Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Januari 31, 2011

FASIHI NI NINI

Wataalam wengi wamelieleza neon hili fasihi. Kwa hivyo fafanuzi na nadharia juu yake ni nyingi. Lakini hata hivyo, karibu wote wamehusika zaidi ama na fasihi kwa jumla au fasihi maandishi.

Katika jitihada yao yote ya kufafanua na kuelezea taaluma ya fasihi, kuna misingi kadhaa ambayo wengi huikubali au huelekea kuikubali, au wasingeipinga kama ingewekwa wazi zaidi.

Ukiitazama fasihi kwa umbo lake la nje na umbo lake la ndani utaona kuwa ni taaluma inayojengwa na maneno, na maneno yenyewe hutumia fani maalum za aina mbalimbali kutolea makusudi au maudhui ambayo humzingatia binadamu maishani. Kama vile mshitakiwa awezavyo kutoka katika hatia, japo awe mkosaji, kwa kutumia ufundi wa maneno, na kama vile awezavyo kuingia hatiani na kuadhibiwa, japo awe si mkosa, kwa utumiaji wa maneno, vivyo hivyo kufanikiwa au kutofanikiwa kwa fasihi kumo katika utumiaji wa maneno. Kwa ajili hii kushughulikia fasihi, kwa upande mmoja, ni kuhusika na kuchunguza maneno.

Utaona kuwa nimesema “kwa upande mmoja”. Hivyo si kila neon au maneno ni kazi ya fasihi ingawa mwanafasihi huweza pia kujifunza mengi yaliyomo ndani ya maneno matupu. Mfano wake ni kama ule wa mtu awezavyo kujifunza kitu kwa upumbavu wa mpumbavu, akaweza kudai kuwa hakuna upumbavu ulio upumbavu mtupu na kuwa, hata ndani ya upumbavu, mna hekia ambayo mwenye hekima aweza kujifunza.

Tusemapo fasihi hujengwa kwa maneno, lazima maneno hayo yawe ni maneno zaidi ya maneno mengine. Fasihi si kuwa na maneno ya kisanaa, bali ni kutumia maneno ya kila siku kisanaa. Katika fasihi, japo jambo lielezwalo huwa ni la kawaida, lakini umbo lake hujitokeza kwa uzuri na urembo kwa kuyatumia kisanaa maneno yayo hayo ya kawaida.

KIINI CHAKE

Japokuwa sanaa hii ya fasihi mara nyingine huzungumzia vitu, lakini hilo ni umbo lake la nje tu. Umbo lake la ndani hasa hujishughulisha na binadamu na ubinadamu wake maishani. Yaani binadamu ndiye kiini cha fasihi; ndiye shabaha yake. Binadamu ndiye mwanzo ndiye mwisho wa fasihi.

Fasihi humtazama binadamu na uhusiano wake na binadamu wenziwe, na mazingira yake, na viumbe vingine, na itikadi yake kuhusu mambo ya kiroho kama pepo, maruhani, mashetani, majini na MUNGU. Humzingatia binadamu katika hali yake, ya furaha na huzuni, raha na taabu, shida na mashaka. Humzingatia katika hali ya upweke na hali ya kuchanganyikika na wengine. Humfunulia huluka mbalimbali za kibinadamu, na matokeo ya huluka hizo maishani. Humfunza, humwonya, humgutusha, humsisimua, humtumbuiza na pia kumwia dhamiri dhammirini mwake huyu binadamu.

Fasihi humtizama binadamu na mazingira yake, na humtazamisha hayo mazingira yake ili ayaone. Hapo humwangalisha na kumfikirisha ili aweze kuyabadilisha mazingira, tabia na hali ya mambo ilivyo kwa manufaa yake na kuweza kumwendeleza mbele katika maendeleo yake kiuchumi, kisanaa, kisiasa na kijamii.

Fasihi humzingatia binadamu katika uwezo na udhaifu wake; kufanikiwa na kushindwa kwake; katika uvumilivu na kukata tama kwake. Na kila wakati humpa nafasi ya kujirekebisha ili awe mtu bora zaidi katika utu wake kati ya jamii, nay eye mwenyewe akiwa sehemu ya jamii yake.

CHANZO CHAKE

Chanzo cha fasihi ni hisi, ya mtu mmoja au watu katika jamii. Hisi za binadamu hujitokeza katika njia nyingi: kwaa vinyago, kwa ujenzi, kwa vifaa, zana, ususi, kilimo, ufundi, uongozi, siasa, kwa njia za uchumi na kumiliki mali, na hata kwa ngoma. Lakini hisi zitupazo fasihi ni zile zinazojitokeza katika lugha.

UKUBWA WAKE

Kama vile ambavyo hakuna aujuaye ubinadamu wote, vivyo hivyo ni vigumu kujua hisi zote, na kwa hivyo kuimiliki fasihi. Ni vigumu kumpata bingwa kwa maana hasa ya ubingwa katika kazi ya sanaa ya fasihi, hata kati ya hao wataalam wa fasihi. Fasihi kina chake katika kumzingatia binadamu ni kirefu; tena ina upana wa kiasu cha kuwapa uhuru wa kuranda wasanii na wataalamu wayo. Ama urefu wake ni vigumu kuuona mwisho au mwanzo wake.

FASIHI NA UTAMADUNI

Kutokana na ufafanuzi huu mfupi wa kijumla, tunaweza kusema kuwa fasihi ina uhusiano mkubwa na utamaduni. Maana kati ya vipengele vya utamaduni kimoja ni lugha. Lugha kama sehemu ya utamaduni ina yabia ya kuwapambanua watu. Japo siku hizi kuna jitihada ya watu kujifunza lugha mbali mbali, lakini lugha ya kujifunza haiwi yako, na mara nyingi wenyeji wa lugha hiyo uliyojifunza huweza kujua kuwa wewe si mmoja wao.

Hii ndiyo sababu leo Afrika tunasema kuwa ni vyema kujua lugha mbali mbali za kigeni katika kujenga uelewano, lakini hata hivyo ni vyema zaidi kutotegemea lugha ya kigeni kuwa lugha ya taifa. Heri kila nchi Afrika ijichagulie lugha ya Kiafrika kuwa lugha ya taifa. Tanzania, Uganda na Kenya, zote zimeamua Kiswahili kiwe lugha rasmi na lugha ya taifa. Zaire hivi sasa imo mbioni; na ingefaaa zaidi kama nchi nyingine zingeamua kutumia lugha moja ya kienyeji kuwa lugha yao ya taifa. Ni kweli uamuzi huo si rahisi, lakini ni muhimu sana.

Kwa kuwa lugha ni kipengele kimojawapo cha utamaduni, na kwa kuwa fasihi hutumia lugha, basi fasihi na ni sehemu ya utamaduni. Na iwapo utamaduni ni utashi na uhai wa taifa, ni mti wa mgongo wa taifa, basi hapana budi fasihi nayo kuwa sehemu ya uhai na utashi wa taifa hilo.Fasihi (na maelezo haya yaweza kuingia katika fasihi kwa jumla, fasihi maandishi na fasihi simulizi) si sehemu tu ya utamaduni, bali ni chombo cha utamaduni pia. Ndiyo chombo cha kukuzia, kuhifadhia, kuendelezea na kuelezea huo utamaduni. Ni chombo cha pekee kati ya taaluma mbali mbali za utamaduni. Hutokea hivyo kwa kuwa taaluma hii huhusika na jinsi lugha inavyosema na jambo linalosemwa. Kwa hivyo hutoa tafsiri mbali mbali ambazo pengine taaluma zingine hushindwa kuzitoa.

Jumatano, Januari 26, 2011

MORNING STAR RADIO 105.3 FM-DSM

Njozi za kuanzishwa kwa Radio hii, ilianzia katika miaka ya tisini, ambapo mwaka 2000 viongozi wa makanisa ya Dar es salaam walikutana na kuweka mkakati madhubuti wa kuanzisha radio hii kwa wakati huo ikijulikana kama TAWR (Tanzania Adventist World Radio).

Mwaka 2001, uchunguzi yakinifu wa kuanzishwa kwa Kituo hiki ulianza chini ya kitengo cha mawasiliano cha Makao makuu ya Kanisa Tanzania kijulikanacho kama TAMC (Tanzania Adventist Media Center).

Baada ya mikakati madhubuti kukamilika, ujenzi wa kituo cha radio ulianza rasmi mnamo mwaka 2002, katika eneo la Mikocheni B, jijini Dar es salaam, ujenzi ambao uliendelea na kukamilika kwa sehemu kubwa mnamo mwaka 2003.

Mnamo tarehe moja mwezi wa kumi mwaka 2003, kituo kilirusha matangazo yake kwa mara ya kwanza kama majaribio, kwa kutumia mtambo wa kurushia matangazo wenye uwezo wa watt 500, na tangu hapo safari ya matangazo kusikika hewani iliendelea!

Mwezi wa kumi na moja mwaka wa 2003, kituo kilifunguliwa rasmi na Mgeni aliyehudhuria
shughuli hiyo, Mchungaji Jan Paulsen, akija kama Rais wa kanisa la Waadventista wasabato Duniani, akitoea Nchini Marekani ambako ndiko makao makuu ya Kanisa Duniani, yalipo.

Majuma mawili baada ya kufunguliwa rasmi kwa kituo, Mtambo wa kurushia matangazo
uliokuwa umefungwa mikocheni B mahali zilipo studio, ulishindwa kufanya kazi kutokana na hitilafu iliyosababishwa na umeme, tatizo lililojitokeza baada ya mvua kali kunyesha.

Jitihada za kujaribu kuirejesha katika hali ya kuendelea kufanya kazi zilishindikana, jambo lililopelekea muingiliano na vyombo vingine vya habari, na kituo kufungwa kwa muda na tume ya mawasilianona, ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa marekebisho. Kituo kilirejea tena katika hali yake na kuendelea na matangazo baada ya miaka miwili baadae.

Mwaka 2005 mwezi wa tano,vifaa vipya vya kurushia matangazo viliagizwa ili kurejesha matangazo tena. Uagizaji huo ulichukua muda wa miezi mitatu, na mwezi wa nane vifaa viliwasili na ufungaji ukaanza mara moja, wakati huu mtambo ukiwa umehamishiwa eneo la kisarawe, mkoa wa Pwani.

Baada ya ufungaji mtambo kukamilika, mnamo mwezi wa nane mwaka 2005, urushaji wa matangazo ya majaribio ulianza mara moja, ambapo majaribio hayo yalichukua takribani mwezi mmoja, hadi mnamo mwezi wa tisa!

Ilipofika tarehe 26, mwezi wa tano mwaka 2006, saa 11:00 jioni, kituo kilirusha matangazo moja kwa moja kwa mara ya kwanza, baada ya matangazo ya majaribio
kukamilika!

Tangu hapo, Morning Star Radio imeendelea kurusha matangazo yake hadi hivi sasa, ambapo watu mbali mbali wamekuwa wakibarikiwa sana na matangazo haya, na kwa hakika kituo hiki kimekuwa ni mbaraka sana kwa ma elfu ya wakaazi wa Tanzania na dunia kwa ujumla ambapo matangazo ya Redio hii yanasikika!


Morning Star Radio inakuletea habari za dunia katika eneo lote la Afrika Mashariki na kati pamoja na kanda ya Maziwa Makuu kwa lugha ya Kiswahili kutoka Dar es Salaam, Tanzania, chimbuko la lugha adhimu ya Kiswahili inayokua kwa kasi.

Idhaa ya Kiswahili ya Morning Star Radio inakuletea habari, makala na uchambuzi pia taarifa za burudani kwa lugha ya Kiswahili kwa wasikilizaji wa Afrika ya Mashariki na kati pamoja na kanda ya Maziwa Makuu kupitia mtandao wa vituo 17 vilivyo jiunga na Morning Star Radio kwa Masafa ya FM kupitia satelite.

Sikiliza matangazo ya Morning Star Radio kila siku kwa muda wa masaa 24 saa za afrika mashariki
.

Tutakuwa tunawafikia watu milioni 100 hadi milioni 150 wanaotumia lugha ya Kiswahili kila siku. Morning Star Radio kwa sasa inarusha hewani matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili na kwa uchache sana pia lugha ya kiingereza kwa njia ya Satellite kupitia Hope Channel International.

Jumapili, Januari 23, 2011

Muziki wa JibutiBowl Lyre, Xylophone and Ndingidi Players. Dance Drumming Accompanists

Kuhusu Jibuti

Jibuti ni taifa dogo lipatikanalo katika Pembe ya Afrika ambayo imekuwa na mitimdo mingi ya kimuziki humo nchini. Watu wa huko wamejikidhi kwa wengi katika mji wa uvuo ambao pia huitwa Mji wa Jibuti. Nchi hiyo imekuwa ikishirikishwa na mataifa mengi, hivi maajuzi ikiwa Ufaransa. Jibuti ilikuwa nchi ya mwisho kupata uhuru kutoka Ufaransa.


Jibuti ina matabaka mawili:

Kabila na Somali pamoja na wafaransa na waarabu. Muziki wa Afra una fanana na muziki wa Ethiopia ukiwa na vipengele vya muziki wa Kiarabu. Historia ya muziki huu imenakiliwa katika ushairi na nyimbo za watu wake ambao ni wafugaji wa kuhama hama na inaanzia katika maelfu ya miaka iliyopita hadi wakati Jibuti ikifanya biashara ya kubadilishana ngozi kwa manukato na Wamisri, Waindia na Wachina. Ngano za Kisomali hujumuisha Ushairi na Methali, nyingi zao zikiwalenga Mitume wa Sufi na maisha yao. Fasihi ya watu wa Afar imeundwa kimuziki na ni ya aina nyingi, ikijumuisha nyimbo za Ndoa, Vita, Kusifu na Kujigamba.

Wimbo wa Taifa wa Jibuti
Ulioundwa mnamo 1977 huku maneno yake yakitoka kwa

Aden Elmi

Na muziki ulitungwa na Abdi Robleh

Balwa

“Miniature Poetry” au “Ushairi Mdogo” ulivumbuliwa na mwendeshaji wa lori aliyekuwa akiitwa Abdi Deeqs,

unajulikana sana nchini Jibuti. Haya ni mashairi mafupi (bwalo), san asana yanayohusu mapenzi. “Bwalo” pia ni mtindo wa muziki wa Somalia wa aina ya Pop.

Vyombo vya Muziki:
Vyombo vya muziki vya Jibuti vinashirikisha Tanbura, Move your curser over the Tanbura to play it.

Ambayo ni aina ya kisahani

Online Catalog-MR420-Irish Clay Pipe Bowl Lyre-one side star.

Bowl Lyre
The ndongo (eight-string bowl lyre) of the Baganda Ndongo Audio Sample.

Kwa Ufupi:
Kihistoria,
ACAPPELLA ndio asili ya uimbaji kabla hata BINADABU hajastukia kuwa sauti inahitaji kusaidiwa na vyombo kama ngoma , MAGITAA , piano au tu makopo yagongwegonwe ndio kieleweke!

Hivi ndivyo Mwanafalsafa ambaye pia ni Mwanablog na Mdau SIMON KITURURU alivyothibitisha wakati alipochangia nyongeza kuhusu DHAHABU ISIYOOZA.