Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Aprili 30, 2011

Majibu Yafanyayo Kazi....I Need a Break!!!


Bubombi ni kikundi ambacho kilianzishwa mwaka 2010 na watu4. Kikundi hiki kinajihusisha na muziki wa acapella na mpaka sasa wanaimbaji wapo 6. Kikundi hiki kinachangamoto nyingi kweli na ukiangali sisi ni vijana chipukizi kwanza hatuna mwalimu wa uimbaji. Pili ni wanafunzi na mwisho hatuna mfadhili.

Tunahitaji mfadhili ambaye atakuwa mfadhili wetu tunamkaribisha sana na aje kanisani kwetu. Sisi tunapatikana kanisa la "KIJICHI SDA CHURCH". Na kama unahitaji kuimba na sisi we njoo kanisani kwetu. Mwisho tunasema tuna mengi ya kusema ila ukitaka zaidi we njoo kanisani. Jina hili BUBOMBI maana yake ni ISIYOELEWEKA .

Sio kama sisi hatueleweki ila pindi tulipokuwa tunaanza kuimba watu wakaanza kutuita BUBOMBI. Na asili ya upatikanaji wa jina hili ni Arusha mtaa wa Burka. Jina hili tumeamua kulitumia mpaka sasa kwa sababu ya changamoto zetu na siku tukiwa na nafasi kubwa ya kufanya kazi hii tutabadilisha jina kadri tutakavyoendelea. Namba zetu za mawasiliano ni kama ifuatavyo:


+255 657 338 433

+255 718 604 580 au

+255 682 499 603.

MUNGU AWABARIKI.

Bubombi Acappella Sing'ers


Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo, kwamba: MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Dr. Carlton P. Byrd

Anapotwambia: “I Need a Break”.


Alhamisi, Aprili 28, 2011

SIKU YA FURAHA AKIWA PEKE YAKE

Asubuhi kila mara alikutwa peke yake akiomba. Kutoka katika eneo hilo alienda kuendelea na kazi zake, nasi tumekuwa mateka wa mateso. Utakuta kwenye account za bank mapesa yamejaa lakini kuna wanao teseka KIHISIA.Na kuna yanayotutesa kisaikolojia.

Tunaishi katika jamii mbovu. Kila mtu anaweza kutenda na kupata matendo mema na hata mabaya pia. Kila mtu anaye mtu ambaye ndie tumaini lake. Tuendeshe mipango yetu ili tusiwe hafifu mbele za watu japo muhimu ni MUNGU. Na ni kweli kuwa tumekutana na hali hizi katika kuishi kwetu tangu tulipoanza na hata tunapoendelea.

Jumanne, Aprili 26, 2011

SIKU YA KWANZA ....M a J i/WATER

Maji huwa ni kiini cha uhai duniani na pia kiini cha utamaduni wa kibinadamu. Hakuna mtu anayeweza kuishi bila maji kwa sababu asilimia 50 - 65 za mwili wa mwandamu huwa ni maji. Hata miili ya mimea na wanyama kwa kiasi kikubwa ni maji.Kikemia ni kampaundi ya elementi za oksijeni na hidrojeni zikiunganisha atomi mbili za hidrojeni na atomi moja ya oksijeni kuwa molekuli ya H2O au maji.

Jina la maji hutumika hasa kwa hali ya kiowevu ya H2O. Hali mango huitwa barafu na hali ya gesi huitwa mvuke. Yenyewe haina rangi wala ladha au herufu.

Maji huwa ni kiowevu kinachopatikana kwa wingi duniani. Yajaza mito, maziwa na bahari. Theluthi mbili za uso wa dunia hufunikwa na maji.

Upatikanaji wa maji ulikuwa jambo muhimu katika historia ya utamaduni wa kibinadamu tangu mwanzo. Njia za maji zilikuwa kati ya njia za kwanza za mawasiliano kwa watu; mabonde ya mito inakata milima na kurahisisha usafiri.

Hata kwa watu kwenye ngazi ya wavindaji kando la mto au la ziwa lilikuwa mahali muhimu walipopata wanyama waliokuja kunywa. Watu wenyewe walipanga makazi yao penye maji. Binadamu walipoanza kulima maji kwa mashamba yalikuwa muhimu zaidi hasa katika maeneo pasipo na mvua wa mara kwa mara.

Wataalamu wengi huona ya kwamba ugawaji wa maji ulikuwa chanzo cha hisabati, sayansi na serikali. Madola makubwa ya kwanza yametambuliwa katika mabonde ya mito kwenye nchi yabisi kama mto Naili, Frati na Hidekeli au Indus. Haja ya kugawa maji, kujenga mifereji, kuitunza na kusimamia shughuli hizi zilileta haja ya kujenga uwezo wa kuhesabu, kutunza kumbukumbu, kuanzisha mwandiko na kuwa na vyombo vya utawala.

**************************************************************

SIKU YA KWANZA NI SIMULIZI INAYOGUSA MAISHA HALISI YA BINADAMU, NI KIPENGELE KITAKACHOKUWA KINAKUIJIA KILA JUMANNE.

**************************************************************

Issue Hii ni Kwa Msaada wa WiKiPeDia

Jumatatu, Aprili 25, 2011

N e N o

Katika Blog ya Simon-Kitururu Nimekuta jambo hili:

Kuna maisha ya NENO yaishiyo kwenye MANENO!

Nikwambie Jambo rafiki;

Neno ni sehemu fupi ya lugha yenye maana. Ni sauti inayotamkwa au kuandikwa pamoja na kutaja jambo fulani.

Neno linaweza kuwa fupi lenye mofimu (yaani sauti inayowakilisha maana fulani) moja tu au kuwa ndefu lenye mofimu mbalimbali.

Wataalamu wanaona neno ni sehemu ya lugha yenye kituo kidogo mbele na nyuma yake, au kwa maandishi jumla ya herufi zenye maana zilizotengwa kwa nafasi nyuma na mbele.

Katika mazungumzo wakati mwingine si rahisi kutofautisha maneno kama ni maneno marefu au maneno mawili. Kwa mfano kuna maneno yaliyobuniwa juzi tu kwa kutaja mambo ya teknolojia na sayansi ambayo yanaunganisha maneno mawili kuwa moja:

  • garimoshi (gari + moshi) kama kifupi cha "gari la moshi" iliyokuwa kawaida zamani
  • mawasilianoanga (mawasiliano + anga - "telecommunication")

Si wazi mara moja kwa wakilizaji wanaosikia haya mara ya kwanza kama ni neno moja au maneno mawili.

Wataalamu wa lugha hutofautiana aina za maneno kama vile nomino, kitenzi, kivumvishi, kielezi, kiunganishi na vingine.

Maneno kwa pamoja yanaunda sentensi yakifuata masharti ya sarufi katika lugha.


Kuna Muungano Day 26th, April, 2011!!! Hebu angalia muungano wa herufi hapo juu.