Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Februari 28, 2012

VITA VYA HAR-MAGEDONI




Jina “HAR-MAGEDONI” hushtua kwa hofu na kuashiria hatari katika mawazo ya wengi. Wengine wanadhani ni vita kuu ya ulimwengu kuzunguka Mashariki ya Kati. Wengine hutazamia Mpinga Kristo akipigana ili kupata ukuu wa ulimwengu wote. Na bado wengine hawajui nini cha kuamini au kutegemea. Neno “Har-Magedoni” lenyewe  utafsiriwa “jina la alama” (angalia Strong's Exhaustive Concordance, #717). Na bado Maandiko hayafundishi kwamba kutakuwepo vita halisi vinatakavyohusisha ulimwengu wote! Vita hii na mapambano havitapiganwa kwa kutumia silaha halisi, kama bunduki, mizinga, ndege za vita, au majeshi yenye silaha.

Lakini vitapiganwa, tayari vimeanza kupiganwa, na vitaendelea kupanuka kwa nguvu zaidi mpaka kila mtu katika ulimwengu anahusishwa. “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote; kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake. Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.” Ufunuo16:13-16.

Kama inavyoweza kuonekana, Maandiko hufundisha kwamba vita hivi vinapiganwa kati ya majeshi makuu mawili: Mungu, Kristo na wafuasi wake wasafi au wenye haki, dhidi ya Ibilisi, roho za uovu, na wafuasi wake wachafu au waovu. Kwa hiyo vita vya Har-Magedoni ni alama inayoeleza pambano kuu na mgongano unaondelea kwa nguvu kati ya Mungu na Shetani--kati ya ukweli na ufisadi. Na vita hivi vya kiroho hatimaye vitahusisha kila mtu katika dunia kwani kila mmoja lazima aamue nani wa kufuata--Kristo na ukweli, au Ibilisi na ufisadi: uzima wa milele pamoja na Kristo, au maangamivu milele pamoja na Shetani. Vita hivi na mapambano kati ya Kristo na Shetani vilianza mbinguni.

“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahalipao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na
malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufunuo 12:7-9. Hata kama Ibilisi alitupwa kutoka mbinguni, aliendelea na mapambano yake dhidi ya Kristo na Mungu katika dunia hii. Kwa karibu miaka elfu sita mgongano huu umeendela na kuzidi kupanuka. Lakini vita vya mwisho vya kupiganwa katika pambano hili kuu, kilele ambacho matukio yote yamekuwa yanaelekeza, ni kile ambacho Biblia hufafanua kama siku kuu ya Mungu Mwenyezi--vita vya Har-Magedoni.

Vita hivi vya mwisho kati ya ukweli na ufisadi vinaonyeshwa wazi katika Ufunuo sura zifuatazo 12, 13, 14, & 18. Na wanadamu wote wameingia katika vita hii leo. Kutokana na kwamba Har-Magedoni ni alama inayoeleza vita vya kiroho kati ya ukweli na ufisadi, ni silaha gani ambazo Ibilisi anatumia katika pambano hili kuu? Vitu vinavyofananishwa na vyura vilitoka katika kinywa cha Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo. Sasa vyura hukamata mawindo yao kwa kutumia ndimi zao, na kinachotoka katika vinywa vyao ni maneno yanayopangiliwa pamoja katika misingi ya imani. Kwa hiyo hawa viumbe watatu hukamata mawindo yao kwa kusema au kufundisha mafundisho mbalimbali ya ufisadi.

Kwa wale wanaotamani kumfuata Kristo na ukweli, ni kitu cha maana sana kwamba tuweze kupambanua wazi nani ni Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo kusudi tuweze kuepuka kudanganywa kwa mafundisho mbalimbali ya uongo na hivyo kupotea. Kama ilivyodhihirishwa katika Ufunuo 12, Joka kimsingi ni Shetani. Na kauli gani za misingi ya makosa na mafundisho ya uongo zimetoka katika kinywa cha Shetani? Mafundisho mbalimbali ya umizimu, upagani, na uchawi ambayo falme za ulimwengu zimejengwa juu yake--ikiwa ni pamoja na Himaya ya Kirumi ya kipagani ya zamani. Wakati wengi wanaamini upagani kuwa kitu cha zamani, bado kuna mamilioni leo wanaojihusisha na imani zake za kikafiri na ibada ya Ibilisi.

Ishara za awali za dini ya kipagani ni kuabudu vitu vya asili. Kutokana na kwamba umbo lililo juu zaidi katika asili ni mwili wa binadamu, na hasa mawazo, mwanadamu anaongozwa kuabudu nguvu za mawazo na hivyo kuinua maoni ya mwanadamu juu ya ufunuo wa Mungu. Mamlaka zote kuu zilizotawala dunia zilidhihirisha ukweli kwamba katika upagani, Kanisa na serikali havikutengana--lakini vilikuwa vimeungana pamoja. Katika Babeli, Umedi-
Uajemi, Uyunani, na Rumi, serikali mara zote ilitumiwa kuunga mkono na kutoa nguvu kwa dini ya kipagani ya wakati huo. Majira na tena sheria zilipitishwa na mamlaka ya serikali ili kutumika kulazimisha kuabudu miungu ya kipagani na mafundisho ya uongo.

Leo, kama ilivyokuwa katika nyakati za zamani, roho ya kuinua na kuabudu maoni ya mwanadamu, taasisi, na Kanisa na serikali ili kusudi Kanisa liweze kupatiwa nguvu kupitisha maamuzi na mafundisho yake makuu, ni roho ya Joka. Na roho hii itaongezeka zaidi na zaidi kwa kujulikana mpaka itakapoishia katika kipindi kikuu cha taabu kwa watu wa Mungu. Siyo roho hii tu ya uchafu ambayo inafanya kazi leo kupitia nadharia ya kibinadamu na falsafa zingine za ubatili-- kumwinua mwanadamu juu ya Mungu, kuinua ufisadi juu ya ukweli--lakini kuna roho nyingine ya pili ambayo inatoka kwenye kinywa cha Mnyama.

Katika Ufunuo 13, Mnyama ambaye aliinuka kutoka kwenye mabaki ya Roma ya kipagani; Mnyama ambaye alijiunganisha mwenyewe na upagani ili kuongeza idadi yake; Mnyama ambaye alitawala kwa siku za kinabii 1260 (Ufunuo 12:6), au miaka ya unabii 3 1/2 (Ufunuo 12:14), au miezi ya unabii 42 (Ufunuo 13:3)--kila moja ikileta jumla ya miaka halisi 1260 (angalia Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6), si mwingine bali Kanisa Katoliki la Kirumi Mfumo huu mkuu wa kidini wa Ukatoliki huliinua Kanisa lililopangiliwa juu ya dhamiri ya mtu, na wakati kuna mgongano kati ya Biblia na Kanuni za Kanisa, kanuni daima huwekwa juu zaidi ya ukweli wa Biblia. Kama kuna kutokubaliana kati ya dhamiri ya mtu na fundisho kuu la Kanisa, Kanisa kwa njia ya mapokeo yake na maoni mara zote huchukua sehemu ya kwanza.

Kwa kutofautisha na utawala huu na utawala wa Kanisa, Paulo anawasifia Waberoya waungwana kwa sababu “walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo” Matendo 17:11. Hakuna mahali popote tunapomkuta Paulo akiwataka waumini kukubali mafundisho kwa msingi wa mamlaka ya Mitume, lakini badala yake aliwahamasisha kuyachunguza Maandiko wao wenyewe ili kuthibitisha ukweli wa mambo waliyokuwa wamefundishwa. Wazo la neno la Mungu kama mamlaka ya juu na mwongozo wa maisha ni dini na ukweli wa Biblia (angalia Yohana 5:39; 2 Timotheo 3:16-17; Isaiya 8:20), na maarifa haya yanatuweka huru (angalia Yohana 8:32).

Roho ya tatu ya uchafu ni roho ya Nabii wa Uongo. Nabii ni mmoja wa wanaodai kuwa wamepokea ujumbe kutoka kwa Mungu, na kisha hudai kuwa mnenaji wa Mungu katika kueneza kwa haraka ujumbe huu kwa watu (angalia Hesabu 12:6; Kumbukumbu la Torati 18:22). Nabii wa uongo hatimaye angekuwa mtu yeyote anayedai kuwa ananena kwa ajili ya Mungu, wakati katika hali halisi hafanyi hivyo (angalia Yeremia 14:14). Nabii wa Uongo haiwezekani kurejewa kama upapa, kwa sababu umedai siku zote kupokea utamaduni juu ya ufunuo wa Biblia na haki ya kubadilisha amri za Mungu kadiri wapendavyo. Lakini Makanisa mbalimbali ya Kiprotestanti yamedai kufuata Biblia tu kama msingi wa imani yao na  mafundisho. Na bado, tunayaona yakifuata katika nyayo za Roma kwa kuinua utamaduni [mapokeo] juu ya ukweli wa neno la Mungu! Kwa hiyo Makanisa hayo ni nabii wa uongo
yaking’ang’ania, kuongea yakiunga mkono, makosa na huku bado yanadai ni ukweli wa Mungu!

Wakati yakitofautiana katika baadhi ya mambo fulani, Makanisa ya Kiprotestanti yote yanaungana pamoja katika mafundisho yasiyoleta hitilafu, na zaidi na zaidi yanafanana na Ukatoliki wa Kirumi. Wakati, katika harakati za kufikia malengo yake, huyu Nabii wa Uongo wa Uprotestanti anapofuata katika nyayo zile zile za Rumi, kwa kuungana na kutegemea nguvu za kiserikali kumwunga mkono katika mafundisho yake na kukanyaga haki ya uhuru wa kuabudu ili kulazimisha mafundisho yake makuu, atakuwa pia Sanamu ya Mnyama (angalia Ufunuo 13). Kwa kukataa ukweli, watu wanakataa Mwanzilishi wa ukweli na kujiandaa wenyewe kuwa upande wa Ibilisi katika vita hii kuu ya mwisho. Kwa kuendelea kukaidi kukubali mamlaka ya Mungu--Mtoa sheria, na kutii sheria zake, wanaume,  wanawake, na watoto wanajifunga wenyewe kwa mwasi mkuu katika ufisadi.

Hakuna kosa linalojeruhi sana moja kwa moja dhidi ya mamlaka na serikali ya Mbinguni na linapingwa zaidi katika maamuzi ya hiari kuliko wazo kwamba sheria ya Mungu si ya lazima tena. Sheria ndiyo msingi wa serikali yote, na ni kukosa hekima kikamilifu au kuungwa mkono kuamini kwamba Mtawala wa ulimwengu amestaafu katika wajibu wake na kutuacha bila sheria yake! Iwe Ibilisi amekudaka wewe kwa kuweka mbali sheria ya Mungu yote, au kukataa moja ya mausia yake, matokeo yake ni yale yale. Yeyote anayejikwaa “katika neno moja” hudhihirisha dharau kwa sheria yote; mvuto wake na mfano viko upande wa uasi; anakuwa “amekosa juu ya yote” (angalia Yakobo 2:10). Popote pale mausia ya Mungu yanapotupiliwa mbali, dhambi hukoma kuwa ya kuchukiza au haki kuwa kitu cha kutamaniwa.

Maandiko yanatangaza kwamba roho za mashetani zitafanya kazi kwa nguvu miujiza ambayo itawadanganya karibu ulimwengu wote, na kisha kuwakusanya watu wote pamoja kwa ajili ya vita kuu ya mwisho. Kigezo kikuu cha mgongano kitakuwa ni sheria ya Mungu, na hasa Sabato, ambayo inamwonyesha Mtoa sheria kama Muumbaji pekee na hivyo tunayepaswa kutoa utii kwake kama sehemu ya lazima ya urithi. Ni kazi ya ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12 & 18:1-5 kubatilisha mashambulizi haya dhidi ya sheria ya Mungu kwa kuleta kwa ulimwengu ibada inayostahili kwa Mungu kama Muumbaji wetu. Kwa muungano wa nguvu hizi tatu za Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo, watu wote walioko duniani watalazimika kuungana katika jukwaa la uovu dhidi ya

Mungu na ukweli wa Biblia. Na wale ambao hawafuati maamuzi yao [nguvu hizi tatu] watauawa. Hivyo, kupitia mafundisho ya udanganyifu na mafundisho ya muungano huu wa nguvu tatu za umizimu, Ukatoliki, na Uprotestanti, wakazi wote wa dunia watatakiwa kukata shauri kuwa upande wa, au kinyume cha, Mungu na ukweli wake (angalia Ufunuo13:15- 17). Mungu halazimishi utashi wa dhamiri, lakini Shetani mara kwa mara hujaribu kutumia njia mbalimbali za nguvu na ukatili ili apate utawala juu ya wale ambao hawezi, kwa njia yoyote, kuwadanganya. Kwa njia ya woga, au kwa nguvu halisi, Shetani hupanga kutawala dhamiri na kujipatia utukufu mwenyewe. Kutimiza hili, hufanya kazi kupitia mamlaka ya kidini na pia ile ya serikali za dunia, akiwasukuma kupitisha sheria za wanadamu ambazo humpinga kabisa Mungu na sheria yake.

Jumamosi, Februari 25, 2012

Majibu Yafanyayo Kazi...SINAGOGI vs KANISA.


Sinagogi ni nyumba ya dini na ya jamii ya Wayahudi inayotumika hasa kusali.

Etimolojia

Neno linatokana na Kigiriki  sinagoge likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya Kiebrania  beit knesset yaani "nyumba ya mkutano". Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kutajia sinagogi.

Muundo

Chumba kikuu ni ukumbi wa sala lakini mara nyingi kipo pamoja na vyumba vya pembeni kama vile madarasa, ofisi na vingine. 

Historia

Katika Israeli ya Kale (kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 587 KK) inaonekana hakukuwa na sinagogi: walau halitajwi kabisa katika Agano la Kale.
Hakuna uhakika kamili lakini inaonekana ya kwamba masinagogi yalianzishwa baada ya hekalu ya Yerusalemu kubomolewa pamoja na kuanza uhamisho wa Wayahudi kwenda nchi mbalimbali.
Tangu kuharibiwa kwa Hekalu la Pili mwaka 70 Wayahudi wana masinagogi tu kufanyia ibada.



Kanisa

Kwanza kabisa neno Kanisa linamaanisha "mkusanyiko wa waamini" kama ule wa Waisraeli chini ya Musamlima Sinai walipopewa Amri za Mungu. kwenye
Neno hilohilo lilitumiwa na Wakristo wa kwanza kwa ajili yao wenyewe kusema wameshika nafasi ya Israelitaifa la Mungu hata wasipokuwa Wayahudi bali watu wa mataifa mengine. kama
Jina hilo lilitumika kwa jumuia mama ya Yerusalemu, kwa kila mojawapo ya jumuia za Kikristo zilizotokana na umisionari wa wafuasi wa Yesu Kristo, na kwa umoja wao wa kimataifa uliotazamwa na Mtume PauloMwili wa Kristo, ukiwa na Yesu kama kichwa chake. kuwa

Kanisa kama jengo


Wakristo walipoanza kujenga mahali pa ibada, pakaja kuitwa vilevile "kanisa" kwa sababu ndani yake lilikusanyika Kanisa hai.
Hivyo mara nyingi neno hilo linatumika kwa maana ya jengo, ambalo ni mfano mwingine uliotumiwa na Paulo kuhusu umoja wa Wakristo, ukiwa na Yesu kama jiwe kuu la msingi.
Majengo hayo ya ibada yanaweza kuwa na ubora tofauti hata upande wa sanaa; baadhi yake yanatembelewa na watalii na kuhifadhiwa kwa bidii kwa sababu hiyo.
Kwa namna ya pekee ni muhimu Kanisa kuu la kila jimbo (dayosisi), halafu Basilika na Patakatifu.


 

Madhehebu

Baada ya umoja wa Wakristo kuanza kuvunjika, kwa kawaida madhehebu yaliyotokea yaliendelea kujiita makanisa, ingawa kwa maana mbalimbali: hasa Kanisa Katoliki na Waorthodoksi wanadai kuwa la kwao ndilo linaloendeleza Kanisa pekee la kweli; kumbe Waprotestanti hawatii maanani sana umoja wa Wakristo upande wa miundo, bali ule wa kiroho.
Ndani ya Kanisa Katoliki, linalokubali uongozi wa Papa wa Roma, neno Kanisa linatumika pia kumaanisha kila jimbo na makundi ya majimbo yanayochanga mapokeo yaleyale upande wa teolojia, liturujia, maisha ya kiroho, sheria n.k.
Kwa msingi huo Kanisa la Kilatini, ambalo lilienea kwanza upande wa magharibi wa Dola la Roma (Kanisa la Magharibi), linatofautishwa na Makanisa ya Mashariki yaliyoenea kwanza upande wa mashariki wa dola hilo na nje ya mipaka yake.

Mfumo  wa Waadventista Wasabato

 

Agizo la utume wa Mwokozi kwa kanisa kupeleka injili ulimwnegunu mwote (Mat. 28:19-20; Marko 16:15) halikumaanisha tu kuhubiri ujumbe bali kuhakikisha ustawi wa wale walioupokea ujumbe ule. Hii ilhusisha kuchuga na pia kulipatia kundi makazi, na pia kukabiliana na matatizo ya mahusiano. Hali kama hiyo ilihitaji mfumo (Oganaizaisheni).

Mwanzoni mitume wao wenyewe waliunda baraza ambalo liliongoza shughuli  katika kila kanisa (Mdo.14:23).Kanisa lile changa kutoka Yerusalemu (Mdo. 6:2; 8:14). Pale kundi la jijini lilipokuwa kubwa kiasi kwamba uendeshaji wa shughuli zao za dhati ukawa tatizo,mashemasi waliteuliwa kusimamia shughuli za kanisa (Mdo. 6:2-4). Pia inaonekana wazi kutokana na kumbukumbu za Mungu kwamba upanuzi wa kazi katika majimbo mbalimbali ya Dola ya Kirumi ulihitaji mfumo wa kanisa katika kile mabacho kinaweza kuitwa konferensi. Zilijumuisha makanisa katika ,jimbo mahsusi, kama vile makanisa ya Galatia(Waga.1:2); likawa na mfumo(oganaizesheni). Kadri mahitaji yalivyojitokeza Mungu aliwaongoza na kuwaelekeza viongozi wa kazi yake.

Madaraja katika mfumo wa kiutawala wa Waadventista Wasabato

Miongoni mwa Waadventista wasabato kuna madaraja manne ya uwakilishi kuanziamuumini mmoja hadi mfumo(oganaizesheni)mzima wa kazi ya kanisa ulimwenguni pote.

1. Kanisa moja;
Jamii iliyoungana katika mfumowa kundi la waumini mmoja mmoja.

2. Konferensi, fildi au misheni ya sehemu moja
Muungano wa jamii ya makanisa katika nchi, mkoa au eno la nchi.

3. Union inayojitegmea
Hii ni jamii ya muungano wa koferensi, fildi au misheni kadhaa ndani ya eneo kubwa la nchi.

4. Halmasahuri kuu
Ambayo ni sehemu kubwa ya mfumo wa utawala, unaounganisha union zote pande zote za ulimwengu. Divisheni ni shemu ya Halmashauri kuu, zikiwa na mamlaka katika maeneo maalumu yaliyotengwa
kijiografia.

Kila mshiriki wa kanisa ana sauti katika kuchagua maofisa wa kanisa. Kanisa huchagua maofisa wa fildi au konferensi. Wajumbe waliochaguliwa na fildi au konferensi huwachagua maofisa wa union zilizo konferensi au union misheni, na wajumbe waliochaguliwa na union konferensi au union misheni huwachagua maofisa wa halmashauri kuu. Kwa mpangilio huu kila konferensi au fildi, kila taasisi, kila kanisa na kila mshiriki binafsi, aidha moja kwa moja au kupitia wawakilishi, ana sauti kwa uchaguzi wa watu wanaobeba majukumu makubwa katika halmashauri kuu.

Halmashauri kuu , Mamlaka ya Juu Zaidi

Halmashauri kuu katika kikao rasmi cha kila miaka mitano,na Kamati ya Utendaji ikutanikayo katikati ya vikao rasmi, ndicho chombo cha juu zaidi katika utawala wa shuguli za kanisa uimwenguni kote, na chombo hicho kimepewa mamalaka na katiba yake kuunda mashirika yalio chini yake ili kuendeleza maslahi mahsusi katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa hiyo basi imeeleweka wazi kwamba mashirika yote madogomadogo na taasisi ulimwenguni kote zitatambua Halmashari kuu kama mamalaka iliyo juu zaidi, chini ya Mungu miongoni wa Waadventista Wasabato. “Mara kwa mara nimeagizwa na Bwana ya kwamba maamuzi ya mtu yasisalimishwe kwa maamuzi ya mtu mwingine yeyote. Kamwe nia ya mtu mmoja au nia za watu wachache zisichukuliwe kama zatosha kwa hekima na uwezo kudhibiti kazi na kusema ni mipango ipi ndo itakayofuatwa. 

Lakini katika kikao rasmi cha halmashauri kuu, wakati maamuzi ya ndugu waliokusanyika pamoja kutoka sehemu zote za kazi ulimwenguni yanapotolewa, basi ushupavu binafsi na maamuzi binafsi ya pekee yasishiikiliwe kwa ukaidi, ila sharti yasalimishwe. Kamwe mtenda kazi asichukulie kuwa ni sifa kushikilia kwa ushupavu msimamao wake wa kutoambilika, kinyume cha uamuzi wa watu wote kwa ujumla. Nyakati nyingine kikundi, wakati ambapo kikundi kidogo cha watu kwa jumla waliokabidhiwa kusimamia kazi, kwa jina la Halmashauri kuu, wamejaribu kuendesha mipango isiyo ya busara nahivyo kuzuia kazi ya Mungu, hapo nimesema kuwa nisingeweza tena kuendelea kuheshimu sauti ya Halmashauri kuu iliyowakilishwa na watu hao wachache, kama sauti ya Mungu. Lakini hii siyo kusema kwamba maamuzi ya halmashauri kuu yenye wajumbe waliochaguliwa rasmi kutoka sehemu zote za kazi ulimwenguni hayapaswi kuheshimiwa. Mungu ameagiza kwamba wawakilishi wa kanisa lake kutoka sehemu zote za kazi duniani, wanapokusanyikakatika kikao cha Halmashauri kuu, watakuwa na mamlaka"-EG White

  ********************************

Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Doug Batchelor  

a n a p o t w a m b i a    k u h u s u:

Who are the Seventh-day Adventists?

(AmazingFacts)



KARIBU TENA

Ijumaa, Februari 24, 2012

UKANDA WA GAZA


...ni eneo dogo kwenye mwabao wa Mediteranea ya Mashariki lililopo sehemu ya mamlaka ya Palestina. Lina urefu wa kilomita 40 na upana kati ya 6 km na 14 km. Eneo lote halizidi 360 km². Gaza imepakana na bahari halafu nchi za Israel na Misri. Israel inatenganisha Gaza na maeneo upande wa magharibi ya Yordan yaliyo pia sehemu ya mamlaka ya Palestina.

Ni kati ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu likiwa na wakazi milioni 1.4 yaani zaidi ya watu 4,100 kwa km².

MJI MKUBWA WA GAZA.

Kanda hili ni kati ya mabaki ya Palestina ya Kiingereza yasiyotwaliwa na Israel wakati wa vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948 na kuwa kimbilio kwa wakimbizi wengi Wapalestina waliowahi kukaa katika sehemu zilizokuwa Israel. Kati ya 1948 hadi 1967 lilitawaliwa na Misri. Tangu vita ya siku sita ya 1967 kanda lilikuwa chini ya Israel. Tangu 1994 ilikabidhiwa kwa mamlaka ya Palestina lakini Israel iliendelea kuwa na vijiji vya Waisraeli na vituo vya kijeshi ndani yake. Mapigano ya intifada yaliongezeka kuwa makali na kusababisha vifo vingi. Tangu 2005 Israel iliondoa wakazi na wanajeshi wake wote.

Baada ya uchaguzi wa 2006 chama cha Hamas chini ya Ismael Haniya kilipata kura nyingi na kushika serikali ya Palestina. Farakano kati ya Hamas na Fatah wa rais Mahmud Abas liliongezeka hadi Hamas kuchukua mamlaka yote katika Gaza kwa nguvu ya silaha mwezi wa Juni 2007. Tangu mwezi ule Gaza iko chini ya serikali ya Hamas lakini maeneo mengine yako chini ya mamlaka ya rais Abas.

Hali ya wakazi ni vigumu. Israel imefunga mipaka na kuzuia wakazi wa Gaza wasitoke nje kwa sababu wanamigambo Wapalestina wanaendelea kurusha roketi ndogo kutoka Gaza kwenda Israel. Kutokana na kufungwa kwa mipaka yote uchumi ni duni hakuna ajira. Hata huduma za kimsingi kama vile maji na umeme zinavurugika kabisa.

PALESTINA



Ni nchi mpya katika mwendo wa kuzaliwa lakini kwa sasa hakuna uhakika kama tendo litakamilika na lini. 

Kwa sasa kuna idadi ya maeneo yanayotawaliwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina.

Maeneo haya yametengwa kati yao na maeneo yanayosimamiwa na Israeli.

Maeneo haya yako kati ya mto Yordani na pwani ya Mediteranea: ni hasa Ukingo wa Magharibi wa Yordani na Ukanda wa Gaza.

Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina ina kiwango fulani cha madaraka ya kiserikali katika baadhi ya maeneo haya.

Mamlaka hiyo hutambuliwa na nchi nyingi za Waarabu kama serikali halisi. 

Jumuia ya kimataifa kwa ujumla imetambua mamlaka kwa viwango mbalimbali lakini si kama serikali kamili ya nchi huru. 

Hivyo Mamlaka ina kiti cha mtazamaji kwenye Umoja wa Mataifa.

Maeneo ya Palestina yamepakana na Israel, Yordani na Misri. Kanda la Gaza lina pwani kwenye Mediteranea.

Alhamisi, Februari 23, 2012

Unamkumbuka Mwalimu wa Kike Aliyebaka Wanafunzi 11?

  


Mwaka jana mwalimu Cindy Clifton mwenye umri wa miaka 41 alikabiliwa na kifungo cha muda mrefu jela kwa kosa la kuwanywesha pombe wanafunzi wake wa 11 wa kiume wenye umri kati ya miaka 14 na 17 na kisha kufanya nao mapenzi.

Taarifa ya televisheni ya ABC ilisema kuwa mwalimu huyo wa shule ya msingi ya Crestview Middle School aliwalewesha wanafunzi wake wakati wa sherehe alizoziandaa kwenye nyumba yake na kufanya nao mapenzi katika kipindi cha kuanzia aprili 11 hadi julai 15.

Mwalimu huyo aliyejizolea umaarufu katika shule hiyo kutokana na ufundishaji wake alikabiliwa na mashtaka ya kufanya mapenzi na watoto wenye umri mdogo usiofika miaka 18.

Miongoni mwa wanafunzi waliofanya mapenzi na mwalimu huyo, walikuwa ni marafiki wa binti wa mwalimu huyo.

Mwalimu huyo alifunguliwa mashtaka miezi mitatu baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa polisi ulioanzishwa baada ya malalamiko mengi toka kwa wazazi.

"Uchunguzi wa polisi ulianza baada ya malalamiko ya wazazi ambao walilalamika watoto wao walinyeshwa pombe kwenye sherehe zilizoandaliwa na mwalimu Clifton", ilisema taarifa ya polisi.

JE UNAFAHAMU HABARI YOYOTE YA SASA KUHUSU HUYU MWALIMU?
 

Jumapili, Februari 19, 2012

Je, Roma Itatawala Ulimwengu Tena?


 KANISA LA MTAKATIFU PETRO, ROMA


Photo Credit by: www.minutetravelguide.com

Maridhiano ya Kufisha

Mtume Paulo, katika Waraka wake wa Pili kwa Wathesalonike, alitabiri juu ya uasi mkuu ambao ungeleta
matokeo ya kuianzisha mamlaka ile ya upapa. Alitangaza kwamba siku ile ya kuja Kristo isingeweza kuja, “usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa mtu yule wa dhambi (kuasi), mwana wa uharibifu; yule  Mpingamizi [Mpinga Kristo], ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu [kanisa] la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” Tena, zaidi ya hayo, Mtume huyo anawaonya ndugu zake kwamba “ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 Wakorintho 2:3,4,7. 

Hata katika kipindi kile cha mwanzo kabisa aliona yakiingia ndani ya kanisa mafundisho potofu
ambayo yangetayarisha njia ya kujitokeza kwa upapa. Kidogo kidogo, mwanzoni kwa siri na kimya kimya, na baadaye kwa wazi zaidi, ikaongezeka nguvu yake na kuitawala mioyo ya wanadamu, ile “siri ya kuasi” ikaiendeleza mbele kazi yake kwa kutumia madanganyo na makufuru. Karibu bila kutambulikana kabisa desturi zile za kikafiri zikaingia ndani ya kanisa la Kikristo. Roho ile ya maridhiano na kufanana-fanana
[na dunia] ilizuiwa kwa wakati fulani kutokana na mateso makali ambayo kanisa lilistahimili chini ya wapagani. Lakini mateso yale yalipokoma, na Ukristo ulipoingia katika mabaraza na majumba ya kifalme, ndipo kanisa lile lilipouweka kando unyenyekevu ule wa Kristo na Mitume wake na kujitwalia
ufahari na kiburi cha makuhani na watawala wale wa kipagani; na mahali pa matakwa ya Mungu likaweka nadharia zawanadamu pamoja na desturi zao. 

Kuongoka kwa jina tu kwa Konstantino, mapema katika karne ile ya nne, kulileta shangwe kubwa; na  ulimwengu [upagani], ukiwa umevikwa joho la mfano wa haki, ukatembea na kuingia ndani ya kanisa. Basi,
kazi ile ya uharibifu ikasonga mbele kwa haraka sana. Upagani, wakati ukionekana kana kwamba umeshindwa kabisa, ukawa ndio mshindi. Roho yake ikalitawala kanisa lile. Mafundisho yake ya dini, sherehe zake, na ushirikina wake vikaingizwa katika imani na ibada ya wale waliojidai kuwa ni wafuasi wake Kristo.

CHANZO CLICK HAPA

Jumamosi, Februari 18, 2012

MAJIBU YAFANYAYO KAZI...”THE WINGS OF OUR FLIGHT”


NINAPENDA KUKUJULISHA KIJIWE HIKI AMBACHO NINA UHAKIKA KUNA MAMBO MAKUBWA MAZURI YATAKAYOKUSAIDIA KTK MAISHA IKIHUSISHA ZAIDI SUALA LA KIROHO KWA YULE ANAYEWIWA.

NI WEBSITE YA SOUTHERN HIGHLANDS CONFERENCE IKIHUSISHA MIKOA YA MBEYA, IRINGA  (Mikoa mingine nimeisahau kidogo ila itembelee wewe mwenyewe). UNAWEZA UKAITEMBELEA KUPITIA ANUANI IFUATAYO:
 http://www.shcadventist.org

Makao makuu yapo Iganzo, Chunya Road - Mbeya
Mawasiliano        info@shcadventist.org
Telephone:     +255 753 199020
Fax:               +255 25 2502367
Mobile Phone Number:     +255 718 378837 


********************************
Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Napenda kukujulisha kuwa lile Kongamano la Mawasiliano la Union litmefanyika na leo ndio hitimisho Februari 18, 2012 kama ilivyopangwa katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Mwenge Dar es salaam.

Wahudumu wa Kongamano hili lenye Motto :
”THE WINGS OF OUR FLIGHT”  
wametoka General Conference, East-Central Africa Division, Tanzania Union na wataalamu wetu wa ndani waliobobea.

Kando ya Maofisa wetu wa Union, Konferensi/Fildi, Wakurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Jamii, Wataalamu wa IT wa Fild na Konferensi, Wajumbe wa Kongamano hili walijumuishwa pia wachungaji wa mitaa, wazee wa kanisa, viongozi wa kanisa wa mawasiliano na uhusiano na jamii, wataalamu wa Teknohama na washiriki wote.

Kongamano hili lilijadili Nyanja nne kuu za mawasiliano:
 
(A) - Print Media, 
(B) - ICT, 
(C) - Radio na 
(D) - Television Broadcasting.
  
The topics include though not limited to: 
* Production Playback and Feedback, 
* Ethics and Adventist Communication Issues, 
* Writing Adventist News, 
* Quality Production and Maintenance of high Production 
* Standards, 
* Public Relations, 
* Writing For Broadcasting, 
* Interface with Public Print and Broadcast Media, 
* Writing for Print, 
* Effective Interview, 
* Podocasting, 
* Magazine formats , 
* Adventist Websites, 
* NetAdventist, 
* A week of Prayer through Social networks, 
* Twitting  for Commission, 
* The Communication Secretary (for Church), 
* Crisis management issues.

Wapendwa sasa vifaa vya mawasiliano vya kisasa zaidi vinaendelea kuwekwa makanisani. Hii ni fursa yako muafaka kujifunza kuvitumia ili kutimiza utume wa kanisa kwa mafanikio makubwa. Naamini hutadiriki kukosa fursa hii. 

Alhamisi, Februari 16, 2012

AMRI YA JUMAPILI KWA ULIMWENGU MZIMA



1.     Biblia inasemaje juu ya kuinuka tena ulimwenguni kote kwa uongozi ule wa Roma ya Kikatoliki kabla ya mwisho wa wakati? Ufunuo 13:3,8.

Photo by: www.veteransnewsnow.com


1. Ni Taifa gani lililopata upendeleo litakaloongoza katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili?


a. "Kundi lilo hilo lilitoa madai yake ya kwamba kuenea haraka kwa ufisadi kwa sehemu kubwa kulichangiwa na kuinajisi ile wanayoiita 'Sabato ya Kikristo,' na ya kwamba kule kulazimisha utunzaji wa Jumapili kungeyaboresha sana maadili ya jamii. Madai hayo yanasisitizwa hasa katika Amerika, ambako fundisho la Sabato ya Kweli limehubiriwa karibu kwa mapana yake yote." GC 587.

 
b. "Mataifa ya kigeni yatafuata mfano wa Marekani. Japokuwa Taifa hili linaongoza, hata hivyo hatari iyo hiyo itawajia watu wetu katika sehemu zote za ulimwengu." 6T 395.

 
2. Ni mataifa mangapi yatakayofuata mfano huo wa Marekani?

 
a. "Amerika, nchi yenye uhuru wa dini, itakapoungana na upapa katika kuzitenda jeuri dhamiri za watu na kuwalazimisha watu kuiheshimu sabato hiyo ya uongo [Jumapili], hapo ndipo watu wa kila nchi ulimwenguni watakapoongozwa kufuata mfano wake." 6T 18 (Angalia GCB 1-28- 1893).


b. " '[A]liwanywesha Mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake [mafundisho yake potofu]' Ufunuo 14:6-8. Hii inakuwaje? Kwa kuwalazimisha watu kuikubali sabato bandia [Jumapili]." 8T 94.
c. "Suala hili la Sabato ndilo litakuwa hoja kuu katika Pambano Kuu la mwisho ambalo kwalo ulimwengu wote utakuwa na sehemu yake ya kufanya." 6T 352.

 
4. Ni dini gani hasa ya ulimwengu mzima inayohusika na kulazimisha utunzaji huu wa Jumapili?


a. "Kwa vile Sabato imekuwa jambo la pekee la mabishano katika Mataifa ya jamii za Kikristo, na wenye mamlaka ya dini [ya Muungano] na serikali wameungana katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili, basi, wale walio wachache sana watakaoendelea kukataa kukubaliana na madai hayo yanayopendwa na wengi watakuwa watu wa kuchukiwa mno ulimwenguni kote." GC 615.


b. "Jamii yote ya Kikristo itagawanyika katika makundi makuu mawili, wale wanaozishika amri [kumi] za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomsujudu mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa yake." GC 450; 9T 16; 2SM 55.

 
5. Ni jambo gani litakalowapata Waadventista Wasabato ambao hawawezi kukubaliana na Amri hiyo ya Jumapili?

a. "Amri ile itakayoitia nguvu ibada ya siku hii [ya Jumapili] itatangazwa ulimwenguni kote.... Maonjo na mateso yatawajia wale wote ambao, kwa kulitii Neno la Mungu, watakataa kuisujudu sabato hiyo ya uongo [Jumapili]." 7BC 976.
b. "Ulimwengu wote utachochewa kuwa na uadui dhidi ya Waadventista Wasabato, kwa sababu hawatakubali kumsujudu papa kwa njia ya kuiheshimu Jumapili, siku iliyowekwa na mamlaka hiyo ya Mpinga Kristo. Ni kusudi lake Shetani kusababisha wafutiliwe mbali duniani, ili ukuu wake humu duniani usipate kupingwa." TM 37; RH 8-22-1893.

 
c. "Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo." GC 604.

6. Ni athari gani zitakazoletwa na uamsho huo wa bandia juu ya karibu wote wanaojiita Wakristo kwa jina tu?


"Wakatangaza ya kwamba wao walikuwa na ile kweli; ya kwamba miujiza ilitendeka kati yao; ya kwamba uwezo mkuu na ishara na maajabu yalitendeka miongoni mwao; na ya kwamba hiyo ilikuwa ndiyo ile Milenia [miaka elfu moja] waliyokuwa wanaingojea kwa muda mrefu sana. Ulimwengu wote uliongolewa na kuafikiana na Amri ile ya Jumapili." Letter 6, 1884. 7.


Ni alama gani mbili zinazopingana zitapokewa na makundi hayo mawili ya watu katika ulimwengu huu hapo Jumapili itakapotiwa nguvu kwa kuitungia sheria?


a. "Wakati utunzaji wa sabato hiyo ya uongo [Jumapili] kwa kuitii amri ya serikali, kinyume na amri ile ya nne, utakuwa ni kiapo cha utii kwa mamlaka ile inayopingana na Mungu, utunzaji wa Sabato ya Kweli, kwa kuitii Sheria ya Mungu [Amri Kumi], ni ushahidi wa utii kwa Muumbaji. Wakati kundi moja, kwa uikubali alama ya utii kwa mamlaka za duniani, linapokea Alama (chapa) ya Mnyama, lile jingine, kwa kuichagua ishara ya utii kwa Mamlaka ile ya Mbinguni, litapokea Muhuri wa Mungu." GC 605.


c. "Matokeo ni ya kuogofya ambayo kwayo ulimwengu huu utakabiliwa nayo. Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo.

Kwa upande mwingine, Sheria ya Mungu [Amri Kumi] inayoamuru Siku ya Mapumziko iliyowekwa na Muumbaji inataka watu wote waitii na kutishia ghadhabu dhidi ya wote wanaozivunja amri zake [kumi]. "Jambo hilo likiwa limewekwa wazi hivyo mbele yake [kila mtu], hapo ndipo ye yote atakayeikanyaga sheria ya Mungu chini ya miguu yake ili kuitii amri ile iliyotungwa na binadamu atapokea Alama ya Mnyama...." GC 604. 

Photo by: www.lahore.olx.com.pk

8. Je, Amri hiyo ya Jumapili kwa ulimwengu mzima ina uhusiano gani na kufungwa kwa mlango wa rehema?


a. "Mungu anayapa Mataifa muda fulani wa majaribio." 4BC 1143.

 
b. "Kwa usahihi usioweza kukosewa Yule wa Milele angali bado anatunza akaunti ya Mataifa yote. Ingawa rehema zake hutolewa, zikiwa na mwito wa kuwataka wanadamu kutubu, akaunti hiyo itaendelea kubaki wazi; lakini hesabu hizo zitakapofikia kiwango fulani ambacho Mungu amekiweka, utekelezaji wa ghadhabu yake utaanza. Akaunti hiyo itafungwa. Uvumilivu wa


Mungu utakoma. Hakuna tena maombezi ya rehema kwa ajili yao." 5T208.


c. "Mungu anatunza kumbukumbu ya Mataifa: hesabu zinajaa dhidi yao katika vitabu vile vya mbinguni; na wakati ule itakapokuwa imepitishwa sheria kwamba uvunjaji wa siku ya kwanza ya juma utakabiliwa na adhabu, hapo ndipo kikombe chao kitakuwa kimejaa." 7BC 910.

d. "Hesabu zinazozidi kuongezeka katika vitabu vile vya kumbukumbu vya mbinguni zitakapoonyesha kiwango cha jumla ya maovu kuwa kimetimia, ndipo ghadhabu itakapokuja, pasipo kuchanganywa na maji, na hapo ndipo itakapojulikana ya kuwa ni jambo kubwa mno jinsi gani kuuchosha uvumilivu wa Mungu. Hatari hiyo kubwa itafikiwa wakati ule mataifa yote yatakapokuwa yameungana kuibatilisha Sheria ya Mungu." 5T 524.e. "Dunia hii karibu sana imefikia mahali ambapo Mungu atamruhusu yule mharabu [mwangamizaji] kufanya mapenzi yake juu yake. Kule kuziweka sheria za wanadamu mahali pa Sheria ya Mungu, kule kuitukuza Jumapili kwa amri za kibinadamu tu, badala ya Sabato ile ya Biblia, ndilo tendo la mwisho katika mfululizo wa matukio hayo. Tendo hilo la kubadilisha [siku ya ibada] litakapoenea ulimwenguni kote, hapo ndipo Mungu atakapojidhihirisha Mwenyewe. Atasimama katika utukufu wake wa kifalme kuitetemesha sana nchi hii. Atatoka mahali pake kuja kuwaadhibu wakazi wa dunia hii kwa ajili ya maovu yao, na nchi itaifunua damu yake, wala haitawafunika tena hao waliouawa." 7T 141.


f. "Kuweka ile iliyo ya uongo mahali pa ile iliyo ya kweli ndilo tendo la mwisho katika mfululizo wa matukio haya. Tendo hilo la kubadilisha [siku ya ibada] litakapoenea ulimwenguni kote, hapo ndipo Mungu atakapojidhihirisha Mwenyewe. Sheria za wanadamu zinapotukuzwa kuliko sheria za Mungu, mamlaka za dunia hii zinapojaribu kuwalazimisha watu kuitunza siku ya


kwanza ya juma, basi, jueni ya kwamba wakati umewadia kwa Mungu kutenda kazi yake. Atasimama katika utukufu wake wa kifalme, na kuitetemesha sana nchi. Atatoka mahali pake kuja kuwaadhibu wakazi wa dunia hii kwa ajili ya maovu yao." 7BC 980.

 
9. Je, hivi Waadventista Wasabato wote wanaamini kwamba Amri ya Jumapili kwa ulimwengu wote itapitishwa kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema?

La, hawaamini hivyo wote. Baadhi ya wanafunzi wa Biblia na Roho ya Unabii wanatazamia kwamba kutungwa kwa Amri ya Jumapili hakutaenea duniani kote mpaka kipindi fulani kipite baada ya kufungwa kwa mlango wa rehema.


Madondoo yaliyoorodheshwa chini ya Swali la 8 juu yanatafsiriwa kwa njia kama hii. Usemi mwingine wa kuwaunga mkono wanaoutumia ni huu: "Yesu atakapoondoka patakatifu pa patakatifu, Roho wake anayezuia ataondolewa kutoka kwa watawala na watu. Wataachwa katika udhibiti wa malaika waovu. Hapo ndipo sheria kama hizo zitatungwa kwa ushauri na uongozi wake Shetani, kama wakati usingekuwa mfupi sana, hakuna mwenye mwili ambaye angeweza kuokoka." 1T 204.