Kwa mjibu wa nyaraka za MOSSAD, CIA, RAW na FSB juu ya elimu ihusuyo
"kiwango cha hali ya hatari katika eneo la kiraia" ambacho hupimwa kwa
kipimo kiitwacho Def Cond, inasema, "Pale majadiliano ya meza
yanaposhinwa kuleta jibu chanya, wanamjadala hususia meza, ambapo katika
kipimo husomeka Def Cond 0001".
Ikitokea kuwa hata huko
walikoamua wanamjadala hao kupeleka hisia zao nako kukazuiwa, hasira ya
wanamjadala hao huongezeka na kuwa Def Cond 0002.
Hatua ya mwisho ya wanamjadala hawa huwa ni kwenda kwenye mahakama ya umma, hapa kipimo husomeka Def Cond 0003.
Hiki ni kipimo kikubwa katika medani ya kiusalama kwa mambo ya ndani,
ambapo matokeo yake shughuli katika jamii husimama, serikali hushindwa
kutawala wala kuongoza. Katika lugha nyingine huitwa mgogoro wa
ndani,kisiasa,kikatiba nk...
Zingatia hali hii haizai vita, kwani
ili vita kamili ya ndani izaliwe lazima hali ya hatari isomeki Def Cond
0006. Na ili vita kamili izaliwe katika ya taifa na taifa lazima hali
ya hatari isomeke Def Cond 0008.
Mzigo ukiwa dukani tayari kwa mauzo, Bei ya rejareja 30,000/= Bei ya Jumla 25,000/=
Fika Dukani House of Wisdom Bookshop lililopo Dar es Salaam, Posta, mtaa wa Samora jengo la NHC Ghorofa ya kwanza.
Kwa walio nje ya Jiji la Dar wanaweza kununua kwa M-Pesa +255755865544
Yericko Nyerere. Utaletewa mahali ulipo kwa njia ya Posta.
PIA KWA MAUZO YA JUMLA LIPA KUPITIA BANK YA CRDB AC NO: 0152241955000. Name: YERICKO YOHANESY NYERERE. BRANCH NAME: HOLAND HOUSE BRANCH CODE: 3319 BANK NAME: CRDB BANK PLC SWIFT CODE: CORUTZTZ CURRENCY: TZS.
WANAKARIBISHWA WAFANYABIASHARA WALIOTAYARI KUWEKEZA KATIKA BIASHARA HII.
Asilimia
kubwa ya wanamuziki hapa Tanzania wanapiga muziki bila ya kuwa na elimu yoyote
ya awali ya muziki, hili si jambo la ajabu kwani hali hii iko sehemu nyingi
duniani, lakini kitu ambacho ni wazi kinakosekana ni elimu kuhusu utendaji wa
taasnia ya muziki.
Pamoja na kauli nyingi nzuri za viongozi wa Nchi kusifu
sanaa hii na wasanii wa sanaa hii lakini ni nadra kusikia kiongozi akiongelea
matayarisho rasmi katika sanaa hii na kwa kweli hata katika sanaa nyingine.
Kumekuwepo
na ombwe la elimu ya uendeshaji wa tasnia ya sanaa. Ombwe la elimu kwa
wataalamu ambao huwezesha wasanii kufika walipo, kuwaendeleza kukaa walipo,
kulinda haki za kimaslahi za wasanii na hata kuwapa maelekezo ya kujitayarisha
kwa wakati ambapo umaarufu utakuwa umekwisha.
Tasnia ya
muziki huhiyaji shule za kujifunza muziki, vyuo vya uongozi wa muziki, au kozi
fupi ambapo taaluma za umeneja, uproducer, upublisher, usambazaji, ujuzi wa
sheria za hakimiliki na watendaji wengine wa aina hiyo hupata elimu, ujuzi wa
sheria za hakimiliki na watendaji wengine wa aina hiyo hupata elimu. Kukosekana
kwa elimu hii kumefanya watu kujifunza kwa vitendo kwa kujaribu na hata
kubahatisha hivyo mara chache kufanikiwa.
Kukosa elimu
sahihi kumewafanya wasanii wengine wenye uwezo mkubwa kupotea kwenye taaluma na
wengine kujikuta wakishindwa kuingia kwenye ulingo huu japo uwezo wanao. Pia
kumetoa nafasi ya wasio na uwezo kujikita katika uongozi wa sanaa na kuleta
matatizo makubwa kwenye sanaa, aidha kwa kuaminika kuwa wanatoa ushauri sahii
na hivyo maamuzi yenye hasara kubwa kufanyika.
Pamoja na mafanikio
yaliyoonekana taifa linakwenda kihobela hobela katika tasnia ya sanaa ya
muziki. Ushahidi wa
wazi upo kwa kupata elimu ya muziki kuanzia umri mdogo kuna faida nyingi sana.
Kwanza humuwezesha motto kukuza sehemu ya ubongo ambayo huhusika na hesabu na
pia kukuza uwezo wake wa kutafakari.
Inaeleweka
kuwa ubongo huendelea kupata maendeleo miaka mingi baada ya kuzaliwa, hivyo
muziki huendelea kuboresha upande wa kushoto wa ubongo ambao ndio huhusika na
ujuzi wa lugha na tafakari na hesabu. Muziki husaidia sana watoto kukumbuka
mambo mbalimbali, ndio maana hata matangazo ya biashara ya kawaida husindikizwa
na muziki ili kukaa katika kumbukumbu kwa urahisi. Kwa watoto muziki husaidia
sana katika kazi zao za elimu ya kila siku.
Wasanii
waliopata elimu sahihi huwa na uwezo wa kubuni majibu mbalimbali kwa tatizo
moja, hii unaweza kuiona kwa mfano ukiwapa wanamuziki kumi semina kuhusu jambo.
Kwa mfano: Ukimwi kasha ukawaambia watunge wimbo kuhusu elimu waliyopewa,
utashangaa watakuja na tungo tofauti za mtizamo mpya kabisa wa kuelezea elimu
hiyo waliyoipata.
Elimu ya
muziki hufungua ubongo kuruhusu kuachana na mawazo mengi yaliyopita na kujaribu
mawazo mapya. Wasanii kote duniani huwa waanzilishi wa mambo mengi ikiwemo
mitindo ya nguo, uvaaji na mambo mengi katika maisha kutokana na ubongo wao
kuwa na uwezo wa kuruhusu kufikiria vitu katika mtazamo mpya.
Elimu ya
awali ya muziki imeonesha kuwa wanafunzi wa elimu hii hfanya vizuri zaidi
katika masomo mengine tofauti sana na mawazo ya kawaida kuwa muziki huharibu
watoto. Katika muziki, kosa huwa ni kosa, ukikosea beat, usipotune chombo
chako, ukiimba vibaya ni kosa hakuna mbadala, sauti ikiwa juu mno, au chini mno
na kadhalika, na wanamuziki hulazimika kurudia tena na tena mpaka atakapopata
kitu sahihi na kabisa.
Elimu hii
ikiwa kichani kwa watoto toka umri mdogo humsaidia katika kuboresha mambo yake
mengine na kuyafanya vizuri zaidi kila mara. Elimu ya awali ya muziki humjenga
motto kujua kufanya kazi na watu wengine kama kundi, kutokana na kuelewa kuwa
katika muziki watu wengi hutegemeana ili kuleta ubora katika wimbo mmoja, hii
huwasaidia katika maisha kila siku.
Kuna mengi
yanayopatikana katika elimu bora ya sanaa, pia kubwa likiwa ni kwenda sambamba
kitaaluma na ulimwengu, kuna bahati mbaya sana kwa vijana wetu kutaka kuingia
katika soko la muziki duniani lakini bila kuwa na matayarisho yanayostahili
kufikia huko, wengi ni ndoto zao hazitatimia kwani elimu ya kufikia huko
hawana.
Ni wazi kuna
haja ya kuanza kutoa elimu ya sanaa kuanzia ngazi ya shule za awali, kuna haja
sasa ya kuwasaidia wanamuziki walioko kwenye taaluma kupata elimu ya haki
zao.
Ni wasanii
wangapi wanaojua kuwa katika kila tungo, kuna haki tofauti kumi
wanazostahili?
Watunzi
wangapi wanajua wana haki kwa kazi zao kutumika kibiashara?
Wakati
viongozi wakisifia wasanii wan je wakumbuke kuwa kinachowafanya wawe na
mafanikio ni kutumia kila njia sahihi kukamua mapato kutoka kwenye haki zao
hizo zinazolindwa kisheria.
Ni ukweli usiopingika kwamba mwanadamu anakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi, kiafya, kijamii na kadhalika.
Changamoto zote hizo huongezeka zaidi pindi mwadamu anapofikia umri wa utu uzima, kwa maana ya umri wa kubebeshwa majukumu ya kimaisha, kama vile kusaidia wanafamilia, wanaukoo na jamii kiujumla.
Hata hivyo, changamoto kubwa za kiafya zinazomkabili mwanadamu huyu, karibu kote ulimwenguni ni ugonjwa wa Mkazo, ambao kitaalamu wanaita Stress pamoja na kupanda kwa Shinikizo la Damu, kitaalamu Hypertension.
Baadhi ya vitu vinavyosababisha ugonjwa huu wa Mkazo kwa mujibu wa wataalamu wa afya, ni pamoja na hofu au wasiwasi kuhusiana na jambo lolote linaloweza kumkumba mwanadamu, hasa ukosefu wa fedha mfukoni au kutamani utajiri ambao hajui ataupataje.
Lakini pia, ratiba za shughuli za kiuchumi na huduma zenye mambo mengi yasiyokuwa na mpangilio huweza kumsababisha ugonjwa huo binadamu, pamoja na ugomvi usiokwisha ndani ya familia, kukumbana na matukio ya kutisha kama vile ya ugaidi na kadhalika.
Watu wengi ulimwenguni wamezoea kutumia kilevi, kama vile pombe, tumbaku na vileo vingine ili kukabiliana na maradhi hayo ya Mkazo na kupanda kwa Shinikizo la Damu.
Hali hiyo, inatokana na wengi wao hao kushidwa hata kula vizuri, huku baadhi yao wakilazimika kutumia muda mwingi kuangalia matukio katika televisheni au kutumia vifaa vya kielektroniki kama vile kompyuta na simu za mkononi kwa muda mrefu ili tu kujisahaulisha na msongo wa mawazo kichwani.
Mkazo na Kupanda kwa Shinikizo la Damu, ni vitu vinavyoendana sana katika maisha ya mwanadamu, ndiyo maana ili kudhibiti magonjwa hayo, mhusika hushauriwa kudhibiti kwanza hali yake ya Mkazo.
Kituo kimoja cha Matibabu ya Akili kilichoko nchini Uingereza, zinabainisha kwamba katika kila kundi la watu watano ulimwenguni, basi mtu mmoja hukumbwa na maradhi ya Mkazo unaotokana na mazingira ya mahali pake pa kazi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, kushindwa kukabiliana na hali hiyo ya Mkazo mwingi, mtu mmoja kati ya watu wanne, hujikuta akilia peke yake bila kupigwa wala kukasirishwa na yeyote, akiwa kazini kwake.
Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mwanadamu ameumbwa kwa njia ya kipekee kabisa, kwa kuwekewa mifumo mbalimbali mwilini inayofanya kazi mbalimbali usiku na mchana ili tu kumweka vizuri na salama katika maisha yake.
Kwa mfano, mwanadamu amewekewa mfumo wa hisia za dharura, ambao ni kichochea kikuu cha mwili pindi mwanadamu huyu anapopatwa na Mkazo mwingi. Vichocheo hivyo, ndivyo vinavyomfanya binadamu huyo anapopatwa na hali hiyo aweze kupumua haraka, moyo wake uende mbio na kadhalika hali inayochangia kuongezeka kwa Shinikizo la Damu.
Aidha, vichocheo hivyo, ndivyo huongeza chembe za damu na sukari kwenye damu.
Kwa kawaida, mfumo huo wa hisia za dharura unafanya kazi kubwa ya kumtayarisha mwanadamu kukabiliana na kitu chochote au mtu yeyote anayemsababishia hali hiyo ya Mkazo.
Hata hivyo, baada ya jambo hilo linalosababisha Mkazo kupita, mwili hurudi katika hali yake ya kawaida, ingawa baadhi ya wataalamu wanaweka wazi kuwa endapo hali hiyo ya hisia za dharura inajirudia mara kwa mara, mtu anaweza akakumbwa na ugonjwa mwingine wa hofu au wasiwasi, ambao kitaalamu unajulikana kama 'Anxiety Disorder'.
Kwa hiyo, kwa kila binadamu awaye yeyote yule, ni muhimu kujifunza mbinu za kukabiliana na maradhi hayo Mkazo na kupanda kwa Shinikizo la Damu. Kwa sasa zipo njia kuu rahisi 10 za kukabiliana na hali hiyo.
mediaphotos/Getty Images
Mosi, ni kuhakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala usingizi, Kutopata usingizi wa kutosha kunaathiri hisia, akili, kiwango cha nishati mwilini pamoja na afya kiujumla. Wataalamu wa afya wanashauri mtu mzima apate usingizi wa walau saa nane (8) katika kila saa 24 za siku.
Pili, katika kujipangia mipango ya maisha, unashauriwa kutanguliza mambo muhimu yanayokuwezesha kuishi maisha yenye kiasi. Kwa maneno mengine, binadamu anatakiwa kufikiri jinsi ya kurahisisha maisha yake, pengine kwa kupunguza gharama za maisha pamoja na kupunguza muda anaotumia kufanya kazi kazini kwake.
Tatu, jifunze mbinu za kupumzisha mwili. Kutafakari kwa kina (Meditation), mazoezi ya kuvuta pumzi na yoga ni njia imara za kuondoa Mkazo.
Nne, mtu inampasa kuimarisha mtandao wake wa kijamii. Kujiunga na vikundi mbalimbali kama vile vya masomo, kutoa misaada kama vile kwa watoto, yatima na wajane au vikundi vya wajasiriamali.
Mwaka 2008, baadhi ya watafiti raia wa Uingereza waligundua njia moja ya kubaki imara pindi mtu anapopatwa na Mkazo. Katika utafiti wao, wanasema moja ya njia ya kubakia imara, ni kujitolea kuwasaidia wengine kwa njia fulani fulani.
Tano, mtu inampasa kujitahidi kuelewa vizuri hisia za wengine, kitu kitakachomsaidia kupunguza hasira, na wakati huo huo awe mwepesi kusamehe kwa kuwa ni jambo jema pia kimaisha. Utafiti uliofanywa mwaka 2001 nchini Uingereza, ulionyesha kwamba mtu anapokuwa na kinyongo fulani kwa mtu, humsababishia kupanda kwa Shinikizo la Damu pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo. Hali hiyo, kwa mujibu wa utafiti huo, inaweza kuondolewa kwa mtu kuwa mwepesi wa kusamehe haraka.
Sita, kwa gharama yoyote, mtu anatakiwa kujiepusha na ugomvi wa aina yoyote ile. Kugombana na wengine kunaweza kumletea au kumsababishia mtu Mkazo mwingi. Mtu anapokuchokoza jitahidi kutulia, usimwage ugali kwa kuwa yeye kamwaga mboga. Inashauriwa kujitenga naye kwa kukaa faragha, hivyo kusuluhisha mambo kwa hekima na busara nyingi.
Saba, jipangie ratiba ya matumizi ya muda kwa kuandaa muda wa kutatua matatizo ya familia na ya kazini, kwa kutumia mbinu bora za makubaliano. Aidha, mtu anaweza akatunza muda wake wa kazi na familia kwa ufanisi hivyo kupunguza kiwango cha Mkazo kwake.
Nane, inampasa mtu ajitahidi kupunguza hali zitakazomwongezea Mkazo kadri awezavyo, kwa kutoruhusu hali zenye kuongeza Mkazo. Kwa mfano, kujiepusha kuwaza mambo mabaya yanayoweza kutokea na kuchota hisia zake.
Tisa ni kuhakikisha mwili mzima unatunzwa. Baada ya kazi nzito, jitahidi kuukanda mwili kwa maji ya uvuguvugu, kabla ya kula chakula. Mazoezi ya kutembea na kusikiliza muziki unaoifurahisha nafsi yako ni muhimu pia.
10, ni kuondokana na woga wa kuomba msaada kwa jamaa na marafiki au majirani.
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba kuzungumza na marafiki au watu wa familia kuhusu hali inayokupata, husaidia kuondoa ugonjwa wa Mkazo.
Hata hivyo, pamoja na njia zote hizo 10 rahisi, inashauriwa na wataalamu wa akili na mifumo ya miili kwamba endapo Mkazo na hali ya wasiwasi itaendelea, ni muhimu kutafuta msaada zaidi kwa Daktari, ikiwezekana upatiwe dawa za kutibu hali hiyo.
Wengi hawafahamu kuwa ni Viatu hatari
kwa afya ya miguu ya wanawake japo pia wapo wanaofahamu hilo ila
wanakaidi tu. ‘Mchuchumio’ ama viatu vyenye visigino virefu, ni mojawapo
ya vitu vinavyopendwa na baadhi ya wanawake mbalimbali, si katika
Tanzania bali dunia nzima.
Wataalamu wanaeleza kuwa viatu hivi
huharibu pingili za uti wa mgongo na huvunjavunja mifupa ya visigino.
Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa
wakipendelea viatu virefu. Kwa kiasi kikubwa wasichana wafupi, wamekuwa
wakipendelea kuvaa viatu virefu ili angalau na wao waonekane warefu
ingawa vinawatesa.
Kuna maelezo yanayosema kuwa viatu virefu
vinaharibu visigino na misuli ya miguu na kutengeneza vigimbi ambavyo
baadaye husababisha maumivu makali. Wasichana wengi wanafahamu
‘mchuchumio’ husababisha maumivu makali lakini je, ndiyo kutimiza usemi
wa ukitaka uzuri shurti udhurike? Kwa kawaida, urembo hauwezi
kusababisha maumivu, lakini kuvaa viatu virefu kuna athari kubwa.
Utafiti mbalimbali unaonesha kuwa viatu virefu havifai hata kidogo.
Kimsingi, uvaaji wa viatu virefu husababisha maumivu makali ya misuli ya
miguu pamoja na nyama za nyuma kwenye maungio ya magoti na enka.
Uharibifu ni mkubwa pia huweza kutokea ndani ya magoti kwa kuhamisha
maungio (dislocate). Kwa jinsi mhusika anapovaa viatu virefu kwa muda
mrefu, ndipo inaposababisha madhara ya muda mrefu.
Mbali na hayo,
vilevile, husababisha mwili kukosa usawa wakati wa kutembea, misuli ya
miguu kubana, kupoteza mwelekeo wa mwendo halisi na wakati mwingine
husababisha mhusika kuanguka na kumsababishia maumivu makali. Katika
uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la Journal of Applied Physiology,
Dk Cronin anasema wanawake wengi waliofanyiwa utafiti wamebainika
kutokuwa imara katika miguu yao, kupatwa na maumivu makali na kuharibiwa
misuli na enka ya mguu.
Naye Dk Orly Avitzur, Mganga Mshauri
kwenye kitongoji cha Tarrytown, New York, Marekani anasema kuwa alifanya
utafiti kwa wanawake wa zaidi ya miaka 40 kuwa hawawezi kuvaa viatu
virefu kwa kuwa miguu yao tayari imeharibiwa. Katika uchunguzi
uliochapishwa kwenye jarida la Journal of Applied Physiology, Dk Cronin
anasema wanawake wengi waliofanyiwa utafiti wamebainika kutokuwa imara
katika miguu yao, kupatwa na maumivu makali na kuharibiwa misuli na enka
ya mguu.
Mtaalamu wa Mifupa katika Hospitali ya TMJ, Dar es
Salaam, Dk Edemeza Machange alieleza kuwa matatizo ni makubwa kwa
mtumiaji wa viatu virefu na athari zaidi huwakumba wanawake wanene. “Ni
mbaya sana…kwa wanawake wanene haishauriwi watumie viatu virefu kwa kuwa
vitawaletea matatizo mengi katika miili yao,” anasema.
“Kwa
kawaida mtu anapoteza mwendo halisi, sasa kutotembea kwa mpangilio,
huharibu mfumo wa pingili za mgongo, hata kiuno na kusababisha maumivu
makali”. Anawashauri kinamama hasa wasichana, wafahamu kuwa pamoja na
kutaka urembo, lazima wajali afya zao kwa kuvaa viatu virefu katika
kipindi kifupi na zaidi ni kuangalia madhara kwa baadaye kuliko
kukimbilia kuvaa viatu virefu kwa ajili ya urembo.
Msukumo unaozidi nguvu za uvutano
kwa mara 80 hadi 100 unaweza kukufanya upoteze fahamu. Hata hivyo,
kigogota anaweza kuhimili msukumo unaozidi nguvu za uvutano kwa mara
1,200 hivi anapopigapiga mti kwa mdomo wake. Ndege huyo anafanyaje kazi
hiyo, bila kupoteza fahamu au hata kupata maumivu ya kichwa?
Fikiria hili:
Watafiti wamegundua sehemu nne za kichwa cha kigogota zinazofanya kichwa chake kiweze kuhimili mshtuko huo:
1. Ana mdomo wenye nguvu lakini unaonyumbulika
2. Ana kitu kinachoitwa hyoid kilichofanyizwa kwa mfupa na tishu inayoweza kutanuka kinachofunika fuvu la kichwa
3. Ana eneo fulani la mfupa ulio kama sifongo ndani ya fuvu
4. Ana nafasi ndogo kati ya fuvu na ubongo iliyo na umajimaji unaofanana na ule unaopatikana kwenye uti wa mgongo
Kila moja ya sehemu hizo huhimili
mshtuko, na kumwezesha kigogota kuugonga mti mara 22 hivi kwa sekunde
bila kuumiza ubongo wake.
Wakichochewa na muundo wa kichwa
cha kigogota, watafiti wametokeza kifaa fulani kinachoweza kuhimili
msukumo unaozidi nguvu za uvutano kwa mara 60,000. Huenda hilo
likawawezesha kutokeza vifaa bora zaidi kutia ndani, vile vinavyolinda
vifaa vya kurekodia jinsi ndege inavyoruka, ambavyo kwa sasa vinaweza
kuhimili msukumo unaozidi nguvu za uvutano kwa mara 1,000 tu.
Kim
Blackburn, injinia katika Chuo Kikuu cha Cranfield huko Uingereza,
anasema kwamba mambo ambayo yamegunduliwa kuhusu kichwa cha kigogota
yanatoa “mfano mzuri wa jinsi vitu vya asili vinavyoweza kutusaidia
kutokeza miundo tata na pia kutatua mambo ambayo hapo awali yalionekana
kuwa hayawezi kutatuliwa.”
Una maoni gani?
Kichwa cha kigogota kinachoweza kuhimili mshtuko kilijitokeza chenyewe?
● Madaktari wapasuaji huunganisha
mifupa ilivyovunjika kwa kutumia pini, mabati ya aina fulani, na skrubu,
lakini ni vigumu sana kutumia vifaa hivyo kuunganisha mifupa midogo.
Watafiti wametatizwa kwa muda mrefu jinsi wanavyoweza kutokeza gundi
inayoweza kunata ndani ya mwili wa mwanadamu ulio na umajimaji. Walipata
suluhisho kwa kuchunguza mnyoo anayeitwa sandcastle!
Fikiria hili:
Mnyoo
huyo hujenga makao yake chini ya maji kutokana na mchanga na makombe.
Kila chembe huunganishwa kwa kutumia gundi ambayo mnyoo huyo hutokeza
ndani ya tezi fulani iliyo kifuani mwake. Gundi hiyo inanata kuliko
gundi za kisasa zinazotengenezwa na wanadamu. Ina mchanganyiko fulani wa
protini ambazo zinapounganishwa zinafanya gundi hiyo ishikamane upesi
sana chini ya maji! Mnyoo huyo amesemekana kuwa mwashi stadi, na inafaa
sana kwamba anaitwa hivyo. Russell Stewart, wa Chuo Kikuu cha Utah,
anasema kwamba mnyama huyo mdogo amesuluhisha “tatizo tata sana kuhusu
gundi.”
Watafiti wametokeza gundi kama ya
mnyoo huyo ambayo inanata kwa nguvu zaidi kuliko hata ya mnyoo huyo.
Gundi ambayo mwishowe itatumiwa katika upasuaji inapaswa kuwa na uwezo
wa kuoza ili inapotumiwa kuunganisha mifupa iliyovunjika, iweze pia
kuyeyuka mfupa unapopona. Iwapo gundi hiyo itawasaidia wanadamu, bila
shaka itakuwa ugunduzi muhimu wa kitiba.
Una maoni gani?
Je, gundi ya pekee ya mnyoo anayeitwa sandcastle ilijitokeza yenyewe?
Au ilibuniwa?
Watafiti wanatumaini wataweza kurekebisha mifupa iliyovunjika bila kutumia vifaa vya chuma
1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.
2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.
3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.
4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.
5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.
6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.
7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.
8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi. Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).
9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k
10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.
11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya), Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).
12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.
13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.
14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.
15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.
16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.
17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).
18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.
19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.
20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.
21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.
22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.
24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.
24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).
25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.
26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.
Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.
Sababu zifuatazo zinaweza kuwa na ukweli mtupu; 1. Kushindwa kuamua haraka fursa zinapojitokeza kwao 2. Fursa kali Zikitokea wanaziona kama ni uongo na utapeli wa mjini 3. Kung'ang'ania kuajiriwa hata kama ajira hiyo hailipi 4. Kudhania unajua sana hivyo huoni jipya la kujifunza 5. Kukosa ujasiri wa kuanza. Unapanga mwezi huu au mwaka huu ntafanya hili au lile. Lakini mwaka unaisha hujaanza!!! 6. Kutokuwa na ndoto ya kiasi cha pesa unazotaka kwa siku, kwa wiki mwezi au mwaka. Unataka shs ngapi kwa siku? Wiki? Mwezi? Mwaka? Kwa nini unataka kiasi hicho? Matumizi yako ya lazima ni yapi? Ya starehe zako ni yapi? 7. Kununua vitu vya bei kubwa sana na visivyo na tija yoyote katika kuongeza kipato chako. 8. Kuwaza kwamba maendeleo yanapatikana uzeeni na siyo ujanani? Eti kumiliki mamilioni ya pesa mpaka uwe mzee kama Reginald Mengi vile. 9. Kufikiri eti huwezi kufanikiwa kuwa na fedha kuubwa mpaka uwe freemason au fisadi. Ujinga. 10. Kuwa na wategemezi kibao nyumbani kwako wakati kipato chenyewe kinatosha kula watu 2 tu kwa mwezi. Hatari!! 11. Kusubiri siku utakayopata pesa nyingi sana eti ndipo utafanya biashara hii au ile! Utasubiri sana. 12. Kutokuweka akiba yoyote kwa malengo ya maendeleo ya watoto na wajukuu zao. 13. Kufikiria kuwa kuna siku utapata msaada kutoka kwa wafadhili, serikali au wazungu au washikaji zako. Utangoja sana. 14. Kubadilisha mshahara wako au kipato chako kuwa mali ya ukoo mzima. Kila mtu kwenye ukoo wenu anakuomba pesa na wewe unampatia. Usimpe mtu samaki mfundishe kuvua samaki naye hatakuomba tena samaki. Usimpatie maziwa ndugu yako mfundishe kufuga ng'ombe wa maziwa. Mpendwa wewe umeguswa na sababu ipi ktk hizo? Nakutakia Februari Njema?
TUNASAFIRI kwa ndege katikati ya
mawingu mazito na hivyo hatuwezi kuona chochote. Kwa ghafula, ndege yetu
inatoka kwenye mawingu na chini yetu tunaona eneo la Aktiki
lililofunikwa kwa theluji. Mandhari hiyo inapendeza kama nini!
Tunapotazama mabamba ya barafu, mikono ya bahari, na milima iliyofunikwa
kwa theluji, tunastaajabu. Ni kana kwamba eneo hilo lisilo na mimea
lililofunikwa kwa theluji na barafu halina mwisho. Tumekuja kutembelea
Svalbard, visiwa vilivyo karibu na Ncha ya Kaskazini, kati ya digrii 74
za latitudo na digrii 81 kuelekea kaskazini!
Jina Svalbard, linalomaanisha “Pwani
Baridi,” lilionekana kwa mara ya kwanza mnamo 1194 katika maandishi ya
Waiceland. Lakini eneo hilo “liligunduliwa” miaka 400 baadaye, mnamo
1596 na hivyo likajulikana ulimwenguni pote. Mwaka huo kikundi cha
wagunduzi Waholanzi kikiongozwa na Willem Barents kilikuwa kikisafiri
kwa meli kuelekea kaskazini wakati ambapo mmoja kati yao aliona kwenye
upeo wa macho yake eneo lisilojulikana, safu ya milima yenye ncha.
Wagunduzi hao walikuwa kwenye eneo la kaskazini-magharibi mwa Svalbard,
naye Barents aliita eneo hilo “Spitsbergen” jina linalomaanisha “Milima
Iliyochongoka.” Hilo ndilo jina la kisiwa kikubwa zaidi kati ya visiwa
hivyo. Ugunduzi wa Barents ulianzisha kipindi chenye utendaji mwingi
huko Svalbard. Utendaji huo ulitia ndani kuvua nyangumi, sili,
kuwakamata wanyama, kugundua maeneo mapya, kuchimba makaa ya mawe,
kufanya utafiti wa kisayansi, na utalii. Kwa miaka mingi, nchi kadhaa
zimeshiriki katika utendaji huo, lakini kuanzia mwaka wa 1925 visiwa
hivyo vimekuwa chini ya utawala wa Norway.