Leo kampuni ya reli Tanzania TRL kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo CHAMA CHA KUTETEA ABIRIA (Chakua), kwa pamoja tumezinduwa treni ya abiria itakayofanya safari zake kuanzia stesheni ya dsm kwenda pugu.
Katibu idara ya reli,, Godfrey Mali, kulia,, Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki, Wilson Sylvester na muheshimiwa waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa wakiwa kwenye uzinduzi wa treni ya abiria ya kwenda pugu leo.
Katika Uzinduzi hua Chama Cha Kutetea Abiria (Chakua) iliwakilishwa na mkurugenzi wa kanda ya mashariki, Wilson na katibu idara ya reli, Godfrey Mali.
Pongezi kwa Katibu mkuu idara ya reli, hiyo ni kazi nzuri sana.
Ni safari ambayo itaanza saa 10:45 alfajiri kwenda pugu tripu ya kwanza na tripu ya mwisho 4:20 asubuhi hiyo routi ya asubuhi.
Routi
nyingine itaanza saa 09 :55 alasiri kuekea pugu mwisho wa routi za
jioni ni saa 4:15 usiku. Nauli kwa mkubwa Tsh 400 mwanafunzi Tsh 100.
Hizi zitakuwa nauli za majaribio mpaka hapo sumatra watakapotoa muongozo
wa nauli.
Uzinduzi
wa treni ya abiria ya kwenda Gongolamboto Pugu tayari umezindiliwa na
walielekea pugu viongozi mbali mbali akiwemo waziri wa uchukuzi
pia mea wa jiji halikadhalika mkuu wa mkoa,, na viongozi wa shirika la
reli
Tanzania.
Kama unavyoona kwenye Picha hapo Juu Mh.Makame Mbarawa akiwa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda.
Kesho (Jumatano) Chakua itafanya mazungumzo na mkurugenzi mtendaji wa
shirika la reli Tanzania TRL ofisini kwake makao makuu ya reli
tanzania kuanzia saa tisa kamili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni