliza kuukagua!
Inaelezwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kujua ni maeneo gani ya msitu ambapo watu huwa wanamazoea ya kupita au kutembelea, ni eneo gani la msitu limejificha zaidi, ni upande gani wa msitu unakuwa rahisi kuifikia barabara, ni eneo gani la msitu lina umajimaji na eneo gani ni kavu na kadhalika na kadhalika.. Inaelezwa kuwa Carl angeutafiti huo msitu na kuufahamu kuliko hata wenyeji wa eneo hilo husika.. Angeufahamu msitu nukta kwa nukta!

Baada ya kuufanyia tafiti msitu, inaelezwa kuwa Carl alikuwa anageukia kuitafiti bank yenyewe na wafanya kazi wake.. Kuhusu bank, angetafiti je hiyo bank inafungwa na kufunguliwa saa ngapi, ni siku zipi huwa wanachelewa kufunga, ni siku gani wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha n.k! Kisha akimaliza hapo anageukia kuwatafiti wafanyakaxi wa bank husika.. Hapa alitafiti kuhusu 'shifti' zao za kazini, nanj ni teller, nani ni manager na pia kitu kingine cha msingi alijitahidi kuwasoma personality zao..

Baada ya kumaliza kufanya 'tafiti' zake Carl alienda hatua ya pili ya maandalizi ambapo ilikuwa ni kuandaa 'makazi na stoo' yake ya muda katika msitu uliopo karibu na bank ambapo alichimba handaki dogo kwa ustadi mkubwa na kulificha kabisa kwa juu mtu asiweze kujua kwa namna yoyote ile.. Moja ya wapelelezi ambao walihusika kufanikisha kumkamata Carl anaeleza Bw. Carr anaeleza kuwa siku ambayo walifanikiwa kugundua na kuliona handani mojawapo ambalo lilichimbbwa na Carl walistaajabu (kumbuka Carl alikuwa na zaidi ya mahandaki 30 sehemu tofauti tofauti za nchi ya marekani)! Inaelezwa kuwa kinachostaajabisha kuhusu mahandaki ya Carl ni jinsi yalivyo chimbwa kiustadi na kujengewa kwa ndani kwa vitofali vidogo vidogo.. Pia handaki lilikuwa linampangilio wa hali ya juu wa kiwango cha kijeshi (military precision). Ndani ya handaki kulikuwa na kila kitu ambacho angekihitaji, silaha, nyaraka za 'research', kifurushi cha kujikimu (survival kit), madawa ya dharura (first aid kit), vinyago vya kuficha sura (masks), fedha taslimu, majarida ya mazoezi ya kawaida na kijeshi na vitu vingine vingi..

Baada ya kumaliza maandalizi haya ya msingi Carl alijichimbia katika maktaba ya umma ya Philadelphia ambapo ndio alipafanya kama ofisi yake kwani inaelezwa kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia muda mwingi hapo akifanya 'tafiti' na angekuwa hapo kwa wiki kadhaa ili ku-fainalize mpango wake na kufanya conclusion ya jinsi atakavyotekeleza tukio lenyewe..

#2

UTEKELEZAJI WA TUKIO

Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema!
Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la 'The Friday Night bank robber'..
Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza kipindi cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika Masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha kuwa ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.. Lakini pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..

Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka 'harufu' kwenye nyumba zote zilizo karibu na bank ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu kutafuta trail ya alikoelekea!

Now; siku ambayo Carl alikuwa anafanya tukio alivaa kinyago cha kutisha usoni ambacho kili-fit sawa sawa kabisa ili kuficha ngozi yake na! Pia alivaa manguo mengi ili kuleta muonekano kwamba ni mnene.. Na alikuwa akiingia ndani ya bank alitembea dizaini kama amechuchumaa mfano wa Kaa (crab)! Vitu vyote hivi alivyovifanya watu walihisi labda alikuwa na matatizo ya akili lakini hawakujua kuwa alivifanya kwa kusudi kabisa.. Alivaa kinyago cha kutisha ili kuleta effect ya kuogofya na kuficha tone ya ngozi yake, pia alivaa manguo mengi ili kuficha body size, na alitembea kama kaa akiwa kama amechuchumaa ili kuficha height!! Hii ilimsaidia sana kwani kwa miaka 30 FBI walishindwa kung'amua mtu wanayemtafuta alikuwa wa size gani, height gani au skin color ipi???

#3
Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia..
Akishavamia bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimuangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ma-teller na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimuangalie na kabla hawajang'amua kinachoendelea Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya bank na kutokomea katika msitu ulio karibu..
Inaelezwa kuwa katika matukio yake yote aliyatekeleza ndani ya muda usiozidi dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari amevamia, amekomba hela na ameshatokomea msituni..

Carl anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu alikuwa anakimbia kwa dakika kadhaa kama kumi hivi mpaka mahala ambapo anakuwa ameficha baisikeli kisha anaendesha mpaka ndani ndani kabisa ya msitu kulipo na handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha alizoiba, masks, nguo, gloves etc kisha anavaa nguo nyingine za kawaida anaendesha baisikeli anaondoka! Carl anasema kuwa ataendesha baisikeli kwa muda wa kama dakika ishirini au zaidi mpaka upande wa pili wa msitu ambapo kuna barabara na hapo kunakuwa kuna gari amepaki linamsubiri.. then anawek baisikeli ndani ya gari anaendesha kama raia wa kawaida na kuelekea nyumbani..

Carl anasema alikuwa anacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio la ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua 'hela zake'... Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza 'tafiti' kwa ajili ya tukio linalofuata..

#4

KUKAMATWA NA MAZINGAOMBWE YA HUKUMU

Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno!
Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa.. Baada ya kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao wakashauri vipelekwe polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani.. Polisi walipoifuatilia ile ramani ikawqpeleka moja kwa moja kwenye handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana na vitu vilivyokutwa ndani ya handaki hilo polisi wakapata wasiwasi kuwa inawezekana wanadeal na ishu serious kuliko uwezo wao hivyo wakawataarifu FBI! Baada ya FBI kuwasili iliwachukua masaa kadhaa tu kung'amua kuwa vitu hivyo vinahusiana moja kwa moja na Jambazi wanayemtafuta kwa miaka 30, The Friday night bank robber.

FBI walitumia alama za vidole walizozikuta kwenye ile handaki na pia walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo cha mafunzo ya karate kumtrack down Carl mpaka wakampata.
Siku Carl anakamatwa alikutwa "ofisini kwake" Maktaba ya Philadelphia Free Library akiwa anafanya "tafiti"

Baada ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani ilikuwa ni dhahiri kuwa Carl atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo uwezekano wa kupata parole kutokana na mashitaka yanayomkabili lakini mwisho wa siku Carl alikubaliana deal na FBI kuwa awaeleze nukta kwa nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na FBI kutengeneza programu maalum kuwasaidia maafisa wa FBI kutambua namna ya kuwabaini 'serial criminals', na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo perfect.!
Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..

Hivyo basi ikifika 2021 Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa huko gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na ameendeleza desturi yake ya kupenda mazoezi hivyo yuko katika afya njema sana na wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salimini.

Alhamisi, Juni 23, 2016

SOMA KITABU CHA UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI


Kwa mjibu wa nyaraka za MOSSAD, CIA, RAW na FSB juu ya elimu ihusuyo "kiwango cha hali ya hatari katika eneo la kiraia" ambacho hupimwa kwa kipimo kiitwacho Def Cond, inasema, "Pale majadiliano ya meza yanaposhinwa kuleta jibu chanya, wanamjadala hususia meza, ambapo katika kipimo husomeka Def Cond 0001".

Ikitokea kuwa hata huko walikoamua wanamjadala hao kupeleka hisia zao nako kukazuiwa, hasira ya wanamjadala hao huongezeka na kuwa Def Cond 0002.

Hatua ya mwisho ya wanamjadala hawa huwa ni kwenda kwenye mahakama ya umma, hapa kipimo husomeka Def Cond 0003.

Hiki ni kipimo kikubwa katika medani ya kiusalama kwa mambo ya ndani, ambapo matokeo yake shughuli katika jamii husimama, serikali hushindwa kutawala wala kuongoza. Katika lugha nyingine huitwa mgogoro wa ndani,kisiasa,kikatiba nk...

Zingatia hali hii haizai vita, kwani ili vita kamili ya ndani izaliwe lazima hali ya hatari isomeki Def Cond 0006. Na ili vita kamili izaliwe katika ya taifa na taifa lazima hali ya hatari isomeke Def Cond 0008.

Mzigo ukiwa dukani tayari kwa mauzo,
Bei ya rejareja 30,000/=
Bei ya Jumla 25,000/=

Fika Dukani House of Wisdom Bookshop lililopo Dar es Salaam, Posta, mtaa wa Samora jengo la NHC Ghorofa ya kwanza.

Kwa walio nje ya Jiji la Dar wanaweza kununua kwa M-Pesa +255755865544 Yericko Nyerere. Utaletewa mahali ulipo kwa njia ya Posta.

PIA KWA MAUZO YA JUMLA LIPA KUPITIA BANK YA CRDB
AC NO: 0152241955000.
Name: YERICKO YOHANESY NYERERE.
BRANCH NAME: HOLAND HOUSE
BRANCH CODE: 3319
BANK NAME: CRDB BANK PLC
SWIFT CODE: CORUTZTZ
CURRENCY: TZS.

WANAKARIBISHWA WAFANYABIASHARA WALIOTAYARI KUWEKEZA KATIKA BIASHARA HII.


Wasiliana kwa simu: +255 715 865 544

Jumapili, Juni 12, 2016

UMUHIMU WA ELIMU YA MUZIKI NA ELIMU YA UENDESHAJI WA MUZIKI

Photo By: www.borgenmagazine.com


Asilimia kubwa ya wanamuziki hapa Tanzania wanapiga muziki bila ya kuwa na elimu yoyote ya awali ya muziki, hili si jambo la ajabu kwani hali hii iko sehemu nyingi duniani, lakini kitu ambacho ni wazi kinakosekana ni elimu kuhusu utendaji wa taasnia ya muziki. 

Pamoja na kauli nyingi nzuri za viongozi wa Nchi kusifu sanaa hii na wasanii wa sanaa hii lakini ni nadra kusikia kiongozi akiongelea matayarisho rasmi katika sanaa hii na kwa kweli hata katika sanaa nyingine.

Kumekuwepo na ombwe la elimu ya uendeshaji wa tasnia ya sanaa. Ombwe la elimu kwa wataalamu ambao huwezesha wasanii kufika walipo, kuwaendeleza kukaa walipo, kulinda haki za kimaslahi za wasanii na hata kuwapa maelekezo ya kujitayarisha kwa wakati ambapo umaarufu utakuwa umekwisha.

Tasnia ya muziki huhiyaji shule za kujifunza muziki, vyuo vya uongozi wa muziki, au kozi fupi ambapo taaluma za umeneja, uproducer, upublisher, usambazaji, ujuzi wa sheria za hakimiliki na watendaji wengine wa aina hiyo hupata elimu, ujuzi wa sheria za hakimiliki na watendaji wengine wa aina hiyo hupata elimu. Kukosekana kwa elimu hii kumefanya watu kujifunza kwa vitendo kwa kujaribu na hata kubahatisha hivyo mara chache kufanikiwa.

Kukosa elimu sahihi kumewafanya wasanii wengine wenye uwezo mkubwa kupotea kwenye taaluma na wengine kujikuta wakishindwa kuingia kwenye ulingo huu japo uwezo wanao. Pia kumetoa nafasi ya wasio na uwezo kujikita katika uongozi wa sanaa na kuleta matatizo makubwa kwenye sanaa, aidha kwa kuaminika kuwa wanatoa ushauri sahii na hivyo maamuzi yenye hasara kubwa kufanyika. 

Pamoja na mafanikio yaliyoonekana taifa linakwenda kihobela hobela katika tasnia ya sanaa ya muziki. Ushahidi wa wazi upo kwa kupata elimu ya muziki kuanzia umri mdogo kuna faida nyingi sana. Kwanza humuwezesha motto kukuza sehemu ya ubongo ambayo huhusika na hesabu na pia kukuza uwezo wake wa kutafakari. 

Inaeleweka kuwa ubongo huendelea kupata maendeleo miaka mingi baada ya kuzaliwa, hivyo muziki huendelea kuboresha upande wa kushoto wa ubongo ambao ndio huhusika na ujuzi wa lugha na tafakari na hesabu. Muziki husaidia sana watoto kukumbuka mambo mbalimbali, ndio maana hata matangazo ya biashara ya kawaida husindikizwa na muziki ili kukaa katika kumbukumbu kwa urahisi. Kwa watoto muziki husaidia sana katika kazi zao za elimu ya kila siku.

Wasanii waliopata elimu sahihi huwa na uwezo wa kubuni majibu mbalimbali kwa tatizo moja, hii unaweza kuiona kwa mfano ukiwapa wanamuziki kumi semina kuhusu jambo. Kwa mfano: Ukimwi kasha ukawaambia watunge wimbo kuhusu elimu waliyopewa, utashangaa watakuja na tungo tofauti za mtizamo mpya kabisa wa kuelezea elimu hiyo waliyoipata.

Elimu ya muziki hufungua ubongo kuruhusu kuachana na mawazo mengi yaliyopita na kujaribu mawazo mapya. Wasanii kote duniani huwa waanzilishi wa mambo mengi ikiwemo mitindo ya nguo, uvaaji na mambo mengi katika maisha kutokana na ubongo wao kuwa na uwezo wa kuruhusu kufikiria vitu katika mtazamo mpya.

Elimu ya awali ya muziki imeonesha kuwa wanafunzi wa elimu hii hfanya vizuri zaidi katika masomo mengine tofauti sana na mawazo ya kawaida kuwa muziki huharibu watoto. Katika muziki, kosa huwa ni kosa, ukikosea beat, usipotune chombo chako, ukiimba vibaya ni kosa hakuna mbadala, sauti ikiwa juu mno, au chini mno na kadhalika, na wanamuziki hulazimika kurudia tena na tena mpaka atakapopata kitu sahihi na kabisa.

Elimu hii ikiwa kichani kwa watoto toka umri mdogo humsaidia katika kuboresha mambo yake mengine na kuyafanya vizuri zaidi kila mara. Elimu ya awali ya muziki humjenga motto kujua kufanya kazi na watu wengine kama kundi, kutokana na kuelewa kuwa katika muziki watu wengi hutegemeana ili kuleta ubora katika wimbo mmoja, hii huwasaidia katika maisha kila siku.

Kuna mengi yanayopatikana katika elimu bora ya sanaa, pia kubwa likiwa ni kwenda sambamba kitaaluma na ulimwengu, kuna bahati mbaya sana kwa vijana wetu kutaka kuingia katika soko la muziki duniani lakini bila kuwa na matayarisho yanayostahili kufikia huko, wengi ni ndoto zao hazitatimia kwani elimu ya kufikia huko hawana.

Ni wazi kuna haja ya kuanza kutoa elimu ya sanaa kuanzia ngazi ya shule za awali, kuna haja sasa ya kuwasaidia wanamuziki walioko kwenye taaluma kupata elimu ya haki zao. 

Ni wasanii wangapi wanaojua kuwa katika kila tungo, kuna haki tofauti kumi wanazostahili? 

Watunzi wangapi wanajua wana haki kwa kazi zao kutumika kibiashara? 

Wakati viongozi wakisifia wasanii wan je wakumbuke kuwa kinachowafanya wawe na mafanikio ni kutumia kila njia sahihi kukamua mapato kutoka kwenye haki zao hizo zinazolindwa kisheria.
  
Makala hii ni kwa msaada wa John Kitime

Ijumaa, Juni 03, 2016

UGONJWA WA MKAZO (STRESS)

Photo Credit By:  http://luxuryspablog.com/


Ni ukweli usiopingika kwamba mwanadamu anakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi, kiafya, kijamii na kadhalika. 

Changamoto zote hizo huongezeka zaidi pindi mwadamu anapofikia umri wa utu uzima, kwa maana ya umri wa kubebeshwa majukumu ya kimaisha, kama vile kusaidia wanafamilia, wanaukoo na jamii kiujumla. Hata hivyo, changamoto kubwa za kiafya zinazomkabili mwanadamu huyu, karibu kote ulimwenguni ni ugonjwa wa Mkazo, ambao kitaalamu wanaita Stress pamoja na kupanda kwa Shinikizo la Damu, kitaalamu Hypertension. 

Baadhi ya vitu vinavyosababisha ugonjwa huu wa Mkazo kwa mujibu wa wataalamu wa afya, ni pamoja na hofu au wasiwasi kuhusiana na jambo lolote linaloweza kumkumba mwanadamu, hasa ukosefu wa fedha mfukoni au kutamani utajiri ambao hajui ataupataje. 

 Lakini pia, ratiba za shughuli za kiuchumi na huduma zenye mambo mengi yasiyokuwa na mpangilio huweza kumsababisha ugonjwa huo binadamu, pamoja na ugomvi usiokwisha ndani ya familia, kukumbana na matukio ya kutisha kama vile ya ugaidi na kadhalika.  

Watu wengi ulimwenguni wamezoea kutumia kilevi, kama vile pombe, tumbaku na vileo vingine ili kukabiliana na maradhi hayo ya Mkazo na kupanda kwa Shinikizo la Damu. Hali hiyo, inatokana na wengi wao hao kushidwa hata kula vizuri, huku baadhi yao wakilazimika kutumia muda mwingi kuangalia matukio katika televisheni au kutumia vifaa vya kielektroniki kama vile kompyuta na simu za mkononi kwa muda mrefu ili tu kujisahaulisha na msongo wa mawazo kichwani. 

Mkazo na Kupanda kwa Shinikizo la Damu, ni vitu vinavyoendana sana katika maisha ya mwanadamu, ndiyo maana ili kudhibiti magonjwa hayo, mhusika hushauriwa kudhibiti kwanza hali yake ya Mkazo.

Kituo kimoja cha Matibabu ya Akili kilichoko nchini Uingereza, zinabainisha kwamba katika kila kundi la watu watano ulimwenguni, basi mtu mmoja hukumbwa na maradhi ya Mkazo unaotokana na mazingira ya mahali pake pa kazi. Kwa mujibu wa taarifa hizo, kushindwa kukabiliana na hali hiyo ya Mkazo mwingi, mtu mmoja kati ya watu wanne, hujikuta akilia peke yake bila kupigwa wala kukasirishwa na yeyote, akiwa kazini kwake. 

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mwanadamu ameumbwa kwa njia ya kipekee kabisa, kwa kuwekewa mifumo mbalimbali mwilini inayofanya kazi mbalimbali usiku na mchana ili tu kumweka vizuri na salama katika maisha yake. 

Kwa mfano, mwanadamu amewekewa mfumo wa hisia za dharura, ambao ni kichochea kikuu cha mwili pindi mwanadamu huyu anapopatwa na Mkazo mwingi. Vichocheo hivyo, ndivyo vinavyomfanya binadamu huyo anapopatwa na hali hiyo aweze kupumua haraka, moyo wake uende mbio na kadhalika hali inayochangia kuongezeka kwa Shinikizo la Damu. 

Aidha, vichocheo hivyo, ndivyo huongeza chembe za damu na sukari kwenye damu. Kwa kawaida, mfumo huo wa hisia za dharura unafanya kazi kubwa ya kumtayarisha mwanadamu kukabiliana na kitu chochote au mtu yeyote anayemsababishia hali hiyo ya Mkazo. 

Hata hivyo, baada ya jambo hilo linalosababisha Mkazo kupita, mwili hurudi katika hali yake ya kawaida, ingawa baadhi ya wataalamu wanaweka wazi kuwa endapo hali hiyo ya hisia za dharura inajirudia mara kwa mara, mtu anaweza akakumbwa na ugonjwa mwingine wa hofu au wasiwasi, ambao kitaalamu unajulikana kama 'Anxiety Disorder'. 

 Kwa hiyo, kwa kila binadamu awaye yeyote yule, ni muhimu kujifunza mbinu za kukabiliana na maradhi hayo Mkazo na kupanda kwa Shinikizo la Damu. Kwa sasa zipo njia kuu rahisi 10 za kukabiliana na hali hiyo. 

mediaphotos/Getty Images


Mosi, ni kuhakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala usingizi, Kutopata usingizi wa kutosha kunaathiri hisia, akili, kiwango cha nishati mwilini pamoja na afya kiujumla. Wataalamu wa afya wanashauri mtu mzima apate usingizi wa walau saa nane (8) katika kila saa 24 za siku. 

 Pili, katika kujipangia mipango ya maisha, unashauriwa kutanguliza mambo muhimu yanayokuwezesha kuishi maisha yenye kiasi. Kwa maneno mengine, binadamu anatakiwa kufikiri jinsi ya kurahisisha maisha yake, pengine kwa kupunguza gharama za maisha pamoja na kupunguza muda anaotumia kufanya kazi kazini kwake. 

Tatu, jifunze mbinu za kupumzisha mwili. Kutafakari kwa kina (Meditation), mazoezi ya kuvuta pumzi na yoga ni njia imara za kuondoa Mkazo. 

 Nne, mtu inampasa kuimarisha mtandao wake wa kijamii. Kujiunga na vikundi mbalimbali kama vile vya masomo, kutoa misaada kama vile kwa watoto, yatima na wajane au vikundi vya wajasiriamali. Mwaka 2008, baadhi ya watafiti raia wa Uingereza waligundua njia moja ya kubaki imara pindi mtu anapopatwa na Mkazo. Katika utafiti wao, wanasema moja ya njia ya kubakia imara, ni kujitolea kuwasaidia wengine kwa njia fulani fulani. 

Tano, mtu inampasa kujitahidi kuelewa vizuri hisia za wengine, kitu kitakachomsaidia kupunguza hasira, na wakati huo huo awe mwepesi kusamehe kwa kuwa ni jambo jema pia kimaisha. Utafiti uliofanywa mwaka 2001 nchini Uingereza, ulionyesha kwamba mtu anapokuwa na kinyongo fulani kwa mtu, humsababishia kupanda kwa Shinikizo la Damu pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo. Hali hiyo, kwa mujibu wa utafiti huo, inaweza kuondolewa kwa mtu kuwa mwepesi wa kusamehe haraka. 

Sita, kwa gharama yoyote, mtu anatakiwa kujiepusha na ugomvi wa aina yoyote ile. Kugombana na wengine kunaweza kumletea au kumsababishia mtu Mkazo mwingi. Mtu anapokuchokoza jitahidi kutulia, usimwage ugali kwa kuwa yeye kamwaga mboga. Inashauriwa kujitenga naye kwa kukaa faragha, hivyo kusuluhisha mambo kwa hekima na busara nyingi. 

Saba, jipangie ratiba ya matumizi ya muda kwa kuandaa muda wa kutatua matatizo ya familia na ya kazini, kwa kutumia mbinu bora za makubaliano. Aidha, mtu anaweza akatunza muda wake wa kazi na familia kwa ufanisi hivyo kupunguza kiwango cha Mkazo kwake. 

Nane, inampasa mtu ajitahidi kupunguza hali zitakazomwongezea Mkazo kadri awezavyo, kwa kutoruhusu hali zenye kuongeza Mkazo. Kwa mfano, kujiepusha kuwaza mambo mabaya yanayoweza kutokea na kuchota hisia zake. 

Tisa ni kuhakikisha mwili mzima unatunzwa. Baada ya kazi nzito, jitahidi kuukanda mwili kwa maji ya uvuguvugu, kabla ya kula chakula. Mazoezi ya kutembea na kusikiliza muziki unaoifurahisha nafsi yako ni muhimu pia. 10, ni kuondokana na woga wa kuomba msaada kwa jamaa na marafiki au majirani. 

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba kuzungumza na marafiki au watu wa familia kuhusu hali inayokupata, husaidia kuondoa ugonjwa wa Mkazo. Hata hivyo, pamoja na njia zote hizo 10 rahisi, inashauriwa na wataalamu wa akili na mifumo ya miili kwamba endapo Mkazo na hali ya wasiwasi itaendelea, ni muhimu kutafuta msaada zaidi kwa Daktari, ikiwezekana upatiwe dawa za kutibu hali hiyo.