Photo Credit By: https://en.wikipedia.org/ |
Je, Ni Kazi ya Ubunifu?
● Madaktari wapasuaji huunganisha
mifupa ilivyovunjika kwa kutumia pini, mabati ya aina fulani, na skrubu,
lakini ni vigumu sana kutumia vifaa hivyo kuunganisha mifupa midogo.
Watafiti wametatizwa kwa muda mrefu jinsi wanavyoweza kutokeza gundi
inayoweza kunata ndani ya mwili wa mwanadamu ulio na umajimaji. Walipata
suluhisho kwa kuchunguza mnyoo anayeitwa sandcastle!
Fikiria hili:
Mnyoo
huyo hujenga makao yake chini ya maji kutokana na mchanga na makombe.
Kila chembe huunganishwa kwa kutumia gundi ambayo mnyoo huyo hutokeza
ndani ya tezi fulani iliyo kifuani mwake. Gundi hiyo inanata kuliko
gundi za kisasa zinazotengenezwa na wanadamu. Ina mchanganyiko fulani wa
protini ambazo zinapounganishwa zinafanya gundi hiyo ishikamane upesi
sana chini ya maji! Mnyoo huyo amesemekana kuwa mwashi stadi, na inafaa
sana kwamba anaitwa hivyo. Russell Stewart, wa Chuo Kikuu cha Utah,
anasema kwamba mnyama huyo mdogo amesuluhisha “tatizo tata sana kuhusu
gundi.”
Watafiti wametokeza gundi kama ya
mnyoo huyo ambayo inanata kwa nguvu zaidi kuliko hata ya mnyoo huyo.
Gundi ambayo mwishowe itatumiwa katika upasuaji inapaswa kuwa na uwezo
wa kuoza ili inapotumiwa kuunganisha mifupa iliyovunjika, iweze pia
kuyeyuka mfupa unapopona. Iwapo gundi hiyo itawasaidia wanadamu, bila
shaka itakuwa ugunduzi muhimu wa kitiba.
Una maoni gani?
Je, gundi ya pekee ya mnyoo anayeitwa sandcastle ilijitokeza yenyewe?
Au ilibuniwa?
Watafiti wanatumaini wataweza kurekebisha mifupa iliyovunjika bila kutumia vifaa vya chuma
Sandcastle worm: © Peter J. Bryant, University of California, Irvine
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni