Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Februari 24, 2012

UKANDA WA GAZA


...ni eneo dogo kwenye mwabao wa Mediteranea ya Mashariki lililopo sehemu ya mamlaka ya Palestina. Lina urefu wa kilomita 40 na upana kati ya 6 km na 14 km. Eneo lote halizidi 360 km². Gaza imepakana na bahari halafu nchi za Israel na Misri. Israel inatenganisha Gaza na maeneo upande wa magharibi ya Yordan yaliyo pia sehemu ya mamlaka ya Palestina.

Ni kati ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu likiwa na wakazi milioni 1.4 yaani zaidi ya watu 4,100 kwa km².

MJI MKUBWA WA GAZA.

Kanda hili ni kati ya mabaki ya Palestina ya Kiingereza yasiyotwaliwa na Israel wakati wa vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948 na kuwa kimbilio kwa wakimbizi wengi Wapalestina waliowahi kukaa katika sehemu zilizokuwa Israel. Kati ya 1948 hadi 1967 lilitawaliwa na Misri. Tangu vita ya siku sita ya 1967 kanda lilikuwa chini ya Israel. Tangu 1994 ilikabidhiwa kwa mamlaka ya Palestina lakini Israel iliendelea kuwa na vijiji vya Waisraeli na vituo vya kijeshi ndani yake. Mapigano ya intifada yaliongezeka kuwa makali na kusababisha vifo vingi. Tangu 2005 Israel iliondoa wakazi na wanajeshi wake wote.

Baada ya uchaguzi wa 2006 chama cha Hamas chini ya Ismael Haniya kilipata kura nyingi na kushika serikali ya Palestina. Farakano kati ya Hamas na Fatah wa rais Mahmud Abas liliongezeka hadi Hamas kuchukua mamlaka yote katika Gaza kwa nguvu ya silaha mwezi wa Juni 2007. Tangu mwezi ule Gaza iko chini ya serikali ya Hamas lakini maeneo mengine yako chini ya mamlaka ya rais Abas.

Hali ya wakazi ni vigumu. Israel imefunga mipaka na kuzuia wakazi wa Gaza wasitoke nje kwa sababu wanamigambo Wapalestina wanaendelea kurusha roketi ndogo kutoka Gaza kwenda Israel. Kutokana na kufungwa kwa mipaka yote uchumi ni duni hakuna ajira. Hata huduma za kimsingi kama vile maji na umeme zinavurugika kabisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni