Jina “HAR-MAGEDONI”
hushtua kwa hofu na kuashiria hatari katika mawazo ya wengi. Wengine
wanadhani ni vita kuu ya
ulimwengu kuzunguka Mashariki ya Kati. Wengine hutazamia Mpinga Kristo
akipigana ili kupata ukuu wa ulimwengu wote. Na bado
wengine hawajui nini cha kuamini au kutegemea. Neno “Har-Magedoni” lenyewe utafsiriwa “jina la alama” (angalia Strong's
Exhaustive Concordance, #717). Na bado Maandiko hayafundishi kwamba kutakuwepo
vita halisi vinatakavyohusisha ulimwengu wote! Vita hii na mapambano
havitapiganwa kwa kutumia silaha halisi, kama bunduki, mizinga, ndege za vita,
au majeshi yenye silaha.
Lakini vitapiganwa,
tayari vimeanza kupiganwa, na vitaendelea kupanuka kwa nguvu zaidi mpaka kila
mtu katika ulimwengu anahusishwa. “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na
vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama,
na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani,
zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote; kuwakusanya
kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. Tazama, naja kama mwivi. Heri
akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake. Wakawakusanya
hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.” Ufunuo16:13-16.
Kama inavyoweza
kuonekana, Maandiko hufundisha kwamba vita hivi vinapiganwa kati ya majeshi
makuu mawili: Mungu, Kristo na wafuasi
wake wasafi au wenye haki, dhidi ya Ibilisi, roho za uovu, na wafuasi wake
wachafu au waovu. Kwa hiyo vita vya Har-Magedoni ni alama inayoeleza pambano
kuu na mgongano unaondelea kwa nguvu kati ya Mungu na Shetani--kati ya ukweli
na ufisadi. Na vita hivi vya kiroho hatimaye vitahusisha kila mtu katika dunia
kwani kila mmoja lazima aamue nani wa kufuata--Kristo na ukweli, au Ibilisi na
ufisadi: uzima wa milele pamoja na Kristo, au maangamivu milele pamoja na
Shetani. Vita hivi na mapambano kati ya Kristo na Shetani vilianza mbinguni.
“Kulikuwa na vita
mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye
akapigana nao pamoja na malaika zake;
nao hawakushinda, wala mahalipao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka
akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa
zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata
nchi, na
malaika zake wakatupwa
pamoja naye.” Ufunuo 12:7-9. Hata kama Ibilisi alitupwa kutoka mbinguni,
aliendelea na mapambano yake dhidi ya
Kristo na Mungu katika dunia hii. Kwa karibu miaka elfu sita mgongano huu
umeendela na kuzidi kupanuka. Lakini
vita vya mwisho vya kupiganwa katika pambano hili kuu, kilele ambacho matukio
yote yamekuwa yanaelekeza, ni
kile ambacho Biblia hufafanua kama siku kuu ya Mungu Mwenyezi--vita vya
Har-Magedoni.
Vita hivi vya mwisho kati
ya ukweli na ufisadi vinaonyeshwa wazi katika Ufunuo sura zifuatazo 12, 13, 14,
& 18. Na wanadamu wote wameingia katika vita hii leo. Kutokana na kwamba
Har-Magedoni ni alama inayoeleza vita vya kiroho kati ya
ukweli na ufisadi, ni silaha gani ambazo Ibilisi anatumia katika pambano hili
kuu? Vitu vinavyofananishwa na
vyura vilitoka katika kinywa cha Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo. Sasa vyura
hukamata mawindo yao kwa kutumia
ndimi zao, na kinachotoka katika vinywa vyao ni maneno yanayopangiliwa pamoja
katika misingi ya imani. Kwa
hiyo hawa viumbe watatu hukamata mawindo yao kwa kusema au kufundisha
mafundisho mbalimbali ya ufisadi.
Kwa wale wanaotamani
kumfuata Kristo na ukweli, ni kitu cha maana sana kwamba tuweze kupambanua wazi
nani ni Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo kusudi tuweze kuepuka kudanganywa kwa
mafundisho mbalimbali ya uongo na hivyo kupotea. Kama ilivyodhihirishwa katika
Ufunuo 12, Joka kimsingi ni Shetani. Na kauli gani za misingi ya makosa na
mafundisho ya uongo zimetoka katika kinywa cha Shetani? Mafundisho mbalimbali
ya umizimu, upagani, na uchawi ambayo falme za ulimwengu zimejengwa juu
yake--ikiwa ni pamoja na Himaya ya Kirumi ya kipagani ya zamani. Wakati wengi wanaamini
upagani kuwa kitu cha zamani, bado kuna mamilioni leo wanaojihusisha na imani
zake za kikafiri na ibada ya Ibilisi.
Ishara za awali za dini
ya kipagani ni kuabudu vitu vya asili. Kutokana na kwamba umbo lililo juu zaidi
katika asili ni mwili wa binadamu, na
hasa mawazo, mwanadamu anaongozwa kuabudu nguvu za mawazo na hivyo kuinua maoni ya mwanadamu juu ya
ufunuo wa Mungu. Mamlaka zote kuu zilizotawala dunia zilidhihirisha ukweli kwamba katika upagani,
Kanisa na serikali havikutengana--lakini vilikuwa vimeungana pamoja. Katika
Babeli, Umedi-
Uajemi, Uyunani, na Rumi,
serikali mara zote ilitumiwa kuunga mkono na kutoa nguvu kwa dini ya kipagani
ya wakati huo. Majira na
tena sheria zilipitishwa na mamlaka ya serikali ili kutumika kulazimisha
kuabudu miungu ya kipagani na mafundisho ya uongo.
Leo, kama ilivyokuwa
katika nyakati za zamani, roho ya kuinua na kuabudu maoni ya mwanadamu,
taasisi, na Kanisa na serikali ili
kusudi Kanisa liweze kupatiwa nguvu kupitisha maamuzi na mafundisho yake makuu,
ni roho ya Joka. Na roho hii
itaongezeka zaidi na zaidi kwa kujulikana mpaka itakapoishia katika kipindi
kikuu cha taabu kwa watu wa Mungu. Siyo roho hii tu ya uchafu ambayo inafanya
kazi leo kupitia nadharia ya kibinadamu na falsafa zingine za ubatili-- kumwinua
mwanadamu juu ya Mungu, kuinua ufisadi juu ya ukweli--lakini kuna roho nyingine
ya pili ambayo inatoka kwenye kinywa cha Mnyama.
Katika Ufunuo 13, Mnyama
ambaye aliinuka kutoka kwenye mabaki ya Roma ya kipagani; Mnyama ambaye alijiunganisha mwenyewe
na upagani ili kuongeza idadi yake; Mnyama ambaye alitawala kwa siku za kinabii
1260 (Ufunuo 12:6), au miaka
ya unabii 3 1/2 (Ufunuo 12:14), au miezi ya unabii 42 (Ufunuo 13:3)--kila moja
ikileta jumla ya miaka halisi 1260 (angalia Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6), si mwingine
bali Kanisa Katoliki la Kirumi Mfumo huu mkuu wa kidini wa Ukatoliki huliinua
Kanisa lililopangiliwa juu ya dhamiri ya mtu, na wakati kuna mgongano kati ya
Biblia na Kanuni za Kanisa, kanuni daima huwekwa juu zaidi ya ukweli wa Biblia.
Kama kuna kutokubaliana kati ya dhamiri ya mtu na fundisho kuu la Kanisa,
Kanisa kwa njia ya mapokeo yake na maoni mara zote huchukua sehemu ya kwanza.
Kwa kutofautisha na
utawala huu na utawala wa Kanisa, Paulo anawasifia Waberoya waungwana kwa
sababu “walilipokea lile neno
kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo
hayo ndivyo yalivyo” Matendo 17:11. Hakuna mahali popote tunapomkuta Paulo
akiwataka waumini kukubali mafundisho kwa msingi wa mamlaka ya Mitume, lakini badala
yake aliwahamasisha kuyachunguza Maandiko wao wenyewe ili kuthibitisha ukweli
wa mambo waliyokuwa wamefundishwa. Wazo la neno la Mungu kama mamlaka ya juu na
mwongozo wa maisha ni dini na ukweli wa Biblia (angalia Yohana 5:39; 2 Timotheo
3:16-17; Isaiya 8:20), na maarifa haya yanatuweka
huru (angalia Yohana 8:32).
Roho ya tatu ya uchafu ni
roho ya Nabii wa Uongo. Nabii ni mmoja wa wanaodai kuwa wamepokea ujumbe kutoka kwa Mungu, na kisha hudai
kuwa mnenaji wa Mungu katika kueneza kwa haraka ujumbe huu kwa watu (angalia
Hesabu 12:6; Kumbukumbu la Torati 18:22). Nabii wa uongo hatimaye angekuwa mtu
yeyote anayedai kuwa ananena kwa ajili ya Mungu, wakati katika hali halisi hafanyi
hivyo (angalia Yeremia 14:14). Nabii wa Uongo haiwezekani kurejewa kama upapa,
kwa sababu umedai siku zote kupokea utamaduni juu ya ufunuo wa Biblia na haki ya
kubadilisha amri za Mungu kadiri wapendavyo. Lakini Makanisa mbalimbali ya
Kiprotestanti yamedai kufuata Biblia tu
kama msingi wa imani yao na mafundisho. Na bado, tunayaona yakifuata katika
nyayo za Roma kwa kuinua utamaduni
[mapokeo] juu ya ukweli wa neno la Mungu! Kwa hiyo Makanisa hayo ni nabii wa
uongo
yaking’ang’ania, kuongea
yakiunga mkono, makosa na huku bado yanadai ni ukweli wa Mungu!
Wakati yakitofautiana
katika baadhi ya mambo fulani, Makanisa ya Kiprotestanti yote yanaungana pamoja
katika mafundisho yasiyoleta
hitilafu, na zaidi na zaidi yanafanana na Ukatoliki wa Kirumi. Wakati, katika
harakati za kufikia malengo yake, huyu Nabii
wa Uongo wa Uprotestanti anapofuata katika nyayo zile zile za Rumi, kwa
kuungana na kutegemea nguvu za
kiserikali kumwunga mkono katika mafundisho yake na kukanyaga haki ya uhuru wa
kuabudu ili kulazimisha mafundisho
yake makuu, atakuwa pia Sanamu ya Mnyama (angalia Ufunuo 13). Kwa kukataa
ukweli, watu wanakataa Mwanzilishi wa ukweli na kujiandaa wenyewe kuwa upande
wa Ibilisi katika vita hii kuu ya mwisho. Kwa kuendelea kukaidi kukubali mamlaka
ya Mungu--Mtoa sheria, na kutii sheria zake, wanaume, wanawake, na watoto
wanajifunga wenyewe kwa mwasi mkuu katika ufisadi.
Hakuna kosa linalojeruhi
sana moja kwa moja dhidi ya mamlaka na serikali ya Mbinguni na linapingwa zaidi
katika maamuzi ya hiari kuliko
wazo kwamba sheria ya Mungu si ya lazima tena. Sheria ndiyo msingi wa serikali
yote, na ni kukosa hekima kikamilifu
au kuungwa mkono kuamini kwamba Mtawala wa ulimwengu amestaafu katika wajibu wake na kutuacha bila
sheria yake! Iwe Ibilisi amekudaka wewe kwa kuweka mbali sheria ya Mungu yote,
au kukataa moja ya mausia yake,
matokeo yake ni yale yale. Yeyote anayejikwaa “katika neno moja” hudhihirisha
dharau kwa sheria yote; mvuto wake
na mfano viko upande wa uasi; anakuwa “amekosa juu ya yote” (angalia Yakobo 2:10). Popote pale mausia ya
Mungu yanapotupiliwa mbali, dhambi hukoma kuwa ya kuchukiza au haki kuwa kitu
cha kutamaniwa.
Maandiko yanatangaza
kwamba roho za mashetani zitafanya kazi kwa nguvu miujiza ambayo itawadanganya karibu ulimwengu wote, na
kisha kuwakusanya watu wote pamoja kwa ajili ya vita kuu ya mwisho. Kigezo
kikuu cha mgongano kitakuwa ni
sheria ya Mungu, na hasa Sabato, ambayo inamwonyesha Mtoa sheria kama Muumbaji
pekee na hivyo tunayepaswa kutoa utii kwake kama sehemu ya lazima ya urithi. Ni
kazi ya ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12 & 18:1-5 kubatilisha
mashambulizi haya dhidi ya sheria ya Mungu kwa kuleta kwa ulimwengu ibada inayostahili
kwa Mungu kama Muumbaji wetu. Kwa muungano wa nguvu hizi tatu za Joka, Mnyama,
na Nabii wa Uongo, watu wote walioko duniani watalazimika kuungana katika
jukwaa la uovu dhidi ya
Mungu na ukweli wa
Biblia. Na wale ambao hawafuati maamuzi yao [nguvu hizi tatu] watauawa. Hivyo,
kupitia mafundisho ya udanganyifu na mafundisho ya muungano huu wa nguvu tatu za
umizimu, Ukatoliki, na Uprotestanti, wakazi wote wa dunia watatakiwa kukata
shauri kuwa upande wa, au kinyume cha, Mungu na ukweli wake (angalia
Ufunuo13:15- 17). Mungu halazimishi utashi wa dhamiri, lakini Shetani mara kwa
mara hujaribu kutumia njia mbalimbali za nguvu na ukatili ili apate utawala
juu ya wale ambao hawezi, kwa njia yoyote, kuwadanganya. Kwa njia ya woga, au
kwa nguvu halisi, Shetani hupanga
kutawala dhamiri na kujipatia utukufu mwenyewe. Kutimiza hili, hufanya kazi
kupitia mamlaka ya kidini na pia
ile ya serikali za dunia, akiwasukuma kupitisha sheria za wanadamu ambazo humpinga
kabisa Mungu na sheria yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni