Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Novemba 28, 2014

Kusasisha Masharti na Sera Zetu: Kukusaidia kufahamu jinsi Facebook inavyofanya kazi na jinsi ya kudhibiti maelezo yako

 
Kwa mwaka uliopita, tumeanzisha vipengele na vidhibiti vipya ili kukusaidia kupata mengi kutoka kwa Facebook, na tumewasikiliza watu ambao wametuomba tufafanue zaidi tunavyopata na kutumia maelezo.
 
Sasa, ukiwa na Misingi ya Faragha, utapata vidokezo na mwongozo wa jinsi ya kufanya kwa kushughulikia uzoefu wako kwenye Facebook. Pia tunasasisha masharti, sera ya data na sera yetu ya vidakuzi ili kuonyesha vipengele vipya ambavyo tumekuwa tukivishughulikia na kuvirahisisha kueleweka. Na tunazindua maboresho kwenye matangazo kulingana na programu na tovuti unazotumia nje ya Facebook (matangazo ya kitabia za mtandaoni) na kukudhibiti. 
 
Visasisho hivi vinaanza kutumika Januari, 1, 2015. Kama kawaida, tunakaribisha maoniyako kuhusu sera zetu.

Misingi ya Faragha
 
Misingi ya Faragha hutoa mwongozo ingiliani wa kujibu maswali mengi yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu jinsi unavyoweza kudhibiti maelezo yako kwenye Facebook. Kwa mfano, unaweza kujifunza kuhusu kuondoa utambulisho, kuondoa urafiki, kuzuia na jinsi ya kuchagua hadhirira kwa kila chapisho lako. Maelezo haya yanapatikana kwa lugha 36.
 
Pamoja na ukaguzi wetu wa sera, ukumbusho kwa watu wanaochapisha kwa umma na wateuzi wa hadhira rahisi, Misingi ya Faragha ni hatua ya sasa tuliyoichukua ili kukusaidia kuhakikisha kuwa unashiriki na watu unaotaka.

Kukusaidia kupata mengi kutoka kwa Facebook
 
Kila siku, watu hutumia programu na huduma zetu kuunganika na watu, maeneo na vitu wanavyovijali. Visasisho kwa sera zetu vinaonyesha bidhaa mpya tulivyokuwa tukivishughulikia ili kuboesha uzoefu wako wa Facebook. Pia vinaelezea jinsi ambavyo huduma zetu hufanya kazi kwa njia rahisi ya kuelewa. Hapa kuna baadhi ya viangazio:
 
  • Gundua kinachoendelea karibu na wewe:Tunasasisha sera zetu ili kufafanua jinsi tunavyopata maelezo ya eneo kulingana na vipengele unavyotumia kutumia. Mamilioni ya watu huingia katika maeneo wanayopenda na kutumia vipengele vya hiari kama Marafiki wa Karibu (inapatikana tu katika baadhi ya maeneo). Tunashughulikia njia za kukuonyesha maelezo yanayofaa zaidi kulingana na mahali ulipo na yale marafiki wako wanayafanya. Kwa mfano, baadaye, ukiamua kushiriki uko wapi, unaweza kuona menyu kutoka kwa mikahawa iliyo karibu au visasisho kutoka kwa marafiki katika eneo.
 
  • Kufanya ununuzi kuwa rahisi zaidi:Katika baadhi ya maeneo, tunajaribu kitufe cha Nunua ambacho huwasaidia watu kugundua na kununua bidhaa kutoka kwa makampuni mengine bila kuondoka kwa Facebook. Pia tunashughulikia nia mpya za kufanya miamala hata kwa urahisi zaidi.
 
  • Pata maelezo kuhusu faragha kwenye Facebook wakati unahitaji.Ili kuvifanya kupatika zaidi, tulihamisha vidokezo na mapendekezo kwa Misingi ya Faragha. Serea yetu ya data ni fupi na wazi zaidi, kwa hivyo kuifanya iwe rahisi zaidi kusoma.
 
  • Fahamu jinsi tunavyotumia maelezo tunayoyapokea.Kwa mfano, kufahamu nguvu ya betri na mawimbi husaidia kuhakikisha programu zetu zinafanya kazi vizuri kwenye kifaa chako. Tunaomba idhini ili kutumia eneo lako la simu tunapotoa vipengele vya hiari kama kuingia au kuongeza eneo lako la machapisho.
 
  • Jua familia ya kampuni na programu za Facebook zinazofanya kazi pamoja.Kwa miaka michache iliyopita, Facebook imekua na tunataka kuhakikisha unajua kuhusu familia yetu ya makampuni, programu na huduma. Tunatumia maelezo tunayokusanya kuboresha uzoefu wako. Kwa mfano, ikiwa umefungiwa nje ya akaunti yako ya Instagram, unaweza kutumia maelezo yako ya Facebook kupata nenosiri lako. Hakuna chochote katika visasisho vyetu hubadilisha ahadi ambayo Instragram, WahatsApp na makampuni mengine imetoa ili kulinda maelezo yako na faragha yako.
 
  • Maelezo yako na utangazaji:Wakati mwingine watu huuliza jinsi maelezo yao husambazwa kwa watangazaji. Hakuna jambo linalobadilika kwa visasishi hivi—tunawasaidia watangazaji kufikia watu kwa matangazo muhimu bila kuwaambia wewe ni nani. 
 
Jifunze zaidi kuhusu matangazo na jinsi unavyoweza kudhibiti matangazo unayoyaona.

Kukupata udhibiti zaidi wa matangazo
 
Tumesikia kutoka kwa baadhi yenu kwamba inawezakuwa vigumu kudhibiti aina za matangazo unazoona ukitumia vifaa na vivinjari tofauti. Hapo awali, ikiwa ungechagua kutoka kwenye aina fulani za matangazo kwenye kompyuta yako ndogo, chaguo hilo huenda halikutekelezwa kwenye simu yako. Tunajua kuwa watu wengi wanatumia zaidi ya simu moja, kompyuta ndogo au kivinjari ili kufikia Facebook, kwa hivyo inafaa kuwa rahisi kwako kufanya chaguo moja linalotekelezwa kwenye vifaa vyako vyote.
 
Hiyo ndiyo maana Facebook uheshimu chaguo unalofanya kuhusu matangazo unayoona, kwenye kila kifaa. Unaweza kuchagua kutoka kuona matangazo kwenye Facebook kulingana na programu na tovuti unazotumia kupitia Muungano wa Matangazo ya Dijitali. Unaweza pia kuchagua kutoka kwa kutumia vidhibiti kwenye iOS na Android. Unapotueleza hutaki kuona matangazo ya aina hii, uamuzi wako hutumika kiotomatiki kwa kila kifaa unachokitumia kufikia Facebook. Pia, sasa tunatengeneza mapendeleo ya matangazo yapatikane katika nchi zaidi, kuanzia Australia, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Ayalandi na Uingereza.
 
Tunatumaini visasisho hivi vitaboresha matumizi yako. Kulinda maelezo ya watu na kutoa vidhibiti maalum vya ufaragha tunavipa kipaumbele, na tunaamini matangazo haya ni hatua muhimu.
 
 Chanzo: INGIA HAPA

Jumatano, Novemba 26, 2014

Mdomo wa Ndege aitwaye Mdiria

Kule Japani, treni inayosafiri mwendo wa kilomita 300 kwa saa ndiyo yenye mwendo wa kasi zaidi ulimwenguni. Kwa kiasi fulani, mdiria ambaye ni ndege mdogo sana, amechangia sana kufanikiwa kwa treni hiyo. Jinsi gani?

 

Fikiria hili: Mdiria anaweza kuzama ndani ya maji bila kuyafanya yaruke sana anapotafuta chakula. Jambo hilo lilimvutia sana Eiji Nakatsu, injinia aliyesimamia majaribio ya treni hiyo. Alijiuliza jinsi mdiria anavyoweza kustahimili badiliko hilo kutoka hewani kuingia majini. Jibu la swali hilo lingetatua tatizo kubwa lililokuwa likiikumba treni hiyo inayosafiri kwa kasi. Nakatsu anaeleza hivi: “Treni inapoingia chini ya ardhi kwa kasi sana inatokeza mawimbi ya shinikizo la hewa ambayo huongezeka zaidi na zaidi. Mawimbi hayo hufika mwisho wa barabara hiyo ya chini ya ardhi kwa kasi ya mwendo wa sauti na hivyo kutokeza sauti kama ya mlipuko na tetemeko kubwa hivi kwamba wakazi wanaoishi umbali wa mita 400 walilalamika.”

  
Uamuzi ulifanywa ili kuunda treni hiyo kwa umbo la mdomo wa mdiria. Kulikuwa na matokeo gani? Sasa treni hiyo inasonga kasi zaidi kwa asilimia 10 na kutumia nguvu kidogo zaidi kwa asilimia 15. Zaidi ya hilo, shinikizo la hewa linalotokezwa na treni hiyo limepungua kwa asilimia 30. Kwa sababu hiyo, hakuna sauti ya mlipuko treni hiyo inapopita katika barabara hiyo ya chini ya ardhi.


Una maoni gani? Je, mdomo wa mdiria ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?

Samaki Anayetumia Nishati Yake Vizuri

Ili watokezeshe gari lenye nguvu, lisilotumia nishati nyingi, na lisiloharibu mazingira, wanasayansi walichunguza eneo ambalo wengi hawakutarajia, chini ya bahari! Samaki anayeitwa boxfish anayepatikana kwenye matumbawe yaliyo kwenye bahari za tropiki ana muundo unaofaa kutengeneza gari jepesi, linaloenda kwa kasi na kutumia nishati kidogo.


Fikiria hili: Samaki huyo anaweza kuogelea kwa kasi akisonga umbali unaolingana na mara sita ya urefu wa mwili wake kwa sekunde. Lakini hatumii nguvu ili asonge kasi hivyo. Umbo lake humwezesha kusonga kwa kasi bila kutumia nishati nyingi. Wahandisi walitengeneza gari lenye muundo wa samaki huyo na kulijaribu kwenye barabara yenye upepo mkali iliyo chini ya ardhi na wakagundua kwamba gari hilo hukata upepo kwa njia bora zaidi kuliko magari mengine.

 
Samaki huyo ana ngozi ya nje yenye mifupa ambayo humfanya asonge kwa nguvu lakini bado awe mwepesi. Maji yanayozunguka kwa kasi kando ya samaki huyo humfanya asiyumbeyumbe bahari inapochafuka. Kwa hiyo, samaki huyo ana uwezo mkubwa wa kudhibiti mwili wake hata anaposonga kwa kasi na anakingwa asiumie.Wahandisi wanaamini kwamba samaki huyo atawasaidia kutokeza gari salama, jepesi, na lisilotumia mafuta mengi. Dakt. Thomas Weber, mtafiti na mbuni anasema hivi: “Kusema kweli tulishangazwa kwamba kati ya viumbe wote, samaki huyo anayeonekana mzembe ndiye angechaguliwa kutokeza muundo wa gari linaloenda kwa kasi na kutumia nishati kidogo.”

Una maoni gani? Je, samaki huyo anayetumia nishati yake vizuri alijitokeza mwenyewe? Au alibuniwa?

Jumapili, Novemba 23, 2014

SAIKOLOJIA NA MAUMBILE
Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni:

1. INTROVANT: Watu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina, katika eneo hili hapa kuna makundi mawili nayo ni; 1.Melancolin 2. Fragmetic

2. EXTROVANTS: Wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za kina katika mambo yao
Hapa pia kuna makundi mawili nayo ni; 1. Sanguine 2. Colerick
Sasa tuangalie tabia za kila kundi na mienendo yao

1.MELANCOLIN

Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo
-wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
-ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
-wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
-ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
-wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
-Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)
-Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
-Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
-Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
-Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasanu si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
-Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
-Wakata tamaa wanapokosolewa.
-Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
-Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
-Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo
-Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
-Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
-Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa)
-Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
-Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana
-Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe
-Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
-Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
-Wana busara na hekima nyingi
-Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
-Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
-Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
-Ni kundi la watu wanoridhika haraka
-Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa
-Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
-Kundi linalopenda amani na utulivu
-Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
-Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu
-Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
-Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
-Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
-Wakati mwingine hupenda kujikataa.
-Ni waaminifu na wasema ukweli
-Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
-Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
-Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
-Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
-kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tama mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani]
-Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
-Kwa upamnde wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua

2: FLAGMETIC

-Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
-Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini
-Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda kupalili shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia)
-Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe
-Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao
-Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea
-Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
-Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili
-Ni watu wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hatawaliwa na mifano na takwimu halisia
-Wanapenda kufuatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu)
-Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili
-Ni watu wasioumizwa kufanya makosa
-Hawapendi kuwaamini wenzao
-Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo mbalimbali
-Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika
-Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao)
-Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)
-Ni wagumu wa kuomba msamaha (i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi) ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi sana kuamka)
-Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera, vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera walizozipokea
-Si watu wanaojali muda na ratiba
-Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.
-Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani
-Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao
-Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao)
-Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani
-Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu)
-Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko
-Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama
-Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers)
-Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote
-Hawapendi kuelekezwa na mara nyingi eidha huwadharau viongozi wao ama hutengeneza mitazamo na hoja za kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao.
-Wanapenda kutekeleza maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuia
-Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.

3.SANGUINE

-Wana uwezo wa kawaida kiakili (mara nyingine mdogo)
-Ni wacheshi sana
-Watu walio na maneno mengi na wasiopumzika kuongea
-Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza
-Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine
-Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika kundi hili
-Wanapenda sana kujisifu na kujikweza
-Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana uhalisia
-Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya.
-Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo huvionesha kwa uhakika
-Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine)
-Muda wote wako nadhifu (ni wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu)
-Wana kiherehere sana.
-Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau
-Ni vinyonga katika tabia zao (wanuwezo wa kuigiza tabia zisizo zao kiuhalisia na watu wasiowajua wasiwagundue kirahisi)
-Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini ni rahisi kuyaacha
-Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi
-Ni kundi linaloathiriwa sana na love affairs (i.e wao ni multiple lovers-ni kawaida kumkuta sanguine akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja: __inasemekana kutokana na maneno yao mengi na ufundi wa kuigiza hisia na tabia wavulana wanaume wa kundi hili huwanasa wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa.)
-Wawapo kwenye jamii hukubalika sana hasa kutokana na ucheshi wao na ukarimu walio nao.
-Wanapenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha
-Ni wahamasishaji wakubwa na wenye ushawishi wenye kukubalika kirahisi
-Ni kundi la wainjilisti wanaoongoza kwa kurudisha kondoo wengi kwa Bwana (wengi wana karama za kuhubiri kwa mvuto na ushawishi wa pekee)
-Hawaumii wanapokosolewa, ama wanaposhindwa jambo
-Ni kundi la watu waoga sana (wanajiamini sana kwa maneno lakini kivitendo ni kunguru)
-Si watunzaji wazuri wa siri (waropokaji)
-Wanapenda kujaribu kila jambo linalokuja mbele yao
-Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko wengine
-Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine
-Hawana aibu hata mbele ya watu wasiowafahamu wala kuwazoea
-Wanaume wa kundi hili huamini kuwa walizaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake
-Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala (wanapenda kuwaza jinsi ya kupata bahati nasibu, kuzawadiwa fedha na hata kuokota fedha ama madini)
-Ni watu wasiojua namna ya kupanga na kuimudu bajeti kwa ustadi)
-Ni watu wa mipango isiyoona mbali (wakurupukaji) (Ministers of emmergency affairs)
-Ni wazuri katika kusifia(i.e wanazikubali kazi za wengine kirahisi na kwa dhati)
-Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na hivyo kuwa maarufu
-Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina.
Mfano ni Petro mtume wa Biblia: alipenda kujaribu kila kitu (alipomwona Yesu anatembea juu ya maji alitaka na yeye kufanya hivyo) alipenda kufahamu kila kitu (aliuliza habari za siku za mwisho) alipenda kujionesha kuwa ni jasiri (aliahidi kuteswa na Yesu), alikuwa ni muoga sana (alimkana Yesu mara tatu kwa kuhofia kuteswa na wayahudi), alikuwa ni mwinjilisti wa kutumainiwa (alihubiri siku ya Pentekoste), alikuwa ni mwepesi wa kukubali pindi anapokosolewa (alikiri makosa baada ya kuonywa na Paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri kuwa hakuna wokovu kwa wasiotahiriwa)

4. COLERICK

-Wana uwezo wa kawaida kiakili
-Ni wa wakali na wakaidi
-Hawana huruma wala unyenyekevu
-Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa
-Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote
-Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa
-Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa
-Watu wasiokata tamaa mapema
-Wanajiamini kupita kiasi
-Hawana uoga ni majasiri sana
-Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
-Kundi la watu wenye nguvu nyingi
-Ni madikteta
-Hawapendi kabisa kupingwa wala kukosolewa
-Watu wa kulipiza visasi
-Watu wa vitendo kuliko maneno
-Ni waonevu, wanapenda dhuruma na ubabe
-Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
-Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani eneo fulani
-Wanafaa sana kuwa viongozi kutokana na uhodari wao wa kuwaongoza watu kwa sera za ushawishi wenye mlengo -wa kiukandamizaji
-Hawajui kubembeleza
-Hawaongei wala kucheka ovyo
-Wanapotenda jambo huwa wanawaza namna ya kunufaika na hata kama akimsaidia mtu anawaza namna ya kurudishiwa hicho alichokitoa
-Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa kutokana na uimara wao katika kuthubutu kutenda mambo na hali zao za kutoogopa hasara
-Si watu wanaopenda suluhu na amani
-Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
-Hawapendi starehe kwa wingi
-Ni watu wanaoweza kufurahia mazingira yenye dhiki na shida
-Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe hata baada ya kufariki
-Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha
-Mifano ya watu wa kundi hilo: Idd Amin, Hitler, etc
*SI TABIA ZOTE ZA KUNDI LAZIMA ZIANGUKIE SEHEMU MOJA

MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU

-Kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe katika kundi fulani
-Huwezi kujibadilisha kundi
-Kujifahamu kundi lako kunakuwezesha kurekebisha madhaifu uliyonayo na kuimarisha mazuri uliyonayo. Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kuwa makini namna ya kuishi nao
-Inawezekana kabisa kujifahamu upo kundi gani na pia kwa kusoma na kutazama ni rahisi kutambua makundi ya wengine

*NITATAMBUAJE MIMI NI WA KUNDI GANI?

-Watu wengi wana tabia za makundi zaidi ya moja-Kwa wale tabia zaidi ya asilimia themanini kutoka kundi fulani hao wanaitwa pure (i.e pure sanguine etc)-Kama una tabia kutoka kundi zaidi ya moja, unaunganisha majina ya makundi mawili yenye tabia nyingi zaidi, unaanza jina la lile lenye asilimia nyingi zaidi. *Mfano: flag-coleick; cole-flagmetic, flag-colerick , sangu-melancolic, melanco-sanguine: etc —

Jumatatu, Novemba 17, 2014

MUZIKI WA JADI CHINABw. Liu Tianhua (1895---1932) alikuwa mtungaji muziki mashuhuri, mwanamuziki na mwalimu wa ala za muziki za jadi. Bw. Liu Tianhua alizaliwa mwaka 1895 katika ukoo wa msomi wa wilaya ya Jiangyin, mkoani Jiangsu. 

Ndugu watatu wa ukoo huo wote ni hodari. Mwaka 1912 Bw. Liu Tianhua alishiriki kwenye bendi moja mjini Shanghai, na kujifunza nadharia ya muziki, piano, fidla na za aina nyingine. Alirejea kwao mwaka 1914 na kufundisha masomo ya muziki katika shule moja ya sekondari. 

Mwaka 1915 Bw. Liu Tianhua alifiwa na baba yake, ambapo katika majonzi makubwa alitunga muziki “kupiga kite”, na kuanza kushika njia ya utungaji wa muziki. 

Ili kujifunza muziki ya jadi ya China Bw. Liu Tianhua aliwatembelea wanamuziki wa jadi na kujifunza kutumia ala za muziki za kijadi. Alifanya mageuzi kuhusu upigaji wa zeze la kijadi na kufanya upigaji wa ala hiyo ya muziki kuoneshwa katika maonesho ya muziki na kufundishwa katika vyuo vya muziki. 

Katika miaka 10 ya kutoka mwaka 1922 hadi 1932, Bw. Liu Tianhua alikuwa profesa wa ala za muziki za zeze ya kijadi, gambusi na fidla. Katika utungaji wa muziki alirithi ufundi wa utungaji wa muziki wa kijadi huku akijifunza mbinu ya utungaji wa muziki ya nchi za magharibi. 

Toka alipokuwa na umri wa miaka 17 Bw. Liu Tianhua alianza kufundisha muziki katika shule za msingi na sekondari, na alikuwa na uzoefu mwingi wa kufundisha, na aliweka msingi wa mfumo wa elimu ya muziki wa kijadi. 

Alipoanza kuwa na mafanikio makubwa Bw. Liu Tianhua alianza kuugua, mwezi Mei mwaka 1932. Wakati alipofariki alikuwa na umri wa miaka 38 tu. 

Muziki safi aliotunga Bw. Liu Tianhua ni pamoja na “Kupiga kite”, “wimbo wa majonzi” na “Usiku mwema”. 

Chanzo:http://swahili.cri.cn

Jumatano, Novemba 12, 2014

WAMILIKI WA BLOG TANZANIA WATAKIWA KUFUATA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI

Mhandisi wa TCRA,Andrew Kisaka akiwasilisha Mada kuhusu maadili ya Uandishi  na Utangazaji  wa Habari


 Serikali imewataka wamiliki na waandishi wa blog nchini kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari wakati wa mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi ujao na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.Wamiliki wa blog mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo

 Akizungumza jijini Dar es salaam hii leo wakati wa ufungaji wa mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Wamiliki wa blog mbalimbali nchini Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Tanzania Assah Mwambene amesema serikali inatambua blog zinafanya kazi ya kutoa habari sawa na vyombo vingine vya habari lakini vinapaswa kuzingatia uandishi wa mambo ya msingi kwa kufuata maadili ya uandishi wa habari.Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo nchini Tanzania Assah Mwambene


 Mwambene ambaye pia ni Msemaji wa serikali ameeleza kuwa lazima wamiliki na waandishi wa blog wajue wamechukua wajibu mkubwa unaoendana na wajibu wa kuwajibika kwa wananchi wanaowandikia habari wa kuzingatia maadili.


Kamati ya muda ya wamiliki wa blog iliyochaguliwa leo

 Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Habbi Gunze amesema waandishi na wamiliki wa blog wananafasi ya kusaidia umma kuweza kuelewa masuala mbalimbali ya uchaguzi pasipo upendeleo wowote wala uchochezi.Mwenyekiti wa Kamati ya wamiliki wa blog Joachim Mushi


Kumekua na malalamiko toka kwa  wananchi kutokana na habari mbalimbali zinazoandikwa kwenye baadhi ya blog kwa kutozingatia maadili ya uandishi wa habari na utamaduni wa mtanzania jambo ambalo ni changamoto kwa serikali kutokana na uhuru uliopo kwa wamiliki wa blogi hizo na ukosefu wa sheria zinazowaongoza.