Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Mei 31, 2014

Mazoezi Ya Kujenga Misuli Ya Mwili Bila Kunyanyua Vyuma.

Tofauti na unyayuaji vyuma vizito, zipo njia nyingine za kukuza misuli na kufanya mwili kuwa katika hali ya mvuto kuliko hata ya myanyua vyuma, na kuufanya mwili kujijenga kwa usawa bila kuwa na utofauti wa ukubwa wa misuli ambao wanyanyua vyuma vizito wengi wao walivyo, haya hapa ni mazoezi kumi na matano yatakayokuweka vizuri kiafya na kimuonekano...
 • Push up
  Ni zoezi linalopanua kifua, kujenga kifua, kukuza misuli ya mikono ya ndani na nje na ni zoezi zuri la kuanzia, kama unataka kuwa na mwili wa kujijenga vizuri anza na hili zoezi.

 • Pull ups
 Pull ups inafanyisha kazi kila misuli mwilini, hasa misuli ya mikono na mgongo, ukitaka uwe na nundu za mikono kama za Jean Claud Vandame hili ndo hasa zoezi lako.

 • Plank
Ukishikilia hili zoezi bila kutingishika kwa dakika kadhaa, wewe kweli utakua una nia na kuubadilisha mwili wako liwe hekalu la mvuto. Zoezi hili linahitaji mabega yaliyoshiba na linafanyisha kazi misuli ya mikono, kiuno, mgongo, shingo na miguu na zoezi hili lina zawadi moja, linafanya tumbo lako likatike mara sita.

 • Roll Out
  Hili zoezi linafanana na la nusu push up(Plank), ila linachobadilisha ni kusukuma nondo kuelekea mbele na kurudi, na jinsi unavyoendelea kusukuma nondo ndo ambavyo zoezi linavyozidi kuwa gumu, kwa hio unahitaji nia na kujitoa kweli, faida zake linajenga misuli ya mgongo, kiuno, kifua na kutanua mabega. 

 •  Glute bridge
  Zoezi hili linajenga mgongo na misuli yote inaouzunguka, ukiwa mkufunzi wa hili zoezi kinachofuata ni kuombwa namba tu na wasichana.

 • Iverted Row
  Hili zoezi ni la mgongo, fuata kama picha inavyolionyesha, faida zake linafanya kifua kiwe kipana zaidi na mikono iwe na stamina zaidi.

 • Close Hands Push ups
  Hili zoezi ni kwa ajili ya mikono, na ni kwa ajili ya nundu za ndani na nje ya mikono, na misuli yako inakua inakua kwa pamoja bila kutegeana, fanya hili zoezi na utaona mabadiliko makubwa kwenye mikono yako.

 • Star Plack
  Hili zoezi kidogo ni zito kidogo, na zoezi hili linalenga kifua na mabega pamoja na misuli ya miguu na mikono, na ni zuri kwa kukata tumbo.

 • Burpee
  Zoezi la kupunguza mafuta mwilini, zoezi hili linafanya mwili mzima uchemke kwa pamoja, ukiwa unafanya hili, unakua unafanyisha kazi kila kiungo cha mwili na kuondoa sehemu dhaifu mwilini.

 • Dip
  Zoezi la misuli ya nyuma ya mkono na linasaidia pia kwenye misui ya kifua na upanuaji wa mabega na kufanya kifua kikae vizuri, zoezi hili linahitaji nia na nguvu ili lifanyike kwa mpangilio unaotakiwa na linamzidi yule aliyelala kwenye benchi akinyanyua vyuma vizito.

 • Bulgaria Split Squart
  Kichura chura cha mguu mmoja nyuma, kinafanyisha kazi misuli ya mapajani na kukufanya uwe na stamina zaidi, ukifanya hili kwa wiki kadhaa, kama kichura chura cha kawaida kilikua kinakupiga chenga basi utakua unafanya mara mbili ya zaidi ulivyokua unafanya.

 • Suspended Push ups
   
  Push ups ni nzuri, ila ukiiongezea ugumu kidogo kwa kuiongezea suspenda, ni njia mojawapo ya kuiongezea misuli uzito, na kufanya iwe misuli yenye ujazo na ya muda mrefu tofauti na yule anaebeba vyuma vizito.

 • Prone Back Extension
  Hili zoezi linahimalisha kiuno, tumbo na mgongo kwa ujumla.

 • Pike Push ups
  Ukiwa mkongwe wa push ups, hili ndilo zoezi la mwisho la push ups na linasaidia kuimalisha mabega na kuongeza ubora wa viazi vyako vya mikono.

 • Swiss Ball Ro-------+++++++llout
  Zoezi linavyozidi kuwa gumu ndo misuli inavyozidi kuongezeka, ukiweza kuzingatia haya mazoezi utajishangaa baada ya wiki tatu mfululizo ukiwa unayafanya.
 Chanzo: waulize wanaume
 •  

Jumatatu, Mei 26, 2014

Watu mashuhuri katika china ya kale wengine DAKTARI WA AJABU HUATUO

Photo Cretid By: www.itmonline.org


Watu wanapougua wanakwenda kuonana na daktari wakitumai kupona, lakini kama ugonjwa ukiwa suguwatu hao husema "laiti daktari ajabu Huatuo angekuwa hai". Huyu Huatuo alikuwa mganga wa miaka zaidi ya elfu mbili iliyopita, kutokana na uhodari wake watu walimmsifu kuwa ni "daktari wa ajabu". 

Huatuo alikuwa ni mwenyeji wa mkoa wa Anhui, tarehe yake ya kuzaliwa haiwezi kuthibitishwa, lakini aliuawa kabla ya mwaka 208. Inasemekana kwamba Huatuo alikuwa na afya nzuri na alipokuwa na umri wa miaka mia moja afya yake bado ilikuwa njema. Kutokana na maandishi ya historia, alikuwa mganga wa kienyeji na alikuwa na nafasi nyingi za kuwa ofisa, lakini alikataa. Jemadari mkubwa Cao Cao (155-220) alikuwa na ugonjwa wa kuumwa na kichwa kwa muda mrefu, alimwomba Huatuo amtibu, muda si mrefu Cao Cao alipona kabisa. Tokea hapo Cao Cao alimlazimisha Huatuo aishi naye na kutunza afya yake. Lakini siku chache baadaye Huatuo alirudi nyumbani kwa kisingizio kuwa mkewe alikuwa anaumwa. Ingawa Cao Cao alimhimiza mara kadhaa arudi kwake, lakini Huatuo hakurudi. Cao Cao aliamua kumtia gerezani na baada ya muda alimwua. 

Huatuo alikuwa na elimu nyingi za tiba ambazo zinahusika na magonjwa ya maambukizi, minyoo, wanawake na watoto, mfumo wa kupumua na ngozi, na hasa elimu ya kufa ganzi kwa mwili mzima na upasuaji. 

Huatuo alikuwa mtu anayependwa sana na watu, kwa kiasi fulani uhodari wake katika matibabu umeonesha maendeleo ya tiba katika miaka elfu mbili iliyopita nchini China. Huatuo alikuwa mmoja wa watu waliotangulia kutumia dawa za ganzi duniani.
Huatuo alikuwa hodari wa kufanya upasuaji. Aliwahi kumfanyia upasuaji msichana mmoja mwenye umri wa miaka 20 ambaye alikuwa na kidonda kwenye goti kwa miaka minane. Huatuo alifunika dawa ya unga kwenye kidonda baada ya kutoa kipande kimoja cha mfupa, msichana huyo alipona baada ya siku saba. Watu wa leo wanaona kuwa kipande cha mfupa alichotoa kilikuwa ni kipande kilichokufa. Kulikuwa na mgonjwa mwingine mzee ambaye alikwenda kumwona, baada ya kuchunguza ugonjwa wake Huatuo alimwambia kuwa ugonjwa wake umekuwa mkubwa na anaweza tu kufayiwa upasuaji wa tumbo, lakini hata hivyo, anaweza kuishi kwa miaka 10 hivi, na bila ya upasuaji pia ataishi muda huo huo, kwa hiyo ni afadhali aache upasuaji. Lakini kutokana na usumbufu wa ugonjwa wenyewe alimwomba Huatuo amfanyie upasuaji, maumivu yalipungua lakini mzee huyo hakuishi zaidi ya miaka 10. 

Huatuo pia alikuwa hodari wa kugundua ugonjwa kwa kuangalia sura ya mtu. Siku moja alipokuwa katika baa, aliwaona watu kadhaa wakinywa pombe, aligundua mmoja kati yao alikuwa na ugonjwa mkubwa, alimwambia asinywe zaidi na kurudi nyumbani haraka. Mtu huyo alipokuwa njiani alianguka kutoka kwenye gari na baada ya kufika nyumbani siku chache alikufa. 

Watu wa leo wanatilia maanani sana mazoezi ya kuimarisha afya. Miaka elfu mbili iliyopita Huatuo alivuni mazoezi mepesi ili kuimarisha afya, "mchezo wa wanyama wa aina tano" ambayo yalikuwa ni mazoezi mepesi kwa vitendo vya aina tano za wanyama: chui, swala, dubu, nyani na ndege. Watu wanaofanya mchezo huo wananyoosha mishipa, kuongeza mzunguko wa damu, kuongeza uwezo wa kujikinga na maradhi. Wanafunzi wa Huatuo walikuwa wengi, na kati yao watatu walikuwa maarufu ambao walitoa mchango mkubwa katika tiba ya Kichina. Baada ya Huatuo kufariki, watu walimjengea mahekalu mengi kumkumbuka katika mahali alipowahi kutoa matibabu. 

Chen Sheng na Wu Guang Wafanya Uasi
 
Chen Sheng na Wu Guang walikuwa ni viongozi mashuhuri wa uasi wa wakulima, uasi ulioongozwa nao ulikuwa mkubwa na wa kwanza katika historia ya China ambao ulizuka katika karne ya tatu mwishoni mwa Enzi ya Qin. 

Mwaka 210 mfalme wa kwanza wa Enzi ya Qin alifariki, mtoto wake Hu Hai alirithi kiti cha ufalme. 

Mfalme Hu Hai alikuwa mpumbavu, chini ya utawala wake raia waliishi vibaya na kutozwa kodi nyingi. 

Mwaka 209 mfalme Hu Hai aliamuru wakulima 900 kwenda kulinda mji wa Yu Yang (wilaya ya Miyun karibu na Beijing). 

Chen Sheng aliteuliwa kuwa kiongozi wa wakulima hao. Lakini walipokuwa njiani walizuiliwa na mvua kubwa, walikuwa hawawezi kufika mji wa Yu Yang kwa wakati uliopangwa. Kutokana sheria, wangechelewa wote wangeuawa. Chen Sheng na Wu Guang aliwaambia wakulima kuwa ni afadhali kufanya uasi kuliko kuuawa. Wakulima hao waliwachagua Cheng Sheng kuwa jemadari na Wu Guang kuwa msaidizi wake na kuunda jeshi la kwanza la wakulima katika historia ya China. 

Katika muda mfupi jeshi hilo liliteka miji sita mikuu ya wilaya na popote jeshi hilo lilipopita raia waliliunga mkono na kujiunga nalo. Jeshi hilo lilikuwa na askari wengi siku hadi siku na kuwa jeshi kubwa lenye askari laki kadhaa. 

Jeshi hilo liligawanyika katika sehemu tatu, wakati jeshi hilo lilipokuwa na askari laki kadhaa walianza kushambulia mji mkuu wa Enzi ya Qin. 

Mfalme Hu Hai alishikwa na hofu wakati jeshi la Cheng Sheng na Wu Guang lilipokaribia mji mkuu, alihamisha askari laki kadhaa kuja mji mkuu na kushirikiana na jeshi la kifalme kupambana na jeshi la uasi kutoka mbele na nyuma, na Wu Guang aliuawa. Mwezi Desemba mwaka 209 Cheng Sheng pia aliuawa katika pambano kali na jeshi la Enzi ya Qin. 

Ingawa viongozi wa uasi huo Chen Sheng na Wu Guang wate waliuawa, lakini askari wao walijiunga na jeshi jingine lililoongozwa na Xiang Yu na Liu Bang na kuendelea kupambana na jeshi la Enzi ya Qin. Mwaka 206 Enzi ya Qin iliangushwa na jeshi la uasi la wakulima. 

Wang Zhaojun
 
Katika historia ya kale ya China migogoro kati ya kabila la Wahan na makabila mengine ikitokea, ilikuwa inatatuliwa kwa vita, lakini pia iliwahi kutokea njia nyingine ya kutatua migogoro kati ya makabila, nayo ni kumwoza binti wa mfalme kwenye kabila jingine na kupata urafiki na kabila hilo. 

Karne ya kwanza ilikuwa ni kipindi cha Enzi ya Han. Kabila la Waxiongnu lililokuwa katika sehemu ya kusini magharibi ya China lilikumbwa na migogoro kutokana na watemi kugombea madaraka. Wakati huo mtemi mmoja aliyejulikana kwa jina la Han Xie alikuja kwa mfalme wa Enzi ya Han kuomba msaada. Mfalme wa Enzi ya Han alimkaribisha kwa ukarimu na alimsaidia kwa nafaka nyingi, na baada ya kurudi alifanikiwa kupata utawala wa kabila la Waxiongnu. 

Ili kupata urafiki wa daima mwaka 33 K.K. Han Xie kwa mara nyingine alikuja mji mkuu kuonana na mfalme na kuomba amwoe binti yake. Mfalme wa Enzi ya Han mara alikubali ombi lake. Mfalme aliwaambia vijakazi wake "kati yenu atakayekubali kuwa mke wa mfalme wa kabila la Xiongnu atakuwa binti yangu." 

Kulikuwa na msichana mmoja mwenye sura nzuri na werevu, aliitwa Wang Zhaojun. Msichana huyo alikuwa mwerevu na kupenda kusoma, aliweza kutunga mashairi na kupiga kinanda, alikubali kuolewa na mfalme wa kabila la Waxiongnu kwa ajili ya urafiki wa makabila mawili. 

Kwa kusindikizwa na maofisa wa Enzi ya Han Wang Zhaojun alisafiri mbali na kufika sehemu ya kabila la Waxiongnu. Mwanzoni maisha ya kabila hilo yalikuwa magumu kwake lakini baada ya muda alizoea na kuishi vema na Waxiongnu. 

Yanzi 

Katika kitabu maarufu cha "Rekodi ya Historia" kilichoandikwa na Simaqian, walielezwa wanadiplomasia kadhaa mashuhuri, mmoja wao alikuwa Yan Zi aliyeishi katika karne ya sita. 

Kipindi kati ya mwaka 770 K.K. hadi 481 K.K. katika historia ya China kinaitwa kipindi cha Spring na Autumn. Wakati huo utawala wa Enzi ya Zhou ulikuwa umeanza kudhoofika, madola yaliyo chini ya himaya kake aylikuwa yanapigana kugombea ardhi na mwishowe yalitokea madola kadhaa yenye nguvu kubwa, na pia walitokea wanasiasa mashuhuri. Yan Zi alikukwa mmojawapo. 

Kwa mujibu wa maandishi ya historia, kimo cha Yan Zi kilikuwa mita moja na sentimita arobaini tu, lakini elimu yake ilikuwa pana na alikukwa mtu mwerevu na mcheshi.
Yan Zi aliwahi kwenda kwenye madola mengine mara nyingi akiwa mjumbe wa Dola la Qi, kati ya safari zake, hadithi katika safari mbili alipokuwa katika Dola la Chu zilikuwa maarufu. Mfalme wa Dola la Chu alijua yeye ni mbilikimo, alitaka kumdhihaki. Katika safari ya kwanza alipokuwa kwenye Dola la Chu mfalme aliamuru watu wake wamwingize mjini kutoka kwenye kilango kidogo pembeni mwa lango kubwa. Yan Zi alielewa mfalme Chu akitaka kumdhalilisha, alikataa kabisa na kusema, "Nikifika kwenye dola la mbwa nitaingia kwenye kilango cha mbwa, sasa nimekuja kwenye dola la Chu nikiwa mjumbe wa dola, niwezaje kuingia mjini kupitia kilango cha mbwa!" Walinzi walikuwa hawana budi ila kumpitisha kutoka kwneye mlango mkubwa. Mfalme wa Chu alipokutana na Yan Zi alimwuliza kwa makusudi: "Kwani dola la Qi linashindwa kumchagua mtu mwingine aje kwenye dola la Chu badala yako?" Yan Zi alimjibu kwa utaratibu, "Dola la Qi lina mazoea ya kutuma wajumbe wenye maadili mema kwenye madola yenye maadili mema, na kutuma wajumbe wapumbavu kwenye madola ya wapumbavu. Mimi ni mpumbavu kabisa kati ya wajumbe wote, ndio maana nimetumwa hapa." 

Safari ya pili alipokwenda kwenye dola la Chu, mfalme wa Chu alitaka kumwaibisha Yan Zi hadharani. Wakati mfalme wa Chu alipomkaribisha kwenye chakula, ghafla askari wawili walileta mtu mmoja aliyefungwa kamba mbele ya mfalme, wakisema mtu huyo ni mtu wa dola la Qi, aliiba mali yao. Mfalme alimtupia macho Yan Zi akisema, "Kwani watu wa dola la Qi walizaliwa na wezi?" Mwerevu Yan Zi mara alikumbuka mto Huaihe uliokuwa mpaka wa madola mawili, alitumia michungwa kumjibu mfalme: "Machungwa yaliyopatikana kwenye ukingo wa kusini wa mto ni matamu, lakini yaliyoko kwenye ukingo wa kaskazini ni machungu, sababu udongo wenyewe ni tofauti. Watu wanaoishi katika dola la Qi hawaibi, lakini wanaoishi katika dola la Chu wana tabia ya kuiba, kwani ardhi ya Chu inalea wizi?" 

Mambo kama hayo yalikuwa mengi ambayo Yan Zi aliwashinda wapinzani wake waliojaribu kumdhihaki na kuharibu heshima ya dola lake. Alikuwa mwanadiplomasia mashuhuri katika hitoria ya China. 

Su Wu
 
Kuna hadithi moja kuhusu Su Wu nchini China, nayo ni hadithi ya "Mchugaji Kondoo Su Wu". 

Su Wu alikuwa mtu wa Enzi ya Han katika karne ya kwanza. Ili kuweka urafiki na kabila la Waxiongnu lililoko katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China Su Wu alitumwa na mfalme kwenda kwa Waxiongnu akiwa na zawadi nyingi, na baada ya kumaliza kazi aliyopewa na mfalme tayari kurudi nyumbani, alibakizwa huko kwa kusingiziwa kuwa alishiriki katika mgogoro uliotokea ndani ya kabila la hilo, na alilazimishwa kuhaini Enzi ya Han. 

Mwanzoni Su Wu alishawishiwa kuwa ofisa kwa mshahara mkubwa, lakini Su Wu alikataa, baadaye aliadhibiwa na Xiongnu kwa kutompa chakula na maji. Siku zilikwenda, Su Wu alifungiwa ndani ya shimo, akiwa na kiu alikula theluji, akiwa na njaa alikula koti lake ya ngozi. Mwishowe aliachiwa huru kutokana na nia yake thabiti ya kutohaini Enzi yake ya Han. Lakini hakuruhusiwa kurudi nyumbani bali alifukuziwa mbali kwenye sehemu ya baridi Siberia kuchunga kondoo, aliambiwa kuwa ataruhusiwa kurudi nyumbani pindi kondoo dume akizaa. 

Su Wu alifukuziwa kando ya ziwa la Baikal na kuchunga kondoo kwa miaka nenda miaka rudi, nywele zikawa na mvi na ndevu zikawa nyeupe. 

Aliishi kwenye ziwa la Baikal miaka 19. katika muda wa miaka zaidi ya kumi mfalme aliyemfukuzia alikufa, na mfalme wake wa Enzi ya Han pia alifariki, aliyeathiri kiti cha ufalme alikuwa mtoto wake. Wakati huo mfalme mpya alitekeleza sera mpya na mfalme huyo mpya alimtuma mtu kumrudisha Su Wu nyumbani. 

Su Wu alikaribishwa kwa shangwe na wananchi katika mji mkuu wa Enzi ya Han, maofisa wa serikali walimheshimu kutokana na uzalendo wake. 

Guan Zhong na Bao Shuya
 
Guan Zhong na Bao Shuya walikuwa wanasiasa katika karne ya saba na walikuwa marafiki. Guan Zhong alikuwa maskini na Bao Shuya alikuwa tajiri, na hao wawili walifahamiana na kuamiana na hata walishirikiana kufanya biashara, kutokana na umaskini Guan Zhong alitoa raslimali chache, lakini walipogawana faida alipewa pesa nyingi zaidi kuliko Bao Shuya ili aweze kuwatunza jamaa zake. 

Baadaye watu hao wawili wote walishiriki katika mambo ya siasa, ambayo wote wawili waliwafundisha watoto wawili wa mfalme wa Dola la Qi katika madola mengine tofauti. Baadaye uasi ulitokea katika Dola la Qi, mfalme aliuawa. Baada ya kusikia habari kuhusu kifo cha baba yao, watoto wote wawili walikimbilia nyumbani dola la Qi ili kurithi kiti cha ufalme. Njiani mtoto Qi Huan Gong na ndugu yake walikutana. Guan Zhong alimfyatulia mshale Qi Huan Gong ili ndugu wa Qi Huan Gong apate nafasi ya ufalme. Mshale huo ulimkwaruza tu Qi Huan Gong kiunoni, lakini alijidai kuwa amepigwa na kuanguka kama amekufa. Ndugu yake alidhani amekwisha kufa, na kiti cha utawala hakika kitakuwa chake, akapunguza mwendo wa safari. Lakini Qi Huan Gong hakuumia, aliharakisha safari yake usiku na mchana na alifika nchini mapema kwa siku sita kuliko ndugu yake, mawaziri walimwunga mkono awe mtawala wa dola la Qi. 

Baada ya kuwa mfalme wa dola la Qi, Qi Huan Gong aliwapokea watu wengi wenye busara hata hakuwa na kinyongo na yule Guan Zhong aliyemfyatulia mshale na kumteua kuwa waziri wa dola lake. 

Guan Zhong alikuwa waziri kwa miaka mingi na alitoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuimarisha dola lake. 

Bao Shuya alipofariki, Guan Zhong alilia sana mbele ya kaburi lake, alisema, "nilizaliwa na mama yangu lakini aliyenielewa ni Bao Shuya!" 

Mfalme Chu Zhuangwang
 
China ni nchi yenye uvumilivu mkubwa, watu wanaona kuwa uvumilivu unaweza kuyeyusha fitina. Hadithi ya "kuondoa kishungi kwenye kofia" inawafundisha watu wenye uvumilivu watalipwa mema. 

Katika kipindi cha Spring na Autumn, karne ya saba, kulikuwa na madola mengi kwa wakati mmoja. Mfalme wa Dola la Chu, Chu Zhuangwang alikuwa mwerevu, na chini ya utawala wake dola hilo liliimarika sana. 

Siku moja, mfalme Chu Zhuangwang aliwakaribisha maofisa kwenye chakula na kuburudika kwa nyimbo na ngoma. Giza lilikuwa linaingia, mfalme aliwaambia kuwasha mishumaa. Watu walikula na kunywa kwa furaha. 

Ghafla upepo ulivuma, mishumaa ilizimika, wakati huo mke wa mfalme alisikia kuna mkono mmoja ulimshika shika, mke wa mfalme alighadhabika akang'oa kishungi cha kofia ya yule aliyemtomasa, akaenda kwa mfalme na kumnong'oneza, "washa mishumaa na kuona kama nani alikosa kishungi kwenye kufia na kumwadhibu." Lakini mfalme alipaaza sauti na kusema, "Msiwashe mishumaa, ni furaha pekee kunywa pombe gizani." Baadaye mfalme aliwauliza maofisa, "Mnafurahia chakula?" wote walijibu "Ndio!" Mfalme aliendelea, "kama kweli mnafurahia chakula, basi ng'oeni vishungi kwenye kofia zenu!" wote waling'oa. Kisha mfalme aliwaambia wawashe mishumaa. Maofisa walipoona kofia zote zilibadilika sura wote walicheka, waliendelea kula na kunywa mpaka kupambazuka. 

Baada ya kurudi kwenye kasri la kifalme, mke wa mfalme alihasirika sana alisema, "Wewe mfalme unawadekeza sana maofisa, hivyo utashindwa kuwatawala." Mfalme alicheka na kusema, "Nawakaribisha maofisa kwenye chakula kwa lengo la kuwafurahisha. Ni jambo la kawaida kwa mtu akizidiwa na pombe na kufanya kitendo kisicho cha kawaida. Nikimwadhibu ofisa huyo kwa jambo hilo dogo nitaharibu furaha na kuwafedhehesha maofisa. Hilo silo lengo la kuwaandalia chakula." 

Baadaye dola la Chu lilishambulia dola la Zheng. Kulikuwa na jemadari mmoja aliyekuwa shupavu mkubwa katika mapambano dhidi ya askari wa dola la Chu, na alifanya mashambulizi mpaka karibu na mji mkuu wa dola la Chu. Jemadari huyo ndiye aliyemshikashika mke wa mfalme wa dola la Chu. 

Hadithi ya "kuondoa kishungi kofiani" inawaambia watu wawe wavumilivu. 

Yu Boya na Zhong Ziqi
 
Katika kipindi cha Spring na Autumn, katika dola la Chu kulikuwa mwanamuziki mmoja ajulikanaye kwa jina la Yu Boya. Huyu Yu Boya alikuwa mwerevu toka alipokuwa mtoto, na alipenda sana muziki. Baadaye alijifunza kupiga kinanda kwa mwalimu wake Lian Cheng. 

Baada ya kujifunza kwa miaka mitatu, alikuwa mwanamuziki mashuhuri, lakini Yu Boya hakuridhika, aliona kiwango chake kilikuwa bado si kikubwa kileleni. Mwalimu wake Lian Cheng alifahamu Yu Boya aliyofikiri moyoni, alimwambia kwamba atamwongoza kwa mwalimu wake ambaye ufahamu wake wa muziki ni wa juu sana. Yu Boya alikubali.
Baada ya kutayarisha chakula cha kutosha hao wawili walipanda mashua na kufika kwenye mlima wa Penglai. Mwalimu wake Lian Cheng alimwambaia, "Nisubiri hapa, nakwenda kumtafuta mwalimu wangu." kisha akaondoka. Siku nyingi zilipita, lakini mwalimu wake Lian Cheng hakurudi. Boya aliangalia bahari isiyo na mwisho na misitu mlimani alihuzunika sana, kwa kusukumwa na moyo alipiga kinanda chake. Muziki ulijaa huzuni, lakini tokea hapo alikuwa mwanamuziki mkubwa. Kwa kweli mwalimu wake Lian Cheng alifanya hivyo kwa makusudi ili Yu Boya apate hisia za kweli moyoni.
Kuishi katika kisiwa kilichojitenga, usiku na mchana kitu alichoona ni bahari, ndege na misitu, siku nenda siku rudi hisia zake zilibadilika na kuelewa zaidi muziki, alitunga muziki maarufu uliowagusa mioyo wasikilizaji. Yu Boya alikuwa mwanamuziki mkubwa, lakini watu waliofahamu muziki wake walikuwa wachache. 

Siku moja Yu Boya alisafiri kwa mashua, alipofika karibu na mlima, mvua kubwa ilinyesha, aliegesha mashua yake kukimbia mvua. sauti ya mvua na mandhari nzuri ya ukungu uliokuwa kwenye uso wa mto ilimsisimua, alipata msukumo wa kupiga kinanda. Muziki alioupiga ulikuwa ni sauti kutoka moyoni mwake. Kulikuwa na mtu mmoja kwenye ukingo wa mto akisikiliza muziki wake, mtu huyo aliitwa Zhong Ziqi.
Baada ya kusalimiana Yu Boya alimkaribisha Zhong Ziqi ndani ya mashua yake na kumpigia muziki. Zhong Ziqi alisikiliza kwa msisimko. Yu Boya alisema, "Katika dunia hii ni wewe tu unayefahamu sauti ya moyoni mwangu, wewe ndiye mwelewa sauti yangu!" Hao wawili walikuwa ndugu wa kuchanjiana. 

Yu Boya aliahidiana na Zhong Ziqi kuwa watakutana baadaye. Siku moja Yu Boya alikwenda kwa Zhong Ziqi kama walivyoahidiana, lakini wakati huo Zhong Ziqi alikuwa amefariki. Baada ya kusikia habari hiyo Yu Boya alikimbilia kwenye kaburi la Zhong Ziqi na kumpigia muziki kwa huzuni kubwa, kisha alisimama na kuvunja kabisa kinanda chake. Tokea hapo Yu Boya aliacha kabisa kupiga kinanda. 

Sun Wu
 
Sun Wu aliyeishi katika karne ya sita K.K. ni mtu maarufu sana nchini na duniani, kitabu chake cha "Mbinu za Kivita za Sun Zi" kilikuwa ni maandishi makubwa ya kivita katika China ya kale. 

Sun Wu alizaliwa mwaka 551 K.K. kilikuwa ni kipindi cha Spring na Autumn katika historia ya China. Alikuwa mtu wa dola la Qi, alipokuwa na umri wa miaka 19 alikwenda dola la Wu, na katika kiunga cha mji mkuu wa dola la Wu (mji wa Suzhou wa leo) aliandika kitabu chake cha mbinu za kivita na kumpa mfalme wa dola la Wu. Mfalme alifurahi sana, lakini hakujua kama mbinu zenyewe zinaweza kutumika, alimtaka Sun Wu afanye mazoezi kwa masuria waliokuwa ndani ya kasri la kifalme. 

Sun Wu aliwagawa masuria 180 kwa vikundi viwili na kuwateua wawili waliopendwa sana na mfalme kuwa viongozi wa vikundi viwili, kimoja kulia na kingine kushoto, na kufanya mazoezi. 

Sun Wu alisimama kwenye jukwaa na kuwafahamisha mpango wa mazoezi yake. Sun Wu alipiga ngoma ya kuanzisha mazoezi. Lakini masuria walikuwa kama hawajasikia mdundo wa ngoma, bali walichekacheka na kuchezacheza, safu zao zilivurugika, ingawa Sun Wu aliwaasa mara kadhaa, lakini haikusaidia kitu. Kutokana na hali hiyo, Sun Wu aliamuru kuwaua viongozi wawili. 

Mfalme alipoona kweli Sun Wu alitaka kuwaua wapendwa wake wawili alimsihi awaache. Lakini Sun Wu hakubali ombi la mfalme, aliwaua. Kisha akaanza tena mazoezi, safari hii masuria walifanya mazoezi kwa makini, walipiga hatua mbele na nyuma, waliviringika na kutambaa kifudi fudi, kila mmoja alifanya vizuri. Kuona hali hiyo mfalme alifurahi, akamteua Sun Wu kuwa jemadari. 

Chini ya uongozi wa Sun Wu jeshi la dola la Wu lilikuwa hodari sana na lilipata ushindi kila mara katika vita vya kupigana na madola mengine. 

Mwaka 482 K.K. mfalme wa dola la Wu alikuwa mbabe kati ya madola yote kutokana na mbinu zilizoandaliwa na Sun Wu. 

Kutokana na ushindi, mfalme alikuwa anavimba kichwa. Kwa kuona jinsi mfalme alivyokuwa, Sun Wu aliondoka na kuishi mbali na mfalme milimani. 

Kitabu cha "Mbinu za Kivita za Sun Zi" ingawa kilikuwa na maneno elfu 6 katika makala 13, lakini kilionesha kikamilifu mbinu zake za kivita. Kitabu hicho kilisifiwa na watu wa baadaye kuwa ni "kitabu cha kwanza duniani kuhusu mbinu za kivita", na kilitumika sana katika mambo ya kijeshi, kisiasa na uchumi. 

Qi Jiguang
 
Katika mlima wa Yu Shan mkoani Fujian kuna hekalu moja lililowekwa sanamu ya Qi Jiguang, watalii wanapofika huko hawakosi kwenda kutoa heshima kwake kutokana na uzalendo wake na mchango wake katika mapambano dhidi ya wavamizi. 

Qi Jiguang alikuwa jemadari katika Enzi ya Ming, alizaliwa katika ukoo wa jemadari. Kwa kuathiriwa na baba yake, Qi Jiguang toka alipokuwa mtoto alipenda sana mambo ya kijeshi na kuwa na nia ya kuwa mwanajeshi hodari. Wakati huo wavamizi wa Japan walikuwa mara kwa mara wanashambulia China. Alipokuwa na umri wa miaka 17 alirithi wadhifa wa baba yake na kuanza maisha yake ya kijeshi. Alipokuwa tu jemadari tatizo lililomkabili lilikuwa ni mashambulizi ya Japan. 

Tokea mwishoni mwa Enzi ya Yuan na mwanzoni mwa Enzi ya Ming maharamia wa Japan mara kwa mara walikuwa wakipora mali na kuua watu kwenye mwambao. Katika nusu ya pili ya karne ya 15 maharamia wa Japan walikuwa wanashirikiana na wafanyabiashara wabaya wa China kufanya uovu. 

Mwaka 1555 Qi Jiguang alitumwa kwenye mwambao, aliunda jeshi la wakulima na wachimba migodi. Walitumia mishale na mikuki kuwaua baada ya kuwatega mitegoni.
Jeshi lake lilikuwa na askari elfu 4, na baada ya kuwafundisha na kuwafahamisha askari mbinu za kivita, jeshi hilo lilikuwa hodari sana, na kutokana na kuwa na nidhamu kali liliungwa mkono na wananchi. 

Mwaka 1561 maharamia wa Japan elfu kadhaa na mashua zaidi ya mia walifanya mashambulizi katika sehemu ya Taizhou mkoani Zhejiang. Qi Jiguang kwa haraka aliwaongoza askari wake kupambana nao na kuwaangamiza maharamia wote.
Kutokana na juhudi za Qi Jiguang na majemadari wengine, maharamia wa Japan walitoweka, mikoa ya Zhejiang na Fujian ilikuwa tulivu, na uchumi ulistawi. Qi Jiguang alitoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya maharamia wa Japan na alisifiwa sana na watu wa China. 

Jumapili, Mei 04, 2014

Vita vya YOM-KIPPUR na funzo kwa dunia


Photo Credit By: Wikipedia

Tupo kwenye miaka 40 toka vita vya YOM-KIPPUR kuanza vita hii ilianza tarehe 06-10-1973 nchi za kiarabu zilijipanga vilivyo ili tu kurejesha ardhi zao walizopoteza katika vita vilivyovunja record ya Dunia vita vilivyopiganwa kati ya nchi za Ki-arabu na Israel kwa mda wa siku sita Mwaka 1967 na majeshi ya nchi za Ki-arabu kusalimu Amri na kuacha ardhi zao kutekwa na askari wao kwa mamia kupoteza maisha yao na Maelfu kutekwa.

 Vita hii iliacha maumivu na makovu makubwa sana katika ulimwengu wa Kiarabu hata kupelekea nchi hizo hasa Misri na syria kuanza mikakati ya kukomboa ardhi zao zilizotekwa na Mjeshi ya Israel,kwa maana syria milima ya Ki-mbinu ya Golan ilikuwa imetekwa na kwa upande wa Misri ilipoteza Jangwa lote la sinai ikiwa pamoja na Mfereji wa Suez nchi hizi zilikuwa na machungu sana hasa ikichukuliwa kuwa nchi iliyowashinda ni ndogo sana hivyo mipango iliyofanywa mwaka 1973 ni kuzikomboa ardhi zilizotekwa baadaye kuifutilia mbali Israel katika uso wa Dunia.

 Mipango ya kuivamia Israel ilipangwa ifanyike siku ya Jumamosi ambapo kulikuwa na sikukuu ya Kiyahudi inayojulikana kama YOM-KIPPUR,Siku hiyo Israel ilipata changamoto kubwa ambayo katika historia ya nchi hiyo Kivita haijawahi kutokea, maana siku hiyo Maelfu ya vifaru na Makumi elfu ya Majeshi na ndege za kijeshi zilifanya shambulizi la kushitukiza na kwa pamoja katika mipaka ya Israel ya kusini na kaskazini hii ilikuwa Ishara tosha kuwa Syria na Misri zilikuwa zinataka kurudisha ardhi zao zilizotekwa katika vita vya siku sita vya mwaka 1967.

 CHANZO CHA VITA YA YOM-KIPPUR.  Baada ya Israel kushinda vita vya 1967 Israel ilipata ardhi kubwa ambayo ilipaswa kulindwa kwa gharama yoyote ili kupata Muafaka wa kisiasa kati ya nchi hiyo na nchi za Kiarabu kwa upande wa Misri Israel ilichukua Sinai na Suez canal hivyo Jeshi la Israel lilipata changamoto kubwa sana kulinda mpaka wote wa sinai na Mfereji wa Suez,Majeshi ya Israel yaliweka vituo vya ulinzi vilivyojulikana kama BAR-LEV line,na kwa upande wa Syria Israel ilichukua Milima ya Golan ambayo kwa Israel lilikuwa eneo jipya lililotakiwa kulindwa kwa nguvu zote maana Ki-Jeshi lilikuwa ni strategic la kimbinu sana Maana milima hiyo ya Golan iko kwenye mwinuko kwa hiyo eneo hilo likishikiliwa na Syria ina maana Majeshi ya Syria yana Uwezo wa kumiliki Kijeshi ndani ya Israel kilomita zaidi ya 25 na wakati huohuo Israel haingekuwa na uwezo wa kupata target Shabaha nzuri kupiga majeshi ya Syria yaliyoko kwenye milima hiyo ya Golan na ndiyo maana mpaka leo Israel haiwezi kuiachia milima hiyo maana kufanya hivyo ni sawa na kujitoa MHANGA kwa jeshi la Israel,Badala yake Inataka kuirudisha milima hiyo kwa kubadilisha na AMANI na Syria ili wawekeane mkataba wa AMANI na kutoshambuliana na Israel ili iweze kupata uhakika wa kutoshambuliwa toka milima hiyo ya Golan.

 Baada ya vita vya 1967 Msri na Syria zilianza kujenga majeshi yao ili waweze kukomboa ardhi zao zilizotekwa, Nchi hizo zilihitaji zana za kivita zaa kisasa ili kuweza kummaliza adui yao Israel walihitaji sana kupata silaha toka Urusi wakati huo USSR Walihitaji kupata Ndege aina ya MIG na vifaru aina ya T-62 Vilevile makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-2,3,6 na SA-7 pamoja na silaha za kubomolea Vifaru aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES.

 Kufikia mwezi October 1972 Rais wa misri wakati huo Anwar Sadat aliwahi kuongea na makamanda wake kuhusu kuishambulia israel na ilipofikia mwezi may 1973 vyombo vya kijasusi vya Israel vilikuwa vimepata habari kuwa Misri itaishambulia Israel kupitia mfereji wa Suez Misri walikuwa wanajua kuwa kama Misri itaishambulia Israel basi Syria nayo ingejiunga na kuishambulia Israel kutokea Kaskazini. Vilevile Israel walidaganyika kuwa Misri itaishambulia Israel mara tu itakapopokea ndege aina ya MIG-23 na SCUD-D toka Urusi Jeshi la Israel lilijua kuwa Misri haijapokea silaha hizo toka Urusi hivyo iliamini Misri haiwezi kuanzisha vita hivyo kabla ya kupokea silaha hizo toka Urusi.

 Mwezi May na Mwezi August 1973 Majeshi ya Misri yalifanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la mpaka na Israel,Israel nayo ilipoona hivyo ilianza kukusanya askari wake kwa maandalizi ya vita lakini baada ya pale hakukuwa na harakati zingine za kijeshi katika eneo hilo la mpaka hivyo Jeshi la Israel liliona kuwa hiyo ilikuwa kawaida tu yaani waliona kama yalikuwa mazoezi ya kawaida tu.

 Septemba 25,1973 Mfalme hussein wakati huo alikutana na waziri mkuu wa Israel wakati huo Mama Gold Meir wakati huo Mfalme Hussein alishakutana na Rais Sadat na Assad wa Syria na alimwonya waziri mkuu wa Israel kuhusiana na kukalia eneo la Syria la milima ya Golan na Sinai eneo la Misri,Baada ya kumalizika kikao hicho na Mfalme Hssein waziri mkuu wa Israel pamoja na waziri wa ulinzi wa Israel wakati huo MOSHE DAYAN pamoja na vyombo vya Kijasusi vya Israel waligundua moja kwa moja kuwa Misri ingewashambulia wakati wowote.

 Masaa machache tu kabla ya Misri kuishambulia Israel tarehe 06-10-1973 waziri mkuu Golda Meir na waziri wa Ulinzi Moshe Dayan na Mkuu wa utawala jeshini Gen.David Elazar kwa pamoja waliamua kuwaita wanajeshi wa anga wale wa akiba na wale wa vifaru wale wa akiba maana walijua hapo sasa vita haiepukiki.

 Kabla ya vita siku hiyo majeshi ya pande zote mbili yalikuwa na zana zilizokuwa zinakisiwa kuwa hivi:
 ISRAEL        
       
 Ndege za kivita 358 
 Vifaru 2100
   Meli za kivita 37

MAADUI ZAKE

Ndege za kivita 998
Vifaru 4350
Meli za kivita 137
 Ilipofika saa nane kamili mchana majeshi ya Msri na yale ya Syria yalianza kumimina makombora kuelekea katika sehemu zilizokuwa zinakaliwa na Israel,Misri na Syria zilichagua siku ya jumanosi maana ilikuwa ni sikukuu ya kiyahudi ya YOM KIPPUR waliona siku hiyo wayahudi wote huwa wanasherehekea hivyo ilikuwa upenyo mzuri sana kwao.

 Kwa upande wa Sinai majeshi ya Msri yaliweza kuvuka mfereji wa Suez kupitia sehem tano tofauti na kwa upande wa mizinga Misri iliweza kukipiga kituo cha wanaanga wa Israel waliokuwa Refidim katika jangwa la sinai na vikosi vingine vya mizinga vya Israel vilishasmbuliwa na mizinga ya Misri,na kufikia saa 11 jioni maelfu ya Wanajeshi wa misri walikuwa wamefika upande na kulikamata eneo lote la mashariki mwa mfereji wa Suez na wakati wa usiku vikosi vya vifaru vilivuka mfereji wa Suez hapo ndipo hali ya uwanja wa vita ilibadirika kabisa kwa Israel uwepo wa askari wa miguu wa Israel na mizinga yao hakukuweza kuyasimamisha majeshi ya Misri. Division ya 252 na Brigedi ya 14 ya kikosi cha vifaru viliadhirika vibaya sana asilimia kubwa ya vifaru vyao vilikuwa vimeangamizwa na silaha aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES toka Misri.

 Jeshi la anga la Israel lilipoitwa ili kudhibiti majeshi ya Misri,Ndege hizo zilijikuta zinaangushwa na mizinga ya kuangushia ndege, Misri iliweza kuzitungua ndege za Israel kiasi cha kuzimalizia uwezo wa kushambulia na baada ya kujipanga vizuri na kujua namna ya kukwepa makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-7 ndege za Israel ziliweza kuziangamiza helcopter zilizokuwa zimebeba Makamandoo wa misri na kuweza kuzitungua ndege 7 aina ya MIG kwenye uwanja wa mapambano. mapambano hayo yalifanyika kusini mwa mfereji wa Suez ndege hizo ziliangushwa na ndege za Israel aina ya PHANTOM.

 Kwa upande wa milima ya Golani majeshi ya Syria yaliweza kusonga mbele huku mizinga na vifaru pamoja na askari wa miguu waliweza kumiminia mizinga,risasi majeshi ya Israel kwa saa nzima mfululizo wakati huo Israel ilikuwa na Brigedi mbili za vifaru Division ya 36th ndiyo ilikuwa mstari wa mbele na Brigedi 188th nayo ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kusini ya mlima wa Golani na Brigedi ya 7th ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kaskazin mwa mlima Golan hivyo vifaru vya Israel havikuweza kuvishambulia vikosi vya Syria sababu havikuwa kwenye RANGE ya kuweza kushambuliwa.

 Mapigano ya vifaru yalianza tu siku hiyo baada ya jua kuzama majeshi ya Syria yaliweza kupenya ngome za Majeshi ya Israel kwa kuwa walikuwa wanatumia NIGHT-VISION viona usiku hivyo vilisaidia sana majeshi ya vifaru vya Syria vifaru vya Israel vilivyokuwa upande wa kaskazini havikuweza kufua dafu mbele ya vikosi vya Syria,vifaru vya Syria viliweza kushika sehemu ya kusini mwa mlima Golan na ilipofika asubuhi ya tarehe 07-10-1973 vifaru zaidi ya 600 vilikuwa vimeingia ndani ya ardhi ya Israel na vilikimbilia kwenda kulishika Daraja mhimu la nto Jordan na kambi ya kijeshi ya Nafar,Israel pia ilipoteza mlima wa HELMON ambao ulikuwa wa kimbinu strategic nao uliangukia mikononi mwa majeshi ya Syria hili lilikuwa pigo kubwa kwa majeshi ya Israel.

 Kwa upande wa majini majeshi ya Israel yaliweza kuziangamiza boat zilizokuwa zinabeba makombora za Syria na miji yote iliyokuwa inazunguka milima ya Golan wakazi wake waliondolewa na majeshi ya Israel.na baada ya siku 18 Majeshi ya Israel yaliweza kujijenga upya na kuchukua tena eneo lote la milima ya Golan na mlima Hermon.

Chanzo: http://wikileaks01.wordpress.com