Mtayarishaji

Morning Star Radio

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mahusiano. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mahusiano. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, Februari 24, 2014

Je una mpango au tayari una mahusiano na mkubwa wako wa kazi (bosi)?



Nini kinafuata? 

Ukweli ni kuwa, mahusiano katika eneo la kazi si jambo geni. Mahusiano yanaathiri (zaidi kwa wasichana, na hasa warembo), walioelimika na wasioelimika, matajiri kwa maskini, kwenye makampuni madogo na makubwa sehemu zote. Kama umeingia au una mpango wa kuingia katika mahusiano hayo, fahamu kuwa unayafanya maisha yako ya kazini kuwa magumu na tata. 

Ni kweli pia kuwa si mara zote watu hutoka na kudhamiria kuwa na mahusiano kazini ila hujikuta tayari wamo.

Kabla hujaanza mahusiano na bosi wako, au katika hali yoyote ambayo umejikuta tayari una mahusiano hayo, tafiti na jiulize haya yafuatayo:-

1. Je, Kampuni unayofanya kazi ina sheria inayohusu mahusiano kazini? Kama ni ndiyo, jua kuwa unajiwekea mazingira magumu na kuhatarisha kazi yako. Hata kama mtu unayeingia naye kwenye mahusiano ni bosi wako, wewe ndiye utakayeondoka . Mtu mwenye cheo mara zote anabaki kwenye kampuni, kampuni haiwezi kuingia gharama ya kumpoteza bosi kwaajili ya mahusiano yako, ila wewe itabidi uondolewe kwakuwa gharama ya kumpata bosi ni kubwa kuliko kupata mtu kama wewe.

2. Je, Uliajiriwa kwa ujuzi wako na si vinginevyo, baada ya kuanza mahusiano mambo yanaanza kuwa tata kikazi. Bosi wako ni bosi wako tu, yeye ndiye anayeamua nani apandishwe cheo, kupata nyongeza za mishahara na mengine mengi. Hivyo mambo yataanza moto moto ila siku za usomi huanza kufifia na kinachobakia ni kutojisikia vizuri unapokuwa kazini. Hivyo uwe makini na maamuzi unayoyafanya hasa kuhusu mahusiano kazini.
3. Jua kuwa mahusiano hayo yatafika mwisho. Je, utajisikiaje kwenda ofisini ukiwa umeshaachana na bosi? Utendaji na ufanisi wa kazi utakuwaje? Hakuna ubishi kuwa utakuwa na maumivu makubwa, ingawaje wengi hujifanya hawajaumia.

Kama Bosi wako ameoa au kuolewa

1. Fahamu kuwa ni 10% tu ya mahusiano kazini ndiyo humea kwa muda mrefu; Mengi huvunjika.
2. Je, haya ni mahusiano yako ya kwanza? Fahamu kuwa watu wana vitu vingi vinavyoendelea kwenye maisha yao, tabia, hulka na mahusiano huwa tofauti. Kuwa makini kujua mtu anapitia nyakati gani.
Kama unaamua kuingia kwenye mahusiano

1. Kuwa makini, na tumia akili nyingi kutambua unamwambia nani hapo kazini. Hii inaweza kuhatarisha kazi na vyeo vyako unavyostahili kupandishwa kihalali uwapo kazini.
2. Kama umeoa au kuolewa, jua kuwa wewe ni mdanganyifu kwenye ndoa yako. Kuwa na mahusiano nje ya ndoa si suluhisho ya tatizo, bali kuwa jasiri kwa kujadili na mwenzi wako kutafuta njia ya kutatua kile kinachopungua kwenye ndoa yenu. Hiyo ndiyo namna ya kuonyesha upendo kwa mtu uliyeamua kuishi naye kwenye ndoa.
3. Tafuta ushauri kwa washauri wa masuala ya ndoa na mahusiano. 
Fikiria kwa makini na tafakari kabla maji hayajamwagika ukajutia. Bado unao uamuzi!

Jumatano, Februari 06, 2013

WAJIBIKA KUTAFUTA FURAHA KATIKA UHUSIANO ULIONAO


Kila Mmoja Bila Kutegeana.


Inawezekana kuwa na furaha na amani katika ndoa au uhusiano ulionao kama wote wawili mtawajibika bila kutegeana,kwani ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha uhusiano alionao unakuwa na furaha wakati wote,haiwezekani katika muungano wa watu wawili kama mke na mume mmoja akaonekana kufaidi zaidi ya mwingine tupeane haki sawa kila mmoja amfurahishe mwenzie.




Inapendeza kuwa na amani na furaha kwa wote wawili kwani kila mmoja anajua jukumu lake kwa mwenzi wake ikiwa ni baba au mama alimradi kuwepo na maelewano baina yao,na kama utafahamu nini mwenzio anakipenda naye pia akawa anatambua kipi unapenda ni rahisi kudumu katika ndoa hata mahusiano kutokana na maelewano mazuri






Kama itatokea mahusiano yana mapungufu ya mmoja kukosa kujituma ili  kutimiza mahitaji ya ndoa kwasababu zilizo ndani ya uwezo,,basi uwezekano wa kuwepo na migogoro ni mkubwa,na katika hali kama hii haitashangaza suala la uaminifu kukosekana kutokana na kwamba mmoja anaona hapati mahitaji ya msingi kutoka kwa mwenzake mume au mke.maisha ya ndoa yanaitaji mawasiliano ya mara kwa mara,kwani kwa kufanya hivyo inaleta ushirikiano ,na uwazi ukiwa ni silaha ya kujenga zaidi..usinyamaze kimya kwa matatizo yanayojitokeza kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha mahusiano yenu.