Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Juni 19, 2012

MELI KAMA HII JE UMEWAHI KUONA


Hili Limeli linaitwa In Explorer of the seas,au kwa kiswahili ''Mvumbuzi wa bahari''.Meli hii ina kila aina ya huduma anayohiitaji mwanadamu,na baadhi ya huduma ni bora kuliko zinazotolewa na baadhi ya miji katika nchi mbali mbali.Meli hii yenye uwezo wa kubeba watu 3,100 inamilikiwa na kampuni ya kifalme ya kimataifa Caribbea.
 


 Dubwasha hii lina uzito wa zaidi tani 100,000,lina maduka yanayouza bidhaa mbali mbali kiasi cha kukufanya upate kila unachokihitaji,Lina viwanja vya michezo,kwa mfano uwanja wa mpira wa kikapu,mabwawa 3 makubwa ya kuogelea (swimming pools),kiwanja cha tenesi na gofu.

 

Lakini pia ukibahaitika kwenda kutanua kwenye dubwasha hili itakupasa kulipa kuanzia dola 400 kwa siku,na ndani yake utafaidi ukumbi wa sinema wa kisasa zaidi.Aidha ndani yake ili kukufanya ujihisi upo peponi,kuna kumbi za disko,baa za kisasa 3,sehemu za kutereza kwenye barafu na kiwanja cha kupanda kwenye milima.



 Kwa wale wanaopenda kufanya mazoezi ya kupunguza vitambi au kujiweka fiti ndani ya dubwasha hili kuna kiwanja malum cha Joging na sehemu ya kufanya mazoezi 'GIM'. Kwa upande wa hoteli ndio usiseme zipo hoteli za bei chee na za wenye nazo (matawi ya juu).Pia kuna Studio,Ukumbi wa wazi wa sinema 'Theatre',sehemu ya muziki wa dansi,garden kwaajili ya kupumzikia,sehemu ya kasino ya kawaida na ile ya maalum kwa watu wanaopenda mambo ya wakubwa.



Kuna maduka ya kubadilisha fedha,hospitali,kumbi za mikutano,ukumbi wa makumbusho ya picha za zamani,ukumbi wa michezo ya pool na darts.Katika meli hiii pia kuna sehemu maalum kwa wale wanaotumia internet,wanaokutana faragha,sehemu ya michezo ya kutereza kwenye maji.Kuna kituo cha kutoa ushauri nasaha wa mambo mbalimbali kimaisha,bila kukosekana kituo cha Polisi




.Baadhi ya watu badala ya kwenda 'Honey moon' hotelini kama tulivyozoea,wao hutumia muda huo wa kubembelezana kwenye meli hiyo.Cha kushangaza wenzetu huenda kupitisha bajeti zao ndani ya meli hii.

Jumapili, Juni 03, 2012

MATUKIO YA WEEKEND KIJUMAMOSI KTK STUDIO ZA MORNING STAR RADIO....HII NI KWAYA YA VIJANA USHINDI WALIPOKFANYIWA MAHOJIANO YA MOJA KWA MOJA REDIONI.




















































JE! CHAKULA KINAWEZA KUATHIRI AKILI YAKO?


(SOMA DANIELI 1 YOTE)

SOMA DANIELI 1 YOTE)
Amini usiamini, chakula kinaweza kuathiri akili yako, na afya yako ya kimwili na kiroho. Kwa maelezo zaidi juu ya somo hili la afya soma vitabu vya Afya na Lishe, kama vile Afya na Raha na Uponyaji wa Mungu ambamo zimefafanuliwa Kanuni 8 za Afya ----- Lishe bora, Mazoezi ya mwili, Hewa safi, Maji safi
na salama, Mwanga wa jua, Pumziko, Kiasi, na Kumwamini Mungu. Ukizifuata utaepukana na magonjwa mengi na kupunguza gharama ya matibabu. Yatabaki magonjwa yanayokuja kwa njia zingine zisizozuilika.

Chakula cha daraja la kwanza ambacho Mungu alimpa mwanadamu kilikuwa cha nafaka, kokwa na matunda (Mwanzo 1:29). Dhambi ilipoingia ilileta laana sio tu kwa viumbe vyote bali hata kwa ardhi. Kwa hiyo Mungu akamwongezea mwanadamu mboga za majani katika lishe yake ya awali (Mwanzo 3:18). Gharika ilikaa juu ya nchi kwa miezi mitano au siku 150 na kuharibu mimea yote (Mwanzo 7:24). Kwa hiyo Mungu akamwongezea mwanadamu katika lishe yake "nyama" kutoka kwa wanyama safi tu (Mwa. 8:3,4 imebainishwa na Law. 11:1-47; Kum. 14:1-21). Injini ya petroli hutumia petroli tu; injili ya dizeli ni dizeli tu. Ukitaka gari lako life weka dizeli katika injini ya petroli au petroli katika injini ya dizeli. Mtengenezaji ndiye anayejua gari lake litatumia mafuta gani, sio mtumiaji. Vile vile, Mungu anajua chakula kinachofaa kwa mwili wa mwanadamu, sio mwanadamu kujichagulia cho chote kuwa chakula. Wabishi wataharibu injini za magari yao (miili yao).

Mungu aliumba wanyama safi na wanyama najisi juma lile la kwanza la uumbaji. Kifo cha Yesu msalabani hakikuwa kwa kusudi la kuwabadilisha wanyama najisi kuwa wanyama safi, bali wanadamu wenye dhambi kuwa watakatifu. Wale wanaotaka kuwa watakatifu watajiepusha kula nyama inayotokana na wanyama najisi; lakini wale wasiotaka utakatifu wataswaga kila kitu (Law. 11:41,43,46,47; Kum. 14:1-4). Mungu hamlazimishi mtu, kama vile mtengenezaji wa injini ya gari asivyomlazimisha mtu kutumia
mafuta aliyopendekeza. Lakini matokeo mwilini ni ya hakika.

Kisa cha Petro katika Matendo 10:9-16 kimetafsiriwa chini yake katika fungu la 25 hadi 29. Hayo yalikuwa ni maono tu, si kitu halisi; hata hivyo Petro alikataa katakata kuchinja na kula wanyama najisi ingawa ni Mungu mwenyewe aliyemwamuru kufanya hivyo mara tatu. Mungu hana kigeugeu; alisema wanyama
najisi wasiliwe, basi, hawawezi kuliwa milele (Mal. 3:6; Zab. 89:34). Watu wanamsingizia bure Petro wanapochinja wanyama najisi na kula; yeye alikataa katakata. Lakini kuna adhabukali sana kwa wale wanaoendelea kula nguruwe, panya, na machukizo yote ya Mataifa (wapagani). Soma Isaya 65:2-6;
66:15-17).

Pombe haikuwa sehemu ya kinywaji ambacho Mungu alimpa mwanadamu; maji safi na salama ndicho kinywaji bora kuliko vyote kwa mwanadamu (Mithali 20:1; 23:29-35). Walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Kor. 6:9,10; Gal. 5:21). Kuna wengi wanaosema, "Mimi nakunywa sana, lakini silewi." Tatizo
la pombe sio kulewa tu, bali ni zile athari zinazotokana na kunywa pombe ambayo ina sumu mbaya ya alkoholi. Sumu hiyo huathiri vibaya moyo, mishipa ya fahamu, nyama za mwili na kadhalika. Mungu atamharibu mtu ye yote anayeuharibu mwili wake kwa makusudi kwa njia yo yote ile ----- pombe, tumbako, madawa ya kulevya, na kadhalika (1 Kor. 3:16,17). Pia kuna vinywaji vinavyopendwa na watu wengi aina ya 'Cola', Kahawa, na Majani ya Chai ambavyo huidhuru mishipa ya fahamu, ubongo na mwili.
Viepukwe.

Hebu sasa na tuwaangalie wale vijana wanne wa Kiebrania, mateka kutoka Yerusalemu, wakiwa katika jiji lile la Babeli mwaka ule wa 606 au 605 K.K. Walikuwa na umri kati ya miaka 18 na 20. Kutokana na hekima yao walichaguliwa kujiunga na vijana wengine wa Babeli katika Chuo cha Kishenzi [Kipagani] cha Babeli kwa mafunzo ya miaka mitatu. Wakapewa majina ya miungu ya Babeli ----- Danieli akaitwa Belteshaza, Hanania akaitwa Shadraka, Mishaeli akaitwa Meshaki, na Azaria akaitwa Abednego
(Dan. 1:6,7). Mfalme akaamuru wale chakula cha mfalme ili wanenepe na kuwa na akili nyingi. Kusudi lake lilikuwa zuri sana. Lakini, je! chakula kile cha mfalme ambacho kilikuwa na nyama najisi, kilikolezwa kwa viungo vingi vinavyodhuru mwili, na huenda kilikuwa na vileo kingeweza kuleta afya bora na akili safi? (Dan. 1:1-5). Vijana hao wanne wa Kiebrania walikuwa wamelelewa katika mazingira tofauti. Walifuata kanuni za afya  na chakula ambacho Mungu aliwapa wanadamu kula. Walijiepusha na nyama ya aina yo yote ile pamoja na divai (maji matamu ya zabibu) kwa vile wao walikuwa wanadhiri wa Bwana (Hesabu 6:1-5).
Kwa hiyo agizo hilo la mfalme kwao likawa mtihani mgumu sana.

"Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi" (Dan. 1:8). Ni ujasiri ulioje! Ombi lake halikuwa rahisi kukubaliwa na msimamizi yule kwa vile angekatwa kichwa kama
wangeonekana wamekondeana (Dan. 1:10). Basi Danieli akamwambia, "Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mtama [nafaka, kokwa, mboga za majani, matunda] tule, na
maji tunywe. Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme..." (Dan. 1:13). Akawakubalia ombi hilo. Je! mambo yalikuwaje kiafya baada ya siku zile kumi tu? "Nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi [wanawake wanaohangaika na vipodozi vinavyodhuru afya wangezingatia hilo], na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme. Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula [cha mfalme], na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama [nafaka, kokwa, mboga za majani, matunda] tu" (Dan. 1:15,16).

Chakula cha matajiri au wafalme tunachokitamani sana hakileti afya mwilini. Chakula rahisi cha mimea na maji safi na salama ni lishe bora. Kwa akili safi na mwili wenye afya, ulionenepa kiafya sio kwa ugonjwa, tumia vyakula vya mimea na maji safi na salama, na kufuata Kanuni zile 8 za Afya. Wana sayansi wamegundua kuwa wale wanaokula vyakula vya mimea bila nyama wanaishi maisha marefu sana kuliko wanaokula nyama. Danieli naye aliishi zaidi ya miaka 80 kufikia kipindi cha utawala wa Koreshi (Dan. 1:21; 10:1). Hebu tuwafuatilie vijana wale wanne mwisho wa mafunzo yao ya miaka mitatu. Mfalme Nebukadreza aliwaonaje?

"Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria... Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa wanafaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake" (Dan.1:19,20).

Kwa nini tuhangaike sana na suala la afya ya mwili wetu, je! maisha ya kiroho si bora zaidi? "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako [kimwili], kama vile roho yako ifanikiwavyo" (3 Yohana 2). Wahenga walisema, "Akili timamu katika mwili wenye afya." Ni shauri la kuzingatiwa sana.
Kanuni ya Biblia ni hii: "Basi, mlapo, mnywapo, au mtendapo neno lo lote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (1 Kor. 10:31). Tunawajibika kuitunza miili yetu katika hali ya afya nzuri kadiri iwezekanavyo (l Kor. 6:19,20; 1 Pet. 1:18,19; Rum.12:1,2). Suala la afya linahusu wokovu wetu. Mungu anaweza
kututumia kama Danieli (Dan. 1:17).

Jumatano, Mei 23, 2012

Hellow Wote Mtandaoni...!!.


Tahadhari: Rangi ya Tshirt haihusiani na Chama chochote cha kisiasa. Ni kwa kuwa tulikosa rangi nyingine wakati tumeamua kuprint kwa ajili ya ACAPPELLA KWANZA.
 
Ni yangu imani kuwa haujambo msomaji wa blog hii.
Ni kwa siku nyingi nimekuwa kimya bila kuendeleza nia ya fikra zangu.
 
Namshukuru Mungu kwa jinsi anavyoendelea kuniweka katika namna ambayo kwa hakika sikuitaraji....kwa ufupi napenda kusema nimerejea tena.
 
MUZIKI WA ACAPPELLA NDIO JAMBO AMBALO LIMENICHUKULIA MDA WANGU MWINGI LENGO NIKUUFANIKISHA KWA KUUFIKISHA KATIKA NGAZI ILIYOFIKIWA.

Jumanne, Mei 22, 2012

HISIA HARIBIFU NA MAHUSIANO MAPYA



Msingi wa tiba mbadala (Alternative medicine) tofauti na tiba ya jadi (traditional medicine) na tiba ya hospitalini (Converntional medicine) ni kuwa 'Mgonjwa/mtu atibiwe kwanza na ugonjwa wake ufuatie baadaye' .

Msingi hasa wa kumtibu mgonjwa unaanzia kwenye mahusiano mapya na hisia haribifu za maisha yake ya kila siku KIMATENDO.


Kitu hasa cha kufanya ni hiki: TAMBUA BILA KUKWEPA , Hisia haribifu kila zinapojitokeza: Hiyo inatosha kabisa. Utakuwa umeshamaliza wajibu wako kwa Utambuzi huo!

Hasira, woga, chuki, wasiwasi na hisia haribifu nyingine, Zikijitokeza na kurudia tena na tena, tumia NGUVU YA UTAMBUZI wako kwa kupitia machapisho yahusuyo masuala ya kiroho ama nyimbo za injili zilizotulia, mfano; Gospel Classics. Hii itasaidia kuzitambua tena na tena. Usichoke! Jenga tabia ya kudumu ya kuzitambua tena na tena, kila zikijitokeza na kuzipuuzia mara moja!

Fanya hivyo kwa utulivu na utaratibu, usigombane nazo, kuvutana wala kupambana na hisia haribifu. Zitambue, tizama, tambua-tena, TULIA! Alafu endelea na shughuli zako. Jenga mazoea hayo ya kiutu, busara na hekima. Kuzitambua, kujiachamanisha na kuzipuuzia kwa utulivu! Ikiwezekana fanya tabia hiyo kuwa mtindo wa maisha yako yaani KUMUOMBA MUNGU MARA NYINGI NYINGI!

Hisia haribifu ni nyonge na dhaifu kwa UTAMBUZI wa mtu anayezitizama na KUTAMBUA TU , zimefichuliwa, zina- AIBIKA kwa hatua ulizochokua. Udhibiti wa namna hii unaupa mwili nguvu hai iliyo msingi wa afya na tiba ya kweli kwa kizazi cha sasa!


Huu ndio ukweli na siri ya udhaifu wa hisia haribifu, Msingi wa tiba kwenye chanzo.
Tumia BIBLIA yaani soma NENO LA MUNGU 'Tulia na utambue'. Fanya zoezi la kujenga tafakari ya utambuzi na kudhoofisha hisia haribifu kwa njia hiyo MUNGU ATAKUSAIDIA.

Jumatatu, Mei 21, 2012

Sasa....Tukirejea: twatofautiana uelewa juu ya hili ama haya.



Hapa ntahitaji msaada kidogo 

Ninalomaanisha ni kuwa kama halijatokea kwako ama hujalisikia laweza kuendelea kuwa ndoto kwako, lakini kama ulishalisema kwa mtu na akaliona likitendeka huko aliko anaweza kuona ni ufunuo.
  
Unadhani ni mangapi unayaota usiku ama ulalapo na unashindwa kuyatendea kazi? 

Lakini, JE ni kweli kuwa hakuna haja ya kutilia maanani yale mema tuotayo? Je kuyasimulia?
Kumbuka yale upendayo ambayo umekuwa ukitamani kuota, na kujaribu kuyatekeleza licha ya KUTHUBUTU lakini hukupata nafasi ya kujaribu.

Jumatano, Mei 16, 2012

Nyumba Ilivyopinduliwa na Wasanii Juu Chini Yani

 Pichani juu ni kazi ya Wasanii wa ujenzi, bwana Klaudiusz Golos na Sebastian Mikiciuk, ambao wameamua kujenga nyumba ambayo fikira yake ni kuigeuza juu-chini, chini-juu kama ionekanavyo pichani.

Ujenzi wa ndani ya jiko ukiendelea na mmoja wa wasaidizi wa nyumba hiyo.
  
 
Ujenzi wa sehemu ya kulia chakula ukipata ukarabati na ribiti za mwisho mwisho.
 
 Sofa la kukalia likiwa katika marekebisho ya mwisho mwisho katika sehemu ya kupumzikia ya nyumba hiyo.
 
Choo kinapata vipodozi vya mwisho mwisho na mmoja wa wasaidizi wa ujenzi.
  
  Jikoni kunapata vipodozi vya mwisho mwisho kabla wenye nyumba kuhamia.

  Ujenzi wa ndani ya choo ukiendelea na mmoja wa wasaidizi wa wasanii wa nyumba hiyo.
  
Upande wa dirisha moja-wapo kati ya madirisha ya nyumba hiyo.
  
 
 Kiti cha kupumzikia kikiwekwa vizuri katika kona ya nyumba
   
 Utakapotembelea Baltic Sea Island, Usedom, Germany, usije ukashtuka ukiona hiyo nyumba kama ambayo iliyopeperushwa na upepo au iliyopeperushwa na kimbunga.
Madhumuni ya nyumba hiyo ni moja ya kuvutia watalii katika mji huo na watalii watapata fursa ya kujisikia wakiwa wakitembea ndani ya nyumba hiyo kama wakining'inia kichwa chini miguu juu.