Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Novemba 19, 2013

Namna Sinema ZinavyotengenezwaKATIKA miongo kadhaa iliyopita sinema nyingi zenye mafanikio zimetokezwa huko Hollywood. Hilo limekuwa na uvutano mkubwa ulimwenguni pote kwani sinema nyingi za Marekani hutazamwa katika nchi nyingine majuma machache au hata siku chache tu baada ya kuonyeshwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani. Sinema fulani hata zimeonyeshwa kwa mara ya kwanza tarehe ileile duniani kote. Dan Fellman, rais wa usambazaji wa filamu nchini Marekani wa shirika la Warner Brothers anasema hivi: “Soko la ulimwenguni kote la uuzaji wa sinema linazidi kukua nalo linasisimua sana, kwa hiyo tunapotengeneza sinema, huwa tunaitengeneza kwa ajili ya soko la ulimwenguni kote.” Sasa kuliko wakati mwingine wowote, kile kinachotendeka huko Hollywood huathiri biashara ya sinema ulimwenguni. 

Lakini kupata faida kutokana na sinema si rahisi kama unavyowazia. Sinema nyingi zinahitaji zaidi ya dola milioni 100 ili kulipia gharama ya kuzitengeneza na kuziuza. Na kufanikiwa kwake kunategemea watazamaji ambao mtu hawezi kutabiri watapendezwa na nini. David Cook, profesa wa masomo ya sinema katika Chuo Kikuu cha Emory anasema hivi: “Huwezi kujua ni lini jambo fulani litawavutia au kuwasisimua watazamaji.” Kwa hiyo watengenezaji wa sinema huongezaje uwezekano wa sinema yao kufanikiwa? Ili kupata jibu, tunahitaji kuelewa mambo machache ya msingi yanayohusika katika utengenezaji wa sinema.

Matayarisho Yanayofanywa Kabla ya Kutengeneza Sinema

Mara nyingi, matayarisho yanayofanywa kabla ya upigaji picha ndiyo sehemu muhimu zaidi ambayo huchukua muda mrefu katika utengenezaji wa sinema. Kama tu ilivyo na mradi wowote mkubwa, mafanikio yake hutegemea sana matayarisho. Inatumainiwa kwamba pesa zozote zinazotumiwa wakati wa matayarisho zitapunguza sana gharama za kutengeneza sinema yenyewe.

Kutengenezwa kwa sinema huanza na hadithi fulani ambayo huenda ikabuniwa au ikategemea matukio halisi. Mwandikaji huandika hadithi hiyo kwenye hati. Hati hiyo inaweza kufanyiwa marekebisho mengi kabla ya hati ya mwisho kutokezwa. Hati hiyo ya mwisho huwa na wahusika pamoja na maelezo mafupi kuhusu kitendo kitakachofanywa. Pia hati hiyo hutoa maagizo mengine kama vile mahali ambapo kamera zitakuwa na mabadiliko yatakayofanywa katika kila onyesho.

Hata hivyo, hati hiyo inapokuwa katika hatua za kwanza, mtayarishaji atakayeinunua huanza kutafutwa. Mtayarishaji anaweza kupendezwa na hati ya aina gani? Kwa kawaida sinema ambayo hutolewa msimu wa kiangazi hukusudiwa iwavutie vijana wa kati ya miaka 13 hadi 25 hivi. Kwa hiyo mtayarishaji atapendezwa hasa na sinema ambayo itawavutia vijana.

Hati inayofaa hata zaidi ni ile itakayowavutia watu wa umri mbalimbali. Kwa mfano, bila shaka sinema inayotegemea shujaa anayetajwa katika vitabu vya vibonzo itawavutia watoto wadogo ambao wanamfahamu shujaa huyo. Na bila shaka wazazi wao wataambatana nao kuitazama sinema hiyo. Lakini watengenezaji wa sinema huwavutiaje vijana walio na umri wa kati ya miaka 13 na 25 hivi? Katika gazeti The Washington Post Magazine, Liza Mundy anasema kwamba “habari inayosisimua” ndiyo jambo muhimu. Ili sinema “ilete faida kubwa na kuwavutia watu wa umri mbalimbali bila kupuuza yeyote,” lugha chafu, jeuri nyingi, na picha nyingi za ngono hutiwa ndani.

Mtayarishaji akiona kwamba hati inaweza kuwa sinema nzuri, huenda akainunua na kumpa kandarasi mwelekezi na mwigizaji maarufu. Kuwa na mwelekezi na mwigizaji maarufu kutafanya sinema hiyo ivutie sana wakati itakapotolewa. Hata katika hatua hii ya kwanza, waelekezi na waigizaji maarufu wanaweza kuwavutia wawekezaji wanaohitajika ili kugharimia utayarishaji wa sinema hiyo.

Hatua nyingine ya matayarisho ni kuchora vibonzo mbalimbali vya filamu hiyo hasa vile vinavyohusisha mapigano. Michoro hiyo humwongoza mpiga-picha za sinema nayo husaidia kupunguza wakati unaotumiwa kupiga picha. Mwelekezi aliye pia mwandikaji wa hati, Frank Darabont, anasema: “Hakuna jambo baya zaidi kama kupoteza wakati wa kupiga picha kwa sababu tu ya kutojua mahali ambapo kamera inapaswa kuwa.”

Kuna mambo mengine mengi muhimu yanayopaswa kushughulikiwa wakati wa matayarisho. Kwa mfano, picha zitapigiwa wapi? Je, itakuwa lazima kusafiri? Je, kuna picha zitakazopigwa ndani ya nyumba, nayo itapambwaje? Je, mavazi maalumu yatahitajika? Ni nani atakayeshughulikia mwangaza, kupamba na kutengeneza nywele za waigizaji? Na vipi kuhusu sauti, madoido, na yule atakayeigiza sehemu hatari badala ya mwigizaji mkuu? Hayo ni baadhi ya mambo yanayohitaji kufikiriwa hata kabla ya kupiga picha za filamu. Ukitazama majina yanayoonyeshwa mwishoni mwa sinema inayotazamiwa kuleta faida kubwa, huenda ukaona kwamba mamia ya watu walihusika kuitayarisha! Fundi mmoja wa mitambo ambaye amehusika katika kutengeneza sinema nyingi anasema kwamba “watu wengi sana huhusika katika kutengeneza filamu nzuri.”

Kutengeneza Sinema Yenyewe

Kupiga picha za sinema kunaweza kuchukua wakati mwingi, kunaweza kuchosha, na pia kunaweza kugharimu pesa nyingi. Kwa kweli, kupoteza dakika moja tu kunaweza kugharimu maelfu ya dola. Nyakati nyingine inabidi waigizaji, wafanyakazi, na vifaa visafirishwe hadi sehemu ya mbali. Hata hivyo, haidhuru picha hizo zitapigiwa wapi, lazima pesa nyingi sana zitatumika kila siku.

Watu wanaoshughulikia mwangaza, wale watakaowapamba na kuwatengeneza nywele waigizaji huwa kati ya watu wa kwanza kufika mahali ambapo picha zitapigiwa. Kila siku ya kupiga picha, waigizaji wakuu hupambwa kwa saa kadhaa. Kisha picha hupigwa kwa siku nzima.

Mwelekezi husimamia kwa uangalifu kupigwa picha kwa kila onyesho. Inaweza kuchukua siku nzima kupiga picha za onyesho fupi sana. Picha za maonyesho mengi katika sinema hupigwa kwa kutumia kamera moja, kwa hiyo, onyesho moja linaweza kupigwa picha kadhaa kutoka pembe tofauti-tofauti. Isitoshe, huenda onyesho lilelile likapigwa picha mara kadhaa ili kupata picha bora zaidi au kurekebisha tatizo la kiufundi. Ikiwa onyesho ni refu, huenda picha 50 au zaidi zikapigwa! Kwa kawaida, mwishoni mwa kila siku, mwelekezi huchunguza picha zote na kuamua ni zipi zitakazotumiwa. Kazi ya kupiga picha inaweza kuchukua majuma au hata miezi kadhaa.

Hatua ya Kuunganisha Sinema Iliyotengenezwa

Katika hatua hii, picha zilizopigwa huboreshwa na kupangwa zinavyopaswa kufuatana. Kwanza, muziki utakaotumiwa huambatanishwa na sinema hiyo. Kisha, mhariri huunganisha sehemu za sinema hiyo na kufanyiza nakala ya kwanza isiyo kamili.

Madoido ya sauti na picha pia huongezwa katika hatua hiyo. Nyakati nyingine kompyuta hutumiwa kutia madoido hayo katika hatua hii ambayo ni mojawapo ya sehemu ngumu zaidi za utengenezaji wa filamu. Kazi inayofanywa katika hatua hii inaweza kuifanya sinema ivutie na ionekane kuwa halisi.

Muziki uliotungwa hasa kwa ajili ya sinema hiyo huongezwa katika hatua hiyo, na jambo hilo ni muhimu katika filamu za leo. Edwin Black anaandika hivi katika gazeti Film Score Monthly: “Sasa watengenezaji wa sinema hutaka muziki uliotungwa hasa kwa ajili ya sinema, nao hawataki muziki wa dakika ishirini tu au vipindi vifupi vya muziki, bali wao hutaka muziki utakaochezwa kwa muda unaozidi saa nzima.”

Nyakati nyingine filamu iliyoboreshwa huonyeshwa watu wachache ambao wanaweza kutia ndani rafiki za mwelekezi au wafanyakazi wenzake ambao hawakuhusika katika kutengeneza filamu hiyo. Ikitegemea jinsi watakavyoitikia, mwelekezi anaweza kupiga picha upya maonyesho fulani au kuyaondoa kabisa. Katika visa fulani, umalizio wote wa filamu ulibadilishwa kwa sababu watu walioitazama kwanza hawakuupenda.

Hatimaye, filamu iliyokamilika huonyeshwa kwenye majumba ya sinema. Ni wakati huo tu ndipo inaweza kujulikana ikiwa sinema hiyo itafanikiwa au haitafanikiwa, au itakuwa ya wastani. Lakini mambo mengi yanahusika kuliko kupata faida. Sinema kadhaa zikikosa kufanikiwa zinaweza kuharibu sifa ya mwelekezi na matarajio ya mwigizaji kupata kazi. Anapofikiria miaka yake ya mapema ya kutengeneza filamu, mwelekezi John Boorman anasema hivi: “Niliwaona waelekezi wenzangu wakikosa kandarasi baada ya sinema kadhaa walizoelekeza kukosa kufanikiwa. Ukweli wenye kusikitisha ni kwamba katika biashara ya kutengeneza sinema, usipowaletea faida mabwana zako, unapoteza kazi yako.”

Bila shaka, watu wanapotazama ubao wa kutangazia sinema, kwa ujumla hawafikirii ikiwa watengenezaji wa sinema hiyo watapoteza kazi zao au la. Yaelekea wao huhangaikia mambo kama: ‘Je, nitafurahia sinema hii? Je, inafaa nitumie pesa zangu ili kuitazama? Je, sinema hii itanivutia au itanichukiza? Je, inawafaa watoto wangu?’ Unaweza kujibuje maswali hayo unapoamua sinema utakazotazama?

[Maelezo ya Chini]

Anita Elberse, ambaye ni profesa wa Chuo cha Biashara cha Harvard, anasema kwamba “ingawa mara nyingi pesa zinazopatikana kutokana na mauzo ya sinema katika nchi za ng’ambo ni nyingi kuliko zile za mauzo nchini Marekani, jinsi watu wanavyoipokea sinema nchini Marekani huamua jinsi itakavyopokelewa katika nchi nyingine.”

Ingawa huenda njia ambazo hutumiwa kutengeneza sinema zikatofautiana, mambo yanayoelezwa hapa yanaonyesha njia moja inayoweza kutumiwa.

Nyakati nyingine mtayarishaji hupewa muhtasari wa hadithi badala ya hati yenyewe. Ikiwa atavutiwa na hadithi hiyo, anaweza kununua haki za kuimiliki na kuitengeneza kuwa hati.

“Huwezi kujua ni lini jambo fulani litawavutia au kuwasisimua watazamaji.”—David Cook, profesa wa masomo ya sinema

JINSI YA KUFANYA SINEMA IVUTIE NA ILETE FAIDA KUBWA

  Sinema imekamilishwa. Iko tayari kutazamwa na mamilioni ya watu. Je, itafanikiwa? Fikiria njia mbalimbali ambazo watengenezaji wa sinema hutumia ili sinema yao ivutie na ilete faida kubwa.

UVUMI: Mojawapo ya njia zenye mafanikio za kuwafanya watu wawe na hamu ya kutazama sinema fulani ni kupitia uvumi. Nyakati nyingine uvumi kuhusu sinema fulani huanza miezi kadhaa kabla ya sinema hiyo kuonyeshwa kwa umma. Huenda ikatangazwa kwamba kutakuwa na sinema itakayokuwa mwendelezo wa sinema fulani iliyofanikiwa hapo awali. Je, itakuwa na waigizaji walewale maarufu wa sinema ya awali? Je, itakuwa nzuri (au mbaya) kama ile ya kwanza?

  Katika visa fulani, uvumi huanzishwa kuhusu jambo fulani katika sinema, labda kuonyesha picha za ngono waziwazi katika sinema itakayotazamwa na watu wote. Je, sinema hiyo ni mbaya sana? Je, sinema hiyo imepita mipaka kabisa? Watengenezaji wa sinema hunufaika watu wanapotoa maoni mbalimbali yanayopingana kuihusu, kwa kuwa hiyo ni njia moja ya kuitangaza bila malipo. Nyakati nyingine mijadala hiyo huwafanya watu wengi waitazame sinema hiyo inapoonyeshwa kwa mara ya kwanza.

VYOMBO VYA HABARI: Njia za kawaida za kutangaza sinema zinatia ndani mabango, matangazo ya magazeti, matangazo ya biashara ya televisheni, kuonyeshwa kwa sehemu ndogo ya sinema hizo katika majumba ya sinema kabla ya sinema nyingine, na kasheshe. Sasa Intaneti imekuwa njia kuu ya kutangaza sinema.

KUUZA BIDHAA: Kuuza bidhaa zinazotangaza sinema fulani kunaweza kuifanya ivutie inapotolewa. Kwa mfano, sinema moja iliyotegemea shujaa anayetajwa katika kitabu fulani cha kibonzo ilitangazwa katika vifaa vya kubebea vyakula, vikombe, vito, mavazi, minyororo ya funguo, saa, taa, na michezo ya dama, na kadhalika. Joe Sisto anaandika hivi katika jarida la vitumbuizo la Shirika la Mawakili la Marekani: “Kwa kawaida, asilimia 40 ya bidhaa za kutangaza sinema huwa zimeuzwa hata kabla ya sinema hiyo kutolewa.”

KANDA ZA VIDEO: Sinema ambayo haileti faida kubwa inapoonyeshwa katika majumba ya sinema inaweza kuleta faida inaporekodiwa katika kanda za video. Bruce Nash, ambaye huchunguza faida zinazotokana na sinema anasema kwamba “kanda za video huchangia asilimia 40 hadi 50 ya mapato ya sinema.”

VIWANGO VYA SINEMA: Watengenezaji wa sinema wamejifunza kutumia viwango vinavyowekwa vya sinema ili kujifaidi. Kwa mfano, huenda mambo fulani yakaingizwa kimakusudi katika sinema ili kuifanya iwekewe kiwango cha juu zaidi kinachowafaa watu wazima pekee. Kwa upande mwingine, sehemu chache zinaweza kuondolewa ili sinema isipewe kiwango cha watu wazima na kuifanya iwavutie vijana. Liza Mundy anaandika katika gazeti The Washington Post Magazine kwamba kuwekea sinema kiwango cha vijana “kumekuwa njia ya kutangaza sinema: Majumba ya kurekodia sinema hutumia kiwango hicho kupitisha ujumbe kwa vijana na watoto wanaotamani sana kuwa vijana kwamba sinema hiyo itakuwa yenye kuvutia sana.” Mundy anasema kwamba kiwango hicho “hutokeza uvutano kati ya mzazi na mtoto kwani humwonya mzazi na kumvutia mtoto.”

JINSI SINEMA ZINAVYOTENGENEZWA

HATI
MICHORO
MAVAZI
KUPAMBWA
UPIGAJI PICHA
KUTIA MADOIDO
KUREKODI MUZIKI
KUINGIZA SAUTI
KUTENGENEZA VIBONZO KWA KUTUMIA KOMPYUTA
KUBORESHA NA KUPANGA PICHA

Jumamosi, Novemba 16, 2013

KUKOMESHA MAUAJI YA TEMBO


Tumekuwa tukisoma na kuangalia habari tofauti kuhusu tembo wanavyouwawa na pembe zao kuchukuliwa. Ujangili dhidi ya tembo umeshamiri licha ya kauli mbalimbali kutoka katika vyombo tofauti vya kitaifa na kimataifa za kusimamisha mauaji hayo zinazotolewa.

Tanzania inaoongoza kwa uuzaji nje wa pembe za ndovu.
Inakadiriwa kuwa wastani wa tembo 10,000 huuwawa kila mwaka nchini Tanzania.

Je, nini ni chanzo cha kuuwawa kwa tembo hao?

Huku tukipambana na jinsi ya kumaliza mauwaji ya tembo wetu,soko la pembe za ndovu limekuwa likishamiri huko Asia(China).Pembe za ndovu ambazo si halali zikifanikiwa kuingia nchini China basi hugeuka kuwa halali.

Kwa mtazamo wangu nadhani vitaa hii inabidi ipiganiwe pande zote yaani ni jinsi gani tutakomesha uwindaji huu haramu nchini mwetu na pili ni jinsi gani tutashughulika na wanunuzi wa pembe haramu.
Nadhani hapa ndipo penye changamoto zaidi kwani kunapokuwa na mwanya katika sheria ndipo watu hufanya yao.Kama wanunuzi wangebanwa na sheria za manunuzi ya pembe za ndovu sidhani kama ujangili huu ungekuwepo kwa kiasi hiki tunachoona sasa. Ni vizuri kukawa na sheria za kitaifa na kimataifa zisizokinzana katika kutekeleza hili. Kwa kufanya hivi tunasuru si tembo tu bali maliasili yote kwa ujumla.


Kukamatwa kwa vipande saizi ya 700 za pembe za ndovu inaonyesha jinsi gani uzao wa mnyama huyo asiye na hatia unavoelekea kumalizwa nchini.Inasikitisha na kutia hasira.Hivi tutavieleza nini vizazi vijavyo?

Tumeona wachina waliokamatwa na pembe za ndovu walivyojiamini na kuja kukusanya pembe nchini kwetu kama vile hakuna sheria.Wameonyesha jinsi gani walivyojihalalishia ukusanyaji wa nyara hizo.Watu wetu wakimatwa na madawa ya kulevya kwao wanawanyonga au kuwafunga kifungo cha muda mrefu,sisi tutawafanya nini hawa tuliowakamata?Sheria zetu zinasemaje?

NINI KIFANYIKE KUTOKOMEZA BIASHARA YA MENO YA TEMBO?

Hili ni swala la kuingizwa katika katiba mpya (kama halipo) kuwa atakayeshikwa na nyara za serikali ,au kujihusisha na uwindaji haramu ahukumiwe kama mhaini iwe ni raia au siyo na tusikubali kubadilishana wafungwa(extradiction) wa aina hii.

Sijui sheria yetu inasemaje kuhusu kukamatwa na nyara ila hawa Wachina inabidi wawe somo kwa wawindaji na wanunuzi haramu wengine wote kwani wamekutwa na kielelezo mikononi mwao.Kikubwa wautaje mtandao wao ili sheria ichukuwe mkondo wake.

Watanzania tuisaidie serikali yetu katika kutokomeza tatizo hili.Nina imani kuwa wapo wanaowajua watu wanaojishughulisha na biashara hii haramu.Tuwe na moyo wa uzalendo katika kulinda maliasili zetu.

Kingine "tugomee kununua bidhaa zote zilizotengenezwa kwa pembe za ndovu!Tukigoma kununua bidhaa mauwaji ya tembo yatakwisha.

Maelezo kwa hisani ya Rainbo-tz

Jumatano, Novemba 13, 2013

MTANDAO SAYANSI

Photo Credit By: http://theamazingworldofpsychiatry.wordpress.com


Unaweza kuwa mtumiaji ulie makini wa Mtandao, lakini hii kozi ya utangulizi katika Mtandao Sayansi itakusaidia kuelewa Mtandao wote kama mfumo wa kijamii na mfumo wa kiufundi: habari za kimataifa, miundombinu inajengwa kutokana na mwingiliano wa watu wataalamu wa teknolojia.

Inachunguza asili na mageuzi ya Mtandao na fikirisha maswali muhimu ya Usalama, Mtandao wa Demokrasia na Uchumi kutoka mitazamo yote Computational na sayansi ya jamii.

Kwa kufuata kozi hii, utakuwa na uelewa mkubwa wa Mtandao na kuanza kuendeleza ujuzi kwa ajili ya zama hizi za kidigitali - ujuzi ambao ni muhimu kwa ajili ya maisha ya kila siku kwa upana uliopendekezwa na teknolojia unaoongoza na waajiri wa leo.

Huu ni mwanzo wa safari ambayo inaweza kusaidia sura ya baadaye ya mtandao wa dunia nzima.

Jumatatu, Novemba 11, 2013

TEKNOHAMA: NI UFANISI AU CHANZO CHA UGOIGOI KWENYE AFYA? - Sehemu ya 1Nikiwa kama mjukuu kipenzi wa bibi yangu, huwa napenda sana kutumia muda wangu wa mapumziko kujadiliana naye mambo mbalimbali yanayohusu jamii, iwe yaliyokuwa yanatokea hapo awali au yanayoendelea kutokea. Ilikuwa ni siku ya jumapili baada ya kutoka kwenye mihangaiko, niliingia ndani na kumuita bibi kwa jina lake la utani ‘Nyaksi’ ili twende nje tukapunge upepo na mazungumzo ya hapa na pale.
 
Kama ilivyo ada yangu, huwa napenda sana kutafiti mambo mbalimbali, nikamuuliza bibi, eti bibi nimewahi kusikia kuwa wakati wa enzi zenu mlikuwa hamruhusiwi kula mayai wakati wa ujauzito kwa kuwa mtoto atazaliwa bila nywele? Bibi Nyaksi huku akitabasamu akanigeukia na kusema, "umeshaanza, kwanza usikumbushe enzi zile bado nipo mbichi" akimaanisha wakati yupo msichana. Wote tukatabasamu kwa pamoja. Nyaksi akaendelea kusema sio mayai tu, bali vyakula vyote nyenye virutubisho kwa wingi ambavyo ninyi vijana wa leo mnaviita ‘purotini’, akiitamka protini kwa lafudhi ya kizee. Nyaksi alisema tulizuiliwa kula vyakula hivyo kwa mlengo wa mwiko, akaendela kusema, unajua Babu (jina langu alilopenda sana kuniita Nyaksi) wazee walitumia mwiko ili kututisha lakini ukweli ni kuwa wakati ule hakukuwa na tekenolojia (akimaanisha teknolojia) hivyo kama utakula vyakula vyenye virutubisho sana vitamfanya mtoto awe mkubwa, na hivyo kama utashindwa kujifungua kwa njia ya kawaida basi hakutakuwa na njia nyingine ya kukusaidia. Nyaksi akaendelea ninyi vijana wa siku hizi mna raha, hospitali nyingi, madaktari wengi huku mna njia nyingi mbadala ikiwemo ya upasuaji na nyinginezo.

   Nilimuacha Bibi Nyaksi amalizie maneno yake, halafu nikamuuliza, kama sisi tuna teknolojia na njia nyingi za kisasa, sasa inakuwaje urefu wa maisha wa vizazi vyetu unazidi kupungua kadri teknolojia inavyozidi kukua? Nyaksi alicheka sana, huku akipigapiga makofi ili kuvuta hisia alisema " hakuna kizuri kisicho na kasoro". Baada ya hapo tukaacha kuongelea masuala ya afya na kuketi chini ili kupunga upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi kutokea Kinyanyiko.

  
Kipindi chote naburudika na upepo uliokuwa unavuma ukitokea kwenye mabonde ya Kinyanyiko nilikuwa natafakari mambo mengi kuhusu maneno ya Nyaksi. Misemo yake ilikuwa inazungukazunguka kichwani kwangu , huku maneno "Hakuna kizuri kisicho na kasoro " na " ninyi mnaishi kwenye ulimwengu wenye tekinolojia" vikijitokeza mara kwa mara. Lakini je, hizi teknolojia zinatunufaisha vipi? Zipi faida na hasara zake? Hivyo nikawa nachorachora chini nikiainisha viambatanishi vyote vya hii tunayoiita teknolojia, nikarudi haraka nyumbani na kuchukua iPad yangu kuanza kuandika makala hii ambapo tutaiangalia teknolojia kwa mapana na jinsi gani teknolojia inavyoweza kuongeza ufanisi katika medani ya afya.

Teknolojia ni nini?

   Teknolojia ni utengenezaji,matumizi,maarifaya vifaa,machine,mitambo,uashi ili kutatua tatizo au ketenda kazi husika, iwe ni kwenye matibabu au kwenye michezo. Katika makala yetu ya leo tutaangalia sana hii teknolojia ya mawasiliano ya mtandao yaani ICT. Kwa wale maveterani kama mimi mtakumbuka teknolojia hii ilianza kuibukia kwa kasi sana nyumbani katika miaka ya tisini, katika wakati huo teknolojia hii siyo tu ilionekana kuwa ni kitu cha anasa bali pia ni kwa wenye nazo tu. Teknolojia hii ilihusishwa na viashiria chungu mzima kama kwenda na wakati, usomi, umjini n.k. kitu ambacho kimetufikisha hapa tulipo.


Mtazamo wa jamii juu ya teknolojia

   Kama nilivyoelezea hapo juu, asili na historia juu ya ujio wa teknolojia hii ya mawasiliano ya mtandao inachangia sana katika ujengekaji wake, kwa mfano hapa kwetu wengi bado wana mtazamo hasi kuwa teknolojia hii ni kwa ajili ya wasomi au wenye uwezo, ingawa dhana hii inaendelea kubadirika siku hadi siku, lakini tatizo bado lipo. Nani wa kulaumiwa? Ni wanajamii au sisi wana mawasiliano? Jibu ni fupi. Hakuna wa kulaumiwa bali hatuna budi kutafakari juu ya namna ya kuliboresha na kulihalisisha kwa jamii yetu.

Muundo wa teknolojia kwenye karne ya 21

   Katika makala yake ya sababu za watoto wachanga kulia, Dk Paul Mwanyika amefafanua kwa undani hatua ambazo mtoto hupitia katika ukuaji, kwa muktadha huohuo nami naufananisha ukuaji wa teknolojia na ule wa mtoto. Kwa ufupi, teknolojia imepitia hatua nyingi. Kwa mfano hapo zamani teknolojia ilikuwa ni kwa ajili ya kurahisisha kazi au utendaji, lakini leo hii teknolojia imegeuzwa kuwa sehemu ya kazi na siyo tena kitendea au kirahisisha kazi.
   Si kitu cha kushangaza kusikia mtu anauza madawa mtandaoni (online) bila kuwa na duka nje ya mtandao (brick shop). Aidha leo hii madaktari wanaweza kupata muongozo au kushiriki kwenye upasuaji bila kizuizi cha umbali. Huu ndiyo muundo wa teknolojia ya sasa, tunatumia teknolojia kama huduma/kazi (Technology As A Service) na siyo tu kitendea kazi.

Faida/Matumizi za teknolojia kwenye Afya

   Lengo la makala hii ni kuwaamsha (kumbusha) wanajamii umuhimu au njia mahususi za kutumia teknolojia katika kujenga afya bora. Msukumo wa makala hii umekuja kutokana na matokea ya utafiti
niliyofanya kwenye tovuti ya TanzMED.com. Ndani ya tovuti hii kuna sehemu ambayo mtumiaji anaweza kujisajiri akawa anapokea taarifa mbalimbali kuhusiana na afya (milisho ya afya). Nilichogundua ni kuwa uwiano wa wanaojisajili kwa wanaotembelea ni chini ya 1%. Baada ya kuwauliza watembeleaji wengi kwanini hawajisajili, karibu 20% walisema hawafahamu jinsi ya kutumia njia hiyo, wengine 20% hawajui uwepo wa programu hii na waliobaki ni kutotambua umuhimu wa kufanya hivyo. Hii ni sehemu ndogo tu ambayo matumizi ya teknolojia yanaweza kukurahisishia kujenga afya bora.

Hivyo tuangalie kwa kila kundi ni jinsi gani linaweza kunufaika na teknolojia.

Madaktari 

   Wakiwa ndio watendaji wakuu, ni dhahiri kuwa madaktari ni moja ya watu wenye heshima kubwa sana kwenye jamii yetu. Wengi tumekuwa tukiwaamini na kuwakubali madaktari kwa kiwango kikubwa zaidi. Leo hii kuna mitandao jamii kama Facebook, Twitter na hata TanzMED.com (Jumuiya), kwa kutumia mtandao jamii daktari anaweza kuwasiliana na wanajamii akawapa mustakabali wa masuala ya afya, kwa mfano nimewahi kuona vipachiko kadhaa vya Dk Fabian Mghanga kwenye Facebook, akiwa anapachika mambo yaliyo motomoto kwenye jamii yetu kwa sasa, wanajumuiya wote wanaomfuata huweza kuona vipachiko vyake na kubadilishana naye mawazo au kutolea maoni. Si hayo tu daktari pia anaweza kutumia programu za mawasiliano kubadilishana mawazo (kuchat) na wagonjwa walioruhusiwa ili kufuatilia hali zao na kuwafariji. Vilevile daktari anaweza kutumia simu kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa wagonjwa walio hospitali akiwakumbusha kunywa dawa na kufanya mazoezi ya asubuhi au jioni. Wagonjwa watafarijika sana endapo wanapokea ujumbe toka kwa daktari unaomsisitizia jambo fulani. Hivyo muda umefika sasa kwa madaktari wetu kubadirika na kuanza kutumia fursa hizi ambazo zinawezekana na kupatikana kwenye mazingira yetu ya Tanzania.

 Chukulia mfano, kwanini mahospitali yasichukue namba za simu za wagonjwa wote na kuzipanga kulingana na aina ya magonjwa yao halafu wakawa wanawatumia ujumbe au taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo au tahadhari muhimu juu ya magonjwa yao?

Vyombo vya habari & Wasanii

   Hii ni moja ya sehemu ambazo zina ushawishi na upenzi mkubwa mno kwenye jamii. Katika baadhi ya nchi zilizoendelea, unaweza kukuta uwepo wa televisheni au redio zinazohusu masuala ya afya pekee. Kwa nchi kama Tanzania wamiliki wa hizi televisheni, magazeti au redio wanaweza kutumia vituo vyao kufikisha maarifa, ufahamu na hata ujumbe juu ya afya. Kwa kushirikiana na watu maarufu na wasanii dhana hii inaweza kukubalika na kufika mbali zaidi.

Makampuni ya teknolojia

   Makampuni yanayojihusisha na mawasiliano ya mtandao, kuanzia makampuni ya simu, watengeneza programu nk, yanatakiwa kushirikiana na wadau wa medani ya afya katika kuhakikisha wanainufaisha jamii. Kwa mfano kampuni ya Dudumizi Solutions imejiunga na kundi la madaktari na kuanzisha mtandao wa Afya ujulikanao kama www.tanzmed.com. Hii ni chachu na changamoto kwa wadau kuonesha kuwa sasa teknolojia ni sehemu ya jamii hivyo tunatakiwa kujihusisha zaidi, tubadilishe utendaji au mfumo wa teknolojia. Kwa mfano makampuni ya simu yanaweza kuja na programu ambazo zitawawezesha wanajamii kutuma namba fulani halafu wakapata elimu au taarifa fupi za masuala ya afya (kama ile inayofanya kwa mama wajawazito). Aidha wataalamu wa programu wanaweza kuja na programu inayoweza kutumika kwenye simu kumuwezesha mtu kukokotoa afya yake (BMI Calculator), kujua siku ya kujifungua nk, hii ni mifano michache ambayo wadau wa ICT wanaweza kuitumia kujenga jamii yenye afya njema. Nimeongelea kwa ufinyu wake kutokana na hali halisi ya maendeleo ya ICT kwa nchi yetu ingawa tunaweza kwenda mbali zaidi ya hapo.

Wanajamii

   Wakiwa ndio walengwa namba moja, wanajamii wanatakiwa kuanza kutumia teknolojia kama sehemu ya kujenga afya yao. Kwa mfano unaweza jiunga kwenye milisho (Subscription) ya tovuti mbalimbali za afya ambapo utakuwa unapokea taarifa mbalimbali za afya kama; mabadiriko ya hali ya hewa, magonjwa ya milipuko, kinga na mengineyo. Mara nyingi makala hizi huwa zinachujwa kuhakikisha unatumia taarifa inayojieleza. Hivyo jijengee mazoea ya kutumia teknolojia kwa ajili ya afya yako, iwe kuuliza maswali juu ya afya au kusoma dalili na kinga za magonjwa mbalimbali. Mtandao wa www.tanzmed.com una yote haya kwa ajili ya afya yako.

   Nilipomaliza kuainisha baadhi ya faida za teknolojia, kuna maneno ya Bibi Nyaksi yakawa yaniumiza," Hakuna kizuri kisicho na kasoro". Hivyo tuangalie athari za hii teknolojia.

Kuvunja maadili na mipaka ya teknolojia

   Kutokana na ujio wake, wengi wamekuwa wakitumia teknolojia bila mipaka. Maadili ya teknolojia yamepigwa kumbo. Kwa mwandishi wa TanzMED Dk Fabian Mghanga ameeleza jinsi gani dawa za kuongeza makalio zinavyoshabikiwa, huku zikiwa hazina maelezo ya kuridhisha juu ya matumizi na namna zinavyofanya kazi. Ushabiki huu pia huchochewa sana na matumizi ya mitandao jamii kama vile Facebook, ambapo baadhi ya watu hutuma matangazo au picha zenye mvuto na kuwafanya akina dada wengi wahamasike kwa kutaka kuwa na mvuto kama waliouona kwenye picha. Si hayo tu, tumeona pia jinsi mwandishi Dk Henry Mayala alivyotuelezea jinsi vumbi la viwandani linavyoweza kukusababishia pumu au magonjwa ya mfumo wa hewa, haya yote ni kwa sababu ya kuvukwa kwa mipaka ya maadili ya teknolojia kwa watoa huduma. Uvukaji wa mipaka siyo tu kwa watengenezaji (watoa huduma) za teknolojia bali pia kwa wanajamii. Kwa mfano katika makala yake ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi Dk Khamisi Bakari amesema sababu mojawapo ni matumizi ya intaneti kwa muda mrefu, hii ni inatuonesha mifano dhahiri ya athari zinazosababishwa na utokaji nje ya maadili ya teknolojia kwa mtumiaji. Hivyo maadili ya teknolojia ni lazima yaheshimiwe.
 

Maadili na mipaka ya kazi

   Nakumbuka kuna wimbo mmoja wa wanamuziki wa kizazi kipya wanaoitwa Wagosi wa Kaya uitwao wauguzi kuna kipande cha mstari kinasema; "...nesi anaongea kwa simu na bwana wa kizigua". Hii ni moja ya athari za teknolojia. Kuna wakati unatamani hata upigane, maana unaenda hospitalini huku kuna foleni kubwa inasubiri kumuona daktari, lakini yeye yupo bize kwenye simu akicheka kuhusu matokeo ya mpira wa jana. Hapo sizungumzii muda wanaotumia kuangalia picha na maoni kwenye Facebook au kuchat kwenye Yahoo na rafiki yake aliye Wuhan. Idara husika lazima iweke mipaka na maadili ya kazi yatakayomuongoza muhusika katika matumizi ya teknolojia. Tukumbuke kuwa teknolojia sasa imekuwa ni kazi na maisha hivyo haiepukiki.

   Wakati namalizia haya maneno ya mwisho chaji nayo ikawa imeisha kwenye iPad yangu, ni bahati mbaya kwamba jana sikuichaji kutokana kukatika kwa umeme. Sasa basi inanibidi kusubiri umeme urudi ili niweze kuichaji na kumalizia makala hii ambayo nitaituma kwenye jarida lijalo, makala ambayo itazungumzia mambo ambayo ningependa kuishauri jamii/serikali ifanye ili kujenga na kudumisha afya bora kwenye karne hii ya teknolojia

Chanzo: INGIA HAPA

Je unamfahamu Ludwig van Beethoven? 
Alizaliwa 16 Desemba 1770 na kufariki 26 Machi 1827. Alikuwa mtungaji wa muziki na mpiga piano kutoka nchi ya Ujerumani.
Alizaliwa mjini Bonn akiwa mtoto wa mwanamuziki aliyemfundisha kinanda tangu utoto. 1787 akiwa kijana alisafiri Vienna iliyokuwa mji mkuu wa Dola Takatifu la Kiroma kwa matumaini ya kukutana na Wolfgang Amadeus Mozart akarudi 1792 alipopata mafunzo kuoka Joseph Haydn.

Tangu 1793 alikuwa maarufu mjini Vienna kama mpiga kinanda akaendelea kutunga muziki yake. Alipata usaidizi na wateja kati ya makabaila wa makao makuu ya Kaisari.

Tangu miaka ya 1796 alianza kupoteza uwezo wake wa kusikia wake akaendelea kuwa kiziwi lakini aliamua kuendelea na muziki yake. Kuna hadithi ya kwamba alioongoza simfonia ya tisa na mwishowe watu walimgeuza aangalie wasikilizaji kwa sababu hakusikia jinsi walivyopiga makofi.

Aliweza kuendelea kutunga na kuongoza musiki na kupiga piano. Alifunga fimbo kwenye kinanda akaishika kwa meno na kusikia tetemeko la piano kupitia fimbo na meno yake.

Aliaga dunia alipokuwa na umri wa miaka 57.

SWALI:UNAIELEWAJE HII PICHA?

KUFAFANUA BIDHAA
Tutaweza kuhoji dhana ya 'kijinga' kwa kusikia kutoka mitazamo tofauti. Kama wewe unaangalia na kusoma, fikiri kuhusu jinsi mawazo ya bidhaa yalivyoelezewa.

Kuna mambo ya kimawazo kwa pamoja juu ya tofauti au hata migongano. Kuangalia kwenye bodi ya majadiliano itatufikisha katika hatua.

Je umefikiri kuhusu namna utakavyoongeza zaidi mawazo yaliyowasilishwa POPOTE ULIPOPITA ama KUSOMA?.

Jumapili, Novemba 10, 2013

DARASA LA UIMBAJIJohn Shabani akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake wa sauti

(SIFA NA MBINU ZA KUWA MWIMBAJI BORA)

SINGING COURSE 

Jinsi ya kuponya na kutunza Sauti yako
 
Weka  sauti yako katika afya nzuri ili uweze kuendelea kuimba!
Kila mtu anaweza kutumia sauti yake, lakini si kila mtu anajua jinsi ya kutunza afya ya sauti yake, au nini cha kufanya kunapotokea tatizo katika sauti. Makala hii itasaidia kila mtu kujifunza jinsi ya kuponya sauti zao  na pia kutoa ushauri wa jinsi ya kutunza afya yake na kuwa nguvu ile ile kwa ajili ya siku zijazo.
Mambo  unayo hitaji au ya kuzingatia kama mwimbaji
 • maji kwa uwingi
 • ngumu pipi, mints, nk
 • mvuke (moto oga)
 • Koo kanzu chai
 • asali
 • limao
Maelekezo
o    1 Kama sauti yako imejeruhiwa,  jambo muhimu zaidi la kufanya hivi sasa ni kuacha kutumia kwa muda. Sauti inahitaji kupumzika pia. Punguza mazungumzo yako na hasa kupayuka na kupaza sauti, kujifunza kuzungumza zaidi kwa ufupi, na kutumia zaidi kidogo muda katika ukimya.

o    2  Jambo jingine kubwa ambalo husaidia sauti iliojeruhiwa ni  chai ya moto pamoja na limau kidogo na asali. chai nzuri ni ile iliyo shauriwa ki afya na si kila chai ni bora. Unaweza kupata na dawa za mitishamba katika duka la dawa,  ambazo ni maalumu kwa ajili ya sauti, Kunywa angalau kikombe asubuhi na kikombe wakati wa usiku.

Mwl. John akielekeza matumizi ya asali

 
MAFUNZO YA SAUTI

By John Shabani
Mobile: 0716560094, 0754818767
Facebook: John ShabaniMambo ya msingi yanayofunzishwa katika program hii:
Ø  Historia ya uimbaji
Ø  Tofauti ya mwimbaji na mwanamuziki
Ø  Vyakula na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa
Ø  Sifa na mbinu za kuwa mwimbaji bora
Ø  Jinsi ya kuitunza na kuiponya sauti yako
Ø  Amri 10 za sauti
Ø  Matumizi ya kipaza sauti (Microphone technique)
Ø  Utunzi wa nyimbo
Ø  Mazoezi ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
Ø  Ushauri kwa wanaotaka kurekodi nyimbo

Kuimba ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia twaweza kusema ni kutamka maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya muziki, tuni) au ghani

Kama vile tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye pia anazo ala mbili muhimu:
·         Mdomo wenye uwezo wa kutoa sauti ya uimbaji
·         Mwili
Kumbuka moja ya vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy) “As you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must useless”. Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa na nguvu za kimwili unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri pamoja na  mazoezi ya viungo. 

MAZOEZI NA FAIDA ZAKE
 
 
Pamoja na faida nyingi za mazoezi lakini pia mazoezi huchangamsha mwili, hulainisha koo, husaidia kuwa na pumzi ya kutosha, hukuhepusha au kupunguza baadhi ya magonjwa kama kisukari, presha n.k, hung’arisha ngozi, na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu, MAZOEZI HUSAIDIA KATIKA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA KUWA MZURI , KUKUPA NGUVU NA KUWEZA KUFANYA KAZI KWA NGUVU ZAKO BILA KUJISKIA UMECHOKA NA MWISHO WA SIKU HUPUNGUZA MAFUTA MWILINI,  HUPUNGUZA UZITO, KUNYOOSHA NA KUIMARISHA MISULI YA MWILI, HUSAIDIA MAPIGO MAZURI YA MOYO KWA KUONGEZA KASI YA MAPIGO YAKE WAKATI WA MAZOEZI, UNGUZA MRUNDIKO WA DAMU KWENYE MISHIPA, HII NI MUHIMU KWA SABABU MGANDO WA DAMU HUSABABISHA MAGONJWA YA MOYO PAMOJA NA KUPOTEZA FAHAMU, MAZOEZI HUIMARISHA MIFUPA YA MWILI, HUBORESHA USINGIZI.

Fikiria mwenyewe kama mwanamichezo au mtu wa fani fulani na jifunze kuwa mtu wa kula na kunywa kulingana na fani yako: Aina ya chakula na kinywaji na muda  wa kutumia ni jambo la kuzingatia sana. Kula na kunywa ni muhimu lakini Jiepushe na ulafi kwani huleta uchovu, mfumo wa kupumua kuathirika na wakati mwingine kusababisha magonjwa.


Kuna misimu fulani kama msimu wa vumbi au baridi kali au alegi au matatizo mengine kibao, wakati mwingine aina fulani ya dawa kwa ajili ya ugonjwa fulani, Wakati mwingine husababisha mafua au kutokwa na kamasi mara kwa mara au kukausha koo kabisa, hivyo husumbua sana na kuathiri mfumo wako wa kuimba. Wakati mwingine mazingira ya shughuli au kazi tuzifanyazo au pia mazingira ya makazi huweza kuathiri sauti zetu. Hivyo masomo ya utunzaji wa sauti ni ya muhimu sana.

Vilaji na vinywaji visivyofaa Kabla ya kuimba

Kuhusu chakula, ni muhimu ili kuepuka kuimba  tumbo likuwatupu kabisa. Kuimba ni kama riadha, inahitajika nguvu kwa ajili ya utendaji wako. Hata hivyo, ni muhimu pia kuepuka kuimba tumbo likiwa limeshiba sana. Yapo madhara mengi yanayotokana na shibe. Unaweza ukawasiliana na mwalimu wa sauti ili kujua madhara hayo. Kumbuka kuimba ni kazi ngumu, unahitaji mafuta (you need fuel), hivyo inashauriwa kuwa na mlo wa kawaida wa saa moja au mbili kabla ya uimbaji ni bora zaidi.

Kulingana na mazoea yetu vipo vyakula na vinywaji ambavyo ni vigumu kuachana navyo ghafla, mengine huchukua muda. Lakini hata hivyo kwa ajili ya kutunza koo (Mashine inayozalisha sauti) pamoja na kujihepusha na madhara yanayoweza kujitokeza unapokuwa na shughuli nzito ya uimbaji, ni muhimu ujihepushe navyo. Nitakuambia kwa ufupi kuhusu vyakula visivyofaha unapokuwa na shughuli za uimbaji. Kwasababu za msingi si rahisi kukutajia kwa undani madhara ya baadhi ya vyakula au vinywaji, wasiliana na mwalimu kwa wakati wako.

Baadhi ya vyakula na vinywaji vya kuepuka kabla ya kuimba ni kama vile:

 • Vinavyoleta mwasho au kukera koo (throat irritants): vyakula au vinywaji vinavyochangamsha, kusisimua au kulewesha (Overly spicy foods) ,  kama vile kahawa na pilipili, vinywaji baridi sana, sukari iliyosafishwa, chocolate.
 • Jamii ya vitu vyenye alkoholi, Sigara, tumbako, bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya
·         Vyakula vinavyoongeza mucous (sehemu ya kiwambo cha seli inayozunguka mfereji wa chakula): maziwa, koni, malai/maziwa yenye ubarafu (ice cream), maziwa mgando na aina nyingine ya maziwa (dairy products)
 • Vyakula vinavyofanya koo kuwa kavu: matunda jamii ya machungwa, pombe
 • Soda na aina ya vinywaji vinavyochemsha au vinavyojaza gesi au hewa katika tumbo
 • Vyenye ubaridi sana au barafu: husababisha koo kubana, kuminywa au kunyongwa.
·         Vyakula vinywaji vyenye ubarafu na pombe (ikiwa ni pamoja na mvinyo na bia). Kuna baadhi ya watu pia huwa na alegi (kwa mfano, baadhi ya waimbaji wana shida na matunda jamii ya machungwa, ngano, karanga, samakigamba au soya).
·         Vyakula vyenye mafuta mengi

Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na katika uimbaji wako zingatia :
·         Punguza  matumizi mengi ya sukari, ongeza matumizi ya matunda
·         Punguza kula nyama nyekundu, ongeza matumizi ya mbogamboga
·         Punguza matumizi ya soda, ongeza matumizi ya maji
·         Punguza kuendesha, ongeza kutembea kwa miguu
·         Punguza kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa wakati
·         Punguza msongo wa mawazo, ongeza kupumzika

Zingatia :
·         Maji ya moto au aina ya chai mitishamba (herbal tea) ni bora, Mwimbaji mzuri hutumia class 8 za maji kwa siku, wapo ambao hutumia hadi lita 4 pia yapo maji ya ziada kutoka katika vyakula.
·         Kupasha sauti kwa kukohowa kohowa sio njia ya kukusaidia kuimba vizuri, badala yake hukata sauti
·         Pamoja na umuhimu wa maji, lakini acha matumizi ya maji mengi saa moja au mbili kabla ya kuanza uimbaji badala yake asali ni bora zaidi. Lakini pia sauti ikipatwa na tatito unaruhusiwa kupata maji ya moto pamoja na asali
·         Angalizo kuhusu mazoezi: Mazoezi huwa yana ugumu wake hasa pale unapokuwa unaanza, usikate tamaa wala usikubali uvivu au maumivu yakakurudisha nyuma. Jitengee muda maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi na usianze kwa kufanya mazoezi magumu bali anza na mepesi mepesi ili kuupa mwili nafasi ya ku-adopt mabadiliko

koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa na:

Aina fulani ya pipi, asali, mvuke, chai fulani ya mitishamba au mchaichai, kusafisha koo kwa maji chumvi, baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari n.k

Jinsi ya kulinda na kuiponya Sauti yako

 

 

Kila mtu anawezakuitumia sauti yake, lakini si kila mtu anajua jinsi ya kuitunza au kuiponya inapopatwa na tatizo. afya yake, au nini cha kufanya wakati si tu kufanya kazi haki. Makala hii itasaidia kila mtu kujifunza jinsi ya kuponya sauti  na pia kutoa ushauri wa jinsi ya kuitunza na kuifanya kuwa na afya na nguvu kwa ajili ya siku zijazo
Masomo haya yanawafaha walimu, wainjilisti, wanasiasa, wazazi, wanasheria, madaktari, na waimbaji, na kila mtu ambaye shughuli zake hulazimi kakuongea sana.

·         Kama sauti yako  imejeruhiwa vibaya, basi jambo muhimu zaidi la kufanya sasa hivi ni kuacha kutumia hiyo Sauti,  ipumzishe. Punguza pia kuzungumza kwa muda mrefu na hasa kwa kupaza sauti kubwa na kutumia muda kidogo zaidi katika ukimya.
·         Jambo jingine kubwa ambayo husaidia sauti iliyojeruhiwa ni chai ya moto (Kama vile coat tea). Unaweza kupata pia  dawa za mitishamba zilizohifadhiwa kitaalam katika maduka ya dawa, lakini ikiwa dini yako au tamaduni yako haina shida katika hili. Kunywa angalau kikombe asubuhi na kikombe wakati wa usiku.
·         kama kuna kitu ambacho kinaweza kusaidia kuponya sauti yako na pia inaweza kutumika kulinda kwa haraka  ni unywaji wa maji ya kila siku. Maji husaidia na sauti yako katika afya nzuri
 
Source:http://johnshabani.blogspot.com