Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Septemba 07, 2016

SHUKRANI MUNGU KWA ZAWADI HII YA MAISHA KTK SIKU YANGU YA KUZALIWA

LEO TAREHE 7 SEPTEMBA NI MAPENZI YA MUNGU KUNIFIKISHA KATIKA TAREHE NA MWEZI NILIOZALIWA NA SASA NIMETIMIZIA MIAKA ZAIDI. NICHUKUE FURSA HII KUWAKUMBUKA KWA KUWASHUKURU WALIOTENDA YALIYOTENDEKA.

Si mnakumbuka mapitio ya udogoni, kucheza pamoja, kukaa pamoja katika shida na raha wakati mwingine kupigana pale tulipoudhiana, ila tulisameheana kwa vile tulifundishwa upendo. Mara zote tuliamini kwamba japo tulizaliwa katika hali ya umasikini ila hatutakufa masikini, kwa vile si lengo la Mungu watu wake wataabike katika dhiki.


Kwa watoto yatima wote na wale waishio katika mazingira magumu;


..Nawapenda sana na daima nakuwa na amani sana kuwaona mkitabasamu na kufurahi, bila kujali matatizo mliyonayo maishani. Sio lengo la Mungu mteseke kwa kuwakosa wazazi ama ndugu mliowapenda na kuwategemea kwa namna moja ama nyingine. Mungu si mwanadamu hata tuseme anakosea kufanya maamuzi..ishini mkimtegemea Mwenyezi Mungu, baba wa mbinguni ajuaye idadi ya nywele kichwani nina hakika ipo siku majonzi yenu yatageuka kuwa Furaha..hamtanung'unika tena..nawapenda sana!


Nichukue fursa ya awali kumshukuru Mungu baba wa mbinguni kwa kunifanya moja kati ya viumbe alivyoviumba chini ya jua ..ni kwa neema yake tu kuwepo kwangu hadi leo hii kwani sina haki kuliko wale wote waliotangulia umautini. Namshukuru zaidi kwa kunipa ufahamu wa kuelewa mambo..asante Mungu kwa kunijaalia karama nyingi mbalimbali..naomba uniwezeshe kuzitumia vizuri kwa wengine!
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani..nawapenda sana na daima napenda kuona mnaishi maisha ya ujana, yenye kila aina ya furaha..narudia kusema nawapenda sana na kuna kitu nitafanya kwa ajili yenu! 


Shukrani za kipekee ziwafikie walimu wangu tangu shule ya msingi hadi wakufunzi wa chuo kwa juhudi kubwa walizofanya za kunifuta ujinga..hakika nisingakuwa nilipo kama si jitihada zenu! Mungu akujaalieni kheri popote mlipo!


Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisiposhukuru majirani na waumini wenzangu kwa kuwa mentor, influencer na watu mlioni-jengea hekima ya hali ya juu! Niwaombe radhi wale tuliocharuana kwa sababu moja ama nyingine pale tulipopishana!


Wapo pia ambao siwezi kuwaacha japo majina ni mengi ila kazi yao ilinifanya niwaone kuwa role model wangu katika vipindi vya radio walivyokuwa wanarusha kupitia SAUTI YA UJERUMA, BBC SWAHILI, SAUTI YA AMERIKA, RADIO TANZANIA DSM, KBC SWAHILI NA ENGLISH SERVICE na nyingine nyiiingi popote zilipo. 


Mungu awajaalie miaka 900 kama enzi za Adamu na Hawa bila kujali mapungufu mliyonayo! Nyote mmechangia kupata zawadi nzuri sana ya maisha tangu kuzaliwa, kukua kwangu hadi kufikia leo ninapotimiza umri huu nilionao.

MUNGU WEWE NI MUWEZA WA VYOTE HAKIKA UNATUPENDA SANA. 

p>

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni