Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Oktoba 30, 2011

MFUMO WA MAWASILIANO ULIVYO

Mawasiliano ni mchakato ambapo habari hupakiwa na kutumwa na kupashwa na anayetuma kwa anayepokea kupitia kwa njia maalum. Kisha anayepokea hupakua ujumbe ule na kumpatia aliyetuma (ma)jibu. Aina zote za mawasiliano huhitaji anayetuma, ujumbe, na anayepokea. Mawasiliano huhitaji kwamba wale wanaohusika katika mawasiliano wawe na jambo linalowaunganisha kimawasiliano. Kuna njia zinazohusisha kusikia, kama vile unenaji, wimbo, na toni ya sauti, na kuna zile zisizohusisha kusikia, kama vile miondoko ya mwili, lugha ishara, kugusa, kuwasiliana kwa macho, na kuandika.

Mabadiliko katika mawasiliano

Kadri ambavyo wakati umepita , teknolojia imeendelea kukua na kuibua aina mpya ya na mawazo kuhusu mawasiliano. Maendeleo haya ya kiteknolojia yalibadilisha jinsi mawasiliano yanavyofanyika. Watafiti wamegawanya jinsi mawasiliano yalivyobadilika katika hatua tatu.

Mabadiliko ya mwanzo katika Mawasiliano: mawasiliano ya kwanza katika maandishi yalianza na michoro. Maandishi haya yaliandikwa kwenye mawe, ambayo yalikuwa mazito mno kuhamishwa. Wakati huo, mawasiliano katika maandishi hayangeweza kubebwa, ingawa yalikuwepo.

Mabadiliko ya pili katika Mawasiliano: Maandishi yalianza kufanyiwa kwenye karatasi, mavunjo, udongo, nta, nk Herufi za alfabeti zilibuniwa, hivyo basi kuruhusu mfanano wa lugha katika maeneo makubwa. Baada ya muda, shirika la uchapishaji la Gutenberg lilianzishwa. Gutenberg alitayarisha kitabu cha kwanza cha kuchapishwa akitumia mashine yake, na kitabu hicho kilikuwa ni Biblia. Maandiko haya yaliweza kusafirishwa kwa watu wengine duniani ili wayaone. Mawasiliano ya maandishi sasa yanaweza kuhifadhiwa na kubebwa.


Mabadiliko ya tatu ya Mawasiliano: Taarifa sasa inaweza kuhamishwa kupitia mawimbi, na ishara za kielektroniki.


Kwa hivyo mawasiliano ni njia inayotumiwa katika kutoa na kufikisha maana katika jaribio la kusababisha ufahamu wa kijumla. Utaratibu huu unahitaji mkusanyiko mkubwa wa ujuzi wa mawasiliano miongoni mwa na baina ya watu, kusikiliza, kutazama, kuongea, kuhoji, kuchambua, na kutathmini. Ni kupitia kwa mawasiliano ambapo kushirikiana na ushirikiano hutokea......


Pia kuna vikwazo vingi vya kawaida katika mawasiliano. Viwili kati ya vikwazo hivyo vikiwa ni kupasha ujumbe kupita kiasi (mtu anapopokea ujumbe mwingi mno kwa wakati mmoja), na ujumbe changamano. Mawasiliano ni mchakato unaoendelea.

Aina za mawasiliano

Kuna sehemu tatu kuu katika mawasiliano ya binadamu ya ana kwa uso ambayo ni miondoko ya kimwili, toni ya sauti, na maneno. Kulingana na utafiti:

  • 55% ya athari hulingana na miondoko ya kimwili-jinsi mtu alivyokaa, ishara za uso au mikono, na mawasiliano kupitia kwa macho,
  • 38% hulingana na toni ya sauti, na
  • 7% kwa ujumbe au maneno yaliyotumika katika mchakato wa mawasiliano.

Ingawa asilimia ya ushawishi inaweza ikabadilika kulingana na sababu tofauti kama vile mkilizaji na msemaji, mawasiliano kwa jumla hulenga kutimiza lengo moja kwa hivyo, katika baadhi ya matukio, huwa yanafanana kote duniani. Mfumo wa ishara, kama vile sauti, kiimbo au uzito wa sauti, ishara za mikono au uso au ishara zilizoandikwa ambazo huwasilisha mawazo au hisia. Ikiwa lugha inahusu kuwasiliana kwa ishara, sauti, mlio, ishara za uso au mikono, au ishara zilizoandikwa, je, mawasiliano ya wanyama yanaweza kuchukuliwa kama lugha? Wanyama hawana lugha iliyoandikwa, lakini wao hutumia lugha ya kuwasiliana miongoni mwao. Katika hali hiyo, mawasiliano ya wanyama yanaweza kuchukuliwa kama lugha kivyake.

Lugha za Binadamu zinazozungumzwa na kuandikwa zinaweza hufafanuliwa kama mfumo wa ishara (zinazojulikana wakati mwingine kama [[leksia) na sarufi (kanuni)|leksia) na sarufi (kanuni)]]) ambayo ishara hizo huzingatia. Neno "lugha" pia hutumika kurejelea sifa bainifu za lugha. Kujifunza Lugha ni jambo la kawaida katika utoto wa binadamu. Lugha nyingi za binadamu hutumia mifumo ya sauti au ishara ambazo huwezesha mawasiliano baina ya mtu na wenzake. Kuna maelfu ya lugha za binadamu, na huwa na sifa bainifu, ingawa nyingi ya sifa hizi huwa na upekee.


Hakuna mgawanyo dhahiri kati ya lugha na lahaja, lakini mwanaisimu Weinreich Max anatambuliwa kwa kusema kuwa "lugha ni lahaja iliyo na jeshi la nchi kavu na la majini ". Lugha za kuundwa kama vile Kiesperanto, lugha za tarakilishi, na maumbo mbalimbali ya hisabati haziko chini ya sifa bainifu zinazohusisha lugha za binadamu.

Mawasiliano kwa Ishara

Mawasiliano kwa ishara ni mchakato wa kuwasiliana kwa njia ya kutuma na kupokea ujumbe usiohusisha maneno. Ujumbe kama huo unaweza kuwasilishwa kupitia ishara za uso au mikono, miondoko ya kimwili au jinsi ya kukaa; ishara ya uso na kutazamana machoni [[, mawasiliano kwa vitu kama vile mavazi uliyovalia,, jinsi ulivyotengeza nywele, au hata kwa michoro, pia kupitia jumla ya njia zilizoandikwa hapo juu, kama vile mawasiliano kupitia kwa tabia.|, mawasiliano kwa vitu kama vile mavazi uliyovalia,, jinsi ulivyotengeza nywele, au hata kwa michoro, pia kupitia jumla ya njia zilizoandikwa hapo juu, kama vile mawasiliano kupitia kwa tabia.]] Mawasiliano kwa ishara huwa na jukumu muhimu katika maisha ya kila siku ya kila mtu, iwe ni katika uhusiano wa kiajira hadi wa kimapenzi.


Mazungumzo pia huwa na vipengele vya mawasiliano kwa ishara yanayojulikana kama 'paralanguage' au 'viziada-lugha', ambayo huhusisha ubora wa sauti, hisia na mitindo ya kuzungumza, ikiwa pamoja na sifa za kiarudhi kama vile mdundo, lafudhi na msisitizo. Aidha, matini zilizoandikwa zina vipengele vya mawasiliano kwa ishara kama vile mtindo wa kuandika, mpangilio wa maneno, au matumizi ya hisia. Neno lililounganisha maneno ya Kiingereza ya hisia (au emote) na ikoni (icon), kihisishi (an emoticon) ni ishara au muungano wa ishara zinazotumiwa kupitisha hisia katika maandishi.


Aina zingine za mawasiliano kama vile telegrafia huwa katika kategoria hii, ambapo ishara hupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia tofauti. Ishara hizi zinaweza kuwa viwakilishi vya maneno, vifaa au makadirio tu. Majaribio yameonyesha kwamba binadamu wanaweza kuwasiliana moja kwa moja kupitia kwa njia hii bila miondoko ya kimwili, toni ya sauti au maneno.


Kategoria na sifa GW Porter anagawanya mawasiliano kwa ishara katika kategoria nne:


Kimwili. Hii ni aina ya mawasiliano ya kibinafsi. Mawasiliano haya yanahusisha ishara za uso, toni ya sauti, kugusa, kunusa, na miondoko ya mwili.


Ujumi Hii ni aina ya mawasiliano ambayo hufanyika kupitia kwa njia za ubunifu: kucheza ala ya muziki, dansi, uchoraji na uchongaji.


Ishara. Hii ni aina ya mawasiliano, ambayo inajumuisha matumizi ya bendera za ishara, milio 21 ya bunduki, pembe, na ving'ora.


Kiashiria. Hii ni aina ya mawasiliano ambayo inatumia alama za kidini, hadhi, au za kujenga nafsi.


Sifa zisizobadilika


Umbali. Umbali mtu mmoja anaosimama kutoka kwa mtu mwingine kwa kawaida huwasilisha ujumbe fulani. Katika baadhi ya tamaduni hii ni ishara ya mvuto, na kwa wengine inaweza kuonyesha hadhi au umuhimu wa ujumbe unaopitishwa.


Namna ya kujiwasilisha. Watu wanaweza kujiwasilisha kwa njia mbalimbali: uso kwa uso, ubavu kwa ubavu, au hata wakifuatana. Kwa mfano, watu walio na ushirikiano kuna uwezekano watakaa ubavu kwa ubavu na washindani wakati mwingi hutazamana.


Namna ya kukaa. Kwa kawaida mtu anaweza kuwa amelala chini, ameketi, au amesimama. Hivi sio vipengele vya mkao vinavyowasilisha ujumbe. Je, sisi tunatembea kwa kujikokota au tumesimama wima? Tunakunja miguu au mikono yetu? Njia kama hizi za kukaa huwasilisha kiwango cha urasmi na kiwango cha mapumziko katika mawasiliano.


Mgusano wa Kimwili. Kusalimiana kwa mikono, kugusana, kushikana, kukumbatiana, kusukumana, au kupiga kikofi mgongoni, haya yote huwasilisha ujumbe. Huwa yanaashiria urafiki au hisia za (au ukosefu wa) mvuto.



Sifa Badilifu


Ishara za Uso. Tabasamu, kukunja uso, kuinua nyusi, piga miayo, na kukenua, hivi vyote huwasilisha habari. Ishara za uso hubadilika mara kwa mara wakati wa mawasiliano na hufuatiliwa sana na mpokeaji. Kuna ushahidi kuwa maana ya ishara hizo inaweza kuwa sawa katika tamaduni mbalimbali.


Ishara. Mojawapo ya ishara zinazotumiwa, lakini zisizoeleweka, ni vidokezo katika mwondoko wa mkono. Watu wengi hutumia miondoko ya mkono mara kwa mara wakati wanapoongea. Wakati baadhi ya ishara (mfano, kukunja ngumi) zina maana bia, nyingi za ishara huwa kila mtu anajifunza kibinafsi na zina upekee.


Kutazama. Kipengele kikubwa cha mawasiliano ya kijamii ni kutazamana macho. Kipengele hiki kinaweza kuwasilisha hisia, ashiria wakati wa kuzungumza au kuwacha kuzungumza, au chuki. Marudio ya kutazamana yanaweza kuonyesha aidha shauku au kuchoka.

Mawasiliano ya Kutazama

Mawasiliano ya kutazama kama jina linavyopendekeza ni mawasiliano kwa njia ya vielelezo. Ni kupitisha wa mawazo na habari katika aina ambazo zinaweza kusomwa au kutazamwa. Kimsingi yanahusishwa na vipimo vya aina mbili , na yanahusisha: ishara, tipagrafia, kuchora, miundo ya kigrafiki, mchoro, rangi na rasilimali za kielektroniki. Mawasiliano haya hutegemea tu kutazama. Ni aina ya mawasiliano iliyo na athari za kuona. Imejengwa kwenye wazo kwamba ujumbe unaoonekana ukiunganishwa na maandishi huwa na uwezo mkubwa wa kutaarifu, kuelimisha au kumshawishi mtu. Ni mawasiliano kwa kuwasilisha taarifa kupitia vielelezo.


Tathmini ya muundo mzuri wa kutazamwa hujikita kwenye kupima ufahamu na watazamaji, na wala siyo kwenye ujumi au upendeleo wa kisanii. Hakuna-kanuni bia za uzuri na ubaya. Kuna njia mbalimbali za kuwasilisha taarifa kwa kutazama, kama vile kutumia ishara, miondoko ya kimwili, video na TV. Hapa, lengo liko kwenye kuwasilisha matini, picha, michoro, na kadhalika, zikiunganishwa kwenye maonyesho ya tarakilishi. Dhana wasilisho la kutazama hutumiwa kurejelea uwasilishaji halisi wa taarifa. Utafiti wa hivi karibuni katika sehemu hii umelenga miundo ya tovuti na matumizi ya grafiti. Waundaji wa grafiti hutumia mbinu za mawasiliano ya kutazama katika kazi yao.

Aina nyingine ya mawasiliano

Aina nyingine za mawasiliano maalum ni kama vile:

Mawasiliano ya Mdomo

Mawasiliano kwa mdomo ni mchakato ambapo habari hupitishwa kutoka kwa msemaji hadi kwa msikilizaji kupitia kwa mdomo lakini vielelezo vinaweza kutumiwa kusaidia katika mchakato huu .. Msikilizaji anaweza kuwa mtu mmoja, kikundi au hata hadhira. Kuna aina chache za mawasiliano ya mdomo: majadiliano, hotuba, mawasilisho, nk. Hata hivyo, mara nyingi wakati unawasiliana ana kwa ana miondoko ya mwili na toni ya sauti yako huwa na athari kubwa kuliko maneno halisi unayoyasema. Kulingana na utafiti fulani:

55% ya athari hulingana na miondoko ya mwili. Kwa mfano: mkao, ishara, mawasiliano kwa macho, nk.

38% hulingana na toni ya sauti yako

7% hulingana na maudhui ya maneno yako katika mchakato wa mawasiliano.


Unaweza kuona kwamba maudhui au neno unalolitumia silo litakalo amua sehemu ya mawasiliano mazuri. "Jinsi unavyowasilisha ujumbe" huwa na athari kubwa kwa msikilizaji. Ni lazima unase makini ya hadhira na uhusiane na wao. Kwa mfano, watu wawili wanaosema kichekesho, mmoja wao anaweza kuifanya hadhira kuangua kicheko kutokana na miondoko mizuri ya kimwili na toni ya sauti. Hata hivyo, mtu wa pili anayewasilisha kichekesho kile kwa maneno yale yale anaweza kuifanya hadhira itazamane.


Katika mawasiliano ya mdomo, inawezekana kutumia vielelezo ili kukusaidia kuwasilisha habari kwa usahihi zaidi. Mara nyingi, tunaweza kutumia 'PowerPoint' katika mawasilisho yanayohusiana na hotuba zetu ili kuwezesha au kuboresha mchakato wa mawasiliano. Ingawa, hatuwezi kuwasiliana kwa kutumia vielelezo tu kwa sababu sisi hatutakuwa tukizungumza kuhusu mawasiliano ya mdomo tena.

Mipango ya kodi za mawasiliano

Mawasiliano kwa kawaida hufafanuliwa kwa kuzingatia mitazami michache mikuu: Ujumbe (mambo ya aina gani yanayosemwa), chanzo / mtumaji / Msemaji / Mfumbaji (ambaye anatuma), aina (ujumbe ni wa aina gani), njia (unatumwa kupitia njia gani), unapokwenda / mpokeaji / lengo / mpokeaji (anayepokea ujumbe), na lengo au kipengele cha kipragramatiki. Kati ya vikundi, mawasiliano yanahusisha vitendo vinavyotunukia maarifa na tajriba, kupatia mawaidha na amri, na kuuliza maswali. Matendo haya yanaweza kuchukua sura nyingi, katika mojawapo ya njia mbalimbali za mawasiliano. Sura hizi hutegemea uwezo wa kikundi kinachowasiliana. Pamoja, maudhui na sura za mawasiliano kukamilisha ujumbe unaotumwa mahali. Mpokeaji anayelengwa anaweza kuwa msemaji mwenyewe, mtu mwingine au kiumbe kingine, kikundi kingine (kama vile shirika au kikundi cha viumbe).


Mawasiliano yanaweza kuonekana kama mchakato wa kusambaza habari unaoongozwa na viwango vitatu vya sheria za elimu ishara:

  1. Kiwango cha kisintaksia (sifa rasmi za ishara na viashiria),
  2. Kiwango cha kipragmatiki (kinahusika na mahusiano kati ya ishara / maneno na watumiaji wake) na
  3. Kiwango cha kisemantiki (utafiti wa uhusiano kati ya ishara na viashiria na yale vinayowasilisha).


Kwa hiyo, mawasiliano ni mwingiliano wa kijamii ambapo angalau vitu au watu wawili wanaotagusana hutumia seti moja ya ishara na seti moja ya kanuni za kielimu ishara. Sheria hizi zinazozingatiwa wakati mwingine huwa zinapuuza mawasiliano ambayo hutokea bila kupangiwa, yaliwemo mawasiliano ya mtu na nafsi yake kupitia kwa shajara au mazungumzo-nafsi, yote ambayo ni matukio ya sekondari yaliyofuatia kujifunza lugha katika maingiliano ya kijamii.


Katika mfano rahisi, habari au maudhui (mfano ujumbe katika lugha asilia) hutumwa katika njia fulani (kama lugha ya mazungumzo) kutoka kwa mtumaji / msemaji / mfumbaji kwa mahali maalum / mpokeaji / mfumbuaji. Katika njia changamano zaidi, msemaji na mpokeaji huwa wameunganishwa kwa wakati mmoja. Mfano mmoja wa mawasiliano ni kama tendo usemi. Namna ya kutafsiri ujumbe ya msemaji inaweza kuwa tofauti na ya msikilizaji kulingana na desturi na tamaduni za eneo walilomo, au jinsia; mambo ambayo yanaweza kuathiri ujumbe uliokusudiwa. Uwepo wa "kelele za mawasiliano" katika njia inayotumiwa (ikiwa ni hewa, katika kesi hii), mapokezi na ufumbuaji wa ujumbe unaweza kuathiriwa, hivyo basi tendo usemi linaweza kutofikia matokeo yaliyotarajiwa. Tatizo moja la mfano huu wa kupakia-kutuma-kupokea-kupakua ni kwamba mchakato wa kupakia na kupakua huashiria kwamba mtumaji na mpokeaji, kila mmoja ana kitu kinachofanya kazi kama kitabu cha kodi , na kwamba vitabu hivi viwili vya kodi vinafanana kwa kiasi ikiwa si kabisa. Ingawa kitu kama vitabu vya kodi kimetajwa na mfano huu, havijawakilishwa kwenye sehemu yoyote ya mfano huu, jambo ambalo linaibua matatizo mengi ya kuelewa.


Nadharia za urekebishaji-pamoja huelezea mawasiliano kama mchakato wa ubunifu na unaobadilika badilika, unaoendelea wala si kubadilishana tu kwa habari. Mwanataaluma wa vyombo vya habari kutoka Kanada Innis Harold alikuwa na nadharia kwamba watu hutumia njia mbalimbali kuwasiliana na njia watakayochagua kutumia itawapa uwezekano tofauti wa kuumba na kudumisha jamii (Wark, McKenzie 1997). Mfano wake maarufu wa kufafanua haya ni kutumia Misri ya kale na kuangalia vile wao walijijenga wenyewe nje ya vyombo vya habari kwa aina tofauti za mawe na mafunjo. Mafunjo ndiyo aliyoyaita 'Kufunga Nafasi (Space Binding)'. Kufunga huku kuliwezesha kupitishwa kwa maandishi kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuwezesha kufanyika kwa kampeni za kijeshi za mbali na utawala wa kikoloni. Mengine ni jiwe na 'Kufunga Wakati (Time Binding)', kupitia ujenzi wa mahekalu na piramidi, wanaweza kuendeleza mamlaka yao kizazi hadi kizazi, kwa kupitia njia hii ya kupitisha habari, wanaweza kubadilika na kuumba ya mawasiliano katika jamii yao (Wark, McKenzie 1997).


Krishi Vigyan Kendra Kannur chini ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Kerala amebuni tawi jipya la mawasiliano ya kilimo linaloitwa Upanuzi kwa Ubunifu (Creative Extension).


Bila mawasiliano ya watu

Mawasiliano katika mingi ya mitazamo yake hayajajifungia tu kwa binadamu, au hata kwa sokwe. Kila mabadilishano ya habari kati viumbe vilivyo hai - yaani kubalishana kwa ishara kunakohusiha mtumaji na mpokeaji walio hai - kunaweza kuchukuliwa kama njia ya mawasiliano. Kwa hivyo, kuna uwanja mpana wa mawasiliano ya wanyama, ambayo yanahusisha mengi ya masuala katika ethnolojia. Pia wanyama waasili kama mwamba tumbawe wanaweza kuwasiliana. Katika ngazi ya kimsingi zaidi, kuna kupatiana ishara kati ya seli, mawasiliano ya seli, na mawasiliano ya kemikali kati ya viumbe asili kama bakteria, na miongoni mwa mimea na himaya za kuvu. Michakato hii yote ya mawasiliano huhusisha mitagusani inayoshirikisha ishara zilizo na ratibu bainifu mbalimbali.


Mawasiliano ya wanyama ni tabia yoyote kwa upande wa mnyama mmoja iliyo na athari ya sasa au baadaye kwenye tabia ya mnyama mwingine. Bila shaka, mawasiliano ya binadamu yanaweza kujumlishwa kama mawasiliano ya wanyama yaliyoendelezwa. Utafiti wa mawasiliano ya wanyama, uitwao zuosemiotiki (zoosemiotics) (tofauti na athroposemiotiki (anthroposemiotics), utafiti wa mawasiliano ya binadamu) umechangia pakubwa katika ukuzaji wa etholojia, biolojia-jamii, na masomo ya uwezo wa mnyama wa kutambua. Jambo hili ni dhahiri kwani binadamu huwa wanaweza kuwasiliana na wanyama, hasa pomboo na wanyama wengine ambao hutumika katika sarakasi. Hata hivyo, hawa wanyama hulazimika kujifunza njia za kipekee za mawasiliano. Mawasiliano ya wanyama, na haswa kuelewa ulimwengu wa mnyama kwa ujumla, ni taaluma inayokua kwa kasi, na hata katika karne ya 21 kufikia sasa, uelewa mwingi wa hapo awali kuhusiana na nyanja mbalimbali kama vile matumizi ya kiishara ya jina, [[hisia za wanyama, utamaduni na kujifunza kwa wanyama|hisia za wanyama, utamaduni na kujifunza kwa wanyama]], na hata tabia za kingono, zilizofikiriwa kwa muda mrefu kuwa zimeeleweka vizuri, zibadilika pakubwa.

Mimea na kuvu

Miongoni mwa mimea, mawasiliano huonekana ndani ya mmea wenyewe , yaani, ndani ya na kati ya seli za mimea, kati ya mimea ya spishi moja au spishi zinazohusiana, na kati ya mimea na viumbe visivyohai, hasa katika sehemu ya mizizi. Mizizi ya mimea huwasiliana na bakteria za rhizobia, na kuvu pamoja na wadudu walio kwenye ardhi. Mitagusano hii sambamba inayohusisha ishara na inayoongozwa na kanuni za kisintaksia, kipragmatiki na kisemantiki hutokea kwa sababu ya "mfumo wa neva" wa mimea uliogatuka. Maana asilia ya neno nyuro katika Kigiriki ni "nyuzinyuzi za mboga" na kama utafiti wa hivi karibuni unavyoonyesha, mengi ya mawasiliano ya ndani ya mmea hufanana na ya nyuro. Mimea pia kuwasiliana kupitia kwa mivuke katika kisa cha tabia za wakati wa mashambulizi na wanyama wala mimea, ili kuonya mimea jirani. Sambamba na hayo, mimea hiyo hutoa mivuke ya kuvivutia vimelea ambavyo huwashambulia wale wanyama. Katika hali ya dhiki mimea inaweza kubadilisha kodi ya kinasaba iliyorithi kutoka kwa wazazi wao na kurudi kwa ile ya mababu zao.


Kuvu huwasiliana ili kuratibu na kupanga ukuaji wao wenyewe na maendeleo yao kama vile malezi ya seli zake na sehemu za kuota. Aidha, kuvu huwasiliana spishi zinazofanana au kuhusiana pamoja na spishi zisizokuvu katika mitagusano ya kimfaano, haswa na bakteria, 'unicellular eukaryotes' , mimea na wadudu. Kemikali za kisemiotiki zinazotumiwa huwa za asili ya kibayotiki na hufanya kuvu kuonyesha athari maalum, ambapo, katika tofauti wakati hata huo kemikali za molekuli huwa si sehemu ya ujumbe wa biotiki unaosababisha msisimko wa viumbe-kuvu. Ina maana kuwa, kuvu zinaweza kutambua tofauti katika molekuli ambazo ni sehemu ya ujumbe wa kibayotiki au kutokuwepo kwa sifa hizi. Hadi sasa kuna molekuli tano tofauti na za msingi zinazojulikana ambazo huratibisha ruwaza tofauti za kitabia kama vile 'nyuzi za hisia', kuzaana, ukuaji, usababishaji wa magonjwa. Uratibu wa tabia na uzalishaji wa vitu kama hivi unaweza tu kufikiwa kupitia michakato fasili: ya kibinafsi au isiyo ya kibinafsi, kiashiria cha kibayotiki, ujumbe wa kibayotiki kutoka kwa spishi zinazofanana, zinazohusiana au zisizohusiana, au hata "kelele", yaani, molekuli zinazofanana lakini hazina ujumbe wa kibayotiki.

Mawasiliano kama taaluma ya kiakademia

Mawasiliano kama taaluma ya kiakademia, ambayo wakati mwingine huitwa "komunikolojia," inahusiana na njia zote tunazozitumia kuwasiliana, hivyo basi inahusisha sehemu kubwa ya utafiti na maarifa. Taaluma ya mawasiliano inahusisha mawasiliano ya kimaongezi na yasiyo ya kimaongezi. Mkusanyiko wa maarifa kuhusu mawasiliano umewakilishwa na kufafanuliwa katika vitabu, machapisho ya kielektroniki, na majarida ya kiakademia. Katika majarida, ripoti za kitafiti ndizo matokeo ya tafiti ambazo ni msingi wa uelewa, unaoendelea kupanuka, wa jinsi sisi wote tunavyowasiliana.


Mawasiliano hufanyika katika ngazi tofauti (hata kwa tendo moja), katika njia mbalimbali, na kwa viumbe wengi, na vilevile kwa mashine fulani. Baadhi ya taaluma za utafiti , ikiwa siyo zote, hutenga sehemu ya mafunzo yake kwa mawasiliano, hivyo basi wakati wa kuzungumza kuhusu mawasiliano, ni muhimu sana kuwa na uhakika kuhusu nyanja ya mawasiliano inayozungumziwa. Ufafanuzi wa mawasiliano hutofautiana sana, baadhi yake ukitambua kwamba wanyama wanaweza kuwasiliana na wenzao na binadamu pia, na baadhi ni finyu zaidi, ukihusisha binadamu katika mitagusano ya kibinadamu iliyo na maana.

*******************************************************

Mawasiliano ni mchakato wa kuhamisha taarifa kutoka chombo kimoja hadi kingine. Michakato ya mawasiliano ni mwingiliano unaohusisha ishara kati ya angalau wakala wawili walio na mkusanyiko wa ishara na sheria za elimu ishara . Mawasiliano kwa kawaida hufafanuliwa kama "kupasha au kubadilishana kwa mawazo, maoni, au habari kwa kunena, maandishi, au ishara". Ingawa kuna kitu kama mawasiliano ya njia moja, mawasiliano yanaweza kueleweka vyema kama mchakato kati ya wahusika wawili ambapo kuna mabadilishano na kukuza kwa fikra, hisia au mawazo (nishati) kufikia lengo lililokubaliwa au mwelekeo uliokubaliwa (habari).

*******************************************************