Hili Limeli linaitwa In Explorer of the seas,au kwa kiswahili ''Mvumbuzi
wa bahari''.Meli hii ina kila aina ya huduma anayohiitaji mwanadamu,na
baadhi ya huduma ni bora kuliko zinazotolewa na baadhi ya miji katika
nchi mbali mbali.Meli hii yenye uwezo wa kubeba watu 3,100 inamilikiwa
na kampuni ya kifalme ya kimataifa Caribbea.
Dubwasha hii lina uzito wa
zaidi tani 100,000,lina maduka yanayouza bidhaa mbali mbali kiasi cha
kukufanya upate kila unachokihitaji,Lina viwanja vya michezo,kwa mfano
uwanja wa mpira wa kikapu,mabwawa 3 makubwa ya kuogelea (swimming
pools),kiwanja cha tenesi na gofu.
Lakini pia ukibahaitika kwenda kutanua
kwenye dubwasha hili itakupasa kulipa kuanzia dola 400 kwa siku,na
ndani yake utafaidi ukumbi wa sinema wa kisasa zaidi.Aidha ndani yake
ili kukufanya ujihisi upo peponi,kuna kumbi za disko,baa za kisasa
3,sehemu za kutereza kwenye barafu na kiwanja cha kupanda kwenye
milima.
Kwa wale wanaopenda kufanya mazoezi ya kupunguza vitambi au
kujiweka fiti ndani ya dubwasha hili kuna kiwanja malum cha Joging na
sehemu ya kufanya mazoezi 'GIM'. Kwa upande wa hoteli ndio usiseme zipo
hoteli za bei chee na za wenye nazo (matawi ya juu).Pia kuna
Studio,Ukumbi wa wazi wa sinema 'Theatre',sehemu ya muziki wa
dansi,garden kwaajili ya kupumzikia,sehemu ya kasino ya kawaida na ile
ya maalum kwa watu wanaopenda mambo ya wakubwa.
Kuna maduka ya
kubadilisha fedha,hospitali,kumbi za mikutano,ukumbi wa makumbusho ya
picha za zamani,ukumbi wa michezo ya pool na darts.Katika meli hiii pia
kuna sehemu maalum kwa wale wanaotumia internet,wanaokutana
faragha,sehemu ya michezo ya kutereza kwenye maji.Kuna kituo cha kutoa
ushauri nasaha wa mambo mbalimbali kimaisha,bila kukosekana kituo cha
Polisi
.Baadhi ya watu badala ya kwenda 'Honey moon' hotelini kama
tulivyozoea,wao hutumia muda huo wa kubembelezana kwenye meli hiyo.Cha
kushangaza wenzetu huenda kupitisha bajeti zao ndani ya meli hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni