Mtayarishaji

Morning Star Radio

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Imani. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Imani. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, Aprili 04, 2014

Uwezo Wetu Na Nguvu Za Kuvumilia

Kila asubuhi tunapoamka, tunakumbana na siku mpya iliyojaa changamoto za maisha. Changamoto hizi huja kwa aina nyingi: changamoto za kimwili, pingamizi za kifedha, matatizo na mahusiano, majaribio ya kihisia, na hata mapambano na imani ya mtu.


Nyingi za changamoto tunazokabiliana nazo maishani zinaweza kutatuliwa na kushindwa, hata hivyo, nyengine huenda zikawa ngumu kuelewa na kutowezekana kushindwa na zitakuwa nasi mpaka tutakapoaga duniani. Tunapovumilia kwa muda changamoto tunazoweza kutatua na tunapoendelea kuvumilia changamoto ambazo hatuwezi kutatua, ni muhimu kukumbuka kwamba nguvu ya kiroho tunayokuza zitatusaidia kuvumilia vyema changamoto zote tunazokabiliana nazo maishani.


Ndugu na dada, tunaye Baba wa Mbinguni, anayetupenda, ambaye amesanifu kuwepo kwetu duniani ili tuweze kibinafsi kujifunza masomo tunayohitaji kujifunza ili kufuzu kwa ajili ya uzima wa milele katika uwepo wake.


Kipindi katika maisha ya Nabii Joseph Smith kinaeleza kanuni hii. Nabii na wenzi kadhaa walikuwa wamekuwa wafungwa kule Liberty, Missouri, kwa miezi. Wakiteseka gerazani, Nabii Joseph alimsihi Bwana katika maombi ya unyenyekevu kwamba Watakatifu wangeweza kufarijiwa kutokana na mateso yao ya sasa. Bwana alijibu kwa kumfundisha Nabii Joseph, na sisi sote, kwamba changamoto tunazokumbana nazo, zikivumiliwa vyema, zitatusaidia mwishowe. Hili ndilo jibu la Bwana kwa dua ya Joseph:

“Mwanangu, amani iwe katika nafsi yako, taabu yako na mateso yako yatakuwa kwa muda mfupi;

“Na halafu, kama utastahimili vyema, Mungu atakuinua juu.”


Baba wa Mbinguni amepanga safari yetu maishani kuwa mtihani wa silka zetu. Tunaachwa tushawishiwe na mema na mabaya na kisha kupewa wakala wa kimaadili kujichagulia wenyewe njia tutakayochukua. Kama vile nabii Samweli wa Kitabu cha Mormoni wa kale alivyofundisha, “Mko huru, mmekubaliwa kujichagulia, kwani tazama, Mungu amewapatia elimu na amewafanya huru.”


Baba wa Mbinguni pia alielewa kwamba kutokana na hali yetu ya kidunia hatungefanya chaguo sahihi au la haki kila wakati. Kwa sababu sisi si wakamilifu na kwa sababu sisi hufanya makosa, tunahitaji usaidizi ili kurudi kwa uwepo Wake. Msaada unaohitajika hutolewa kupitia mafundisho, mfano, na dhabihu ya upatanisho wa Yesu Kristo. Dhabihu ya upatanisho wa Mwokozi huwezesha wokovu wetu wa baadaye na utukufu kupitia kanuni ya toba. Tukitubu kwa uaminifu na dhati, Upatanisho unaweza kutusaidia kuwa wasafi, kubadilisha asili yetu, na kuvumilia vyema changamoto zetu.


Uvumilivu ni kanuni muhimu inayopatikana katika mafundisho ya Yesu Kristo. Ni muhimu kwa sababu uzuri wa maisha yetu ya baadaye ya milele unalingana na uwezo wetu wa kuvumilia katika wema.

Katika 2 Nefi 31 nabii Nefi anatufundisha kwamba baada ya kupokea agizo lile lile la wokovu la ubatizo ambalo Yesu Kristo alipokea na kisha tupokee karama ya Roho Mtakatifu, lazima “tusonge mbele tukila na kusheherekea neno la Kristo, na tuvumilie hadi mwisho, tazama, [na basi] hivyo ndivyo asema Baba: [Sisi] tutapokea uzima wa milele.”


Hivyo basi, ili kupokea baraka kuu ya zote za Baba yetu wa Mbinguni, ambayo ni uzima wa milele, lazima tukamilishe kazi ya agano inayostahili na kisha tuendelee kutii maagano yanayohusika. Yaani, lazima tuvumilie vyema.


Uwezo wetu wa kuvumilia hadi mwisho katika wema utakuwa unalingana moja kwa moja na nguvu ya ushuhuda wetu na kina cha uongofu wetu. Wakati shuhuda zetu ziko imara na tumeongoka kwa kweli kwa injili ya Yesu Kristo, chaguo zetu zitasawishiwa na Roho Mtakatifu, zitakuwa na msingi katika Kristo, na zitahimili hamu yetu ya kuvumilia katika wema. Ikiwa shuhuda zetu ni dhaifu na uongofu wetu ovyo, hatari ni zaidi kwamba tutashawishiwa na tamaduni za uongo za dunia ili kufanya chaguo mbaya.


Ningependa kushiriki tukio linaloonyesha juhudi inayohitajika kuvumilia kimwili na kisha kulilinganisha kwa juhudi inayohitajika kuvumilia kiroho. Baada ya kurudi kutoka misheni yangu, nilikuwa na nafasi ya kucheza mpira wa vikapu na kocha mwenye ushawishi mkubwa na mwandishi katika chuo kule California. Kocha huyu alikuwa makini sana kuhusu wachezaji wake kuwa katika hali nzuri ya kimwili kabla ya kuanza kwa msimu wa mpira wa vikapu. Moja ya mahitaji yake ya zoezi kabla ya yeyote kati yetu kuweza kugusa mpira wa kikapa kwenye kiwanja cha mazoezi ilikuwa ni kukimbia mzunguko wa mbio za nyika katika milima karibu na shule kwa wakati maalum na ngumu sana. Ninakumbuka jaribio langu la kwanza kabisa katika kukimbia kozi hii ya mbio za nyika punde baada ya kurejea kwangu kutoka misheni: Nilifikiria ningekufa.
Ilichukua wiki nyingi za mafunzo makali ili hatimaye kuvunja rekodi ya wakati ambao kocha alikuwa ameweka kama lengo. Ilikuwa ni hisia nzuri si ​​tu kuweza kukimbia mzunguko lakini pia kuharakisha hadi kwenye uhondo wa mwisho hadi kwenye laini ya kumaliza.


Ili kucheza mpira wa vikapu vyema, unahitaji kuwa katika hali nzuri ya kimwili. Kuwa katika hali nzuri ya kimwili huja kwa gharama, na gharama hiyo ni kujitolea, uvumilivu, na nidhamu ya kibinafsi. Uvumilivu wa kiroho pia huja kwa gharama. Ni gharama ile ile: kujitolea, uvumilivu, na nidhamu ya kibinafsi.


Ushuhuda, kama mwili wako, unahitaji kuwa katika hali nzuri kama unautaka hudumu. Hivyo basi ni jinsi gani tunaweka ushuhuda wetu katika hali nzuri? Hatuwezi kufanya miili yetu kuwa katika hali nzuri ya kucheza mpira wa vikapu kwa kutazama tu mpira wa vikapu kwenye televisheni. Vile vile, hatutaweza kuweka shuhuda zetu katika hali nzuri kwa kutazama tu mkutano mkuu kwenye televisheni. Tunahitaji kusoma na kujifunza kanuni za msingi za injili ya Yesu Kristo, na kisha ni lazima tufanye tuwezavyo kuizitumia maishani. Hivyo ndivyo tunavyokuwa wafuasi wa Yesu Kristo, na hivyo ndivyo tunavyojenga ushuhuda wa kudumu.

Tunapokabiliwa na shida maishani na hamu yetu ni kuiga sifa za Yesu Kristo, ni muhimu kuwa tayari kiroho. Kuwa tayari kiroho kunamaanisha tumekuza sulubu na nguvu ya kiroho---tutakuwa katika hali nzuri ya kiroho. Tutakuwa katika hali nzuri kiroho hata kwamba tutachagua wema kila mara. Tutakuwa hatuhamashiki katika hamu na uwezo wetu wa kuishi injili. Kama vile mwandishi mmoja asiyejulikana aliwahi kusema, “Ni lazima uwe mwamba ambao mto hauwezi kuondoa.”


Kwa sababu sisi tunakabiliwa na changamoto kila siku, ni muhimu kwamba tufanye kazi juu ya ushupavu wetu wa kiroho kila siku. Sisi  tunapokuza ushupavu wa kiroho, tamaduni za uongo za dunia, pamoja na changamoto zetu za kibinafsi za kila siku, zitakuwa na athari ndogo kwa uwezo wetu wa kuvumilia katika wema.


Mifano mizuri ya ushupavu wa kiroho huja kutoka historia za familia zetu wenyewe. Miongoni mwa hadithi nyingi kutoka kwa mababu zetu, tutaweza kupata mifano ambayo inaonyesha tabia chanya ya uvumilivu.

Hadithi kutoka kwa historia ya familia yangu mwenyewe inaeleza kanuni hii. Baba ya babu yangu mkuu Joseph Maynes Watson alizaliwa mnamo 1856 kule Hull, Yorkshire, Uingereza. Familia yake ilijiunga na Kanisa kule Uingereza na kisha kwenda Jijini Salt Lake. Alimuoa Emily Keep mnamo 1883, na wakawa wazazi wa watoto wanane. Joseph aliitwa kuhudumu misheni ya muda mnamo Juni 1910, alipokuwa na umri wa miaka 53. Na kwa usaidizi wa mke wake na watoto wanane, alirudi nchi yake ya asili Uingereza kuhudumu misheni yake.

Baada ya kuhudumu kwa uaminifu kwa takriban miaka miwili, alikuwa akiendesha baiskeli yake pamoja na mwenziwe kwenda misa ya Shule ya Jumapili kule Gloucester, Uingereza, ambapo tairi yake ikapasuka. Alishuka kutoka wa baiskeli yake ili kutathmini uharibifu. Alipoona ya kuwa ilikuwa imeharibika sana na ingechukua muda kurekebisha, alimwaambia mwenziwe amtangulie na kuanza ibada ya Jumapili na angefika pale baada ya muda mfupi. Punde tu alipomaliza kusema hayo, alianguka chini. Alikufa ghafula kutokana na mshtuko wa moyo.

Joseph Watson Maynes kamwe hakumwona mke wake na watoto wanane tena katika maisha haya. Waliweza kusafirisha mwili wake kurudi katika Jiji la Salt Lake na kuwa na huduma ya mazishi yake katika ukumbi mzee wa Waterloo Assembly Hall. Kauli iliyotolewa katika mazishi yake na Mzee Anthony W. Ivins wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili inatufundisha somo muhimu kuhusu maisha, kifo, na uvumilivu: “Hii ndiyo injili inatupa---si kinga kutokana na kifo, lakini ushindi juu yake kupitia matumaini ambayo tunayo katika ufufuo mtukufu. … Unamgusia [Joseph Maynes] . …Ni furaha, na jambo la kuridhisha na shangwe kujua kwamba wanadamu hujitolea maisha yao kwa haki, kwa imani, wakiwa wakweli kwa imani.”


Hadithi hii ya familia yangu inanishawishi kujaribu niwezavyo kufuata mfano wa uvumilivu na sulubu ya kiroho iliyoonyeshwa na baba ya babu yangu. Ninavutiwa pia na imani ya mke wake, Emily, ambaye maisha yake baada ya kifo cha Joseph hakika yalikuwa mzigo mzito kubeba. Ushuhuda wake ulikuwa imara na uongofu wake kamili akiishi maisha yake yote baadaye akiwa mwaminifu kwa imani akiwasaidia watoto wake wanane pekee yake.


Mtume Paulo alisema, “Na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi, na tupige mbio kwa subira katika yale mashinidano yaliyowekwa mbele yetu.” Mashindano yaliyowekwa mbele yetu katika dunia hii ni mbio ya uvumilivu, iliyojaa vizuwizi. Vizuwizi katika mashindano haya ni changamoto tunazoamka nazo kila asubuhi. Tuko hapa duniani ili kukimbia mbio, kutumia wakala wetu wa kimaadili, na kuchagua kati ya mema na mabaya. Ili kukamilisha mbio kwa heshima na mafanikio na kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni, tutalazimika kulipa gharama ya kujitolea, uvumilivu na nidhamu ya kibinafsi. Tunahitaji kuwa katika hali nzuri ya kiroho. Tunahitaji kukuza sulubu ya kiroho. Tunahitaji shuhuda imara zitakazoelekeza kwa uongofu wa kweli, na kwa matokeo tupate ndani yetu amani ya ndani na nguvu inayohitajika kuvumilia changamoto zozote huenda tukakabilina nazo.


Hivyo basi bila kujali changamoto unazoamkia kila asubuhi, kumbuka---na nguvu ya kiroho unayokuza, pamoja na msaada wa Bwana, mwishoni mwa mashindano utaweza kufurahia hakikisho ambalo Mtume Paulo alionyesha aliposema:


“Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.

“Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda:

“Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile.”

Nawatolea ushuhuda na ushahidi wangu wa uhalisi wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo na mpango wake wa furaha mkuu na wa milele, ambao umetuleta kwenye dunia hii wakati huu. Roho wa Bwana awavutie kukuza ndani yenu nguvu ya kuvumilia. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Chanzo:   INGIA HAPA 

Jumamosi, Machi 17, 2012

Tufanye Nini Na Mashaka!!!?....Majibu Yafanyayo Kazi.



 
WATU wengi, hasa wale walio wachanga katika maisha yao ya Kikristo, siku
nyingine husumbuliwa na mashauri yatolewayo na wale waonao mashaka juu ya mambo
ya dini na kuyakosoa. Kuna mambo mengi ndani ya Biblia wasiyoweza kuyafafanua, au
hata kuyaelewa, na Shetani huyatumia mambo hayo kuitikisa imani yao katika Maandiko
ili wasipate kuyaamini kuwa ni ufunuo utokao kwa Mungu. Wanauliza, wanasema,
“Nawezaje kujua njia ya kweli? Kama kweli Biblia ni Neno la Mungu, nawezaje
kuondolewa mashaka haya moyoni mwangu, nisije nikachanganyikiwa?”
Mungu hatuombi sisi kuamini bila ya kutupa ushahidi wa kutosha ambao juu yake
tunaweza kujenga imani yetu. Kuwako kwake, tabia yake, na ukweli wa Neno lake,
mambo haya yote yamehakikishwa kwetu kwa ushuhuda unaovutia katika akili zetu; na
ushuhuda huo upo tele. Hata hivyo Mungu hajaondoa kabisa uwezekano wa kuwapo
mashaka. Imani yetu ni lazima ijengwe juu ya ushahidi, siyo juu ya ufafanuzi utumiao
sababu zinazoonyesha mifano fulani. Wale wanaotaka kuona mashaka wataipata nafasi
hiyo; ambapo wale wanaotaka kweli kweli kuijua ile kweli watapata ushahidi mwingi
ambao juu yake wanaweza kuitegemeza imani yao.

Haiwezekani kabisa kwa akili za kibinadamu kuelewa kwa ukamilifu tabia au
kazi za Mungu yule wa milele. Kwa yule aliye na akili kali kabisa, kwa yule aliyepata
elimu ya juu kabisa, Mtakatifu huyo hana budi kubaki amefunikwa katika siri. “Je!
wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo
Mwenyezi? Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina
kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?” Ayubu 11:7,8.
Mtume Paulo asema, “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu!
hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani.” Warumi 11:33. Na ingawa
“Mawingu na giza vyamzunguka,” “haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.” Zaburi
97:2. Mpaka hapo tunaweza kufahamu anavyotushughulikia sisi, na kuyafahamu
makusudi yake yanayomsukuma kufanya hivyo, kiasi kwamba tunaweza kutambua
upendo wake usio na kikomo na rehema yake ifungamanayo na uweza wake usio na
mipaka. Tunaweza kufahamu mengi kuhusu makusudi yake kama aonavyo yeye kuwa ni
vyema kwetu kuyajua; na zaidi ya hapo bado yatupasa kuutegemea mkono wake wenye
uwezo wote, na moyo wake uliojaa upendo.

Neno la Mungu, kama ilivyo tabia ya Mwasisi wake wa kimbingu, lina mambo ya
siri yasiyoweza kufahamika kamwe kwa ukamilifu na wanadamu. Jinsi dhambi
ilivyoingia ulimwenguni, jinsi Kristo alivyofanyika mwili halisi wa kibinadamu,
kuzaliwa upya kulivyo, ufufuo, na masomo mengine mengi yaliyoelezwa katika Biblia, ni
mafumbo makubwa mno kushinda akili za kibinadamu kuyaeleza, wala hata kufahamu
maana yake kwa ukamilifu. Lakini hatuna sababu ya kuwa na shaka juu ya Neno la
Mungu kwa ajili ya kutozifahamu siri za maongozi yake. Katika ulimwengu huu wa asili
tunazungukwa daima na mafumbo tusiyoweza kuyafahamu. Vitu duni kabisa vyenye
uhai huwa tatizo kwetu, hata wanafalsafa wenye hekima nyingi sana hawana uwezo
kabisa wa kutupa maelezo yake. Mahali pote pana maajabu tusiyoweza kuyafahamu. Je! hivi tungeweza kushangaa basi, kuona kwamba katika ulimwengu wa kiroho kuna siri pia
tusizoweza kuzifahamu kabisa? Shida hasa inatokana kabisa na udhaifu na ufinyu wa
akili za kibinadamu. Katika Maandiko Mungu ametupa ushahidi wa kutosha kuonyesha
jinsi yalivyo na tabia ya kimbingu, nasi hatupaswi kuwa na mashaka na Neno lake kwa
sababu tu ya kukosa kuyaelewa mafumbo yote ya maongozi yake.

Mtume Petro amesema kwamba katika Maandiko “yamo mambo ambayo ni
vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa
… kwa uvunjifu wao wenyewe.” 2 Pet. 3:16. Ugumu upatikanao katika Maandiko hayo
umesisitizwa na wale wanaoyaonea mashaka mambo ya kidini kuwa ndiyo hoja yao
wanayotoa kuipinga Biblia; lakini mbali sana na ugumu huo, yenyewe yanatoa ushahidi
wenye nguvu kuonyesha kwamba uvuvio wake watoka kwa Mungu. Kama Biblia
ingekuwa haina habari za Mungu, ila tu mambo yale tuwezayo kuyaelewa kwa urahisi;
kama ukuu na utukufu wake ungeweza kufahamika na akili za kibinadamu, basi Biblia
isingekuwa na vitambulisho visivyokosea vionyeshavyo kwamba ina mamlaka ya
Mungu. Utukufu wenyewe hasa na siri ya mafundisho yake makuu yaliyotolewa humo,
mambo hayo yangeitia nguvu imani kuwa hilo ni Neno la Mungu kweli.

Biblia inaifunua kweli kwa maneno yanayoeleweka na yanayofaa kwa mahitaji na
matakwa ya moyo wa kibinadamu kiasi cha kuwashangaza na kuwavutia wale walio na
elimu ya juu kabisa, wakati inawawezesha walio duni kabisa na wasioelimika kuitambua
njia ya wokovu. Na hata hivyo kweli hizi zilizoelezwa kwa njia iliyo rahisi kueleweka
zinagusa masomo yaliyo juu mno, yenye maana pana mno, yapitayo kabisa upeo wa
ufahamu wa kibinadamu, hata twaweza kuyakubali tu kwa sababu Mungu ndiye
aliyeyatangaza. Hivyo mpango wa Mungu juu ya ukombozi wa wanadamu umewekwa
wazi kwetu, ili mtu awaye yote apate kujua hatua zinazompasa kuchukua katika toba
yake kwa Mungu, na kuwa na imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ili apate kuokolewa
kwa njia aliyoiweka Mungu. Walakini chini ya kweli hizo zinazoeleweka kwa urahisi
yapo mafumbo ambayo husitiri utukufu wake - mafumbo yanayozishinda akili za mtu
katika utafiti wake, lakini yanayomvutia yule aitafutaye kweli kwa moyo mnyofu na
kicho na imani. Kadiri anavyozidi kuichunguza Biblia, ndivyo imani yake inavyozidi
kuwa na kina kusadiki ya kwamba hilo ni neno la Mungu aliye hai, na hoja za
kibinadamu husalimu amri chini ya mfalme huyo wa mafunuo ya kimbingu.
Kukiri kwamba hatuwezi kuzielewa kweli kuu za Biblia kwa ukamilifu ni
kukubali tu kwamba akili finyu ya mwanadamu haitoshi kumwelewa Mungu wa milele,
kwamba mwanadamu, pamoja na maarifa yake ya kibinadamu yaliyowekewa mipaka,
hawezi kuyaelewa makusudi ya Mungu ajuaye yote.

Wenye kumkana Mungu hulitupilia mbali Neno lake kwa sababu hawawezi
kuyafahamu mafumbo yake yote; tena si wote wanaojidai kuwa wanaisadiki Biblia
ambao wameikwepa hatari hiyo katika suala hilo. Mtume asema, “Angalieni, ndugu
zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na
Mungu aliye hai.” Ebr. 3:12. Ni vizuri kujifunza sana mafundisho ya Biblia, na
kuyachunguza “hata mafumbo ya Mungu” (1 Kor. 2:10), kwa kadiri yanavyofunuliwa
katika Maandiko. Wakati “mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu,” yale
“yaliyofunuliwa ni yetu sisi.” Kum. 29:29. Lakini ni kazi yake Shetani kuipotosha akili
ya kibinadamu inayofanya uchunguzi huo. Kwa kiasi fulani kiburi huchanganyika na
mawazo yao wakati wa kuitafakari kweli ya Biblia, hata watu hao wanajisikia ya kuwa
wamekosa uvumilivu na kushindwa kama hawawezi kuielezea vizuri kila sehemu ya Maandiko hadi wametosheka kabisa. Wanaona wamejidhalilisha mno kukiri kwamba
hawayaelewi maneno hayo yaliyovuviwa. Hawako tayari kungoja kwa uvumilivu mpaka
Mungu atakapoona inafaa kuwafunulia hiyo kweli. Wanaona kwamba hekima yao ya
kibinadamu pasipo msaada wa Mungu inatosha kuwawezesha kuyaelewa Maandiko
hayo, nao wakishindwa kufanya hivyo, wanayakana kabisa kuwa si ya Mungu. Ni kweli
kwamba nadharia nyingi na mafundisho mengi yanayodhaniwa kuwa yametoka katika
Biblia hayana msingi wo wote kama huo katika mafundisho yake, na kwa kweli
yanapingana na mfumo mzima wa uvuvio. Kwa wengi mambo hayo yamekuwa sababu
ya kuingiwa na mashaka na kuchanganyikiwa. Walakini, shutuma hizo haziwezi
kutolewa dhidi ya Neno la Mungu kutokana na hali hiyo; ila zinaweza kutolewa dhidi ya
upotoshaji wa neno hilo unaofanywa na mwanadamu.

Kama wanadamu wangeweza kufahamu kwa ukamilifu jinsi Mungu alivyo hasa,
pamoja na matendo yake yalivyo, basi, wakiisha kufika hapo, wasingeweza kuvumbua
kweli yo yote mpya, wasingeweza kuongeza maarifa yao, wasingeweza kukua zaidi
kiakili au kiroho. Mungu asingekuwa Mwenye enzi tena; na, mwanadamu, baada ya
kufika mwisho wa maarifa na mafanikio yake, angekoma kusonga mbele. Na tumshukuru
Mungu kwamba mambo hayajawa hivyo. Mungu ni wa milele; na ndani yake zimo
“hazina zote za hekima na maarifa.” Kol. 2:3. Na milele hata milele wanadamu
wataweza kuendelea kuchunguza, na kujifunza, lakini hawataweza kamwe kuzimaliza
hazina zote za hekima yake, wema wake, na nguvu zake.

Mungu amekusudia ya kuwa kweli za Neno lake ziendelee kufunuliwa daima kwa
watu wake hata katika maisha haya. Kuna njia moja tu ambayo kwayo maarifa hayo
yanaweza kupatikana. Tunaweza kuufikia ufahamu wa Neno la Mungu kwa njia moja tu
ya kuelimishwa na Roho ambaye kwa njia yake Neno hilo lilitolewa. “Mambo ya Mungu
hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu,” kwa “maana Roho huyachunguza yote, hata
mafumbo ya Mungu.” 1 Kor. 2:11,10. Na ahadi yake Mwokozi kwa wafuasi wake
ilikuwa ni hii, “Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye
kweli yote;…atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.” Yoh. 16:13,14.

Mungu ataka mwanadamu atumie akili zake; na kule kujifunza Biblia
kutaiimarisha na kuikuza akili yake kwa namna ambayo hakuna njia nyingine yo yote
iwezavyo kufanya. Lakini tujiangalie tusiifanye akili yetu kuwa mungu wetu, akili
inayokabiliwa na udhaifu wa kibinadamu na kupungua nguvu yake. Kama hatutaki
Maandiko hayo yatuletee hali ya kuchanganyikiwa katika mawazo yetu, kiasi cha
kuzifanya kweli zile zinazoeleweka kwa urahisi sana tusiweze kuzielewa, basi, ni lazima
tujishushe na kuwa na imani kama ya mtoto mdogo, tukiwa tayari kujifunza, na kuomba
sana ili tupate msaada wa Roho Mtakatifu. Hisia ya kutambua uwezo na hekima aliyo
nayo Mungu, na kutambua kutoweza kwetu kuufahamu ukuu wake, mambo hayo
yangetuamsha sisi ili tupate kuwa na unyenyekevu, nasi tungelifungua Neno lake kwa
kicho kitakatifu, kana kwamba tuko mbele zake. Tunapoisoma Biblia, ni lazima akili
zetu zikiri kwamba ina mamlaka kuu mno kuliko zilivyo akili zetu zenyewe, na moyo na
akili zetu ni lazima zimpigie magoti huyo MIMI NIKO aliye mkuu.

Kuna mambo mengi ambayo yanaonekana dhahiri kuwa ni magumu au ni
mafumbo, ambayo Mungu atayafanya kuwa wazi na rahisi kwa wale ambao kweli
wanataka kuyafahamu. Lakini bila uongozi wa Roho Mtakatifu tutaendelea daima
kuyapotoa Maandiko hayo au kuyafasiri vibaya. Kuna usomaji mwingi wa Biblia
usioleta faida yo yote, na katika mifano mingi huleta madhara yaliyo dhahiri. Neno la Mungu linapofunuliwa bila heshima na bila maombi; mawazo ya mtu na mapenzi yake
yasipokazwa kwa Mungu, au yasipopatana na mapenzi yake, hapo ndipo mawazo ya mtu
huyo hufunikwa na wingu la mashaka; na katika kujifunza kuko huko kwa Biblia
mashaka ya kutoliamini Neno la Mungu huimarishwa. Adui anayatawala mawazo ya
mtu huyo, tena anamshawishi kutoa tafsiri zisizo sahihi. Kila mara wanadamu
wasipopatana na Mungu katika maneno na matendo yao, hapo ndipo, licha ya wao kuwa
wasomi sana kama walivyo hasa, wanakuwa na mwelekeo wa kukosea katika uelewa
wao wa Maandiko, wala si salama kuyategemea maelezo yao. Wale wanaoyaangalia
Maandiko ili kugundua hitilafu hawana ufahamu wa kiroho. Wakiwa na mtazamo
uliopotoka wataona sababu nyingi za kuwa na mashaka na kutosadiki mambo yale
ambayo ni wazi na rahisi kweli kweli.

Hata ifichwe namna gani, sababu hasa ya kuwa na mashaka na kulishuku Neno
la Mungu, kwa hali nyingi, ni kupenda dhambi. Mafundisho na vizuizi vya Neno la
Mungu havipendezi kwa wenye moyo wa kujisifu na kupenda dhambi, na wale
wasiotaka kuyatii matakwa ya Biblia huwa wepesi kutosadiki ya kuwa hilo ni Neno halisi
la Mungu. Ili kuweza kuipata kweli ni lazima tutamani kuijua hiyo kweli, na kuwa na
moyo ulio tayari kulitii. Na wote wanaokuja kujifunza Biblia wakiwa na roho hiyo
watapata ushahidi mwingi uonyeshao kuwa hilo ndilo Neno la Mungu, nao wataweza
kuzijua kweli zake zitakazowahekimisha hata wapate wokovu.

Kristo amesema, “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi Yake, atajua habari ya yale
mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu.” Yoh. 7:17. Badala ya kuona mashaka na
kuyakosoa mambo msiyoweza kuyafahamu, izingatieni nuru ambayo tayari inaangaza juu
yenu, nanyi mtapokea nuru kubwa zaidi. Kwa neema yake Kristo tekelezeni kila wajibu
uliofunuliwa wazi katika ufahamu wenu, ndipo mtawezeshwa kuujua na kuutekeleza ule
ambao mnauonea mashaka sasa.
Uko ushahidi ulio wazi kwa wote - kwa wasomi sana, na kwa wasiojua kabisa
kusoma na kuandika - huo ni ushahidi unaoonekana katika matukio ya maisha ya mtu
mwenyewe. Mungu anatualika tujihakikishie sisi wenyewe ukweli wa Neno lake, na
ukweli wa ahadi zake. Anatuagiza, anasema, “Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu
mwema.” Zab. 34:8. Badala ya kulitegemea neno la mtu mwingine, yatupasa kuonja sisi
wenyewe. Anatutangazia, “Ombeni, nanyi mtapata.” Yoh. 16:24. Ahadi zake
zitatimia. Hazijapata kushindwa kamwe; kamwe haziwezi kushindwa. Na wakati
tunapomkaribia Yesu, na kufurahishwa na upendo wake, mashaka yetu na giza
linalotufunika vitatoweka katika nuru ya kuwako kwake.

Mtume Paulo asema ya kwamba Mungu alituokoa “na nguvu za giza,
akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.” Kol. 1:13. Na
kila mmoja ambaye “amepita kutoka mautini kuingia uzimani” anaweza kutia “muhuri ya
kwamba Mungu ni kweli.” Yoh. 5:24; 3:33. Anaweza kushuhudia hivi, “Nilihitaji
msaada, niliupata ndani yake Yesu. Mahitaji yangu yote nilipewa, njaa ya moyo wangu
ilishibishwa; na sasa Biblia imekuwa kwangu ufunuo wa Yesu Kristo. Waniuliza mbona
namwamini Yesu? - Kwa sababu ni Mwokozi wangu kutoka mbinguni. Kwa nini
naisadiki Biblia? - Kwa sababu nimeiona kuwa ni sauti ya Mungu kwa moyo wangu.”
Twaweza kuwa na ushuhuda ndani yetu wenyewe uonyeshao kwamba Biblia ni ya kweli,
na ya kwamba Kristo ni Mwana wa Mungu. Twajua kwamba hatufuati “hadithi
zilizotungwa kwa werevu.” 2 Petro 1:16. Petro awasihi ndugu zake anasema, “Kueni katika neema, na katika kumjua
Bwana wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.” 2 Petro 3:18. Watu wa Mungu
wakiendelea kukua katika neema yake, wataendelea zaidi kulifahamu Neno lake.
Wataitambua nuru na uzuri mpya na kweli zake takatifu. Jambo hili limedhihirika kuwa
ni la kweli katika historia ya kanisa katika vizazi vyote, na litaendelea kuwa hivyo mpaka
mwisho. “Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, ikizidi kung’aa hata mchana
mkamilifu.” Mithali 4:18.

Kwa imani twaweza kutazama mbele, na kuishikilia sana ahadi ya Mungu
kwamba akili zetu zitakua, uwezo wetu wa kibinadamu utaunganika na ule wa Mungu, na
kila nguvu ya kiroho itagusana moja kwa moja na yule aliye Chimbuko la nuru.
Twaweza kushangilia kwamba yote yaliyotufanya tuchanganyikiwe kuhusu maongozi ya
Mungu kwetu, wakati ule yataeleweka wazi; mambo yaliyokuwa magumu kwetu
kuyaelewa, wakati ule tutapata maelezo yake; na pale ambapo akili zetu finyu za
kibinadamu ziliona machafuko tu na makusudi yaliyoshindikana kutekelezwa, tutaona
mwafaka mkamilifu kabisa na mzuri ajabu. “Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo
kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa
sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.” 1 Kor. 13:12.

WIMBO

1st Stanza:
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kukubali neno lake
Nina raha moyoni.

Chorus:
Yesu, Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu, Yesu yu thamani,
Ahadi zake kweli.

2nd Stanza:
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kuamini damu yake
Nimeoshwa kamili.

3rd Stanza:
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kwake daima napata,
Uzima na amani.

4th Stanza:
Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea;
Yesu, M-pendwa, Rafiki,
Uwe nami dawamu.

(Nyimbo za Kristo, 129.. 'Tis so sweet to trust in Jesus’)


********************************

Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Cheryl Fortune

Anapoimba Nyimbo kwa mfululiza wa kwanza tafsiri yake ipo hapo juu unaoitwa

'Tis so sweet to trust in Jesus’

na wa pili unaitwa ‘Oh how I love Jesus’

MARA BAADA YA HIZO NYIMBO

Doug Batchelor  

a t a t w a m b i a    k u h u s u:

The Great Judgment Day





Pata nyimbo KWANZA.

 





                                                               ...sasa tufuatilie Ujumbe unaohusu SIKU YA HUKUMU KUU.

Jumamosi, Februari 25, 2012

Majibu Yafanyayo Kazi...SINAGOGI vs KANISA.


Sinagogi ni nyumba ya dini na ya jamii ya Wayahudi inayotumika hasa kusali.

Etimolojia

Neno linatokana na Kigiriki  sinagoge likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya Kiebrania  beit knesset yaani "nyumba ya mkutano". Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kutajia sinagogi.

Muundo

Chumba kikuu ni ukumbi wa sala lakini mara nyingi kipo pamoja na vyumba vya pembeni kama vile madarasa, ofisi na vingine. 

Historia

Katika Israeli ya Kale (kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 587 KK) inaonekana hakukuwa na sinagogi: walau halitajwi kabisa katika Agano la Kale.
Hakuna uhakika kamili lakini inaonekana ya kwamba masinagogi yalianzishwa baada ya hekalu ya Yerusalemu kubomolewa pamoja na kuanza uhamisho wa Wayahudi kwenda nchi mbalimbali.
Tangu kuharibiwa kwa Hekalu la Pili mwaka 70 Wayahudi wana masinagogi tu kufanyia ibada.



Kanisa

Kwanza kabisa neno Kanisa linamaanisha "mkusanyiko wa waamini" kama ule wa Waisraeli chini ya Musamlima Sinai walipopewa Amri za Mungu. kwenye
Neno hilohilo lilitumiwa na Wakristo wa kwanza kwa ajili yao wenyewe kusema wameshika nafasi ya Israelitaifa la Mungu hata wasipokuwa Wayahudi bali watu wa mataifa mengine. kama
Jina hilo lilitumika kwa jumuia mama ya Yerusalemu, kwa kila mojawapo ya jumuia za Kikristo zilizotokana na umisionari wa wafuasi wa Yesu Kristo, na kwa umoja wao wa kimataifa uliotazamwa na Mtume PauloMwili wa Kristo, ukiwa na Yesu kama kichwa chake. kuwa

Kanisa kama jengo


Wakristo walipoanza kujenga mahali pa ibada, pakaja kuitwa vilevile "kanisa" kwa sababu ndani yake lilikusanyika Kanisa hai.
Hivyo mara nyingi neno hilo linatumika kwa maana ya jengo, ambalo ni mfano mwingine uliotumiwa na Paulo kuhusu umoja wa Wakristo, ukiwa na Yesu kama jiwe kuu la msingi.
Majengo hayo ya ibada yanaweza kuwa na ubora tofauti hata upande wa sanaa; baadhi yake yanatembelewa na watalii na kuhifadhiwa kwa bidii kwa sababu hiyo.
Kwa namna ya pekee ni muhimu Kanisa kuu la kila jimbo (dayosisi), halafu Basilika na Patakatifu.


 

Madhehebu

Baada ya umoja wa Wakristo kuanza kuvunjika, kwa kawaida madhehebu yaliyotokea yaliendelea kujiita makanisa, ingawa kwa maana mbalimbali: hasa Kanisa Katoliki na Waorthodoksi wanadai kuwa la kwao ndilo linaloendeleza Kanisa pekee la kweli; kumbe Waprotestanti hawatii maanani sana umoja wa Wakristo upande wa miundo, bali ule wa kiroho.
Ndani ya Kanisa Katoliki, linalokubali uongozi wa Papa wa Roma, neno Kanisa linatumika pia kumaanisha kila jimbo na makundi ya majimbo yanayochanga mapokeo yaleyale upande wa teolojia, liturujia, maisha ya kiroho, sheria n.k.
Kwa msingi huo Kanisa la Kilatini, ambalo lilienea kwanza upande wa magharibi wa Dola la Roma (Kanisa la Magharibi), linatofautishwa na Makanisa ya Mashariki yaliyoenea kwanza upande wa mashariki wa dola hilo na nje ya mipaka yake.

Mfumo  wa Waadventista Wasabato

 

Agizo la utume wa Mwokozi kwa kanisa kupeleka injili ulimwnegunu mwote (Mat. 28:19-20; Marko 16:15) halikumaanisha tu kuhubiri ujumbe bali kuhakikisha ustawi wa wale walioupokea ujumbe ule. Hii ilhusisha kuchuga na pia kulipatia kundi makazi, na pia kukabiliana na matatizo ya mahusiano. Hali kama hiyo ilihitaji mfumo (Oganaizaisheni).

Mwanzoni mitume wao wenyewe waliunda baraza ambalo liliongoza shughuli  katika kila kanisa (Mdo.14:23).Kanisa lile changa kutoka Yerusalemu (Mdo. 6:2; 8:14). Pale kundi la jijini lilipokuwa kubwa kiasi kwamba uendeshaji wa shughuli zao za dhati ukawa tatizo,mashemasi waliteuliwa kusimamia shughuli za kanisa (Mdo. 6:2-4). Pia inaonekana wazi kutokana na kumbukumbu za Mungu kwamba upanuzi wa kazi katika majimbo mbalimbali ya Dola ya Kirumi ulihitaji mfumo wa kanisa katika kile mabacho kinaweza kuitwa konferensi. Zilijumuisha makanisa katika ,jimbo mahsusi, kama vile makanisa ya Galatia(Waga.1:2); likawa na mfumo(oganaizesheni). Kadri mahitaji yalivyojitokeza Mungu aliwaongoza na kuwaelekeza viongozi wa kazi yake.

Madaraja katika mfumo wa kiutawala wa Waadventista Wasabato

Miongoni mwa Waadventista wasabato kuna madaraja manne ya uwakilishi kuanziamuumini mmoja hadi mfumo(oganaizesheni)mzima wa kazi ya kanisa ulimwenguni pote.

1. Kanisa moja;
Jamii iliyoungana katika mfumowa kundi la waumini mmoja mmoja.

2. Konferensi, fildi au misheni ya sehemu moja
Muungano wa jamii ya makanisa katika nchi, mkoa au eno la nchi.

3. Union inayojitegmea
Hii ni jamii ya muungano wa koferensi, fildi au misheni kadhaa ndani ya eneo kubwa la nchi.

4. Halmasahuri kuu
Ambayo ni sehemu kubwa ya mfumo wa utawala, unaounganisha union zote pande zote za ulimwengu. Divisheni ni shemu ya Halmashauri kuu, zikiwa na mamlaka katika maeneo maalumu yaliyotengwa
kijiografia.

Kila mshiriki wa kanisa ana sauti katika kuchagua maofisa wa kanisa. Kanisa huchagua maofisa wa fildi au konferensi. Wajumbe waliochaguliwa na fildi au konferensi huwachagua maofisa wa union zilizo konferensi au union misheni, na wajumbe waliochaguliwa na union konferensi au union misheni huwachagua maofisa wa halmashauri kuu. Kwa mpangilio huu kila konferensi au fildi, kila taasisi, kila kanisa na kila mshiriki binafsi, aidha moja kwa moja au kupitia wawakilishi, ana sauti kwa uchaguzi wa watu wanaobeba majukumu makubwa katika halmashauri kuu.

Halmashauri kuu , Mamlaka ya Juu Zaidi

Halmashauri kuu katika kikao rasmi cha kila miaka mitano,na Kamati ya Utendaji ikutanikayo katikati ya vikao rasmi, ndicho chombo cha juu zaidi katika utawala wa shuguli za kanisa uimwenguni kote, na chombo hicho kimepewa mamalaka na katiba yake kuunda mashirika yalio chini yake ili kuendeleza maslahi mahsusi katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa hiyo basi imeeleweka wazi kwamba mashirika yote madogomadogo na taasisi ulimwenguni kote zitatambua Halmashari kuu kama mamalaka iliyo juu zaidi, chini ya Mungu miongoni wa Waadventista Wasabato. “Mara kwa mara nimeagizwa na Bwana ya kwamba maamuzi ya mtu yasisalimishwe kwa maamuzi ya mtu mwingine yeyote. Kamwe nia ya mtu mmoja au nia za watu wachache zisichukuliwe kama zatosha kwa hekima na uwezo kudhibiti kazi na kusema ni mipango ipi ndo itakayofuatwa. 

Lakini katika kikao rasmi cha halmashauri kuu, wakati maamuzi ya ndugu waliokusanyika pamoja kutoka sehemu zote za kazi ulimwenguni yanapotolewa, basi ushupavu binafsi na maamuzi binafsi ya pekee yasishiikiliwe kwa ukaidi, ila sharti yasalimishwe. Kamwe mtenda kazi asichukulie kuwa ni sifa kushikilia kwa ushupavu msimamao wake wa kutoambilika, kinyume cha uamuzi wa watu wote kwa ujumla. Nyakati nyingine kikundi, wakati ambapo kikundi kidogo cha watu kwa jumla waliokabidhiwa kusimamia kazi, kwa jina la Halmashauri kuu, wamejaribu kuendesha mipango isiyo ya busara nahivyo kuzuia kazi ya Mungu, hapo nimesema kuwa nisingeweza tena kuendelea kuheshimu sauti ya Halmashauri kuu iliyowakilishwa na watu hao wachache, kama sauti ya Mungu. Lakini hii siyo kusema kwamba maamuzi ya halmashauri kuu yenye wajumbe waliochaguliwa rasmi kutoka sehemu zote za kazi ulimwenguni hayapaswi kuheshimiwa. Mungu ameagiza kwamba wawakilishi wa kanisa lake kutoka sehemu zote za kazi duniani, wanapokusanyikakatika kikao cha Halmashauri kuu, watakuwa na mamlaka"-EG White

  ********************************

Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Doug Batchelor  

a n a p o t w a m b i a    k u h u s u:

Who are the Seventh-day Adventists?

(AmazingFacts)



KARIBU TENA

Jumapili, Februari 19, 2012

Je, Roma Itatawala Ulimwengu Tena?


 KANISA LA MTAKATIFU PETRO, ROMA


Photo Credit by: www.minutetravelguide.com

Maridhiano ya Kufisha

Mtume Paulo, katika Waraka wake wa Pili kwa Wathesalonike, alitabiri juu ya uasi mkuu ambao ungeleta
matokeo ya kuianzisha mamlaka ile ya upapa. Alitangaza kwamba siku ile ya kuja Kristo isingeweza kuja, “usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa mtu yule wa dhambi (kuasi), mwana wa uharibifu; yule  Mpingamizi [Mpinga Kristo], ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu [kanisa] la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” Tena, zaidi ya hayo, Mtume huyo anawaonya ndugu zake kwamba “ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 Wakorintho 2:3,4,7. 

Hata katika kipindi kile cha mwanzo kabisa aliona yakiingia ndani ya kanisa mafundisho potofu
ambayo yangetayarisha njia ya kujitokeza kwa upapa. Kidogo kidogo, mwanzoni kwa siri na kimya kimya, na baadaye kwa wazi zaidi, ikaongezeka nguvu yake na kuitawala mioyo ya wanadamu, ile “siri ya kuasi” ikaiendeleza mbele kazi yake kwa kutumia madanganyo na makufuru. Karibu bila kutambulikana kabisa desturi zile za kikafiri zikaingia ndani ya kanisa la Kikristo. Roho ile ya maridhiano na kufanana-fanana
[na dunia] ilizuiwa kwa wakati fulani kutokana na mateso makali ambayo kanisa lilistahimili chini ya wapagani. Lakini mateso yale yalipokoma, na Ukristo ulipoingia katika mabaraza na majumba ya kifalme, ndipo kanisa lile lilipouweka kando unyenyekevu ule wa Kristo na Mitume wake na kujitwalia
ufahari na kiburi cha makuhani na watawala wale wa kipagani; na mahali pa matakwa ya Mungu likaweka nadharia zawanadamu pamoja na desturi zao. 

Kuongoka kwa jina tu kwa Konstantino, mapema katika karne ile ya nne, kulileta shangwe kubwa; na  ulimwengu [upagani], ukiwa umevikwa joho la mfano wa haki, ukatembea na kuingia ndani ya kanisa. Basi,
kazi ile ya uharibifu ikasonga mbele kwa haraka sana. Upagani, wakati ukionekana kana kwamba umeshindwa kabisa, ukawa ndio mshindi. Roho yake ikalitawala kanisa lile. Mafundisho yake ya dini, sherehe zake, na ushirikina wake vikaingizwa katika imani na ibada ya wale waliojidai kuwa ni wafuasi wake Kristo.

CHANZO CLICK HAPA

Jumamosi, Februari 18, 2012

MAJIBU YAFANYAYO KAZI...”THE WINGS OF OUR FLIGHT”


NINAPENDA KUKUJULISHA KIJIWE HIKI AMBACHO NINA UHAKIKA KUNA MAMBO MAKUBWA MAZURI YATAKAYOKUSAIDIA KTK MAISHA IKIHUSISHA ZAIDI SUALA LA KIROHO KWA YULE ANAYEWIWA.

NI WEBSITE YA SOUTHERN HIGHLANDS CONFERENCE IKIHUSISHA MIKOA YA MBEYA, IRINGA  (Mikoa mingine nimeisahau kidogo ila itembelee wewe mwenyewe). UNAWEZA UKAITEMBELEA KUPITIA ANUANI IFUATAYO:
 http://www.shcadventist.org

Makao makuu yapo Iganzo, Chunya Road - Mbeya
Mawasiliano        info@shcadventist.org
Telephone:     +255 753 199020
Fax:               +255 25 2502367
Mobile Phone Number:     +255 718 378837 


********************************
Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Napenda kukujulisha kuwa lile Kongamano la Mawasiliano la Union litmefanyika na leo ndio hitimisho Februari 18, 2012 kama ilivyopangwa katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Mwenge Dar es salaam.

Wahudumu wa Kongamano hili lenye Motto :
”THE WINGS OF OUR FLIGHT”  
wametoka General Conference, East-Central Africa Division, Tanzania Union na wataalamu wetu wa ndani waliobobea.

Kando ya Maofisa wetu wa Union, Konferensi/Fildi, Wakurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Jamii, Wataalamu wa IT wa Fild na Konferensi, Wajumbe wa Kongamano hili walijumuishwa pia wachungaji wa mitaa, wazee wa kanisa, viongozi wa kanisa wa mawasiliano na uhusiano na jamii, wataalamu wa Teknohama na washiriki wote.

Kongamano hili lilijadili Nyanja nne kuu za mawasiliano:
 
(A) - Print Media, 
(B) - ICT, 
(C) - Radio na 
(D) - Television Broadcasting.
  
The topics include though not limited to: 
* Production Playback and Feedback, 
* Ethics and Adventist Communication Issues, 
* Writing Adventist News, 
* Quality Production and Maintenance of high Production 
* Standards, 
* Public Relations, 
* Writing For Broadcasting, 
* Interface with Public Print and Broadcast Media, 
* Writing for Print, 
* Effective Interview, 
* Podocasting, 
* Magazine formats , 
* Adventist Websites, 
* NetAdventist, 
* A week of Prayer through Social networks, 
* Twitting  for Commission, 
* The Communication Secretary (for Church), 
* Crisis management issues.

Wapendwa sasa vifaa vya mawasiliano vya kisasa zaidi vinaendelea kuwekwa makanisani. Hii ni fursa yako muafaka kujifunza kuvitumia ili kutimiza utume wa kanisa kwa mafanikio makubwa. Naamini hutadiriki kukosa fursa hii. 

Ijumaa, Februari 10, 2012

AMRI YA JUMAPILI KWA TAIFA ZIMA

1.     Biblia yasemaje juu ya Amerika ya Kiprotestanti itakavyoisujudu Mamlaka ile ya Kikatoliki ya Roma? Ufu.13:11-17.

Photo Credit By: temcat.com

2. Je, unabii huo utatimizwa lini?

a. "Unabii wa Ufunuo 13 unatangaza kwamba mamlaka ile iliyowakilishwa na mnyama aliye na pembe kama za mwana-kondoo ita"ifanya dunia na wote wakaao ndani yake wausujudu upapa -----ulioonyeshwa hapo kama mnyama "mfano wa chui."... Unabii huo utatimizwa wakati ule Marekani itakapotunga amri ya kuitunza Jumapili, tendo ambalo Roma inadai kuwa ni kuutambua ukuu wake kwa namna ya pekee." GC 578,579.

b. "Kulazimisha utunzaji wa Jumapili kwa upande wa Uprotestanti ni sawa na kulazimisha ibada ya upapa." GC 448.

3. Shinikizo la kuitungia amri [sheria] Jumapili litatoka wapi?

a. "Viongozi wakuu wa kanisa na serikali wataungana ili kuwahonga, kuwashawishi, au kuwalazimisha watu wa tabaka zote wapate kuiheshimu Jumapili. Kule kukosekana kwa mamlaka ya Mungu [katika Biblia] kutafanya zipate kutungwa amri kali za ukandamizaji. Rushwa katika ngazi za kisiasa inaharibu moyo ule wa kupenda haki na kuijali kweli; hata katika Amerika iliyo huru, watawala na watunga sheria, ili kupata upendeleo wa umma, watakubali madai ya wengi wanaopendelea iwepo amri [sheria] ya kulazimisha utunzaji wa Jumapili." GC 592 (Angalia pia 4SP 410).

b. "Ili kujipatia hali ile ya kupendwa na watu wengi na haki ya kuweza kuteuliwa, watunga sheria watakubaliana na madai ya kuwapo kwa amri ya Jumapili." 5T 451.

c. "Watunga sheria watakubaliana na madai ya kuwapo kwa amri za Jumapili." PK 606.

d. "Waprotestanti wa Marekani watakuwa mstari wa mbele katika kuinyosha mikono yao juu ya ghuba ili kuushika mkono wa Imani ya Mizimu; tena, watainyosha juu ya shimo kubwa lenye kilindi kirefu kushikana mikono na Mamlaka ile ya Roma; hapo ndipo, chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu, nchi hii itafuata katika nyayo za Roma kwa kuikanyaga chini ya miguu yake haki ya mtu kuamini kama dhamiri yake inavyotaka." GC 588.

e. "Iwapo watu wanaweza kushawishika kupendelea iwepo amri ya Jumapili, basi, wachungaji na mapadre wanakusudia kutumia nguvu ya mvuto wao wa pamoja katika kujipatia marekebisho ya dini katika Katiba ya nchi, na kulilazimisha Taifa zima [la Marekani] kuitunza Jumapili." RH, Extra 12-24-1889, uk.2.

4. Je! hao wanaoitetea Amri ya Jumapili wanatambua wanalolitenda?

a. "Pana watu wengi, hata miongoni mwa wale walio katika shughuli hiyo ya kutaka itungwe Amri ya Jumapili, ambao wamepofushwa macho yao wasiweze kuona matokeo yatakayofuata baada ya kitendo hicho kutekelezwa. Hawaoni ya kwamba wanaupiga rungu uhuru wa dini moja kwa moja. Wako wengi ambao hawajapata kuyaelewa kamwe madai ya Sabato ya Biblia na msingi wa uongo ambao Amri ya Jumapili inaukalia." 5T 711. b. "Wanafanya kazi hiyo wakiwa vipofu. Hawaoni ya kwamba kama Serikali yao ya Kiprotestanti inaziachilia mbali kanuni zilizowafanya kuwa Taifa huru, linalojitegemea, na kwa njia ya kutunga sheria wanaingiza katika Katiba ya Nchi, kanuni ambazo zitatangaza uongo wa upapa na madanganyo ya upapa, watakuwa wanajitumbukiza katika utawala wa hofu wa Roma wa Zama zile za Giza." RH, Extra 12-11-1888, uk.4.

c. "Kuna nguvu ya Kishetani inayoliendesha tapo [kundi] hilo la Jumapili, ila imejificha. Hata watu wale waliojiingiza katika kazi hiyo, wamepofushwa macho yao wasiweze kuona matokeo yatakayofuata baada ya kazi ya tapo lao kukamilika." RH 1-1-1889, uk.1; 7BC 975.

5. Ni nani hasa aliye mwanzilishi mwamba mkuu wa kuitungia amri Jumapili?

a. "Hakuna hatua yo yote iliyochukuliwa katika kuitukuza Sabato hiyo ya sanamu, na kuileta Jumapili ipate kutunzwa kwa kuitungia amri [sheria], isipokuwa ni yule Shetani aliye nyuma yake, na ndiye amekuwa mtendaji mkuu." 7BC 977.

b. "Bunge litakapotunga sheria ambazo zinaitukuza siku ya kwanza ya juma, na kuiweka mahali pa siku ile ya saba, hapo ndipo hila ya Shetani itakuwa imekamilika." 7BC 976.

c. "Sabato hiyo ya uongo [Jumapili] italazimishwa kwa njia ya kuitungia sheria [amri] ya ukandamizaji. Shetani na malaika zake wako macho sana, nao wanashughulika vibaya sana, wakifanya kazi kwa nguvu na ustahimilivu kupitia kwa wakala wao wa kibinadamu ili kulitimiza kusudi lake la kufutilia mbali katika mioyo ya watu maarifa ya kumjua Mungu." 7BC 985; RH 12- 13-1892.

6. Je, Amri hiyo ya Jumapili inaonyesha dharau juu ya nani?

"Juhudi zaidi ya wazi itafanyika kuitukuza sabato hiyo ya uongo, na kumwonyesha dharau Mungu Mwenyewe kwa kuibadili siku ile aliyoibariki na kuitakasa. Sabato hiyo ya uongo [Jumapili] italazimishwa kwa sheria ya ukandamizaji." 7BC 985.

7. Je, tutazamie kuziona sheria za Jumapili katika majimbo yanayojitawala (states) fulani fulani tu au Bunge la Marekani litachukua hatua ya kuitunga sheria hiyo[kwa Taifa zima]?

a. "Nchi yetu [ya Marekani] imeingia hatarini. Wakati unakaribia ambapo watunga sheria [Wabunge] wake watakapozikataa kabisa kanuni zile za Uprotestanti na kuunga mkono uasi wa Kanisa Katoliki. Watu hao ambao Mungu amewatendea maajabu makubwa sana, akiwatia nguvu kulitupilia mbali lile kongwa linaloumiza sana la upapa, kwa njia ya sheria ya taifa zima wataitia nguvu nyingi imani potofu ya Roma, na kwa njia hiyo kuuamsha utawala ule wa mabavu ambao unangojea tu uguswe ili uanze tena ukatili wake na udikteta." 4SP 410 (1884); ST, 7-17-1907, uk.1907, uk.7.

b. "Tunaona ya kwamba juhudi zinafanywa ili kutuwekea vizuizi katika uhuru wetu wa dini. Hoja ya Jumapili sasa inafikia viwango vikubwa. Marekebisho ya Katiba yetu ya nchi yanasisitizwa katika Bunge la Marekani, na mara yatakapopatikana, basi, ni lazima ukandamizaji utafuata." RH, 12-18-1888, uk.786 (Angalia pia 5T 711).

c. "Hivi karibuni kitatokea kipindi cha kusisimua sana kwa wote walio hai. Malumbano ya zamani yataanza tena; malumbano mapya yatazuka. Mandhari [picha] ya mambo yale yatakayotendwa kama maigizo katika dunia yetu bado hata hayajapata kuingia katika mawazo yetu. Shetani yuko kazini kupitia kwa mawakala wake wa kibinadamu. Wale wanaofanya juhudi ya kuibadilisha Katiba ya Nchi na kujipatia nafasi ya kutunga sheria inayolazimisha utunzaji wa Jumapili hawatambui hata kidogo matokeo yake yatakavyokuwa. Hatari kubwa imetukabili hivi sasa." 5T 753.

d. "Taifa letu litakapozikataa kabisa kanuni za Serikali yake hata kutunga sheria ya Jumapili, katika kitendo hicho Uprotestanti utakuwa umeshikana mikono na upapa." 5T 712.

e. "Hatari kubwa inawangojea watu wa Mungu. Karibu sana Taifa letu litajaribu kuwalazimisha wote kuitunza siku ya kwanza ya juma kama siku takatifu. Kwa kufanya hivyo, hawatakuwa na haya [aibu] kuwalazimisha wanadamu kinyume cha sauti ya dhamiri zao wenyewe ili kuitunza siku ambayo Taifa linaitangaza kuwa ndiyo Sabato." RH, Extra 12-ll-1888, uk. 4.

e. "Sheria ya Mungu itakapobatilishwa, na uasi kuwa dhambi ya Taifa hili, hapo ndipo Bwana atakapotenda kazi kwa ajili ya watu wake." RH, Extra 12-11-1888, uk.3.

g. "Kwa agizo lile linalolazimisha [utunzaji wa] siku ile iliyowekwa na upapa kwa kukiuka sheria ya Mungu, Taifa letu litajitenga kabisa mbali na haki." 5T 451.


Photo Credit By: Yusuph Mcharia

8. Je, Marekani litaendelea kuwa Taifa lililopata upendeleo wa Mungu baada ya kuchukua hatua ya kisheria na kuiweka kando Sheria ya Mungu?

a. "Watu wa Marekani ni watu waliopata upendeleo; lakini watakapouwekea vizuizi uhuru wa dini, kuachilia mbali Uprotestanti, na kuunga mkono upapa, hapo ndipo kikombe chao cha maovu kitakuwa kimejaa, na 'uasi wa Taifa' hili utaandikwa katika vitabu vile vya mbinguni." RH, 5-2- 1893, uk.274.

b. "...Kwa hiyo, uasi huo na uwe ishara kwetu sisi ya kwamba kikomo cha uvumilivu wa Mungu kimefikiwa, ya kwamba kikombe cha maovu ya Taifa letu kimejaa...." 5T 451.

9. Je, matokeo ya uasi wa Taifa letu hili yatakuwaje?

a. "Wakati unakuja ambapo sheria ya Mungu, kwa maana ya pekee, itabatilishwa katika nchi yetu. Watawala wa Taifa letu, kwa njia ya kutunga sheria Bungeni, wataitia nguvu sheria hiyo ya Jumapili, na kwa njia hiyo watu wa Mungu wataingia katika hatari kubwa sana. Taifa letu, katika vikao vyake vya Bunge, litakapotunga sheria za kuzibana dhamiri za watu kuhusu haki zao za kidini, likilazimisha utunzaji wa Jumapili, na kutumia nguvu ya ukandamizaji dhidi ya wale wanaoitunza Sabato ya Siku ya Saba, hapo ndipo sheria ya Mungu, kwa makusudi na nia kamili, itakuwa imebatilishwa katika nchi yetu; na uasi wa Taifa hili utafuatiwa na maangamizi yaTaifa hili." RH, 12-18-1888, uk. 785; 7BC 977.

b. "Ni katika wakati ule wa uasi wa Taifa hili, wakiwa wanazitekeleza sera za Shetani, watawala wa nchi hii watakapojipanga wenyewe upande wa mtu yule wa dhambi, ----- hapo ndipo, kikombe chao cha maovu kitakuwa kimejaa; uasi wa taifa hili ni ishara ya maangamizi ya Taifa hili." GCB 1891, uk.259.


c. "Matokeo ya uasi huu yatakuwa ni maangamizi ya Taifa hili." RH, 5-2-1893, uk. 274.

d. "Waprotestanti watashughulika sana na watawala wa nchi hii kutunga sheria zitakazourejesha ukuu alioupoteza mtu yule wa dhambi, anayeketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. Kanuni za Ukatoliki wa Roma zitahifadhiwa na kulindwa na Serikali hii. Uasi huo wa Taifa hili utafuatiwa kwa haraka sana na maangamizi ya Taifa hili.... Serikali za Kiprotestanti zitaifikia njia ngeni, nyembamba ipitayo katikati ya milima. Wataongolewa na dunia. Pia, katika kujitenga kwao na Mungu, watafanya kazi kuufanya uongo na uasi wao kwa Mungu viwe ndiyo sheria ya Taifa." RH, 6-15-1897, uk.370.

e. "Makanisa ya Kiprotestanti yatakapoungana na mamlaka za kidunia kuiimarisha dini hiyo ya uongo, ambayo kwa kuipinga mababu zao walistahimili mateso makali sana, hapo ndipo sabato ya papa itakapolazimishwa kwa mamlaka iliyoungana ya kanisa na serikali [dola]. Patakuwa na uasi wa Taifa, ambao utaishia tu katika maangamizi ya Taifa hili. Ev 235 (1899).

f. "Makanisa ya Kiprotestanti yatakapotafuta msaada kutoka kwa mamlaka za kidunia, hivyo kuiga mfano wa kanisa lile asi, ambalo kwa kulipinga babu zao walistahimili mateso makali sana, hapo ndipo patakuwa na uasi wa Taifa ambao utaishia tu katika maangamizi ya Taifa hili." 4SP 410 (1884); ST 7-17-1907, uk. 7.

g. "Makanisa ya Kiprotestanti yatakapoungana na mamlaka za kidunia kuiimarisha dini hiyo ya uongo,... dola hii itakapotumia mamlaka yake kulazimisha amri hizo na kutoa ruzuku kwa taasisi za kanisa ----- hapo ndipo Amerika ya Kiprotestanti itakuwa imeunda sanamu ya upapa, na kutakuwa na uasi wa Taifa ambao utaishia tu katika maangamizi ya Taifa hili." ST, 3-22-1910; 7BC 976.

10. Je, Amerika ya Kiprotestanti itaiundaje sanamu ya mnyama?

a. "Makanisa makuu ya Marekani yatakapoungana katika mafundisho yale wanayoshirikiana pamoja, watakapoishawishi serikali kuyatia nguvu maagizo yao kisheria na kuzipa ruzuku taasisi zao, hapo ndipo Amerika ya Kiprotestanti itakuwa imeunda sanamu ya utawala [wa kidini] wa Roma, na adhabu ya serikali haitaweza kuepukwa kutolewa juu ya wale wasioafiki." GC 445 (Angalia pia 4SP 278).

b. "Katika tendo lile lile la kulazimisha wajibu wa kidini kwa kutumia mamlaka ya kidunia, makanisa yenyewe yangeunda sanamu ya mnyama; kwa hiyo, kulazimisha utunzaji wa Jumapili kule Marekani kungekuwa ndiko kulazimisha ibada ya mnyama na sanamu yake." GC 449.

11. Je, kulazimisha utunzaji wa Jumapili (kuunda sanamu ya mnyama) kule Marekani kutakuja baada au kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema?

a. "Bwana amenionyesha waziwazi ya kwamba sanamu ya mnyama itaundwa kabla ya mlango wa rehema kufungwa; maana hiyo ndiyo itakuwa jaribio kubwa kwa watu wake Mungu.... Hilo ndilo jaribio ambalo watu wa Mungu hawana budi kuwa nalo kabla hawajatiwa muhuri." 7BC 976.

b. "Kwa agizo lile linalolazimisha siku iliyowekwa na upapa, Taifa letu litajitenga kabisa mbali na haki. Uprotestanti utakapounyosha mkono wake ng'ambo ya ghuba kuushika mkono wa Mamlaka ya Roma, utakapounyosha juu ya shimo kubwa lenye kilindi kirefu kushikana mikono na Imani ya Mizimu, nchi yetu, chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu, itakapokuwa imeikataa kila kanuni ya Katiba yake kama Serikali ya Kiprotestanti na ya Jamhuri, na kutunga sheria inayotangaza uongo na madanganyo ya upapa, hapo ndipo tunaweza kujua kwamba wakati umewadia kwa utendaji wa miujiza ya ajabu ya Shetani na ya kwamba mwisho u karibu.

Kama vile kukaribia kwa majeshi yale ya Kirumi kulivyokuwa ishara ya maangamizi ya Yerusalemu yaliyokuwa karibu sana kwa wanafunzi wake wale, hivyo ndivyo uasi huo unavyoweza kuwa ishara kwetu kwamba kikomo cha uvumilivu wa Mungu kimefikiwa, na ya kwamba kikombe cha maovu ya Taifa letu kimejaa, na ya kwamba malaika yule wa rehema karibu ataruka kwenda zake, asirudi tena kamwe." 5T 451.

c. "Njozi za Anna zinaweka kuundwa kwa sanamu ya mnyama baada ya kufungwa kwa mlango wa rehema. Hivyo sivyo mambo yalivyo. Unajidai kuziamini shuhuda; hebu na zikuweke sawa katika suala hili. Bwana amenionyesha mimi waziwazi kwamba sanamu ya mnyama itaundwa kabla ya mlango wa rehema kufungwa; maana hiyo ndiyo itakuwa jaribio kuu kwa watu wa Mungu, ambalo kwalo umilele wao utaamuliwa." 2SM 81.

12. Kwa kuzingatia matarajio ya kutungwa kwa Amri ya Jumapili, Waadventista wanaokaa katika miji mikubwa wanasihiwa kufanya nini upesi iwezekanavyo?

a. "Anataka sisi tuishi mahali palipo na nafasi ya kutosha. Watu wake hawapaswi kusongamana katika miji mikubwa. Anawataka kwenda na familia zao nje ya miji mikubwa, ili wapate kujiandaa vizuri kwa uzima ule wa milele. Kitambo kidogo tu watatakiwa kuiacha miji mikubwa.... Tokeni katika miji mikubwa upesi iwezekanavyo...." 2SM 356.

b. "Hatari kubwa inakuja haraka kuhusiana na utunzaji wa Jumapili.... Kama kwa mpango wa Mungu tunaweza kujipatia mahali palipo mbali kutoka katika miji mikubwa, basi, Bwana atatutaka sisi kufanya hivyo. Kuna nyakati za taabu mbele yetu.... Nauona umuhimu upo wa kuharakisha kuyaweka mambo yote tayari kwa hatari hiyo." 2SM 359.
 
Photo Credit By: Morning Star Radio 105.3 fm

13. Sheria za Jumapili zitatoa onyo gani kwa Waadventista ambao bado wanaendelea kukaa katika miji mikubwa?

"Kama kuzingirwa kwa Yerusalemu na majeshi ya Warumi kulivyokuwa ishara ya kukimbia kwa Wakristo wale wa Yudea, ndivyo kutwaa madaraka kwa upande wa Taifa letu katika kutoa amri iie inayolazimisha sabato ya papa kutakavyokuwa onyo kwetu. Basi huo utakuwa ndio wakati wa kuondoka kwenye miji midogo kwenda kwenye makazi ya upweke mahali pa faragha miongoni mwa milima." 5T 464,465.

14. Je, tutazitumiaje siku za Jumapili baada ya Amri za Jumapili kupitishwa?

a. "Waadventista Wasabato walitakiwa kuonyesha hekima yao kwa kujizuia kufanya kazi zao za kawaida katika siku ile, wakiitumia kwa shughuli za kimishonari. "Kuzipinga Amri za Jumapili kutawaimarisha tu washupavu wa dini wanaojaribu kuzilazimisha kwao ili kuongeza mateso yao. Msiwape nafasi yo yote kuwaita ninyi kuwa wavunjaji wa sheria hizo.... Mtu hapokei alama ya mnyama kwa sababu anaonyesha kwamba anatambua hekima ya kutunza amani kwa kujizuia kufanya kazi inayoleta uvunjaji wa sheria hizo.... "Wakati wo wote inapowezekana, endesheni huduma za kidini katika siku hiyo ya Jumapili.... Waalimu wetu katika shule zetu waitumie Jumapili kwa shughuli za kimishonari." 9T 232,233.

b. "Msifanye maandamano yo yote siku ya Jumapili kupinga sheria hiyo." 9T 235.

c. "Wakati mmoja wale waliokuwa wasimamizi wa shule yetu ya Avondale waliniuliza mimi wakisema: 'Tufanye nini? Mapolisi wanaoilinda sheria hiyo wameagizwa kuwakamata wale wanaofanya kazi siku ya Jumapili.' Mimi niliwajibu hivi: 'Litakuwa ni jambo rahisi sana kuliepuka tatizo hilo. Itoeni siku ya Jumapili kwa Bwana kama siku ya kufanya kazi ya kimishonari. Nendeni nje na wanafunzi wenu kuendesha mikutano mahali mbalimbali, na kufanya kazi ya uganga. Watawakuta watu majumbani mwao, nao watakuwa na wakati mzuri sana wa kuifundisha ile kweli. Njia hii ya kuitumia Jumapili sikuzote inakubaliwa na Bwana." 9T 238.

d. "Tulipokuwa tunaishi mahali paitwapo Cooranbong, ambapo shule yetu ya Avondale imejengwa,... Hoja ya kufanya kazi Jumapili ilikuja kwetu kwa ajili ya kuitafakari. Ilionekana kana kwamba punde kamba zingetufunga sana kila upande hata tusiweze kufanya kazi yo yote siku ya Jumapili. Shule yetu ilikuwa katikati ya misitu, mbali na kijiji cho chote au kituo cha reli.

Hakuna ye yote aliyekuwa anaishi karibu kiasi cha kutosha kutufanya tuingiwe na wasiwasi kwa njia iwayo yote kwa jambo lo lote ambalo tungeweza kulifanya. Hata hivyo, tulikuwa tunachunguzwa. Maofisa wa polisi walishurutishwa kuja kuangalia tulichokuwa tukifanya katika eneo lile la shule; nao walikuja hakika, lakini hawakuweza kuwaona wale waliokuwa wanafanya kazi. Imani yao na heshima yao kwa watu wetu ilikuwa imepatikana kutokana na kazi ile tuliyokuwa tumeifanya kwa wagonjwa katika jumuia ile kiasi kwamba awakutaka kuingilia kati kazi yetu isiyokuwa na madhara yo yote ambayo sisi tuliifanya katika siku ya Jumapili.

"Wakati mwingine ndugu zetu walipotishiwa kuteswa, tena wakawa wanauliza kile ambacho wangeweza kufanya, niliwapa ushauri uo huo niliokuwa nimeutoa kujibu hoja ya kuitumia Jumapili kwa michezo. Niliwaambia, "Itumieni Jumapili kwa kufanya kazi ya kimishonari kwa ajili yake Mungu. Waalimu, nendeni pamoja na wanafunzi wenu.'... "Waalimu katika shule zetu na waitumie Jumapili kwa shughuli za kimishionari." CT 459-551.

15. Je, mtazamo wetu leo uweje? Twawezaje kufanya kazi na kuomba?

a. "Hatufanyi mapenzi ya Mungu tunapokaa kimya tu, bila kufanya kitu cho chote kuuhifadhi uhuru wa dhamiri zetu. Maombi ya bidii, yenye kuleta matokeo yangekuwa yakipanda mbinguni ili janga hilo lipate kuahirishwa mpaka hapo tutakapoweza kuimaliza kazi ambayo imeachwa kwa muda mrefu sana. Hebu na pawe na maombi yanayotolewa kwa bidii sana, kisha na tufanye kazi kulingana na maombi yetu. Yaweza kuonekana kwamba Shetani anashinda na ya kwamba kweli imeshindwa na makosa [mafundisho potofu] na uongo;... Lakini Mungu angetutaka sisi kukumbuka alivyowatendea watu wake wa zamani kuwaokoa kutoka kwa maadui wao. Sikuzote amechagua upeo wa matatizo ili kuonyesha uweza wake, yaani, wakati ule ilipoonekana ya kuwa hakuna uwezekano wo wote wa kuokoka kutoka katika utendaji wa Shetani. Shida ya mwanadamu ni nafasi ya Mungu ya kutenda kazi yake." 5T 714.

b. "Tungejifunza kwa bidii Neno la Mungu, na kuomba kwa imani ili Mungu apate kuzizuia nguvu za giza; maana mpaka sasa ujumbe umekwenda karibu kwa watu wachache mno, na ulimwengu huu unapaswa kuangazwa kwa utukufu wake. Ukweli wa leo ----- amri za Mungu [kumi] na Imani ya Yesu ----- bado haujatangazwa kama unavyopaswa kutangazwa.... Yatupasa kuwa na msimamo thabiti ya kwamba sisi hatutaiheshimu siku ya kwanza ya juma kama sabato...." RH, Extra 12-24-1889, uk.2.

c. "Kwa miaka mingi tumekuwa tukiitazamia Amri ya Jumapili kutungwa katika nchi yetu; na sasa kwa vile tapo hilo liko juu yetu, tunauliza hivi, Watu wetu watafanya nini katika suala hili?...

Tungemtafuta Mungu hasa ili watu wake wapewe neema na nguvu sasa. Mungu wetu yu hai; wala hatuamini kwamba wakati umefika kabisa ambao angeruhusu uhuru wetu uwekewe vizuizi. Nabii aliwaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Malaika mwingine akipanda kutoka maawio ya jua, akawapigia kelele, akisema, 'Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.' Hii inaonyesha kazi tunayopaswa kuifanya sasa, ambayo ni kumlilia Mungu wetu ili malaika wale waendelee kuzizuia pepo zile nne mpaka Wamishonari wapate kutumwa sehemu zote za dunia, na mpaka watakapokuwa wamelitangaza lile onyo juu ya wale wanaoivunja Sheria ya Yehova." RH, Extra 12-11-1888, uk.4,5.

d. "Jukumu zito limekabidhiwa kwa wanaume na wanawake wenye maombi katika nchi nzima, kupeleka dua ili Mungu alifagilie nyuma wingu hili la maovu, na kutupatia miaka michache zaidi ya kufanya kazi kwa ajili ya Bwana." RH, Extra 12-11-1888, uk.4.

e. "Twaona ya kwamba wale ambao sasa wanazishika amri zake Mungu wanahitaji kujishughulisha ili waweze kupata msaada maalum ambao ni Mungu peke yake awezaye kuwapa. Wangefanya kazi kwa bidii zaidi ili kuchelewesha kwa muda mrefu iwezekanavyo janga hilo linalotishia. RH 12-18-1888, uk. 785.

f. "Iwapo hawafanyi lo lote kuielimisha mioyo ya watu, na kwa njia ya ujinga wa kutoijua kweli Mabunge yetu yangeweza kuzikataa kanuni za Uprotestanti, na kuunga mkono na kulitia nguvu kosa la Roma, yaani, sabato ya bandia [Jumapili], basi, Mungu atawashikilia watu wake waliopokea nuru kubwa kuwa wanawajibika kwa utovu wao wa juhudi na uaminifu. Lakini kama suala hili la kutunga sheria ya dini linawekwa mbele ya watu kwa busara na kwa akili, nao wanaona ya kwamba kwa njia hiyo ya kuilazimisha Jumapili uasi wa Roma ulitokea, ya kwamba ulimwengu wa Kikristo ungeweza kuigiza tena kitendo kama hicho, na ya kwamba utawala wa mabavu wa vizazi vile vilivyopita ungerudiwa tena, basi, lo lote lijalo na lije, sisi tutakuwa tumefanya wajibu wetu." RH Extra 12-24-1889, uk.3.

g. "Hebu watu wa Mungu wanaozishika amri zake [kumi] wasinyamaze wakati kama huu, kana kwamba tulikuwa tunaikubali hali hii na kuipenda. Kuna matarajio mbele yetu ya kupigana vita ya kudumu, kwa hasara ya kufungwa, kupoteza mali zetu na hata maisha yenyewe katika kuitetea Sheria ya Mungu [Amri Kumi], ambayo inabatilishwa kwa sheria za wanadamu." RH 1-1-1889, uk.1; 7BC 975.

h. "Ni matumaini yangu kuwa tarumbeta itatoa sauti ya hakika kuhusu tapo [kundi] hili linalotaka kuiweka Amri ya Jumapili. Nadhani kwamba ingekuwa bora sana kama katika magazeti yetu somo la umilele wa Sheria ya Mungu [Amri Kumi] lingetolewa kama somo maalum.... Hivi sasa tungekuwa tunafanya kila tuwezalo kuishinda sheria hiyo ya Jumapili." CW 97,98 (1906).

j. "Wale waliokwisha kuonywa juu ya matukio yaliyo mbele yao hawapaswi kukaa wakiwa wanaingojea kimya kimya dhoruba ile inayokuja, wakijifariji wenyewe kwamba Bwana atawalinda wale walio waaminifu katika siku ile ya taabu. Yatupasa sisi kuwa kama watu wanaomngojea Bwana wao, si kwa kukaa bila kazi, bali kwa kufanya kazi kwa juhudi nyingi, kwa imani isiyotikisika. Huu sasa sio wakati wa kuiacha mioyo yetu kujazwa na mambo yale yasiyo na maana...

Tapo hilo la Jumapili hivi sasa linasonga mbele gizani. Viongozi wake wanaficha hoja halisi, na wengi wanaojiunga na tapo hilo wao wenyewe hawaoni ni wapi mkondo wake wa chini unakokwenda. Itikadi zake ni laini, na mwonekano wake ni wa Kikristo; lakini litakaponena, litaifunua roho ile ya joka. Ni jukumu letu kufanya yote yaliyo katika uwezo wetu kuiepusha hatari hii inayotishia. Tungejitahidi kuzizima hisia za chuki kwa kujiweka wenyewe katika nuru ile inayofaa mbele ya watu. Tungeweka mbele yao hoja halisi ya jambo hilo, hivyo kuingilia kati kwa kupinga kunakofaa dhidi ya hatua za kuuwekea kizuizi uhuru wa dhamiri zetu. Yatupasa kuyachunguza Maandiko, na kuweza kutoa sababu kwa imani yetu." RH Extra 12-11-1888, uk. 4.

k. "Vitabu vya 'Patriarchs and Prophets, Daniel and Revelation, na The Great Controversy' vinahitajika sana sasa kuliko vilivyopata kuhitajika huko nyuma. Vingetawanywa kwa wingi sana kwa sababu kweli zile vinazozisisitizia zitayafungua macho mengi yaliyopofuka.... Wengi miongoni mwa watu wetu wamekuwa vipofu kwa umuhimu wa vitabu vile vile hasa vinavyohitajika sana. Kama busara na ustadi vingekuwa vimeonyeshwa kwa wakati ule katika kuviuza vitabu hivyo, basi, tapo hilo la Sheria ya Jumapili lisingefika hapo lilipo leo." CM 123; RH 12-16-1905.

l. "Hatuwezi kufanya kazi ili kuwafurahisha watu wale watakaoutumia mvuto wao kuukandamiza uhuru wa dini, na kuanzisha hatua za ukandamizaji ili kuwaongoza au kuwalazimisha wanadamu wenzao kuitunza Jumapili kama Sabato. Siku ya kwanza ya juma sio siku ya kuiheshimu. Ni sabato ya bandia, na washiriki wa familia yake Bwana hawawezi kushirikiana na watu hao wanaoitukuza siku hiyo, na kuivunja Sheria ya Mungu [Amri Kumi] kwa kuikanyaga chini ya miguu yao Sabato yake. Watu wa Mungu hawapaswi kupiga kura ili kuwaweka watu kama hao katika ofisi; maana wanapofanya hivyo, wanashiriki pamoja nao dhambi zile watakazozitenda wakiwa ofisini." FE 475; GW 39l,392.

********************

UNA MAONI AU USHAURI WOWOTE?

USISITE KUACHA KTK KIBOSKI CHA MAONI MTAA FLANI HAPO CHINI.

********************