Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Oktoba 17, 2013

VIJANA HUULIZA


Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Kutuma Ujumbe Mfupi?
  • :-) Kunapotumiwa vizuri, kutuma ujumbe mfupi kunaweza kuwa njia nzuri ya kuwasiliana.
  • :-( Kunapotumiwa vibaya kunaweza kuharibu urafiki wako na wengine na kukuharibia sifa.
Makala hii itakueleza mambo unayopaswa kujua kuhusu:
Pia katika makala hii:
 Watu unaotumia ujumbe
Matineja wengi huona kutuma ujumbe mfupi kuwa njia muhimu ya mawasiliano. Kutuma ujumbe mfupi hukusaidia kuwasiliana na watu walio katika orodha yako ya marafiki—⁠isipokuwa iwe wazazi wako hawakuruhusu kufanya hivyo.
“Baba yangu hukasirika mimi na dada yangu tunapoongea na wavulana. Iwapo lazima tuzungumze nao, tunapaswa kufanya hivyo kwa kutumia simu ya kawaida iliyo sebuleni, wengine wakiwapo.”—⁠Lenore.
Unachopaswa kujua: Ukimpa mtu yeyote nambari yako bila kujali, unaweza kujipata matatani.
“Usipokuwa mwangalifu kuhusu ni nani unayempa nambari yako, huenda ukapokea ujumbe au picha mbaya.”—⁠Scott.
“Ukimtumia mtu wa jinsia tofauti ujumbe mara nyingi, unaweza kuanza kuvutiwa naye haraka.”—⁠Steven.
Biblia inasema: “Mtu mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na kujificha.” (Methali 22:3) Ukichukua hatua fulani za kujilinda, hutapatwa na maumivu mengi.
Simulizi halisi: “Mimi na mvulana fulani tulikuwa marafiki na tulitumiana ujumbe mara nyingi. Nilijiambia kwamba tulikuwa tu marafiki wazuri. Sikudhani kwamba kuna tatizo hadi aliponiambia anavutiwa nami kimahaba. Ninapotafakari yaliyotokea, ninatambua kwamba sikupaswa kutumia wakati mwingi pamoja naye wala kumtumia ujumbe mfupi mara nyingi sana.”—⁠Melinda.
Fikiria hili: Unafikiri urafiki wa Melinda na mvulana huyo utakuwaje baada ya mvulana huyo kumweleza hisia zake?
Badili hadithi hiyo! Melinda angefanyaje mambo kwa njia tofauti ili urafiki wake na mvulana huyo usipite mipaka?
 Mambo unayoandika katika ujumbe
Kwa kuwa ni rahisi sana kutuma ujumbe mfupi—⁠na inafurahisha kupokea ujumbe—⁠huenda mtu akasahau kwamba anaweza kueleweka vibaya.
Unachopaswa kujua: Maneno yaliyoandikwa kupitia ujumbe mfupi yanaweza kueleweka vibaya.
“Unapotuma ujumbe mfupi, mtu hawezi kujua hisia zako hata kama umeweka vibonzo vinavyoonyesha jinsi unavyohisi. Hilo linaweza kufanya mtu akuelewe vibaya.”—⁠Briana.
“Ninajua wasichana fulani ambao wamejiharibia sifa na wanajulikana kuwa wanapenda kuwachezea wengine kimapenzi kwa sababu tu ya ujumbe waliowatumia wavulana hao.”—⁠Laura.
Biblia inasema: “Moyo wa mwadilifu hufikiri kabla ya kujibu.” (Methali 15:28, Biblia Habari Njema) Andiko hilo linatufundisha nini? Soma ujumbe ulioandika kabla ya kuutuma!
 Wakati unaofaa kutuma ujumbe
Kwa busara, unaweza kujiwekea sheria kuhusu kutuma ujumbe mfupi ili kuonyesha una adabu.
Unachopaswa kujua: Usipofuata adabu zinazohusiana na kutuma ujumbe mfupi, huenda ukaonekana kuwa huna heshima na hilo litafanya marafiki wakuepuke badala ya kuvutiwa nawe.
“Ni rahisi kusahau kuwa na adabu unapotuma ujumbe mfupi. Nyakati nyingine, mimi hujipata nikituma ujumbe mfupi huku nikiwa ninazungumza na mtu mwingine au nikiwa mezani ninakula.”—⁠Allison.
“Ni hatari kutuma ujumbe mfupi unapoendesha gari. Ukikengeushwa kwa njia hiyo, unaweza kusababisha aksidenti.”—⁠Anne.
Biblia inasema: “Kuna wakati uliowekwa wa kila kitu, . . . wakati wa kukaa kimya na wakati wa kusema.” (Mhubiri 3:1, 7) Kanuni hiyo inatumika pia katika kutuma ujumbe mfupi.
 Madokezo kuhusu kutuma ujumbe mfupi
Watu unaotumia ujumbe
  • ;-) Tii mwongozo wa wazazi wako.—⁠Wakolosai 3:20.
  • ;-) Chagua watu unaowapa nambari yako. Unapokataa kumpa mtu habari za kibinafsi—⁠kutia ndani nambari ya simu yako ya mkononi—⁠unasitawisha stadi ambazo utatumia ukiwa mtu mzima.
  • ;-) Usizoeane isivyofaa na mtu kwa kumtumia ujumbe wa kumchezea kimapenzi. Unapoanza kuvutiwa na mtu kimahaba basi unajitakia maumivu ya moyo na kukatishwa tamaa.
“Nimejijengea jina nzuri pamoja na wazazi wangu kuhusu matumizi ya simu ya mkononi, kwa hiyo wanaamini kwamba nitafanya uamuzi unaofaa kuhusu nambari nitakazoweka katika orodha yangu ya simu.”—⁠Briana.
Mambo unayoandika katika ujumbe
  • ;-) Kabla hujaanza kuandika ujumbe, jiulize, ‘Je, kutuma ujumbe ndio njia inayofaa zaidi ya kuwasiliana katika hali hii?’ Huenda ingefaa upige simu au kusubiri uongee na mtu huyo uso kwa uso.
  • ;-) Usiandike jambo lolote ambalo huwezi kumwambia mtu uso kwa uso. “Ikiwa jambo hilo halipaswi kusemwa kwa sauti, basi halipaswi kuandikwa katika ujumbe mfupi,” anasema Sarah, mwenye umri wa miaka 23.
“Mtu akikutumia picha chafu, waambie wazazi wako. Hilo litakulinda na pia kufanya wazazi wako wakuamini.”—⁠Sirvan.
Wakati unaofaa kutuma ujumbe
  • ;-) Amua kimbele ni wakati gani hutatumia simu yako. Msichana anayeitwa Olivia anasema, “Sibebi simu yangu ya mkononi wakati tunapokula pamoja au ninapojifunza. Mimi huizima wakati wa mikutano ya Kikristo ili nisishawishiwe kuitazama.”
  • ;-) Wajali wengine. (Wafilipi 2:4) Usitume ujumbe mfupi unapozungumza na mtu mwingine.
“Nimejiwekea sheria ya kwamba sitatuma ujumbe ninapokuwa na kikundi cha marafiki wangu isipokuwa iwe ni lazima kufanya hivyo. Pia siwapi watu ambao sina uhusiano wa karibu nambari yangu.”—⁠Janelly.
 Maswali kuhusu kutuma ujumbe
Mfano wa 1
Umekuwa na uhusiano wa karibu na mtu fulani wa jinsia tofauti kwa miezi sita, lakini sasa unagundua kwamba hakufai. Ni ujumbe gani ungefaa kumtumia?
  1. “Uhusiano wetu umekwisha.”
  2. Ningependa kuzungumza nawe. Tunaweza kukutana lini?”
Jibu sahihi: B. Isipokuwa iwe si jambo la hekima kufanya hivyo, ni afadhali kuzungumza na mtu uso kwa uso kuhusu jambo zito kama kukatiza uhusiano.—⁠Luka 6:31.
Mfano wa 2
Unapokea ujumbe mfupi wenye picha chafu ya mwanafunzi mwenzako. Unapaswa kufanya nini?
  1. Kuifuta picha hiyo mara moja.
  2. Kuisambaza picha hiyo kwa marafiki wako wote.
Jibu sahihi: A. Kutuma picha chafu huwashushia heshima wote wanaohusika. Usijihusishe kamwe na jambo hilo!—⁠Waefeso 5:3, 4.
Mfano wa 3
Mnakula pamoja mkiwa familia na unasikia sauti fulani inayokujulisha kwamba umepokea ujumbe mfupi. Unapaswa kufanya nini?
  1. Kusoma ujumbe huo ukitumaini kwamba familia yenu itakuwia radhi.
  2. Kusoma ujumbe huo baada ya mlo.
Jibu sahihi: B. Ujumbe unaweza kungoja. Unapaswa kutanguliza familia.—⁠Wafilipi 1:10.
SOURCE: http://www.jw.org/sw/mafundisho-biblia/familia/matineja/uliza/ninapaswa-kujua-nini-kuhusu-kutuma-ujumbe-mfupi/

Jumanne, Oktoba 15, 2013

SEKTA ZA UCHUMI



Uchumi wa kijadi katika nchi nyingi ulikuwa hasa kilimo cha kujikimu pamoja na biashara ya kubadilishana bishaa kadhaa zenye thamani kubwa. Kwa mfano tangu kale migodi ya Zimbabwe ilichimba dhahabu iliyopelekwa baadaye hadi Asia na dunia ya Mediteranea.
Katika uchumi wa kisasa mara nyinga sekta tatu hutofautishwa:
  • Sekta ya msingi: kutoa na kuzaa malighafi pamoja na mazao katika mazingira asilia. Mifano ni kilimo, uchimbaji wa madini, uvuvi au kuvuna ubao.
  • Sekta ya pili: shughuli za kubadilisha malighafi hizi kuwa bidhaa. Madini ya chuma hubadilishwa kuwa feleji; feleji hutumiwa na viwanda kutengeneza vyuma vya ujenzi, magari, vifaa vya nyumbani. Viwanda vya nguo hutumia pamba kutoka mashambani na kuibadilisha kuwa uzi halafu kitambaa na nguo.
  • Sekta ya tatu: biashara au usambazaji wa bidhaa hizi kwa wateja pamoja na kuwatolea huduma. Mifano ni maduka yanayouza bidhaa zilizotengenezwa viwandani. Mingine ni huduma kama benki, hoteli, sinema na usafiri.
  • Wataalamu wengine hutaja sekta ya nne: shughuli za kusambaza habari na pia utafiti wa teknolojia mpya unaoendelea kuwa muhimu katika nchi zinazoendelea. Wengine huingiza pia elimu (kazi za shule na vyuo) katika sekta hiiy a uchumi.

Sayansi ya Uchumi

Hii ni mkono wa elimu inayochunguza masharti ya uchumi kufaulu au kushindwa.  


Uchumi ni jumla ya shughuli zote za kibinadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji ya watu. Ni hasa shughuli za uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.
Uchumi mara nyingi hutazamiwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au dunia.