Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Februari 19, 2012

Je, Roma Itatawala Ulimwengu Tena?


 KANISA LA MTAKATIFU PETRO, ROMA


Photo Credit by: www.minutetravelguide.com

Maridhiano ya Kufisha

Mtume Paulo, katika Waraka wake wa Pili kwa Wathesalonike, alitabiri juu ya uasi mkuu ambao ungeleta
matokeo ya kuianzisha mamlaka ile ya upapa. Alitangaza kwamba siku ile ya kuja Kristo isingeweza kuja, “usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa mtu yule wa dhambi (kuasi), mwana wa uharibifu; yule  Mpingamizi [Mpinga Kristo], ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu [kanisa] la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” Tena, zaidi ya hayo, Mtume huyo anawaonya ndugu zake kwamba “ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 Wakorintho 2:3,4,7. 

Hata katika kipindi kile cha mwanzo kabisa aliona yakiingia ndani ya kanisa mafundisho potofu
ambayo yangetayarisha njia ya kujitokeza kwa upapa. Kidogo kidogo, mwanzoni kwa siri na kimya kimya, na baadaye kwa wazi zaidi, ikaongezeka nguvu yake na kuitawala mioyo ya wanadamu, ile “siri ya kuasi” ikaiendeleza mbele kazi yake kwa kutumia madanganyo na makufuru. Karibu bila kutambulikana kabisa desturi zile za kikafiri zikaingia ndani ya kanisa la Kikristo. Roho ile ya maridhiano na kufanana-fanana
[na dunia] ilizuiwa kwa wakati fulani kutokana na mateso makali ambayo kanisa lilistahimili chini ya wapagani. Lakini mateso yale yalipokoma, na Ukristo ulipoingia katika mabaraza na majumba ya kifalme, ndipo kanisa lile lilipouweka kando unyenyekevu ule wa Kristo na Mitume wake na kujitwalia
ufahari na kiburi cha makuhani na watawala wale wa kipagani; na mahali pa matakwa ya Mungu likaweka nadharia zawanadamu pamoja na desturi zao. 

Kuongoka kwa jina tu kwa Konstantino, mapema katika karne ile ya nne, kulileta shangwe kubwa; na  ulimwengu [upagani], ukiwa umevikwa joho la mfano wa haki, ukatembea na kuingia ndani ya kanisa. Basi,
kazi ile ya uharibifu ikasonga mbele kwa haraka sana. Upagani, wakati ukionekana kana kwamba umeshindwa kabisa, ukawa ndio mshindi. Roho yake ikalitawala kanisa lile. Mafundisho yake ya dini, sherehe zake, na ushirikina wake vikaingizwa katika imani na ibada ya wale waliojidai kuwa ni wafuasi wake Kristo.

CHANZO CLICK HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni