Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Februari 04, 2016

KWA NINI WATU WENGINE WANABAKI MASKINI?



Sababu zifuatazo zinaweza kuwa na ukweli mtupu;

1. Kushindwa kuamua haraka fursa zinapojitokeza kwao

2. Fursa kali Zikitokea wanaziona kama ni uongo na utapeli wa mjini

3. Kung'ang'ania kuajiriwa hata kama ajira hiyo hailipi

4. Kudhania unajua sana hivyo huoni jipya la kujifunza

5. Kukosa ujasiri wa kuanza. Unapanga mwezi huu au mwaka huu ntafanya hili au lile. Lakini mwaka unaisha hujaanza!!!

6. Kutokuwa na ndoto ya kiasi cha pesa unazotaka kwa siku, kwa wiki mwezi au mwaka.
 Unataka shs ngapi kwa siku? Wiki? Mwezi? Mwaka? Kwa nini unataka kiasi hicho? Matumizi yako ya lazima ni yapi? Ya starehe zako ni yapi? 

7. Kununua vitu vya bei kubwa sana na visivyo na tija yoyote katika kuongeza kipato chako.

8. Kuwaza kwamba maendeleo yanapatikana uzeeni na siyo ujanani? Eti kumiliki mamilioni ya pesa mpaka uwe mzee kama Reginald Mengi vile. 

9. Kufikiri eti huwezi kufanikiwa kuwa na fedha kuubwa mpaka uwe freemason au fisadi. Ujinga.

10. Kuwa na wategemezi kibao nyumbani kwako wakati kipato chenyewe kinatosha kula watu 2 tu kwa mwezi. Hatari!!

11. Kusubiri siku utakayopata pesa nyingi sana eti ndipo utafanya biashara hii au ile! Utasubiri sana. 

12. Kutokuweka akiba yoyote kwa malengo ya maendeleo ya watoto na wajukuu zao. 

13. Kufikiria kuwa kuna siku utapata msaada kutoka kwa wafadhili, serikali au wazungu au washikaji zako. Utangoja sana.

14. Kubadilisha mshahara wako au kipato chako kuwa mali ya ukoo mzima. Kila mtu kwenye ukoo wenu anakuomba pesa na wewe unampatia. Usimpe mtu samaki mfundishe kuvua samaki naye hatakuomba tena samaki. Usimpatie maziwa ndugu yako mfundishe kufuga ng'ombe wa maziwa.

Mpendwa wewe umeguswa na sababu ipi ktk hizo? 

Nakutakia Februari Njema?

Jumatano, Februari 03, 2016

UANDAAJI WA KIPINDI MORNING STAR TV
















ENEO LENYE PWANI YA BARIDI - SVALBARD


TUNASAFIRI kwa ndege katikati ya mawingu mazito na hivyo hatuwezi kuona chochote. Kwa ghafula, ndege yetu inatoka kwenye mawingu na chini yetu tunaona eneo la Aktiki lililofunikwa kwa theluji. Mandhari hiyo inapendeza kama nini! Tunapotazama mabamba ya barafu, mikono ya bahari, na milima iliyofunikwa kwa theluji, tunastaajabu. Ni kana kwamba eneo hilo lisilo na mimea lililofunikwa kwa theluji na barafu halina mwisho. Tumekuja kutembelea Svalbard, visiwa vilivyo karibu na Ncha ya Kaskazini, kati ya digrii 74 za latitudo na digrii 81 kuelekea kaskazini!

Jina Svalbard, linalomaanisha “Pwani Baridi,” lilionekana kwa mara ya kwanza mnamo 1194 katika maandishi ya Waiceland. Lakini eneo hilo “liligunduliwa” miaka 400 baadaye, mnamo 1596 na hivyo likajulikana ulimwenguni pote. Mwaka huo kikundi cha wagunduzi Waholanzi kikiongozwa na Willem Barents kilikuwa kikisafiri kwa meli kuelekea kaskazini wakati ambapo mmoja kati yao aliona kwenye upeo wa macho yake eneo lisilojulikana, safu ya milima yenye ncha. 

Wagunduzi hao walikuwa kwenye eneo la kaskazini-magharibi mwa Svalbard, naye Barents aliita eneo hilo “Spitsbergen” jina linalomaanisha “Milima Iliyochongoka.” Hilo ndilo jina la kisiwa kikubwa zaidi kati ya visiwa hivyo. Ugunduzi wa Barents ulianzisha kipindi chenye utendaji mwingi huko Svalbard. Utendaji huo ulitia ndani kuvua nyangumi, sili, kuwakamata wanyama, kugundua maeneo mapya, kuchimba makaa ya mawe, kufanya utafiti wa kisayansi, na utalii. Kwa miaka mingi, nchi kadhaa zimeshiriki katika utendaji huo, lakini kuanzia mwaka wa 1925 visiwa hivyo vimekuwa chini ya utawala wa Norway.


MATUKIO KATIKA PICHA