Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Februari 24, 2012

PALESTINANi nchi mpya katika mwendo wa kuzaliwa lakini kwa sasa hakuna uhakika kama tendo litakamilika na lini. 

Kwa sasa kuna idadi ya maeneo yanayotawaliwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina.

Maeneo haya yametengwa kati yao na maeneo yanayosimamiwa na Israeli.

Maeneo haya yako kati ya mto Yordani na pwani ya Mediteranea: ni hasa Ukingo wa Magharibi wa Yordani na Ukanda wa Gaza.

Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina ina kiwango fulani cha madaraka ya kiserikali katika baadhi ya maeneo haya.

Mamlaka hiyo hutambuliwa na nchi nyingi za Waarabu kama serikali halisi. 

Jumuia ya kimataifa kwa ujumla imetambua mamlaka kwa viwango mbalimbali lakini si kama serikali kamili ya nchi huru. 

Hivyo Mamlaka ina kiti cha mtazamaji kwenye Umoja wa Mataifa.

Maeneo ya Palestina yamepakana na Israel, Yordani na Misri. Kanda la Gaza lina pwani kwenye Mediteranea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni