Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Februari 23, 2012

Unamkumbuka Mwalimu wa Kike Aliyebaka Wanafunzi 11?

  


Mwaka jana mwalimu Cindy Clifton mwenye umri wa miaka 41 alikabiliwa na kifungo cha muda mrefu jela kwa kosa la kuwanywesha pombe wanafunzi wake wa 11 wa kiume wenye umri kati ya miaka 14 na 17 na kisha kufanya nao mapenzi.

Taarifa ya televisheni ya ABC ilisema kuwa mwalimu huyo wa shule ya msingi ya Crestview Middle School aliwalewesha wanafunzi wake wakati wa sherehe alizoziandaa kwenye nyumba yake na kufanya nao mapenzi katika kipindi cha kuanzia aprili 11 hadi julai 15.

Mwalimu huyo aliyejizolea umaarufu katika shule hiyo kutokana na ufundishaji wake alikabiliwa na mashtaka ya kufanya mapenzi na watoto wenye umri mdogo usiofika miaka 18.

Miongoni mwa wanafunzi waliofanya mapenzi na mwalimu huyo, walikuwa ni marafiki wa binti wa mwalimu huyo.

Mwalimu huyo alifunguliwa mashtaka miezi mitatu baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa polisi ulioanzishwa baada ya malalamiko mengi toka kwa wazazi.

"Uchunguzi wa polisi ulianza baada ya malalamiko ya wazazi ambao walilalamika watoto wao walinyeshwa pombe kwenye sherehe zilizoandaliwa na mwalimu Clifton", ilisema taarifa ya polisi.

JE UNAFAHAMU HABARI YOYOTE YA SASA KUHUSU HUYU MWALIMU?
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni