Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Septemba 04, 2012

ONYO LA KUTISHA..!!





Onyo la kutisha mno la adhabu linaloweza kupatikana mahali po pote katika Biblia limo katika Ufunuo 14:9,10: "Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa [alama] katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye ATAKUNYWA katika mvinyo ya GHADHABU YA MUNGU iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo."

Maelezo haya yanaogofya mno na hayafanani kabisa na mafungu mengine yanayoielezea tabia ya Mungu ilivyo, hata tunajikunja kwa hofu. Lakini yanaonyesha wazi kipindi kile ambacho rehema ya Mungu itakapoondolewa kwa wale ambao wanaendelea daima kuikataa mamlaka ya mbinguni. Litakuwa ni tendo lisilo na kifani kwa upande wa Mungu katika uhusiano wake na jamii ya kibinadamu. Kwa karibu

miaka 6000 hukumu zake za adhabu juu ya watu walio waovu sana zimechanganywa na rehema Yake. Lakini sasa uovu unafikia kiwango ambacho kinafanya iwe lazima kwa Mungu kuingilia kati, na kukidhihirisha kiwango cha usaliti wa mwanadamu dhidi ya Serikali ya Mungu.

Hapa ndipo tunataka kujua habari zaidi juu ya dhambi ile inayomfanya Mungu kutenda tendo hilo la ajabu [geni] la kuwaadhibu [waovu] kwa moto. Angalia kwamba jambo hili la mwisho linahusu utii wa uongo kwa mamlaka ile ya Mnyama, ambayo mara nyingi inatajwa katika unabii wa Biblia. Hatimaye dunia hii itasimama

ikiwa imegawanyika katika makambi mawili: 

01. Wale wanaomsujudu Mungu wa kweli na 

02. Wale wanaomsujudu Mnyama yule wa Ufunuo 13. 

Lakini ni jambo gani linaloleta mgawanyo huo mkubwa wa watu wa dunia hii? Baada ya kueleza ajali itakayowapata waabudu hao wa uongo katika Ufunuo 14:9-11, Yohana analo hili la kusema katika fungu lile linalofuata: "HAPA NDIPO PENYE SUBIRA YA WATAKATIFU, HAO WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU, NA IMANI YA YESU." Hapa tunaona tofauti ya kushangaza kati ya wale wanaomfuata yule Mnyama na wale wanaomfuata Mwana-Kondoo.


Angalia, tafadhali, ya kwamba suala linalohusika linazunguka juu ya kuzishika amri za Mungu. Wale ambao hawana alama ya Mnyama wanasemwa ya kuwa wanazitii amri hizo [za Mungu], na wale waliobaki wanateseka kwa ghadhabu ya Mungu. Jambo hili linakubaliana kabisa na usemi wa Paulo katika Warumi 16:16, "Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii,

mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki."

Wajibu wa hali ya juu unahesabika kwa tendo hili la UTII. Mwishowe, sehemu kubwa ya wakazi wa dunia hii wataikubali mamlaka hii ya bandia ya serikali ya Mpinga Kristo, kwa KUZIASI AMRI ZILE KUU KUMI za Mungu. Rafiki zangu, kila mtu mmoja mmoja atakuwa upande mmoja au mwingine. Biblia inaeleza kwa wazi sana ya kwamba UZIMA au MAUTI utategemea UAMUZI WA MWISHO kuhusu Mnyama huyu wa Ufunuo 13.


Ni ajabu kwamba wanathiolojia wa siku hizi wamepuuzia kabisa UJUMBE HUU WA ONYO wa Ufunuo 14, unaohusu ile Alama ya Mnyama. Shauku ya watu wengi imeharibiwa na mvuto wa WACHUNGAJI ambao hawakutaka kuyachukulia maneno haya ya unabii wa Yohana kwa uzito wake. Mara nyingi wanautupilia mbali [unabii huu] kana kwamba ni waraka wenye utata, usiokuwa na maana, ambao ulilihusu

tatizo la mahali pale katika kanisa lile la mwanzo. 

Kwa sababu fulani kitabu hiki kinachoitwa Ufunuo kinahesabika kama vile ni kitabu kilichofungwa [kisichoweza kueleweka], badala ya ukweli wake wa wazi uliofunuliwa [unaoeleweka] kama jina lake linavyomaanisha. Lakini tafadhali zingatia ya kwamba ahadi imetolewa kwa wale wanaoitafuta kweli iliyomo ndani ya kitabu hiki cha ajabu: "Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu." Ufunuo 1:3.


Kabla ya kukichunguza sana kisa hiki kilicho wazi cha Yohana kuhusu pambano lile la mwisho kati ya Kristo na Shetani, hebu na tutumie muda fulani kuwachambua hao wanaopambana katika vita hii. Ni lini na kwa jinsi gani [pambano hili] lilianza, na kwa jinsi gani litafikia mwisho wake?


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni