Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Desemba 02, 2013

WAZO LA MELI KUBWA ILIYO JIJI LINALOTEMBEA


Moja kati ya kampuni nyiiingi iliyopo Florida nchini Marekani imekuja na wazo la kujenga meli iitwayo ‘Freedom Ship’ itakayokuwa na kila kitu cha kuifanya iwe jiji linaloelea juu ya maji.
 
meli-pic1
 
Wabunifu wa wazo la meli hiyo wametoa michoro ya picha za meli hiyo itakavyokuwa pindi itakapokamilika.
 
Roger M Gooch, ambaye ni mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni ya Freedom Ship International ambao ndio wenye mradi huo, amesema hiyo meli itakuwa ndio meli kubwa kuwahi kujengwa, iliyo na muonekano wa jiji la kwanza linaloelea kwenye maji.

meli-pic6
 
Kutakuwa na uwanja wa ndege juu ya meli hiyo, uwanja utakaowezesha ndege kuruka na kutua wakati wakati meli inatembea

Mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni hiyo Gooch, amesema kampuni yake inaendelea kukusanya kiasi cha yuro milioni 600 ni sawa na dola bilioni moja zinazohitajika kuifanya ndoto hiyo iwe kweli aliongeza.
 
meli-pic3
 
Meli hiyo inayotegemewa kuwa na ghorofa 25, itakuwa na uwezo wa kuwapa makazi ya kudumu watu 50,000, lakini itakuwa na nafasi ya ziada ya kupokea wageni wengine 30,000, makazi 20,000 ya wafanyakazi wa meli, na mengine 10,000 kwaajili ya wageni wa usiku mmoja. Freedom Ship, itakuwa na huduma zote za jiji kama vile Shopping center, shule, hospitali, uwanja wa ndege, casino, maegesho ya magari na mengine mengi.

meli-pic4
Hii ndio njia inayotarajiwa kutumiwa na meli hiyo kuizunguka dunia


Meli hiyo itakapokamilika inatazamiwa kuzunguka dunia nzima kupitia nchi moja hadi nyingine, bara moja hadi jingine Afrika ikiwemo na haitakuwa ikikaa sehemu moja kwa muda mrefu.

meli-pic5
 
Meli hiyo itakuwa na huduma zote za muhimu zinazopatikana katika majiji mbalimbali zikiwemo hospitali, shule, maduka, parks, casino, aquarium, kiwanja cha ndege chenye njia ya kuruka na kutua ndege ndogo zenye uwezo wa kubeba watu 40, kitakachokuwa juu kabisa kwenye paa la meli hiyo.
 
meli-pic7
 
Hii meli itakuwa ikitumia umeme wa solar pamoja na ule wa wave energy.
Itakapokamilika, itakuwa na upana wa futi 750, urefu wa kwenda juu futi 350, pamoja na urefu wa futi 4,500 ikiwa ni mara nne ya Queen Mary II Cruise ship iliyokuwa na urefu wa futi 1,132.

meli-pic2
 
Cha ajabu zaidi wageni na wenyeji wanauwezo wa kuondoka na kuingia kwenye jiji hilo linaloelea majini kwa ndege au boti ziendazo kasi.

Floating Island Ship
 

Freedom Ship ni Meli kubwa kulikozote duniani itakayotumika kwa usafirishaji kama jiji linaloelea Meli hii inatarajiwa kugharimu dola bilioni 10 mpaka kukamilika kwake, na itakuwa na uzito wa tani milioni 2.5, lakini mpaka sasa bado ni wazo.

Chanzo: DAILY MAIL..(CLICK HAPA)

Jumapili, Desemba 01, 2013

HUDUMA ZA MUZIKI WA KIADVENTISTA


Huduma za muziki kwenye kanisa la Waadventista Wasabato na kwenye makanisa mengine ya Kikristo ni somo lenye utata na linalovuta usikivu wa watu. Kuna mitazamo inayokinzana iliyopo juu ya namna gani chombo kinaweza kutumika kuboresha huduma zetu za ibada na katika kuongoa roho kwa ajili ya Kristo. Kuvutia usikivu wa watu ni kwa lazima kwa sababu ya kule kuvuka mipaka kunakofanywa na pande zote mbili zinazohusika na somo hili. Shetani husherehekea tunapoenda nje ya mipaka ya misimamo yetu.
Tunauafiki mswaada mzuri kuhusiana na somo hili ulioandaliwa na kuwasilishwa na mchungaji Rei Kesis – Chaplensia wa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki (EUAB), akishirikiana na Idara ya Tiolojia ya UEAB, chini ya usimamizi wa mwenyekiti waIdara – Dr. Lameck Miyayo. Ilikuwa ni kazi njema na tuliyahimiza makanisa yetu yote kunufaika nayo. Unaweza kuupata kwenye ufunguo wa waraka huu.

Katika sehemu hii tutajielekeza kwenye uelewa wa Kanisa la Waadventista Wasabato, kuhusiana na nafasi na usimamizi wa muziki kwenye huduma za ibada. Tutaiangalia Kanuni ya Kanisa, ambacho ni kitabu cha msingi cha sera chenye viwango na kawaida za kanisa zinazotumika kusimamia makanisa yote mawili; lile la mahalia na yale ya ngazi za juu.

Kanuni hizi zilizopo kwenye kanuni za kanisa, zilizojengwa kwenye Biblia na zilizojikita kwa Kristo zinawakilisha uelewa wa kanisa wa wakati huu, kuhusiana na maswala mbalimbali ya kanisa yanayoathiri mahusiano yetu, kama mwili wa waumini, na kama mtu mmoja mmoja. Tunawasihi watumiaji wote wa muziki na viongozi wa kanisa kuwa na hamasa kubwa ya kuelewa kanuni hizi na kuzisimamia kama walinzi waaminifu wa kuta za Zayuni.

Kile Kanuni ya Kanisa inachosema kuhusu Muziki

Angalizo: Nukuu imechukuliwa kutoka “Kanuni ya Kanisa la Waadventista Wasabato ya 2010, toleo la Kiingereza. Kupigiwa mistari, kukolezwa kwa wino na mlalo wa maandishi vimeongezwa. Maoni ni mapendekezo na maelekezo yetu ya uongozi.

“Muziki ulitengenezwa kutumikia makusudi matakatifu, kuyainua mawazo hadi kuwa kitu safi, bora na kilicho juu, na kuamsha rohoni hali ya ibada na shukrani kwa Mungu.” – DA 73, (CM, 143)

“Muziki ni mojawapo ya sanaa ya kiwango cha juu sana. Muziki mzuri si tu unatupatia maburudisho bali pia huyainua mawazo yetu na kukuza viwango vyetu bora. Mungu  mara nyingi ametumia nyimbo za kiroho kugusa mioyo ya wadhambi na kuwaongoza kwenye toba. Kinyume chake, muziki duni unashusha hali ya kiroho na kutupeleka mbali na mahusiano yetu na Mungu.” – (CM, 143)

“Ni lazima tutumie uangalifu mkubwa katika uchaguzi wa nyimbo majumbani mwetu, kwenye mikusanyiko ya kijamii, mashuleni, na makanisani. Mrindimo wowote wenye vionjo vya jazz, rock, au mtindo uliochanganya hayo, au lugha yoyote inayooonesha hisia za kipumbavu au zisizo na maana itaepukwa.” – (Angalia CM, pp. 92, 96, 143.)

MAONI:
 • “Kuimba, kama sehemu ya huduma ya kidini, ni tendo la ibada kama lilivyo ombi.” Patriachs and Prophets Uk. 594. Maombi hukuza tabia kwa sababu kupitia maombi tunauona uso wa Yesu, na kwa kumwangali tunabadilishwa na kufanana naye. Muziki mzuri ni wakala wa ujenzi wa tabia. (2 Wakorintho 3:18).
 • Muziki wa Jazz, Rock au mtindo uliochanganya hayo mawili haipaswi kuruhusiwa makanisani.
 • Angalia kwa makini tuni, mwafaka, na mrindimo; haya yote hayapaswi kufuata muziki wa kidunia.
Nguvu ya muziki – “Muziki unaweza kuwa nguvu kubwa kwa mema, na bado hatulitumii vya kutosha tawi hili la ibada. Uimbaji kwa ujumla unafanyika kwa misisimko au kwa kukidhi jambo maalumu, na kwa nyakati zingine wale waimbao huachwa waendelee kukosea, na muziki hupoteza athari yake stahiki kwenye akili za wale waliopo. Muziki ni lazima uwe na uzuri, uchungu, na nguvu. Hebu sauti ziinuliwe katika nyimbo za sifa na za kujitoa. Vitumie kama nyenzo pale inapowezekana vifaa vya muziki, na uachilie muafaka wa utukufu upande kwa Mungu, zawadi inayokubalika.” – 4T 71 (CM, 114).

MAONI
 • Mwongozaji wa nyimbo ongoza vema. Epuke makosa ya kawaida.
 • Mwongozaji anahitaji kuwa na yafuatayo: Kitabu cha nyimbo chenye alama za muziki za tonic sol-fa au staff notation, chombo cha kuchagulia key kiitwacho Pitch pipe, na kipande cha fimbo kwa kuongozea kunakoonekana na wote.
 • Matumizi ya ala za muziki yameruhusiwa. Matumizi mabaya yamekatazwa. Ni afadhali kutotumia ala kabisa kuliko kutumia vibaya na kuwa mtego na laana kwenye ibada kwako mwenyewe na waabuduo wengine.
Imba kwa roho na uelewa – “Katika jitihada zao za kuwafikia watu, watumishi wa Bwana hawapaswi kufuata njia za dunia. Katika mikutano inayofanyika wasitegemee waimbaji wa kidunia na maonesho ya kwenye majukwaa kuamsha usikivu. Wanawezaje wale wasio na hamu ya Neno la Mungu, ambao kamwe hawajawahi kusoma Neno lake kwa nia ya dhati ya kutamani kuelewa ukweli wake, kutegemewa kuimba kwa roho na kwa kuelewa?... Kwaya ya mbnguni inawezaje kujiunga na muziki ulio wa mtindo tu?... “Uimbaji haupaswi daima kufanywa na wachache. Mara nyingi kwa kadri inavyowezekana, hebu na tuache kusanyiko lote liimbe.” – 9T 143, 144 (CM, 114).

MAONI
 • Huduma zetu za ibada hazipaswi kuongozwa au kuhudumiwa na waimbaji wasiomwabudu Mungu  wa kweli katika njia ya kweli.
 • Muda mwingi unahitaji kutumika kwa uimbaji wa wote, na muda mchache unapaswa kutumika kwa kwaya na vikundi vya uimbaji. Kila Sabato kabla ya vipindi vya Shule ya Sabato, hebu kuwe na angalau dakika za kuimba na kujifunza nyimbo mpya. Dakika 15 zingine zinapaswa kuwa baada ya Shule ya Sabato na kabla ya huduma kuu. Hebu dakika 15 zitengwe baada ya shule ya sabato na kabla ya ibada kuu kwa ajili ya uimbaji wa pamoja. Ratiba ya kwaya na vikundi vya nyimbo iendelezwe ili kuzipa kwaya fursa ya kuimba pamoja na nyimbo nyingine zilizoandaliwa. Ratiba ihusishe ibada za maombi ya katikati ya juma na ufunguzi wa Sabato. Kwaya zinapokuwa nyingi, usiendekeze maombi mengi ya kutaka nyimbo zilizoimbwa au zile zinazopendwa sana zirudiwe. Hii itumike kunapokuwa na kwaya nyingi zinazosubiri zamu yao ya kuimba.
Kila idara inaweza kuwa na viongozi wa muziki. Viongozi wawili wanaosisitizwa sana ni hawa:

Shule ya Sabato:
“Baraza linaweza kumteua Mkurugenzi wa Muziki wa Shue ya Sabato kwa kushauriana na viongozi wa vitengo. Kama namna ya kuonyesha ibada, muziki unapaswa kumtukuza Mungu. Waimbaji na wanamuziki wengine wanapaswa kuchaguliwa kwa uangalifu kama viongozi wa maeneo mengine ya huduma za Shule ya Sabato na wanapaswa kupimwa kwa viwango vilevile. (Angalia uk. 92, 144). Baraza pia linaweza kumteua mpiga kinanda wa vitengo vingine”. (CM, uk. 96)

Vijana Waadventista:
Maafisa wa AYS – “Kanisa huwachagua maafisa hawa wa AYS: Kiongozi wa Vijana, msaidizi wa kiongozi wa vijana, Katibu-mtunza hazina, msaidizi wa Katibu-mtunza hazina, mwongozaji wa nyimbo, mpiga kinanda, na mdhamini (ambaye anaweza kuwa mzee). Kwa kuwa muziki unachukua nafasi muhimu katika kuunda tabia za vijana, waimbaji hawana budi wachaguliwe kwa uangalifu kama maafisa wengine wa AYS”. (Angalia uk. 92, 96.) (CM, 102)

Kuchagua Waratibu wa Muziki – “Kanisa ni lazima lichukue uangalifu mkubwa katika kuwachagua viongozi wa kwaya, ikiwachagua wale tu waliojitoa kabisa na wanaotoa nyimbo sahihi kwa huduma zote za ibada za kanisa na mikutano. Muziki wa kidunia au ule wenye asili iletayo maswali, kamwe usiingizwe kwenye huduma zetu.” (CM, 92).

“Viongozi wa nyimbo ni lazima wafanye kazi kwa ukaribu sana na wachungaji na wazee wa makanisa ili kwamba uchaguzi wa nyimbo uoane na wazo kuu la hubiri. Kiongozi huyu wa nyimbo yupo chini ya usimamizi wa mchungaji au wazee wa kanisa na hafanyi kazi kwa kujitegemea. Kiongozi wa nyimbo anapaswa kushauriana nao kuhusu nyimbo zitakazoimbwa na uteuzi wa waimbaji na wanamuziki.” – (CM, uk. 92)

Idara na Huduma zinatakiwa kuteua Wakurugenzi wa muziki, na kulitaarifu baraza la kanisa ili liwapitishe wale waliochaguliwa. Uchaguzi wa viongozi wa muziki wa idara za Shule ya Sabato na Vijana umefafanuliwa na kusisitizwa.

Uangalifu mkubwa utumike katika kuchagua viongozi wa muziki makanisani. Baraza la kanisa ni lazima libatilishe/liidhinishe viongozi wote wa vikundi/kwaya zote ambazo kanisa limevisajili. Kila idara ichague kiongozi wake na kupeleka kwenye baraza la Kanisa ili kubatilisha au kuidhinisha..

Kanisa linaweza kuwa na viongozi kadhaa wa muziki wanaoongoza nyimbo kwenye idara zao, huduma, au makundi. Lakini kanisa ni lazima lichague mkurugenzi mmoja wa muziki, msaidizi/wasaidizi, kutegemeana na mahitaji ya kanisa, watakaoratibu viongozi wengine wote wa muziki kutoka idara mbalimbali za kanisa, huduma au vikundi. (CM, 171).

Mratibu wa muziki ni mjumbe wa baraza la kanisa. – (CM, 125). Huchaguliwa na kibaraza cha uchaguzi. (CM, uk. 171)

Mkurugenzi/Mratibu/Kiongozi (Mratibu Mkuu) wa muziki wa kanisa):
 • Ni mjumbe wa baraza la kanisa.
 • Ni lazima apimwe na kiwango kile kile cha juu kilichotumika kuwachagua viongozi wengine wa kanisa.
 • Ni kiongozi muhimu asaidiaye maandalizi ya ibada. Hufanya kazi chini ya “Msimamizi wa Mimbari/Ibada”. – (Wachungaji na Wazee wa Kanisa)
 • Ndiye anayepaswa kuchagua nyimbo na waimbaji watakaoendana na wazo kuu la hubiri la siku hiyo.
 • Ndiye atakayeandaa ratiba ya Kwaya (waimbaji)/Vikundi vya Waimbaji, Waimbishaji, na Ala za muziki ikiwa zitakuwepo.
 • Ndiye atakayehamasisha na kusimamia filosofia ya Biblia/Kanisa kuhusu muziki.
 • Makanisa yaweza kuunda Kamati ya Muziki itakazoongozwa na Mratibu wa Muziki wa Kanisa itakayosimamia huduma za muziki kanisani. Wajumbe wa baraza hili wanaweza kuwa wasaidizi wa Mratibu mkuu (anaweza pia kutumika kama katibu wa kamati), waratibu wa muziki kutoka kwenye maidara, na viongozi wakuu wa kwaya. Wajumbe wengine wanaweza kuwa viongozi wa Chama cha Vijana, Mkurugenzi wa Huduma za Watoto, na Mkurugenzi wa Huma za Washiriki. Mzee wa kanisa na mchungaji ni maafisa wa kamati hii.
 • Ukubwa wa kamati utategemea ukubwa na mahitaji ya kanisa. Kamati itafanya vizuri kazi yake kama itakutana walau mara moja kwa mwezi. Baraza la kanisa linaweza kukasimu baadhi ya mambo mepesi yahusianayo na muziki kwa kamati hii.
Kuwachagua Waimbaji – “Muziki mtakatifu ni sehemu muhimu ya ibada ya hadhara. Kanisa ni lazima litumie uangalifu katika kuchagua wanakwaya na wanamuziki wengine watakaowakilisha vizuri kanuni za kanisa. Ni lazima wawe washiriki wa Kanisa, au washiriki wa Shule ya Sabato, au wanachama wa Chama cha Vijana Waadventista. Kwa kuwa wanachukua nafasi inayooneka na watu katika huduma za kanisani, wanatakiwa kuwa kielelezo cha unyenyekevu na tabia njema, katika mwonekano na mavazi yao. Mavazi ya kwaya yatategemea uchaguzi wao. (CM, uk. 92).

Makanisa yanaweza kuwa na kwaya nyingi. Kuwa na kwaya ya watoto ni njia ya kuwasaidia kuwalea kiroho, kuwaunganisha na familia ya kanisa, na kuwashirikisha kwenye ushuhudiaji. (CM, uk. 92)

MAONI
 1. Waimbaji ni lazima wachaguliwe na kanisa
 2. Kanisa ni lazima lisajili kwaya/vikundi vya uimbaji kwa kuwachagua waimbaji na kuwabatilisha/kuwaidhinisha viongozi.
 3. Kwa kuwa waimbaji ni wahubiri, ni lazima wawe kielelezo, hasa katika mwonekano na mavazi.
 4. Waimbaji ni lazima wawe waongofu wa kweli. Kwaya na Vikundi vingi vya uimbaji ni maskani ya Mwovu. Vimejaa wivu, majivuno, migogoro, mashindano, uzinzi, uasherati, ubinafsi n.k.
 5. Hebu na wajiundie sheria na kanuni zao wenyewe. Kanisa lijiepusha kutunga na kusimamia sheria kwa waimbaji. Kanuni ya kanisa imetoa viwango vya kutosha, hebu kanisa livitumie hivyo.
Kanisa linaweza kuwa na zaidi ya kwaya moja, ikiwemo na kwaya ya Watoto. Zote hizo ni kwaya za Kanisa. Epukeni kupendelea kwaya au kikundo kimoja cha uimbaji na kuvipuuza vingine. Kanisa linapaswa kuvipenda vikundi na kwaya zote na kuvitia moyo.