Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Januari 28, 2014

RAIA WALAANI JARIBIO LA AL-SHABAAB KUHUSU INTERNET

Wasomali wanaperuzi intaneti katika mkahawa mjini Mogadishu. [Na Majid Ahmed/Sabahi]

Jaribio la al-Shabaab kupiga marufuku mkonga wa mawasiliano na huduma za mtandao wa intaneti limekumbana na hasira kali kutoka kwa raia wa Somalia na kuchochea onyo kali kutoka kwa serikali.
Katika taarifa iliyochapishwa siku ya tarehe 8 Januari kwenye mtandao wa Somalimemo, al-Shabaab ilitangaza kupiga marufuku intaneti wakiamuru kampuni za simu kuacha kutoa huduma ya intaneti ndani ya siku 15.

Taarifa hiyp pia ilionya kwamba kampuni na watu wasiofuata amri hiyo watachukuliwa kama maadui na kuadhibiwa chini ya sharia.
Al-Shabaab ilihalalisha tangazo lake la marufuku kwa kusema kwamba mashirika ya kijasusi wa Kimagharibi, hasa mashirika ya Marekani na Uingereza, yanatumia intaneti kukusanya taarifa dhidi ya mujahidina.

"Intaneti ya kwenye simu ni hatari kwa kila Muislamu kutumia huduma hiyo [kwani] inamruhusu adui kujua harakati za watu na kukusanya taarifa," lilisema tamko hilo.

"Intaneti ya kwenye simu ni hatari zaidi kwa usalama wa Waislamu wanaopigana na maadui waliokuja, kwa sababu inaongeza fursa ya majasusi [wao] kusambaza taarifa za kijasusi kuhusiana na mujahidina kwa mashirika ya kijasusi yaliyopo nchini," ilisema.

Taarifa hiyo ya al-Shabaab ilisema pia intaneti kwenye simu ya mkononi ilikuwa hatari kwa watoto na vijana ambao wanapata na kusambaza mambo yanayokwenda kinyume na misingi ya Uislamu. Kuendelea kutumia intaneti kwa vijana kutapelekea wawe na "tabia mbaya, ukosefu wa elimu na kupoteza wakati," ilisema taarifa hiyo.

Al-Shabaab iko kwenye shinikizo inayoongezeka

Al-Shabaab ina hofu kubwa na inayoongezeka juu ya huduma za kisasa, ambazo zimelipelekea kundi hilo kufanya uamuzi wa kiholela sana, alisema Abdi Aynte, mkurugenzi wa taasisi ya sera ya Heritage Institute for Policy Studies mjini Mogadishu.

"Wanaogopa kwamba simu zenye huduma ya intaneti zitatumika kuwasiliana na mashirika ya kijasusi ya kimataifa ambayo yanawawinda wapiganaji wa al-Shabaab, hasa ndege zisizo na rubani, ambazo zimepunguza kwa kiasi kikubwa pirika za viongozi wa al-Shabaab," aliiambia Sabahi.

Aynte alisema sababu nyengine ya uamuzi huo wa al-Shabaab ilikuwa ni kampeni yake ya kuwazuia wananchi kupata habari za kilimwengu.

Katika siku za karibuni, al-Shabaab imepiga marufuku upatikanaji wa taarifa muhimu kwenye maeneo inayoyadhibiti, kama vile marufuku yake dhidi ya kuangalia televisheni na unyanyasaji wake dhidi ya raia wanaotumia simu za kisasa.

"Wanataka kuwazuia watu kuishi kwenye ardhi wanazozikalia kuzungumzia ugumu wanaokabiliana nao na kuuwambia ulimwengu juu ya dhila ambayo [al-Shabaab] wanawasabishia," alisema Aynte. "Intaneti inawapa watu uhuru wa kupata habari na al-Shabaab iko dhidi ya uhuru."

Alisema inawezekana pia kwamba al-Shabaab inataka kuchopoa fedha kutoka kwenye kampuni za simu kwa mabadilishano ya kuondosha marufuku ya intaneti.

Aynte alisema hafikirii kuwa marufuku hiyo itatekelezwa kwenye maeneo yasiyo chini ya udhibiti wa al-Shabaab.

Mwezi Novemba, kampuni ya simu ya Liquid Telecommunications ilitangaza mkonga wake wa kwanza wa mawasiliano ndani ya Somalia. Mkonga huo unavuka mpaka wa Kenya na Somalia, na kisha kuunganisha na mtandao wa Hormuud Telekom, unaoongeza kasi ya intaneti katika eneo lote la kusini na kati ya Somalia.

Abdirahman Yusuf al-Adala, mkurugenzi wa idara ya vyombo vya habari katika Wizara ya Habari, Posta na Mawasiliano ya Simu, alisema kwamba jaribio la al-Shabaab kuzuia upatikanaji wa intaneti ya njia ya mkonga litashindwa kwa sababu serikali ilileta huduma hii nchini Somalia na itailinda. 

Hata hivyo, alisema kuwa vitisho vya al-Shabaab vingeweza kuathiri maisha ya watu wanaotumia intaneti jongevu na wanaoishi katika udhibiti wa wanamgambo. 

"Watu wanatumia intaneti kwa ajili ya biashara, elimu, kupata habari, na watayakosa hayo. Tatizo jengine ambalo litasababishwa na suala hili ukosefu wa ajira ambao watu wanaofanyakazi kama watoaji hduma za intaneti," al-Adala aliiambia Sabahi. "Makampuni yana chaguo la kupoteza biashara zao na kwa hivyo kukabiliana na kufilisika, au kudharau amri ya al-Shabaab na kugeuka kuwa lengo la mashambulizi holela ya al-Shabaab." 

Katika kujibu jaribio la al-Shabaab la kupiga marufuku intaneti, Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa alisema itachukua hatua za kupambana na mbinu mpya za al-Shabaab. 

"Wasomali, kama walivyo watu wengine popote pale, wanatuia intaneti kwa ajili ya elimu na kuifikia jamii ya kimataifa ili kupata habari za dunia. Hatutaruhusu wananchi wetu kunyimwa kupata intaneti na kutumia smartphones," Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa Abdikarim Hussein Guled alisema hapo tarehe 11 Januari.

"Serikali ya Somalia itafanya kazi na makampuni yote ya simu ili kuhakikisha uhuru wa kutoa intaneti kwa wananchi wetu, na serikali litafanya kila juhudi katika kulinda maslahi ya umma," alisema. 

Guled aliyaonya makampuni ya mawasiliano ya simu dhidi ya kufanya kazi na magaidi na alisema kwamba serikali ina dhamana ya kuwalinda wananchi wake. 

Makampuni ya mawasliano ya simu ambayo yanatoa huduma jongevu za intaneti hayajatoa kauli yoyote juu ya marufuku ya al-Shabaab na hayakujibu maombi ya Sabahi ya kutoa maoni.

Wananchi wapinga vikali marufuku ya intaneti ya al-Shabaab

Ahmed Mohamud, mwandishi wa habari mwenye umri wa miaka 27 anayefanya kazi na kituo cha redio chenye makao mjini Mogadishu, alisema kuwa alikuwa na matumaini kwamba upatikanaji wa intaneti nchini Somalia utaboreshwa kwa kuunganishwa na mkonga.

"Inanichukua muda mrefu kila mara ninapotaka kupata kitu kidogo chochote kile kutoka intaneti, lakini mkonga ni intaneti ya kasi kubwa sana ambayo inakuwezesha kupata kiasi kikubwa [cha data] kwa muda mdogo sana," aliiambia Sabahi.

Mohamud alisema kwamba njia pekee kwa watu wanaoishi katika maeneo yanayodhbitiwa na al-Shabaab kuwasiliana na dunia na kuwapa taarifa wengine ni kupitia intaneti jongevu. Lakini sasa, alisema, "watakuwa viziwi na vipofu." 

Abdi Ahmed Maalin, mkazi wa kitongoji cha Taleh cha Mogadishu mwenye umri wa miaka 27, alisema kuwa marufuku ya intaneti ya al-Shabaab itakuwa ni ushahidi zaidi kwamba kikundi hiki kiko kinyume na maendeleo na kuboresha maisha ya watu. 

Maalin anayo digirii ya kwanza katika sayansi ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Mogadishu na alikuwa akijitayarisha kujiandikisha na programu ya diplomasia ya kimataifa mtandaoni katika Chuo Kikuu cha Kampala.

"Uamuzi wa al-Shabaab inamaanisha kuwa hakuna elimu kwa ajili yangu," alisema. "Wanasema wanapambana dhidi ya adui, lakini ukweli ni kwamba wao ndio maadui." 

Maalin alisema kwamba matendo yanayoongezeka kwa matendo makali ya al-Shabaab yanatoa wito kwa umma kupambana kukishinda kikundi hiki. 

"Hapo awali tulijua kuwa waliwagawa watu katika makundi mawili: kikundi kinachoishi chini yao ambacho wanakinyanyasa na kikundi ambacho wamekipa jina la makafiri na wanakiuwa," alisema. "Kile wanachofanya sasa kuyafanya watu walio hai wawe wamekufa." 

"Je, tunawasubiri waidai kioa familia itoe mtu mmoja wamle? Hiki ni kikundi kidogo, kwa hivyo tukivamie mara ili tuweze kujikomboa wenyewe dhidi yao," Maalin alisema. "Hatuwezi kusubiri kwa hatua za kijeshi." 

CHANZO: http://sabahionline.com

Jumatatu, Januari 27, 2014

MASHAMBULIZI NA USALAMA WA KOMPYUTA

Picha kwa hisani ya www.cybersecurepakistan.com


Hebu wazia kundi la wahalifu wenye ustadi wa kutumia kompyuta wakitumia Intaneti kuongoza mitandao ya kompyuta walizoteka nyara. Kompyuta hizo zinazojulikana kama botnets (mitandao ya roboti), zinatoa habari za siri zenye madhara zinazolenga taifa fulani. Baada ya dakika chache, Tovuti za kijeshi, kifedha, na kibiashara za taifa hilo zinaacha kufanya kazi. Mashine za benki za kutolea pesa (ATM) pamoja na mitandao ya simu inashindwa kufanya kazi. Usafiri wa ndege unakatizwa na kompyuta pamoja na mifumo ya usalama katika kituo cha kutokeza nguvu za nyuklia inavurugwa. Watu wangetendaje? Wewe ungefanya nini?
Huenda tukio hilo likaonekana kuwa lisilo halisi. Lakini kulingana na Richard A. Clarke, aliyekuwa Msimamizi wa Kitaifa wa Usalama, Ulinzi wa Miundo-Msingi, na Kupambana na Ugaidi nchini Marekani, jambo kama hilo linaweza kufanyika kihalisi. Isitoshe, tayari kumekuwa na mashambulizi kupitia kompyuta Huenda hata wewe umewahi kushambuliwa.

Kwa nini mtu awashambulie wengine kupitia kompyuta? Mashambulizi hayo hufanywaje? Na kwa kuwa ni kawaida kwa mashambulizi hayo kumlenga mtu mmojammoja, unaweza kujilindaje unapotumia Intaneti?

Uwanja wa Vita Kwenye Kompyuta

Kuna sababu kadhaa zinazowafanya watu wawashambulie wengine kupitia kompyuta. Kwa mfano, magaidi au serikali zinaweza kupenya kwenye mitandao ya kompyuta ya maadui wao ili waibe siri au waharibu vifaa vinavyoongozwa na mitandao hiyo. Katika mwaka wa 2010, Waziri Msaidizi wa Ulinzi wa Marekani William J. Lynn wa Tatu alisema kwamba “maadui” wa kigeni walikuwa wamepenya mara nyingi kwenye mitandao ya kompyuta iliyo na habari za siri za Marekani na kuiba “maelfu ya mafaili . . . kutia ndani maagizo ya kutengenezea silaha, habari kuhusu mipango ya kijeshi, na habari za upelelezi.”—Ona sanduku (LINK HAPO MBELE) “Mashambulizi ya Hivi Karibuni Kupitia Kompyuta.”

Wahalifu wanaotumia kompyuta hutumia njia sawa na hizo kuiba habari za kitaaluma au za kifedha kutoka kwa mitandao ya kompyuta ya makampuni na hata kompyuta za watu binafsi. Wahalifu hupata mabilioni ya dola kila mwaka kupitia biashara za ulaghai zinazofanywa kwenye mitandao.

Pia, wahalifu hao wameunganisha kompyuta nyingi sana walizoteka nyara ili waweze kutekeleza mashambulizi yao. Katika mwaka wa 2009, kampuni moja inayoshughulika na usalama wa intaneti iligundua kwamba kundi moja la “wahalifu” lilikuwa likidhibiti kisiri karibu kompyuta milioni mbili kotekote ulimwenguni, nyingi zikiwa ni za watu binafsi. Ripoti ya karibuni ya Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) linakadiria kwamba kompyuta 1 kati ya 3 zilizounganishwa kwenye Intaneti inadhibitiwa kisiri na mhalifu fulani. Namna gani kuhusu kompyuta yako? Je, mtu fulani anaweza kuidhibiti bila wewe kujua?

Maadui Wanaoshambulia Kimyakimya

Wazia tukio hili. Mhalifu fulani anasambaza programu fulani yenye madhara kupitia Intaneti. Programu hiyo inapoingia katika kompyuta yako, inapenya ndani ya programu inayolinda kompyuta yako. Programu hiyo yenye madhara inapopata eneo ambalo halijalindwa vizuri, inapenya ndani hata zaidi na kutafuta-tafuta habari muhimu katika kompyuta yote.

 Kisha programu hiyo inaweza kubadilisha au kufuta mafaili yaliyo kwenye kompyuta yako, na inajituma yenyewe kama barua pepe kwenye kompyuta zingine, au kumtumia mhalifu huyo neno lako la siri la utambulisho, habari za kifedha, au habari nyingine za siri zinazokuhusu.

Wahalifu hao wanaweza kukufanya uingize virusi kwenye kompyuta yako mwenyewe! Jinsi gani? Unaweza kufanya hivyo kwa kufungua barua-pepe inayoonekana kuwa ya kawaida tu, kwa kubonyeza kiunganishi cha Tovuti fulani, kupakua na kuunganisha programu ya bure ya kompyuta, kuingiza kifaa cha kuhifadhi habari kilicho na virusi katika kompyuta yako, au tu kutembelea Tovuti yenye kutiliwa shaka. Mambo yote hayo yanaweza kuingiza programu yenye madhara kwenye kompyuta yako na kuifanya idhibitiwe kisiri na mhalifu.

Unaweza kujuaje ikiwa kompyuta yako imeshambuliwa? Kwa kweli inaweza kuwa vigumu kugundua. Huenda kompyuta au Intaneti ikafanya kazi polepole sana, au programu zisitende kwa njia ya kawaida, au visanduku vijitokeze ghafula vyenye ujumbe unaokuomba uunganishe programu fulani, au kompyuta yako itende kwa njia isiyo ya kawaida. Ukiona mojawapo ya dalili hizo, mwombe mtaalamu wa kompyuta achunguze kompyuta yako.

‘Fikiria Hatua Zako’

Kadiri mataifa na watu mmoja-mmoja wanavyozidi kutegemea teknolojia ya kompyuta, ndivyo inavyotarajiwa kuwa mashambulizi kupitia kompyuta yataongezeka. Kwa sababu hiyo, mataifa mengi yanajitahidi sana kuboresha mbinu za kulinda kompyuta zao, na mataifa mengine yanapima uwezo wa mitandao yao ya kompyuta ili kuona ikiwa inaweza kustahimili mashambulizi. Lakini licha ya jitihada hizo, Steven Chabinsky, mtaalamu wa cheo cha juu wa usalama wa kompyuta wa Shirika la Upelelezi la Marekani anasema kwamba “adui aliyeazimia kabisa, hawezi kamwe—kamwe—kushindwa kupenya mfumo hususa anaolenga iwapo atakuwa na wakati wa kutosha, kichocheo, na pesa.”

Unaweza kufanya nini ili ujilinde unapotumia Intaneti? 

Ingawa huenda usiweze kujilinda kabisa unapotumia Intaneti, unaweza kuchukua hatua zifaazo ili kufanya kompyuta yako iwe salama zaidi. (Ona sanduku “Jilinde!”) Biblia inasema: “Mtu mwerevu huzifikiria hatua zake.” (Methali 14:15) Kwa kweli hilo ni shauri lenye hekima unapotumia Intaneti!


Mashambulizi kupitia kompyuta yamekusudiwa hasa kubadilisha, kukatiza, au kuharibu kabisa mifumo ya kompyuta au mitandao au habari au programu ambazo kompyuta huhifadhi au kusambaza.—Baraza la Kitaifa la Utafiti la Marekani linaeleza.

Katika mwaka wa 2011, wahalifu wa kutumia kompyuta wangeweza kutumia zaidi ya udhaifu 45,000 unaojulikana ili waweze kupenya katika kompyuta nyingine. Kwa kutumia udhaifu huo, wahalifu hao wanaweza kuingiza programu yenye madhara (malware) katika kompyuta za watu binafsi bila watu hao kujua.


Wahalifu wa kutumia kompyuta wameunganisha kompyuta nyingi sana walizoteka nyara. Kulingana na shirika la OECD, kompyuta 1 kati ya 3 zilizounganishwa kwenye Intaneti, inadhibitiwa kisiri na mhalifu fulani


MASHAMBULIZI YA HIVI KARIBUNI KUPITIA KOMPYUTA

  2003: Programu ya kompyuta yenye madhara inayoitwa Slammer ilisambaa haraka sana kwenye Intaneti na kushambulia kompyuta 75,000 hivi kwa dakika kumi tu. Utendaji wa Intaneti ukawa wa polepole sana, Tovuti zikaacha kufanya kazi, mashine za benki za kutolea pesa (ATM) zikashindwa kufanya kazi, usafiri wa ndege ukakatizwa, na kompyuta pamoja na mifumo ya usalama katika kituo cha kutokeza nguvu za nyuklia ikavurugwa.

  2007: Mfululizo wa mashambulizi kupitia kompyuta ulilenga Estonia na kuathiri mifumo ya serikali hiyo, vyombo vya habari, na hata benki. Mengi ya mashambulizi hayo yaliyotoka kwenye mifumo ya kompyuta zilizotekwa nyara (botnets) yaliathiri kompyuta zaidi ya milioni moja zilizoshambuliwa katika nchi 75 kwa kuzifanya zitume ujumbe mwingi wa uwongo wa kuomba habari.

  2010: Programu ya kompyuta yenye madhara na tata sana inayoitwa Stuxnet ilishambulia mifumo inayoendesha kituo cha kutokeza nguvu za nyuklia nchini Iran.


Programu za kompyuta zenye madhara hujinakili zenyewe kutoka kompyuta moja hadi nyingine kupitia Intaneti na programu za aina hiyo hupewa majina kama vile Slammer.

JILINDE!

 1. Weka programu za kuzuia virusi (antivirus), programu za kutambua programu za upelelezi (spyware-detection), na mfumo wa ulinzi (firewall) katika kompyuta yako. Hakikisha kwamba programu hizo pamoja na programu kuu ya kuendesha kompyuta yako inaboreshwa kwa ukawaida.

 2. Fikiria kwa uzito kabla ya kufungua viunganishi (links) au viambatanisho (attachments) vinavyotumwa kwenye barua-pepe au ujumbe wa haraka—hata ule unaotoka kwa marafiki. Jihadhari hasa ikiwa ujumbe huo unatoka kwa mtu usiyemfahamu na unaomba habari za kibinafsi au neno la siri.

 3. Usinakili au kutendesha programu za kompyuta kutoka katika vyanzo usivyovijua.

 4. Tumia neno ya siri la utambulisho lenye angalau herufi nane na utie ndani namba na ishara kadhaa, na uwe na zoea la kubadili neno hilo kwa ukawaida. Tumia maneno tofauti-tofauti ya siri kwa ajili ya kila akaunti yako.

 5. Fanya biashara kwenye Intaneti na mashirika yenye kuaminika ambayo yana mifumo salama.

 6. Usitoe habari zako za siri au za akaunti zako unapotumia vifaa ambavyo havijaunganishwa kwa nyaya [Wi-Fi], kama vile vinavyopatikana katika sehemu za umma.

 7. Zima kompyuta yako wakati ambapo huitumii.

 8. Uwe na kawaida ya kunakili habari zako, na uzihifadhi mahali salama.


Vituo vya intaneti salama vina ishara fulani, kama vile ishara ya kufuli na “https://” kwenye kisanduku cha anwani. Herufi “s” inamaanisha salama (secure).

Fanya yote uwezayo ili kujilinda unapotumia Intaneti

Alhamisi, Januari 23, 2014

JAMII KWANZA KUZINDUA TUZO YA JAMII MWEZI JUNI 2014

Kampeni ya Jamii Kwanza inatarajia kuzindua Tuzo ya Jamii ifikapo mwezi Juni 2014.

Tuzo ya Jamii itatolewa kwa watu binafsi (Individuals) ambao wanatumia muda, Elimu, nguvu na Rasilimali zao katika kusaidia, kutumikia, na kuhudumia Jamii.

Tuzo ya Jamii inaratibiwa na Kampuni ya Tanzania Awards International Limited iliyosajiliwa kisheria na Msajili wa Makampuni Nchini Tanzania. 


Tanzania Awards International Limited ni kampuni inayojihusisha na masuala ya Utafiti, Ushauri wa Kitaalam (Consultancy) na Uratibu wa Matukio ikiwemo utoaji wa Tuzo za Kimataifa.

Chanzo: INGIA HAPA

Jumatano, Januari 22, 2014

TUZO ZA MAWASILIANO ZA KIDIJITALI KUFANYIKA DAR ES SALAAM MWAKA HUU



Opt Media Information Solutions kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa Tanzania, inakuleteeni Tunzo za Njia za Mawasiliano za Kidijitali, zijulikanazo kama “Tanzania Digital Media Awards” (TDMA)


"Tanzania Digital Media Awards " ( TDMA ) inalenga kusherehekea na kutambua uvumbuzi unaotumia Wavuti, Tovuti, na Mitandao ya Kijamii katika kutoa huduma bora kwa wateja hasa kwa kutumia mawasiliano ya digitali kwa makampuni na mashirika mbalimbali hapa Tanzania.

TDMA, mradi unaosimamiwa na Opt Media Information Solutions (OMIS ), mnano Aprili, 2014, jijini Dar es Salaam, tutakuwa na tukio la sherehe za tunzo za utoaji tunzo zitakazo kusherehekea uvumbuzi na ubora katika mawasiliano ya kidigitali ya kisasa na yale ya kawaida yanayotumiwa na makampuni na mashirika mbalimbali ndani ya Tanzania, ili kuwafikia wateja au wadau wao. Toleo hili la Tunzo pia litatoa tuzo maalum za heshima na kutambua watu maarufu na wa kawaida wanaotumia teknologia za mawasiliano kuleta mabadiliko chanya katika jamii, ama wale wanaotengeneza teknologia zilizo na manufaa kwa jamii.

Ili kuhakikisha kwamba tunzo hizi zinapata heshima na sifa chanya kutoka kwa wadau na umma kwa ujumla, washindi wa tuzo watapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na umma pamoja na zile zinakazopigwa na jopo la majaji waliona mapenzi, shauku, utaalamu na watumiaji wa njia hizi za mawasiliano ya kidigitali hapa Tanzania, kutoka katika taasisi mahususi za umma na binafsi – yaani watalamu wa TEKNOHAMA, waandishi wa habari, watu wa masoko na mawasiliano pamoja na upashaji habari.


Katika siku za nyuma ikumbukwe kuwa, tovuti ilikuwa chombo cha kawaida tu ili kufanya wamiliki wake wawe mtandaoni, lakini hili miaka ya karibuni limebadilika. Kwani leo watumiaji ama  wasomaji wa tovuti wamebadilika zaidi. Pia mageuzi katika mawasiliano kwa kutumia mitandao ya kijamii yameleta mtazamo mpya katika tasnia ya ‘mawasiliano ya kisasa’ katika biashara, serikali, na asasi za kiraia. Kwa pamoja, mtandao, na mageuzi ya teknologia ya simu za mkononi imefanya watumiaji wa mitandao na wasiliano ya dijitali wadai uzoefu wa kudumu na tija kutokana na mawasiliano ya makampuni na mashirika mbalimbali kwa wadau wao. Kwa minajili hiyo unaweza kuona jinsi mawasiliano ya kisasa yalivyoleta mafanikio makubwa kwa mawasiliano ya makampuni, mashirika na asasi za kiraia. Hivyo katika zama hizi bidhaa si tena ile ambayo tunawaambia walaji kuwa ilivyo...bali bidhaa ile ambayo wateja wanaambiana jinsi wanavyoiona kwa mitazamo yao. Hiyo ndiyo nguvu mpya ya mawasiliano digitali na mitandao ya kijamii.

Tunzo za “Tanzania Digital Media Awards” zitafanyika katika moja ya hoteli za nyota 5 hapa Dar es Salaam, Aprili hii ya mwaka 2014. Taarifa zaidi juu ya mgeni rasmi na wa heshima, ukumbi pamoja na tarehe kamili zitatolewa katika mkutano wa waandishi wa habari ambao utafanyika Februari 28, 2014 hapa Dar es Salaam.


Ombi letu kwa umma na wadau wenye kutakia mafanikio ya Tunzo za TDMA, ni kuwa sote tunatambua umuhimu, na matumizi ya mawasiliano ya kidijitali kama mitandao ya kijamii, tovuti, wavuti nk kama sehemu muhimu ya kufanikisha mawaliano ya makampuni, mashirika na serikali. Tuendelee kutumia mawasiliano haya kwa tija na weredi kwani habari na wasiliano ni muhimu kwa kila mtu, kila kampuni , serikali, na mashirika, hivyo tuizitegemeze Tunzo hizi za Chaguo la Watu.


Ahadi yetu kwa umma ni kuwa tukio hili litaendelea kufanyika katika miaka ijayo na litakuwa ndiyo tukio kubwa litakalo kutanisha watu wakaliba mbalimbali wa ulimwengu wa biashara na mashirika. Pia lengo letu ni kuhakikisha viwango vya juu ambavyo ndio msingi wamafanikio ya Tunzo hizi unafuatwa ili kulinda heshima na taswira za wadau na wafadhili wetu kwa kuwalete usiku wa sherehe zilizoandaliwa kwa uweredi mkubwa.



IMETOLEWA NA:


JONATHAN N. MNYELA

GENERAL MANAGER

OPT MEDIA INFORMATION SOLUTIONS


jonathan.mnyela@omis.co.tz

+255714060608

CHANZO: MaishanaTeknohama.blogspot.com

Jumapili, Januari 19, 2014

UTOFAUTI KIUTENDAJI KATIKA UBONGO WA KULIA NA WA KUSHOTO



PICHA HII INAONESHA MAPANDE MAWILI YA UBONGO NA NAMNA YANAVYOTAWALA DOMINANT CHARACTER YA MTU. HAPA UBONGO WA MTU UNA MAPANDE MAWILI; PANDE  LA KULIA NA LA KUSHOTO. WATU AMBAO PANDE LAO LA KUSHOTO LA UBONGO NI DOMINANT WANAVIUNGO VYAO VYA MWILI UPANDE WA KULIA VYENYE NGUVU AMA WEPESI WA KUTUMIKA ZAIDI NA VIUNGO VYAO VYA KUSHOTO NI VIZITO AMA HAVINA NGUVU ZAIDI. VILE VILE WATU WENYE PANDE  LA UBONGO LA KULIA WANAVIUNGO VYAO VYA MWILI (mikono, miguu, macho n.k) NA WA UPANDE WA KUSHOTO WANA VIUNGO VYENYE NGUVU NA WEPESI KULIKO VIUNGO VYAO VYA KULIA (hawa ndo mashoto). 

Picha hii inaonesha general dominant characteristics ya wanaotumia viungo vya upande wa kulia na wale wanotumia viungo va upande wa kusho. KUTUMIA KUSHOTO AMA KULIA NI CREATION ORDER MTU ANAZALIWA HIVO. Kitabu cha Wakorintho 12 kinapozungumzia diversity ya talents kanisani, kinadokeza vionjo maridhawa vya elimu ya "Hemispheric Brain Specialization" Mashoto sio laana ama balaa ni karama na ni talent.

Hivyo unavyoona kama vi-DARAJA NI MFANO WA CORPAS CALOSUM kitu kinachowezesha mawasiliano na masaidiano kati ya left na right brain hemispheres. Ktk mawasiliano hayo uta- enjoy kuona kuwa pande la kulia lahusika na big-pictures, creativity, n.k pande la kushoto ni wadadisi, extreme curiosity kiasi kwamba wanaogopa hata ku-take risk. ni wanasayansi, lakini mashoto wengi  wako motivated na big pictures bila ku- undergo critical analysis ndo maana wao ni risk takers zaidi. MFANO: MANDELA, OBAMA, CLINTON, ABRAHAM LINKOLIN, SHEIKH OSAMA, NEWTON ISAAC...n.k.

KAMA WEWE NI MWANAJESHI, TENGENEZA KIKOSI CHA MASHOTO MAANA KUNA HUJUMA AMBAZO ZINANYIMA UWEZO WA MASHOTO KU-utilize talent ZAO VIZURI. USILAZIMISHE WALE JKT WALOTOKA FORM SIX WAKUKABIDHI VITU KWA MKONO WA KULIA....HIYO NI tradition WALA SIYO HESHIMA. HATA Training ZA KWATA/parade, MASHOTO KWA KAWAIDA WANAANZA NA MGUU WA KULIA LAKINI MWAWALAZMISHA WAANZE NA KUSHOTO! VIVYO HIVYO KTK SHABAHA. 

MFALME DAUDI ALIKUWA NA KIKOSI CHA "AMBIDEXTROUS" WENYE KUTUMIA MIKONO YOTE SAWA SAWA 1wafalme 12:2; NA KULIKUWA NA KIKOSI CHA MASHOTO TUPU MAKOMANDO 700!!!! 

Chanzo: CLICK HAPA 

Ijumaa, Januari 17, 2014

ANGUKO LA MARCUS GARVEY KIELELEZO CHA MTU MWEUSI KUTOJITAMBUA

Marcus Garvey


Katika kuiweka falsafa yake Garveyism hai, Marcus Garvey alihimiza wamarekani weusi chini ya umoja wao wa UNIA (Universal Negro Improvement Association) badala ya kulalama kwa watesi wao waanzishe miradi itakayowapa ajira na kuonyesha kwamba mweusi anao uwezo wakufanya yale yote watesi wao wanayoyafanya.

Miradi walioianzisha ni pamoja na Makampuni ya uchapaji wa magazeti, Migahawa, vituo vya afya, Vituo vya mashine za kuoshea nguo, kumbi za mikutano na Shirika la kwanza la Watu weusi la Meli lililojulikana kama Black Star Line mwaka 1919.

Shirika la meli mbali na kulianzisha kufanya biashara na kutoa ajira lilikuwa na lengo jingine la kuwarudisha watu weusi barani Afrika (Back to Africa Movement). Mwaka 1920 ikiwa ni mwaka mmoja toka kuanzishwa shirika la meli, UNIA chini ya Garvey waliitisha kongamano la kwanza la kimataifa la watu weusi mwezi mzima wa August lililopewa jina la “The First International Convention of the Negro Peoples of the World”. Kongamano lilijumuisha weusi toka Marekani, Canada, Amerika Kusini na Afrika Magharibi.

Kutokana na ushawishi wa Garvey, Wamarekani weusi wengi walianza kujiunga na umoja wa UNIA na walipoanzisha shirika la meli serikali ya Marekani ilistuka na ikaanza mipango ya kuwahujumu akina Garvey chini ya kitengo cha Upelelezi cha Marekani cha Bureau of Investigation kwa sasa ni FBI.

KUKAMATWA, KUFUNGWA NA KURUDISHWA JAMICA

Utengenezaji wa kesi unaonyeshwa kwenye memo ya FBI iliyoandikwa na J. Edgar Hoover, msaidizi wa Mwanasheria mkuu wa Marekani mwaka 1919 kwamba hakuna ushahidi wowote unaonyesha kwamba Garvey ametenda makosa yanayoweza kuifanya serikali ya shirikisho kumtia hatiani kisha kumrudisha kwao Jamaica.

Mwaka 1919 FBI waliajili mashushu wa kwanza weusi James Edward Amos, Arthur Lowell Brent, Thomas Leon Jefferson, James Wormley Jones, and Earl E. Titus ambao kazi yao ilikuwa kujiunga na umoja wa Garvey wa UNIA kupenyeza vibaraka wengine ili waweze kupata ushaidi wowote wa kumfungulia kesi Garvey na kumrudisha kwao Jamaica.

HUJUMA DHIDI YA GARVEY

Wakati wa ununuzi wa meli UNIA chini ya Garvey walimtuma mwanachama na mhandisi wa umekaniki wa meli mweusi Kpt. Joshua Cockburn kwenda kuikagua meli ili waweze kushauliana kuhusu bei ya manunuzi ya meli yao ya kwanza iliyojulikana kama Yarmouth. Mhandisi huyo alishafanywa kibaraka wa FBI hivyo alirudisha ripoti ya ukaguzi wa meli kwamba ni nzuri wakati akijua ni mbovu ilipagana vita ya kwanza ya dunia.

Katika manunuzi ya meli bei alitaja mara sita zaidi ya bei halisi ya meli hiyo. Bei halisi ya meli ilikuwa haizidi dola 25,000 lakini yeye alimwambia Garvey kwamba bei yake ni dola 165,000 na umoja wa UNIA ukalipa bei hiyo. Mhadisi Kpt Joshua Cockburn alilipa dola 25,000 na iliyobaki akaweka mfukoni. Haya yote aliyafanya akiwa na mgongo wa FBI.

Meli ya pili The "S. S. Shadyside” ilinunuliwa kwa dola 200,000 gharama isiyostahili kwa mtindo kama ule wa meli ya kwanza kwa weusi wanaotumwa kukagua na kushauriana bei kuongeza dau lao na huku wakijua meli ni mbovu. Meli hii ilizama kwenye mto wa Hudson ikiwa na abiria weusi wamarekani.

Baadhi ya wafanyakazi wa meli wengi walifanywa vibaraka wa FBI hivyo kwa maelekezo ya FBI walipewa vitu vya kuweka kwenye injini za meli ili ziharibike. Meli ya tatu "S. S. Antonio Maceo" ililipuka injini kutokana na hujuma hizo.

Wafanyakazi wa meli hawakuzisimamia vizuri mfano meli ya Kwanza Yarmouth ilipakia mizigo kwenda Cuba kabla ya vikwazo bila vibali vya kuifanya itie nanga. Muda wote ilikaa kwenye mwambao bila kutia nanga matokeo yake vitu vikaharibika. Na hili pia linahusishwa na FBI kwa kuwapa maelekezo watu waliokuwa kwenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Miaka mitatu toka shirika la meli kuanzishwa weusi wakaliua wenyewe, likafilisika. Shirika likawa mhanga wa kubambikiziwa bei na wahandisi, wizi wa wawakilishi na maofisa wa UNIA bila kusahau hujuma za FBI. Biashara nyingine pia weusi walikuwa wanafuja mali zake. Hapa FBI wakaanza kutengeneza kesi kumtia hatiani Marcus Garvey.

Februari mwaka 1922 Marcus Garvey alitangaza kusitishwa kwa shughuli za Black Star Line baada ya FBI kumfungulia mashtaka ya njama za kutapeli kwa njia ya barua (mail fraud).

MASHTAKA DHIDI YA GARVEY

Garvey alishitakiwa kwa njama za kutapeli kutumia barua na kesi ya FBI dhidi yake ilijikita kwenye barua zilizokuwa zinatumwa kwa wamarekani weusi zikiwa na picha ya meli wakati meli zenyewe zilikuwa hazijanunuliwa.

Vipeperushi vilivokuwa vikitumwa vilikuwa na lengo la kuwahimiza wanachama kuchangia kuanzisha biashara na mrejesho wake kuwa asilimia ya kiasi cha mtu alichochanga. Hivyo biashara zao hazikuwa biashara kama biashara nyingine kampuni kutangaza kuuza hisa bali watu wanaoamua kuanzisha umoja ili kujiinua kiuchumi na mambo mengine ya kijamii.

FBI waliandaa mashaidi weusi na kuwatengenezea ushaidi watakaoutoa mahakamani kuonyesha kwamba ile miradi ilikuwa ya Marcus Garvey ili kuweza kumuhukumu Garvey. Wengine walikuja kusema kwamba walilaghaiwa na FBI wakati huo tayari Garvey anatumikia kifungo gerezani cha miaka mitano.

Mwendesha mashtaka msaidizi wa New York ndiye alikuwa shahidi namba moja wa FBI na ikumbukwe kwamba mwendesha mashtaka huyo ndiye alikuwa mwanasheria wa kampuni iliyowauzia akina Garvey meli ya kwanza. Alikuwa akijua mchezo wote uliochezwa na Kpt Joshua Cockburn wa kuwauzia meli mbovu na bei mara 6 ya gharama ya kawaida.

KUFUNGWA NA MWISHO WA HARAKATI ZAKE

Alifungwa mwezi wa 6 mwaka 1923 miaka mitano na lakini alianza kutumikia kifungo chake mwaka 1925 baada ya rufaa zake kutupwa. Alipewa msamaha na rais mwaka 1927 na kurudishwa Jamaica. Huo ndio ukawa mwisho wa harakati zake. Badae aliamia Uingereza na kufariki mwaka 1940 jijini London.

Anguko lake ni kutokana na watu weusi kutojitambua kama ilivyo sasa kwenye nchi nyingi za kiafrika. Wachambuzi wa historia wanasema harakati zake ndo zilimhukumu na si mashtaka ya ulaghai.


Chanzo: tudadisiforums

UDUKUZI

Rais Barack Obama





 Ufichuzi wa hivi karibuni uliochapishwa siku ya alhamisi unadai kuwa idara hiyo ya ujasusi ilidukua mamilioni ya ujumbe katika simu za watu za mkononi duniani kila siku.

Upelelezi huo wa simu zilizopigwa pamoja na mitandao umezua hisia kali kutoka kwa wanaharakati na makundi ya kijamii nchini marekani na washirika wake.

Hata hivyo vitengo vya ujasusi vimeonya kuwa uchunguzi zaidi wa mienendo yake huenda ukaathiri usalama wa marekani.

Rais Barrack Obama anajiandaa kutangaza ambavyo atarudisha imani katika idara ya ujasusi nchini humo kufuatia kufichuliwa kwa taarifa za idara hiyo na aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya kijasusi nchini humo Edward Snowden.

Chanzo: BBC


Jumapili, Januari 05, 2014

Jinsi ya Kufanya Utafiti



MFALME SOLEIMANI ‘alitafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi.’ Kwa nini? Kwa sababu alitaka kuandika “maneno ya kweli.” (Mhu. 12:9, 10) Luka ‘alifuatisha kwa uangalifu mambo yote tangu awali kwa usahihi’ ili asimulie kwa utaratibu matukio ya maisha ya Kristo. (Luka 1:3) Watumishi hao wa Mungu walifanya utafiti.

Utafiti ni nini? Utafiti ni kuchunguza kwa makini habari inayohusu jambo fulani. Unatia ndani kusoma na kufuata kanuni za kujifunza. Pia unaweza kutia ndani kuhoji watu.

Tufanyie utafiti mambo gani? Ifuatayo ni mifano michache. Unapokuwa na funzo la binafsi au unaposoma Biblia, huenda ukapata mambo yanayotokeza maswali muhimu. Labda ungependa kupata habari fulani ili ujibu swali la mtu ambaye ulimhubiria. Au huenda umepewa mgawo wa kutoa hotuba.

Ebu fikiria kuhusu mgawo huo wa kutoa hotuba. Huenda ikaonekana kwamba hotuba hiyo ina mambo ya kawaida tu. Unaweza kufanyaje ili hotuba hiyo ifae hali za kwenu? Uiboreshe kwa kufanya utafiti. Ukitumia habari chache zinazohusu idadi katika hotuba au ukitumia mfano mzuri unaohusu wasikilizaji, jambo ambalo huenda lilionekana kama ni la kawaida tu linakuwa lenye kufundisha, na hata lenye kuchochea moyo. Habari zilizo katika hotuba yako huenda zilichapishwa kwa manufaa ya wasomaji ulimwenguni pote, lakini inatakikana uonyeshe faida ya hotuba hiyo kwa kuifafanua, kutumia mifano, na kwa kuonyesha jinsi kutaniko au mtu mmoja-mmoja anavyoweza kufuata mashauri yake maishani. Ufanyeje?

Kabla ya kuanza kufanya utafiti, uwafikirie wasikilizaji. 
Tayari wamejua nini? 
Wanahitaji kujua nini? 
Na kusudi lako ni nini? 
Je, ni kufafanua habari hiyo? 
ni kusadikisha? ni kukanusha? 
au ni kuchochea? 
Kufafanua kunamaanisha kuandaa habari zaidi ili jambo lieleweke wazi. Ingawa huenda mambo makuu yanaeleweka, inafaa kuonyesha wasikilizaji wakati wanapoweza kutumia habari hiyo au jinsi wanavyoweza kutumia habari hiyo. Kusadikisha kunamaanisha kutoa uthibitisho unaoonyesha kwa nini jambo tunalosema ni kweli. Ili tuweze kukanusha jambo, tunahitaji kujua kabisa pande zote mbili za suala hilo pamoja na kuchunguza kwa makini uthibitisho unaotumiwa. Bila shaka, hatutoi tu sababu zenye nguvu bali pia sisi hujaribu kutoa sababu kwa njia ya fadhili. Kuchochea kunahusu kufikia moyo. Kunamaanisha kuhimiza wasikilizaji na kufanya watamani kufuata mashauri ya hotuba yako. Mifano ya watu halisi ambao wamechukua hatua hiyo, hata wajapokabili magumu, inaweza kusaidia kufikia moyo.

Je, sasa u tayari kuanza? La, bado. Fikiria kiasi cha habari unachohitaji. Huenda ikawa muhimu kufikiria wakati. Kama utatoa hotuba hiyo mbele ya wengine, utaitoa kwa muda gani? Dakika tano? Dakika 45? Je, umewekewa wakati kama ilivyo na mikutano ya kutaniko au hujawekewa wakati, kama ilivyo na funzo la Biblia au ziara ya uchungaji?

Hatimaye, una vifaa gani vya kufanyia utafiti? Kwa kuongezea vifaa ulivyo navyo nyumbani, je kuna vifaa zaidi kwenye maktaba ya Jumba lenu la Ufalme? Je, ndugu ambao wamekuwa wakimtumikia Mungu kwa miaka mingi wanaweza kukuruhusu utumie vifaa vyao vya kufanyia utafiti? Je, kuna maktaba ya umma huko kwenu ambayo ina vitabu vya marejeo ambavyo vinaweza kutumiwa?

Kutumia Biblia, Kitabu Chetu Kikuu cha Utafiti

Ikiwa utafiti unaofanya unahusu maana ya andiko fulani, anza na Biblia yenyewe.
Chunguza Muktadha. Jiulize: ‘Andiko hili lilielekezewa nani? Mistari inayotangulia na inayofuata andiko hilo inaonyesha nini kuhusu sababu inayotajwa au inaonyesha nini kuhusu watu wanaotajwa?’ Mara nyingi mambo kama hayo yanaweza kutusaidia kuelewa andiko fulani, na pia yakitumiwa yanaweza kufanya hotuba yako ipendeze zaidi.

Kwa mfano, mara nyingi Waebrania 4:12 hunukuliwa kuonyesha uwezo wa Neno la Mungu wa kugusa mioyo na kubadili maisha. Muktadha unatusaidia kufahamu jambo hilo zaidi. Unasimulia mambo ambayo Waisraeli walipitia wakati wa ile miaka 40 wakiwa jangwani kabla hawajaingia katika nchi ambayo Mungu aliahidi Abrahamu. (Ebr. 3:7–4:13) “Neno la Mungu,” yaani ahadi yake ya kuwaleta mahali pa pumziko kulingana na agano lake pamoja na Abrahamu, halikuwa limeshindwa; bado lilielekea kutimizwa. Waisraeli walikuwa na sababu nzuri za kuliamini. Lakini, walirudia-rudia kuonyesha ukosefu wa imani kwa Mungu alipokuwa akiwatoa Misri na kuwaongoza hadi Mlima Sinai na kuelekea Nchi ya Ahadi. Basi, itikio lao kwa jinsi Mungu alivyotimiza neno lake, lilidhihirisha yaliyokuwa mioyoni mwao. Katika siku zetu vilevile, ahadi ya neno la Mungu huonyesha yaliyomo mioyoni mwa wanadamu.

Chunguza Marejeo. Baadhi ya Biblia zina marejeo. Je, yako inayo? Ikiwa inayo, hayo yanaweza kukusaidia. Ebu ona mfano mmoja katika New World Translation of the Holy Scriptures. Andiko la 1 Petro 3:6 linaonyesha kwamba Sara ni mfano ambao wake Wakristo wanastahili kuiga. Marejeo kwenye Mwanzo 18:12 yanakazia jambo hilo kwa kufunua kwamba Sara alimwita Abrahamu bwana “moyoni mwake.” Kwa hiyo, alitii kutoka moyoni. Mbali na ufahamu kama huo, marejeo yanaweza pia kukuelekeza kwenye maandiko ambayo yanaonyesha utimizo wa unabii wa Biblia au utimizo wa jambo lililofananishwa na agano la Sheria. Lakini, marejeo fulani hayakusudiwi kutoa maelezo kama hayo. Huenda ikawa yanaonyesha tu mawazo yanayolingana na habari hiyo, au maelezo ya maisha ya mtu au habari kuhusu mahali.

Tumia Itifaki ya Biblia. Itifaki ya Biblia ni orodha ya maneno ambayo yametumiwa katika Biblia. Orodha hiyo imepangwa katika alfabeti. Inaweza kukusaidia kupata maandiko yanayohusiana na habari unayofanyia utafiti. Unapoyachunguza, utajifunza mambo mengine yenye faida. Utaona uthibitisho wa kwamba kuna “kiolezo” cha kweli katika Neno la Mungu. (2 Tim. 1:13) Biblia ya Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ina orodha ya msingi ya “Maneno ya Biblia Yaliyofaharishwa.” Itifaki inayoitwa Comprehensive Concordance ina mambo mengi sana. Ikiwa inapatikana katika lugha unayoelewa, itakuonyesha maneno yote makuu yanayotumiwa katika Biblia.