Mtayarishaji

Morning Star Radio

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Teknolojia Ya Mawasiliano. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Teknolojia Ya Mawasiliano. Onyesha machapisho yote

Jumatano, Septemba 09, 2015

MASHAMBULIZI KUPITIA KOMPYUTA



HEBU wazia kundi la wahalifu wenye ustadi wa kutumia kompyuta wakitumia Intaneti kuongoza mitandao ya kompyuta walizoteka nyara. Kompyuta hizo zinazojulikana kama botnets (mitandao ya roboti), zinatoa habari za siri zenye madhara zinazolenga taifa fulani. Baada ya dakika chache, Tovuti za kijeshi, kifedha, na kibiashara za taifa hilo zinaacha kufanya kazi. Mashine za benki za kutolea pesa (ATM) pamoja na mitandao ya simu inashindwa kufanya kazi. Usafiri wa ndege unakatizwa na kompyuta pamoja na mifumo ya usalama katika kituo cha kutokeza nguvu za nyuklia inavurugwa. 

Watu wangetendaje?  

Wewe ungefanya nini?

Huenda tukio hilo likaonekana kuwa lisilo halisi. Lakini kulingana na Richard A. Clarke, aliyekuwa Msimamizi wa Kitaifa wa Usalama, Ulinzi wa Miundo-Msingi, na Kupambana na Ugaidi nchini Marekani, jambo kama hilo linaweza kufanyika kihalisi. Isitoshe, tayari kumekuwa na mashambulizi kupitia kompyuta.* Huenda hata wewe umewahi kushambuliwa.

Kwa nini mtu awashambulie wengine kupitia kompyuta? Mashambulizi hayo hufanywaje? Na kwa kuwa ni kawaida kwa mashambulizi hayo kumlenga mtu mmojammoja, unaweza kujilindaje unapotumia Intaneti?


Uwanja wa Vita Kwenye Kompyuta


Kuna sababu kadhaa zinazowafanya watu wawashambulie wengine kupitia kompyuta. Kwa mfano, magaidi au serikali zinaweza kupenya kwenye mitandao ya kompyuta ya maadui wao ili waibe siri au waharibu vifaa vinavyoongozwa na mitandao hiyo. Katika mwaka wa 2010, Waziri Msaidizi wa Ulinzi wa Marekani William J. Lynn wa Tatu alisema kwamba “maadui” wa kigeni walikuwa wamepenya mara nyingi kwenye mitandao ya kompyuta iliyo na habari za siri za Marekani na kuiba “maelfu ya mafaili . . . kutia ndani maagizo ya kutengenezea silaha, habari kuhusu mipango ya kijeshi, na habari za upelelezi.”—Ona sanduku “Mashambulizi ya Hivi Karibuni Kupitia Kompyuta.”

Wahalifu wanaotumia kompyuta hutumia njia sawa na hizo kuiba habari za kitaaluma au za kifedha kutoka kwa mitandao ya kompyuta ya makampuni na hata kompyuta za watu binafsi. Wahalifu hupata mabilioni ya dola kila mwaka kupitia biashara za ulaghai zinazofanywa kwenye mitandao.

Pia, wahalifu hao wameunganisha kompyuta nyingi sana walizoteka nyara ili waweze kutekeleza mashambulizi yao. Katika mwaka wa 2009, kampuni moja inayoshughulika na usalama wa intaneti iligundua kwamba kundi moja la “wahalifu” lilikuwa likidhibiti kisiri karibu kompyuta milioni mbili kotekote ulimwenguni, nyingi zikiwa ni za watu binafsi. Ripoti ya karibuni ya Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) linakadiria kwamba kompyuta 1 kati ya 3 zilizounganishwa kwenye Intaneti inadhibitiwa kisiri na mhalifu fulani. 

Namna gani kuhusu kompyuta yako? 

Je, mtu fulani anaweza kuidhibiti bila wewe kujua?



Maadui Wanaoshambulia Kimyakimya

Wazia tukio hili. Mhalifu fulani anasambaza programu fulani yenye madhara kupitia Intaneti. Programu hiyo inapoingia katika kompyuta yako, inapenya ndani ya programu inayolinda kompyuta yako. Programu hiyo yenye madhara inapopata eneo ambalo halijalindwa vizuri, inapenya ndani hata zaidi na kutafuta-tafuta habari muhimu katika kompyuta yote.* Kisha programu hiyo inaweza kubadilisha au kufuta mafaili yaliyo kwenye kompyuta yako, na inajituma yenyewe kama barua pepe kwenye kompyuta zingine, au kumtumia mhalifu huyo neno lako la siri la utambulisho, habari za kifedha, au habari nyingine za siri zinazokuhusu.

Wahalifu hao wanaweza kukufanya uingize virusi kwenye kompyuta yako mwenyewe! Jinsi gani? Unaweza kufanya hivyo kwa kufungua barua-pepe inayoonekana kuwa ya kawaida tu, kwa kubonyeza kiunganishi cha Tovuti fulani, kupakua na kuunganisha programu ya bure ya kompyuta, kuingiza kifaa cha kuhifadhi habari kilicho na virusi katika kompyuta yako, au tu kutembelea Tovuti yenye kutiliwa shaka. Mambo yote hayo yanaweza kuingiza programu yenye madhara kwenye kompyuta yako na kuifanya idhibitiwe kisiri na mhalifu.

Unaweza kujuaje ikiwa kompyuta yako imeshambuliwa? 
Kwa kweli inaweza kuwa vigumu kugundua. Huenda kompyuta au Intaneti ikafanya kazi polepole sana, au programu zisitende kwa njia ya kawaida, au visanduku vijitokeze ghafula vyenye ujumbe unaokuomba uunganishe programu fulani, au kompyuta yako itende kwa njia isiyo ya kawaida. Ukiona mojawapo ya dalili hizo, mwombe mtaalamu wa kompyuta achunguze kompyuta yako.


‘Fikiria Hatua Zako’


Kadiri mataifa na mtu mmoja-mmoja wanavyozidi kutegemea teknolojia ya kompyuta, ndivyo inavyotarajiwa kuwa mashambulizi kupitia kompyuta yataongezeka. Kwa sababu hiyo, mataifa mengi yanajitahidi sana kuboresha mbinu za kulinda kompyuta zao, na mataifa mengine yanapima uwezo wa mitandao yao ya kompyuta ili kuona ikiwa inaweza kustahimili mashambulizi. Lakini licha ya jitihada hizo, Steven Chabinsky, mtaalamu wa cheo cha juu wa usalama wa kompyuta wa Shirika la Upelelezi la Marekani anasema kwamba “adui aliyeazimia kabisa, hawezi kamwe—kamwe—kushindwa kupenya mfumo hususa anaolenga iwapo atakuwa na wakati wa kutosha, kichocheo, na pesa.”

Unaweza kufanya nini ili ujilinde unapotumia Intaneti?
 Ingawa huenda usiweze kujilinda kabisa unapotumia Intaneti, unaweza kuchukua hatua zifaazo ili kufanya kompyuta yako iwe salama zaidi.  Biblia inasema: “Mtu mwerevu huzifikiria hatua zake.” (Methali 14:15) Kwa kweli hilo ni shauri lenye hekima unapotumia Intaneti!.

Ijumaa, Novemba 28, 2014

Kusasisha Masharti na Sera Zetu: Kukusaidia kufahamu jinsi Facebook inavyofanya kazi na jinsi ya kudhibiti maelezo yako

 
Kwa mwaka uliopita, tumeanzisha vipengele na vidhibiti vipya ili kukusaidia kupata mengi kutoka kwa Facebook, na tumewasikiliza watu ambao wametuomba tufafanue zaidi tunavyopata na kutumia maelezo.
 
Sasa, ukiwa na Misingi ya Faragha, utapata vidokezo na mwongozo wa jinsi ya kufanya kwa kushughulikia uzoefu wako kwenye Facebook. Pia tunasasisha masharti, sera ya data na sera yetu ya vidakuzi ili kuonyesha vipengele vipya ambavyo tumekuwa tukivishughulikia na kuvirahisisha kueleweka. Na tunazindua maboresho kwenye matangazo kulingana na programu na tovuti unazotumia nje ya Facebook (matangazo ya kitabia za mtandaoni) na kukudhibiti. 
 
Visasisho hivi vinaanza kutumika Januari, 1, 2015. Kama kawaida, tunakaribisha maoniyako kuhusu sera zetu.

Misingi ya Faragha
 
Misingi ya Faragha hutoa mwongozo ingiliani wa kujibu maswali mengi yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu jinsi unavyoweza kudhibiti maelezo yako kwenye Facebook. Kwa mfano, unaweza kujifunza kuhusu kuondoa utambulisho, kuondoa urafiki, kuzuia na jinsi ya kuchagua hadhirira kwa kila chapisho lako. Maelezo haya yanapatikana kwa lugha 36.
 
Pamoja na ukaguzi wetu wa sera, ukumbusho kwa watu wanaochapisha kwa umma na wateuzi wa hadhira rahisi, Misingi ya Faragha ni hatua ya sasa tuliyoichukua ili kukusaidia kuhakikisha kuwa unashiriki na watu unaotaka.

Kukusaidia kupata mengi kutoka kwa Facebook
 
Kila siku, watu hutumia programu na huduma zetu kuunganika na watu, maeneo na vitu wanavyovijali. Visasisho kwa sera zetu vinaonyesha bidhaa mpya tulivyokuwa tukivishughulikia ili kuboesha uzoefu wako wa Facebook. Pia vinaelezea jinsi ambavyo huduma zetu hufanya kazi kwa njia rahisi ya kuelewa. Hapa kuna baadhi ya viangazio:
 
  • Gundua kinachoendelea karibu na wewe:Tunasasisha sera zetu ili kufafanua jinsi tunavyopata maelezo ya eneo kulingana na vipengele unavyotumia kutumia. Mamilioni ya watu huingia katika maeneo wanayopenda na kutumia vipengele vya hiari kama Marafiki wa Karibu (inapatikana tu katika baadhi ya maeneo). Tunashughulikia njia za kukuonyesha maelezo yanayofaa zaidi kulingana na mahali ulipo na yale marafiki wako wanayafanya. Kwa mfano, baadaye, ukiamua kushiriki uko wapi, unaweza kuona menyu kutoka kwa mikahawa iliyo karibu au visasisho kutoka kwa marafiki katika eneo.
 
  • Kufanya ununuzi kuwa rahisi zaidi:Katika baadhi ya maeneo, tunajaribu kitufe cha Nunua ambacho huwasaidia watu kugundua na kununua bidhaa kutoka kwa makampuni mengine bila kuondoka kwa Facebook. Pia tunashughulikia nia mpya za kufanya miamala hata kwa urahisi zaidi.
 
  • Pata maelezo kuhusu faragha kwenye Facebook wakati unahitaji.Ili kuvifanya kupatika zaidi, tulihamisha vidokezo na mapendekezo kwa Misingi ya Faragha. Serea yetu ya data ni fupi na wazi zaidi, kwa hivyo kuifanya iwe rahisi zaidi kusoma.
 
  • Fahamu jinsi tunavyotumia maelezo tunayoyapokea.Kwa mfano, kufahamu nguvu ya betri na mawimbi husaidia kuhakikisha programu zetu zinafanya kazi vizuri kwenye kifaa chako. Tunaomba idhini ili kutumia eneo lako la simu tunapotoa vipengele vya hiari kama kuingia au kuongeza eneo lako la machapisho.
 
  • Jua familia ya kampuni na programu za Facebook zinazofanya kazi pamoja.Kwa miaka michache iliyopita, Facebook imekua na tunataka kuhakikisha unajua kuhusu familia yetu ya makampuni, programu na huduma. Tunatumia maelezo tunayokusanya kuboresha uzoefu wako. Kwa mfano, ikiwa umefungiwa nje ya akaunti yako ya Instagram, unaweza kutumia maelezo yako ya Facebook kupata nenosiri lako. Hakuna chochote katika visasisho vyetu hubadilisha ahadi ambayo Instragram, WahatsApp na makampuni mengine imetoa ili kulinda maelezo yako na faragha yako.
 
  • Maelezo yako na utangazaji:Wakati mwingine watu huuliza jinsi maelezo yao husambazwa kwa watangazaji. Hakuna jambo linalobadilika kwa visasishi hivi—tunawasaidia watangazaji kufikia watu kwa matangazo muhimu bila kuwaambia wewe ni nani. 
 
Jifunze zaidi kuhusu matangazo na jinsi unavyoweza kudhibiti matangazo unayoyaona.

Kukupata udhibiti zaidi wa matangazo
 
Tumesikia kutoka kwa baadhi yenu kwamba inawezakuwa vigumu kudhibiti aina za matangazo unazoona ukitumia vifaa na vivinjari tofauti. Hapo awali, ikiwa ungechagua kutoka kwenye aina fulani za matangazo kwenye kompyuta yako ndogo, chaguo hilo huenda halikutekelezwa kwenye simu yako. Tunajua kuwa watu wengi wanatumia zaidi ya simu moja, kompyuta ndogo au kivinjari ili kufikia Facebook, kwa hivyo inafaa kuwa rahisi kwako kufanya chaguo moja linalotekelezwa kwenye vifaa vyako vyote.
 
Hiyo ndiyo maana Facebook uheshimu chaguo unalofanya kuhusu matangazo unayoona, kwenye kila kifaa. Unaweza kuchagua kutoka kuona matangazo kwenye Facebook kulingana na programu na tovuti unazotumia kupitia Muungano wa Matangazo ya Dijitali. Unaweza pia kuchagua kutoka kwa kutumia vidhibiti kwenye iOS na Android. Unapotueleza hutaki kuona matangazo ya aina hii, uamuzi wako hutumika kiotomatiki kwa kila kifaa unachokitumia kufikia Facebook. Pia, sasa tunatengeneza mapendeleo ya matangazo yapatikane katika nchi zaidi, kuanzia Australia, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Ayalandi na Uingereza.
 
Tunatumaini visasisho hivi vitaboresha matumizi yako. Kulinda maelezo ya watu na kutoa vidhibiti maalum vya ufaragha tunavipa kipaumbele, na tunaamini matangazo haya ni hatua muhimu.
 
 Chanzo: INGIA HAPA

Jumatano, Februari 19, 2014

Fahamu nyenzo za usalama na faragha zinazotolewa kwako na Google


Ukiwa na Google, una zana mbalimbali zinazokusaidia kuwa salama na kuweka maelezo yako salama na faragha. Hapa kuna baadhi ya zana maarufu kabisa ambazo zinasaidia kufanya Google ikufanyie kazi nzuri zaidi.

Kuwa salama na faragha

Uthibitishaji wa hatua -2

Pindi tu unapounda nenosiri la Akaunti yako ya Google, tunakuhimiza uongeze safu ya ziada ya usalama kwa kuwezesha uthibitishaji wa hatua mbili. Uthibitishaji wa hatua mbili unakuhitaji kufikia simu yako, pamoja na jina lako la mtumiaji na nenosiri, unapoingia. Hii inamaanisha kuwa ikiwa mtu fulani ataiba au kudadisi nenosiri lako, mwingiaji kwenye akaunti bila idhini aliyepo bado hawezi kuingia kwenye akaunti yako kwa sababu hana simu yako. Sasa unaweza kujilinda kwa jambo ambalo unajua ( nenosiri lako) na jambo ulilo nalo (simu yako).

Hali fiche katika Chrome

Katika modi chini kwa chini, kurasa unazofungua na faili unazopakua hazirekodiwi katika historia ya kuvinjari au kupakua ya Chrome. Unaweza pia kutumia kipengele hiki katika Chrome ya Android – na Chrome ndio kivinjari chaguo-msingi kwa ajili ya bidhaa mpya za Android, kukuruhusu uvinjari mtandao kwenye simu yako au kompyuta ndogo kwa faragha. Fahamu jinsi ya kufikia modi chini kwa chini.

Google Talk

Google Talk, kipengele cha gumzo katika Gmail na bidhaa nyingine za Google, inakuruhusu kutokuhifadhi gumzo. Gumzo ambazo zimeondolewa kwenye rekodi hazihifadhiwi kwenye au historia ya gumzo za anwani ya Gmail. Unapoacha kupiga gumzo, ujumbe utaonekana kwako na katika anwani yako ukithibitisha kuwa gumzo zijazo hazitahifadhiwa, isipokuwa mmoja wenu abadilishe mipangilio.

Durara za Google+

Durara za Google+ hukusaidia kudhibiti marafiki zako na anwani. Kwa hivyo unaweza kuweka marafiki zako katika durara mmoja, familia yako katika nyingine na bosi katika durara akiwa peke yake - kama vile katika maisha halisi! Kisha unaweza kushiriki maudhui yanayolingana, kama vile chapisho za Google+, video za YouTube, au orodha za Eneo, na watu sahihi wakati wowote unapochagua.

Video za siri na zisizoorodheshwa kwenye YouTube

YouTube iliundwa ili watu washiriki mawazo na dunia nzima. Lakini wakati mwingine ungependelea kushiriki video na kundi dogo la marafiki au ujiwekee. Unaweza kufanya hivyo kwa kuchagua isiyoorodheshwa au ya faragha wakati unapakia video yako.

Angalia na udhibiti maelezo yako

Mipangilio ya Akaunti ya Google

Kwenye ukurasa wako wa mipangilio ya Akaunti, unaweza kuona huduma na maelezo yanayohusiana na Akaunti yako ya Google na ubadilishe mipangilio yako ya usalama na faragha.

Dashibodi ya Google

Dashibodi ya Google hukuonyesha kilichohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google. Kutoka kwa eneo moja la kati, unaweza kutazama na kusasisha kwa urahisi mipangilio yako ya huduma kama vile Blogger, Kalenda, Hati, Gmail, Google+ na zaidi.

Mimi kwenye Wavuti

Mimi katika Wavuti inaweza kukusaidia kuelewa na kudhibiti watu wanachokiona wanapokutafuta kwenye Google. Inakusaidia kuweka Tahadhari za Google ili uweze kufuatilia maelezo yanayokuhusu yakitokea mtandaoni, na inapendekeza otomatiki baadhi ya hoja za utafutaji unazoweza kutaka kufuatilia kwa umakini.

Shughuli ya Akaunti

Shughuli za Akaunti zinafanya iwe rahisi kwako kukagua jinsi unavyotumia huduma za Google wakati umeingia, na kuhakikisha ni wewe tu umekuwa ukiitumia akaunti yako. Ukifungua akaunti, utapata ufikiaji kwa ripoti ya kila mwezi penye utaona vitu kama idadi ya barua pepe zilizotumwa na kupokewa kutoka kwa akaunti yako, akaunti yako imefikiwa kutoka nchi zipi, na utafutaji wa Google unaoongoza kutoka akaunti yako.

Google Takeout

Google Takeout hukupa zana rahisi kutumia ya kupakua data yako binafsi, kama vile hati au picha, ili daima uweze kuwa na nakala au uweze kupakia maelezo yako kwa huduma nyingine.

Vidhibiti vya Historia ya Wavuti ya Google

Ikiwa umeingia kwenye Akaunti ya Google, Historia ya Wavuti inakusaidia kukupa matokeo na mapendekezo yanayohusiana zaidi. Ukichagua, unaweza kufuta maingizo, sitisha ukusanyaji au zima huduma hiyo kabisa. Unaweza kufanya vivyo hivyo na Historia ya YouTube.

Dhibiti wanachoona watangazaji na tovuti

Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo

Matangazo husaidia kulipia huduma nyingi za bila malipo mtandaoni ambazo unapenda na kutumia kila siku. Ukiwa na Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo ya Google, unaweza kuelewa jinsi matanagazo yanavyochaguliwa kwa ajili yako, dhibiti maelezo yanayotumika kuchagua matangazo, na zuia watangazaji maalum.

Chaguo la Kujiondoa kwenye Google Analytics

Google Analytics huzalisha takwimu kuhusu wageni katika tovuti, kama vile idadi ya maoni ya ukurasa au nyakati za kilele cha trafiki ili kusaidia wachapishaji wa tovuti kuboresha tovuti zao. Ikiwa hutaki data ya kivinjari chako ishirikiwe na wachapishaji unapotembelea wavuti zinazotumia Google Analytics, unaweza kusakinisha kuchagua kutoka.

Jumatatu, Januari 27, 2014

MASHAMBULIZI NA USALAMA WA KOMPYUTA

Picha kwa hisani ya www.cybersecurepakistan.com


Hebu wazia kundi la wahalifu wenye ustadi wa kutumia kompyuta wakitumia Intaneti kuongoza mitandao ya kompyuta walizoteka nyara. Kompyuta hizo zinazojulikana kama botnets (mitandao ya roboti), zinatoa habari za siri zenye madhara zinazolenga taifa fulani. Baada ya dakika chache, Tovuti za kijeshi, kifedha, na kibiashara za taifa hilo zinaacha kufanya kazi. Mashine za benki za kutolea pesa (ATM) pamoja na mitandao ya simu inashindwa kufanya kazi. Usafiri wa ndege unakatizwa na kompyuta pamoja na mifumo ya usalama katika kituo cha kutokeza nguvu za nyuklia inavurugwa. Watu wangetendaje? Wewe ungefanya nini?
Huenda tukio hilo likaonekana kuwa lisilo halisi. Lakini kulingana na Richard A. Clarke, aliyekuwa Msimamizi wa Kitaifa wa Usalama, Ulinzi wa Miundo-Msingi, na Kupambana na Ugaidi nchini Marekani, jambo kama hilo linaweza kufanyika kihalisi. Isitoshe, tayari kumekuwa na mashambulizi kupitia kompyuta Huenda hata wewe umewahi kushambuliwa.

Kwa nini mtu awashambulie wengine kupitia kompyuta? Mashambulizi hayo hufanywaje? Na kwa kuwa ni kawaida kwa mashambulizi hayo kumlenga mtu mmojammoja, unaweza kujilindaje unapotumia Intaneti?

Uwanja wa Vita Kwenye Kompyuta

Kuna sababu kadhaa zinazowafanya watu wawashambulie wengine kupitia kompyuta. Kwa mfano, magaidi au serikali zinaweza kupenya kwenye mitandao ya kompyuta ya maadui wao ili waibe siri au waharibu vifaa vinavyoongozwa na mitandao hiyo. Katika mwaka wa 2010, Waziri Msaidizi wa Ulinzi wa Marekani William J. Lynn wa Tatu alisema kwamba “maadui” wa kigeni walikuwa wamepenya mara nyingi kwenye mitandao ya kompyuta iliyo na habari za siri za Marekani na kuiba “maelfu ya mafaili . . . kutia ndani maagizo ya kutengenezea silaha, habari kuhusu mipango ya kijeshi, na habari za upelelezi.”—Ona sanduku (LINK HAPO MBELE) “Mashambulizi ya Hivi Karibuni Kupitia Kompyuta.”

Wahalifu wanaotumia kompyuta hutumia njia sawa na hizo kuiba habari za kitaaluma au za kifedha kutoka kwa mitandao ya kompyuta ya makampuni na hata kompyuta za watu binafsi. Wahalifu hupata mabilioni ya dola kila mwaka kupitia biashara za ulaghai zinazofanywa kwenye mitandao.

Pia, wahalifu hao wameunganisha kompyuta nyingi sana walizoteka nyara ili waweze kutekeleza mashambulizi yao. Katika mwaka wa 2009, kampuni moja inayoshughulika na usalama wa intaneti iligundua kwamba kundi moja la “wahalifu” lilikuwa likidhibiti kisiri karibu kompyuta milioni mbili kotekote ulimwenguni, nyingi zikiwa ni za watu binafsi. Ripoti ya karibuni ya Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) linakadiria kwamba kompyuta 1 kati ya 3 zilizounganishwa kwenye Intaneti inadhibitiwa kisiri na mhalifu fulani. Namna gani kuhusu kompyuta yako? Je, mtu fulani anaweza kuidhibiti bila wewe kujua?

Maadui Wanaoshambulia Kimyakimya

Wazia tukio hili. Mhalifu fulani anasambaza programu fulani yenye madhara kupitia Intaneti. Programu hiyo inapoingia katika kompyuta yako, inapenya ndani ya programu inayolinda kompyuta yako. Programu hiyo yenye madhara inapopata eneo ambalo halijalindwa vizuri, inapenya ndani hata zaidi na kutafuta-tafuta habari muhimu katika kompyuta yote.

 Kisha programu hiyo inaweza kubadilisha au kufuta mafaili yaliyo kwenye kompyuta yako, na inajituma yenyewe kama barua pepe kwenye kompyuta zingine, au kumtumia mhalifu huyo neno lako la siri la utambulisho, habari za kifedha, au habari nyingine za siri zinazokuhusu.

Wahalifu hao wanaweza kukufanya uingize virusi kwenye kompyuta yako mwenyewe! Jinsi gani? Unaweza kufanya hivyo kwa kufungua barua-pepe inayoonekana kuwa ya kawaida tu, kwa kubonyeza kiunganishi cha Tovuti fulani, kupakua na kuunganisha programu ya bure ya kompyuta, kuingiza kifaa cha kuhifadhi habari kilicho na virusi katika kompyuta yako, au tu kutembelea Tovuti yenye kutiliwa shaka. Mambo yote hayo yanaweza kuingiza programu yenye madhara kwenye kompyuta yako na kuifanya idhibitiwe kisiri na mhalifu.

Unaweza kujuaje ikiwa kompyuta yako imeshambuliwa? Kwa kweli inaweza kuwa vigumu kugundua. Huenda kompyuta au Intaneti ikafanya kazi polepole sana, au programu zisitende kwa njia ya kawaida, au visanduku vijitokeze ghafula vyenye ujumbe unaokuomba uunganishe programu fulani, au kompyuta yako itende kwa njia isiyo ya kawaida. Ukiona mojawapo ya dalili hizo, mwombe mtaalamu wa kompyuta achunguze kompyuta yako.

‘Fikiria Hatua Zako’

Kadiri mataifa na watu mmoja-mmoja wanavyozidi kutegemea teknolojia ya kompyuta, ndivyo inavyotarajiwa kuwa mashambulizi kupitia kompyuta yataongezeka. Kwa sababu hiyo, mataifa mengi yanajitahidi sana kuboresha mbinu za kulinda kompyuta zao, na mataifa mengine yanapima uwezo wa mitandao yao ya kompyuta ili kuona ikiwa inaweza kustahimili mashambulizi. Lakini licha ya jitihada hizo, Steven Chabinsky, mtaalamu wa cheo cha juu wa usalama wa kompyuta wa Shirika la Upelelezi la Marekani anasema kwamba “adui aliyeazimia kabisa, hawezi kamwe—kamwe—kushindwa kupenya mfumo hususa anaolenga iwapo atakuwa na wakati wa kutosha, kichocheo, na pesa.”

Unaweza kufanya nini ili ujilinde unapotumia Intaneti? 

Ingawa huenda usiweze kujilinda kabisa unapotumia Intaneti, unaweza kuchukua hatua zifaazo ili kufanya kompyuta yako iwe salama zaidi. (Ona sanduku “Jilinde!”) Biblia inasema: “Mtu mwerevu huzifikiria hatua zake.” (Methali 14:15) Kwa kweli hilo ni shauri lenye hekima unapotumia Intaneti!


Mashambulizi kupitia kompyuta yamekusudiwa hasa kubadilisha, kukatiza, au kuharibu kabisa mifumo ya kompyuta au mitandao au habari au programu ambazo kompyuta huhifadhi au kusambaza.—Baraza la Kitaifa la Utafiti la Marekani linaeleza.

Katika mwaka wa 2011, wahalifu wa kutumia kompyuta wangeweza kutumia zaidi ya udhaifu 45,000 unaojulikana ili waweze kupenya katika kompyuta nyingine. Kwa kutumia udhaifu huo, wahalifu hao wanaweza kuingiza programu yenye madhara (malware) katika kompyuta za watu binafsi bila watu hao kujua.


Wahalifu wa kutumia kompyuta wameunganisha kompyuta nyingi sana walizoteka nyara. Kulingana na shirika la OECD, kompyuta 1 kati ya 3 zilizounganishwa kwenye Intaneti, inadhibitiwa kisiri na mhalifu fulani


MASHAMBULIZI YA HIVI KARIBUNI KUPITIA KOMPYUTA

  2003: Programu ya kompyuta yenye madhara inayoitwa Slammer ilisambaa haraka sana kwenye Intaneti na kushambulia kompyuta 75,000 hivi kwa dakika kumi tu. Utendaji wa Intaneti ukawa wa polepole sana, Tovuti zikaacha kufanya kazi, mashine za benki za kutolea pesa (ATM) zikashindwa kufanya kazi, usafiri wa ndege ukakatizwa, na kompyuta pamoja na mifumo ya usalama katika kituo cha kutokeza nguvu za nyuklia ikavurugwa.

  2007: Mfululizo wa mashambulizi kupitia kompyuta ulilenga Estonia na kuathiri mifumo ya serikali hiyo, vyombo vya habari, na hata benki. Mengi ya mashambulizi hayo yaliyotoka kwenye mifumo ya kompyuta zilizotekwa nyara (botnets) yaliathiri kompyuta zaidi ya milioni moja zilizoshambuliwa katika nchi 75 kwa kuzifanya zitume ujumbe mwingi wa uwongo wa kuomba habari.

  2010: Programu ya kompyuta yenye madhara na tata sana inayoitwa Stuxnet ilishambulia mifumo inayoendesha kituo cha kutokeza nguvu za nyuklia nchini Iran.


Programu za kompyuta zenye madhara hujinakili zenyewe kutoka kompyuta moja hadi nyingine kupitia Intaneti na programu za aina hiyo hupewa majina kama vile Slammer.

JILINDE!

 1. Weka programu za kuzuia virusi (antivirus), programu za kutambua programu za upelelezi (spyware-detection), na mfumo wa ulinzi (firewall) katika kompyuta yako. Hakikisha kwamba programu hizo pamoja na programu kuu ya kuendesha kompyuta yako inaboreshwa kwa ukawaida.

 2. Fikiria kwa uzito kabla ya kufungua viunganishi (links) au viambatanisho (attachments) vinavyotumwa kwenye barua-pepe au ujumbe wa haraka—hata ule unaotoka kwa marafiki. Jihadhari hasa ikiwa ujumbe huo unatoka kwa mtu usiyemfahamu na unaomba habari za kibinafsi au neno la siri.

 3. Usinakili au kutendesha programu za kompyuta kutoka katika vyanzo usivyovijua.

 4. Tumia neno ya siri la utambulisho lenye angalau herufi nane na utie ndani namba na ishara kadhaa, na uwe na zoea la kubadili neno hilo kwa ukawaida. Tumia maneno tofauti-tofauti ya siri kwa ajili ya kila akaunti yako.

 5. Fanya biashara kwenye Intaneti na mashirika yenye kuaminika ambayo yana mifumo salama.

 6. Usitoe habari zako za siri au za akaunti zako unapotumia vifaa ambavyo havijaunganishwa kwa nyaya [Wi-Fi], kama vile vinavyopatikana katika sehemu za umma.

 7. Zima kompyuta yako wakati ambapo huitumii.

 8. Uwe na kawaida ya kunakili habari zako, na uzihifadhi mahali salama.


Vituo vya intaneti salama vina ishara fulani, kama vile ishara ya kufuli na “https://” kwenye kisanduku cha anwani. Herufi “s” inamaanisha salama (secure).

Fanya yote uwezayo ili kujilinda unapotumia Intaneti

Jumatano, Januari 22, 2014

TUZO ZA MAWASILIANO ZA KIDIJITALI KUFANYIKA DAR ES SALAAM MWAKA HUU



Opt Media Information Solutions kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa Tanzania, inakuleteeni Tunzo za Njia za Mawasiliano za Kidijitali, zijulikanazo kama “Tanzania Digital Media Awards” (TDMA)


"Tanzania Digital Media Awards " ( TDMA ) inalenga kusherehekea na kutambua uvumbuzi unaotumia Wavuti, Tovuti, na Mitandao ya Kijamii katika kutoa huduma bora kwa wateja hasa kwa kutumia mawasiliano ya digitali kwa makampuni na mashirika mbalimbali hapa Tanzania.

TDMA, mradi unaosimamiwa na Opt Media Information Solutions (OMIS ), mnano Aprili, 2014, jijini Dar es Salaam, tutakuwa na tukio la sherehe za tunzo za utoaji tunzo zitakazo kusherehekea uvumbuzi na ubora katika mawasiliano ya kidigitali ya kisasa na yale ya kawaida yanayotumiwa na makampuni na mashirika mbalimbali ndani ya Tanzania, ili kuwafikia wateja au wadau wao. Toleo hili la Tunzo pia litatoa tuzo maalum za heshima na kutambua watu maarufu na wa kawaida wanaotumia teknologia za mawasiliano kuleta mabadiliko chanya katika jamii, ama wale wanaotengeneza teknologia zilizo na manufaa kwa jamii.

Ili kuhakikisha kwamba tunzo hizi zinapata heshima na sifa chanya kutoka kwa wadau na umma kwa ujumla, washindi wa tuzo watapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na umma pamoja na zile zinakazopigwa na jopo la majaji waliona mapenzi, shauku, utaalamu na watumiaji wa njia hizi za mawasiliano ya kidigitali hapa Tanzania, kutoka katika taasisi mahususi za umma na binafsi – yaani watalamu wa TEKNOHAMA, waandishi wa habari, watu wa masoko na mawasiliano pamoja na upashaji habari.


Katika siku za nyuma ikumbukwe kuwa, tovuti ilikuwa chombo cha kawaida tu ili kufanya wamiliki wake wawe mtandaoni, lakini hili miaka ya karibuni limebadilika. Kwani leo watumiaji ama  wasomaji wa tovuti wamebadilika zaidi. Pia mageuzi katika mawasiliano kwa kutumia mitandao ya kijamii yameleta mtazamo mpya katika tasnia ya ‘mawasiliano ya kisasa’ katika biashara, serikali, na asasi za kiraia. Kwa pamoja, mtandao, na mageuzi ya teknologia ya simu za mkononi imefanya watumiaji wa mitandao na wasiliano ya dijitali wadai uzoefu wa kudumu na tija kutokana na mawasiliano ya makampuni na mashirika mbalimbali kwa wadau wao. Kwa minajili hiyo unaweza kuona jinsi mawasiliano ya kisasa yalivyoleta mafanikio makubwa kwa mawasiliano ya makampuni, mashirika na asasi za kiraia. Hivyo katika zama hizi bidhaa si tena ile ambayo tunawaambia walaji kuwa ilivyo...bali bidhaa ile ambayo wateja wanaambiana jinsi wanavyoiona kwa mitazamo yao. Hiyo ndiyo nguvu mpya ya mawasiliano digitali na mitandao ya kijamii.

Tunzo za “Tanzania Digital Media Awards” zitafanyika katika moja ya hoteli za nyota 5 hapa Dar es Salaam, Aprili hii ya mwaka 2014. Taarifa zaidi juu ya mgeni rasmi na wa heshima, ukumbi pamoja na tarehe kamili zitatolewa katika mkutano wa waandishi wa habari ambao utafanyika Februari 28, 2014 hapa Dar es Salaam.


Ombi letu kwa umma na wadau wenye kutakia mafanikio ya Tunzo za TDMA, ni kuwa sote tunatambua umuhimu, na matumizi ya mawasiliano ya kidijitali kama mitandao ya kijamii, tovuti, wavuti nk kama sehemu muhimu ya kufanikisha mawaliano ya makampuni, mashirika na serikali. Tuendelee kutumia mawasiliano haya kwa tija na weredi kwani habari na wasiliano ni muhimu kwa kila mtu, kila kampuni , serikali, na mashirika, hivyo tuizitegemeze Tunzo hizi za Chaguo la Watu.


Ahadi yetu kwa umma ni kuwa tukio hili litaendelea kufanyika katika miaka ijayo na litakuwa ndiyo tukio kubwa litakalo kutanisha watu wakaliba mbalimbali wa ulimwengu wa biashara na mashirika. Pia lengo letu ni kuhakikisha viwango vya juu ambavyo ndio msingi wamafanikio ya Tunzo hizi unafuatwa ili kulinda heshima na taswira za wadau na wafadhili wetu kwa kuwalete usiku wa sherehe zilizoandaliwa kwa uweredi mkubwa.



IMETOLEWA NA:


JONATHAN N. MNYELA

GENERAL MANAGER

OPT MEDIA INFORMATION SOLUTIONS


jonathan.mnyela@omis.co.tz

+255714060608

CHANZO: MaishanaTeknohama.blogspot.com

Jumatano, Novemba 13, 2013

MTANDAO SAYANSI

Photo Credit By: http://theamazingworldofpsychiatry.wordpress.com


Unaweza kuwa mtumiaji ulie makini wa Mtandao, lakini hii kozi ya utangulizi katika Mtandao Sayansi itakusaidia kuelewa Mtandao wote kama mfumo wa kijamii na mfumo wa kiufundi: habari za kimataifa, miundombinu inajengwa kutokana na mwingiliano wa watu wataalamu wa teknolojia.

Inachunguza asili na mageuzi ya Mtandao na fikirisha maswali muhimu ya Usalama, Mtandao wa Demokrasia na Uchumi kutoka mitazamo yote Computational na sayansi ya jamii.

Kwa kufuata kozi hii, utakuwa na uelewa mkubwa wa Mtandao na kuanza kuendeleza ujuzi kwa ajili ya zama hizi za kidigitali - ujuzi ambao ni muhimu kwa ajili ya maisha ya kila siku kwa upana uliopendekezwa na teknolojia unaoongoza na waajiri wa leo.

Huu ni mwanzo wa safari ambayo inaweza kusaidia sura ya baadaye ya mtandao wa dunia nzima.

Jumatatu, Novemba 11, 2013

TEKNOHAMA: NI UFANISI AU CHANZO CHA UGOIGOI KWENYE AFYA? - Sehemu ya 1



Nikiwa kama mjukuu kipenzi wa bibi yangu, huwa napenda sana kutumia muda wangu wa mapumziko kujadiliana naye mambo mbalimbali yanayohusu jamii, iwe yaliyokuwa yanatokea hapo awali au yanayoendelea kutokea. Ilikuwa ni siku ya jumapili baada ya kutoka kwenye mihangaiko, niliingia ndani na kumuita bibi kwa jina lake la utani ‘Nyaksi’ ili twende nje tukapunge upepo na mazungumzo ya hapa na pale.
 
Kama ilivyo ada yangu, huwa napenda sana kutafiti mambo mbalimbali, nikamuuliza bibi, eti bibi nimewahi kusikia kuwa wakati wa enzi zenu mlikuwa hamruhusiwi kula mayai wakati wa ujauzito kwa kuwa mtoto atazaliwa bila nywele? Bibi Nyaksi huku akitabasamu akanigeukia na kusema, "umeshaanza, kwanza usikumbushe enzi zile bado nipo mbichi" akimaanisha wakati yupo msichana. Wote tukatabasamu kwa pamoja. Nyaksi akaendelea kusema sio mayai tu, bali vyakula vyote nyenye virutubisho kwa wingi ambavyo ninyi vijana wa leo mnaviita ‘purotini’, akiitamka protini kwa lafudhi ya kizee. Nyaksi alisema tulizuiliwa kula vyakula hivyo kwa mlengo wa mwiko, akaendela kusema, unajua Babu (jina langu alilopenda sana kuniita Nyaksi) wazee walitumia mwiko ili kututisha lakini ukweli ni kuwa wakati ule hakukuwa na tekenolojia (akimaanisha teknolojia) hivyo kama utakula vyakula vyenye virutubisho sana vitamfanya mtoto awe mkubwa, na hivyo kama utashindwa kujifungua kwa njia ya kawaida basi hakutakuwa na njia nyingine ya kukusaidia. Nyaksi akaendelea ninyi vijana wa siku hizi mna raha, hospitali nyingi, madaktari wengi huku mna njia nyingi mbadala ikiwemo ya upasuaji na nyinginezo.

   Nilimuacha Bibi Nyaksi amalizie maneno yake, halafu nikamuuliza, kama sisi tuna teknolojia na njia nyingi za kisasa, sasa inakuwaje urefu wa maisha wa vizazi vyetu unazidi kupungua kadri teknolojia inavyozidi kukua? Nyaksi alicheka sana, huku akipigapiga makofi ili kuvuta hisia alisema " hakuna kizuri kisicho na kasoro". Baada ya hapo tukaacha kuongelea masuala ya afya na kuketi chini ili kupunga upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi kutokea Kinyanyiko.

  
Kipindi chote naburudika na upepo uliokuwa unavuma ukitokea kwenye mabonde ya Kinyanyiko nilikuwa natafakari mambo mengi kuhusu maneno ya Nyaksi. Misemo yake ilikuwa inazungukazunguka kichwani kwangu , huku maneno "Hakuna kizuri kisicho na kasoro " na " ninyi mnaishi kwenye ulimwengu wenye tekinolojia" vikijitokeza mara kwa mara. Lakini je, hizi teknolojia zinatunufaisha vipi? Zipi faida na hasara zake? Hivyo nikawa nachorachora chini nikiainisha viambatanishi vyote vya hii tunayoiita teknolojia, nikarudi haraka nyumbani na kuchukua iPad yangu kuanza kuandika makala hii ambapo tutaiangalia teknolojia kwa mapana na jinsi gani teknolojia inavyoweza kuongeza ufanisi katika medani ya afya.

Teknolojia ni nini?

   Teknolojia ni utengenezaji,matumizi,maarifaya vifaa,machine,mitambo,uashi ili kutatua tatizo au ketenda kazi husika, iwe ni kwenye matibabu au kwenye michezo. Katika makala yetu ya leo tutaangalia sana hii teknolojia ya mawasiliano ya mtandao yaani ICT. Kwa wale maveterani kama mimi mtakumbuka teknolojia hii ilianza kuibukia kwa kasi sana nyumbani katika miaka ya tisini, katika wakati huo teknolojia hii siyo tu ilionekana kuwa ni kitu cha anasa bali pia ni kwa wenye nazo tu. Teknolojia hii ilihusishwa na viashiria chungu mzima kama kwenda na wakati, usomi, umjini n.k. kitu ambacho kimetufikisha hapa tulipo.


Mtazamo wa jamii juu ya teknolojia

   Kama nilivyoelezea hapo juu, asili na historia juu ya ujio wa teknolojia hii ya mawasiliano ya mtandao inachangia sana katika ujengekaji wake, kwa mfano hapa kwetu wengi bado wana mtazamo hasi kuwa teknolojia hii ni kwa ajili ya wasomi au wenye uwezo, ingawa dhana hii inaendelea kubadirika siku hadi siku, lakini tatizo bado lipo. Nani wa kulaumiwa? Ni wanajamii au sisi wana mawasiliano? Jibu ni fupi. Hakuna wa kulaumiwa bali hatuna budi kutafakari juu ya namna ya kuliboresha na kulihalisisha kwa jamii yetu.

Muundo wa teknolojia kwenye karne ya 21

   Katika makala yake ya sababu za watoto wachanga kulia, Dk Paul Mwanyika amefafanua kwa undani hatua ambazo mtoto hupitia katika ukuaji, kwa muktadha huohuo nami naufananisha ukuaji wa teknolojia na ule wa mtoto. Kwa ufupi, teknolojia imepitia hatua nyingi. Kwa mfano hapo zamani teknolojia ilikuwa ni kwa ajili ya kurahisisha kazi au utendaji, lakini leo hii teknolojia imegeuzwa kuwa sehemu ya kazi na siyo tena kitendea au kirahisisha kazi.
   Si kitu cha kushangaza kusikia mtu anauza madawa mtandaoni (online) bila kuwa na duka nje ya mtandao (brick shop). Aidha leo hii madaktari wanaweza kupata muongozo au kushiriki kwenye upasuaji bila kizuizi cha umbali. Huu ndiyo muundo wa teknolojia ya sasa, tunatumia teknolojia kama huduma/kazi (Technology As A Service) na siyo tu kitendea kazi.

Faida/Matumizi za teknolojia kwenye Afya

   Lengo la makala hii ni kuwaamsha (kumbusha) wanajamii umuhimu au njia mahususi za kutumia teknolojia katika kujenga afya bora. Msukumo wa makala hii umekuja kutokana na matokea ya utafiti
niliyofanya kwenye tovuti ya TanzMED.com. Ndani ya tovuti hii kuna sehemu ambayo mtumiaji anaweza kujisajiri akawa anapokea taarifa mbalimbali kuhusiana na afya (milisho ya afya). Nilichogundua ni kuwa uwiano wa wanaojisajili kwa wanaotembelea ni chini ya 1%. Baada ya kuwauliza watembeleaji wengi kwanini hawajisajili, karibu 20% walisema hawafahamu jinsi ya kutumia njia hiyo, wengine 20% hawajui uwepo wa programu hii na waliobaki ni kutotambua umuhimu wa kufanya hivyo. Hii ni sehemu ndogo tu ambayo matumizi ya teknolojia yanaweza kukurahisishia kujenga afya bora.

Hivyo tuangalie kwa kila kundi ni jinsi gani linaweza kunufaika na teknolojia.

Madaktari 

   Wakiwa ndio watendaji wakuu, ni dhahiri kuwa madaktari ni moja ya watu wenye heshima kubwa sana kwenye jamii yetu. Wengi tumekuwa tukiwaamini na kuwakubali madaktari kwa kiwango kikubwa zaidi. Leo hii kuna mitandao jamii kama Facebook, Twitter na hata TanzMED.com (Jumuiya), kwa kutumia mtandao jamii daktari anaweza kuwasiliana na wanajamii akawapa mustakabali wa masuala ya afya, kwa mfano nimewahi kuona vipachiko kadhaa vya Dk Fabian Mghanga kwenye Facebook, akiwa anapachika mambo yaliyo motomoto kwenye jamii yetu kwa sasa, wanajumuiya wote wanaomfuata huweza kuona vipachiko vyake na kubadilishana naye mawazo au kutolea maoni. Si hayo tu daktari pia anaweza kutumia programu za mawasiliano kubadilishana mawazo (kuchat) na wagonjwa walioruhusiwa ili kufuatilia hali zao na kuwafariji. Vilevile daktari anaweza kutumia simu kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa wagonjwa walio hospitali akiwakumbusha kunywa dawa na kufanya mazoezi ya asubuhi au jioni. Wagonjwa watafarijika sana endapo wanapokea ujumbe toka kwa daktari unaomsisitizia jambo fulani. Hivyo muda umefika sasa kwa madaktari wetu kubadirika na kuanza kutumia fursa hizi ambazo zinawezekana na kupatikana kwenye mazingira yetu ya Tanzania.

 Chukulia mfano, kwanini mahospitali yasichukue namba za simu za wagonjwa wote na kuzipanga kulingana na aina ya magonjwa yao halafu wakawa wanawatumia ujumbe au taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo au tahadhari muhimu juu ya magonjwa yao?

Vyombo vya habari & Wasanii

   Hii ni moja ya sehemu ambazo zina ushawishi na upenzi mkubwa mno kwenye jamii. Katika baadhi ya nchi zilizoendelea, unaweza kukuta uwepo wa televisheni au redio zinazohusu masuala ya afya pekee. Kwa nchi kama Tanzania wamiliki wa hizi televisheni, magazeti au redio wanaweza kutumia vituo vyao kufikisha maarifa, ufahamu na hata ujumbe juu ya afya. Kwa kushirikiana na watu maarufu na wasanii dhana hii inaweza kukubalika na kufika mbali zaidi.

Makampuni ya teknolojia

   Makampuni yanayojihusisha na mawasiliano ya mtandao, kuanzia makampuni ya simu, watengeneza programu nk, yanatakiwa kushirikiana na wadau wa medani ya afya katika kuhakikisha wanainufaisha jamii. Kwa mfano kampuni ya Dudumizi Solutions imejiunga na kundi la madaktari na kuanzisha mtandao wa Afya ujulikanao kama www.tanzmed.com. Hii ni chachu na changamoto kwa wadau kuonesha kuwa sasa teknolojia ni sehemu ya jamii hivyo tunatakiwa kujihusisha zaidi, tubadilishe utendaji au mfumo wa teknolojia. Kwa mfano makampuni ya simu yanaweza kuja na programu ambazo zitawawezesha wanajamii kutuma namba fulani halafu wakapata elimu au taarifa fupi za masuala ya afya (kama ile inayofanya kwa mama wajawazito). Aidha wataalamu wa programu wanaweza kuja na programu inayoweza kutumika kwenye simu kumuwezesha mtu kukokotoa afya yake (BMI Calculator), kujua siku ya kujifungua nk, hii ni mifano michache ambayo wadau wa ICT wanaweza kuitumia kujenga jamii yenye afya njema. Nimeongelea kwa ufinyu wake kutokana na hali halisi ya maendeleo ya ICT kwa nchi yetu ingawa tunaweza kwenda mbali zaidi ya hapo.

Wanajamii

   Wakiwa ndio walengwa namba moja, wanajamii wanatakiwa kuanza kutumia teknolojia kama sehemu ya kujenga afya yao. Kwa mfano unaweza jiunga kwenye milisho (Subscription) ya tovuti mbalimbali za afya ambapo utakuwa unapokea taarifa mbalimbali za afya kama; mabadiriko ya hali ya hewa, magonjwa ya milipuko, kinga na mengineyo. Mara nyingi makala hizi huwa zinachujwa kuhakikisha unatumia taarifa inayojieleza. Hivyo jijengee mazoea ya kutumia teknolojia kwa ajili ya afya yako, iwe kuuliza maswali juu ya afya au kusoma dalili na kinga za magonjwa mbalimbali. Mtandao wa www.tanzmed.com una yote haya kwa ajili ya afya yako.

   Nilipomaliza kuainisha baadhi ya faida za teknolojia, kuna maneno ya Bibi Nyaksi yakawa yaniumiza," Hakuna kizuri kisicho na kasoro". Hivyo tuangalie athari za hii teknolojia.

Kuvunja maadili na mipaka ya teknolojia

   Kutokana na ujio wake, wengi wamekuwa wakitumia teknolojia bila mipaka. Maadili ya teknolojia yamepigwa kumbo. Kwa mwandishi wa TanzMED Dk Fabian Mghanga ameeleza jinsi gani dawa za kuongeza makalio zinavyoshabikiwa, huku zikiwa hazina maelezo ya kuridhisha juu ya matumizi na namna zinavyofanya kazi. Ushabiki huu pia huchochewa sana na matumizi ya mitandao jamii kama vile Facebook, ambapo baadhi ya watu hutuma matangazo au picha zenye mvuto na kuwafanya akina dada wengi wahamasike kwa kutaka kuwa na mvuto kama waliouona kwenye picha. Si hayo tu, tumeona pia jinsi mwandishi Dk Henry Mayala alivyotuelezea jinsi vumbi la viwandani linavyoweza kukusababishia pumu au magonjwa ya mfumo wa hewa, haya yote ni kwa sababu ya kuvukwa kwa mipaka ya maadili ya teknolojia kwa watoa huduma. Uvukaji wa mipaka siyo tu kwa watengenezaji (watoa huduma) za teknolojia bali pia kwa wanajamii. Kwa mfano katika makala yake ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi Dk Khamisi Bakari amesema sababu mojawapo ni matumizi ya intaneti kwa muda mrefu, hii ni inatuonesha mifano dhahiri ya athari zinazosababishwa na utokaji nje ya maadili ya teknolojia kwa mtumiaji. Hivyo maadili ya teknolojia ni lazima yaheshimiwe.
 

Maadili na mipaka ya kazi

   Nakumbuka kuna wimbo mmoja wa wanamuziki wa kizazi kipya wanaoitwa Wagosi wa Kaya uitwao wauguzi kuna kipande cha mstari kinasema; "...nesi anaongea kwa simu na bwana wa kizigua". Hii ni moja ya athari za teknolojia. Kuna wakati unatamani hata upigane, maana unaenda hospitalini huku kuna foleni kubwa inasubiri kumuona daktari, lakini yeye yupo bize kwenye simu akicheka kuhusu matokeo ya mpira wa jana. Hapo sizungumzii muda wanaotumia kuangalia picha na maoni kwenye Facebook au kuchat kwenye Yahoo na rafiki yake aliye Wuhan. Idara husika lazima iweke mipaka na maadili ya kazi yatakayomuongoza muhusika katika matumizi ya teknolojia. Tukumbuke kuwa teknolojia sasa imekuwa ni kazi na maisha hivyo haiepukiki.

   Wakati namalizia haya maneno ya mwisho chaji nayo ikawa imeisha kwenye iPad yangu, ni bahati mbaya kwamba jana sikuichaji kutokana kukatika kwa umeme. Sasa basi inanibidi kusubiri umeme urudi ili niweze kuichaji na kumalizia makala hii ambayo nitaituma kwenye jarida lijalo, makala ambayo itazungumzia mambo ambayo ningependa kuishauri jamii/serikali ifanye ili kujenga na kudumisha afya bora kwenye karne hii ya teknolojia

Chanzo: INGIA HAPA

Jumapili, Juni 30, 2013

VIFAA VYA KUTUNZIA KUMBUKUMBKUMBU NJE YA KOMPYUTA VIJULIKANAVYO KAMA REMOVABLE DEVICES.


Kama ilivyo kwa mashine kadhaa na vyombo mbalimbali, kompyuta inaweza kupata hitilafu na hatimaye kupoteza kumbukumbu muhimu sana katika maisha ya kawaida ya jamii. Hivyo panapaswa kuwa na njia mbadala ya kutunza kumbukumbu pindi ikitokea tatizo kama hilo. Kuna vifaa maalum vya kutunzia kumbukumbu ambazo ni muhimu mno. Vifaa hivi huweza kuingizwa katika kompyuta, kuchukua kumbukumbu na kuvitoa kwenda kuvihifadhi mahali ambako ni salama zaidi. Vifaa hivi vinafahamika kama storage devices. Kwa sababu vifaa hivi huweza kutolewa ndani ya system case ya kompyuta hufahamika pia kama removable devices.

Vifaa hivi huingizwa katika Kompyuta kwa kupitia matundu maalum yafahamikayo kama ports na milango maalum ifahamikayo kama drivers. Vyote hivi hujengwa katika system case na huonekana sehemu ya mbele na ama sehemu ya nyuma ya system case.
System case ikiwa na milango na tundu vifahamikavyo kama drivers na port

CD ni nini?

Hiki ni kifaa cha kutunzia kumbukumbu na ambacho kinaonekana kuwa kama kimekuwa mbadala
wa tapes zilizozoeleka kwa muda mrefu katika utunzaji wa muziki na habari mbalimbali. Ni kifaa
ambacho kinatunza kumbukumbu za aina zote; ikiwa na maana text (maneno na picha), sauti na
video. Kifaa hiki kina umbo bapa la mviringo na kina sehemu iliyo kama kioo ambako habari na
data huwekwa. Bila shaka umekwisha kutana na kifaa hiki katika maisha ya kila siku.
 
Picha ya CD

CD ni kifupi cha maneno Compact Disc. Disc hii imetengenezwa kuhifadhi habari na data katika mfumo wa digital, teknolojia mpya ya kuhifadhi kumbukumbu ambayo imeiweka kando teknolojia ya zamani iliyofahamika kama analogue. Kwa mfano mikanda ya muziki na filamu ambayo ilikuwa na mkanda ulioviringishwa katika kifaa kilichoweza kuzunguka na hatimaye kutoa sauti ama kuonesha picha (tazama picha hapa chini) ilikuwa imeundwa kutumia teknolojia ya analogue.      
VHS tapes

CD huingizwa katika kompyuta ili kuwekewa ama kuingiza data na habari katika kompyuta.Kitendo cha kupeleka data na habari kwenye kompyuta hufanywa na kifaa maalum kilicho namlango ambao hufunguka na kufunga na ambao unaweza kubeba CD. Kifaa hiki hufahamika kama CD driver. Mlango huu huwa na taa yenye rangi ya njano-kijani ambayo huwaka pindi CDinapokuwa imewekwa na inafanya kazi ya kusoma data na habari. Kwa kawaida utasikia sauti ya CD kuzunguka katika CD driver. CD driver hufanya kazi ya kuiwezesha kompyuta kuitambua CD na kuifanya ipeleke data au kutoa data. Kazi hii ya kupeleka data au kuifanya kompyuta ipokee habari na data kutoka kwenye CD huitwa reading ama kusoma kwa kiswahili. Kama mtu anakwambia kompyuta inasoma data au habari zilizo katika CD anakuwa anamaanisha kuwa kompyuta hiyo inahamisha data kutoka kwenye CD kwenda katika sehemu ambayo huwezesha data kuonekana kwenye monitor, sehemu ambayo hufahamika kama random access memory

(RAM). Pia kitendo cha kuhamisha data kutoka kwenye kompyuta (yaani hard disk) kwenda kwenye CD hufahamika kama writing ama kuandika. Kitendo cha kuandika habari na data katika CD kutoka mahali zilipohifadhiwa (hard disk) kinawezekana tu kama CD driver ambako CD hiyo huwapo inaweza kuandika habari na data kama itakavyoelezwa hapo baadaye.

Kwa kawaida CD ina uwezo wa kuhifadhi habari ama data zenye ukubwa wa MB 700. Kwa hiyo Kama una habari ama data zenye ukubwa huo na unataka kuzihamishia kwenye kompyuta basi utakuwa unahamisha MB 700 na kama unataka kuzihamisha kutoka hard disk kwenda CD basi utakuwa unahamisha MB 700. Kwa kawaida software nyingi huja zikiwa zimehifadhiwa ndani yaCD na huingizwa katika kompyuta kwa njia ya hizi. Kwa mfano Kama tulivyo sema software mamayaani OS hutakiwa kuingizwa katika hard ware part ya kompyuta ili kuifanya kompyuta ifanyekazi. Software hii huwa ndani ya CD. Kitendo cha kuingiza software ndani ya kompyuta kupitia
CD hujulikana kama installation. Kuna hatua za kufuata katika kufanya kitendo hiki na mara nyingi ni wataalam wa masuala ya kompyuta wanafanya kazi hii. CD pia huhifadhi habari mbalimbali kama muziki, picha za video na za kawaida na data za aina nyingine.

 
Kuna aina kadhaa za CD kulingana na teknolojia ya kuzitengeneza

CD kwa kawaida zimegawanyika katika makundi kadhaa

DVD – aina ya CD yrnyr uwezo mkubewa wa kuhifadhi habari na Data

DVD ni kifupisho cha maneno Digital Versatail Disc. Ni aina ya CD ambao ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi data na habari na hakika ni kutokana na uvumbuzi wa kifaa hiki kumeweza kuwa na ubebaji wa data au habari nyingi kwa wakati mmoja. Kifaa hiki kinafanana kabisa kabisa na CD ya kawaida kimuonekano. Tofauti yake na CD ya kawaida ni teknolojia iliyotumika katika utengenezaji. Kwa kawaida CD hutengenezwa ikiwa na sehemu ndogondogo zijulikanazo kama tracks. Tracks hizi huwa katika mpangilio maalum wa mviringo. Kwa sababu CD ni ya Duara, kuna duara nyingi zilizobeba tracks zinazofahamika kama sectors. Data au habari hutunzwa katika kila track ambazo kusanyiko wa tracks huzaa sectors.

Utengenezaji wa CD hutofautiana na ule wa DVD kutokana na mpangilio wa sectors na tracks. Katika DVD kuna tracks nyingi katika sector moja kuliko katika CD ya kawaida. Kwa namna nyingine tunaweza kusema kuwa DVD ina sector nyingi kuliko CD. Kwa namna hii DVD inakuwa na uwezo wa kubeba data nyingi sana kuliko CD. Tuliona kuwa CD ina uwezo wa kubeba data katika uwezo wa kikomo cha MB 700. Hii ni tofauti kwa DVD ambayo ina uwezo wa kubeba data mpaka mara saba zaidi ya ile ya CD. DVD inaweza kubeba data au habari mpaka kufukia MB5000 au GB 5. Ni kwa namna hii ndiyo maana watengenezaji wa filamu na muziki hupenda
kuhifadhi filamu zaidi ya moja (mpaka kufikia 20) katika DVD.

Kama CD pia DVD inaweza kuwa tupu na ukahifadhi data au habari kwa kutumia kompyuta. Hizihuwa zinakuwa katika mfumo wa kuweza kuandikwa. Kuna DVD – R na DVD – RW. DVD – R inasimama badala ya DVD – Recordable ikiwa na maana kuwa unaweza kuhifadhi data kwa kuiandika (writing) mara moja pekee na baada ya hapo inakuwa DVD ya kawaida (yaani ya kusoma tu). DVD – RW inasimama badala ya DVD – Rewritable ikiwa na maana kuwa ina uwezo wa kuhifadhi data au habari zaidi ya mara moja; ikiwa na maana kwamba unaweza kuhifadhi data ukazifuta na kuweka nyingine tena. Hata hivyo kuna ukomo wa kuandika data katika DVD ambapo
inakuwa haina uwezo tena wa kufutwa.

Ili uweze kutumia DVD katika kompyuta inakubidi uwe na DVD river. Hii ni tofauti na DC driver ambayo huwezesha CD kutambulika katika kompyuta. DVD driver imetengenezwa katika tekonlojia ambayo inawezesha kusoma DVD. Kwa kawaida DVD driver huwekwa ktika system case mahali ambako CD driver huwekwa na kuunganisishwa na mothreboard kwa kutumia nyaya zilezile zitumikazo kuunganishia CD driver.

System case ya kompyuta huwa na milango zaidi ya mmoja (inaweza kufikia mitatu) inayowezesha drivers kufungwa na kuunganishwa na motherboard. DVD driver inaweza kuwekwa katika mlango ambao CD driver inatumia. Hata hivyo habari nzuri ni kwamba teknolojia iliyotumika kutengenezea CD driver iitangulia kabla ya ile ya kutengenezea DVD driver, hali inayoifanya DVD driver kuweza kusoma (kutambua) CD na DVDs. Kwa maana hiyo ukiwa na DVD driver katika kompyuta unakuwa na uwezo wa kutumia CD na DVD. DVD driver huwa zimeandikwa DVD ROM au DVD RW katika milango ya kupachika CD au DVD na CD driver huwa zimeandikwa CD ROM au CD RW katika mlango wa kuwekea CD. 

CD & DVD Driver



CD na DVD huweza kutunza data na kumbukumbu kwa muda ambao hutegemea na utunzaji wake. Kwa kawaida CD au DVD huwa na tundu katikati ambalo hutumika kama kishikio

kinachomwezesha mtumiaji kutogusa sehemu ya nyuma ambayo huonekana iking’aa na inayoweza kuonesha taswira mathalani ya uso wa mtu. Sehemu hii ndiyo huwa na data. Kama sehemu hii ikiguswa na uchafu mathalan vumbi na mafuta kutoka mikono ya mtumiaji inaweza kusababisha data kutotumika vyema. Athari ya uchafu katika CD au DVD huonekana mara unapoingiza katika driver ya kompyuta. Haitakuwa inazunguka vyema na itakuwa inakwama kila mara na hii hatimaye hufanya data kutosomeka vyema au kupotea kabisa.

Kwa kawaida CD na DVD huwa zimehfadhiwa katika mifuko laini ya nailoni ambayo huzuia vumbi na uchafu mwingine. Kwa maana hiyo unapotumia CD au DVD inakupasa kuhakikisha kuwa unaiihifadhi vyema katika mifuko ya nailoni na hakikisha kuwa haugusi sehemu zinazong’aa. Kama utahakikisha kuwa unafanya matunzo mazuri basi CD au DVD kitakuwa chombo kizuri cha kuhifadhi data.

Floppy Disk - Kifaa cha kwanza kutunzia na kuhamisha habari au Data katika
Kompyuta

Floppy Disk ni kifaa chenye umbo la penbe nne kama msitatili hivi ambacho kwa muda mrfu kiliyumika kuhifadhi data au kuhamisha data kutoka kompyuta moja kwenda nyingine. Kifaa hiki kina sehemu ndogo laini yenye umbo la mviringo ambayo kwa kawaida huwa imefichwa katika sehemu ngumu ya nyuma na ya mbele. Sehemu ya mbele inaweza kusukumwa mbele na nyuma ili kuwezesha data au habari kuandikwa na kusomwa na kompyuta ndani ya driver ifahamikayo kama floppy driver. Floppy Disk ni tofauti kabisa na Cd au DVD katika ubebaji wa kumbukumbu na data kwani inatumia teknolojia tofauti.







Tofauti na CD au DVD drivers, Floppy driver haina mlango ambao unaweza kufunguka na kufungwa badala yake huwa na tundu dogo la pembe nne ambalo huwezesha floppy disk kuchomekwa kwa kusukuma ndani taratibu. Floppy disk hutolewa ndani ya kompyuta kwa kubonyeza kitufe kidogo kilicho pembeni ya tundu la kuuingizia. Kuna aina mbili za floppy disk drivers, ile ambayo inakuwa kama sehemu ya system case ya kompyuta kama inavyoonekana katika picha A hapo juu na ile ambayo inaweza kuungwa katika kompyuta kwa kutumia waya wa
kuingiza na kutoa data (cable) ifahamikayo kama external floppy driver picha B hapo juu.

Floppy disk inaonekana kutotumika katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu teknolojia yake inaonekana kupitwa na wakati. Hii inachangiwa na ukweli kwamba ina uwezo mdogo wa kuhifadi data na kumbukumbu. Ina uwezo wa kubeba na kuhifadhi data na habari zenye ukubwa wa MB 1.35 tu. Hii inaifanya kuweza kubeba habari na data zenye ukubwa mdogo sana ambazo mara nyingi ni maandishi (text files). Kumbuka kuwa kiwango hiki kinazidiwa na DVD kwa zaidi ya mara 5000!

Zip Disk – kifaa cha kutunzia na kubebea kumbukumbu kinachofananishwa
na CD

Kabla ya uzinduzi wa CD palikuwa na kifaa ambacho kiliweza kubeba data na kumbukumbu kwa kiasi kikubwa kama kile cha CD ya kawaida. Kifaa hiki hufahamika kama Zip Disk. Kina umbo sawa na lile la Floppy disk. Ni kifaa ambacho kina uwezo wa kuhifadhi data na kumbukumbu zenye kufikia kiwango cha MB 700. hata hivyo kifaa hiki kinaonekana kutotumika tena na ni wachache sana ambao wanakitumia ni nadra kukuta kompyuta za kisasa zikiwa na Zip Driver, driver ya kuwezesha kompyuta kuitambua Zip Disk.

Hata hivyo system case nyingi za kisasa huwa na CD au DVD driver pamoja na Flopp Driver
pekee.

Memory Stick almaarufu Kama Flash Disk

Hiki ni kifaa ambacho kinatumika sasa katika miaka ya hivi karibuni katika ubebaji na uhfadhi wa data. Ni kifaa kidogo ambacho kinaweza kulingana na kidole gumba cha mtu mzima. Memory stick kinafahamika sana kama Flash Disk kwa watumiaji wengi wa kompyuta na kinaundwa katika maumbo na mtindo mbalimbali. Kinafahamika kama Flash Disk kwa sababu data zake au kumbukumbu zinazohifadhiwa zinaweza kufutwa na kuandikwa kwa muda mfupi na mara nyingi kuliko kifaa kingine kinachoitwa removable storage device. Kifaa hiki kinatofautiana ukubwa wa kuhifadhi data tofauti na vifaaa vingine tulivoviona hapo juu. Memory stick huwa na ukubwa unaoanzia MB 128 mpaka GB zaidi ya 10. Ni kifaa ambacho kinapendwa na watu katika kuhifadhia kumbukumbu kwa sababi ni kidogo kwa umbo na kinaweza kubebwa kwa urahisi hata katika mfuko wa suruali.

Memory stick huwasiliana na kompyuta kupitia matundu maalum yajulikanayo kama (USB ports) Universal serial Bus ports. Haya ni matundu ambayo huwa nyuma na ama mbele ya system case ya kompyuta. Kwa kawaida matundu haya hutumika pia kwa kupachika vifaa kama Mouse, Camera na printers. Memory stick huandikwa ukubwa ilio nao katika sehemu ya nje. Unaweza kukuta memory stick ya kampuni ya Sony ikiwa na MB 512, kwa mfano.

Memory sticks zinatunika sana sasa katika uhamishaji na ukusanyaji wa data na habari na kuhamisha kati ya kompyuta moja na nyingine. Tutaona baadaye madhara ya matumizi ya CD, DVD, Floppy Disk, na Memory stick katika kompyuta.

Memory stick kama vilivyo vifaa vingi vya kielektroniki, imeundwa kwa kutumia muunganiko wa sakiti ndogo ambayo huwa imehifadiwa ndani ya material aina ya plastiki. Unapoishika flash disk unakuwa unaona umbo au material haya ya nje tu ambayo ndani yanakuwa yamehifadhi sakiti inayohifadhi data au habari. Sakiti hii huwa na sehemu iliyotokeza nje ambayo hapa tunaweza kuiita mdomo ambao ndio huingizwa katika tundu la kompyuta (USB port).

Removable devices zina umri wa kuishi!

Kwa kawaida CD, Floppy disk, DVD, na vifaa vinginevyo vya kuhifadhiwa ambavyo vinabuniwa kila kukicha vina muda maalum wa kuhifadhi kumbukumbu. Baada ya muda fulani ambao hutegemea na utunzaji wa kifaa husika kifaa hicho kinakuwa hakina uwezo tena wa kuhifadhi kumbukumbu hizo. Kuna sababu kadhaa ambazo zinafanya vifaa hivi kuishiwa na ama kukosa kabisa uwezo wa kuhifadi tena kumbukumbu. Zifuatazo ni baadhi ya sababu hizo:

Uchafu

Hapa inamaanisha hasa vumbi katika vifaa hivi. Kwa kawaida vifaa kama CD na Floppy Disk huwa na sehemu ambayo huakisi mwanga ambao ndio hufanya kazi ya kutafsiri data na habari. Sehemu hizi kwa kawaida hutakiwa kuwa safi kabisa. Endapo itatokea vumbi na chembechembe zozote za uchafu zikakutana na sehemu hizi basi kumbukumbu zilizohifadhiwa juwakatika hatari ya kupotea. Na mara nyingi dalili ya kutofanya kazi kwa ufanisi ni kukwama-kwama kwa CD au kuchukua muda mrefu kufunguka kwa floppy disk pindi zinapokuwa katika drivers. Hali hii hatimaye husdababisha kompyuta kutosoma kabisa kumbukumbu hizi. Na ndiyo maana watengenezaji wa CD huziweka katika makasha na vifuko maalum ambavyo huzuia vumbi na vitu vingine kuingia katika sehemu ya nyuma ambayo ukiitazama vyema utagundua kuwa ni kama kioo. Pia floppy disk huiifadhi sehemu ya kusoma data ndani ya plastiki ngumu ambayo hufunguka na kubaki wazi pindi inapoingizwa kwenye floppy driver.

Plastiki ama aluminium ambayo huhifadhi sehemu ya kusoma data ambayo hubaki wazi pindi inapoingizwa kwenye kompyuta

Maji ama unyevu

Haya huweza athiri vifaa fivi kwa maana kwamba pindi yanapoingia katika vifaa g