Mtayarishaji

Morning Star Radio

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Muziki. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Muziki. Onyesha machapisho yote

Jumapili, Aprili 27, 2014

Ubora wa Sauti

 
Unahitaji kufanya nini?

Unahitaji kuboresha sauti yako kwa kupumua vizuri na kutuliza misuli yako badala ya kuiga mtu mwingine.

Kwa Nini Ni Muhimu?

Sauti nzuri hufanya wengine watulie na kufurahia kusikiliza. Sauti mbaya huharibu mawasiliano, na inaweza kumfadhaisha msemaji na wasikilizaji.

KWA KAWAIDA watu hawavutiwi tu na mambo yanayosemwa, bali wanavutiwa pia na jinsi yanavyosemwa. Ikiwa mtu anayezungumza nawe ana sauti nzuri, changamfu, ya kirafiki, na yenye fadhili, utafurahia kumsikiliza kuliko kama ana sauti kali isiyo ya kirafiki, sivyo?

Kukuza sifa hizo nzuri hakutegemei tu kuboresha sauti. Kunaweza kuhusu utu wa mtu pia. Mtu anapoendelea kujifunza kweli ya Biblia na kuifuata, kwa wazi njia yake ya kuzungumza inabadilika. Sauti yake huonyesha sifa kama vile upendo, shangwe, na fadhili. (Gal. 5:22, 23) Anapojali wengine sana, sauti yake inaonyesha. Anapokuwa mwenye shukrani badala ya kulalamika daima, maneno anayosema na sauti yake inaonyesha hivyo. (Wim. 3:39-42; 1 Tim. 1:12; Yuda 16) Hata kama huelewi lugha fulani, ni rahisi kujua ikiwa mtu anazungumza kwa njia ya ufidhuli, hana uvumilivu, anachambua, ni mkali, na pia ni rahisi kujua kama mwingine anazungumza kwa unyenyekevu, subira, fadhili, na upendo.

Nyakati nyingine sauti isiyofaa inaweza kusababishwa na kasoro fulani ambayo mtu amezaliwa nayo au ugonjwa uliodhuru zoloto. Huenda kasoro hizo zisiweze kurekebishwa katika mfumo huu wa mambo. Lakini, unaweza kuboresha sauti yako ukijifunza kutumia vizuri viungo vya usemi.

Kwanza, tufahamu kwamba sauti za watu hutofautiana. Kwa hiyo, usijaribu kuiga sauti ya mtu mwingine. Badala yake, boresha sauti yako mwenyewe pamoja na hali zake. Unawezaje kufaulu? Kuna mambo mawili makuu.

Pumua Vizuri. Ili sauti yako iwe nzuri, unahitaji hewa ya kutosha na unahitaji kupumua vizuri. Bila kufanya hivyo, sauti yako inaweza kuwa dhaifu mno na unaweza kukata-kata maneno katika hotuba yako.
Sehemu kubwa za mapafu haziko juu kifuani; sehemu hizo huonekana kubwa kwa sababu tu ya mifupa ya mabega. Lakini, sehemu za mapafu zilizo pana zaidi ziko chini, juu tu ya kiwambo. Kiwambo kinashikana na mbavu za chini na kinatenganisha kifua na tumbo.

Ukivuta pumzi na kujaza tu sehemu za juu za mapafu, utakosa pumzi haraka. Sauti yako itakosa nguvu na utachoka haraka. Ili uvute pumzi vizuri, unahitaji kuketi au kusimama vizuri na kurejesha mabega nyuma. Jaribu sana usipanue sehemu ya juu pekee ya kifua unapovuta pumzi. Kwanza vuta pumzi kabisa. Sehemu za chini za mapafu zikijaa hewa, mbavu zako za chini zitapanuka. Kwa wakati huohuo, kiwambo kitasonga chini, kikisukuma chini kwa utaratibu sehemu za tumbo hivi kwamba utasikia mkazo kwenye mshipi wako au kwenye vazi katika eneo la tumbo. Lakini mapafu hayako kwenye eneo la tumbo; yamefunikwa na mbavu. Unaweza kuthibitisha jambo hilo kwa kuweka mkono mmoja kila upande wa mbavu za chini. Kisha vuta pumzi kabisa. Kama unavuta pumzi vizuri, utaona kwamba huingizi hewa tumboni na kuinua mabega. La, badala yake, utasikia mbavu zikisonga juu kidogo na kupanuka.

Kisha, jaribu kushusha pumzi. Usishushe pumzi kwa ghafula. Ishushe polepole. Usijaribu kuzuia pumzi kwa kukaza koo kwa sababu sauti itajikaza au itakuwa nyembamba sana. Mkazo wa misuli ya tumbo na mkazo wa misuli iliyo kati ya mbavu huondosha pumzi, lakini kiwambo hudhibiti mwendo wa pumzi hiyo.
Msemaji anaweza kudhibiti jinsi anavyopumua kwa kujizoeza kama vile tu mwanariadha anavyofanya mazoezi ya mbio. Simama vizuri kama umerejesha nyuma mabega, vuta pumzi kabisa ili sehemu za chini za mapafu zijae hewa, kisha shusha pumzi polepole na kwa utaratibu ukihesabu kwa kadiri uwezavyo kabla ya kuvuta tena pumzi. Kisha jizoeze kusoma kwa sauti ukipumua kwa njia hiyo.

Tuliza Mkazo wa Misuli. Jambo jingine muhimu linalotokeza sauti nzuri ni utulivu! Unaweza kuboresha sana sauti yako ukijifunza kutulia unapozungumza. Ni lazima akili na mwili zitulie, kwa kuwa mkazo wa akili husababisha mkazo wa misuli.

Ondoa mkazo wa akili kwa kuwa na maoni mazuri juu ya watu unaozungumza nao. Ikiwa unakutana nao katika huduma ya shambani, kumbuka kwamba hata kama umejifunza Biblia kwa miezi michache tu, unajua mambo mazuri sana kuhusu kusudi la Yehova ambayo unaweza kuwaeleza. Na unawatembelea kwa sababu wanahitaji msaada, iwe wanatambua jambo hilo au la. Na kama unatoa hotuba katika Jumba la Ufalme, wengi wa wasikilizaji ni watu wa Yehova. Wao ni rafiki zako na wanataka ufaulu. Hakuna wasemaji wengine duniani ambao huhutubia wasikilizaji wenye urafiki na wenye upendo kama sisi.

Ifikirie misuli ya koo na kujaribu kuituliza. Kumbuka kwamba nyuzi zako za sauti hutikisika zinapopitisha hewa. Sauti hubadilika misuli hiyo ikikazika au ikitulia kama tu vile uzi wa gitaa hubadili sauti ukikazwa au ukilegezwa. Sauti hurudi chini nyuzi za sauti zinapotulia. Kutuliza misuli ya koo pia hufanya mianzi ya pua ibaki wazi, na hiyo huboresha sauti.

Tuliza mwili wako mzima—magoti, mikono, mabega, na shingo. Ukifanya hivyo, utaweza kuvumisha sauti vizuri ili isikike wazi. Sauti huvumishwa wakati mwili wote unapohusika kuitokeza, lakini mkazo huizuia. Sauti hutokezwa kwenye zoloto nayo huvumishwa katika mianzi ya pua, kwenye mifupa ya kifua, meno, na kaakaa ya mdomo na mianya iliyo katika mifupa ya pua. Sehemu hizo zote zinaweza kuchangia ubora wa sauti. Ukiweka kitu kwenye kibao cha gitaa cha kupaazia sauti, sauti itafifia; ni lazima kibao hicho kisiwe na kitu ili kitikisike na kutoa sauti vizuri. Ndivyo ilivyo pia na mifupa ya mwili wetu ambayo imeshikiliwa na misuli. Uvumishaji mzuri wa sauti unakuwezesha kuwa na ubadilifu wa sauti na kuweza kuonyesha hisia mbalimbali unapozungumza. Pia utaweza kuhutubia watu wengi zaidi bila kukaza sauti.

JINSI YA KUFAULU

Kuza sifa za utu wa Kikristo.
Fanya mazoezi ya kuvuta pumzi, ukijaza sehemu za chini za mapafu kwa hewa.
Unapozungumza, tuliza misuli yako ya koo, shingo, mabega, na mwili wote mzima.

MAZOEZI: 

 (1) Kwa dakika chache kila siku katika juma, fanya mazoezi ya kuvuta pumzi kabisa mpaka uzijaze sehemu za chini za mapafu yako. 

(2) Jaribu kutuliza misuli ya koo unapoongea, angalau mara moja kwa siku.

SAUTI HUTOKEZWAJE?

  Sauti zote hutokezwa na hewa inayotoka mapafuni. Mapafu hupiga hewa kama pampu kupitia koo na kuingia ndani ya zoloto ambayo iko katikati ya koo. Ndani ya zoloto mna misuli miwili midogo inayoitwa nyuzi za sauti, msuli mmoja uko upande mmoja na msuli mwingine upande mwingine. Nyuzi hizo za sauti ndizo vitokezaji vikuu vya sauti. Misuli hiyo hufungua na kufunga njia ya hewa katika zoloto ili kuingiza hewa na kuitoa na vilevile kuzuia vitu visivyotakikana visiingie kwenye mapafu. Tunapopumua kwa njia ya kawaida nyuzi za sauti hazitokezi sauti wakati hewa inapopita. Lakini mtu akitaka kuzungumza, misuli hufinya nyuzi za sauti, na nyuzi hizo hutikisika wakati hewa inayotoka mapafuni inaposukumwa kuzipitia. Utaratibu huo hutokeza sauti.

  Kadiri nyuzi za sauti zinavyokazika, ndivyo zinavyotikisika kwa kasi zaidi na ndivyo sauti inavyoinuka. Na kadiri nyuzi hizo zinavyolegea, ndivyo sauti inavyopungua. Mawimbi ya sauti yanayotoka kwenye zoloto huingia sehemu ya juu ya koo inayoitwa koromeo. Kisha mawimbi hayo hupitia mdomo na pua. Hapo sauti nyinginezo huongezwa ili kurekebisha, kukuza, na kuimarisha sauti ya awali. Kaakaa la mdomo, ulimi, meno, utaya, na midomo huungana pamoja ili kutawanya mawimbi ya sauti, na kutokeza usemi unaoeleweka.
  Sauti ya mwanadamu ni ajabu sana, na haina kifani ikilinganishwa na chombo chochote kile ambacho binadamu ametengeneza. Ina uwezo wa kuonyesha hisia mbalimbali kama vile upendo na chuki kali. Sauti ikikuzwa na kuzoezwa vizuri, inaweza kubadilikana sana na kutokeza nyimbo tamutamu na semi zinazogusa mioyo.


KUSHINDA MATATIZO FULANI HUSUSA

  Sauti dhaifu. Sauti ndogo huenda isiwe dhaifu. Ikiwa nzuri na yenye kuvutia, wengine wanaweza kufurahi kuisikiliza. Lakini ni lazima sauti iwe yenye kiasi kinachofaa ili iweze kufaidi wengine.

  Ili uboreshe ukubwa wa sauti yako, unahitaji kuivumisha zaidi. Unahitaji kutuliza mwili wote mzima, kama ilivyoonyeshwa katika somo hili. Pamoja na kutuliza mwili, fanya mazoezi ya kuimba hali umefunga midomo. Midomo inapaswa kugusana kidogo, isishikane sana. Unapoimba kwa njia hiyo, sikia mitikisiko ya wimbo huo akilini na kifuani.

  Nyakati nyingine sauti husikika kuwa dhaifu au kukazika kwa sababu ya ugonjwa au kukosa usingizi. Bila shaka, hali hiyo ikiboreka, sauti itaboreka.

  Sauti inayoinuka juu sana. Mkazo kwenye nyuzi za sauti hufanya sauti iinuke. Sauti yenye mkazo hufanya wasikilizaji wawe na mkazo. Unaweza kupunguza sauti nyembamba kwa kutuliza misuli ya koo ili kupunguza mkazo kwenye nyuzi za sauti. Jaribu kufanya hivyo, ukifanya mazoezi kila siku unapozungumza. Pia ni vizuri kuvuta pumzi kabisa.

  Sauti ya kubana pua. Nyakati nyingine pua iliyofungika hutokeza tatizo hilo, lakini mara nyingi hali hiyo husababishwa na jambo jingine. Nyakati nyingine kwa kukaza misuli ya koo na mdomo, mtu hufunga mianya ya pua na kuzuia hewa isipite vizuri. Jambo hilo hutokeza sauti inayobana pua. Unahitaji kutulia ili kuepuka jambo hilo.

  Sauti nzito na kali. Sauti kama hiyo haitokezi mazungumzo ya kirafiki. Inaweza kutisha wengine.
  Katika hali fulani, jambo muhimu ni kuendelea kujitahidi kubadili utu wako. (Kol. 3:8, 12) Ikiwa tayari umefanya hivyo, kujaribu kutumia kanuni za kurekebisha sauti kunaweza kusaidia. Tuliza koo na taya. Kufanya hivyo kutafanya sauti yako ipendeze zaidi na kufanya maneno mengine yasitokee vibaya kwa kuyalazimisha kupitia meno.

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Viungo vya Matamshi
 Kaakaa
Ulimi
Meno
Midomo
Taya

Mkondo wa Hewa Mwilini
 Tundu la pua
Kinywa
Koo
Nyuzi za sauti
Njia ya chakula
Mapafu
Kiwambo

Nyuzi za Sauti (zikitazamwa kutoka juu)
Unapozungumza
Unapovuta pumzi
Unapovuta pumzi kabisa

Jumapili, Machi 02, 2014

Muziki ni wa maana kwako kadiri gani?


□ Si wa lazima.
□ Siwezi kuishi bila muziki.

Wewe husikiliza muziki wakati gani?

□ Ninaposafiri
□ Ninaposoma
□ Wakati wote

Ni muziki wa aina gani unaopenda sana?

YAELEKEA sote tuliumbwa tukiwa na uwezo wa kufurahia muziki. Na kwa vijana wengi, muziki ni wa lazima. “Siwezi kuishi bila muziki,” anasema Amber mwenye umri wa miaka 21. “Mimi husikiliza muziki karibu kila wakati, ninapofanya usafi, ninapopika, ninapotembea, au hata ninaposoma.”

Hata muziki wenye mdundo wa kawaida tu unaweza kupenya ndani sana na kuchochea hisia zetu. Kama vile “neno linalosemwa wakati unaofaa ni jema kama nini!” wimbo unaochezwa wakati unaofaa unaweza kuburudisha sana! (Methali 15:23) “Nyakati nyingine unahisi kwamba hakuna mtu anayekuelewa,” anasema Jessica mwenye umri wa miaka 16. “Lakini ninaposikiliza nyimbo za bendi fulani ninayopenda, najihisi kwamba siko peke yangu.”

Je, Muziki Hutokeza Vita au Amani?

Ingawa unapenda muziki, huenda wazazi wako wakawa na maoni tofauti. Kijana mmoja anasema: “Baba yangu husema, ‘Zima hiyo kilele! Inaniumiza masikio!’” Ugomvi unapotokea, huenda ukaona kwamba wazazi wako wanachemka bure. “Ilikuwaje walipokuwa vijana?” anauliza msichana mmoja. “Kwani wazazi wao pia hawakufikiri kwamba muziki walioupenda ulikuwa mbaya?” Ingred mwenye umri wa miaka 16 analalamika: “Watu wazima hawapendi mabadiliko. Ingekuwa afadhali kama wangetambua kwamba kizazi chetu kinapenda muziki tofauti!”

Kuna ukweli fulani katika maneno ya Ingred. Kama ujuavyo, tangu zamani mapendezi ya vijana na ya watu wazima yametofautiana sana. Hata hivyo, haimaanishi kwamba lazima mgombane kwa sababu ya muziki kila siku. Siri ni kujaribu kutafuta maelewano kuhusu muziki. Ikiwa wazazi wako wanaiheshimu Biblia, basi kuna matumaini. Kwa nini? Kwa kuwa Neno la Mungu linaweza kukusaidia wewe na wazazi wako kutambua mambo yanayofaa na yanayotegemea mapendezi ya kibinafsi. Ili kufanya hivyo, unahitaji kuchanganua mambo mawili makuu: (1) ujumbe ulio katika muziki unaosikiliza na (2) muda unaotumia kusikiliza muziki. Kwanza, tufikirie swali hili . . .

Muziki Ninaopenda Una Ujumbe Gani?

Muziki ni kama chakula. Unahitaji aina inayofaa kwa kiasi kinachofaa. Aina mbaya, hata iwe ni kiasi gani, ni hatari. Kwa kusikitisha, katika ulimwengu wa muziki, aina mbaya ya muziki ndiyo inayovutia zaidi. “Kwa nini miziki yote yenye midundo mitamu huwa na maneno machafu hivyo?” alalamika kijana anayeitwa Steve.

Ikiwa unapendezwa na mdundo, kuna haja ya kuzingatia ujumbe uliopo? Ili kujibu swali hilo, jiulize: ‘Ikiwa mtu fulani angetaka ninywe sumu, angetumia mbinu gani ili kunifanya niinywe? Je, angeichovya katika kitu kichungu au katika sukari?’ Yule mwanamume mwaminifu, Ayubu, aliuliza: “Je, sikio halipimi maneno kama kaakaa linavyoonja chakula?” (Ayubu 12:11) Kwa hiyo, badala ya kusikiliza muziki kwa sababu tu unapenda mdundo wake—utamu wake wa kijuujuu—‘pima maneno yake’ kwa kufikiria kichwa cha muziki na maneno yaliyomo. Kwa nini? Kwa sababu maneno yaliyo katika muziki yataathiri kufikiri kwako na mtazamo wako.

Inasikitisha kwamba miziki inayopendwa sana leo ina maneno yanayosifu ngono, jeuri, na matumizi ya dawa za kulevya. Ikiwa huoni kwamba kusikiliza maneno hayo kunaweza kukuathiri, basi “sumu” yake imeanza kukuingia.

Usifuate Upepo

Vijana wenzako wanaweza kukushinikiza usikilize muziki usiofaa. Pia, soko la muziki lina uvutano mkubwa. Kukiwa na redio, Intaneti, na televisheni, muziki umekuwa biashara kubwa. Wataalamu wa mauzo wameajiriwa ili kukuchochea upendezwe na muziki wa aina fulani.

Lakini unapoacha marafiki au vyombo vya habari vikuamulie muziki utakaosikiliza, unapoteza uhuru wako wa kuchagua. Unakuwa mtumwa, mtu asiyetumia akili yake. (Waroma 6:16) Biblia inakuhimiza uepuke uvutano wa ulimwengu katika mambo kama hayo. (Waroma 12:2) Hivyo, unapaswa kuzoeza ‘nguvu zako za ufahamu ili zitofautishe yaliyo sawa na yaliyo makosa pia.’ (Waebrania 5:14) Unaweza kutumia jinsi gani nguvu zako za ufahamu unapochagua muziki? Fikiria mapendekezo yanayofuata:

Chunguza picha na maandishi yaliyo kwenye kasha. Mara nyingi unaweza kujua yaliyomo katika kanda kwa kutazama kasha. Unapoona picha zinazoonyesha jeuri, ngono, au kuwasiliana na pepo, tahadhari. Inaelekea muziki wenyewe pia haufai.

Soma maneno ya wimbo. Ni nini kinachosemwa? Je, kweli ungependa kusikiliza maneno hayo tena na tena? Je, ujumbe wa wimbo huo unapatana na sifa na kanuni za Kikristo?—Waefeso 5:3-5.

Chunguza athari zake. Kijana anayeitwa Philip anasema: “Niligundua kwamba muziki na maneno niliyosikiliza yalinifanya nishuke moyo.” Kwa kweli, muziki unaweza kuathiri watu kwa njia mbalimbali. Lakini muziki unaosikiliza unaamsha hisia gani? Jiulize: ‘Je, mimi huwa na mawazo yasiyofaa baada ya kusikiliza muziki au maneno ya muziki fulani? Je, nimeanza kutumia lugha ya mitaani inayotumiwa katika muziki?’—1 Wakorintho 15:33.

Wafikirie wengine. Wazazi wako wana maoni gani kuhusu muziki unaosikiliza? Waulize maoni yao. Pia, fikiria maoni ya Wakristo wenzako. Je, wengine wanaweza kukwazwa? Kubadili mwenendo wako ili usiumize hisia za wengine kunaonyesha kwamba wewe ni mkomavu.—Waroma 15:1, 2.

Kujiuliza maswali yaliyo hapo juu kutakusaidia kuchagua muziki ambao utakuchangamsha moyo pasipo kuangamiza hali yako ya kiroho. Hata hivyo, kuna jambo lingine la kufikiria.

Ni Wakati Gani Muziki Unapita Kiasi?

Muziki unaofaa kama vile chakula kizuri unaweza kuwa wenye faida. Hata hivyo, methali yenye hekima inaonya: “Je, umepata asali? Kula kiasi cha kukutosha, ili usiile kupita kiasi kisha uitapike.” (Methali 25:16) Asali ni dawa. Lakini kitu chochote hata kiwe kizuri kinapopita kiasi kinaweza kukudhuru. Kwa hiyo, vitu vizuri vinapaswa kufurahiwa kwa kiasi.

Hata hivyo, maisha ya vijana fulani hutawaliwa na muziki. Kwa mfano, Jessica aliyetajwa mapema, anakiri: “Mimi husikiliza muziki kila wakati—hata ninapojifunza Biblia. Mimi huwaambia wazazi wangu kwamba muziki hunisaidia kukaza fikira. Lakini hawaniamini.” Je, umewahi kuwa na maoni kama ya Jessica?
Unaweza kujua jinsi gani ikiwa unapita kiasi katika kusikiliza muziki? Jiulize maswali yanayofuata:

Kila siku mimi hutumia saa ngapi kusikiliza muziki? ․․․․․
Ninatumia pesa ngapi kwa muziki kila mwezi? ․․․․․

Je, muziki unaharibu uhusiano kati yangu na wengine katika familia? Ikiwa ndivyo, andika hapa chini jinsi unavyoweza kurekebisha hali hiyo. ․․․․․

Badili Mazoea Yako

Ikiwa muziki unachukua wakati mwingi kupita kiasi, unapaswa kujiwekea mipaka na kuwa na usawaziko kuhusiana na mazoea yako ya kusikiliza muziki. Kwa mfano, huenda ukahitaji kuacha mazoea ya kuweka masikioni vidude vya kusikilizia muziki siku nzima au mazoea ya kuwasha redio mara tu unapofika nyumbani.
Kwa nini usijifunze kufurahia pindi za utulivu, pasipo kelele yoyote? Kufanya hivyo kutakusaidia katika masomo yako. 

Steve aliyetajwa mapema anasema: “Unaweza kujifunza mambo mengi zaidi ikiwa muziki umezimwa.” Jaribu kusoma bila muziki, na uone iwapo utakazia fikira zaidi mambo unayojifunza.
Pia, utahitaji kupanga wakati wa kusoma na kujifunza Biblia na vitabu vinavyotegemea Biblia. Nyakati nyingine, Yesu Kristo alitafuta mahali patulivu ili kusali na kutafakari. (Marko 1:35) Je, wewe pia hujifunza katika mazingira matulivu, yasiyo na kelele? Ikiwa hufanyi hivyo, huenda unazuia ukuzi wako wa kiroho.

Fanya Uchaguzi Unaofaa

Kwa kweli, muziki ni zawadi kutoka kwa Mungu, lakini unapaswa kujihadhari usiitumie vibaya. Usiwe kama msichana anayeitwa Marlene, anayesema: “Nina muziki ambao ninajua ninapaswa kuutupilia mbali. Lakini ni mtamu wee.” Fikiria madhara anayosababisha katika akili na moyo wake kwa kusikiliza muziki usiofaa! Usinaswe na mtego huo. Usikubali muziki ukupotoshe au utawale maisha yako. Chagua muziki unaopatana na viwango vya Kikristo. Mwombe Mungu akusaidie. Tafuta marafiki walio na maoni kama yako.

Muziki unaweza kukustarehesha na kukuburudisha. Unaweza kukuondolea hisia za upweke. Hata hivyo, hautatui matatizo yako. Isitoshe, nyimbo haziwezi kulinganishwa na marafiki wa kweli. Kwa hiyo, usiruhusu muziki uwe jambo kuu maishani mwako. Furahia muziki, lakini usikubali ukutawale.


Unahitaji kujiburudisha mara kwa mara. Kanuni za Biblia zinaweza kukusaidia jinsi gani unufaike kutokana na pindi hizo zenye kufurahisha?

MAANDIKO MUHIMU

Je, sikio halipimi maneno kama kaakaa linavyoonja chakula?Ayubu 12:11.

PENDEKEZO

Ikiwa unataka wazazi wako waelewe ni kwa nini unapenda muziki au bendi fulani, kwanza jaribu kupendezwa na baadhi ya miziki wanayofurahia.

JE, WAJUA . . .?

Ikiwa hupendi wazazi wako wasikilize muziki unaopenda sana, basi huenda muziki unaosikiliza una kasoro.

HATUA ZA KUCHUKUA!

Ninaweza kuwa na usawaziko kuelekea muziki niki ․․․․․
Vijana wenzangu wakinishurutisha nisikilize muziki usiofaa, nitawaambia ․․․․․
Mambo ambayo ningependa kuuliza mzazi (wazazi) wangu kuhusu habari hii ni ․․․․․

UNA MAONI GANI?

Kwa nini uchaguzi wako wa muziki ni wa maana sana?
Unaweza kuamua jinsi gani ikiwa wimbo fulani unafaa au haufai?
Unaweza kufanya nini ili ujifunze kufurahia miziki ya aina nyingine?

‘‘Wakati mwingine mimi hujikuta nikisikiliza muziki usiofaa. Nauzima bila kukawia. Nisipofanya hivyo mara moja, nitaanza kutafuta visababu vya kuusikiliza.’’—Cameron

Jifunze Kufurahia Miziki ya Aina Nyingine

  Je, unapenda aina nyingi zaidi za chakula leo kuliko ulipokuwa na umri wa miaka mitano? Ikiwa ndivyo, ni kwa sababu umejizoeza kufurahia ladha ya vyakula vipya. Ndivyo ilivyo na muziki. Usisikilize muziki wa aina moja tu. Jifunze kupendezwa na miziki ya aina nyingine.

  Njia moja ya kufanya hivyo ni kujifunza kupiga ala fulani ya muziki. Kufanya hivyo kunaweza kukuchangamsha na kukuridhisha na pia kutakufanya upendezwe na aina nyingine ya muziki mbali na ile inayopigiwa debe na wafanyabiashara. Utapata wapi wakati wa kujifunza? Unaweza kupunguza wakati unaotumia kutazama televisheni au kucheza michezo ya kompyuta. Ona yale ambayo vijana hawa wanasema.

“Kupiga ala ya muziki ni raha na kunaweza kuwa njia bora ya kuonyesha hisia zako. Kujifunza kupiga nyimbo mpya kumenisaidia kupenda aina mbalimbali za muziki.”—Brian, mwenye umri wa 18, ambaye hupiga gitaa, ngoma, na piano.

“Unahitaji kufanya mazoezi ikiwa unataka kujifunza kupiga vizuri chombo fulani cha muziki. Na mazoezi hayafurahishi sikuzote. Lakini kuwa stadi wa kupiga muziki fulani ni jambo lenye kufurahisha na kuridhisha kwelikweli.”—Jade, mwenye umri wa miaka 13, ambaye hupiga fidla.

“Ninapokuwa nimechoka au kushuka moyo, kupiga gitaa hunisaidia kustarehe. Kutunga muziki mzuri na wenye kutuliza na kuburudisha ni jambo lisilo na kifani.”—Vanessa, mwenye umri wa miaka 20, hupiga gitaa, piano, na zumari.

“Nilikuwa nikijiambia, ‘Sitawahi kuwa na ustadi kama fulani wa fulani.’ Lakini niliendelea kufanya mazoezi, na sasa ninapata uradhi ninapopiga wimbo fulani vizuri. Sasa, nawavulia kofia wanamuziki wengine stadi.”—Jacob, mwenye umri wa miaka 20, hupiga gitaa.

Muziki ni kama chakula. Unahitaji aina inayofaa kwa kiasi kinachofaa. Aina mbaya, hata iwe ni kiasi gani, ni hatari

Ijumaa, Februari 14, 2014

MPIGAJI MZURI WA PIANO


Eldar Nebolsin wa nchi ya Uzbekistani ni mpigaji wa piano mwenye kujulikana katika mataifa mengi. Alicheza piano katika vikundi vya wanamuziki huko Londres, Moscow, Saint Petersburg, New York, Paris, Roma, Sydney, Tokyo, na Vienna.

Eldar alikulia katika Muungano wa Kisovieti na hakuamini kwamba kuna Mungu. Lakini baadaye alikubali kwamba wanadamu waliumbwa na Muumbaji mwenye upendo.

KISA CHA AJABU...

Sikuzote nyumba yetu ilijaa vitabu ambavyo baba yangu alinunua katika mji wa Moscow. Kuna kitabu ambacho kilinivutia sana ni kitabu kilichokuwa na habari za Mungu. Biblia ilieleza kuhusu mwanzo wa mwanadamu na mambo ambayo yaliwapata Waisraeli.

Nilipohamia Hispania katika mwaka wa 1991 ili kujifunza muziki, nilibeba kitabu hicho na nikakisoma mara nyingi. Nilivumbua imani ambayo haitegemei tu namna mtu anavyojisikia moyoni lakini pia mambo yenye kupatana na akili na yenye nguvu ya kiroho.

Fundisho ambalo lilinivutia kabisa ni ahadi ya Biblia kwamba wanadamu wanaweza kuishi milele. Fundisho hilo lilikuwa lenye kueleweka bayana kabisa!

USHAURI WAKE...

Biblia ni kama muziki mzuri sana wa PIANO wenye mpangilio wa ajabu, na ina ujumbe wenye kuchochea kwa ajili ya wanadamu wote.

Jumapili, Februari 02, 2014

SANAA NA MUZIKI WA INJILI

Mpendwa katika Bwana ni ombi langu kwa Mungu akubariki unaposoma somo hili ili uweze kufahamu mambo ambayo ulikuwa huyajuwi au kukumbuka yale ambayo unayajua lakini ulikuwa umeyasahau. Kipengele hiki kidogo cha somo hili nimekitoa katika makala ninayoandaa na hivyo, ni tamanio la moyo wangu kuwa litaeleweka vizuri kama somo lililokamilika kwa lengo hili na kwa wakati huu. Kama wewe ni mwanamuziki, mwimbaji au tu mdau wa muziki, basi naamini utapata jambo la kujifunza kwa kipindi hiki unaposoma.

Muziki, pasipo kujali unatumikaje, ki taaluma huwa uko katika eneo la Sanaa. Vitu vyote vyema vinatoka kwa Mungu(Yakobo1:17). Tunafahamu kuwa vitu vyote tulivyonavyo chanzo chake ni Mungu mwenyewe na vikitumika vyema, huonyesha sura fulani ya Mungu wetu. Hivyo mwana sayansi mkuu ni Mungu na mwana sanaa mkuu pia ni Mungu mwenyewe. Mungu kama mwana sanaa alipanga vitu vyote katika picha na kama mwana sayansi akatumia sayansi na sanaa kuviumba na kuviweka viwepo hata leo. Naamini kupitia sanaa ya Mungu, ndipo usemi maarufu wa Biblia, “Mungu akaona yakuwa ni vyema” ulirudiwa mara kwa mara katika kitabu cha Mwanzo.

Saana ina uwezo mkubwa sana kuunganisha vyema vitu visivyoonekana wala kusikika na kuvileta katika ulimwengu unaoonekana na kusikika. Mchoraji anaweza kuunganisha mistari na kuonyesha picha ya kitu fulani. Hivyo hivyo, mwana muziki au mwimbaji anaweza kuweka nota na milio tafauti tofauti na kutengeneza wimbo au muziki unaosikika vizuri.

Ni jambo la ajabu sana kuwa neno ‘Msanii’ limetumika vibaya sana katika sehemu hii ya dunia tunayoishi kufikia wasanii kuanza kuchukia kuitwa/kutambulishwa hivyo. Hata hivyo, ingekuwa ajabu pia kwa Ndovu kukataa kuitwa Ndovu kwa kukuta Fisi akiitwa Ndovu. Daktari hawezi kukataa kutambulishwa kama Daktari kama jina Daktari litatumika vibaya. Kwa nini Msanii akatae kuitwa hivyo kwa sababu jina hilo limetumika vibaya? Kwa hivyo, Msanii katika Kanisa lazima ajivunie kuwa Mungu amempa huduma ya kutumia Sanaa hiyo kumtumikia kama vile Injinia anavyoweza kujivunia kutumia taaluma yake ya ujenzi kwa ajili ya kujenga nyumba ya kuabudia Mungu. Mungu ameweka Sanaa ya Muziki ili utaalamu huo utumike kuleta sifa nyumbani mwake. Kwa maana hiyo, ni vyema wana muziki wakajitahidi kukuza taaluma hiyo kwa elimu ya kiroho na ya asili pia inayohusu muziki.

Ki ujumla, sanaa hutumia uwezo wa kuwaza na kufikiria na kutumia (imagination)
kwa upana sana, ambako huleta picha hiyo kuonekana au kusikika. Tofauti na taaluma nyingine, sanaa hutumia ubunifu(creativity) mwingi kwa sababu sheria na kanuni zake hazijabana sana tofauti na sayansi ambayo kanuni zake na mahesabu yake yako ya ki-vipimo zaidi. Hivyo, sanaa ina uwezo wa kubuni mambo mapya sana. Kwa mfano, muziki wa Jazz ulipobuniwa na watu weusi huko Marekani, watu walipinga uhalali wake huku wakisema kuwa kanuni za ki-muziki zimevunjwa. Lakini baada ya muda, muziki wa Jazz uliongezeka umaarufu wake na baadae ukakubalika kuwa muziki halali.

Muziki kama sanaa nyingine hutumia hisia nyingi ili kufikia walengwa.  Kwenye taasisi tatu za mtu, yaani roho, nafsi na mwili ambazo humfanya mwanadamu kuwa mwanadamu, nafsi hutumika kwa asilimia kubwa sana kufanya kazi ili kutengeneza na kuhudumu katika sanaa. Katika nafsi, kitengo cha hisia ndicho kinachofanya kazi kubwa ya ziada kufanya sanaa,(sisi hapa tukihusika na muziki.) Kwa hivyo tunapoenda kuongea muziki moja kwa moja, tunafahamu kuwa mambo mengi yanayowaathiri wana muziki na waimbaji, basi yanaathiri wana sanaa kwa ujumla wake.

Naamini kuwa wote tunakubaliana kuwa wanamuziki na waimbaji ni watu wa hisia nyingi. Ndivyo Mungu alivyowaweka duniani ili watumike kufariji, kufurahisha na kuonyesha huzuni ili kuhudumia jamii. Kwa sababu ya hisia nyingi zinazotumika katika muziki, wakati mwingine, ni rahisi kwa wanamuziki na waimbaji hawa kukosa mwelekeo, mizani na vipimo(balance), wingi au upungufu wa hisia unapotokea. Jinsi ya kujitunza ki-hisia, basi, huwa ni jambo la muhimu sana, jambo ambalo wengi wao hawajui, ili wasije wakafanyika kituko badala ya suluhisho katika jamii.

Kupitia hisia kuwa na sehemu kubwa ya mchango katika maisha ya mwanamuziki na mwimbaji, itaonekana jinsi ya kuvaa na staili zake za maisha kwa ujumla zilivyo tofauti sana na za watu wengine katika jamii. Hapa, hatuwezi kuwaambia wabadilike wasiwe hivyo, maana mara nyingi hicho huwa ni kitambulisho cha taaluma yao, ila wanahitaji tu kudumisha kiasi tu, ili wasipitilize, na pia wasifanye kwa kuiga.

Sasa, mtu yeyote anayetoa huduma katika jamii, lazima ajifundishe kurudisha katika maisha yake kile kinachotoka anapohudumia jamii ile. Kwa mfano, mwana riadha anahitaji ale chakula kizuri, apumzike, ajiweke vizuri ki saikolojia ili asihudumie jamii na baadae maisha yake yakaharibika. Anapofanya mazoezi na hatimae kushindana, anahitaji ajue ni chakula gani cha kutumia ili arudishe nguvu na kadhalika. Mtumishi wa kiroho, kama mchungaji anahitaji aombe na kuabudu Mungu, asome neno na kuwa na ushirika mzuri na pia kupumzika ili arudishe nguvu anazotumia katika huduma yake. Vile vile, mwanamuziki na mwimbaji wa nyimbo za injili  lazima ajue jinsi ya kurudisha nguvu anayotumia ikiwemo ya ki hisia ili aweze kuhudumu bila maisha yake mwenyewe kuharibika.

Huduma ya muziki na uimbaji ina shamrashamra nyingi, makelele mengi na kuhudumia mbele ya umati au watu wengi. Ni rahisi jambo hili likaingia vibaya katika akili ya mwimbaji au mwanamuziki huyo na kuanza kuishi katika ‘ulimwengu’ usiyo halisi. Ile kushangiliwa na muonekano wa kugusa umati au watu wengi unaweza ukaweka picha isio ya halisi katika maisha ya mtu huyo na akaanza kuishi maisha tu ya juu juu. Ikumbukwe kuwa mwanamuziki na mwimbaji wa nyimbo za Injili ni mwanadamu na hivyo ana mapito yake katika maisha. Tafakari sasa kuwa amekuwa na wakati mbaya katika maisha yake na sasa ana huzuni lakini hapo hapo anatakiwa kusimama mbele za watu na kuwafurahisha au kuwatia moyo. Anatakiwa hapo hapo atumie hisia yake kuwafurahisha watu wakati yeye mwenyewe ki-hisia yuko chini. Pasipo Mungu kuwa naye na kumsaidia katika huduma yake, hali hii inapotokea mara kwa mara, inaweza ikamchanganya ki-hisia.  

Kwa sababu ya umuhimu wa hisia katika maisha ya mwanadamu yeyote, hisia zinapochanganyikiwa, mwanadamu hujikuta katika ulimwengu usiyo halisi na  kuwa kituko katika jamii, huku yeye akiona kuwa yuko sawa.

Kwa nini Neno ‘Msanii’ limetumika vibaya?

Kwa nini neno Msanii limetumika kuonyesha utovu wa maadili? Ningependa (nikiwa na uchungu mwingi moyoni) kuangalia sababu ya jina Msanii kutumika kuonyesha sifa mbaya katika jamii. Hili linaniumiza kwa sababu na mimi nina taaluma ya sanaa. Imekuwa tabia ya watu wengi katika sehemu hii ya ulimwengu tunayoishi kutumia neno hili kuonyesha mtu tapeli, muongo asiyeeleweka na kadhalika.

Sifa ya sanaa ni kuonyesha picha ya kitu kilichopo au ambayo msanii anataka  kuitengeneza ili ionekana kama wazo katika jamii. Kwa mfano, msanii mwimbaji anaweza kutumia sanaa kukuonyesha mambo yaliyopo katika jamii. Anaweza kuimba wimbo wenye hadithi ya fulani hata kama sio picha halisi ya maisha yake. Anaweza kuimba wimbo kuwa anataka kuolewa na kupata watoto wengi hata kama ki halisi hataki hata mtoto mmoja. Mwimbaji anaweza kukupa picha ya maisha ukafikiri kuwa ndivyo alivyo, kumbe sivyo hivyo. Kupitia hili, Msanii ameonekana kama kuwa mwongo fulani hivi. Ameonekana kama mtu anayeweza kuichora picha yoyote  na kujionyesha mtu ambaye siye katika jamii.

Muziki umetumika kujibizana na hata kugombana na kutukanana, mwimbaji mmoja na mwingine. Mambo ambayo yameleta picha ya sanaa kutumika kuwa chombo cha (kumfagilia) kumsafishia jina msanii husika. Kwa sababu ya nguvu ya sanaa, wasanii wengi wameitumia kwa faida binafsi kujitengenezea nafasi katika jamii, badala ya kuihudumia jamii ile.

Kwa sababu hapa tunaangalia sanaa ya muziki katika nyumba ya Mungu, ni vyema tutoe tahadhari kuwa Muziki wa Mungu unatakiwa kumtukuza Yeye, kuhudumia kundi lake na kusaidia kuleta wengi katika kundi hilo. Muziki na vipawa vyote katika nyumba ya Mungu vinatakiwa kutumika kwa utukufu wa Mungu na hivyo sio kwa ubinafsi. Kwa sababu hiyo wana muziki katika nyumba ya Mungu wasiwe kama wa dunia ambao wanaimba nyimbo kuhamasisha jamii kuhusu jambo moja huku wao wakifanya kinyume. Mwanamuziki au muimbaji wa Mungu asiimbe kuwa yeye anapenda kuomba wakati sio kweli maana hapo ndipo atakapoonekana na watu kuwa ‘Msanii’ kwa kinyume cha matumizi ya jina hilo. Hili limeonekana kwa watu wengi wanaoimba nyimbo za injili na za kusifu na kuabudu kuwa wanachoimba na wanachofanya ni vitu viwili tofauti. Mungu asaidie ili neno hili linapotumika kinyume duniani, katika nyumba ya Mungu, Msanii awe ni chombo cha heshima cha kumtukuza Mungu na si vinginevyo.

Jambo lingine ambalo hufanya neno ‘Msanii’ kutumika vibaya ni kwa sababu ya kitu ambacho nimegusia awali kuwa, wengi wao huchanganyikiwa kwa kuzidiwa na msongamano wa hisia katika maisha yao na hivyo kuonekana kuishi maisha yasio halisi, na hivyo mtu yeyote anayeonekana kudhihirisha aina hii ya maisha hufananishwa na wasanii waliofanyika hivyo. Hivyo huonekana kama vile ndio maisha ya wasanii kuishi katika maisha ambayo sio ya kawaida na watu wengine, kwa kuvaa kwao labda na hali zingine ambazo huonekana maishani mwao. Wanamuziki na waimbaji wanaohudumu katika nyumba ya Mungu wanatakiwa kuonyesha mfano katika maisha yao ili waonekane kuwa ni wahudumu zaidi kuliko tu kuonekana kuwa ni waimbaji, kwani vipawa vyao vinatakiwa kudhihirisha tabia fulani ya Mungu.Njia ya kufuta dhana hii katika waimbaji na wanamuziki walio katika nyumba ya Mungu ni kushinda majaribu ambayo huwalenga na kuishi kwa Imani zaidi kuliko ki hisia, kwani, Biblia inasema tunaishi kwa Imani na sio kwa yale tunayoyaona na kuyahisi. Kwa hivyo wajenge nguvu ya kiroho katika maisha yao na waongozwe na Roho Mtakatifu.

Jambo jingine ni kuomba uongozi wa Mungu kwa Roho Mtakatifu ili nyimbo zao ziwe zinatokana na njaa na kiu ya Mungu na haki yake katika maisha yao, ili wasije wakaimba nyimbo ambazo wanawaelekeza watu wafanye yale ambayo wenyewe hawayafuati.

La mwisho, katika somo hili, ni kuomba kipawa chao kiambatane na neema iliyo juu ya maisha yao ili kipawa kisiwapeleke juu zaidi kuliko neema inayoweza kuwalinda katika kiwango  hicho. Pia waweze kuwa na afahamu wa kujua milango inayofunguka kwao, kama ni  Mungu aliyefungua au ni wanadamu maana mara nyingi hapo ndipo watu hupandishwa  na kujikuta mahali ambapo hakuna neema ya kumlinda mtu katika kiwango alichopandishwa. Hivyo wawe pia na ujasiri wa kufuata tu njia ambayo Mungu anatengeneza.

Muziki una nguvu yake wenyewe.Ni jambo la muhimu kujua kuwa Muziki kama Muziki una nguvu ya ajabu sana, ukiachilia mbali kuwa unaweza kuubeba upako. Kwa maana nyingine, muziki una uwezo ndani yake wa kujitegemea bila kujali ni nani anayeutumia. Muziki una nguvu kwa sababu ya asili ya ulivyoumbwa. Kama chombo cha mawasiliano, kuna uwezo ndani ya muziki ambao husaidia kuleta ujumbe katika jamii lengwa. Labda kwa sababu hii, ndio maana huduma ya muziki na uimbaji imebeba umuhimu mkubwa sana nyumbani mwa Mungu. Inawezekana umuhimu mkubwa ni ukubwa wa muziki wenyewe na sio tu kutokana na wana muziki na waimbaji wenyewe. Kwa sababu hii, watu walio katika huduma hii wanaweza kujibebea heshima kubwa bila kujua kuwa chombo chenyewe ndicho muhimu kuliko wenyewe.
Muziki ni chombo cha muhimu sana katika uumbaji wa Mungu kwa hiyo kinabeba nguvu nyingi sana na hivyo kinatumika kwa ajili ya kuleta mabadiliko makubwa sana katika uumbaji mwingine wa Mungu. Kipawa cha muziki, basi, kina uwezo wa kumuonyesha mwanamuziki na muimbaji katika hali fulani ambayo asipojiangalia, anaweza akajitafsiri katika hali ambayo sio halisi katika maisha yake. Anaweza kujisifu na kujiona yuko katika kiwango fulani cha ki-maisha ambacho sio halisi katika maisha yake, kumbe tu ni kwa sababu ya nguvu iliyo katika muziki wenyewe. Hata hivyo, nguvu ya muziki iko sana katika kugusa hisia za nafsi, na hivyo kutegemea nguvu ya kiroho kuleta mguso katika maisha ya kiroho. Katika muziki, maisha ya watu wanaohudumiwa, wanaweza kuguswa katika kiwango cha ki-hisia tu au, wakaguswa katika kiwango kingine, wakafikiwa katika maisha ya kiroho.

Sasa hapa ndipo tunapogundua umuhimu wa kipawa au talanta ya muziki kushukiwa na kipawa au karama ya kiroho. Wako wanamuziki wengi wa duniani kwa kujua hili wanatafuta nguvu za giza kwa kwenda kwa waganga/wachawi au hata kutafuta kuabudu mashetani ili wawe na mguso wa kiroho. Sisi tulio katika nyumba ya Mungu tunatafuta kwa Mungu uwezo na vipawa vya kiroho ili karama ishuke juu ya talanta na hivyo kugusa, sio tu nafsi na hisia zake bali roho ya mtu au maisha yake ya kiroho. Kipawa cha kimwili(talanta/kipaji) hakiwezi kugusa rohoni. Kipawa cha kiroho(karama) hugusa rohoni. Kwa hivyo vyote ni muhimu, ila tunajua kuwa vitu vya kimwili ni vya muda na vya kiroho ni vya kudumu.

Kuna mifano mingi katika Biblia ambayo inaonyesha talanta za ki-muziki ambazo zilishukiwa na karama za rohoni. Tunafahamu hadithi ya Daudi katika 1Samueli 16:23 “Ikawa ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa na, na ile roho mbaya ikamwacha.” Hapa kuna ufunuo mwingi sana. Kwanza, muziki ulimburudisha Sauli, kama vile tulivyoona hapo juu kuwa muziki una nguvu wenyewe na la pili, Sauli aliondokewa na roho mbaya, ambayo ni kipawa au karama ya kiroho ambayo ilifanya kazi hiyo. Pia kuna wazo hilo la ‘roho mbaya kutoka kwa Mungu’ ambapo watumishi wengi hutafsiri kuwa ni roho iliyoruhusiwa na sio kuwa ilitoka kwa Mungu wakisema kuwa Mungu hana roho mbaya. Wengine pia husema ni aina ya roho ya ghadhabu ambayo inatafsirika kuwa ni mbaya. Hata hivyo la muhimu kujua hapa ni kwamba ukombozi ulitokea kwa Sauli wakati Daudi alipopiga muziki.

Andiko jingine ni pale Nabii Elisha alipohitaji mwanamuziki katika 1Wafalme 3:14-15. “Elisha akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe. Ila, sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga mkono wa Bwana ukamjia juu yake. Akasema, Bwana asema hivi……..” Hapa, kuna hadithi ya nabii ambaye amekwazika kumuona adui ambaye alikuwa mfalme muovu. Lakini kwa ajili ya Yehoshefati, Elisha akaheshimu uwepo wake na akaomba mwanamuziki ambaye alipopiga muziki ule, upako ukaja juu ya Elisha na akatabiri. Hapa tunaona talanta/kipaji ya muziki ikishukiwa na karama ya unabii ambayo ilifanya kazi juu ya nabii Elisha. Kwanza nguvu ya muziki ilimuondolea Elisha kukwazika kwa kumfurahisha na pili, karama ya unabii ilichochewa na karama iliyokuwa juu ya mwanamuziki yule.

Na mwisho, kwa sasa katika mifano, tunaona katika 1Mambo ya Nyakati 25, mara kwa mara ikisemekana kuwa wana muziki waliochaguliwa na mfalme Daudi na viongozi wa kiserikali walipewa kazi ya kutabiri kupitia muziki, katika msari wa 2, “…..walioamriwa na Asafu aliyetabiri kwa amri ya mfalme” na mstari wa 3, “…..watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu Bwana.” Wana muziki na waimbaji wanatakiwa kuheshimu kuwa Mungu amewapa talanta za kumtumikia Yeye, lakini pia watafute karama za Roho Mtakatifu ili wanapogusa watu wa Mungu, basi iwe katika maisha yao yote kwa ujumla.

Ninaamini kuwa Mungu amekupa kitu chema cha kukusaidia ili uweze kutoa mchango wako katika huduma hii kwa ajili ya kuiboresha.

Jumapili, Desemba 01, 2013

HUDUMA ZA MUZIKI WA KIADVENTISTA


Huduma za muziki kwenye kanisa la Waadventista Wasabato na kwenye makanisa mengine ya Kikristo ni somo lenye utata na linalovuta usikivu wa watu. Kuna mitazamo inayokinzana iliyopo juu ya namna gani chombo kinaweza kutumika kuboresha huduma zetu za ibada na katika kuongoa roho kwa ajili ya Kristo. Kuvutia usikivu wa watu ni kwa lazima kwa sababu ya kule kuvuka mipaka kunakofanywa na pande zote mbili zinazohusika na somo hili. Shetani husherehekea tunapoenda nje ya mipaka ya misimamo yetu.
Tunauafiki mswaada mzuri kuhusiana na somo hili ulioandaliwa na kuwasilishwa na mchungaji Rei Kesis – Chaplensia wa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki (EUAB), akishirikiana na Idara ya Tiolojia ya UEAB, chini ya usimamizi wa mwenyekiti waIdara – Dr. Lameck Miyayo. Ilikuwa ni kazi njema na tuliyahimiza makanisa yetu yote kunufaika nayo. Unaweza kuupata kwenye ufunguo wa waraka huu.

Katika sehemu hii tutajielekeza kwenye uelewa wa Kanisa la Waadventista Wasabato, kuhusiana na nafasi na usimamizi wa muziki kwenye huduma za ibada. Tutaiangalia Kanuni ya Kanisa, ambacho ni kitabu cha msingi cha sera chenye viwango na kawaida za kanisa zinazotumika kusimamia makanisa yote mawili; lile la mahalia na yale ya ngazi za juu.

Kanuni hizi zilizopo kwenye kanuni za kanisa, zilizojengwa kwenye Biblia na zilizojikita kwa Kristo zinawakilisha uelewa wa kanisa wa wakati huu, kuhusiana na maswala mbalimbali ya kanisa yanayoathiri mahusiano yetu, kama mwili wa waumini, na kama mtu mmoja mmoja. Tunawasihi watumiaji wote wa muziki na viongozi wa kanisa kuwa na hamasa kubwa ya kuelewa kanuni hizi na kuzisimamia kama walinzi waaminifu wa kuta za Zayuni.

Kile Kanuni ya Kanisa inachosema kuhusu Muziki

Angalizo: Nukuu imechukuliwa kutoka “Kanuni ya Kanisa la Waadventista Wasabato ya 2010, toleo la Kiingereza. Kupigiwa mistari, kukolezwa kwa wino na mlalo wa maandishi vimeongezwa. Maoni ni mapendekezo na maelekezo yetu ya uongozi.

“Muziki ulitengenezwa kutumikia makusudi matakatifu, kuyainua mawazo hadi kuwa kitu safi, bora na kilicho juu, na kuamsha rohoni hali ya ibada na shukrani kwa Mungu.” – DA 73, (CM, 143)

“Muziki ni mojawapo ya sanaa ya kiwango cha juu sana. Muziki mzuri si tu unatupatia maburudisho bali pia huyainua mawazo yetu na kukuza viwango vyetu bora. Mungu  mara nyingi ametumia nyimbo za kiroho kugusa mioyo ya wadhambi na kuwaongoza kwenye toba. Kinyume chake, muziki duni unashusha hali ya kiroho na kutupeleka mbali na mahusiano yetu na Mungu.” – (CM, 143)

“Ni lazima tutumie uangalifu mkubwa katika uchaguzi wa nyimbo majumbani mwetu, kwenye mikusanyiko ya kijamii, mashuleni, na makanisani. Mrindimo wowote wenye vionjo vya jazz, rock, au mtindo uliochanganya hayo, au lugha yoyote inayooonesha hisia za kipumbavu au zisizo na maana itaepukwa.” – (Angalia CM, pp. 92, 96, 143.)

MAONI:
  • “Kuimba, kama sehemu ya huduma ya kidini, ni tendo la ibada kama lilivyo ombi.” Patriachs and Prophets Uk. 594. Maombi hukuza tabia kwa sababu kupitia maombi tunauona uso wa Yesu, na kwa kumwangali tunabadilishwa na kufanana naye. Muziki mzuri ni wakala wa ujenzi wa tabia. (2 Wakorintho 3:18).
  • Muziki wa Jazz, Rock au mtindo uliochanganya hayo mawili haipaswi kuruhusiwa makanisani.
  • Angalia kwa makini tuni, mwafaka, na mrindimo; haya yote hayapaswi kufuata muziki wa kidunia.
Nguvu ya muziki – “Muziki unaweza kuwa nguvu kubwa kwa mema, na bado hatulitumii vya kutosha tawi hili la ibada. Uimbaji kwa ujumla unafanyika kwa misisimko au kwa kukidhi jambo maalumu, na kwa nyakati zingine wale waimbao huachwa waendelee kukosea, na muziki hupoteza athari yake stahiki kwenye akili za wale waliopo. Muziki ni lazima uwe na uzuri, uchungu, na nguvu. Hebu sauti ziinuliwe katika nyimbo za sifa na za kujitoa. Vitumie kama nyenzo pale inapowezekana vifaa vya muziki, na uachilie muafaka wa utukufu upande kwa Mungu, zawadi inayokubalika.” – 4T 71 (CM, 114).

MAONI
  • Mwongozaji wa nyimbo ongoza vema. Epuke makosa ya kawaida.
  • Mwongozaji anahitaji kuwa na yafuatayo: Kitabu cha nyimbo chenye alama za muziki za tonic sol-fa au staff notation, chombo cha kuchagulia key kiitwacho Pitch pipe, na kipande cha fimbo kwa kuongozea kunakoonekana na wote.
  • Matumizi ya ala za muziki yameruhusiwa. Matumizi mabaya yamekatazwa. Ni afadhali kutotumia ala kabisa kuliko kutumia vibaya na kuwa mtego na laana kwenye ibada kwako mwenyewe na waabuduo wengine.
Imba kwa roho na uelewa – “Katika jitihada zao za kuwafikia watu, watumishi wa Bwana hawapaswi kufuata njia za dunia. Katika mikutano inayofanyika wasitegemee waimbaji wa kidunia na maonesho ya kwenye majukwaa kuamsha usikivu. Wanawezaje wale wasio na hamu ya Neno la Mungu, ambao kamwe hawajawahi kusoma Neno lake kwa nia ya dhati ya kutamani kuelewa ukweli wake, kutegemewa kuimba kwa roho na kwa kuelewa?... Kwaya ya mbnguni inawezaje kujiunga na muziki ulio wa mtindo tu?... “Uimbaji haupaswi daima kufanywa na wachache. Mara nyingi kwa kadri inavyowezekana, hebu na tuache kusanyiko lote liimbe.” – 9T 143, 144 (CM, 114).

MAONI
  • Huduma zetu za ibada hazipaswi kuongozwa au kuhudumiwa na waimbaji wasiomwabudu Mungu  wa kweli katika njia ya kweli.
  • Muda mwingi unahitaji kutumika kwa uimbaji wa wote, na muda mchache unapaswa kutumika kwa kwaya na vikundi vya uimbaji. Kila Sabato kabla ya vipindi vya Shule ya Sabato, hebu kuwe na angalau dakika za kuimba na kujifunza nyimbo mpya. Dakika 15 zingine zinapaswa kuwa baada ya Shule ya Sabato na kabla ya huduma kuu. Hebu dakika 15 zitengwe baada ya shule ya sabato na kabla ya ibada kuu kwa ajili ya uimbaji wa pamoja. Ratiba ya kwaya na vikundi vya nyimbo iendelezwe ili kuzipa kwaya fursa ya kuimba pamoja na nyimbo nyingine zilizoandaliwa. Ratiba ihusishe ibada za maombi ya katikati ya juma na ufunguzi wa Sabato. Kwaya zinapokuwa nyingi, usiendekeze maombi mengi ya kutaka nyimbo zilizoimbwa au zile zinazopendwa sana zirudiwe. Hii itumike kunapokuwa na kwaya nyingi zinazosubiri zamu yao ya kuimba.
Kila idara inaweza kuwa na viongozi wa muziki. Viongozi wawili wanaosisitizwa sana ni hawa:

Shule ya Sabato:
“Baraza linaweza kumteua Mkurugenzi wa Muziki wa Shue ya Sabato kwa kushauriana na viongozi wa vitengo. Kama namna ya kuonyesha ibada, muziki unapaswa kumtukuza Mungu. Waimbaji na wanamuziki wengine wanapaswa kuchaguliwa kwa uangalifu kama viongozi wa maeneo mengine ya huduma za Shule ya Sabato na wanapaswa kupimwa kwa viwango vilevile. (Angalia uk. 92, 144). Baraza pia linaweza kumteua mpiga kinanda wa vitengo vingine”. (CM, uk. 96)

Vijana Waadventista:
Maafisa wa AYS – “Kanisa huwachagua maafisa hawa wa AYS: Kiongozi wa Vijana, msaidizi wa kiongozi wa vijana, Katibu-mtunza hazina, msaidizi wa Katibu-mtunza hazina, mwongozaji wa nyimbo, mpiga kinanda, na mdhamini (ambaye anaweza kuwa mzee). Kwa kuwa muziki unachukua nafasi muhimu katika kuunda tabia za vijana, waimbaji hawana budi wachaguliwe kwa uangalifu kama maafisa wengine wa AYS”. (Angalia uk. 92, 96.) (CM, 102)

Kuchagua Waratibu wa Muziki – “Kanisa ni lazima lichukue uangalifu mkubwa katika kuwachagua viongozi wa kwaya, ikiwachagua wale tu waliojitoa kabisa na wanaotoa nyimbo sahihi kwa huduma zote za ibada za kanisa na mikutano. Muziki wa kidunia au ule wenye asili iletayo maswali, kamwe usiingizwe kwenye huduma zetu.” (CM, 92).

“Viongozi wa nyimbo ni lazima wafanye kazi kwa ukaribu sana na wachungaji na wazee wa makanisa ili kwamba uchaguzi wa nyimbo uoane na wazo kuu la hubiri. Kiongozi huyu wa nyimbo yupo chini ya usimamizi wa mchungaji au wazee wa kanisa na hafanyi kazi kwa kujitegemea. Kiongozi wa nyimbo anapaswa kushauriana nao kuhusu nyimbo zitakazoimbwa na uteuzi wa waimbaji na wanamuziki.” – (CM, uk. 92)

Idara na Huduma zinatakiwa kuteua Wakurugenzi wa muziki, na kulitaarifu baraza la kanisa ili liwapitishe wale waliochaguliwa. Uchaguzi wa viongozi wa muziki wa idara za Shule ya Sabato na Vijana umefafanuliwa na kusisitizwa.

Uangalifu mkubwa utumike katika kuchagua viongozi wa muziki makanisani. Baraza la kanisa ni lazima libatilishe/liidhinishe viongozi wote wa vikundi/kwaya zote ambazo kanisa limevisajili. Kila idara ichague kiongozi wake na kupeleka kwenye baraza la Kanisa ili kubatilisha au kuidhinisha..

Kanisa linaweza kuwa na viongozi kadhaa wa muziki wanaoongoza nyimbo kwenye idara zao, huduma, au makundi. Lakini kanisa ni lazima lichague mkurugenzi mmoja wa muziki, msaidizi/wasaidizi, kutegemeana na mahitaji ya kanisa, watakaoratibu viongozi wengine wote wa muziki kutoka idara mbalimbali za kanisa, huduma au vikundi. (CM, 171).

Mratibu wa muziki ni mjumbe wa baraza la kanisa. – (CM, 125). Huchaguliwa na kibaraza cha uchaguzi. (CM, uk. 171)

Mkurugenzi/Mratibu/Kiongozi (Mratibu Mkuu) wa muziki wa kanisa):
  • Ni mjumbe wa baraza la kanisa.
  • Ni lazima apimwe na kiwango kile kile cha juu kilichotumika kuwachagua viongozi wengine wa kanisa.
  • Ni kiongozi muhimu asaidiaye maandalizi ya ibada. Hufanya kazi chini ya “Msimamizi wa Mimbari/Ibada”. – (Wachungaji na Wazee wa Kanisa)
  • Ndiye anayepaswa kuchagua nyimbo na waimbaji watakaoendana na wazo kuu la hubiri la siku hiyo.
  • Ndiye atakayeandaa ratiba ya Kwaya (waimbaji)/Vikundi vya Waimbaji, Waimbishaji, na Ala za muziki ikiwa zitakuwepo.
  • Ndiye atakayehamasisha na kusimamia filosofia ya Biblia/Kanisa kuhusu muziki.
  • Makanisa yaweza kuunda Kamati ya Muziki itakazoongozwa na Mratibu wa Muziki wa Kanisa itakayosimamia huduma za muziki kanisani. Wajumbe wa baraza hili wanaweza kuwa wasaidizi wa Mratibu mkuu (anaweza pia kutumika kama katibu wa kamati), waratibu wa muziki kutoka kwenye maidara, na viongozi wakuu wa kwaya. Wajumbe wengine wanaweza kuwa viongozi wa Chama cha Vijana, Mkurugenzi wa Huduma za Watoto, na Mkurugenzi wa Huma za Washiriki. Mzee wa kanisa na mchungaji ni maafisa wa kamati hii.
  • Ukubwa wa kamati utategemea ukubwa na mahitaji ya kanisa. Kamati itafanya vizuri kazi yake kama itakutana walau mara moja kwa mwezi. Baraza la kanisa linaweza kukasimu baadhi ya mambo mepesi yahusianayo na muziki kwa kamati hii.
Kuwachagua Waimbaji – “Muziki mtakatifu ni sehemu muhimu ya ibada ya hadhara. Kanisa ni lazima litumie uangalifu katika kuchagua wanakwaya na wanamuziki wengine watakaowakilisha vizuri kanuni za kanisa. Ni lazima wawe washiriki wa Kanisa, au washiriki wa Shule ya Sabato, au wanachama wa Chama cha Vijana Waadventista. Kwa kuwa wanachukua nafasi inayooneka na watu katika huduma za kanisani, wanatakiwa kuwa kielelezo cha unyenyekevu na tabia njema, katika mwonekano na mavazi yao. Mavazi ya kwaya yatategemea uchaguzi wao. (CM, uk. 92).

Makanisa yanaweza kuwa na kwaya nyingi. Kuwa na kwaya ya watoto ni njia ya kuwasaidia kuwalea kiroho, kuwaunganisha na familia ya kanisa, na kuwashirikisha kwenye ushuhudiaji. (CM, uk. 92)

MAONI
  1. Waimbaji ni lazima wachaguliwe na kanisa
  2. Kanisa ni lazima lisajili kwaya/vikundi vya uimbaji kwa kuwachagua waimbaji na kuwabatilisha/kuwaidhinisha viongozi.
  3. Kwa kuwa waimbaji ni wahubiri, ni lazima wawe kielelezo, hasa katika mwonekano na mavazi.
  4. Waimbaji ni lazima wawe waongofu wa kweli. Kwaya na Vikundi vingi vya uimbaji ni maskani ya Mwovu. Vimejaa wivu, majivuno, migogoro, mashindano, uzinzi, uasherati, ubinafsi n.k.
  5. Hebu na wajiundie sheria na kanuni zao wenyewe. Kanisa lijiepusha kutunga na kusimamia sheria kwa waimbaji. Kanuni ya kanisa imetoa viwango vya kutosha, hebu kanisa livitumie hivyo.
Kanisa linaweza kuwa na zaidi ya kwaya moja, ikiwemo na kwaya ya Watoto. Zote hizo ni kwaya za Kanisa. Epukeni kupendelea kwaya au kikundo kimoja cha uimbaji na kuvipuuza vingine. Kanisa linapaswa kuvipenda vikundi na kwaya zote na kuvitia moyo.