Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Septemba 22, 2011

Elimunafsia...(Saikoojia)

 ...Pia: kutoka Kigiriki  psikhologia.
Elimunafsia ni fani ya elimu jamii inayolenga kujua nafsi ya binadamu ili kurahisisha ukomavu wake na uhusiano wake na wenzake.



Kujifahamu
Hakuna mtu wa jana, leo au kesho aliye sawasawa na mwingine: kila mmoja ni wa pekee. Mungu ametufanya tofauti ili tutimilizane. Kila mmoja anahitaji wengine, na kila mmoja ni muhimu kwa wenzake. Katika maisha ya jamii kuna sehemu ambayo yeye tu anaweza kuijaza. Wazo hilo linaweza kumsaidia kijana ambaye ni mwepesi kukata tamaa na kujitupa. Daima uhai ni zawadi nzuri kwa mhusika na kwa wenzake wote. Kijana ni zawadi yenye nguvu na wema hata kwa [[taifa, kiasi kwamba kujali ustawi wa kijana ni kujenga taifa. Tunataka kujifahamu tulivyoumbwa (mwili, nafsi na roho, ambavyo vyote vinafungamana ndani mwetu):
1. ili tuweze kujithamini hasa kwa kuona sisi ni nani mbele ya Mungu;
2. ili tufahamu mipaka yetu na kuikabili inavyofaa;
3. ili tufahamu vipawa tulivyojaliwa tuwashirikishe wenzetu;
4. ili tubadilike kuwa bora zaidi na kuchangia ustawi wa jamii;
5. ili tuhusiane vizuri zaidi na wenzetu;
6. ili tuweze kujieleza kwa watu fulanifulani na kupata mashauri ya kutufaa.

Kujikubali

Daima ni muhimu tukubali hali ilivyo, halafu tujitahidi kuifanya bora zaidi. Tusipojikubali kwanza tutahangaika tu hata kukata tamaa. Wajue wasijue vijana wapokua wanashindwa kujikubali walivyo. Pengine wanaficha silika zao wasitambulikane na watu, hata wakashindwa kujielewa, wakapatwa na vilema vya ukuaji pia. Ni lazima waache kujifunika uso kwa vinyago hivyo; badala yake wakabili ukweli wao, wenye sifa na kasoro. Hivyo tu watapitia vizuri mabadiliko ya ujana upande wa mwili, nafsi, jamii, maadili na roho. Hatimaye watakomaa na kushika nafasi yao maishani. 

Kwa kila mtu ni muhimu kuwa na marafiki; hasa kijana anahitaji kikundi. Lakini hiyo isiwe njia ya kukwepa nafsi yake mwenyewe wala ya kuficha tabia yake kwa kuzungumza, kutembea au kutenda namna fulani wanavyofanya wenzake. Kwa hiyo asijifananishe nao. Kila mtu anakua kwa namna yake, akibadilika kwa kiasi tofauti na muda tofauti. Ni lazima ajifunze kuyapokea mabadiliko hayo pia yanayomfanya geugeu sana, hasa msichana katika mzunguko wake wa kila mwezi: mara anaonekana jasiri au korofi, mara amejaa wasiwasi.

 Kujistawisha

Uhai unasukuma kiumbe chochote kistawi. Mimea inakua namna yake, wanyama namna yao, na binadamu polepole zaidi kwa kuwa ndiye kiumbe bora anayehitaji kukomaa pande zake zote. Kulingana na haja yetu ya kukomaa hivyo, sio tu kufikia umri au kimo fulani, ndani mwetu zimo nguvu zinazotuhimiza tujilinde ili tuzidi kuishi wenyewe, tuendeleze uhai tulionao kwa kuzaa, tujitegemee (yaani tumiliki maisha yetu), tutawale vitu na watu ili mambo yaende tunavyotaka, n.k. Haja iliyoota mizizi mirefu ndani mwetu ni ile ya kujikamilisha tusiwe watu wanaoishi ili mradi tu. Kadiri tunavyokua tunajisikia kuwajibika. Haja hizo zinafanya tujiwekee pia malengo katika utendaji. Basi, baada ya kujifahamu, kila mmoja wetu achague na kuazimia awe bora vipi, kwa sababu wenyewe tunaamua tuweje. 

Ni wajibu wetu kujipenda na kwa hiyo kujitunza na kujistawisha kimwili, kinafsi, kijamii, kimaadili na kiroho. Kazi hiyo inahitaji nia na bidii za kudumu. Tufuate taratibu za kulinda afya ya mwili, heshima ya mavazi, usafi wa mazingira. Tujiepushe na uvivu unaosababisha mawazo na matendo mabaya. Tujihadhari na maandishi, picha na maneno yasiyofaa, yasije yakatupotosha kimawazo au kusisimua ashiki. Tuhusiane vema na wengine (adabu, lugha nzuri n.k.). Hasa tufuate dhamiri na kustawisha roho iliyo sehemu bora ya utu wetu ambamo tunashirikiana na Mungu. Mbali ya motisha kutoka nje (yaani kupewa tuzo au adhabu), sisi binadamu tuna maarubu yanayotuongoza kwa ndani na kututia nguvu tutende namna fulani na kukwepa mambo mengine. Yanaweza kuwa ya aina mbalimbali: 

1.         tusiyofundishwa kwa kuwa ni haja za mwili (kupumua, kunywa, kula, kujisaidia, kupumzika, kutumia jinsia n.k.) au haja za nafsi (kupendwa, kufungamana, kukubaliwa, kufanikiwa, kujitokeza, kusaidia, kushindana, kushinda, kutawala, kujihami, kuwa salama, kuongozwa, kujishusha, kujitawala, kumiliki, kupanga, kubadili, kujua, kuhemka, kujamiiana, kucheza); 

2.         yaliyorithiwa kwa wazazi na ukoo (silika, maelekeo, vipawa n.k.); 

3.          ya kujipatia, yaani tusiyozaliwa nayo, ambayo tunayapata maishani mwetu hasa kutoka kwa watu wanaotuzunguka (mazoea, mila, tunu, imani n.k.). Maarubu hayo yanasaidia kukua na kuelekea ukomavu, yaani hali ya kuwa jinsi Muumba alivyokusudia kisha kupitia hatua kadhaa.

Jumanne, Septemba 20, 2011

Hivi Ni lazima Wazazi, Walimu na Viongozi wa Dini wawalinde vijana wakati wote?


Nchini kwangu, wazazi wangu wamefanya kazi miaka mingi, walimu na viongozi wa dini katika kuwaongoza vijana kutoka katika vitendo vya utumiaji nguvu na uhalifu kwenda katika maisha ya kuwahudumia wengine. Kwa kawaida vijana hupendelea kujitoa kikamilifu katika kutekeleza lengo fulani au kuwa sehemu ya kundi fulani. Hamasa hii inaweza kuwa jambo zuri kwa jamii pale ambapo vijana wanajitoa kikamilifu katika kuhudumia familia zao, taifa lao na imani yao na kuwahudumia masikini, wagonjwa na kuwatumikia watu kibinaadamu kwa njia nyingi tofauti.
 Hamasa ya vijana kupenda kuwa sehemu ya kundi fulani huweza kuleta matokeo mazuri pale kundi hilo linapokuwa na malengo mazuri. Hata hivyo, tabia hii ya vijana kupenda kujihusisha na lengo au kundi fulani inaweza kutumiwa vibaya na kuwafanya vijana kujitumbukiza katika vitendo viovu na uhalifu. Kuna mifano mingi duniani kote ambapo vijana wameongozwa na kuhamasishwa na wanasiasa wenye malengo mabaya na ya kibinafsi, makundi ya kihalifu au yale yenye imani kali kufanya uhalifu wa kutisha (Rwanda mwaka 1994, Kenya mwaka 2007).
------------------------------------------------
Na sasa tuelekee katika hoja ambayo ndio msingi mkuu wa kipindi hiki, pamoja na yote hayo niliyoyaeleza kwa ufupi, kuna baadhi ya vijana bado wanawaza namna ya kujikomboa kutoka katika lindi la umasikini.
------------------------------------------------


MADA

Hivi Ni lazima Wazazi, Walimu na Viongozi wa Dini wawalinde vijana wakati wote?

------------------------------------------------

Mwaka 1978 huko Marekani, Bwana mmoja aliyejiita "Mchungaji" Jim Jones alianzisha dhehebu (cult) ambalo lililokuwa likifuata baadhi ya mafundisho katika imani ya Kikristo na msimamo mkali wa kisiasa. Wafuasi wake walifanya maovu mbalimbali ikiwemo mauaji, udanganyifu wa kughushi nyaraka na wizi. Hatimaye, kwa amri yake, zaidi ya waumini 900 walijiua katika makazi yao huko Guyana.
Siwezi kabisa kulihusianisha dhehebu la Jones na Ukristo, japokuwe yeye alidai kuwa ni kiongozi wa Kikristo. Vivyo hivyo, ninakataa kuhusianisha madhehebu au viongozi wanaowatuma waumini wao kufanya mauaji na Uislamu. Viongozi na makundi haya yanatumia jina la mojawapo ya dini adhimu kabisa kwa mwanadamu yenye historia iliyotukuka ya ustaarabu, elimu na Amani na kupotosha mafundisho yake ili kuwalaghai vijana na wengine kufanya mauaji na uharibifu badala ya kutengeneza na kujenga.
------------------------------------------------

Kuna baadhi ya wasichana waliopata virusi hivyo kutokana tamaa za kutaka kuishi maisha ya gharama na fahari kubwa, kwa hiyo wakalazimika kufanya ngono na wanaume wenye fedha ambao ni waathirika.

Wapo walioathirika baada ya kufanya ngono na watu ambao hawana fedha za kutisha, bali walijiingiza katika mahusiano na watu hao pengine kwa bahati mbaya au kwa sababu ya vishawishi vidogo vidogo, huku wengine wakiwa wameathirika na Ukimwi baada ya kufanya biashara ya uchangudoa katika maeneo mbalimbali.

Baada ya kusadifu yote hayo, nahitimisha kwa kuwaomba vijana wenzagu,  na watanzania wenzangu kwamba pamoja na haraka waliyonayo kuna haja ya kusubiri na waitazame Serikali kama kweli itatekeleza na kutimiza maazimio yake hata kama itatugharimu miaka mingi.
------------------------------------------------

Katika kundi hilo kuna kila aina ya vijana; kuna waliosoma na kutunukiwa vyeti, stashahada, shahada na shahada za juu, huku wengine wakiwa ni mbumbumbu kabisa kwa maana hawakwenda shule na kuna walioishia darasa la tatu, tano na la saba.
Kimsingi, wako tofauti lakini linapokuja suala la kuukimbia umasikini fikra zao zina fanana kwa kiwango kikubwa kwani mawazo yao makuu  yanawiana kwa namna moja ama nyingine.
Kwa mfano, kuna kijana anayehitaji mtaji wa Shilingi milioni mbili ili aweze kufanya biashara zitakazomsaidia kupunguza hali ngumu ya maisha aliyonayo, na wakati huyo akiwa hivyo kuna kijana mwingine anahitaji Shilingi elfu tano tu, ili aende Tandale kununua mahindi mabichi ambayo atakuja nayo mtaani tayari kwa kuyachoma kisha ayauze.
…kama nilivyosema mwanzo kwamba fikra zao zinafanana ila michakato na michanganuo yao ndio inatofautiana, kwani mmoja anahitaji mtaji mkubwa ili aweze kuendesha shughuli zake wakati mwingine anahitaji mtaji mdogo ili naye aendeshe shughuli zake.
katika kundi lolote lile la vijana iwe wasichana au wavulana kuna ambao hawataki kusubiri, wenyewe kila wakati wana haraka, wanataka wafanikiwe na wafikie kilele kama ilivyo kwa matajiri wengine.
------------------------------------------------

Hatua Za Vitendo Zinahitajika Kuelimisha

Uchambuzi:
Tunaweza sasa kujimudu kama kila tulilokuwa tunaambiwa ni bora, ili mradi litoke magharibi, watu wengi walilikubali na kuliingiza katika mfumo. 

Ayi Kwei Armah, alisema tena linaingizwa hata kama wanasiasa hawajalielewa vizuri. Nasema hivi kwa sababu;
Jambo jipya linaletwa na nchi zilizoendelea (nchi za magharibi) Lakini wanatulazimisha sisi wananchi tulipokee. Kushinikizwa tuukubali ushoga ama na mambo mengine ni matokeo ya tabia ya kukubali kwetu kila kitu.
                                                                                                                          Hasara ya Mwafrika wa leo na Mtanzania ni kukosa anachoweza kujivunia kama itikadi yake, elimu yake, dini yake, mila na desturi yake:
                                                                                                                   Mwafrika anaonekana akiwa mbioni kuukimbia utu wake, na kila kinachofungamana na hicho eti  afananane na umagharibi. 

Wamagharibi wamefanikiwa kutufanya nusu watu!!
------------------------------------------------

Hebu fikiri kuhusu thamani, neno thamani pekee linavyosikika masikioni na hata linavyotamkika. Linganisha na kitu ama kifaa chochote chenye sifa hiyo.

------------------------------------------------

Kila siku ni ya heka heka ndani ya jiji la Dar es salaam.

Ni rahisi kufikiri kwamba wale wanaowatumikisha vijana na watoto wanawasaidia, lakini kama ni hivyo wengine wasingeishia kuchoma mishikaki na vitumbua na kuhifadhi pesa peke yao.
------------------------------------------------

Jumamosi, Septemba 17, 2011

INJILI...MAJIBU YAFANYAYO KAZI.

Injili ni neno lenye asili ya Kigiriki linalotafsiriwa Habari Njema, yaani habari ya Yesu Kristo kufa na kufufuka.
Jina hilo linatumika pia kuhusu vitabu vinavyoeleza maisha na mafundisho ya Yesu kufuatana na kile cha Mtakatifu Marko ambacho kwa wataalamu wengi ndiyo Injili iliyowahi kuandikwa (65-70 B.K.)
Kati ya vitabu vyote vya namna hiyo, Ukristo tangu karne II unakubali vile vinne vya kwanza tu, ambavyo viliandikwa wakati wa Mitume wa Yesu.
Hivyo vinashika nafasi ya kwanza katika orodha ya vitabu vya Agano Jipya kama ifuatavyo: Injili ya Mathayo, Injili ya Marko, Injili ya Luka na Injili ya Yohane.
Injili tatu za kwanza zinafanana kwa kiasi kikubwa katika mpangilio, habari na maneno yenyewe, na kwa sababu hiyo zinaitwa Injili-Ndugu. Kadiri ya wataalamu wengi mfanano unatokana na kwamba Injili ya Marko ilitumiwa na waandishi wa zile nyingine.
Ile ya Mtume Yohane ni ya pekee na inategemea ushahidi wa Mtume ambaye alipendwa zaidi na Yesu akamfuata kiaminifu hadi msalabani.
Vinahesabiwa na Wakristo kuwa moyo wa Maandiko Matakatifu yote (Biblia) yanayotunza ufunuo wa Mungu, kwa kuwa ndivyo shuhuda kuu juu ya Neno aliyefanyika mwili.
Vile vingi vilivyoandikwa kuanzia karne II havitumiwi na Kanisa katika kufundisha imani na katika liturujia. Vinaitwa kwa kawaida apokrifa yaani za bandia.
Waislamu wanakiri Injili kuwa iliteremshwa toka mbinguni kwa nabii Isa, lakini hawakubali vitabu 4 vya Wakristo kama vilivyo.

Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)
Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Golden Gate Quartet

Wanapotwambia: 

Early Songs

 

Au tufanye jambo mbadala kwa ujumbe huu usemao: "Nobody knows the troubles I've seen" kutoka kwa hawa waimbaji waitwao Negro spiritual (1982)