Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Januari 22, 2014

TUZO ZA MAWASILIANO ZA KIDIJITALI KUFANYIKA DAR ES SALAAM MWAKA HUU



Opt Media Information Solutions kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa Tanzania, inakuleteeni Tunzo za Njia za Mawasiliano za Kidijitali, zijulikanazo kama “Tanzania Digital Media Awards” (TDMA)


"Tanzania Digital Media Awards " ( TDMA ) inalenga kusherehekea na kutambua uvumbuzi unaotumia Wavuti, Tovuti, na Mitandao ya Kijamii katika kutoa huduma bora kwa wateja hasa kwa kutumia mawasiliano ya digitali kwa makampuni na mashirika mbalimbali hapa Tanzania.

TDMA, mradi unaosimamiwa na Opt Media Information Solutions (OMIS ), mnano Aprili, 2014, jijini Dar es Salaam, tutakuwa na tukio la sherehe za tunzo za utoaji tunzo zitakazo kusherehekea uvumbuzi na ubora katika mawasiliano ya kidigitali ya kisasa na yale ya kawaida yanayotumiwa na makampuni na mashirika mbalimbali ndani ya Tanzania, ili kuwafikia wateja au wadau wao. Toleo hili la Tunzo pia litatoa tuzo maalum za heshima na kutambua watu maarufu na wa kawaida wanaotumia teknologia za mawasiliano kuleta mabadiliko chanya katika jamii, ama wale wanaotengeneza teknologia zilizo na manufaa kwa jamii.

Ili kuhakikisha kwamba tunzo hizi zinapata heshima na sifa chanya kutoka kwa wadau na umma kwa ujumla, washindi wa tuzo watapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na umma pamoja na zile zinakazopigwa na jopo la majaji waliona mapenzi, shauku, utaalamu na watumiaji wa njia hizi za mawasiliano ya kidigitali hapa Tanzania, kutoka katika taasisi mahususi za umma na binafsi – yaani watalamu wa TEKNOHAMA, waandishi wa habari, watu wa masoko na mawasiliano pamoja na upashaji habari.


Katika siku za nyuma ikumbukwe kuwa, tovuti ilikuwa chombo cha kawaida tu ili kufanya wamiliki wake wawe mtandaoni, lakini hili miaka ya karibuni limebadilika. Kwani leo watumiaji ama  wasomaji wa tovuti wamebadilika zaidi. Pia mageuzi katika mawasiliano kwa kutumia mitandao ya kijamii yameleta mtazamo mpya katika tasnia ya ‘mawasiliano ya kisasa’ katika biashara, serikali, na asasi za kiraia. Kwa pamoja, mtandao, na mageuzi ya teknologia ya simu za mkononi imefanya watumiaji wa mitandao na wasiliano ya dijitali wadai uzoefu wa kudumu na tija kutokana na mawasiliano ya makampuni na mashirika mbalimbali kwa wadau wao. Kwa minajili hiyo unaweza kuona jinsi mawasiliano ya kisasa yalivyoleta mafanikio makubwa kwa mawasiliano ya makampuni, mashirika na asasi za kiraia. Hivyo katika zama hizi bidhaa si tena ile ambayo tunawaambia walaji kuwa ilivyo...bali bidhaa ile ambayo wateja wanaambiana jinsi wanavyoiona kwa mitazamo yao. Hiyo ndiyo nguvu mpya ya mawasiliano digitali na mitandao ya kijamii.

Tunzo za “Tanzania Digital Media Awards” zitafanyika katika moja ya hoteli za nyota 5 hapa Dar es Salaam, Aprili hii ya mwaka 2014. Taarifa zaidi juu ya mgeni rasmi na wa heshima, ukumbi pamoja na tarehe kamili zitatolewa katika mkutano wa waandishi wa habari ambao utafanyika Februari 28, 2014 hapa Dar es Salaam.


Ombi letu kwa umma na wadau wenye kutakia mafanikio ya Tunzo za TDMA, ni kuwa sote tunatambua umuhimu, na matumizi ya mawasiliano ya kidijitali kama mitandao ya kijamii, tovuti, wavuti nk kama sehemu muhimu ya kufanikisha mawaliano ya makampuni, mashirika na serikali. Tuendelee kutumia mawasiliano haya kwa tija na weredi kwani habari na wasiliano ni muhimu kwa kila mtu, kila kampuni , serikali, na mashirika, hivyo tuizitegemeze Tunzo hizi za Chaguo la Watu.


Ahadi yetu kwa umma ni kuwa tukio hili litaendelea kufanyika katika miaka ijayo na litakuwa ndiyo tukio kubwa litakalo kutanisha watu wakaliba mbalimbali wa ulimwengu wa biashara na mashirika. Pia lengo letu ni kuhakikisha viwango vya juu ambavyo ndio msingi wamafanikio ya Tunzo hizi unafuatwa ili kulinda heshima na taswira za wadau na wafadhili wetu kwa kuwalete usiku wa sherehe zilizoandaliwa kwa uweredi mkubwa.



IMETOLEWA NA:


JONATHAN N. MNYELA

GENERAL MANAGER

OPT MEDIA INFORMATION SOLUTIONS


jonathan.mnyela@omis.co.tz

+255714060608

CHANZO: MaishanaTeknohama.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni