Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Juni 16, 2011

TOKENI MIJINI…SEHEMU YA NNE

Kutokana na majukumu, ndio maana sijaweza kutoa kwa wakati chapisho la kitabu hiki.

Kazi Mbalimbali Katika Maeneo ya Vijijini

Ardhi Itupatie Mahitaji Yetu

Kwa mibaraka yake Mungu, ardhi hii ikilimwa itatupatia mahitaji yetu. Tusikate tamaa kwa

mambo ya maisha haya kwa sababu ya kuonekana hali ile ya kushindwa, wala tusivunjike moyo

kwa kuchelewa mambo. Yatupasa kuulima udongo kwa furaha, matumaini, na shukrani, tukisadiki ya kwamba ndani ya udongo huo kuna hazina nyingi za kuweka ghalani mwetu kwa mfanyakazi mwaminifu, yaani, hazina zile zenye utajiri mwingi kuliko dhahabu na fedha. Shutuma ile inayotolewa kwake [huo udongo] kuwa ni mnyimivu [hautupatii mavuno ya kutosha] ni ya uongo.

Kwa kuilima vizuri na kutumia akili ardhi itatoa hazina zake [mazao] kwa manufaa ya

mwanadamu. Milima na vilima hubadilika; dunia huchakaa kama vazi kuukuu; lakini mbaraka wa Mungu, unaoandaa meza [chakula] jangwani kwa ajili ya watu wake, hautakoma kamwe.

Nyakati ngumu sana zi mbele yetu, tena ipo haja kubwa kwa familia kutoka mijini kwenda kule

shamba [vijijini], kweli yaweza kupelekwa katika vichochoro sawasawa tu na vile inavyoweza

kupelekwa katika njia kuu za usafiri za dunia hii. Mengi hutegemea juu ya kupanga mipango yetu kulingana na Neno la Bwana, na kwa juhudi ya kudumu kuitekeleza [mipango hiyo]. Mambo mengi sana hutegemea bidii yetu iliyotolewa wakf pamoja na ustahimilivu wetu kuliko kutegemea akili nyingi isiyo ya kawaida na maarifa yale yapatikanayo katika vitabu ambayo hayatendewi kazi.

Talanta zote na uwezo wote aliowapa mawakala wake wa kibinadamu, visipotumika, basi, havina faida yo yote kwetu. Kuzirudia njia zile rahisi [za utendaji kazi] kutathaminiwa na watoto na vijana wetu. Kazi ya bustanini na shambani italeta badiliko linalokubalika badala ya kawaida zile zinazochosha sana za masomo ya kinadharia, ambayo akili za watoto wao wadogo zisingejihusisha nayo kwa muda mrefu. Kwa mtoto mdogo aliye dhaifu kiakili, ambaye anaona masomo ya vitabuni kuwa yanamchosha sana, na kwake huwa ni vigumu kuyakumbuka, kazi kama hiyo itakuwa na manufaa ya pekee kwake. Kuna afya na furaha kwa ajili yake katika kujifunza maumbile [viumbe vya asili]; na picha inayozama moyoni mwake haitaweza kufifia, kwa maana mambo hayo yatahusishwa na vitu vile vilivyo mbele ya macho yake daima. ----- Testimonies, Gombo la 6, uk. 178,179. (1900)

Mkiwa na Kipande Kidogo cha Ardhi na Nyumba Nzuri ya Kuishi

Ardhi inapaswa kushughulikiwa mpaka iweze kutoa nguvu yake; lakini pasipo kuwapo mbaraka

wa Mungu haiwezi kutoa kitu. Hapo mwanzo, Mungu aliangalia vyote alivyoviumba, na kusema

kwamba vilikuwa vyema sana. Laana ililetwa juu ya nchi [udongo] kama matokeo ya dhambi.

Lakini, je! laana hiyo izidi kuongezeka kwa kuzidi kufanya dhambi? Ujinga unaendelea kuleta

matokeo yake yanayoleta madhara mengi. Watumishi walegevu [wavivu] wanazidisha maovu kwa tabia zao za kivivu. Wengi hawako tayari kujipatia chakula chao kwa jasho la uso wao, wanakataa kuilima ardhi. Lakini ardhi inazo hazina zake zilizojificha chini kwa ajili ya wale walio na ujasiri na nia na uvumilivu wa kuzikusanya hazina zake hizo. Akina baba na mama walio na kipande cha ardhi na nyumba nzuri ya kuishi, hao ni wafalme na malkia.

Wakulima wengi wameshindwa kupata mavuno ya kutosha kutoka katika mashamba yao kwa

sababu wameichukulia kazi hiyo kana kwamba ni kazi ya kudhalilisha mno; hawatambui kwamba kuna mbaraka ndani yake kwa ajili yao wenyewe na familia zao. Yale yote wanayofahamu wao ni kwamba kazi hiyo ni utumwa wa aina fulani. Mashamba yao ya miti izaayo matunda huachwa bila kutunzwa, mazao hayapandwi kwa majira yake yanayofaa, na kazi ya juu juu tu hufanywa katika kuilima ardhi hiyo. ----- Fundamentals of Christian Education, uk. 326,327. (1894)

Matunda, Mboga za Majani, na Kuku Vyapendekezwa kwa Eneo Moja

Katika ujirani huu kuna eneo kubwa la ardhi isiyokaliwa na watu. Baadhi ya watu wetu wanaoishi katika mazingira ya hali ya hewa iliyosumishwa huko mijini wangeweza kunufaika kwa kujipatia ekari chache za ardhi hii. Wangeweza kujipatia mahitaji yao ya maisha kwa kupanda matunda na mboga za majani na kufuga kuku. Hospitali yetu ingefurahi kununua mayai na mboga za majani kutoka kwao. Natamani kwamba mradi fulani kama huo ungeanzishwa hapa. Baraka kubwa ingewajia wazazi hao pamoja na watoto wao, endapo wangeondoka katika miji hiyo miovu, iliyochafuliwa na kwenda katika sehemu zile za shamba [vijijini]. ----- Letter 63, 1904.

Kuishi Mashambani [Vijijini] - Mbaraka Kwa Maskini

Endapo maskini ambao hivi sasa wamesongamana mijini wangepata makazi yao huko

mashambani [vijijini], wasingeweza kujipatia riziki yao tu, bali wangepata afya na furaha ambayo mpaka sasa hawaijui. Mara nyingi [huko mijini] kazi ngumu, chakula duni, na kubana mno matumizi, shida na umaskini, hiyo ndiyo ingekuwa sehemu ya maisha yao. Lakini ni mbaraka ulioje ambao ungekuwa wao kama wangeondoka mjini, na kuviachilia mbali vishawishi vyake vinavyowaelekeza watu maovuni, kuachana na machafuko yake na uhalifu, huzuni na uchafu wake, na kwenda mashambani [vijijini] kwenye utulivu na amani na usafi.

Kwa wengi miongoni mwa wale wanaoishi mijini ambao hawana hata kipande kidogo cha majani mabichi cha kuweza kuweka miguu yao juu yake, ambao mwaka nenda mwaka rudi wameziangalia nyua zao zilizojaa uchafu na njia zile finyu za vichochoroni, kuta zile za matofali ya kuchoma na sakafu za mawe za kutembea juu yake, mbingu zile zilizojaa vumbi na moshi, ----- kama hao wangepelekwa kwenye wilaya moja yenye mashamba ya kulima, yaliyozungukwa na mashamba ya chanikiwiti, misitu midogo, na vilima na vijito, mbingu safi na zenye hewa safi, na hewa safi ile ya mashambani, basi, kwao hao ingekuwa karibu sawa na [kuishi] mbinguni.

Mawasiliano yao yakiwa yamekatwa kwa kiwango kikubwa hata wasiweze kuonana na watu

wengine wala kuwategemea, tena wakiwa wametengwa mbali na semi zile chafu za ulimwengu

pamoja na desturi zake na misisimko yake, wangeweza kukaribia sana kwenye maana ya ndani

kabisa ya maumbile. Kuwako kwake Mungu kungesikika na kuwa dhahiri sana kwao. Wengi

wangejifunza kwake fundisho lile la kumtegemea yeye. Kupitia katika maumbile hayo angeweza kuisikia sauti yake mioyoni mwao ikiwatamkia amani na upendo wake, na akili na roho na mwili wao vingeweza kuitikia uponyaji huo, ulio na uwezo wa kuwapa uzima. ----- The Ministry of Healing, uk. 190-192. (1905).

Viwanda Vidogo Mbalimbali Kwa Familia Zitokazo Mijini

Waumini wale ambao kwa sasa wanaishi mijini inawapasa kwenda shamba [vijijini], ili wapate

kuwaokoa watoto wao na maangamizi. Mawazo yanapaswa kuelekezwa upande wa kuanzisha

viwanda [vidogo] ambamo familia hizo zinaweza kupata kazi. Wale wanaosimamia kazi ya Shule na wangeona kile kinachoweza kufanywa na taasisi hizo zingeweza kuanzisha viwanda [vidogo] kama hivyo, ili watu wetu wanaotaka kuondoka mijini, waweze kujipatia makazi yao yanayofaa bila kutumia fedha nyingi sana, na pia kuweza kupata kazi huko. Katika sehemu zote mbili na kuna hali nzuri ya ardhi ambayo inatia moyo kuweza kuuendeleza mpango kama huo. Jifunzeni hali ya nchi ilivyo.

Yale yote yanayotakiwa kufanywa hayawezi kuelezwa kinagaubaga mpaka hapo mwanzo

utakapofanywa. Liombeeni jambo hilo, tena kumbukeni kwamba Mungu ameshika usukani,

kwamba yeye ndiye anayeongoza katika shughuli zote za kibiashara. Mahali pale kazi

inapoendeshwa kwa njia inayotakiwa panakuwa fundisho la mfano linalopaswa kuigwa na mahali pengine [patakapofunguliwa]. Pasiwe na ufinyu wo wote [wa mawazo], wala ubinafsi, katika kazi hiyo inayofanyika mahali hapo. Kazi hiyo inatakiwa kuwekwa juu ya msingi rahisi, unaoweza kutekelezwa. Wote hawana budi kufundishwa ya kuwa sio tu kukiri kwamba wanaiamini kweli, kama vile kweli yenyewe ilivyo, bali kuionyesha kweli hiyo kwa mfano katika maisha yao ya kila siku. ----- Letter 25, 1902.

Kazi ya Kuuza Chakula Kiletacho Afya

Shughuli [biashara] hiyo ya [kuuza] chakula kiletacho afya inapaswa kuanzishwa hapa

[Avondale]. Hiyo ingekuwa mojawapo ya viwanda vinavyohusiana na Shule. Mungu ameniagiza

mimi kwamba wazazi wanaweza kupata kazi katika kiwanda hicho, na kuwapeleka watoto wao

shuleni. Lakini kila kitu kinachofanyika hapo kinapaswa kufanywa kwa njia iliyo rahisi sana.

Pasiwepo na ubadhirifu [matumizi mabaya] wo wote katika jambo lo lote lile. Kazi thabiti

inapaswa kufanywa, kwa sababu kazi isipofanywa kwa uthabiti, matokeo yake yatakuwa kazi ya

ovyo ovyo tu. ----- Australasian Union Conference Record, Julai 28, 1899.

Nimekusudia jambo, hili ndilo fundisho ninalotamani sote tulipate. Nitafanya muendelezo wa machapisho ya kitabu kiitwacho TOKENI MIJINI. Kwa kuzingatia umuhim wa huduma katika jamii…sina budi kukichapisha kitabu chote hapa kwa msaada wa www.swahilitruth.com. FUATANA NAMI.Jumamosi, Juni 11, 2011

TOKENI MIJINI... SEHEMU YA TATU


Ombi Wazazi Kwa

Waondoeni Watoto Wenu Mbali na Mahali Penye Maovu

Faida yo yote ipatikanayo kutokana na shughuli za kila siku za maisha haya isiruhusiwe

kuwashawishi wazazi kuacha kuwalea watoto wao. Kila inapowezekana, ni wajibu wa wazazi

kujenga makao yao mashambani [vijijini] kwa ajili ya watoto wao. Watoto na vijana wanapaswa

kulindwa kwa uangalifu. Wangeondolewa na kupelekwa mbali na mahali penye maovu mengi

ambapo panapatikana katika miji yetu. Hebu na wazungushiwe mivuto ile inayopatikana katika

nyumba ya kweli ya Kikristo ----- yaani, nyumba ile anamokaa Kristo. ----- Letter 268, 1906.

Kabla Pigo Lile Halijafurika

Kabla pigo lile halijafurika juu ya wakazi wa dunia hii, Bwana anawaagiza wale walio Waisraeli

kweli kweli kujiweka tayari kwa tukio lile. Kwa wazazi anawapelekea kilio cha onyo, akisema,

Wakusanyeni watoto wenu na kuwaleta nyumbani mwenu; wakusanyeni na kuwatenga mbali na

wale wanaozidharau amri [kumi] za Mungu, yaani, wale wanaofundisha watu uovu na kutenda

uovu. Tokeni nje ya miji mikubwa haraka iwezekanavyo. Jengeni shule zinazoendeshwa na kanisa. Wapeni watoto wenu Neno la Mungu kama msingi wa elimu yao yote. ----- Testimonies, Gombo la 6, uk. 195.

Nimeagizwa na Bwana niwaonye watu wetu wasikimbilie kwa wingi mijini ili kujijengea makazi

humo kwa ajili ya familia zao. Kwa akina baba na akina mama nimeagizwa kusema maneno haya, Msikose kuwatunza watoto wenu ili wabaki ndani ya maeneo ya nyumba na viwanja vyenu. -----Manuscript 81, 1900.

Roho za Watoto Wenu au Maisha Rahisi na Starehe Zenu

Ninyi msiendelee tena kuwaweka watoto wenu mahali pale watakapokabiliana na majaribu

yaliyomo mijini, miji ambayo imefikia kilele chake cha kuangamizwa. Bwana ametuma onyo lake kwetu pamoja na ushauri wake ili tutoke mijini. Basi na tusiendelee kuweka vitega uchumi zaidi katika miji hiyo. Akina baba na mama, mnazifikiriaje roho za watoto wenu? Je! Mnawatayarisha waliomo nyumbani mwenu kwa kunyakuliwa kwenda katika majumba yale ya kifalme kule mbinguni? Je! mnawaandaa hao kuwa miongoni mwa familia ile ya kifalme? yaani, watoto wa Mfalme yule wa mbinguni? "Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?" [Mathayo 16:26.] Mtalinganishaje maisha rahisi, starehe,hali ile yenye manufaa isiyo na wasiwasi [iliyomo humo mijini] na thamani ya roho za watoto wenu? -----Manuscript 76, 1905.

Tabia za Kikristo Zinajengeka Vizuri Zaidi Katika Maeneo ya Upweke

Hakuna hata familia moja katika mia ambayo ikiendelea kukaa mjini itakuwa na maendeleo

mazuri kimwili, kiakili, au kiroho. Imani, tumaini, upendo, furaha, vinaweza kupatikana kwa vizuri zaidi katika mahali pa upweke, ambapo pana mashamba na vilima na miti. Nendeni na watoto wenu mbali na mambo yale yanayoonekana waziwazi [tamasha] na sauti za mjini, mbali na makelele ya magari yanayopita mitaani pamoja na makundi ya watu, hapo ndipo akili zao [watoto wenu] zitakuwa na afya zaidi. Itaonekana kuwa ni rahisi zaidi kwao kuikumbuka mioyoni mwao kweli ile ya Neno la Mungu. ----- Manuscript 76, 1905.

Wapelekeni watoto wenu kwenye shule zile zilizomo mjini, ambako kila aina ya majaribu

huwangojea ili kuwatamanisha na kuwadhalilisha, ndipo kazi ile ya kujenga tabia itakuwa ngumu mara kumi kwa pande zote mbili, yaani, kwa wazazi na kwa watoto. ----- Fundamentals of Christian Education, uk. 326. (1894)

Kimbilio Katika Maeneo ya Mashambani

Wazazi na waelewe ya kwamba malezi ya watoto wao ni kazi ya maana katika kuziokoa roho zao. Katika maeneo yale ya mashambani [vijijini] mazoezi ya viungo mengi ya kufanya yenye manufaa [kiafya] yatapatikana kwa kufanya mambo yale yanayopaswa kufanywa, ambayo yatawapa afya ya kimwili kwa kuzikuza neva zao na misuli. Tokeni mijini, huo ndio ujumbe wangu kwa ajili ya kuwalea watoto wetu katika maadili mema.

Mungu aliwapa wazazi wetu wale wa kwanza njia ya elimu ya kweli alipowaagiza kuilima ardhi

na kuyatunza makao yao katika Bustani ile. Baada ya dhambi kuingia, kutokana na utovu wao wa utii kwa matakwa yake Bwana, kazi iliyofanyika kuilima ardhi ikawa imeongezeka sana, maana nchi, kutokana na laana ile, ikazaa magugu na michongoma. Lakini kazi ile yenyewe haikutolewa kwao kwa sababu ya dhambi. Bwana Mkuu Mwenyewe akaibarikia kazi ile ya kuilima ardhi.

"KAMA VILE ILIVYOKUWA ... SIKU ZA NUHU"

Ni kusudi lake Shetani kuwashawishi wanaume na wanawake kwenda mijini, isitoshe, ili kufikia

lengo lake anavumbua kila namna ya mambo mapya [mitindo mipya] na burudani, kila aina ya

mambo ya kusisimua. Na miji ya ulimwengu wa leo inageuka na kuwa kama ilivyokuwa miji ile

kabla ya Gharika. Daima tungebeba mzigo huo [wa kujihadhari] tunapoyaona maneno hayo ya Kristo yakitimia, "Kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu." Mathayo 24:37. Katika siku zile kabla ya Gharika, kila aina ya burudani ilibuniwa ili kuwafanya wanaume na wanawake kuwa na usahaulifu [wa mambo ya Mungu] na kutenda dhambi.

Leo hii, mwaka huu wa 1908, Shetani anafanya kazi yake kwa nguvu nyingi, ili hali zile zile zipate kuwapo. Nao ulimwengu unazidi kuwa mwovu. Uhuru wa dini hautaheshimiwa sana na wale wanaojiita Wakristo, kwa kuwa wengi wao hawayajui kabisa mambo ya kiroho.

Hatuwezi kushindwa kuona ya kwamba mwisho wa ulimwengu huu karibu sana unakuja. Shetani anafanya kazi yake katika mioyo [mawazo] ya wanaume na wanawake, na wengi wanaonekana kana kwamba wamejazwa na tamaa ya kupata burudani na misisimko. Kama vile ilivyokuwa katika siku zile za Nuhu, kila aina ya uovu inazidi kuongezeka. Kwa wakati kama huu, watu wale wanaojaribu kuzishika amri [kumi] za Mungu wangetafuta mahali pa upweke [pa kuishi] mbali na miji hiyo....

SI HASARA KWENU

Ni nani basi atakayeonywa? Tunarudia tena kusema, Tokeni Mijini. Msidhani kwamba ni hasara

kubwa sana kwenu, kwamba ni lazima kwenda vilimani na milimani, bali tafuteni mahali pale pa

upweke [ukimya] ambapo mnaweza kuwa na Mungu peke yenu, mkijifunza mapenzi yake na njia yake....

Ninawasihi watu wetu kuifanya iwe ndiyo kazi yao ya maisha kutafuta maisha yao ya kiroho.

Kristo yu mlangoni. Hii ndiyo maana nawaambia watu wetu, Msifikirie ya kuwa ni taabu

mnapoitwa kuiacha miji na kuhamia katika maeneo ya shamba [vijijini]. Huko mibaraka mingi

inawangojea wale watakaoishikilia. Kwa kuziangalia mandhari zile [sura za nchi] za maumbile,

yaani, kazi ile ya Muumbaji, kwa kujifunza kazi ya mikono yake [uumbaji wake] Mungu, bila

kujitambua mtabadilishwa na kufanana naye. ----- Manuscript 85, 1908.

Kujipatia Matunda Bora Kabisa ya Maisha Haya

Jengo la gharama nyingi, fanicha iliyonakishiwa sana, mapambo, anasa, na raha, mambo hayo

hayaleti hali zile zilizo za muhimu kwa maisha ya furaha, yenye manufaa. Yesu alikuja hapa

duniani kufanya kazi kubwa sana iliyopata kufanywa miongoni mwa wanadamu. Alikuja kama

balozi [mjumbe] wa Mungu, kutuonyesha sisi jinsi ya kuishi ili tuweze kujipatia matunda bora

kabisa ya maisha haya. Ni hali [mazingira] gani basi zilizochaguliwa na Baba yetu wa milele kwa ajili ya Mwanawe?

Ni nyumba ile iliyokaa mahali pale pa upweke [kimya] katika vilima vile vya Galilaya; nyumba iliyopata mahitaji yake kwa kazi ya uaminifu, yenye heshima; maisha yale ya kawaida; kupambana kila siku na matatizo pamoja na shida; kujikana nafsi, matumizi mazuri ya kipato chao, na huduma yao iliyotolewa kwa moyo wa uvumilivu na furaha; saa ile ya kujifunza kando ya mama yake, wakiwa na gombo la Maandiko lililofunguliwa wazi; macheo yale tulivu au utusitusi ule wa asubuhi katika bonde lile la majani mabichi; huduma takatifu ya maumbile yale; kujifunza uumbaji na maongozi ya Mungu; na moyo wake kuwasiliana na Mungu, ----- hizo zilikuwa ndizo hali [mazingira] na nafasi nzuri za maisha ya mwanzo ya Yesu.

WAKUU NI URITHI UTOKANAO NA MAISHA YA SHAMBA

Hivyo ndivyo ilivyo kwa sehemu kubwa ya watu walio bora na wakuu katika vizazi vyote. Someni historia ya Ibrahimu, Yakobo, na Yusufu, na ya Musa, Daudi, na Elisha. Jifunzeni maisha ya watu wa nyakati zilizofuata baadaye waliostahili kabisa kuzijaza nafasi zile za amana na madaraka, watu ambao mvuto wao umekuwa na mafanikio makubwa sana katika kuuinua juu ulimwengu huu.

Ni wangapi miongoni mwa hao walilelewa katika makazi ya mashambani [vijijini]. Hawakuijua

anasa hata kidogo. Hawakuutumia ujana wao katika burudani. Wengi walilazimika kupigana na

umaskini na shida. Walijifunza mapema kufanya kazi [kwa mikono yao], na maisha yao ya

kujishughulisha sana katika maeneo yale yaliyo wazi yaliwapa nguvu za kimwili na kupanuka kwa uwezo wao kiakili. Wakiwa wamelazimika kutegemea rasilimali [nyenzo] zile walizokuwa nazo, walijifunza kupambana na shida na kuvishinda vipingamizi, tena walijipatia ujasiri na uvumilivu. Walijifunza masomo ya kujitegemea na kujitawala nafsi zao.

Wakiwa wamekingwa kwa kiwango kikubwa mbali na marafiki wabaya, walitosheka na furaha za kawaida na urafiki mzuri ujengao. Katika uchu wao wa chakula walifuata chakula cha kawaida na kuwa na kiasi katika mazoea yao. Walitawaliwa na kanuni, tena walikua wakiwa safi [wakiwa na mwenendo mzuri], wakiwa na nguvu na unyofu wa moyo. Walipotakiwa kufanya kazi zao za maisha, walikwenda wakiwa na nguvu za kimwili na kiakili, wakiwa na moyo uliochangamka, na uwezo wa kupanga mipango na kuitekeleza, tena wakiwa na uthabiti wa kuyapinga maovu, mambo ambayo yaliwafanya kuwa na uwezo dhahiri wa kutenda mema ulimwenguni.

BORA KULIKO UTAJIRI

Bora kuliko urithi mwingine wo wote mnaoweza kuwapa watoto wenu itakuwa ni zawadi ile

mtakayowapa ya mwili wenye afya, akili timamu, na tabia nzuri. Wale wanaojua kile kinacholeta

ufanisi wa kweli katika maisha haya mara nyingine watakuwa na busara. Wataweka mbele yao

mambo yale yaliyo bora kwa namna watakavyochagua makazi yao.

Badala ya kuishi mahali pale ambapo kazi za wanadamu zinaweza kuonekana waziwazi, penye

tamasha na sauti zinazoamsha mawazo machafu, mahali pale ambapo misukosuko na ghasia huleta uchovu na wasiwasi, nendeni mahali ambako mnaweza kuangalia kazi za [uumbaji wa] Mungu.

Jipatieni pumziko la nafsi zenu katika uzuri na utulivu na amani ya maumbile [viumbe vya asili]. Jicho lenu na liangalie mashamba ya chanikiwiti, vijisitu, pamoja na vilima. Angalieni mbingu ile ya samawi, isiyozuiwa na vumbi na moshi wa mjini hata isiweze kuonekana, vuteni hewa ile ya mbinguni inayowatia nguvu. Mbali na mambo yale yaliyomo mjini yanayovuta mawazo yenu na kuyatawanya, nendeni pale mnapoweza kukaa kirafiki na watoto wenu, mnapoweza kuwafundisha ili wapate kujifunza habari za Mungu kwa njia ya kazi zake [uumbaji wake], na kuwalea ili wawe na maisha ya unyofu na yenye manufaa [kwao wenyewe na kwa wengine]. ----- The Ministry of Healing, uk. 265-267. (1905)

Faida Nyingi za Shughuli Zinazofanyika Nje

Lingekuwa ni jambo jema kwenu kuweka kando masumbufu yenu yanayowafadhaisha, na kupata mahali pa faragha huko shamba [vijijini], ambako hakuna mvuto wenye nguvu wa kuyaharibu maadili ya watoto na vijana wenu.

Ni kweli, hamtaweza kuondokana kabisa na maudhi yote pamoja na masumbufu yanayofadhaisha; lakini kule mgeweza kuyaepuka maovu mengi na kufunga mlango dhidi ya gharika ya majaribu yanayotishia kuyatawala kabisa mawazo ya watoto wenu. Wanahitaji kazi ya kufanya na mambo mbalimbali tofauti ya kushughulika nayo. Mambo ya jinsi ile ile waliyozoea kufanya nyumbani mwenu huwafanya wasiwe na raha [huwakinai], na kuwa watukutu, kisha wanajiingiza katika tabia ile ya kujichanganya pamoja na vijana wale waovu wa mjini, hivyo hujipatia elimu ya mitaani huko....

Kuishi huko shamba [vijijini] kungewaletea [watoto na vijana] manufaa mengi sana; maisha yao

ya shughuli nyingi nje ya nyumba yangekuza afya yao kiakili na kimwili. Wawe na bustani ya

kupalilia, ambamo watapata furaha na kazi yenye manufaa kwao. Kuitunza mimea na maua kuna

mwelekeo wa kukuza akili za kupambanua mema na mabaya pamoja na kuwa na busara, na wakati uo huo ufahamu wao kuhusu uumbaji mzuri na wenye manufaa wa Mungu una mvuto kwao unaowabadilisha na kuwafanya wawe waungwana katika mawazo yao, wakiuhusisha [uumbaji huo] na Muumbaji na Bwana huyo wa vyote. ----- Testimonies, Gombo la 4, uk. 136. (1876)

Tusitazamie Mwujiza Wo Wote Kuigeuza Njia Yetu Mbaya

Nayaangalia maua haya, na kila wakati ninapoyaangalia nafikiria juu ya Edeni. Hayo yanaonyesha upendo wa Mungu alio nao kwetu. Hivyo anatupatia sisi katika dunia hii mwonjo mdogo tu wa Edeni ile. Anatutaka sisi kufurahia vitu vizuri alivyoviumba, na ndani yake kuona sura [picha] ya kile anachotaka kutufanyia sisi.

Anatutaka sisi kuishi mahali pale palipo na nafasi tele. Watu wake hawatakiwi kusongamana

mijini. Anawataka waende na familia zao nje ya miji, ili wapate kujiandaa vizuri kwa ajili ya uzima ule wa milele. Kitambo kidogo [kilichobaki] watalazimika kuondoka mijini.

Miji hiyo imejaa uovu wa kila namna, ----- pamoja na migomo na mauaji na watu kujiua wenyewe. Shetani yu ndani yake [miji hiyo], akiwaongoza watu katika kazi yao ya maangamizi. Chini ya mvuto wake wanaua kwa sababu tu ya kuua, na kitendo hicho wataendelea zaidi na zaidi kufanya....

Tukijiweka wenyewe chini ya mivuto ile mibaya iliyokatazwa, je! tutazamie kwamba Mungu

atafanya mwujiza wo wote wa kuigeuza njia yetu hiyo mbaya? ----- La, hasha. Tokeni mijini

haraka iwezekanavyo, na kununua sehemu ndogo ya ardhi [vijijini], ambako mnaweza kuwa na

bustani, mahali ambako watoto wenu wanaweza kuyaangalia maua yakuapo, na kujifunza kwayo

mafunzo ya kuwa na maisha ya kawaida na usafi wa moyo. ----- General Conference Bulletin,

Machi 30, 1903.

----------------------------------------------------------

Ndugu msomaji: MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Oldest Living Quartet - (Gaither Homecoming)

Wanapotwambia:Nimekusudia jambo, hili ndilo fundisho ninalotamani sote tulipate. Nitafanya muendelezo wa machapisho ya kitabu kiitwacho TOKENI MIJINI. Kwa kuzingatia umuhim wa huduma katika jamii…sina budi kukichapisha kitabu chote hapa kwa msaada wa www.swahilitruth.com. FUATANA NAMI.