Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Septemba 06, 2016

UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME:01. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshitua.

02. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendae.

03. Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajika.

04. Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiri.

05. Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaume.

06. Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kesho tena.

07. Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maisha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maisha.

08. Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizwe.

09. Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushiba.

10. Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake.. baadae hugombana nae yakishamrudia mwenyewe kwa siku 2 tu.

Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamke kama kuna nyingine ziongezee katika comments hapo chini ili kupeana elimu na maarifa kuhusu saikolojia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni