Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Septemba 27, 2012

TUNAKUZA VIPAJI

Huyu ndiye mwalimu wa muziki katika OMEGA POINT MUSIC ACADEMY iliyopo USHINDI SDA CHURCH.

Hapa ilikuwa ni katika tukio moja hivi.

Calvin mwenye nguo nyeusi kuanzia shati hadi suruali aliyepo nyuma ya pianist akirekebisha mitambo Ushindi SDA Church. Calvin ni rubani wa ndege na hivi sasa yupo kwa Obama anaongeza maujuzi mwanawane .


Huyu mtoto ni kivutia cha wengi kutokana na uwezo wake wa kucheza Piano, ilimchukua muda mfupi sana kuanza kupiga Piano huku akisoma Staff Notation.


Mdada kwa nyuma alikuwa akiimba wimbo uliokuwa ukichezwa na bwana mdogo hapo kwa Piano.


Huyu ndie mkufunzi mwenyewe wa Muziki.


 Mwalimu Heri akitoa maelekezo kwa mwanafunzi

Hapa alipewa paper ngumu, akajiuliza hivi nitaweza kweli kuupiga huu wimbo? Ulimchanganya lakini baada ya kutulia kidogo na kuungalia kwa makini akaanza na akaweza aisee...!!

 Mwalimu Heri akikagua mwanafunzi anachofanya ili kujiridhisha kuwa kaelewa ama anaweza? Ulikuwa ni wimbo mgumu sana.

Hapa anamfunulia ukurasa mwingine ili  kumpima uwezo wake

Dogo hapa kaiva, anapiga piano na kusoma Staff Notation.
Watoto wanaojifunza muziki wakiangalia kwa makini wakati mwalimu Heri akitoa maelekezo.

Hapo je!!


Muziki damuni.

Staff Notation ni moja ya changamoto kwa waimbaji, waalimu na hata wacheza vyombo vya muziki.

UTAPENDA MWANAO AMA WEWE MWENYEWE UJIFUNZE MUZIKI? 
WASILIANA NA MWALIMU HERI KAALE KWA NAMBA HIZI ZIFUATAZO:

+255 713 381883
+255 688 984 442
+255 757 336 090

Jumatano, Septemba 19, 2012

KONGAMANO LA MAISHA BORALile  kongamano la maisha bora, lililoandaliwa na Kanisa la Waadiventista Wasabato USHINDI kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kukabiliana na changamoto za maisha limeshaanza na hivi unavyosoma haya maandishi linaendelea.

Kanisa linatambua wajibu wake kwa jamii na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ili kukabiliana na changamoto hizo, kanisa limeandaa kongamano ambalo litachukua siku kumi kuanzia Septemba 17 hadi 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Kanisa la Waadventista kama sehemu ya jamii, tunatambua changamoto zinazoikabili nchi yetu, ingawa jitihada kubwa zinafanywa na Serikali, mashirika ya dini pamoja na asasi mbalimbali.

 “Leo kuna watoto wanaoitwa wa mtaani ama idadi ya wanaolelewa na mzazi mmoja inaongezeka kutokana na kuongezeka kwa talaka na ndoa zisizo na furaha na hali hii huathiri malezi ya watoto, elimu yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.”

Kongamano hilo la maisha bora limelenga katika kupanua uelewa ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa, ikiwamo ukimwi, maadili kwa jamii, uhuru wa dini, ujasiriamali, mazingira, athari za imani za uchawi na namna ya kudumisha amani katika nchi yetu.

KARIBU WATER FRONT GHOROFA YA 8 KILA SIKU KUANZIA SAA 10 JIONI KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI.

Jumatatu, Septemba 17, 2012

FAIDA YA JUISI YA MATUNDA MCHANYIKO MWILINI


Katika ulimwengu wa vyakula, inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa. Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho. Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.

Leo nitakutajia orodha ya juisi zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na fadia zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama tiba au kinga ya magonjwa.

KAROTI, TANGAWIZI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufaha ndiyo apple kwa Kiingereza.

TUFAHA, TANGO NA FIGILI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani, huondoa lehemu (cholestrol) mwilini, husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.

NYANYA, KAROTI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili mzima kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.
TANGO CHUNGU,

TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.

CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.

NANASI, TUFAHA NA TIKITIMAJI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo.

TUFAHA, TANGO NA ‘KIWI’
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu’.

PEASI NA NDIZI

Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.

KAROTI, PEASI, TUFAHA NA EMBE
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

MASEGA YA ASALI, ZABIBU, TIKITIMAJI NA MAZIWA
Juisi yenye mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2 ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.

PAPAI, NANASI NA MAZIWA
Juisi hii ina kiwango kikubwa cha Vitamin C, E na madini chuma. Huimarisha rangi ya ngozi na mfumo wa usagaji wa chakula tumboni.

NDIZI, NANASI NA MAZIWA

Juisi hii yenye kiasi kikubwa cha vitamini na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huzuia tatizo la ukosefu wa choo.

Ili kupata faida hizo zilizoainishwa katika kundi la matunda hayo, usafi wa matunda yenyewe hauna budi kuzingatiwa wakati wa kutayarisha juisi yake. Vilevile hakikisha unatumia matunda yaliyoiva vizuri na uyatayarishe kwa kuzingatia kanuni ya ‘mtu ni afya’.

Unaweza kutumia mashine maalumu ya kukamulia matunda (blender) au kutumia njia ya asili ya kutwanga kwa kinu maalumu na kupata juisi hiyo. Kama utaongeza sukari, inashauriwa kuweka kiasi kidogo sana. Ni bora zaidi usipoweka sukari, kwa sababu matunda mengi yana sukari ya asili.

Alhamisi, Septemba 13, 2012

Lugha ya adabu yafifia KenyaLugha ya adabu ni lugha wanayotumia wazungumzaji ambayo huficha makali ya baadhi ya maneno wanapoyatamka. Inawezekana pia kusema ni lugha ya heshima. Ni muhimu kujua pia lugha hiyo huambatana na mafumbo ama semi. Katika fasihi inaitwa tasfida. Kenya kufikia sasa kuna ukame wa msamiati wa adabu. Mathalan majina kama tafadhali, naomba, samahani, niwie radhi na kadhalika yanasikika sana katika vinywa vya Watanzania wakiwasiliana japo kwa wakenya sivyo.

Hata hivyo zipo sababu nyingi zilizochangia hali hiyo kuwa ilivyo. Mwanzo upo mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wakenya. Yaani baadhi ya wazungumzaji Kenya hawaoni sababu ya kusema kwa mfano 'haja kubwa' badala ya kutaja neno hilo moja kwa moja. Wengine hawataki kujitaabisha kujipinda huku na kule. Wanaamua kutaja neno hilo moja kwa moja. Ukiwauliza watakwambia kuwa si makosa wakisema mwanamke ana mimba badala ya kusema ni mja mzito.

Aidha mazingira huchangia pakubwa hulka ya watu katika masuala haya ya lugha ya adabu. Kwa mfano nchini Kenya sehemu za pwani kuna idadi kubwa ya watu wanaozungumza lugha ya adabu. Ni huko ndio utapata salamu za shikamoo na majibu ya marahaba kwa wingi. Pengine ni kwa sababu kuwa baadhi yao hawana haraka na hata wanapokutana na mtu wanataka kumjulia hali kikamilifu.Ni huko huko utasikia mara nyingi watu wakisema Fulani ameaga dunia bali si yule mtu amekufa. Katika sehemu hizo utamsikia mtu akisema naenda kutema mate badala ya kusema naenda kukojoa.

Si hayo tu, tofauti za watu kisiasa, kijamii na kiuchumi zina mchango mkubwa katika matumizi ya lugha ya adabu. Kwa mfano mhadhiri wa chuo kikuu nchini Kenya atapata shida sana ya kujitafadhalisha mbele ya mwanafunzi wake. Mara nyingi ni mwanafunzi anayenyenyekea mbele ya mwalimu. Katika bunge la Kenya kwa mfano wabunge ndio watakaolazimika kutumia majina kama mheshimiwa spika wakichangia mijadala bungeni. Ni vigumu spika kujitafadhalisha anapotoa uamuzi. Kwa ufupi idadi kubwa ya wakenya ni waasi wa lugha ya adabu. 

Source: Bbc Swahili - Na Paul Nabiswa.


Jumanne, Septemba 11, 2012

TUNAJIKUMBUSHA SHAMBULIO LA 11, Septemba, 2001.Shambulio la 11 Septemba, 2001 ni tarehe na mwaka uliotokea mashambulio manne ya pamoja yaliyofanywa na kikosi cha Kigaidi cha al-Qaida dhidi ya Marekani. Kwa mujibu wa taarifa za maofisa, yasemekana kwamba kikosi cha Al-Qaida waliziteka nyala ndege nne wakazitumia kama silaha wakigongesha ndege katika majengo mjini New York na Washington DC kwa makusudi. Karibuni watu 3,000 walipoteza maisha katika shambulio hilo.

Ndege zilitumika kufanyia Ughaini huo

 1. American Airlines Flight 11, iliyotumiwa kugonga mnara wa Kaskazini mwa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la mjini New York mnamo saa 8:46:30 asubuhi.
 2. United Airlines Flight 175, ilitumiwa kugonga mnara wa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la Kusini mnamo saa 9:02:59 asubuhi. Watu wengi waliona tukio la pili kwasababu habari zilikuwa tayari zishasambaa katika mji na kila kamera za televisheni zilikuwa zikielekezea macho yao huko katika eneo la tukio, na wakati huo huo ndege ya pili ikagonga tena mnara wa Kusini mwa Jengo hilo.
 3. American Airlines Flight 77, ilitumiwa kugonga jengo la Pentagon la mjini Arlington, Virginia (karibu kidogo na Washington DC), mnamo saa 9:37:46 asubuhi.
 4. United Airlines Flight 93, hii haikubahatika kugonga mahala popote pale, badala yake wakaiangusha chini mnamo saa 10:03:11 asubuhi. Yaaminika ya kwamba magaidi hao walikuwa wakitaka kuigonga ndege hiyo katika jengo la mji mkuu wa Marekani. Abiria walijaribu kuinyang'anya Ndege hiyo kutoka mikononi mwa magaidi hao lakini hawakufanikiwa. Na matokeo Ndege ikashia kuanguka karibu na mji wa Shanksville, Pennsylvania.

  Matokeo ya maafa hayo

  Jumla ya watu waliokufa katika shambulio hilo ni 246. Magaidi 19 waliuawa wakati wa shambulio hilo. Minara yote miwili ya jengo la World Trade Center yalipamba moto baada ya shambulio. Mnara wa Kusini (yaani WTC 2) liliungua kwa muda wa dakika 56 kbla ya kuanguka na kuangamia kabisa.

  Jengo la Kaskazini (WTC 1) liliungua kwa muda wa dakikar 102 nalo pia lilianguka. Kama jengo la WTC lilivyoanguka, sehemu na mmong'onyoko wa jengo hilo lilipelekea majengo mengine yaliyoyazunguka majengo hayo kushika moto na kuharibika pia. Kutokaa na uharibifu uliotokea, jengo la tatu la 7 World Trade Center (7 WTC), nalo likaanguka mnamo saa 5:20 jioni. Baadahi ya mamjengo mengine yaliharibiwa vibaya na hata kuangamia kabisa yaani.  Takriban watu watu 2,602 walipoteza maisha katika Jengo la World Trade Center.
  Ndege iliyogonga Pentagon iligonga chini mwa upande wa Magharibi mwa jengo hilo. Kisha ikagonga mpaka katika nguzo tano zinazoshikiria jengo hilo la Pentagon. Shambulio hilo Pentagon liliuwa watu 125.

  Watu 2,973 walikufa katika shambulio hilo, wakiwemo watu watu wa zima moto waliokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya baadhi ya watu waliopatwa na balaa hilo.

  Hili lilikuwa ndio shambulio kubwa la kwanza kwa watu ambao wasio Waamerika kushambulia nchini humo tangu mnamo mwaka wa 1941, pale Wajapani waliposhambulia kituo cha jeshi la maji kilichopo katika Bandari ya Pearl, Hawaii. Dhana nyingi zilikuwa zikionekana kwamba kuna watu katika Marekani walikuwa wakijua kwamba kutatokea na tukio kama hilo kabla na ni lini itakuwa hivyo.


    Vita dhidi ya ugaidi

  Baada ya shambulio, Wamarekani wakawa wanawalaumu Al-Qaeda kwa kitendo walicho kifanya. Tangu hapo wakaianza vita dhidi ya Ugaidi. Kiongozi wa al-Qaeda, Osama bin Laden, Alikimbilia nchini Afghanistan. Serikali ya Marekani iliwaambia Serikali ya Afghanistan, iitwayo Taliban, kumsalimisha bin Laden mikononi mwao.

   Wataliban hawakufanya hivyo. Kiongozi wa Wataliban, Mullah Muhammad Omar, aliitaka Serikali ya Marekani impe Uthibitisho unaonyesha kwamba Osama anahusika na tukio hilo. Rais wa Marekani bwana George W. Bush akasema kwamba hakuna haja kutaka Uthibitsho wowote ule na Serikali ya Marekani ikaanzisha vita dhidi ya Afghanistan.

  Source: Wikipedia.

  Je huwa unakosa usingizi?

  Msongo
  Tatizo la kukosa usingizi huenda likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya kusahau au ''Alzheimer'' kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana maumbile yanayofananishwa na binadamu.

  Vipande vya protini, kwa lugha ya kitaalamu (plaques) au uchafu kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti inayosababisha maradhi haya.

  Utafiti uliofanywa na kuchapishwa katika jarida la tafsiri ya matukio ya Sayansi, umeonyesha kuwa punde chembe chembe za uchafu ule ulipoanza kukua kwenye ubongo wa panya, usingizi ukaanza kuwa tatizo kwa viumbe hao.

  Taasisi inayosimamia utafiti wa maradhi hayo, (Alzheimer's Research UK) imehimiza kuwa ikiwa uhusiano huo unaweza kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa Madaktari.
  Utafiti wa kutaka kugundua mapema kama mtu anaelekea kukumbwa na maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu katika kutibu maradhi hayo.

  Maradhi ya Alzheimer


  Wagonjwa hawaonyeshi dalili kupitia hisia au kumbukumbu zao hadi baada ya mda mrefu wa maradhi kumkumba mgonjwa. Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika kiasi kwamba tiba inakua vigumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana.

  Ndiyo sababu wataalamu wanafanya juhudi za kuanza mapema kugundua kama mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa kabla ya dalili hizo kujitokeza.

  Viwango vya protini ijulikanayo kama Beta Amyloid kimaumbile hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia panya katika kipindi cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini ambayo hujenga uchafu usiofutika kwenye ubongo na maradhi ya Alzheimer.

  Majaribio yaliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Washington yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala kwa dakika 40 kwa kila saa mchana. Lakini ubongo ulipoanza kupatwa na uchafu panya hawa wakaanza kusinzia kwa dakika 30 pekee.

  Ugonjwa wa sahau
  Mmojapo wa wataalamu, Prof David Holtzman, alisema: "endapo mapungufu katika usingizi huanza mapema kiasi hiki katika ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo yanaweza kutupa ishara ya wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya."

  "ikiwa matatizo haya ya usingizi yapo, hatuelewi hasa yanachukua mfumo gani, kupungua kwa usingizi kikamilifu au ni tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu tofauti kabisa."
  Hata hivyo, utafiti unaofanyika kwa kutumia panya mara nyingi hayafai kutumika kwa binadamu kwa sababu nyingi zinazosababisha kutatizika na usingizi.

  Dr Marie Janson, kutoka shirika la kujitolea Alzheimer's Research UK, ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya matatizo ya kukosa usingizi na ugonjwa wa Alzheimer.

  Aliongezea kuwa: "tayari umekuwepo utafiti unaounganisha mabadiliko katika usingizi huchangia katika matumizi ya ubongo kwa fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna uwezekano wa kuwa mapungufu katika usingizi pia inaweza kuwa ishara na onyo la maradhi ya kusahau au Alzheimer.

  Chanzo: Bbc. Kushuhudia  CLICK HAPA

  Jumatatu, Septemba 10, 2012

  SABABU GANI ‘NIMHESHIMU BABA YANGU NA MAMA YANGU’?
  “WAHESHIMU baba yako na mama yako.”

  Kwa vijana wengi maneno hayo yanasikika kama ni jambo la zile enzi za giza.

  Kijana-msichana Veda alijulisha uasi wa waziwazi dhidi ya baba yake kwa kufanya matembezi na mvulana aliyetumia vibaya madawa ya kulevya na alkoholi. Kwa kukaidi, angelienda pia kucheza dansi mpaka chee.

  “Nilihisi kwamba yeye alikuwa mzuivu mno,” alieleza Veda.

  “Nilikuwa na umri wa miaka 18, na nilifikiri mimi ni mjuzi wa yote. Nilihisi baba yangu alikuwa bahili na hakutaka kamwe nione raha, kwa hiyo mimi nikaenda nje na kufanya nililotaka kufanya.”

  Yawezekana kijana; walio wengi hawatakubaliana na vitendo vya Veda. Lakini, kama wazazi wao wa masomo ya nyumbani, au wawe wamefika nyumbani saa Fulani, wengi wangechacha kwa uchungu wa moyo au, jambo baya hata zaidi, wangekaidi wazazi wake inaweza hatimaye kumaanisha si kama tu itakuwa ni vita au amani nyumbani bali pia uhai wake mwenyewe.

  Kwa maana amri ya ‘kuheshimu wazazi’ inatoka kwa Mungu, na anaambatanisha motisha ufuatao na kutii amri hiyo”. (Waefeso 6:2, 3) Inaweza kumaanisha faida kubwa au hasara kubwa.

  Kwa hiyo, tuangalie upya linalomaanishwa hasa na kumheshimu babako na mamako.

  Jumamosi, Septemba 08, 2012

  MUNGU MUUMBA WA VYOTE ....MAJIBU YAFANYAYO KAZI.

  ********************************

  Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
  MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
  Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
  Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
  (Namaanisha JumaMosi)

  Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo itabidi tuombe.

   

  ********************************

   
   
  OMBI
  TUNAKUSHUKURU   KWA KUTULINDA   NA TUNAKUSHUKURU KWA KUTUAMSHA  SALAMA ASUBUHI  YA LEO  JINA LAKO LIHIMIDIWE.  WAPO WALIOTAMANI  KUFIKA SIKU YA LEO LAKINI HAWAKUWEZA KUFIKA  WENGINE NI WAGONJWA NA WENGINE WANASHIDA MBALIMBALI  MUNGU WASAIDIE WATU WAKO   ILI WATAMBUE  KUWA WEWE NI MUNGU  USIESHIDWA  NA KITU CHOCHOTE.  BARIKI  RADIO  YA MORNING STAR  ILI ATAKAE SIKILIZA AWEZE KUBARIKIWA,  BARIKI VIONGOZI   PAMOJA  NA  WAFANYAKAZI  WAKE.  KWA JINA  LABABA  NA LAMWANA  NA LA ROHO MTAKATIFU  AMINA.


   

  Ijumaa, Septemba 07, 2012

  YUSUPH MCHARIA BIRTHDAY
  Kila mtu ana siku yake ambayo niya pekee sana na mpya katika maisha aliyonayo. Hivyo ndivyo ilivyo na kwangu leo hii. Kiukweli, mara nyingi huwa ni siku inayoashiria kuanza kwa mwaka mwingine mpya kwa mhusika tena ni mwaka ambao unaoanzisha mzunguko mwingine uliyo na mikosi ama Neema katika maisha ya mwanadamu. NI SIKU YA KUZALIWA PEKEE yake ndio NINAYOIZUNGUMZIA HAPA. Naaa.. ukitafakari; kwa kadri na namna maisha yalivyo ni zaidi ya idahaniwayo kuwa ni shule kama sio chuo kikuu chochote hapa Duniani. 

  Tukiachilia mbali ndugu, jamaa, marafiki, majirani! hata ka sio kila mara nina amini huwa unawatolea  WAZAZI wako wote shukrani kwa uwepo wao kwako wewe msomaji. Utakubaliana na mimi kuwa umejifunza mengi kutoka kwa maadui na marafiki uliowahi kuwa nao. Kwa kuwa husemwa palipo na msafara wa mamba kenge hakosi nina uhakika kupitia hao na hayo yote kila mmoja amejifunza mengi yaliyo mabaya na hata mazuri yakiambatana. 

  Unaweza usinitambue mimi kwa sababu ya changamoto ulizozipata lakini kuna mtu mahali fulani huwa unamkumbuka kutokana na mchango wake kwako. Ninashukuru kwa UMOJA uliopo Kwa Baba na Mama yangu. Baba na Mama, Wajomba, Mashangazi, Mabinamu, ndugu wote wa hiari na marafiki na wewe msomaji, kiukweli ninawapenda sana. 

  KWA UFUPI.
  Ilikuwa ni SEPTEMBER 7TH SAA 9:30 ALASIRI SIKU YA IJUMAA ndipo nilipozaliwa katika hospitali kuu iliyopo Wilayani Tarime mkoa wa Mara katika familia ya kiadventista. Awali mama alikuwa ni nesi lakini aliamua kubalisha fani na kuingia katika ualimu wa shule. Hivyo basi Mama yangu ni MWALIMU na Baba yangu ni MCHUNGAJI japo alisha staafu.

  Baada ya siku saba, yaani ilipofika Septemba 14 baada ya mimi kuzaliwa nikapewa jina CHACHA na bibi yangu. 


  Jina hili lina maana tatu kama sio nne.

  Maana ya kwanza ya kiasili
  “Iching’ombe chichele.” yaani kwa tafsri rahisi ni kwamba NG’OMBE ZIMEKUJA. Hii inatokana na ule wakati binti anapoposwa sasa mahari inapoletwa na kwa kawaida mahari yenyewe huwa ni ngombe hivyo mtoto akizaliwa huitwa hilo jina.  Lakini kwangu haikuwa hivyo ila ipo katika maana ya pili na kuendelea, soma hapo chini.

  Maana ya Pili: Ni wa uzao wa kwanza. Maana ya tatu: Ni jina la Babu wa tatu wa baba mzazi wa Chacha aitwaye Daniel Mcharia. Maana nyinge CHACHA NI MTU JASIRI.

  Ilipofika Desember 22  nilipelekwa kanisani kuombewa, wanasema kwa lugha nyingine kuwekwa WAKFU KWA MUNGU. Ilikuwa ni siku ya JUMAMSOI tena ya SABATO ya mtaa. Pr Jackson Magai ambaye kwa sasa ni marehemu, ndiye aliyefanya hiyo huduma ya kuniweka wakfu. Sadaka ya shukrani kwa ajili yangu iliyotolewa na wazazi wangu kwa MUNGU ilikuwa ni shilingi 50. Kwa miaka 1979 kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni kingi sana.

  Katika kukua kwangu; jina Yusuph lilitokana na Baba yangu mdogo ambaye kwa wakati fulani alikuwa akija nyumbani hasa nyakati za likizo, niliona alivyokuwa akipenda kucheza na mimi hatimaye nikaamua kulitumia rasmi hili jina ila maana na yeye alikuwa akiitwa hivyo, nilizidi kupata hamasa na kulipenda mara baada ya kuwa nimesikia simulizi mbalimbali kuhusu YUSUFU WA KWENYE BIBLIA.

  JINA YUSUFU Linatokana na jina la kilatini lililotokana na jina la kiyunani (LOSEPHOS), lililotokana na jina la Kiebrania (YOSEF) likiwa na maana ya: “ATAZIDISHA au ATAONGEZA”.

  Katika agano la kale Biblia takatifu inaeleza Yusufu na Joseph ni mwana wa kumi na moja wa Yakobo (Israel). Kwa sababu ya kupendwa sana na baba yake Yusufu alionewa wivu na ndugu zake, wakamchukia, wakamuuza akapelekwa Misri kisha wakaenda kumweleza baba yao uongo kwamba alikuwa amekufa.

  Lakini huko Misri Yusufu aliongezewa neema ya Mungu akapandishwa cheo na kuwa Mshauri mkuu wa Farao. Jina hili pia limetumiwa na watu wengine wawili ndani ya biblia takatifu waliocheza nafasi muhimu sana ya kiroho na kimaandiko ambao ni Yusufu mume wa Bikira Mariam na Yusufu tajiri wa Arimathaya aliyenunua kaburi la kifahari akalitumia kuhifadhi mwili wa Bwana Yesu Kristo baada ya kufa msalabani. 

  Nililojifunza katika maisha haya ni kwamba KILA MMOJA WETU ANA FUNZO, SHULE NA KILA MTU NI MUHIMU KWA MWENZIE. Hata kama shule hiyo ni kukufunza usichotakiwa kufanya. NINawapenda, ninawathamini na ninawaheshimu sana mno.

  NIWE MUWAZI  
  Maisha ya sasa yasingekuwa yalivyo bila msaada mkubwa wa MUNGU ALIEYEZIUMBA MBINGU NA NCHI NA VYOTE VILIVYOMO.


  ******************************************
  No one can go back and change a bad beggining, 
  but anyone can start now and create a successful ending.
  ******************************************

  Jumanne, Septemba 04, 2012

  UJENZI WA MIJI MIKUBWA

  PHOTO BY: Projects cambodia

  Ilianza katika kingo za mito. Miji ya kwanza ilijengwa India na Iraq Jiji la kale na maarufu lilikuwa Babeli. Tukizungumzia neno 'ustaarabu' tukumbuke kwamba ni tafsiri ya neno linalotokana na lugha ya Kiingereza ambalo maana yake ni 'kuishi katika miji mikubwa'.

  Kabla ya watu hawajaanza kuishi katika vikundi, kila mtu ilimlazimu kujikaza katika kuongezeka mifugo au mavuno ili yeye mwenyewe pamoja na jamaa zake wasife kwa njaa. Lakini baadae binadamu walipojifunza kuishi pamoja kwa wingi, walipata kuendelea vema katika ufundi na ujuzi wa namna mbali mbali katika maisha yao. Kwa maana hiyo kila mtu aliweza kujizoeza kutenda kazi yake maalum na kapata kuifanya vema. Kufuatia hali hiyo kukaibuka wajenzi, wafanyakazi, wahunzi, washoni viatu, wavuvi, wachimba migodi, maserema, askari na wengine wengi.


  Kwa hali hiyo kulikuwa na nyumba bora, viatu na vyombo madhubuti na watu wengi walikuwa katika hali iliyo njema zaidi, kwani waliweza kuishi maisha ya raha, walikuwa na mavazi bora ya kuvaa na ya kutumia tofauti na zama zilizokuwa za ukulima tu. Maeneo ya Afrika na nchi nyingine nyingi za mbali pia binadamu na mataifa walitengwa kwa sababu ya milima na bahari nao hawakupata kujifunza kujenga miji na kukaa pamoja, hivyo watu walidumu kukaa katika hali ile ile ya kutopata 'ustaarabu'. Hivi sasa duniani kuna miji mingi mikubwa tunayoishi ambayo kutokana na ukubwa wake mingine imefikia kuitwa au kupewa hadi ya kuwa majiji.


  Lakini hata hivyo wakati watu wengi hivi sasa wanaishi ama kutembelea katika miji hiyo kama vile Jiji la Dar es Salaam, Nairobi, Kampala, Harare, Cairo, Lagos, New York, London, Moscow na mingineyo, bado hawafahamu nini hasa chimbuko la kukua kwa miji hiyo na msongamano wa watu na maisha ndani yake.


  Kulingana na watafiti wa mambo ya historia na mazingira duniani, imethibitika kwamba miji mingi ambayo sasa ni majiji ilianzia katika kingo za mito mikubwa au kando ya bahari. Katika nchi ya India ambako leo hii kuna miji mingi mikubwa, imeonekana kuwa hapo kale kulikuwa na ustaarabu mwingi hasa kando ya kingo za mto Ganges (unaotamkwa Ganjiz) ambapo wenyeji wa huko walikuwa wakitengeneza vyombo na silaha zao kwa shaba nyeusi katika eneo hilo.


  Hata hivyo katika utafiti huo hakukuwa na habari zaidi juu ya miji hiyo vile wakati huo binadamu walikuwa hawakuhifadhi kumbu kumbu ya maandishi ya mambo yao. Katika nchi ya Uchina ambako leo hii kuna idadi kubwa ya watu katika miji yake yote kuliko nchi nyingine dunani majiji yake yote mashuhuri ya sasa yalianzia kando ya kingo za mto mashuhuri unaoitwa Yang Tse Kiang.


  Miji mingine mikuu ya zamani iliyokuwa maarufu ilikuwa katika nchi ya 'Mito Miwili' (Mesopotamia) ambayo sasa inaitwa Iraq na pia katika kingo za mto Nile huko Misri. Ni rahisi kufikiri kwamba kwa nini miji mikubwa iliyojengwa kando ya kingo za mito ilistawi haraka haraka. Mito hiyo mikubwa siku zote ilikuwa ikileta tope kwa wingi zilizofanya nchi kuneemeka zaidi hata ikawezesha mazao kumea kwa kurahisi. Tope hizo pia ziliweza kutengenezwa matofali kwa urahisi na kuanikwa juani, hivyo watu waliweza kujenga nyumba nzuri upesi.


  Miji mikubwa ya dunia ambayo inatamba kwa uruzi na ukubwa hivi leo ni Beijing, Paris, Mexico City, New York, Berlin, Buenos Aires, New Delhi, Cairo, Mosco na Hong Kong, lakini mji mkubwa wa kale kabisa uliokuwa ukitamba ni Babeli. Katika mji huo ulikuwa akiishi mfalme maarufu aliyekuwa akiitwa Hammurabi ambaye baada ya kuujenga alikuwa akitoa sheria nyingi na kali kwa wakazi wa mji huo kuuenzi na kuuheshimu mji wao. Inaeleza kuwa mfalme huyo hakutaka watu wajenge holela kama ambavyo leo hii tunashuhudia katika Jiji letu pekee la Dar es Salaam.


  Mfalme huyo aliyepata kutawala mji huo alimjengea bustani malkia wake ambaye aliona huzuni kwa sababu ya kukaa mabli na nchi yake, hivyo alijengewa bustani hizo kufurahisha. Inaelezwa katika vitabu kwamba bustani hizo zikawa na sifa katika dunia nzima ya kale ambapo pia fahari ama sifa nyingine katika mji huo wa kale ulikuwa na mkataba kubwa ya kusomea mfalme na wakazi wake, lakini vitabu vyake havikuwa vya karatasi, bali vyote vilikuwa vya mbao na undogo uliochomwa hata ukawa ngumu.


  ONYO LA KUTISHA..!!

  Onyo la kutisha mno la adhabu linaloweza kupatikana mahali po pote katika Biblia limo katika Ufunuo 14:9,10: "Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa [alama] katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye ATAKUNYWA katika mvinyo ya GHADHABU YA MUNGU iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo."

  Maelezo haya yanaogofya mno na hayafanani kabisa na mafungu mengine yanayoielezea tabia ya Mungu ilivyo, hata tunajikunja kwa hofu. Lakini yanaonyesha wazi kipindi kile ambacho rehema ya Mungu itakapoondolewa kwa wale ambao wanaendelea daima kuikataa mamlaka ya mbinguni. Litakuwa ni tendo lisilo na kifani kwa upande wa Mungu katika uhusiano wake na jamii ya kibinadamu. Kwa karibu

  miaka 6000 hukumu zake za adhabu juu ya watu walio waovu sana zimechanganywa na rehema Yake. Lakini sasa uovu unafikia kiwango ambacho kinafanya iwe lazima kwa Mungu kuingilia kati, na kukidhihirisha kiwango cha usaliti wa mwanadamu dhidi ya Serikali ya Mungu.

  Hapa ndipo tunataka kujua habari zaidi juu ya dhambi ile inayomfanya Mungu kutenda tendo hilo la ajabu [geni] la kuwaadhibu [waovu] kwa moto. Angalia kwamba jambo hili la mwisho linahusu utii wa uongo kwa mamlaka ile ya Mnyama, ambayo mara nyingi inatajwa katika unabii wa Biblia. Hatimaye dunia hii itasimama

  ikiwa imegawanyika katika makambi mawili: 

  01. Wale wanaomsujudu Mungu wa kweli na 

  02. Wale wanaomsujudu Mnyama yule wa Ufunuo 13. 

  Lakini ni jambo gani linaloleta mgawanyo huo mkubwa wa watu wa dunia hii? Baada ya kueleza ajali itakayowapata waabudu hao wa uongo katika Ufunuo 14:9-11, Yohana analo hili la kusema katika fungu lile linalofuata: "HAPA NDIPO PENYE SUBIRA YA WATAKATIFU, HAO WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU, NA IMANI YA YESU." Hapa tunaona tofauti ya kushangaza kati ya wale wanaomfuata yule Mnyama na wale wanaomfuata Mwana-Kondoo.


  Angalia, tafadhali, ya kwamba suala linalohusika linazunguka juu ya kuzishika amri za Mungu. Wale ambao hawana alama ya Mnyama wanasemwa ya kuwa wanazitii amri hizo [za Mungu], na wale waliobaki wanateseka kwa ghadhabu ya Mungu. Jambo hili linakubaliana kabisa na usemi wa Paulo katika Warumi 16:16, "Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii,

  mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki."

  Wajibu wa hali ya juu unahesabika kwa tendo hili la UTII. Mwishowe, sehemu kubwa ya wakazi wa dunia hii wataikubali mamlaka hii ya bandia ya serikali ya Mpinga Kristo, kwa KUZIASI AMRI ZILE KUU KUMI za Mungu. Rafiki zangu, kila mtu mmoja mmoja atakuwa upande mmoja au mwingine. Biblia inaeleza kwa wazi sana ya kwamba UZIMA au MAUTI utategemea UAMUZI WA MWISHO kuhusu Mnyama huyu wa Ufunuo 13.


  Ni ajabu kwamba wanathiolojia wa siku hizi wamepuuzia kabisa UJUMBE HUU WA ONYO wa Ufunuo 14, unaohusu ile Alama ya Mnyama. Shauku ya watu wengi imeharibiwa na mvuto wa WACHUNGAJI ambao hawakutaka kuyachukulia maneno haya ya unabii wa Yohana kwa uzito wake. Mara nyingi wanautupilia mbali [unabii huu] kana kwamba ni waraka wenye utata, usiokuwa na maana, ambao ulilihusu

  tatizo la mahali pale katika kanisa lile la mwanzo. 

  Kwa sababu fulani kitabu hiki kinachoitwa Ufunuo kinahesabika kama vile ni kitabu kilichofungwa [kisichoweza kueleweka], badala ya ukweli wake wa wazi uliofunuliwa [unaoeleweka] kama jina lake linavyomaanisha. Lakini tafadhali zingatia ya kwamba ahadi imetolewa kwa wale wanaoitafuta kweli iliyomo ndani ya kitabu hiki cha ajabu: "Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu." Ufunuo 1:3.


  Kabla ya kukichunguza sana kisa hiki kilicho wazi cha Yohana kuhusu pambano lile la mwisho kati ya Kristo na Shetani, hebu na tutumie muda fulani kuwachambua hao wanaopambana katika vita hii. Ni lini na kwa jinsi gani [pambano hili] lilianza, na kwa jinsi gani litafikia mwisho wake?


  Jumatatu, Septemba 03, 2012

  KUKABILIANA NA KUMBUKUMBU YA MAISHA YETU

  PHOTO BY: African lens

   "Kazi ya kila mtu inachunguzwa mbele za Mungu na inaandikwa kama ni ya UAMINIFU ama ya KUKOSA UAMINIFU. Mbele yake kila jina katika vitabu vya mbinguni huandikwa kwa usahihi kabisa kila neno baya, kila tendo la uchoyo [ubinafsi], kila kazi isiyotimizwa, na kila dhambi ya siri, na kila unafiki uliofanywa kwa werevu.

  Maonyo yaliyotumwa kutoka mbinguni na makaripio YALIYOPUUZWA, wakati uliopotezwa bure [kucheza karata, bao, n.k.], nafasi ambazo hazikutumiwa vizuri, mvuto uliotolewa kwa WEMA au kwa UBAYA, pamoja na matokeo yake yafikayo mbali, vyote hivi vinawekwa katika kumbukumbu zenye tarehe na malaika yule anayetunza kumbukumbu hizo.

  HEBU TAFAKARI JAMBO LILILOTOKEA HIVI KARIBUNI:
  WAANDISHI, WANANCHI DODOMA WALAANI MAUAJI YA MWANDISHI - Dodoma Yetu
  This Day Magazine: Jukwaa la Sanaa lamkumbuka Mwandishi aliyeuawa Iringa

   Hali hii ni ya HATARI SANA kwa  wale ambao, wakiwa WAMECHOKA KUKESHA, wanageukia VISHAWISHI vya ulimwengu huu. Mathayo 24:42-5l. 

  Wakati mtu wa BIASHARA amezama mawazo yake yote yako katika KUTAFUTA FAIDA, wakati MPENDA ANASA anaendelea kutafuta kujiridhisha katika hiyo, wakati BINTI WA MITINDO anapanga MAPAMBO yake ----- huenda ni katika SAA hiyo HAKIMU WA DUNIA YOTE atakapotamka hukumu hii, "UMEPIMWA KATIKA MIZANI [AMRI KUMI] NAWE UMEONEKANA KUWA UMEPUNGUKA." Danieli 5:27.