Pichani
juu ni kazi ya Wasanii wa ujenzi, bwana Klaudiusz Golos na Sebastian
Mikiciuk, ambao wameamua kujenga nyumba ambayo fikira yake ni kuigeuza
juu-chini, chini-juu kama ionekanavyo pichani.
Ujenzi wa ndani ya jiko ukiendelea na mmoja
wa wasaidizi wa nyumba hiyo.
Ujenzi wa sehemu ya kulia chakula ukipata
ukarabati na ribiti za mwisho mwisho.
Sofa la kukalia likiwa katika marekebisho
ya mwisho mwisho katika sehemu ya kupumzikia ya nyumba hiyo.
Choo kinapata vipodozi vya mwisho mwisho na
mmoja wa wasaidizi wa ujenzi.
Jikoni kunapata vipodozi vya mwisho mwisho
kabla wenye nyumba kuhamia.
Ujenzi wa ndani ya choo ukiendelea na mmoja
wa wasaidizi wa wasanii wa nyumba hiyo.
Upande wa dirisha moja-wapo kati ya
madirisha ya nyumba hiyo.
Kiti cha kupumzikia kikiwekwa vizuri katika
kona ya nyumba
Utakapotembelea Baltic Sea Island, Usedom,
Germany, usije ukashtuka ukiona hiyo nyumba kama ambayo iliyopeperushwa
na upepo au iliyopeperushwa na kimbunga.
Madhumuni ya nyumba hiyo ni moja ya kuvutia
watalii katika mji huo na watalii watapata fursa ya kujisikia wakiwa
wakitembea ndani ya nyumba hiyo kama wakining'inia kichwa chini miguu
juu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni