Mtayarishaji

Morning Star Radio

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sanaa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sanaa. Onyesha machapisho yote

Jumapili, Juni 12, 2016

UMUHIMU WA ELIMU YA MUZIKI NA ELIMU YA UENDESHAJI WA MUZIKI

Photo By: www.borgenmagazine.com


Asilimia kubwa ya wanamuziki hapa Tanzania wanapiga muziki bila ya kuwa na elimu yoyote ya awali ya muziki, hili si jambo la ajabu kwani hali hii iko sehemu nyingi duniani, lakini kitu ambacho ni wazi kinakosekana ni elimu kuhusu utendaji wa taasnia ya muziki. 

Pamoja na kauli nyingi nzuri za viongozi wa Nchi kusifu sanaa hii na wasanii wa sanaa hii lakini ni nadra kusikia kiongozi akiongelea matayarisho rasmi katika sanaa hii na kwa kweli hata katika sanaa nyingine.

Kumekuwepo na ombwe la elimu ya uendeshaji wa tasnia ya sanaa. Ombwe la elimu kwa wataalamu ambao huwezesha wasanii kufika walipo, kuwaendeleza kukaa walipo, kulinda haki za kimaslahi za wasanii na hata kuwapa maelekezo ya kujitayarisha kwa wakati ambapo umaarufu utakuwa umekwisha.

Tasnia ya muziki huhiyaji shule za kujifunza muziki, vyuo vya uongozi wa muziki, au kozi fupi ambapo taaluma za umeneja, uproducer, upublisher, usambazaji, ujuzi wa sheria za hakimiliki na watendaji wengine wa aina hiyo hupata elimu, ujuzi wa sheria za hakimiliki na watendaji wengine wa aina hiyo hupata elimu. Kukosekana kwa elimu hii kumefanya watu kujifunza kwa vitendo kwa kujaribu na hata kubahatisha hivyo mara chache kufanikiwa.

Kukosa elimu sahihi kumewafanya wasanii wengine wenye uwezo mkubwa kupotea kwenye taaluma na wengine kujikuta wakishindwa kuingia kwenye ulingo huu japo uwezo wanao. Pia kumetoa nafasi ya wasio na uwezo kujikita katika uongozi wa sanaa na kuleta matatizo makubwa kwenye sanaa, aidha kwa kuaminika kuwa wanatoa ushauri sahii na hivyo maamuzi yenye hasara kubwa kufanyika. 

Pamoja na mafanikio yaliyoonekana taifa linakwenda kihobela hobela katika tasnia ya sanaa ya muziki. Ushahidi wa wazi upo kwa kupata elimu ya muziki kuanzia umri mdogo kuna faida nyingi sana. Kwanza humuwezesha motto kukuza sehemu ya ubongo ambayo huhusika na hesabu na pia kukuza uwezo wake wa kutafakari. 

Inaeleweka kuwa ubongo huendelea kupata maendeleo miaka mingi baada ya kuzaliwa, hivyo muziki huendelea kuboresha upande wa kushoto wa ubongo ambao ndio huhusika na ujuzi wa lugha na tafakari na hesabu. Muziki husaidia sana watoto kukumbuka mambo mbalimbali, ndio maana hata matangazo ya biashara ya kawaida husindikizwa na muziki ili kukaa katika kumbukumbu kwa urahisi. Kwa watoto muziki husaidia sana katika kazi zao za elimu ya kila siku.

Wasanii waliopata elimu sahihi huwa na uwezo wa kubuni majibu mbalimbali kwa tatizo moja, hii unaweza kuiona kwa mfano ukiwapa wanamuziki kumi semina kuhusu jambo. Kwa mfano: Ukimwi kasha ukawaambia watunge wimbo kuhusu elimu waliyopewa, utashangaa watakuja na tungo tofauti za mtizamo mpya kabisa wa kuelezea elimu hiyo waliyoipata.

Elimu ya muziki hufungua ubongo kuruhusu kuachana na mawazo mengi yaliyopita na kujaribu mawazo mapya. Wasanii kote duniani huwa waanzilishi wa mambo mengi ikiwemo mitindo ya nguo, uvaaji na mambo mengi katika maisha kutokana na ubongo wao kuwa na uwezo wa kuruhusu kufikiria vitu katika mtazamo mpya.

Elimu ya awali ya muziki imeonesha kuwa wanafunzi wa elimu hii hfanya vizuri zaidi katika masomo mengine tofauti sana na mawazo ya kawaida kuwa muziki huharibu watoto. Katika muziki, kosa huwa ni kosa, ukikosea beat, usipotune chombo chako, ukiimba vibaya ni kosa hakuna mbadala, sauti ikiwa juu mno, au chini mno na kadhalika, na wanamuziki hulazimika kurudia tena na tena mpaka atakapopata kitu sahihi na kabisa.

Elimu hii ikiwa kichani kwa watoto toka umri mdogo humsaidia katika kuboresha mambo yake mengine na kuyafanya vizuri zaidi kila mara. Elimu ya awali ya muziki humjenga motto kujua kufanya kazi na watu wengine kama kundi, kutokana na kuelewa kuwa katika muziki watu wengi hutegemeana ili kuleta ubora katika wimbo mmoja, hii huwasaidia katika maisha kila siku.

Kuna mengi yanayopatikana katika elimu bora ya sanaa, pia kubwa likiwa ni kwenda sambamba kitaaluma na ulimwengu, kuna bahati mbaya sana kwa vijana wetu kutaka kuingia katika soko la muziki duniani lakini bila kuwa na matayarisho yanayostahili kufikia huko, wengi ni ndoto zao hazitatimia kwani elimu ya kufikia huko hawana.

Ni wazi kuna haja ya kuanza kutoa elimu ya sanaa kuanzia ngazi ya shule za awali, kuna haja sasa ya kuwasaidia wanamuziki walioko kwenye taaluma kupata elimu ya haki zao. 

Ni wasanii wangapi wanaojua kuwa katika kila tungo, kuna haki tofauti kumi wanazostahili? 

Watunzi wangapi wanajua wana haki kwa kazi zao kutumika kibiashara? 

Wakati viongozi wakisifia wasanii wan je wakumbuke kuwa kinachowafanya wawe na mafanikio ni kutumia kila njia sahihi kukamua mapato kutoka kwenye haki zao hizo zinazolindwa kisheria.
  
Makala hii ni kwa msaada wa John Kitime

Ijumaa, Desemba 12, 2014

Mapinduzi ya Tasnia ya Filamu Nchini Tanzania



 ZAMARADI MKETEMA ameandika sehemu....

“…Natamani sana siku moja atokee mtu kwenye hii sekta atutambulishe hata kama sio kimataifa basi africa tu.  KANUMBA alianza kuonesha mwangaza na juhudi binafsi zilionekana na kila mtu aliona huenda angefika mbali.. lakini baada ya hapo sioni tena!!!!

Mbona hapa nyumbani ni wakubwa tu..? Nini kinawakwamisha..? Kwanini wasanii wetu wa filamu ukubwa wao unaishia nyumbani tu....!!? Tatizo ni nini!!!????? kiukweli ni kama inakatisha tamaa na inaonekana kabisa watu wamerelax na ustar wa bongo wakati wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi... wana bongo movie tukifika kwa wenzetu unaona kabisa tunapwaya kiasi gani.. 


Ujanja wetu ni nyumbani tu!!?? why!!!?? tukianza utanzania wa kufichaficha tutasifiana uongo lakini tukiwa wakweli na nafsi zetu tutaliona hilo na kuchukulia kama challenge..!!! ukweli ni kwamba hii tasnia inasikitisha!!! tena sana nahisi sasahivi tunafanya filamu kwa ajili ya nyumbani tu na tukiingia kwenye mabendi tukisharushwa tumeridhika!! kweli!! hapa ndio mnapotaka mfike!!? ukifika sehemu ukiwa juu nchini kwako tunachotegemea ni wewe kupasua mawimbi uende mbali zaidi nje ya mipaka!! lakini ukiamua kurelax hapo ulipo inamana unasubiri kushuka sababu kiukweli huwezi kukaa juu milele!!! kwanini mmeridhika hivi!!! kaka JB tatizo ni nini!!!??

Mi nakuangalia wewe kama mfano wa msanii mkubwa sana kwenye tasnia kwa sasa... mbona umerelax!!!??? umeridhika na ustar wa tanzania!!!? una kila kitu cha kukufikisha mbali... kinachohitajika ni juhudi binafsi tu ili kesho na sisi tufike mahala pazuri!! hebu tuongee wapenzi.. mnahisi huku kwenye bongo movie TATIZO LIKO WAPIII…!!???

JB Akajibu;

“Kwako Zamaradi na wengine wote..

Kwanza napenda niwashukuru wote kwa jinsi mnavyotuwazia mema. Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza waigizaji wote wa Tz na waandaaji wa filamuU kwa kuthubutu kutengeneza filamu hizi katiks mazingira magumu. Najua watanzania wengi wangependa kuona tukipeperusha bendera nje,lakini naomba muwape wasanii muda.

Tasnia hii ni changa na ina changamoto ambazo zinakatisha tamaa. Hebu tujiulize kwa nini wasomi wengi waliosomea filamuu UDSM na BAGAMOYO hawafanyi filamu hizi? Wasambazaji wengi wakubwa mamu,wananchi na hata hans pop walijaribu wakakimbia, kuna producer mkubwa hapa nchini JOHN RIBER ambaye ametengeneza filamuu kama NERIA na YELLOW CARD lakini naye ukimwambia njoo kwenye hizi filamu atakupa jibu.

Nakubali tuna makosa mengi kama ubora wa filamu zetu na stori lakini nataka niwaambie mazingira ya kufanya filamu bongo yanakatisha tamaa wizi wa kazi zetu umezidi na wasambazaji wengi wamekimbia. Binafsi najipanga kuwa mtayarishaji zaidi kuliko mwigizaji kwa sasa kupitia JERUSALEM FILMS na ndio maana filamu nyingi natoa nafasi kwa vijana ambao kama mabadiliko ya sera ya filamu yatafanywa watatuwakilisha nje.

Kiswahili kisichukuliwe poa kwani kina nafasi kibwa sana. Tukumbuke SHARUK KHAN ni ‘actor’ tajiri2 dunian lakini filamu zake ni za kihindi. Hebu sote tusaidiane kupambana na changamoto hizi na tuanze na EAST AFRICA kwanza huku tukiboresha, wasomi wa filamu msikimbie njooni tuanze wote na tuwape moyo wasanii wetu waliojaribu kusimamisha tasnia hii kwa vimtaji toka mifukoni mwao na vipaji walivyopewa na mungu bila msaada kutoka popote. Asanteni kwa kutuunga mkono kwemye filamu zetu.”
===================================




===================================


Tulitazame sasa hili suala kwa Pamoja;

Tasnia yetu pendwa nchini, Tasnia ya sanaa ya maigizio, hasa kwenye upande wa Filamu, Sina shaka hata kidogo kwamba baada ya Muziki, Sanaa ya Filamu na Maigizo ndiye inafuatia kupendwa zaidi hapa nchini, Idadi ya watazamaji na wafuatiliaji inathibitisha hilo!

Bahati mbaya Tasnia hii inaelekea kufa kibudu. Narudia, Tasnia ya Filamu nchini inaelekea kufa KIBUDU. Hali ni mbaya sana kwenye upande huu wa sanaa nchini licha ya kuwa ndiyo FANI inayoongoza kwa kutoa Ajira kwa vijana wengi zaidi nchini. Tukubaliane hapo kwanza!

Makosa yapo Mengi. Mbaya zaidi yote si makosa yanayohitaji kuonwa mpaka na Mtaalamu pekee. Hata Asiye na utaalamu wa Sound engineering atajua kwamba sauti kwenye Bongo movies ni tatizo, asiyefahamu mambo ya script akitazama tu atajua, Asiyejua umuhimu wa continuity naye hali kadhalika, achilia mbali yule asiyejua kiingereza kwa ufasaha, inamuhitaji elimu ya kujua tafsiri ya toilet tu kung'amua kwamba kiingereza cha kwenye subtitlles ni majanga. Mtiririko wa hadithi na uhalisia ni tatizo sugu. Inasikitisha sana.

Sitagusia hata moja katika hayo!

Leo Nagusa upande wa Mapinduzi ya Ujumla. Kwanini tasnia hii inaporomoka badala ya kukua zaidi? Kwanini hakuna mabadiliko chanya? Kwanini filamu nchini zimebaki kuwa na mabaka mabaka ya ulalahoi? Kwanini hatuvuki mipaka? Kwanini hatufanyi kweli? Kwanini muziki unatoboa zaidi kuliko filamu? Nini tatizo?

MAONI YANGU:

KWANZA, Wasanii waanze kutengeneza 'Image' nzuri;

Maana kwa sasa imeshachafuka. Nasema ukweli, Tasnia hii ina taswira ya uhuni kupitiliza. Na hii ni kutokana na wasanii wakubwa (vioo) kukumbwa na kashfa chafu. Kucha kutwa magazetini kuandikwa upuuzi, pengine wapo wanaolipwa kwa kuuza gazeti, lakini sidhani kama wanacholipwa kina thamani kubwa kupita kazi ya sanaa wanayoifanya.

PILI, Ianzishwe Mikakati Madhubuti;

Ni wakati sasa kwa wasanii kutengeneza Mipango Madhubuti na mikakati (Action plans) itakayowaongoza kufanya kazi kwa usiriaz. Inawezekana, najua mlishajaribu huko nyuma, lakini bado inawezekana.

TATU, Upekee na Usasa;

Hapa namaanisha kufanya movie kisasa na kwa upekee kabisa. Itazamwe mifano ya filamu kama ya CHUMO (Starred by Sharo Milionea & Jokate), Soap ya Siri ya Mtungi na kadhalika (wataalamu sio kikwazo panapo fedha).

NNE, Kushirikisha Wadau;

Watanzania na wapenzi wa filamu za kibongo ni wengi sana. Hakuna tu utaratibu wa kufanya research ili kuwa na data kamili, lakini kwa observation tu ni dhahiri kwamba Bongo Movie haijatupwa kivile. Ni basi tu wana-tasnia wenyewe mnachosha. Sijui lengo lenu ni nini haswa! Ni ajabu mtu kuua ajira yako kwa mikono yako mwenyewe!

Supporters wapo wengi sana. Wapo watazamaji wa hizi movies ni watu wenye uwezo mkubwa pengine hata wa kuwekeza. Achana na Mapedjee wanaohonga kwa lengo la kufurahisha nafsi zao, kuonekana, au malengo yao binafsi yasiyo na tija (japo wakitumiwa vizuri inaweza kusaidia sehemu). Hapa nazungumzia Matajiri, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa, hata mawakala wa biashara, wakitumika vizuri, watafanya kitu.

Kinachohitajika ni ushawishi tu! Yaani wasanii wenyewe wahakikishe wawe na mipango na uwezo wa kumshawishi mtu/shirika/kampuni kuwekeza (kama si kufadhili) kazi zao. Serikali Pengine Imeshindwa hili!

Na ushawishi huja pale penye tija. Mtu aone umuhimu wa kufanya hivyo. sio kuchoma pesa zake bure. Mbona Michezo Mingi inadhaminiwa? Mpira wa miguu, Ndondi, Riadha n.k., Kwanini isiwe Bongo Movie? - Jikagueni upya kabla hamjachelewa.

TANO, Kuomba Fedha na Access Kubwa zaidi;

Kilio cha wasanii wengi kushindwa kufanya movie zenye ubora ni Mitaji. Wanalalamika hawana fedha za kutosha kuweza kucheza baadhi ya story. Ni kweli kabisa. Na hii pengine ndiyo sababu kubwa hata thamani ya kazi zao kwa wasambazaji inashuka siku hadi siku. Hii ni kutokana na bidhaa kuwa ni low quality.

Sasa basi, katika mikakati yao, Ni vyema wakazingatia ni vipi watapata mitaji ya kucheza story zinazohusika. Kisha watafute Soko zuri la kuuza bidhaa yao kwa bei itakayowanufaisha, sio watakayopangiwa na 'muhindi'.

Hatua za kupata mitaji zaweza kuwa;

* Kuomba udhamini kutoka kwa makampuni rafiki - Hapa namaanisha yale makampuni yanayohusiana na kazi zao. Kwa mfano Makampuni ya bidhaa za Camera, Deki, Simu, na kadhalika. Kwa ufupi, yale makampuni yanayoshabihiana na kazi za filamu yatakuwa rahisi zaidi kuitika!

* Kuomba mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha - Kwa kuwa filamu ni biashara kama zilivyo biashara nyingine kubwa, kampuni za utengenezaji wa hizi filamu (RJ, Jerusalem, 5effects, Timamu African Media n.k) zikiandaliwa mazingira mazuri zinaweza kukopesheka.

* Kutoa fursa kwa wahisani na wawekezaji - Kampuni za utayarishaji wa filamu zinaweza kutoa nafasi kwa wawekezaji kuwekeza kwenye kiwanda cha filamu nchini. Hapa kutawawezesha wawekezaji kuweza kuikuza zaidi tasnia hii kwa kuweka mitaji yao mikubwa na kuisimamia ili ipatikane faida. Inawezekana!

Pia, wasanii waombe access kubwa kutoka serikalini ili waweze kutambulika Rasmi na kuaminiwa. Haya yote yatawezekana endapo shirikisho la filamu nchini (TAFF) litakuwa na makali na sauti ya nguvu.

SITA, Wasanii watumie wataalamu kwenye kazi zao;

Hapa namaanisha ni wakati sasa waandaaji wa filamu pamoja na wasanii kwa ujumla waanze kushirikisha wataalamu kwenye kazi zao. Kwa maana wafanye tafiti ndogo ndogo kuhusiana filamu husika (mfano kwenda maktaba kutafuta vitabu vinavyoelezea let's say masuala ya historia, kama hadithi ya movie inagusia huko) na kupata majibu ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu hao. Hii ni faida kwani 'uhalisia' wa movie utakuwa maradufu!

Ushirikishwaji uanzie kwenye masuala ya story, production mpaka kwenye masuala mazima ya masoko. Uwanja huu ni mpana sana, nadhani mwanga umeanza kuonekana hapo!

===================================


===================================

 
Kwa kipekee kabisa, Niwapongeze Timamu Effects / Timamu African Media, kwa kuonyesha njia. Nathubutu kusema hawa ndio role models kwenye filamu za Kitanzania. Ni wenzetu, walianzia chini, lakini wamejitahidi kukua kifani, kimaudhui na kimapinduzi hususan kwenye ubora wa story na quality ya uandaaji wa filamu zao zote.

Nashauri waigwe na kuwa dira ya tasnia ya filamu nchini, waendelee kufanya mambo makubwa zaidi ili hatimaye na Tanzania tufikie levo angalau za Nigeria na Ghana. Nimefurahi kuona Wamepata tuzo kadhaa za kimataifa, na kubwa zaidi ni za hivi karibuni huko Marekani katika Future Africa Awards. Hongera Timoth Conrady na Timu yako!


Naomba niishie hapa, ili kutoa nafasi kwa wengine kuchangia mawazo yao, na kwa pamoja tuweke mitazamo chanya na yenye taswira ya kimapinduzi kweli ili hatimaye tuwe tumeshiriki kwenye kuboresha tasnia ya filamu nchini.

Nawasilisha....


Chanzo By:  MR. CONFIDENT, on JamiiForums

HATMA YA WASANII TANZANIA NI MBAYA WASIPOBADILIKA

BI CHEKAAA


LAZIMA nimshukuru Mungu sana kuwa mimi ni msanii wa hapa Tanzania na bado sijapotea sana kwenye masikio na macho ya watu. Lakini kuna wenzangu wengi waliokuwa maarufu kuliko mimi waliokuwa na mafanikio ya kisanii na kiuchumi kuliko mimi kwa sasa hali zao za maisha ni mbaya sana. Kuna sababu kadhaa za matokeo haya, lakini kuna moja kubwa nalo ni kukosa ufahamu wa haki zao. 
 
Wakati msanii anapoanza kutafuta umaarufu huwa mtu wa kutaka kupata ushauri, lakini pindi anapojulikana hataki tena ushauri hasa kuhusu haki anazostahili kuzipata kutokana na kazi yake. Hali hii hutokana na sababu mbili kubwa, moja ni kiburi kinachojengeka kutokana na umaarufu hivyo kumfanya muhusika kuona kuwa haiwezekani kamwe akashuka na kuwa mtu wa kawaida. Pili ni mtego ambao wasanii wengi huingia na kujikuta chini ya wafanya biashara wahuni ambao ili waendelee kuwamiliki wasanii huwa wanawakataza kujihusisha na harakati zozote ambazo zitaweza kuwaamsha akili zao kudai haki yao. 

Na wafanyabiashara wengine huweza hata kuwafundisha mambo yasiyo ya ukweli katika biashara na kuwafanya wasanii waamini kuwa hawataweza kufanya kazi bila ya kuwa na wafanya biashara hawa. Lakini ubora wa wanamuziki hawa unaposhuka wafanyabiashara hawa hawa huwatema kama kaa la moto na wasanii kujikuta wakihangaika maisha ya tabu bila msaada wowote.

HAKIMILIKI 

Ni haki zaidi ya kumi anazopata msanii katika kila kazi yake, wasanii wengi hawajui haya na wengi wala hawataki kujua, mmoja aliwahi kunijibu, ‘Hakimiliki ni Ulaya tu”, japo alikuwa hajui hata hiyo hakimiliki ina beba nini. Namjua mfanya biashara mmoja ambaye moja ya kampeni zake kuu ni kuhakikisha wasanii walio chini yake hawajui Hakimiliki, wala hawahudhurii semina au warsha yoyote ya Hakimiliki. Lakini Hakimiliki ni mali ya mtunzi maisha yake yote na miaka 50 baada ya kifo chake kadri ya Sheria ya Hakimiliki ya Tanzania. Kwa kipindi hicho  Hakimiliki inakulindia haki za kiuchumi, ‘Economic Rights’ ambazo ndizo zinazokupa uwezo wa kupata halali yako kiuchumi kutokana na kazi zako. Katika kila kazi, kwa mfano wimbo, kuna haki zifuatazo; 

i. Kurudufu,
ii.Kusambaza,
iii. Kukodisha,
iv. Kuonyesha hadharani (exhibition),
v. Kutafsiri,
vi.Kutangaza hadharani (Public Performance),
vii. Kurusha katika vyombo vya utangazaji (Broadcasting),
viii Kubadili matumizi,
ix. Njia zozote zile nyingine za utangazaji hadharani (ikiwemo Cable network),
x. kuingiza nakala nchini 

Hali ilivyo mbaya hapa Tanzania, wanamuziki wetu siku hizi hawasambazi, wengi hawana album rasmi, japo wanaweza kuwa na nyimbo zinazotosha album, baada ya kurekodi hutumia kipengele cha vi, na kuweka nyimbo zao kwenye mtandao kama youtube  ili kila anaeutaka anaweza kuutumia bure, hiyo ikidhaniwa kuwa ndio njia bora ya promosheni ya wimbo mpya, wajanja hutumia kipengele cha i. na ii, wanarudufu na kusambaza na kutengeneza pesa bila kuwashirikisha wasanii, kisha wasanii huruhusu kazi zao zitumiwe kwa haki na vii, redio na tv huingiza mabilioni ya fedha kutokana na matangazo, kwa kupiga nyimbo hizo bila kulipa hata senti tano.

 Zikiwemo radio za wale wanaotambulika kuwa ni watu wasafi na wakombozi wa vijana na wanyonge, na hata radio ya Taifa nayo imo katika ufisadi huu. Hatimae tunaona nakala za DVD na CD za wasanii wa Kitanzania zikiingizwa nchini kutoka Uchina na kuuzwa mitaani zikiwa zinavunja kipengele x.

Wasanii wengi wakiona kazi zao zimesambaa hujisifu kuwa ‘Kazi yangu inafanya vizuri’.  Umbumbumbu huu wa hakimiliki unawafanya wasione umuhimu wa mikataba itakayoelekeza matumizi yatakayoleta tija kwenye maisha yao, hivyo baada ya muda msanii anajikuta hata fedha ya nauli kwenda kudai chake hana. Na wengine huona njia ni kuendelea kurekodi, bila kujali kilichokwisha rekodiwa kiliingiza na nini na kusababisha hasara gani.

Masikitiko zaidi ni pale unapokuta msanii yuko katika hali mbaya kimaisha wakati kazi zake bado zinaendelea kuingiza mamilioni kutokana na matangazo katika vyombo vya utangazaji na muhusika wala hajui kuwa anastahili mgao wa pesa inayotokana na jasho lake.

Umoja ni nguvu na kila mtu anajua hivyo, hata wale wanyonyaji wa wasanii wanalijua hilo hivyo kati ya vitu vinavyopigwa vita na wanyonyaji ni umoja wowote wa wasanii. Ukionekana unafanikiwa patapenyezwa rupia ili kuchafua jitihada zozote za kuunda umoja wenye nguvu. Japo wanyonyaji hao wao wamejitengenezea umoja wenye nguvu sana kulinda maslahi yao ya kuwanyonya wasanii.

Katika wizi wa kazi za sanaa kadri unavyokuwa maarufu zaidi ndivyo unavyoibiwa zaidi, ungetegemea kuwa wasanii maarufu ndio wangekuwa wakihakikisha kunakuweko na umoja na pia kuhamasisha ulinzi wa haki zao, hilo ndilo kinyume, nadra sana watu maarufu kuhuduhuria mikutano ya wasanii, labda kama huo mkutano umehamasishwa na wafanyabiashara wanaonyonya wasanii hapo utakuta mkutano una wasanii wote muhimu na mara nyingi mada hapa huwa hazina umakini wa kutoa elimu kwa wahusika.


NI jambo la kusikitisha kusikia mama huyu Bi Cheka ambaye miaka miwili tu iliyopita alikuwa kwenye masikio ya kila mtu anaishi kwenye nyumba ya udongo. Tuombee iwe ni hadithi tu na si kweli kuwa hali ni hiyo, japo haitashangaza kamwe kwa nchi hii iliyojaa ufisadi kila kona.


Stori zaidi: Gladness Mallya na Mayasa Mariwata

DAH MASIKINI! Hivi ndivyo unavyoweza kusema wakati unapomuona msanii wa muziki wa kizazi kipya, Cheka Hija, maarufu kama Bi. Cheka kutoka Kundi la Mkubwa na Wanawe, linaloongozwa na Said Fella ‘Mkubwa’ lenye maskani yake, Temeke jijini Dar es Salaam.

Bi Cheka akiwa nje ya nyumba anayoishi.

Mtoa habari wetu aliwasiliana na gazeti hili na kulieleza kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 55, hivi karibuni alianguka ghafla nyumbani kwake na kukata kauli, wakati alipokuwa akienda chooni kujisaidia.

Wikiendi iliyopita, Amani lilifika nyumbani kwa msanii huyo mzee, anayeishi Bunju B, nje kidogo ya jiji la Dar na kumkuta akiwa na wajukuu zake huku hali yake ikiwa tete tokea alipoanguka Oktoba mwaka huu.

Akiwa anaishi katika kijumba chake kilichojengwa kwa miti na kukandikwa udongo, mtu anayemuona katika luninga akifanya vitu vyake, asingeweza kuamini kama hapo ndipo anapoishi.



Upande wa nyumba yake.

“Ukweli nilikuwa na hali mbaya, afadhali sasa, naongea na kusimama kwani nilikuwa siwezi kutembea, wiki iliyopita alikuja meneja wetu, Yusuf Chambuso na akina Dogo Aslay.

“Jamani maisha yangu kwa sasa ni magumu kwani siwezi kufanya kazi yoyote na sina msaada na kwenye muziki sijaona faida yoyote labda ya nguo tu, kwamba nilizoea kuvaa madela na kanzu sasa nina suruali,” alisema Bi Cheka kwa machungu.


Bi Cheka akiwa na wajukuu zake.

Alisema anasikitishwa na maisha yake kwani kutokana na umaarufu wake, mtaani kwao anaonekana kama mtu mwenye uwezo, wakati siyo kweli kwani anaishi kwenye nyumba ya tembe katikati ya nyumba nzuri.

“Kuhusu malipo makubwa kuwahi kupata ni shilingi laki tatu nilizolipwa kwenye shoo ya Fiesta mwaka juzi, hizo ndizo hela kubwa niliyowahi kupata katika muziki.”Gazeti hili lilimtafuta Fella ambaye alikiri Bi. Cheka kuumwa, akisema anasumbuliwa na magonjwa ya uzee na kwamba ahadi yake ya kumsaidia kujenga nyumba imeishia kwenye mchango wake wa matofari.


...Bi Cheka akiimba na Chege.

“Mimi kama Fella nimesaidia ninapoweza, nimemchangia matofari kidogo, kwa hiyo watanzania wenzangu nao tuungane tumchangie ili aweze kurekebisha kibanda chake,” alisema.

Global Publishers inaanzisha kampeni maalum ya kumsaidia na hivyo inawaomba watanzania kumchangia msanii huyu ili apate nyumba nzuri na matibabu yake. Ili kumsaidia tuma fedha kwenye namba 0654-880707 ambayo itasimamiwa na kampuni.

 Chanzo: INGIA HAPA

Jumapili, Februari 02, 2014

SANAA NA MUZIKI WA INJILI

Mpendwa katika Bwana ni ombi langu kwa Mungu akubariki unaposoma somo hili ili uweze kufahamu mambo ambayo ulikuwa huyajuwi au kukumbuka yale ambayo unayajua lakini ulikuwa umeyasahau. Kipengele hiki kidogo cha somo hili nimekitoa katika makala ninayoandaa na hivyo, ni tamanio la moyo wangu kuwa litaeleweka vizuri kama somo lililokamilika kwa lengo hili na kwa wakati huu. Kama wewe ni mwanamuziki, mwimbaji au tu mdau wa muziki, basi naamini utapata jambo la kujifunza kwa kipindi hiki unaposoma.

Muziki, pasipo kujali unatumikaje, ki taaluma huwa uko katika eneo la Sanaa. Vitu vyote vyema vinatoka kwa Mungu(Yakobo1:17). Tunafahamu kuwa vitu vyote tulivyonavyo chanzo chake ni Mungu mwenyewe na vikitumika vyema, huonyesha sura fulani ya Mungu wetu. Hivyo mwana sayansi mkuu ni Mungu na mwana sanaa mkuu pia ni Mungu mwenyewe. Mungu kama mwana sanaa alipanga vitu vyote katika picha na kama mwana sayansi akatumia sayansi na sanaa kuviumba na kuviweka viwepo hata leo. Naamini kupitia sanaa ya Mungu, ndipo usemi maarufu wa Biblia, “Mungu akaona yakuwa ni vyema” ulirudiwa mara kwa mara katika kitabu cha Mwanzo.

Saana ina uwezo mkubwa sana kuunganisha vyema vitu visivyoonekana wala kusikika na kuvileta katika ulimwengu unaoonekana na kusikika. Mchoraji anaweza kuunganisha mistari na kuonyesha picha ya kitu fulani. Hivyo hivyo, mwana muziki au mwimbaji anaweza kuweka nota na milio tafauti tofauti na kutengeneza wimbo au muziki unaosikika vizuri.

Ni jambo la ajabu sana kuwa neno ‘Msanii’ limetumika vibaya sana katika sehemu hii ya dunia tunayoishi kufikia wasanii kuanza kuchukia kuitwa/kutambulishwa hivyo. Hata hivyo, ingekuwa ajabu pia kwa Ndovu kukataa kuitwa Ndovu kwa kukuta Fisi akiitwa Ndovu. Daktari hawezi kukataa kutambulishwa kama Daktari kama jina Daktari litatumika vibaya. Kwa nini Msanii akatae kuitwa hivyo kwa sababu jina hilo limetumika vibaya? Kwa hivyo, Msanii katika Kanisa lazima ajivunie kuwa Mungu amempa huduma ya kutumia Sanaa hiyo kumtumikia kama vile Injinia anavyoweza kujivunia kutumia taaluma yake ya ujenzi kwa ajili ya kujenga nyumba ya kuabudia Mungu. Mungu ameweka Sanaa ya Muziki ili utaalamu huo utumike kuleta sifa nyumbani mwake. Kwa maana hiyo, ni vyema wana muziki wakajitahidi kukuza taaluma hiyo kwa elimu ya kiroho na ya asili pia inayohusu muziki.

Ki ujumla, sanaa hutumia uwezo wa kuwaza na kufikiria na kutumia (imagination)
kwa upana sana, ambako huleta picha hiyo kuonekana au kusikika. Tofauti na taaluma nyingine, sanaa hutumia ubunifu(creativity) mwingi kwa sababu sheria na kanuni zake hazijabana sana tofauti na sayansi ambayo kanuni zake na mahesabu yake yako ya ki-vipimo zaidi. Hivyo, sanaa ina uwezo wa kubuni mambo mapya sana. Kwa mfano, muziki wa Jazz ulipobuniwa na watu weusi huko Marekani, watu walipinga uhalali wake huku wakisema kuwa kanuni za ki-muziki zimevunjwa. Lakini baada ya muda, muziki wa Jazz uliongezeka umaarufu wake na baadae ukakubalika kuwa muziki halali.

Muziki kama sanaa nyingine hutumia hisia nyingi ili kufikia walengwa.  Kwenye taasisi tatu za mtu, yaani roho, nafsi na mwili ambazo humfanya mwanadamu kuwa mwanadamu, nafsi hutumika kwa asilimia kubwa sana kufanya kazi ili kutengeneza na kuhudumu katika sanaa. Katika nafsi, kitengo cha hisia ndicho kinachofanya kazi kubwa ya ziada kufanya sanaa,(sisi hapa tukihusika na muziki.) Kwa hivyo tunapoenda kuongea muziki moja kwa moja, tunafahamu kuwa mambo mengi yanayowaathiri wana muziki na waimbaji, basi yanaathiri wana sanaa kwa ujumla wake.

Naamini kuwa wote tunakubaliana kuwa wanamuziki na waimbaji ni watu wa hisia nyingi. Ndivyo Mungu alivyowaweka duniani ili watumike kufariji, kufurahisha na kuonyesha huzuni ili kuhudumia jamii. Kwa sababu ya hisia nyingi zinazotumika katika muziki, wakati mwingine, ni rahisi kwa wanamuziki na waimbaji hawa kukosa mwelekeo, mizani na vipimo(balance), wingi au upungufu wa hisia unapotokea. Jinsi ya kujitunza ki-hisia, basi, huwa ni jambo la muhimu sana, jambo ambalo wengi wao hawajui, ili wasije wakafanyika kituko badala ya suluhisho katika jamii.

Kupitia hisia kuwa na sehemu kubwa ya mchango katika maisha ya mwanamuziki na mwimbaji, itaonekana jinsi ya kuvaa na staili zake za maisha kwa ujumla zilivyo tofauti sana na za watu wengine katika jamii. Hapa, hatuwezi kuwaambia wabadilike wasiwe hivyo, maana mara nyingi hicho huwa ni kitambulisho cha taaluma yao, ila wanahitaji tu kudumisha kiasi tu, ili wasipitilize, na pia wasifanye kwa kuiga.

Sasa, mtu yeyote anayetoa huduma katika jamii, lazima ajifundishe kurudisha katika maisha yake kile kinachotoka anapohudumia jamii ile. Kwa mfano, mwana riadha anahitaji ale chakula kizuri, apumzike, ajiweke vizuri ki saikolojia ili asihudumie jamii na baadae maisha yake yakaharibika. Anapofanya mazoezi na hatimae kushindana, anahitaji ajue ni chakula gani cha kutumia ili arudishe nguvu na kadhalika. Mtumishi wa kiroho, kama mchungaji anahitaji aombe na kuabudu Mungu, asome neno na kuwa na ushirika mzuri na pia kupumzika ili arudishe nguvu anazotumia katika huduma yake. Vile vile, mwanamuziki na mwimbaji wa nyimbo za injili  lazima ajue jinsi ya kurudisha nguvu anayotumia ikiwemo ya ki hisia ili aweze kuhudumu bila maisha yake mwenyewe kuharibika.

Huduma ya muziki na uimbaji ina shamrashamra nyingi, makelele mengi na kuhudumia mbele ya umati au watu wengi. Ni rahisi jambo hili likaingia vibaya katika akili ya mwimbaji au mwanamuziki huyo na kuanza kuishi katika ‘ulimwengu’ usiyo halisi. Ile kushangiliwa na muonekano wa kugusa umati au watu wengi unaweza ukaweka picha isio ya halisi katika maisha ya mtu huyo na akaanza kuishi maisha tu ya juu juu. Ikumbukwe kuwa mwanamuziki na mwimbaji wa nyimbo za Injili ni mwanadamu na hivyo ana mapito yake katika maisha. Tafakari sasa kuwa amekuwa na wakati mbaya katika maisha yake na sasa ana huzuni lakini hapo hapo anatakiwa kusimama mbele za watu na kuwafurahisha au kuwatia moyo. Anatakiwa hapo hapo atumie hisia yake kuwafurahisha watu wakati yeye mwenyewe ki-hisia yuko chini. Pasipo Mungu kuwa naye na kumsaidia katika huduma yake, hali hii inapotokea mara kwa mara, inaweza ikamchanganya ki-hisia.  

Kwa sababu ya umuhimu wa hisia katika maisha ya mwanadamu yeyote, hisia zinapochanganyikiwa, mwanadamu hujikuta katika ulimwengu usiyo halisi na  kuwa kituko katika jamii, huku yeye akiona kuwa yuko sawa.

Kwa nini Neno ‘Msanii’ limetumika vibaya?

Kwa nini neno Msanii limetumika kuonyesha utovu wa maadili? Ningependa (nikiwa na uchungu mwingi moyoni) kuangalia sababu ya jina Msanii kutumika kuonyesha sifa mbaya katika jamii. Hili linaniumiza kwa sababu na mimi nina taaluma ya sanaa. Imekuwa tabia ya watu wengi katika sehemu hii ya ulimwengu tunayoishi kutumia neno hili kuonyesha mtu tapeli, muongo asiyeeleweka na kadhalika.

Sifa ya sanaa ni kuonyesha picha ya kitu kilichopo au ambayo msanii anataka  kuitengeneza ili ionekana kama wazo katika jamii. Kwa mfano, msanii mwimbaji anaweza kutumia sanaa kukuonyesha mambo yaliyopo katika jamii. Anaweza kuimba wimbo wenye hadithi ya fulani hata kama sio picha halisi ya maisha yake. Anaweza kuimba wimbo kuwa anataka kuolewa na kupata watoto wengi hata kama ki halisi hataki hata mtoto mmoja. Mwimbaji anaweza kukupa picha ya maisha ukafikiri kuwa ndivyo alivyo, kumbe sivyo hivyo. Kupitia hili, Msanii ameonekana kama kuwa mwongo fulani hivi. Ameonekana kama mtu anayeweza kuichora picha yoyote  na kujionyesha mtu ambaye siye katika jamii.

Muziki umetumika kujibizana na hata kugombana na kutukanana, mwimbaji mmoja na mwingine. Mambo ambayo yameleta picha ya sanaa kutumika kuwa chombo cha (kumfagilia) kumsafishia jina msanii husika. Kwa sababu ya nguvu ya sanaa, wasanii wengi wameitumia kwa faida binafsi kujitengenezea nafasi katika jamii, badala ya kuihudumia jamii ile.

Kwa sababu hapa tunaangalia sanaa ya muziki katika nyumba ya Mungu, ni vyema tutoe tahadhari kuwa Muziki wa Mungu unatakiwa kumtukuza Yeye, kuhudumia kundi lake na kusaidia kuleta wengi katika kundi hilo. Muziki na vipawa vyote katika nyumba ya Mungu vinatakiwa kutumika kwa utukufu wa Mungu na hivyo sio kwa ubinafsi. Kwa sababu hiyo wana muziki katika nyumba ya Mungu wasiwe kama wa dunia ambao wanaimba nyimbo kuhamasisha jamii kuhusu jambo moja huku wao wakifanya kinyume. Mwanamuziki au muimbaji wa Mungu asiimbe kuwa yeye anapenda kuomba wakati sio kweli maana hapo ndipo atakapoonekana na watu kuwa ‘Msanii’ kwa kinyume cha matumizi ya jina hilo. Hili limeonekana kwa watu wengi wanaoimba nyimbo za injili na za kusifu na kuabudu kuwa wanachoimba na wanachofanya ni vitu viwili tofauti. Mungu asaidie ili neno hili linapotumika kinyume duniani, katika nyumba ya Mungu, Msanii awe ni chombo cha heshima cha kumtukuza Mungu na si vinginevyo.

Jambo lingine ambalo hufanya neno ‘Msanii’ kutumika vibaya ni kwa sababu ya kitu ambacho nimegusia awali kuwa, wengi wao huchanganyikiwa kwa kuzidiwa na msongamano wa hisia katika maisha yao na hivyo kuonekana kuishi maisha yasio halisi, na hivyo mtu yeyote anayeonekana kudhihirisha aina hii ya maisha hufananishwa na wasanii waliofanyika hivyo. Hivyo huonekana kama vile ndio maisha ya wasanii kuishi katika maisha ambayo sio ya kawaida na watu wengine, kwa kuvaa kwao labda na hali zingine ambazo huonekana maishani mwao. Wanamuziki na waimbaji wanaohudumu katika nyumba ya Mungu wanatakiwa kuonyesha mfano katika maisha yao ili waonekane kuwa ni wahudumu zaidi kuliko tu kuonekana kuwa ni waimbaji, kwani vipawa vyao vinatakiwa kudhihirisha tabia fulani ya Mungu.Njia ya kufuta dhana hii katika waimbaji na wanamuziki walio katika nyumba ya Mungu ni kushinda majaribu ambayo huwalenga na kuishi kwa Imani zaidi kuliko ki hisia, kwani, Biblia inasema tunaishi kwa Imani na sio kwa yale tunayoyaona na kuyahisi. Kwa hivyo wajenge nguvu ya kiroho katika maisha yao na waongozwe na Roho Mtakatifu.

Jambo jingine ni kuomba uongozi wa Mungu kwa Roho Mtakatifu ili nyimbo zao ziwe zinatokana na njaa na kiu ya Mungu na haki yake katika maisha yao, ili wasije wakaimba nyimbo ambazo wanawaelekeza watu wafanye yale ambayo wenyewe hawayafuati.

La mwisho, katika somo hili, ni kuomba kipawa chao kiambatane na neema iliyo juu ya maisha yao ili kipawa kisiwapeleke juu zaidi kuliko neema inayoweza kuwalinda katika kiwango  hicho. Pia waweze kuwa na afahamu wa kujua milango inayofunguka kwao, kama ni  Mungu aliyefungua au ni wanadamu maana mara nyingi hapo ndipo watu hupandishwa  na kujikuta mahali ambapo hakuna neema ya kumlinda mtu katika kiwango alichopandishwa. Hivyo wawe pia na ujasiri wa kufuata tu njia ambayo Mungu anatengeneza.

Muziki una nguvu yake wenyewe.Ni jambo la muhimu kujua kuwa Muziki kama Muziki una nguvu ya ajabu sana, ukiachilia mbali kuwa unaweza kuubeba upako. Kwa maana nyingine, muziki una uwezo ndani yake wa kujitegemea bila kujali ni nani anayeutumia. Muziki una nguvu kwa sababu ya asili ya ulivyoumbwa. Kama chombo cha mawasiliano, kuna uwezo ndani ya muziki ambao husaidia kuleta ujumbe katika jamii lengwa. Labda kwa sababu hii, ndio maana huduma ya muziki na uimbaji imebeba umuhimu mkubwa sana nyumbani mwa Mungu. Inawezekana umuhimu mkubwa ni ukubwa wa muziki wenyewe na sio tu kutokana na wana muziki na waimbaji wenyewe. Kwa sababu hii, watu walio katika huduma hii wanaweza kujibebea heshima kubwa bila kujua kuwa chombo chenyewe ndicho muhimu kuliko wenyewe.
Muziki ni chombo cha muhimu sana katika uumbaji wa Mungu kwa hiyo kinabeba nguvu nyingi sana na hivyo kinatumika kwa ajili ya kuleta mabadiliko makubwa sana katika uumbaji mwingine wa Mungu. Kipawa cha muziki, basi, kina uwezo wa kumuonyesha mwanamuziki na muimbaji katika hali fulani ambayo asipojiangalia, anaweza akajitafsiri katika hali ambayo sio halisi katika maisha yake. Anaweza kujisifu na kujiona yuko katika kiwango fulani cha ki-maisha ambacho sio halisi katika maisha yake, kumbe tu ni kwa sababu ya nguvu iliyo katika muziki wenyewe. Hata hivyo, nguvu ya muziki iko sana katika kugusa hisia za nafsi, na hivyo kutegemea nguvu ya kiroho kuleta mguso katika maisha ya kiroho. Katika muziki, maisha ya watu wanaohudumiwa, wanaweza kuguswa katika kiwango cha ki-hisia tu au, wakaguswa katika kiwango kingine, wakafikiwa katika maisha ya kiroho.

Sasa hapa ndipo tunapogundua umuhimu wa kipawa au talanta ya muziki kushukiwa na kipawa au karama ya kiroho. Wako wanamuziki wengi wa duniani kwa kujua hili wanatafuta nguvu za giza kwa kwenda kwa waganga/wachawi au hata kutafuta kuabudu mashetani ili wawe na mguso wa kiroho. Sisi tulio katika nyumba ya Mungu tunatafuta kwa Mungu uwezo na vipawa vya kiroho ili karama ishuke juu ya talanta na hivyo kugusa, sio tu nafsi na hisia zake bali roho ya mtu au maisha yake ya kiroho. Kipawa cha kimwili(talanta/kipaji) hakiwezi kugusa rohoni. Kipawa cha kiroho(karama) hugusa rohoni. Kwa hivyo vyote ni muhimu, ila tunajua kuwa vitu vya kimwili ni vya muda na vya kiroho ni vya kudumu.

Kuna mifano mingi katika Biblia ambayo inaonyesha talanta za ki-muziki ambazo zilishukiwa na karama za rohoni. Tunafahamu hadithi ya Daudi katika 1Samueli 16:23 “Ikawa ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa na, na ile roho mbaya ikamwacha.” Hapa kuna ufunuo mwingi sana. Kwanza, muziki ulimburudisha Sauli, kama vile tulivyoona hapo juu kuwa muziki una nguvu wenyewe na la pili, Sauli aliondokewa na roho mbaya, ambayo ni kipawa au karama ya kiroho ambayo ilifanya kazi hiyo. Pia kuna wazo hilo la ‘roho mbaya kutoka kwa Mungu’ ambapo watumishi wengi hutafsiri kuwa ni roho iliyoruhusiwa na sio kuwa ilitoka kwa Mungu wakisema kuwa Mungu hana roho mbaya. Wengine pia husema ni aina ya roho ya ghadhabu ambayo inatafsirika kuwa ni mbaya. Hata hivyo la muhimu kujua hapa ni kwamba ukombozi ulitokea kwa Sauli wakati Daudi alipopiga muziki.

Andiko jingine ni pale Nabii Elisha alipohitaji mwanamuziki katika 1Wafalme 3:14-15. “Elisha akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe. Ila, sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga mkono wa Bwana ukamjia juu yake. Akasema, Bwana asema hivi……..” Hapa, kuna hadithi ya nabii ambaye amekwazika kumuona adui ambaye alikuwa mfalme muovu. Lakini kwa ajili ya Yehoshefati, Elisha akaheshimu uwepo wake na akaomba mwanamuziki ambaye alipopiga muziki ule, upako ukaja juu ya Elisha na akatabiri. Hapa tunaona talanta/kipaji ya muziki ikishukiwa na karama ya unabii ambayo ilifanya kazi juu ya nabii Elisha. Kwanza nguvu ya muziki ilimuondolea Elisha kukwazika kwa kumfurahisha na pili, karama ya unabii ilichochewa na karama iliyokuwa juu ya mwanamuziki yule.

Na mwisho, kwa sasa katika mifano, tunaona katika 1Mambo ya Nyakati 25, mara kwa mara ikisemekana kuwa wana muziki waliochaguliwa na mfalme Daudi na viongozi wa kiserikali walipewa kazi ya kutabiri kupitia muziki, katika msari wa 2, “…..walioamriwa na Asafu aliyetabiri kwa amri ya mfalme” na mstari wa 3, “…..watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu Bwana.” Wana muziki na waimbaji wanatakiwa kuheshimu kuwa Mungu amewapa talanta za kumtumikia Yeye, lakini pia watafute karama za Roho Mtakatifu ili wanapogusa watu wa Mungu, basi iwe katika maisha yao yote kwa ujumla.

Ninaamini kuwa Mungu amekupa kitu chema cha kukusaidia ili uweze kutoa mchango wako katika huduma hii kwa ajili ya kuiboresha.

Jumanne, Novemba 19, 2013

Namna Sinema Zinavyotengenezwa



KATIKA miongo kadhaa iliyopita sinema nyingi zenye mafanikio zimetokezwa huko Hollywood. Hilo limekuwa na uvutano mkubwa ulimwenguni pote kwani sinema nyingi za Marekani hutazamwa katika nchi nyingine majuma machache au hata siku chache tu baada ya kuonyeshwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani. Sinema fulani hata zimeonyeshwa kwa mara ya kwanza tarehe ileile duniani kote. Dan Fellman, rais wa usambazaji wa filamu nchini Marekani wa shirika la Warner Brothers anasema hivi: “Soko la ulimwenguni kote la uuzaji wa sinema linazidi kukua nalo linasisimua sana, kwa hiyo tunapotengeneza sinema, huwa tunaitengeneza kwa ajili ya soko la ulimwenguni kote.” Sasa kuliko wakati mwingine wowote, kile kinachotendeka huko Hollywood huathiri biashara ya sinema ulimwenguni. 

Lakini kupata faida kutokana na sinema si rahisi kama unavyowazia. Sinema nyingi zinahitaji zaidi ya dola milioni 100 ili kulipia gharama ya kuzitengeneza na kuziuza. Na kufanikiwa kwake kunategemea watazamaji ambao mtu hawezi kutabiri watapendezwa na nini. David Cook, profesa wa masomo ya sinema katika Chuo Kikuu cha Emory anasema hivi: “Huwezi kujua ni lini jambo fulani litawavutia au kuwasisimua watazamaji.” Kwa hiyo watengenezaji wa sinema huongezaje uwezekano wa sinema yao kufanikiwa? Ili kupata jibu, tunahitaji kuelewa mambo machache ya msingi yanayohusika katika utengenezaji wa sinema.

Matayarisho Yanayofanywa Kabla ya Kutengeneza Sinema

Mara nyingi, matayarisho yanayofanywa kabla ya upigaji picha ndiyo sehemu muhimu zaidi ambayo huchukua muda mrefu katika utengenezaji wa sinema. Kama tu ilivyo na mradi wowote mkubwa, mafanikio yake hutegemea sana matayarisho. Inatumainiwa kwamba pesa zozote zinazotumiwa wakati wa matayarisho zitapunguza sana gharama za kutengeneza sinema yenyewe.

Kutengenezwa kwa sinema huanza na hadithi fulani ambayo huenda ikabuniwa au ikategemea matukio halisi. Mwandikaji huandika hadithi hiyo kwenye hati. Hati hiyo inaweza kufanyiwa marekebisho mengi kabla ya hati ya mwisho kutokezwa. Hati hiyo ya mwisho huwa na wahusika pamoja na maelezo mafupi kuhusu kitendo kitakachofanywa. Pia hati hiyo hutoa maagizo mengine kama vile mahali ambapo kamera zitakuwa na mabadiliko yatakayofanywa katika kila onyesho.

Hata hivyo, hati hiyo inapokuwa katika hatua za kwanza, mtayarishaji atakayeinunua huanza kutafutwa. Mtayarishaji anaweza kupendezwa na hati ya aina gani? Kwa kawaida sinema ambayo hutolewa msimu wa kiangazi hukusudiwa iwavutie vijana wa kati ya miaka 13 hadi 25 hivi. Kwa hiyo mtayarishaji atapendezwa hasa na sinema ambayo itawavutia vijana.

Hati inayofaa hata zaidi ni ile itakayowavutia watu wa umri mbalimbali. Kwa mfano, bila shaka sinema inayotegemea shujaa anayetajwa katika vitabu vya vibonzo itawavutia watoto wadogo ambao wanamfahamu shujaa huyo. Na bila shaka wazazi wao wataambatana nao kuitazama sinema hiyo. Lakini watengenezaji wa sinema huwavutiaje vijana walio na umri wa kati ya miaka 13 na 25 hivi? Katika gazeti The Washington Post Magazine, Liza Mundy anasema kwamba “habari inayosisimua” ndiyo jambo muhimu. Ili sinema “ilete faida kubwa na kuwavutia watu wa umri mbalimbali bila kupuuza yeyote,” lugha chafu, jeuri nyingi, na picha nyingi za ngono hutiwa ndani.

Mtayarishaji akiona kwamba hati inaweza kuwa sinema nzuri, huenda akainunua na kumpa kandarasi mwelekezi na mwigizaji maarufu. Kuwa na mwelekezi na mwigizaji maarufu kutafanya sinema hiyo ivutie sana wakati itakapotolewa. Hata katika hatua hii ya kwanza, waelekezi na waigizaji maarufu wanaweza kuwavutia wawekezaji wanaohitajika ili kugharimia utayarishaji wa sinema hiyo.

Hatua nyingine ya matayarisho ni kuchora vibonzo mbalimbali vya filamu hiyo hasa vile vinavyohusisha mapigano. Michoro hiyo humwongoza mpiga-picha za sinema nayo husaidia kupunguza wakati unaotumiwa kupiga picha. Mwelekezi aliye pia mwandikaji wa hati, Frank Darabont, anasema: “Hakuna jambo baya zaidi kama kupoteza wakati wa kupiga picha kwa sababu tu ya kutojua mahali ambapo kamera inapaswa kuwa.”

Kuna mambo mengine mengi muhimu yanayopaswa kushughulikiwa wakati wa matayarisho. Kwa mfano, picha zitapigiwa wapi? Je, itakuwa lazima kusafiri? Je, kuna picha zitakazopigwa ndani ya nyumba, nayo itapambwaje? Je, mavazi maalumu yatahitajika? Ni nani atakayeshughulikia mwangaza, kupamba na kutengeneza nywele za waigizaji? Na vipi kuhusu sauti, madoido, na yule atakayeigiza sehemu hatari badala ya mwigizaji mkuu? Hayo ni baadhi ya mambo yanayohitaji kufikiriwa hata kabla ya kupiga picha za filamu. Ukitazama majina yanayoonyeshwa mwishoni mwa sinema inayotazamiwa kuleta faida kubwa, huenda ukaona kwamba mamia ya watu walihusika kuitayarisha! Fundi mmoja wa mitambo ambaye amehusika katika kutengeneza sinema nyingi anasema kwamba “watu wengi sana huhusika katika kutengeneza filamu nzuri.”

Kutengeneza Sinema Yenyewe

Kupiga picha za sinema kunaweza kuchukua wakati mwingi, kunaweza kuchosha, na pia kunaweza kugharimu pesa nyingi. Kwa kweli, kupoteza dakika moja tu kunaweza kugharimu maelfu ya dola. Nyakati nyingine inabidi waigizaji, wafanyakazi, na vifaa visafirishwe hadi sehemu ya mbali. Hata hivyo, haidhuru picha hizo zitapigiwa wapi, lazima pesa nyingi sana zitatumika kila siku.

Watu wanaoshughulikia mwangaza, wale watakaowapamba na kuwatengeneza nywele waigizaji huwa kati ya watu wa kwanza kufika mahali ambapo picha zitapigiwa. Kila siku ya kupiga picha, waigizaji wakuu hupambwa kwa saa kadhaa. Kisha picha hupigwa kwa siku nzima.

Mwelekezi husimamia kwa uangalifu kupigwa picha kwa kila onyesho. Inaweza kuchukua siku nzima kupiga picha za onyesho fupi sana. Picha za maonyesho mengi katika sinema hupigwa kwa kutumia kamera moja, kwa hiyo, onyesho moja linaweza kupigwa picha kadhaa kutoka pembe tofauti-tofauti. Isitoshe, huenda onyesho lilelile likapigwa picha mara kadhaa ili kupata picha bora zaidi au kurekebisha tatizo la kiufundi. Ikiwa onyesho ni refu, huenda picha 50 au zaidi zikapigwa! Kwa kawaida, mwishoni mwa kila siku, mwelekezi huchunguza picha zote na kuamua ni zipi zitakazotumiwa. Kazi ya kupiga picha inaweza kuchukua majuma au hata miezi kadhaa.

Hatua ya Kuunganisha Sinema Iliyotengenezwa

Katika hatua hii, picha zilizopigwa huboreshwa na kupangwa zinavyopaswa kufuatana. Kwanza, muziki utakaotumiwa huambatanishwa na sinema hiyo. Kisha, mhariri huunganisha sehemu za sinema hiyo na kufanyiza nakala ya kwanza isiyo kamili.

Madoido ya sauti na picha pia huongezwa katika hatua hiyo. Nyakati nyingine kompyuta hutumiwa kutia madoido hayo katika hatua hii ambayo ni mojawapo ya sehemu ngumu zaidi za utengenezaji wa filamu. Kazi inayofanywa katika hatua hii inaweza kuifanya sinema ivutie na ionekane kuwa halisi.

Muziki uliotungwa hasa kwa ajili ya sinema hiyo huongezwa katika hatua hiyo, na jambo hilo ni muhimu katika filamu za leo. Edwin Black anaandika hivi katika gazeti Film Score Monthly: “Sasa watengenezaji wa sinema hutaka muziki uliotungwa hasa kwa ajili ya sinema, nao hawataki muziki wa dakika ishirini tu au vipindi vifupi vya muziki, bali wao hutaka muziki utakaochezwa kwa muda unaozidi saa nzima.”

Nyakati nyingine filamu iliyoboreshwa huonyeshwa watu wachache ambao wanaweza kutia ndani rafiki za mwelekezi au wafanyakazi wenzake ambao hawakuhusika katika kutengeneza filamu hiyo. Ikitegemea jinsi watakavyoitikia, mwelekezi anaweza kupiga picha upya maonyesho fulani au kuyaondoa kabisa. Katika visa fulani, umalizio wote wa filamu ulibadilishwa kwa sababu watu walioitazama kwanza hawakuupenda.

Hatimaye, filamu iliyokamilika huonyeshwa kwenye majumba ya sinema. Ni wakati huo tu ndipo inaweza kujulikana ikiwa sinema hiyo itafanikiwa au haitafanikiwa, au itakuwa ya wastani. Lakini mambo mengi yanahusika kuliko kupata faida. Sinema kadhaa zikikosa kufanikiwa zinaweza kuharibu sifa ya mwelekezi na matarajio ya mwigizaji kupata kazi. Anapofikiria miaka yake ya mapema ya kutengeneza filamu, mwelekezi John Boorman anasema hivi: “Niliwaona waelekezi wenzangu wakikosa kandarasi baada ya sinema kadhaa walizoelekeza kukosa kufanikiwa. Ukweli wenye kusikitisha ni kwamba katika biashara ya kutengeneza sinema, usipowaletea faida mabwana zako, unapoteza kazi yako.”

Bila shaka, watu wanapotazama ubao wa kutangazia sinema, kwa ujumla hawafikirii ikiwa watengenezaji wa sinema hiyo watapoteza kazi zao au la. Yaelekea wao huhangaikia mambo kama: ‘Je, nitafurahia sinema hii? Je, inafaa nitumie pesa zangu ili kuitazama? Je, sinema hii itanivutia au itanichukiza? Je, inawafaa watoto wangu?’ Unaweza kujibuje maswali hayo unapoamua sinema utakazotazama?

[Maelezo ya Chini]

Anita Elberse, ambaye ni profesa wa Chuo cha Biashara cha Harvard, anasema kwamba “ingawa mara nyingi pesa zinazopatikana kutokana na mauzo ya sinema katika nchi za ng’ambo ni nyingi kuliko zile za mauzo nchini Marekani, jinsi watu wanavyoipokea sinema nchini Marekani huamua jinsi itakavyopokelewa katika nchi nyingine.”

Ingawa huenda njia ambazo hutumiwa kutengeneza sinema zikatofautiana, mambo yanayoelezwa hapa yanaonyesha njia moja inayoweza kutumiwa.

Nyakati nyingine mtayarishaji hupewa muhtasari wa hadithi badala ya hati yenyewe. Ikiwa atavutiwa na hadithi hiyo, anaweza kununua haki za kuimiliki na kuitengeneza kuwa hati.

“Huwezi kujua ni lini jambo fulani litawavutia au kuwasisimua watazamaji.”—David Cook, profesa wa masomo ya sinema

JINSI YA KUFANYA SINEMA IVUTIE NA ILETE FAIDA KUBWA

  Sinema imekamilishwa. Iko tayari kutazamwa na mamilioni ya watu. Je, itafanikiwa? Fikiria njia mbalimbali ambazo watengenezaji wa sinema hutumia ili sinema yao ivutie na ilete faida kubwa.

UVUMI: Mojawapo ya njia zenye mafanikio za kuwafanya watu wawe na hamu ya kutazama sinema fulani ni kupitia uvumi. Nyakati nyingine uvumi kuhusu sinema fulani huanza miezi kadhaa kabla ya sinema hiyo kuonyeshwa kwa umma. Huenda ikatangazwa kwamba kutakuwa na sinema itakayokuwa mwendelezo wa sinema fulani iliyofanikiwa hapo awali. Je, itakuwa na waigizaji walewale maarufu wa sinema ya awali? Je, itakuwa nzuri (au mbaya) kama ile ya kwanza?

  Katika visa fulani, uvumi huanzishwa kuhusu jambo fulani katika sinema, labda kuonyesha picha za ngono waziwazi katika sinema itakayotazamwa na watu wote. Je, sinema hiyo ni mbaya sana? Je, sinema hiyo imepita mipaka kabisa? Watengenezaji wa sinema hunufaika watu wanapotoa maoni mbalimbali yanayopingana kuihusu, kwa kuwa hiyo ni njia moja ya kuitangaza bila malipo. Nyakati nyingine mijadala hiyo huwafanya watu wengi waitazame sinema hiyo inapoonyeshwa kwa mara ya kwanza.

VYOMBO VYA HABARI: Njia za kawaida za kutangaza sinema zinatia ndani mabango, matangazo ya magazeti, matangazo ya biashara ya televisheni, kuonyeshwa kwa sehemu ndogo ya sinema hizo katika majumba ya sinema kabla ya sinema nyingine, na kasheshe. Sasa Intaneti imekuwa njia kuu ya kutangaza sinema.

KUUZA BIDHAA: Kuuza bidhaa zinazotangaza sinema fulani kunaweza kuifanya ivutie inapotolewa. Kwa mfano, sinema moja iliyotegemea shujaa anayetajwa katika kitabu fulani cha kibonzo ilitangazwa katika vifaa vya kubebea vyakula, vikombe, vito, mavazi, minyororo ya funguo, saa, taa, na michezo ya dama, na kadhalika. Joe Sisto anaandika hivi katika jarida la vitumbuizo la Shirika la Mawakili la Marekani: “Kwa kawaida, asilimia 40 ya bidhaa za kutangaza sinema huwa zimeuzwa hata kabla ya sinema hiyo kutolewa.”

KANDA ZA VIDEO: Sinema ambayo haileti faida kubwa inapoonyeshwa katika majumba ya sinema inaweza kuleta faida inaporekodiwa katika kanda za video. Bruce Nash, ambaye huchunguza faida zinazotokana na sinema anasema kwamba “kanda za video huchangia asilimia 40 hadi 50 ya mapato ya sinema.”

VIWANGO VYA SINEMA: Watengenezaji wa sinema wamejifunza kutumia viwango vinavyowekwa vya sinema ili kujifaidi. Kwa mfano, huenda mambo fulani yakaingizwa kimakusudi katika sinema ili kuifanya iwekewe kiwango cha juu zaidi kinachowafaa watu wazima pekee. Kwa upande mwingine, sehemu chache zinaweza kuondolewa ili sinema isipewe kiwango cha watu wazima na kuifanya iwavutie vijana. Liza Mundy anaandika katika gazeti The Washington Post Magazine kwamba kuwekea sinema kiwango cha vijana “kumekuwa njia ya kutangaza sinema: Majumba ya kurekodia sinema hutumia kiwango hicho kupitisha ujumbe kwa vijana na watoto wanaotamani sana kuwa vijana kwamba sinema hiyo itakuwa yenye kuvutia sana.” Mundy anasema kwamba kiwango hicho “hutokeza uvutano kati ya mzazi na mtoto kwani humwonya mzazi na kumvutia mtoto.”

JINSI SINEMA ZINAVYOTENGENEZWA

HATI
MICHORO
MAVAZI
KUPAMBWA
UPIGAJI PICHA
KUTIA MADOIDO
KUREKODI MUZIKI
KUINGIZA SAUTI
KUTENGENEZA VIBONZO KWA KUTUMIA KOMPYUTA
KUBORESHA NA KUPANGA PICHA

Alhamisi, Septemba 27, 2012

TUNAKUZA VIPAJI

Huyu ndiye mwalimu wa muziki katika OMEGA POINT MUSIC ACADEMY iliyopo USHINDI SDA CHURCH.

Hapa ilikuwa ni katika tukio moja hivi.

Calvin mwenye nguo nyeusi kuanzia shati hadi suruali aliyepo nyuma ya pianist akirekebisha mitambo Ushindi SDA Church. Calvin ni rubani wa ndege na hivi sasa yupo kwa Obama anaongeza maujuzi mwanawane .


Huyu mtoto ni kivutia cha wengi kutokana na uwezo wake wa kucheza Piano, ilimchukua muda mfupi sana kuanza kupiga Piano huku akisoma Staff Notation.






Mdada kwa nyuma alikuwa akiimba wimbo uliokuwa ukichezwa na bwana mdogo hapo kwa Piano.


Huyu ndie mkufunzi mwenyewe wa Muziki.


 Mwalimu Heri akitoa maelekezo kwa mwanafunzi





Hapa alipewa paper ngumu, akajiuliza hivi nitaweza kweli kuupiga huu wimbo? Ulimchanganya lakini baada ya kutulia kidogo na kuungalia kwa makini akaanza na akaweza aisee...!!

 Mwalimu Heri akikagua mwanafunzi anachofanya ili kujiridhisha kuwa kaelewa ama anaweza? Ulikuwa ni wimbo mgumu sana.

Hapa anamfunulia ukurasa mwingine ili  kumpima uwezo wake

Dogo hapa kaiva, anapiga piano na kusoma Staff Notation.




Watoto wanaojifunza muziki wakiangalia kwa makini wakati mwalimu Heri akitoa maelekezo.

Hapo je!!


Muziki damuni.

Staff Notation ni moja ya changamoto kwa waimbaji, waalimu na hata wacheza vyombo vya muziki.





UTAPENDA MWANAO AMA WEWE MWENYEWE UJIFUNZE MUZIKI? 
WASILIANA NA MWALIMU HERI KAALE KWA NAMBA HIZI ZIFUATAZO:

+255 713 381883
+255 688 984 442
+255 757 336 090