DO NOT GIVE UP. THE BIGINNING IS ALWAYS THE H a r D e s t. "NI HERI KUFA KATIKA FIKRA ZINAZOISHI KULIKO KUISHI KATIKA FIKRA ZILIZOKUFA."
Mtayarishaji
Morning Star Radio
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Unabii. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Unabii. Onyesha machapisho yote
Jumanne, Septemba 04, 2012
ONYO LA KUTISHA..!!
Onyo la kutisha mno la adhabu linaloweza kupatikana mahali po pote katika Biblia limo katika Ufunuo 14:9,10: "Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa [alama] katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye ATAKUNYWA katika mvinyo ya GHADHABU YA MUNGU iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo."
Maelezo haya yanaogofya mno na hayafanani kabisa na mafungu mengine yanayoielezea tabia ya Mungu ilivyo, hata tunajikunja kwa hofu. Lakini yanaonyesha wazi kipindi kile ambacho rehema ya Mungu itakapoondolewa kwa wale ambao wanaendelea daima kuikataa mamlaka ya mbinguni. Litakuwa ni tendo lisilo na kifani kwa upande wa Mungu katika uhusiano wake na jamii ya kibinadamu. Kwa karibu
miaka 6000 hukumu zake za adhabu juu ya watu walio waovu sana zimechanganywa na rehema Yake. Lakini sasa uovu unafikia kiwango ambacho kinafanya iwe lazima kwa Mungu kuingilia kati, na kukidhihirisha kiwango cha usaliti wa mwanadamu dhidi ya Serikali ya Mungu.
Hapa ndipo tunataka kujua habari zaidi juu ya dhambi ile inayomfanya Mungu kutenda tendo hilo la ajabu [geni] la kuwaadhibu [waovu] kwa moto. Angalia kwamba jambo hili la mwisho linahusu utii wa uongo kwa mamlaka ile ya Mnyama, ambayo mara nyingi inatajwa katika unabii wa Biblia. Hatimaye dunia hii itasimama
ikiwa imegawanyika katika makambi mawili:
01. Wale wanaomsujudu Mungu wa kweli na
02. Wale wanaomsujudu Mnyama yule wa Ufunuo 13.
Lakini ni jambo gani linaloleta mgawanyo huo mkubwa wa watu wa dunia hii? Baada ya kueleza ajali itakayowapata waabudu hao wa uongo katika Ufunuo 14:9-11, Yohana analo hili la kusema katika fungu lile linalofuata: "HAPA NDIPO PENYE SUBIRA YA WATAKATIFU, HAO WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU, NA IMANI YA YESU." Hapa tunaona tofauti ya kushangaza kati ya wale wanaomfuata yule Mnyama na wale wanaomfuata Mwana-Kondoo.
Angalia, tafadhali, ya kwamba suala linalohusika linazunguka juu ya kuzishika amri za Mungu. Wale ambao hawana alama ya Mnyama wanasemwa ya kuwa wanazitii amri hizo [za Mungu], na wale waliobaki wanateseka kwa ghadhabu ya Mungu. Jambo hili linakubaliana kabisa na usemi wa Paulo katika Warumi 16:16, "Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii,
mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki."
Wajibu wa hali ya juu unahesabika kwa tendo hili la UTII. Mwishowe, sehemu kubwa ya wakazi wa dunia hii wataikubali mamlaka hii ya bandia ya serikali ya Mpinga Kristo, kwa KUZIASI AMRI ZILE KUU KUMI za Mungu. Rafiki zangu, kila mtu mmoja mmoja atakuwa upande mmoja au mwingine. Biblia inaeleza kwa wazi sana ya kwamba UZIMA au MAUTI utategemea UAMUZI WA MWISHO kuhusu Mnyama huyu wa Ufunuo 13.
Ni ajabu kwamba wanathiolojia wa siku hizi wamepuuzia kabisa UJUMBE HUU WA ONYO wa Ufunuo 14, unaohusu ile Alama ya Mnyama. Shauku ya watu wengi imeharibiwa na mvuto wa WACHUNGAJI ambao hawakutaka kuyachukulia maneno haya ya unabii wa Yohana kwa uzito wake. Mara nyingi wanautupilia mbali [unabii huu] kana kwamba ni waraka wenye utata, usiokuwa na maana, ambao ulilihusu
tatizo la mahali pale katika kanisa lile la mwanzo.
Kwa sababu fulani kitabu hiki kinachoitwa Ufunuo kinahesabika kama vile ni kitabu kilichofungwa [kisichoweza kueleweka], badala ya ukweli wake wa wazi uliofunuliwa [unaoeleweka] kama jina lake linavyomaanisha. Lakini tafadhali zingatia ya kwamba ahadi imetolewa kwa wale wanaoitafuta kweli iliyomo ndani ya kitabu hiki cha ajabu: "Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu." Ufunuo 1:3.
Kabla ya kukichunguza sana kisa hiki kilicho wazi cha Yohana kuhusu pambano lile la mwisho kati ya Kristo na Shetani, hebu na tutumie muda fulani kuwachambua hao wanaopambana katika vita hii. Ni lini na kwa jinsi gani [pambano hili] lilianza, na kwa jinsi gani litafikia mwisho wake?
Jumanne, Februari 28, 2012
VITA VYA HAR-MAGEDONI
Jina “HAR-MAGEDONI”
hushtua kwa hofu na kuashiria hatari katika mawazo ya wengi. Wengine
wanadhani ni vita kuu ya
ulimwengu kuzunguka Mashariki ya Kati. Wengine hutazamia Mpinga Kristo
akipigana ili kupata ukuu wa ulimwengu wote. Na bado
wengine hawajui nini cha kuamini au kutegemea. Neno “Har-Magedoni” lenyewe utafsiriwa “jina la alama” (angalia Strong's
Exhaustive Concordance, #717). Na bado Maandiko hayafundishi kwamba kutakuwepo
vita halisi vinatakavyohusisha ulimwengu wote! Vita hii na mapambano
havitapiganwa kwa kutumia silaha halisi, kama bunduki, mizinga, ndege za vita,
au majeshi yenye silaha.
Lakini vitapiganwa,
tayari vimeanza kupiganwa, na vitaendelea kupanuka kwa nguvu zaidi mpaka kila
mtu katika ulimwengu anahusishwa. “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na
vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama,
na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani,
zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote; kuwakusanya
kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. Tazama, naja kama mwivi. Heri
akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake. Wakawakusanya
hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.” Ufunuo16:13-16.
Kama inavyoweza
kuonekana, Maandiko hufundisha kwamba vita hivi vinapiganwa kati ya majeshi
makuu mawili: Mungu, Kristo na wafuasi
wake wasafi au wenye haki, dhidi ya Ibilisi, roho za uovu, na wafuasi wake
wachafu au waovu. Kwa hiyo vita vya Har-Magedoni ni alama inayoeleza pambano
kuu na mgongano unaondelea kwa nguvu kati ya Mungu na Shetani--kati ya ukweli
na ufisadi. Na vita hivi vya kiroho hatimaye vitahusisha kila mtu katika dunia
kwani kila mmoja lazima aamue nani wa kufuata--Kristo na ukweli, au Ibilisi na
ufisadi: uzima wa milele pamoja na Kristo, au maangamivu milele pamoja na
Shetani. Vita hivi na mapambano kati ya Kristo na Shetani vilianza mbinguni.
“Kulikuwa na vita
mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye
akapigana nao pamoja na malaika zake;
nao hawakushinda, wala mahalipao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka
akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa
zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata
nchi, na
malaika zake wakatupwa
pamoja naye.” Ufunuo 12:7-9. Hata kama Ibilisi alitupwa kutoka mbinguni,
aliendelea na mapambano yake dhidi ya
Kristo na Mungu katika dunia hii. Kwa karibu miaka elfu sita mgongano huu
umeendela na kuzidi kupanuka. Lakini
vita vya mwisho vya kupiganwa katika pambano hili kuu, kilele ambacho matukio
yote yamekuwa yanaelekeza, ni
kile ambacho Biblia hufafanua kama siku kuu ya Mungu Mwenyezi--vita vya
Har-Magedoni.
Vita hivi vya mwisho kati
ya ukweli na ufisadi vinaonyeshwa wazi katika Ufunuo sura zifuatazo 12, 13, 14,
& 18. Na wanadamu wote wameingia katika vita hii leo. Kutokana na kwamba
Har-Magedoni ni alama inayoeleza vita vya kiroho kati ya
ukweli na ufisadi, ni silaha gani ambazo Ibilisi anatumia katika pambano hili
kuu? Vitu vinavyofananishwa na
vyura vilitoka katika kinywa cha Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo. Sasa vyura
hukamata mawindo yao kwa kutumia
ndimi zao, na kinachotoka katika vinywa vyao ni maneno yanayopangiliwa pamoja
katika misingi ya imani. Kwa
hiyo hawa viumbe watatu hukamata mawindo yao kwa kusema au kufundisha
mafundisho mbalimbali ya ufisadi.
Kwa wale wanaotamani
kumfuata Kristo na ukweli, ni kitu cha maana sana kwamba tuweze kupambanua wazi
nani ni Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo kusudi tuweze kuepuka kudanganywa kwa
mafundisho mbalimbali ya uongo na hivyo kupotea. Kama ilivyodhihirishwa katika
Ufunuo 12, Joka kimsingi ni Shetani. Na kauli gani za misingi ya makosa na
mafundisho ya uongo zimetoka katika kinywa cha Shetani? Mafundisho mbalimbali
ya umizimu, upagani, na uchawi ambayo falme za ulimwengu zimejengwa juu
yake--ikiwa ni pamoja na Himaya ya Kirumi ya kipagani ya zamani. Wakati wengi wanaamini
upagani kuwa kitu cha zamani, bado kuna mamilioni leo wanaojihusisha na imani
zake za kikafiri na ibada ya Ibilisi.
Ishara za awali za dini
ya kipagani ni kuabudu vitu vya asili. Kutokana na kwamba umbo lililo juu zaidi
katika asili ni mwili wa binadamu, na
hasa mawazo, mwanadamu anaongozwa kuabudu nguvu za mawazo na hivyo kuinua maoni ya mwanadamu juu ya
ufunuo wa Mungu. Mamlaka zote kuu zilizotawala dunia zilidhihirisha ukweli kwamba katika upagani,
Kanisa na serikali havikutengana--lakini vilikuwa vimeungana pamoja. Katika
Babeli, Umedi-
Uajemi, Uyunani, na Rumi,
serikali mara zote ilitumiwa kuunga mkono na kutoa nguvu kwa dini ya kipagani
ya wakati huo. Majira na
tena sheria zilipitishwa na mamlaka ya serikali ili kutumika kulazimisha
kuabudu miungu ya kipagani na mafundisho ya uongo.
Leo, kama ilivyokuwa
katika nyakati za zamani, roho ya kuinua na kuabudu maoni ya mwanadamu,
taasisi, na Kanisa na serikali ili
kusudi Kanisa liweze kupatiwa nguvu kupitisha maamuzi na mafundisho yake makuu,
ni roho ya Joka. Na roho hii
itaongezeka zaidi na zaidi kwa kujulikana mpaka itakapoishia katika kipindi
kikuu cha taabu kwa watu wa Mungu. Siyo roho hii tu ya uchafu ambayo inafanya
kazi leo kupitia nadharia ya kibinadamu na falsafa zingine za ubatili-- kumwinua
mwanadamu juu ya Mungu, kuinua ufisadi juu ya ukweli--lakini kuna roho nyingine
ya pili ambayo inatoka kwenye kinywa cha Mnyama.
Katika Ufunuo 13, Mnyama
ambaye aliinuka kutoka kwenye mabaki ya Roma ya kipagani; Mnyama ambaye alijiunganisha mwenyewe
na upagani ili kuongeza idadi yake; Mnyama ambaye alitawala kwa siku za kinabii
1260 (Ufunuo 12:6), au miaka
ya unabii 3 1/2 (Ufunuo 12:14), au miezi ya unabii 42 (Ufunuo 13:3)--kila moja
ikileta jumla ya miaka halisi 1260 (angalia Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6), si mwingine
bali Kanisa Katoliki la Kirumi Mfumo huu mkuu wa kidini wa Ukatoliki huliinua
Kanisa lililopangiliwa juu ya dhamiri ya mtu, na wakati kuna mgongano kati ya
Biblia na Kanuni za Kanisa, kanuni daima huwekwa juu zaidi ya ukweli wa Biblia.
Kama kuna kutokubaliana kati ya dhamiri ya mtu na fundisho kuu la Kanisa,
Kanisa kwa njia ya mapokeo yake na maoni mara zote huchukua sehemu ya kwanza.
Kwa kutofautisha na
utawala huu na utawala wa Kanisa, Paulo anawasifia Waberoya waungwana kwa
sababu “walilipokea lile neno
kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo
hayo ndivyo yalivyo” Matendo 17:11. Hakuna mahali popote tunapomkuta Paulo
akiwataka waumini kukubali mafundisho kwa msingi wa mamlaka ya Mitume, lakini badala
yake aliwahamasisha kuyachunguza Maandiko wao wenyewe ili kuthibitisha ukweli
wa mambo waliyokuwa wamefundishwa. Wazo la neno la Mungu kama mamlaka ya juu na
mwongozo wa maisha ni dini na ukweli wa Biblia (angalia Yohana 5:39; 2 Timotheo
3:16-17; Isaiya 8:20), na maarifa haya yanatuweka
huru (angalia Yohana 8:32).
Roho ya tatu ya uchafu ni
roho ya Nabii wa Uongo. Nabii ni mmoja wa wanaodai kuwa wamepokea ujumbe kutoka kwa Mungu, na kisha hudai
kuwa mnenaji wa Mungu katika kueneza kwa haraka ujumbe huu kwa watu (angalia
Hesabu 12:6; Kumbukumbu la Torati 18:22). Nabii wa uongo hatimaye angekuwa mtu
yeyote anayedai kuwa ananena kwa ajili ya Mungu, wakati katika hali halisi hafanyi
hivyo (angalia Yeremia 14:14). Nabii wa Uongo haiwezekani kurejewa kama upapa,
kwa sababu umedai siku zote kupokea utamaduni juu ya ufunuo wa Biblia na haki ya
kubadilisha amri za Mungu kadiri wapendavyo. Lakini Makanisa mbalimbali ya
Kiprotestanti yamedai kufuata Biblia tu
kama msingi wa imani yao na mafundisho. Na bado, tunayaona yakifuata katika
nyayo za Roma kwa kuinua utamaduni
[mapokeo] juu ya ukweli wa neno la Mungu! Kwa hiyo Makanisa hayo ni nabii wa
uongo
yaking’ang’ania, kuongea
yakiunga mkono, makosa na huku bado yanadai ni ukweli wa Mungu!
Wakati yakitofautiana
katika baadhi ya mambo fulani, Makanisa ya Kiprotestanti yote yanaungana pamoja
katika mafundisho yasiyoleta
hitilafu, na zaidi na zaidi yanafanana na Ukatoliki wa Kirumi. Wakati, katika
harakati za kufikia malengo yake, huyu Nabii
wa Uongo wa Uprotestanti anapofuata katika nyayo zile zile za Rumi, kwa
kuungana na kutegemea nguvu za
kiserikali kumwunga mkono katika mafundisho yake na kukanyaga haki ya uhuru wa
kuabudu ili kulazimisha mafundisho
yake makuu, atakuwa pia Sanamu ya Mnyama (angalia Ufunuo 13). Kwa kukataa
ukweli, watu wanakataa Mwanzilishi wa ukweli na kujiandaa wenyewe kuwa upande
wa Ibilisi katika vita hii kuu ya mwisho. Kwa kuendelea kukaidi kukubali mamlaka
ya Mungu--Mtoa sheria, na kutii sheria zake, wanaume, wanawake, na watoto
wanajifunga wenyewe kwa mwasi mkuu katika ufisadi.
Hakuna kosa linalojeruhi
sana moja kwa moja dhidi ya mamlaka na serikali ya Mbinguni na linapingwa zaidi
katika maamuzi ya hiari kuliko
wazo kwamba sheria ya Mungu si ya lazima tena. Sheria ndiyo msingi wa serikali
yote, na ni kukosa hekima kikamilifu
au kuungwa mkono kuamini kwamba Mtawala wa ulimwengu amestaafu katika wajibu wake na kutuacha bila
sheria yake! Iwe Ibilisi amekudaka wewe kwa kuweka mbali sheria ya Mungu yote,
au kukataa moja ya mausia yake,
matokeo yake ni yale yale. Yeyote anayejikwaa “katika neno moja” hudhihirisha
dharau kwa sheria yote; mvuto wake
na mfano viko upande wa uasi; anakuwa “amekosa juu ya yote” (angalia Yakobo 2:10). Popote pale mausia ya
Mungu yanapotupiliwa mbali, dhambi hukoma kuwa ya kuchukiza au haki kuwa kitu
cha kutamaniwa.
Maandiko yanatangaza
kwamba roho za mashetani zitafanya kazi kwa nguvu miujiza ambayo itawadanganya karibu ulimwengu wote, na
kisha kuwakusanya watu wote pamoja kwa ajili ya vita kuu ya mwisho. Kigezo
kikuu cha mgongano kitakuwa ni
sheria ya Mungu, na hasa Sabato, ambayo inamwonyesha Mtoa sheria kama Muumbaji
pekee na hivyo tunayepaswa kutoa utii kwake kama sehemu ya lazima ya urithi. Ni
kazi ya ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12 & 18:1-5 kubatilisha
mashambulizi haya dhidi ya sheria ya Mungu kwa kuleta kwa ulimwengu ibada inayostahili
kwa Mungu kama Muumbaji wetu. Kwa muungano wa nguvu hizi tatu za Joka, Mnyama,
na Nabii wa Uongo, watu wote walioko duniani watalazimika kuungana katika
jukwaa la uovu dhidi ya
Mungu na ukweli wa
Biblia. Na wale ambao hawafuati maamuzi yao [nguvu hizi tatu] watauawa. Hivyo,
kupitia mafundisho ya udanganyifu na mafundisho ya muungano huu wa nguvu tatu za
umizimu, Ukatoliki, na Uprotestanti, wakazi wote wa dunia watatakiwa kukata
shauri kuwa upande wa, au kinyume cha, Mungu na ukweli wake (angalia
Ufunuo13:15- 17). Mungu halazimishi utashi wa dhamiri, lakini Shetani mara kwa
mara hujaribu kutumia njia mbalimbali za nguvu na ukatili ili apate utawala
juu ya wale ambao hawezi, kwa njia yoyote, kuwadanganya. Kwa njia ya woga, au
kwa nguvu halisi, Shetani hupanga
kutawala dhamiri na kujipatia utukufu mwenyewe. Kutimiza hili, hufanya kazi
kupitia mamlaka ya kidini na pia
ile ya serikali za dunia, akiwasukuma kupitisha sheria za wanadamu ambazo humpinga
kabisa Mungu na sheria yake.
Jumapili, Februari 19, 2012
Je, Roma Itatawala Ulimwengu Tena?
KANISA LA MTAKATIFU PETRO, ROMA
![]() |
Photo Credit by: www.minutetravelguide.com
|
Maridhiano ya Kufisha
Mtume Paulo, katika Waraka wake wa Pili kwa Wathesalonike, alitabiri juu ya uasi mkuu ambao ungeleta
matokeo ya kuianzisha mamlaka ile ya upapa. Alitangaza kwamba siku ile ya kuja Kristo isingeweza kuja, “usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa mtu yule wa dhambi (kuasi), mwana wa uharibifu; yule Mpingamizi [Mpinga Kristo], ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu [kanisa] la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” Tena, zaidi ya hayo, Mtume huyo anawaonya ndugu zake kwamba “ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 Wakorintho 2:3,4,7.
Hata katika kipindi kile cha mwanzo kabisa aliona yakiingia ndani ya kanisa mafundisho potofu
ambayo yangetayarisha njia ya kujitokeza kwa upapa. Kidogo kidogo, mwanzoni kwa siri na kimya kimya, na baadaye kwa wazi zaidi, ikaongezeka nguvu yake na kuitawala mioyo ya wanadamu, ile “siri ya kuasi” ikaiendeleza mbele kazi yake kwa kutumia madanganyo na makufuru. Karibu bila kutambulikana kabisa desturi zile za kikafiri zikaingia ndani ya kanisa la Kikristo. Roho ile ya maridhiano na kufanana-fanana
[na dunia] ilizuiwa kwa wakati fulani kutokana na mateso makali ambayo kanisa lilistahimili chini ya wapagani. Lakini mateso yale yalipokoma, na Ukristo ulipoingia katika mabaraza na majumba ya kifalme, ndipo kanisa lile lilipouweka kando unyenyekevu ule wa Kristo na Mitume wake na kujitwalia
ufahari na kiburi cha makuhani na watawala wale wa kipagani; na mahali pa matakwa ya Mungu likaweka nadharia zawanadamu pamoja na desturi zao.
ambayo yangetayarisha njia ya kujitokeza kwa upapa. Kidogo kidogo, mwanzoni kwa siri na kimya kimya, na baadaye kwa wazi zaidi, ikaongezeka nguvu yake na kuitawala mioyo ya wanadamu, ile “siri ya kuasi” ikaiendeleza mbele kazi yake kwa kutumia madanganyo na makufuru. Karibu bila kutambulikana kabisa desturi zile za kikafiri zikaingia ndani ya kanisa la Kikristo. Roho ile ya maridhiano na kufanana-fanana
[na dunia] ilizuiwa kwa wakati fulani kutokana na mateso makali ambayo kanisa lilistahimili chini ya wapagani. Lakini mateso yale yalipokoma, na Ukristo ulipoingia katika mabaraza na majumba ya kifalme, ndipo kanisa lile lilipouweka kando unyenyekevu ule wa Kristo na Mitume wake na kujitwalia
ufahari na kiburi cha makuhani na watawala wale wa kipagani; na mahali pa matakwa ya Mungu likaweka nadharia zawanadamu pamoja na desturi zao.
Kuongoka kwa jina tu kwa Konstantino, mapema katika karne ile ya nne, kulileta shangwe kubwa; na ulimwengu [upagani], ukiwa umevikwa joho la mfano wa haki, ukatembea na kuingia ndani ya kanisa. Basi,
kazi ile ya uharibifu ikasonga mbele kwa haraka sana. Upagani, wakati ukionekana kana kwamba umeshindwa kabisa, ukawa ndio mshindi. Roho yake ikalitawala kanisa lile. Mafundisho yake ya dini, sherehe zake, na ushirikina wake vikaingizwa katika imani na ibada ya wale waliojidai kuwa ni wafuasi wake Kristo.
kazi ile ya uharibifu ikasonga mbele kwa haraka sana. Upagani, wakati ukionekana kana kwamba umeshindwa kabisa, ukawa ndio mshindi. Roho yake ikalitawala kanisa lile. Mafundisho yake ya dini, sherehe zake, na ushirikina wake vikaingizwa katika imani na ibada ya wale waliojidai kuwa ni wafuasi wake Kristo.
CHANZO CLICK HAPA
Alhamisi, Februari 16, 2012
AMRI YA JUMAPILI KWA ULIMWENGU MZIMA
1. Biblia inasemaje juu ya kuinuka tena ulimwenguni kote kwa uongozi ule wa Roma ya Kikatoliki kabla ya mwisho wa wakati? Ufunuo 13:3,8.
![]() |
| Photo by: www.veteransnewsnow.com |
1. Ni Taifa gani lililopata upendeleo litakaloongoza katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili?
a. "Kundi lilo hilo lilitoa madai yake ya kwamba kuenea haraka kwa ufisadi kwa sehemu kubwa kulichangiwa na kuinajisi ile wanayoiita 'Sabato ya Kikristo,' na ya kwamba kule kulazimisha utunzaji wa Jumapili kungeyaboresha sana maadili ya jamii. Madai hayo yanasisitizwa hasa katika Amerika, ambako fundisho la Sabato ya Kweli limehubiriwa karibu kwa mapana yake yote." GC 587.
b. "Mataifa ya kigeni yatafuata mfano wa Marekani. Japokuwa Taifa hili linaongoza, hata hivyo hatari iyo hiyo itawajia watu wetu katika sehemu zote za ulimwengu." 6T 395.
2. Ni mataifa mangapi yatakayofuata mfano huo wa Marekani?
a. "Amerika, nchi yenye uhuru wa dini, itakapoungana na upapa katika kuzitenda jeuri dhamiri za watu na kuwalazimisha watu kuiheshimu sabato hiyo ya uongo [Jumapili], hapo ndipo watu wa kila nchi ulimwenguni watakapoongozwa kufuata mfano wake." 6T 18 (Angalia GCB 1-28- 1893).
b. " '[A]liwanywesha Mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake [mafundisho yake potofu]' Ufunuo 14:6-8. Hii inakuwaje? Kwa kuwalazimisha watu kuikubali sabato bandia [Jumapili]." 8T 94.
c. "Suala hili la Sabato ndilo litakuwa hoja kuu katika Pambano Kuu la mwisho ambalo kwalo ulimwengu wote utakuwa na sehemu yake ya kufanya." 6T 352.
4. Ni dini gani hasa ya ulimwengu mzima inayohusika na kulazimisha utunzaji huu wa Jumapili?
a. "Kwa vile Sabato imekuwa jambo la pekee la mabishano katika Mataifa ya jamii za Kikristo, na wenye mamlaka ya dini [ya Muungano] na serikali wameungana katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili, basi, wale walio wachache sana watakaoendelea kukataa kukubaliana na madai hayo yanayopendwa na wengi watakuwa watu wa kuchukiwa mno ulimwenguni kote." GC 615.
b. "Jamii yote ya Kikristo itagawanyika katika makundi makuu mawili, wale wanaozishika amri [kumi] za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomsujudu mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa yake." GC 450; 9T 16; 2SM 55.
5. Ni jambo gani litakalowapata Waadventista Wasabato ambao hawawezi kukubaliana na Amri hiyo ya Jumapili?
a. "Amri ile itakayoitia nguvu ibada ya siku hii [ya Jumapili] itatangazwa ulimwenguni kote.... Maonjo na mateso yatawajia wale wote ambao, kwa kulitii Neno la Mungu, watakataa kuisujudu sabato hiyo ya uongo [Jumapili]." 7BC 976.
b. "Ulimwengu wote utachochewa kuwa na uadui dhidi ya Waadventista Wasabato, kwa sababu hawatakubali kumsujudu papa kwa njia ya kuiheshimu Jumapili, siku iliyowekwa na mamlaka hiyo ya Mpinga Kristo. Ni kusudi lake Shetani kusababisha wafutiliwe mbali duniani, ili ukuu wake humu duniani usipate kupingwa." TM 37; RH 8-22-1893.
c. "Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo." GC 604.
6. Ni athari gani zitakazoletwa na uamsho huo wa bandia juu ya karibu wote wanaojiita Wakristo kwa jina tu?
"Wakatangaza ya kwamba wao walikuwa na ile kweli; ya kwamba miujiza ilitendeka kati yao; ya kwamba uwezo mkuu na ishara na maajabu yalitendeka miongoni mwao; na ya kwamba hiyo ilikuwa ndiyo ile Milenia [miaka elfu moja] waliyokuwa wanaingojea kwa muda mrefu sana. Ulimwengu wote uliongolewa na kuafikiana na Amri ile ya Jumapili." Letter 6, 1884. 7.
Ni alama gani mbili zinazopingana zitapokewa na makundi hayo mawili ya watu katika ulimwengu huu hapo Jumapili itakapotiwa nguvu kwa kuitungia sheria?
a. "Wakati utunzaji wa sabato hiyo ya uongo [Jumapili] kwa kuitii amri ya serikali, kinyume na amri ile ya nne, utakuwa ni kiapo cha utii kwa mamlaka ile inayopingana na Mungu, utunzaji wa Sabato ya Kweli, kwa kuitii Sheria ya Mungu [Amri Kumi], ni ushahidi wa utii kwa Muumbaji. Wakati kundi moja, kwa uikubali alama ya utii kwa mamlaka za duniani, linapokea Alama (chapa) ya Mnyama, lile jingine, kwa kuichagua ishara ya utii kwa Mamlaka ile ya Mbinguni, litapokea Muhuri wa Mungu." GC 605.
c. "Matokeo ni ya kuogofya ambayo kwayo ulimwengu huu utakabiliwa nayo. Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo.
Kwa upande mwingine, Sheria ya Mungu [Amri Kumi] inayoamuru Siku ya Mapumziko iliyowekwa na Muumbaji inataka watu wote waitii na kutishia ghadhabu dhidi ya wote wanaozivunja amri zake [kumi]. "Jambo hilo likiwa limewekwa wazi hivyo mbele yake [kila mtu], hapo ndipo ye yote atakayeikanyaga sheria ya Mungu chini ya miguu yake ili kuitii amri ile iliyotungwa na binadamu atapokea Alama ya Mnyama...." GC 604.
![]() |
| Photo by: www.lahore.olx.com.pk |
8. Je, Amri hiyo ya Jumapili kwa ulimwengu mzima ina uhusiano gani na kufungwa kwa mlango wa rehema?
a. "Mungu anayapa Mataifa muda fulani wa majaribio." 4BC 1143.
b. "Kwa usahihi usioweza kukosewa Yule wa Milele angali bado anatunza akaunti ya Mataifa yote. Ingawa rehema zake hutolewa, zikiwa na mwito wa kuwataka wanadamu kutubu, akaunti hiyo itaendelea kubaki wazi; lakini hesabu hizo zitakapofikia kiwango fulani ambacho Mungu amekiweka, utekelezaji wa ghadhabu yake utaanza. Akaunti hiyo itafungwa. Uvumilivu wa
Mungu utakoma. Hakuna tena maombezi ya rehema kwa ajili yao." 5T208.
c. "Mungu anatunza kumbukumbu ya Mataifa: hesabu zinajaa dhidi yao katika vitabu vile vya mbinguni; na wakati ule itakapokuwa imepitishwa sheria kwamba uvunjaji wa siku ya kwanza ya juma utakabiliwa na adhabu, hapo ndipo kikombe chao kitakuwa kimejaa." 7BC 910.
d. "Hesabu zinazozidi kuongezeka katika vitabu vile vya kumbukumbu vya mbinguni zitakapoonyesha kiwango cha jumla ya maovu kuwa kimetimia, ndipo ghadhabu itakapokuja, pasipo kuchanganywa na maji, na hapo ndipo itakapojulikana ya kuwa ni jambo kubwa mno jinsi gani kuuchosha uvumilivu wa Mungu. Hatari hiyo kubwa itafikiwa wakati ule mataifa yote yatakapokuwa yameungana kuibatilisha Sheria ya Mungu." 5T 524.e. "Dunia hii karibu sana imefikia mahali ambapo Mungu atamruhusu yule mharabu [mwangamizaji] kufanya mapenzi yake juu yake. Kule kuziweka sheria za wanadamu mahali pa Sheria ya Mungu, kule kuitukuza Jumapili kwa amri za kibinadamu tu, badala ya Sabato ile ya Biblia, ndilo tendo la mwisho katika mfululizo wa matukio hayo. Tendo hilo la kubadilisha [siku ya ibada] litakapoenea ulimwenguni kote, hapo ndipo Mungu atakapojidhihirisha Mwenyewe. Atasimama katika utukufu wake wa kifalme kuitetemesha sana nchi hii. Atatoka mahali pake kuja kuwaadhibu wakazi wa dunia hii kwa ajili ya maovu yao, na nchi itaifunua damu yake, wala haitawafunika tena hao waliouawa." 7T 141.
f. "Kuweka ile iliyo ya uongo mahali pa ile iliyo ya kweli ndilo tendo la mwisho katika mfululizo wa matukio haya. Tendo hilo la kubadilisha [siku ya ibada] litakapoenea ulimwenguni kote, hapo ndipo Mungu atakapojidhihirisha Mwenyewe. Sheria za wanadamu zinapotukuzwa kuliko sheria za Mungu, mamlaka za dunia hii zinapojaribu kuwalazimisha watu kuitunza siku ya
kwanza ya juma, basi, jueni ya kwamba wakati umewadia kwa Mungu kutenda kazi yake. Atasimama katika utukufu wake wa kifalme, na kuitetemesha sana nchi. Atatoka mahali pake kuja kuwaadhibu wakazi wa dunia hii kwa ajili ya maovu yao." 7BC 980.
9. Je, hivi Waadventista Wasabato wote wanaamini kwamba Amri ya Jumapili kwa ulimwengu wote itapitishwa kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema?
La, hawaamini hivyo wote. Baadhi ya wanafunzi wa Biblia na Roho ya Unabii wanatazamia kwamba kutungwa kwa Amri ya Jumapili hakutaenea duniani kote mpaka kipindi fulani kipite baada ya kufungwa kwa mlango wa rehema.
Madondoo yaliyoorodheshwa chini ya Swali la 8 juu yanatafsiriwa kwa njia kama hii. Usemi mwingine wa kuwaunga mkono wanaoutumia ni huu: "Yesu atakapoondoka patakatifu pa patakatifu, Roho wake anayezuia ataondolewa kutoka kwa watawala na watu. Wataachwa katika udhibiti wa malaika waovu. Hapo ndipo sheria kama hizo zitatungwa kwa ushauri na uongozi wake Shetani, kama wakati usingekuwa mfupi sana, hakuna mwenye mwili ambaye angeweza kuokoka." 1T 204.
Jumanne, Februari 14, 2012
Lady Gaga ni advocate wa Shetani
"Alejandro”
by Lady Gaga.
Very subtly the devil sneaks into our lives to steal and destroy souls!
.We don’t even realise that just by singing the lyrics of a seemingly ‘innocent’ song with a nice tune, we open the door wider for his evil spirit!!
‘
Alejandro’ means: man's defender and protector’ (GOD).
‘Fernando’ means: ardent for peace (JESUS).
‘Roberto’ means: bright or shiningly framed (HOLY SPIRIT).
‘Babe’ is the same as ‘child’
Now the lyrics again:
??"Don't call my name; don't call my name, Alejandro(GOD).I'm not your child, i'm not your child, Fernando (JESUS). Don't call my name; don't call my name, Roberto (HOLY SPIRIT) Alejandro; Alejandro (GOD), Just let me go."
Very subtly the devil sneaks into our lives to steal and destroy souls!
.We don’t even realise that just by singing the lyrics of a seemingly ‘innocent’ song with a nice tune, we open the door wider for his evil spirit!!
‘
Alejandro’ means: man's defender and protector’ (GOD).
‘Fernando’ means: ardent for peace (JESUS).
‘Roberto’ means: bright or shiningly framed (HOLY SPIRIT).
‘Babe’ is the same as ‘child’
Now the lyrics again:
??"Don't call my name; don't call my name, Alejandro(GOD).I'm not your child, i'm not your child, Fernando (JESUS). Don't call my name; don't call my name, Roberto (HOLY SPIRIT) Alejandro; Alejandro (GOD), Just let me go."
People, please stop listening to Lady Gaga!Real name Stefani Joanne Angelina Germanotta. She sold her soul to the devil for fame and fortune, suddenly having 8 million followers on Twitter; top selling artist, and the top winner at the Grammys. This is clearly the devil at work!
Remember the images with her inside the egg carried on a cross? Hatching from an egg signifies the cold blooded rebirth. Implanted horns on her shoulders and cheek bone indicating the transformed BRIDE OF SATAN! (Save a soul and pass this on)
I received it, and I've passed it on. The blood is off my shoulder...
BAADHI YA MAONI:
MTU WA KWANZA:
kusema
ukweli, yule ni advocate wa shetani, shetani lile limevaa mwili wa lady
gaga...hayumo ndani mle anaweza kuwa alishachomolewa muda na pale ni sanamu tu
la shetani..kwasababu kwanza anaabudu kanisa la shetani....so kwakweli,
wanaomsikiliza wanahitaji msaada wa dharura..
MTU WA PILI:
Na sio
Gaga peke yake, maselebriti wengi ni satanic agents, tena na nimesikia kuwa hata wa kibongo
nao wamo..
MTU WA TATU:
Chonde
chonde isiwaingilie Freemassons na Illuminati, tena tuna mpaka ma Rosae Crusis
(Rosecrusins) hapa bongo na wote ni very succesiful.
Somo lao la kwanza ni kujitambua 'self awarenes', ukishajitambua ndipo utakapojua how much power do you posses inside. Sucess huja kwa kuitumia hiyo power on whatever you do, and top you will go!.
Nilimsikia Mchungaji Rwakatare, akishuhudia wito wake wa uchungaji, alitokewa na Mungu na kuambia amemteua aeneze neno lake, yeye Mchungaji akamuomba Mungu, kama kweli anataka aeneze neno pia ampe na utajiri. Kwa sasa ni tajiri mkubwa na anahubiri umasikini ni laana. Jee wewe unapenda umasikini?. Kama lengo ni utajiri, Kuna tofauti gani kuwa illuminati na ukawa tajiri, au kulitumia jina la bwana na ukawa tajiri?. Kwa maoni yangu, yote mawili ni kazi ya Shetani, kwa iluminaji, amejidhihirisha kwao, kwa hawa wengine, ameji disguize kwa jina la Bwana. (Sio wote waitao Bwana Bwana ni Wangu).
Yesu alisema "watakuja watakao toa mapepo kwa jina langu, lakini sii wangu", jee tutawajuaje?.
Fanya utafiti wa hawa wahubiri kwenye TV mbalimbali na utajiri wao, wengine tunao hapa hapa miongoni mwetu, hebu angalia macho yao!
Mwezi Desemba, wachungaji zaidi ya 10 wa kanisa fulani, walikopeshwa mikopo ya nyumba na benki ya kanisa lao, mwezi Desemba wametupiwa vyombo vyao nje na kutimuliwa huku nyumba zikiuzwa kwa mnada kisa hawajakamilisha kulipa deni!, hawa nao wantumikia Mungu?.
Kwa wanaomjua Yesu, alikuwa akitembea peke, hakuja na kitu dunia hii, hakutafuta kitu dunia hii, na aliondoka kama alivyokuja, wanaomfuata Yesu, tumfuate, na wanaomfuata Lady Gaga waache wamfuate!.
Somo lao la kwanza ni kujitambua 'self awarenes', ukishajitambua ndipo utakapojua how much power do you posses inside. Sucess huja kwa kuitumia hiyo power on whatever you do, and top you will go!.
Nilimsikia Mchungaji Rwakatare, akishuhudia wito wake wa uchungaji, alitokewa na Mungu na kuambia amemteua aeneze neno lake, yeye Mchungaji akamuomba Mungu, kama kweli anataka aeneze neno pia ampe na utajiri. Kwa sasa ni tajiri mkubwa na anahubiri umasikini ni laana. Jee wewe unapenda umasikini?. Kama lengo ni utajiri, Kuna tofauti gani kuwa illuminati na ukawa tajiri, au kulitumia jina la bwana na ukawa tajiri?. Kwa maoni yangu, yote mawili ni kazi ya Shetani, kwa iluminaji, amejidhihirisha kwao, kwa hawa wengine, ameji disguize kwa jina la Bwana. (Sio wote waitao Bwana Bwana ni Wangu).
Yesu alisema "watakuja watakao toa mapepo kwa jina langu, lakini sii wangu", jee tutawajuaje?.
Fanya utafiti wa hawa wahubiri kwenye TV mbalimbali na utajiri wao, wengine tunao hapa hapa miongoni mwetu, hebu angalia macho yao!
Mwezi Desemba, wachungaji zaidi ya 10 wa kanisa fulani, walikopeshwa mikopo ya nyumba na benki ya kanisa lao, mwezi Desemba wametupiwa vyombo vyao nje na kutimuliwa huku nyumba zikiuzwa kwa mnada kisa hawajakamilisha kulipa deni!, hawa nao wantumikia Mungu?.
Kwa wanaomjua Yesu, alikuwa akitembea peke, hakuja na kitu dunia hii, hakutafuta kitu dunia hii, na aliondoka kama alivyokuja, wanaomfuata Yesu, tumfuate, na wanaomfuata Lady Gaga waache wamfuate!.
Jumanne, Februari 07, 2012
UTIMILIZO HALISI
Sasa mbele yetu tunayo orodha ya tabia maalum tisa, ambazo zimetolewa toka katika sura ya saba ya Danieli, ili kuifafanua pembe ile ndogo. Kuna mamlaka moja tu katika historia yote ambayo inapatana kabisa na maelezo yaliyotolewa hapa. Kwa shida mno ishara yo yote katika hizo inaweza kutumika kwa mamlaka nyingine, isipokuwa ni UPAPA peke yake. Kanisa Katoliki peke yake linatimiza mambo yote yanayoitambulisha pembe hiyo ndogo ambayo yametajwa katika Danieli 7. Hebu na tuangalie kwa haraka na kuona kwa wazi jinsi jambo hilo linavyotekelezwa.
KWANZA kabisa, UPAPA ulitokea katika
eneo la Ulaya Magharibi, katikati kabisa ya eneo la Dola ya Rumi ya Kipagani
----- katika RUMI yenyewe.
PILI, ulizuka baada ya mwaka 476
B.K. wakati Mfalme Justinian alipomteua Papa kuwa mtawala wa KISIASA na wa KIROHO wa ulimwengu wote. Haya ni mambo ya kweli ya historia ambayo yanaweza kuhakikishwa Kutoka katika chimbuko la mamlaka yo yote ile ya kihistoria.
B.K. wakati Mfalme Justinian alipomteua Papa kuwa mtawala wa KISIASA na wa KIROHO wa ulimwengu wote. Haya ni mambo ya kweli ya historia ambayo yanaweza kuhakikishwa Kutoka katika chimbuko la mamlaka yo yote ile ya kihistoria.
TATU, Upapa ulipotokea ulipingwa na
makabila matatu ambayo yalikuwa yametawala baada ya kuangushwa kwa Dola ya
Kirumi. Wavandali (Vandals), Waostrogothi (Ostrogoths), na Waheruli (Heruli)
walikuwa ni mamlaka zenye imani ya Arius (Arian powers) ambao kwa Nguvu zao
zote walipinga kuzuka kwa Kanisa Katoliki. Majeshi ya Warumi yakayang'oa kabisa
na kuyaangamiza makabila hayo matatu. La mwisho katika hayo matatu
liliangamizwa katika mwaka ule ule wa 538 B.K., wakati RUMI YA KIPAPA
ilipoanza kutawala dunia.
NNE, Katika mfumo wake, Kanisa
Katoliki lilikuwa na MTU akiliongoza.
TANO, Upapa ulikuwa ni UFALME ULIO
TOFAUTI na falme zile nyingine za kisiasa zilizoutangulia. Ulikuwa ni MAMLAKA
YA KIDINI NA KISERIKALI ambayo iliitawala dunia yote. Hakuna mamlaka
iliyofanana kabisa na hiyo ambayo ilipata kuonekana ulimwenguni kabla ya wakati
ule.
Sasa tunaiangalia tabia yake ya SITA
----- ile ya kunena maneno makuu na makufuru dhidi yake Aliye juu. Je, Upapa
unatimiza maelezo hayo? Tunahitaji tu kukumbushwa Kwamba Kanisa Katoliki
limejitwalia lenyewe UWEZO WA KUSAMEHE DHAMBI. Kuhusu maneno yake makuu, hebu
ninukuu kutoka katika makala ya F. Lucii Ferraris, iliyo katika kitabu cha
PROMPTA BIBLIOTHECA CANONICA JURIDICA MORALIS THEOLOGICA. Kitabu hiki
kilichapishwa mjini Roma, na kimeidhinishwa na ensaiklopidia ya Kikatoliki.
Sikiliza madai haya: "Papa ni mkuu mno, naye ametukuzwa sana, kiasi kwamba
yeye si mtu tu, bali kama ilivyo, yeye ni Mungu na Aliye Badala ya Mungu (Vicar
of God). Kama ilivyo, PAPA NI MUNGU DUNIANI. Mfalme mkuu wa wafalme, mwenye
uwezo mwingi." Gombo la VI, uk.25-29. Haya ni maneno machache tu ambayo
Biblia inasema kuwa ni makufuru. UPAPA unatimiza ishara zote za utambulisho na
hivyo kuwa ile PEMBE NDOGO.
hivyo kuwa ile PEMBE NDOGO.
Sasa tunakuja kwenye kitambulisho cha
SABA, tunaona ya kwamba HISTORIA inaunga mkono unabii huu kuhusu MATESO YA
PAPA. Kila mmoja anayejua habari za Kizazi kile cha Kati (Middle Ages) Zama za
Giza anafahamu fika ukweli kwamba mamilioni ya watu waliteswa kikatili mno
na kuuawa na Mahakama Maalum za Kikatoliki (Inquisitions). Kutoka katika kitabu
kilichoandikwa na Kadinali wa Kikatoliki, ambacho pia kimeidhinishwa na Kanisa Katoliki, tunasoma hivi: "Kanisa Katoliki... lina hofu kuu ya kumwaga
damu. Hata hivyo, linapokabiliwa na UZUSHI HERESY... LINALAZIMIKA KUTUMIA NGUVU,
kutoa adhabu ya kupigwa viboko mwilini, na KUTESA. Linaunda mahakama kama ile
ya Inkwizisheni (Inquisition).
Linatumia SHERIA ZA SERIKALI
kulisaidia... Lilifanya hivyo hasa katika karne ile ya 16 kuhusiana na
WAPROTESTANTI... Katika nchi ya Ufaransa, chini ya wafalme Francis I na Henry
II, katika nchi ya Uingereza chini ya Malkia Mary Tudor, Kanisa Katoliki
liliwatesa wazushi." Maneno haya yamenukuliwa kutoka katika kitabu cha
'THE CATHOLIC CHURCH, THE RENAISSANCE AND PROTESTANTISM', uk.182-184. Tunaweza
kuongeza semi nyingi kama hiyo kutoka kwa wanahistoria, Wakatoliki na
Waprotestanti, zinazoelezea MATESO YA KUTISHA ya mamlaka ya kipapa juu ya
Waprotestanti. Kwa njia hiyo tunaweza kuona utimilizo kamili wa maelezo haya ya
pembe ndogo.
Ishara ya NANE, kama ilivyotolewa katika fungu la ishirini na tano, inahusu jaribio lile la kubadili Sheria ya Mungu Amri Kumi. Je, jambo hilo linahusika na Upapa?
Ishara ya NANE, kama ilivyotolewa katika fungu la ishirini na tano, inahusu jaribio lile la kubadili Sheria ya Mungu Amri Kumi. Je, jambo hilo linahusika na Upapa?
Tafadhali zingatia haya: Kanisa
Katoliki limeondoa Amri ya Pili kutoka katika vitabu vyake vya mafundisho ya
dini na Katekisimu zake, kwa sababu inashutumu IBADA YA SANAMU. Kisha Amri ya
Kumi imegawanywa sehemu mbili ili waendelee kuwa na Amri Kumi. Walakini mbili
zinakataza KUTAMANI, na hakuna hata moja inayokataza IBADA YA SANAMU. Kwa njia
hii, Upapa UMEAZIMU UMEFIKIRIA kubadili Sheria ya Mungu, lakini bila
mafanikio. SHERIA YA MUNGU HAIWEZI KUBADILISHWA.
Mwishowe, tunakuja kwenye ishara ile ya TISA ya kitambulisho chake, ambayo inatuambia hasa muda ambao mamlaka hii ya Upapa ingeyatumia mamlaka yake juu ya dunia hii. Tuligundua kwamba ingetawala kwa miaka 1260.
Mwishowe, tunakuja kwenye ishara ile ya TISA ya kitambulisho chake, ambayo inatuambia hasa muda ambao mamlaka hii ya Upapa ingeyatumia mamlaka yake juu ya dunia hii. Tuligundua kwamba ingetawala kwa miaka 1260.
Je, jambo hilo linakubaliana na kumbukumbu
za historia? Kumbuka, ya kwamba tumeona jinsi Upapa ulivyoanza utawala wake,
kwa amri ya Justinian, katika mwaka wa 538 B.K.. Tukihesabu kuja upande wetu miaka
1260 kuanzia mwaka huo tunaletwa kwenye mwaka wa 1798. Katika mwaka uo huo
Jenerali wa Kifaransa, Berthier, aliongoza majeshi yake kuingia mjini Roma na
kumng'oa Papa Pius wa VI Kutoka kwenye kiti chake cha enzi. Alichukuliwa
uhamishoni, na mali zote za Kanisa zikataifishwa zikanyang'anywa. Uongozi wa
Serikali ya Kifaransa ulitoa amri kwamba pasingekuwa na Askofu mwingine wa Roma
kamwe. Kwa kadiri ulimwengu ulivyohusika, na kwa mwonekano wa nje, Kanisa
Katoliki lilikuwa limekufa. Baada ya miaka 1260 kamili, kwa kutimiza unabii
huu, likapoteza utawala wake juu ya dunia hii. Hivyo pointi hii ya mwisho
imetimizwa kwa wazi kabisa katika Upapa, na katika Upapa peke yake.
Kuthibitisha na kujionea maelezo zaidi ya haya click HAPA
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






