Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Februari 16, 2012

AMRI YA JUMAPILI KWA ULIMWENGU MZIMA



1.     Biblia inasemaje juu ya kuinuka tena ulimwenguni kote kwa uongozi ule wa Roma ya Kikatoliki kabla ya mwisho wa wakati? Ufunuo 13:3,8.

Photo by: www.veteransnewsnow.com


1. Ni Taifa gani lililopata upendeleo litakaloongoza katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili?


a. "Kundi lilo hilo lilitoa madai yake ya kwamba kuenea haraka kwa ufisadi kwa sehemu kubwa kulichangiwa na kuinajisi ile wanayoiita 'Sabato ya Kikristo,' na ya kwamba kule kulazimisha utunzaji wa Jumapili kungeyaboresha sana maadili ya jamii. Madai hayo yanasisitizwa hasa katika Amerika, ambako fundisho la Sabato ya Kweli limehubiriwa karibu kwa mapana yake yote." GC 587.

 
b. "Mataifa ya kigeni yatafuata mfano wa Marekani. Japokuwa Taifa hili linaongoza, hata hivyo hatari iyo hiyo itawajia watu wetu katika sehemu zote za ulimwengu." 6T 395.

 
2. Ni mataifa mangapi yatakayofuata mfano huo wa Marekani?

 
a. "Amerika, nchi yenye uhuru wa dini, itakapoungana na upapa katika kuzitenda jeuri dhamiri za watu na kuwalazimisha watu kuiheshimu sabato hiyo ya uongo [Jumapili], hapo ndipo watu wa kila nchi ulimwenguni watakapoongozwa kufuata mfano wake." 6T 18 (Angalia GCB 1-28- 1893).


b. " '[A]liwanywesha Mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake [mafundisho yake potofu]' Ufunuo 14:6-8. Hii inakuwaje? Kwa kuwalazimisha watu kuikubali sabato bandia [Jumapili]." 8T 94.
c. "Suala hili la Sabato ndilo litakuwa hoja kuu katika Pambano Kuu la mwisho ambalo kwalo ulimwengu wote utakuwa na sehemu yake ya kufanya." 6T 352.

 
4. Ni dini gani hasa ya ulimwengu mzima inayohusika na kulazimisha utunzaji huu wa Jumapili?


a. "Kwa vile Sabato imekuwa jambo la pekee la mabishano katika Mataifa ya jamii za Kikristo, na wenye mamlaka ya dini [ya Muungano] na serikali wameungana katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili, basi, wale walio wachache sana watakaoendelea kukataa kukubaliana na madai hayo yanayopendwa na wengi watakuwa watu wa kuchukiwa mno ulimwenguni kote." GC 615.


b. "Jamii yote ya Kikristo itagawanyika katika makundi makuu mawili, wale wanaozishika amri [kumi] za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomsujudu mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa yake." GC 450; 9T 16; 2SM 55.

 
5. Ni jambo gani litakalowapata Waadventista Wasabato ambao hawawezi kukubaliana na Amri hiyo ya Jumapili?

a. "Amri ile itakayoitia nguvu ibada ya siku hii [ya Jumapili] itatangazwa ulimwenguni kote.... Maonjo na mateso yatawajia wale wote ambao, kwa kulitii Neno la Mungu, watakataa kuisujudu sabato hiyo ya uongo [Jumapili]." 7BC 976.
b. "Ulimwengu wote utachochewa kuwa na uadui dhidi ya Waadventista Wasabato, kwa sababu hawatakubali kumsujudu papa kwa njia ya kuiheshimu Jumapili, siku iliyowekwa na mamlaka hiyo ya Mpinga Kristo. Ni kusudi lake Shetani kusababisha wafutiliwe mbali duniani, ili ukuu wake humu duniani usipate kupingwa." TM 37; RH 8-22-1893.

 
c. "Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo." GC 604.

6. Ni athari gani zitakazoletwa na uamsho huo wa bandia juu ya karibu wote wanaojiita Wakristo kwa jina tu?


"Wakatangaza ya kwamba wao walikuwa na ile kweli; ya kwamba miujiza ilitendeka kati yao; ya kwamba uwezo mkuu na ishara na maajabu yalitendeka miongoni mwao; na ya kwamba hiyo ilikuwa ndiyo ile Milenia [miaka elfu moja] waliyokuwa wanaingojea kwa muda mrefu sana. Ulimwengu wote uliongolewa na kuafikiana na Amri ile ya Jumapili." Letter 6, 1884. 7.


Ni alama gani mbili zinazopingana zitapokewa na makundi hayo mawili ya watu katika ulimwengu huu hapo Jumapili itakapotiwa nguvu kwa kuitungia sheria?


a. "Wakati utunzaji wa sabato hiyo ya uongo [Jumapili] kwa kuitii amri ya serikali, kinyume na amri ile ya nne, utakuwa ni kiapo cha utii kwa mamlaka ile inayopingana na Mungu, utunzaji wa Sabato ya Kweli, kwa kuitii Sheria ya Mungu [Amri Kumi], ni ushahidi wa utii kwa Muumbaji. Wakati kundi moja, kwa uikubali alama ya utii kwa mamlaka za duniani, linapokea Alama (chapa) ya Mnyama, lile jingine, kwa kuichagua ishara ya utii kwa Mamlaka ile ya Mbinguni, litapokea Muhuri wa Mungu." GC 605.


c. "Matokeo ni ya kuogofya ambayo kwayo ulimwengu huu utakabiliwa nayo. Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo.

Kwa upande mwingine, Sheria ya Mungu [Amri Kumi] inayoamuru Siku ya Mapumziko iliyowekwa na Muumbaji inataka watu wote waitii na kutishia ghadhabu dhidi ya wote wanaozivunja amri zake [kumi]. "Jambo hilo likiwa limewekwa wazi hivyo mbele yake [kila mtu], hapo ndipo ye yote atakayeikanyaga sheria ya Mungu chini ya miguu yake ili kuitii amri ile iliyotungwa na binadamu atapokea Alama ya Mnyama...." GC 604. 

Photo by: www.lahore.olx.com.pk

8. Je, Amri hiyo ya Jumapili kwa ulimwengu mzima ina uhusiano gani na kufungwa kwa mlango wa rehema?


a. "Mungu anayapa Mataifa muda fulani wa majaribio." 4BC 1143.

 
b. "Kwa usahihi usioweza kukosewa Yule wa Milele angali bado anatunza akaunti ya Mataifa yote. Ingawa rehema zake hutolewa, zikiwa na mwito wa kuwataka wanadamu kutubu, akaunti hiyo itaendelea kubaki wazi; lakini hesabu hizo zitakapofikia kiwango fulani ambacho Mungu amekiweka, utekelezaji wa ghadhabu yake utaanza. Akaunti hiyo itafungwa. Uvumilivu wa


Mungu utakoma. Hakuna tena maombezi ya rehema kwa ajili yao." 5T208.


c. "Mungu anatunza kumbukumbu ya Mataifa: hesabu zinajaa dhidi yao katika vitabu vile vya mbinguni; na wakati ule itakapokuwa imepitishwa sheria kwamba uvunjaji wa siku ya kwanza ya juma utakabiliwa na adhabu, hapo ndipo kikombe chao kitakuwa kimejaa." 7BC 910.

d. "Hesabu zinazozidi kuongezeka katika vitabu vile vya kumbukumbu vya mbinguni zitakapoonyesha kiwango cha jumla ya maovu kuwa kimetimia, ndipo ghadhabu itakapokuja, pasipo kuchanganywa na maji, na hapo ndipo itakapojulikana ya kuwa ni jambo kubwa mno jinsi gani kuuchosha uvumilivu wa Mungu. Hatari hiyo kubwa itafikiwa wakati ule mataifa yote yatakapokuwa yameungana kuibatilisha Sheria ya Mungu." 5T 524.e. "Dunia hii karibu sana imefikia mahali ambapo Mungu atamruhusu yule mharabu [mwangamizaji] kufanya mapenzi yake juu yake. Kule kuziweka sheria za wanadamu mahali pa Sheria ya Mungu, kule kuitukuza Jumapili kwa amri za kibinadamu tu, badala ya Sabato ile ya Biblia, ndilo tendo la mwisho katika mfululizo wa matukio hayo. Tendo hilo la kubadilisha [siku ya ibada] litakapoenea ulimwenguni kote, hapo ndipo Mungu atakapojidhihirisha Mwenyewe. Atasimama katika utukufu wake wa kifalme kuitetemesha sana nchi hii. Atatoka mahali pake kuja kuwaadhibu wakazi wa dunia hii kwa ajili ya maovu yao, na nchi itaifunua damu yake, wala haitawafunika tena hao waliouawa." 7T 141.


f. "Kuweka ile iliyo ya uongo mahali pa ile iliyo ya kweli ndilo tendo la mwisho katika mfululizo wa matukio haya. Tendo hilo la kubadilisha [siku ya ibada] litakapoenea ulimwenguni kote, hapo ndipo Mungu atakapojidhihirisha Mwenyewe. Sheria za wanadamu zinapotukuzwa kuliko sheria za Mungu, mamlaka za dunia hii zinapojaribu kuwalazimisha watu kuitunza siku ya


kwanza ya juma, basi, jueni ya kwamba wakati umewadia kwa Mungu kutenda kazi yake. Atasimama katika utukufu wake wa kifalme, na kuitetemesha sana nchi. Atatoka mahali pake kuja kuwaadhibu wakazi wa dunia hii kwa ajili ya maovu yao." 7BC 980.

 
9. Je, hivi Waadventista Wasabato wote wanaamini kwamba Amri ya Jumapili kwa ulimwengu wote itapitishwa kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema?

La, hawaamini hivyo wote. Baadhi ya wanafunzi wa Biblia na Roho ya Unabii wanatazamia kwamba kutungwa kwa Amri ya Jumapili hakutaenea duniani kote mpaka kipindi fulani kipite baada ya kufungwa kwa mlango wa rehema.


Madondoo yaliyoorodheshwa chini ya Swali la 8 juu yanatafsiriwa kwa njia kama hii. Usemi mwingine wa kuwaunga mkono wanaoutumia ni huu: "Yesu atakapoondoka patakatifu pa patakatifu, Roho wake anayezuia ataondolewa kutoka kwa watawala na watu. Wataachwa katika udhibiti wa malaika waovu. Hapo ndipo sheria kama hizo zitatungwa kwa ushauri na uongozi wake Shetani, kama wakati usingekuwa mfupi sana, hakuna mwenye mwili ambaye angeweza kuokoka." 1T 204.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni