Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Mei 23, 2012

Hellow Wote Mtandaoni...!!.


Tahadhari: Rangi ya Tshirt haihusiani na Chama chochote cha kisiasa. Ni kwa kuwa tulikosa rangi nyingine wakati tumeamua kuprint kwa ajili ya ACAPPELLA KWANZA.
 
Ni yangu imani kuwa haujambo msomaji wa blog hii.
Ni kwa siku nyingi nimekuwa kimya bila kuendeleza nia ya fikra zangu.
 
Namshukuru Mungu kwa jinsi anavyoendelea kuniweka katika namna ambayo kwa hakika sikuitaraji....kwa ufupi napenda kusema nimerejea tena.
 
MUZIKI WA ACAPPELLA NDIO JAMBO AMBALO LIMENICHUKULIA MDA WANGU MWINGI LENGO NIKUUFANIKISHA KWA KUUFIKISHA KATIKA NGAZI ILIYOFIKIWA.

Jumanne, Mei 22, 2012

HISIA HARIBIFU NA MAHUSIANO MAPYA



Msingi wa tiba mbadala (Alternative medicine) tofauti na tiba ya jadi (traditional medicine) na tiba ya hospitalini (Converntional medicine) ni kuwa 'Mgonjwa/mtu atibiwe kwanza na ugonjwa wake ufuatie baadaye' .

Msingi hasa wa kumtibu mgonjwa unaanzia kwenye mahusiano mapya na hisia haribifu za maisha yake ya kila siku KIMATENDO.


Kitu hasa cha kufanya ni hiki: TAMBUA BILA KUKWEPA , Hisia haribifu kila zinapojitokeza: Hiyo inatosha kabisa. Utakuwa umeshamaliza wajibu wako kwa Utambuzi huo!

Hasira, woga, chuki, wasiwasi na hisia haribifu nyingine, Zikijitokeza na kurudia tena na tena, tumia NGUVU YA UTAMBUZI wako kwa kupitia machapisho yahusuyo masuala ya kiroho ama nyimbo za injili zilizotulia, mfano; Gospel Classics. Hii itasaidia kuzitambua tena na tena. Usichoke! Jenga tabia ya kudumu ya kuzitambua tena na tena, kila zikijitokeza na kuzipuuzia mara moja!

Fanya hivyo kwa utulivu na utaratibu, usigombane nazo, kuvutana wala kupambana na hisia haribifu. Zitambue, tizama, tambua-tena, TULIA! Alafu endelea na shughuli zako. Jenga mazoea hayo ya kiutu, busara na hekima. Kuzitambua, kujiachamanisha na kuzipuuzia kwa utulivu! Ikiwezekana fanya tabia hiyo kuwa mtindo wa maisha yako yaani KUMUOMBA MUNGU MARA NYINGI NYINGI!

Hisia haribifu ni nyonge na dhaifu kwa UTAMBUZI wa mtu anayezitizama na KUTAMBUA TU , zimefichuliwa, zina- AIBIKA kwa hatua ulizochokua. Udhibiti wa namna hii unaupa mwili nguvu hai iliyo msingi wa afya na tiba ya kweli kwa kizazi cha sasa!


Huu ndio ukweli na siri ya udhaifu wa hisia haribifu, Msingi wa tiba kwenye chanzo.
Tumia BIBLIA yaani soma NENO LA MUNGU 'Tulia na utambue'. Fanya zoezi la kujenga tafakari ya utambuzi na kudhoofisha hisia haribifu kwa njia hiyo MUNGU ATAKUSAIDIA.

Jumatatu, Mei 21, 2012

Sasa....Tukirejea: twatofautiana uelewa juu ya hili ama haya.



Hapa ntahitaji msaada kidogo 

Ninalomaanisha ni kuwa kama halijatokea kwako ama hujalisikia laweza kuendelea kuwa ndoto kwako, lakini kama ulishalisema kwa mtu na akaliona likitendeka huko aliko anaweza kuona ni ufunuo.
  
Unadhani ni mangapi unayaota usiku ama ulalapo na unashindwa kuyatendea kazi? 

Lakini, JE ni kweli kuwa hakuna haja ya kutilia maanani yale mema tuotayo? Je kuyasimulia?
Kumbuka yale upendayo ambayo umekuwa ukitamani kuota, na kujaribu kuyatekeleza licha ya KUTHUBUTU lakini hukupata nafasi ya kujaribu.

Jumatano, Mei 16, 2012

Nyumba Ilivyopinduliwa na Wasanii Juu Chini Yani

 Pichani juu ni kazi ya Wasanii wa ujenzi, bwana Klaudiusz Golos na Sebastian Mikiciuk, ambao wameamua kujenga nyumba ambayo fikira yake ni kuigeuza juu-chini, chini-juu kama ionekanavyo pichani.

Ujenzi wa ndani ya jiko ukiendelea na mmoja wa wasaidizi wa nyumba hiyo.
  
 
Ujenzi wa sehemu ya kulia chakula ukipata ukarabati na ribiti za mwisho mwisho.
 
 Sofa la kukalia likiwa katika marekebisho ya mwisho mwisho katika sehemu ya kupumzikia ya nyumba hiyo.
 
Choo kinapata vipodozi vya mwisho mwisho na mmoja wa wasaidizi wa ujenzi.
  
  Jikoni kunapata vipodozi vya mwisho mwisho kabla wenye nyumba kuhamia.

  Ujenzi wa ndani ya choo ukiendelea na mmoja wa wasaidizi wa wasanii wa nyumba hiyo.
  
Upande wa dirisha moja-wapo kati ya madirisha ya nyumba hiyo.
  
 
 Kiti cha kupumzikia kikiwekwa vizuri katika kona ya nyumba
   
 Utakapotembelea Baltic Sea Island, Usedom, Germany, usije ukashtuka ukiona hiyo nyumba kama ambayo iliyopeperushwa na upepo au iliyopeperushwa na kimbunga.
Madhumuni ya nyumba hiyo ni moja ya kuvutia watalii katika mji huo na watalii watapata fursa ya kujisikia wakiwa wakitembea ndani ya nyumba hiyo kama wakining'inia kichwa chini miguu juu.

Jumanne, Mei 15, 2012

UNAPOKUWA KATIKA HALI YA UPWEKE

Picha kwa hisani ya: www.blogs.suntimes.com
Ni hali inayoathiri namna mtu anavyofikiria kuhisi na hata anavyotenda matendo yake. Mtu aliyeathiriwa na hali hii huwa na shida ya kutambua mambo ya kufikiri tu na yale ya maisha halisi. Huenda hata wasiitike wakiituwa na wana shida kusema namna wanavyohisi katika hafla za kufangamana.

Hali hii si nafsi moja au nyingi. Watu wengi wakiwa na hali hii huwa si wabaya wa kujiumiza au kuumiza wengine. Haisababishwi na hali aliyoipitia katika utoto, malezi mabaya na kukosa moyo wa kufanya mambo sababu haijajulikana haswa. Sababu inaweza kuwa ya kuurithishwa katika familia, hali ya kizinaa na shida za kukosa kinga.

Kila mtu huwa na dalili zake za kipekee. Zinaweza kujitokeza polepole kwa muda wa miezi ama miaka ama hata itokee tu ghafla bila kutarajiwa. Ugonjwa huu huweza kuwenda na kurudi.

Ni nini baadhi ya dalili zake? 
Kusikia ama kuona vitu ambavyo haviko
Kuhisi kuwa unaangaliwa kila mara
Kuongea ama kusema vitu ambavyo havina maana. (Havieleweki)
Kutojishughulisha na mambo ambayo ni ya muhimu sana
Kudidimia kimasomo au namna unavyofanya kazi
Kutojishughulisha na unadhifu au hata namna unavyofanana
Kutoonekana kabisa mahali ambapo watu wametengana
Maamuzi yasiyofaa, hasira, ama kuonesha hisia za kuogopa wale unaowapenda
Kushindwa kulala au kizingatia kufanya jambo
Tabia zisizokubalika au za kiajabuajabu
Kushikilia sana dini au mambo yaliyokuwa kawaida
Imani ya uwongo kuhusu uwezo na nguvu zako au umuhimu wako
Imani kuwa mengine wanathibiti matendo yako

Unatibuje hali hii? 
Wewe au mtu yeyote unayemjua aliye na dalili hizi kwa zaidi ya majuma mawili anaweza kupata msaada mara moja. Mpigie simu daktari, hospitali ama kwenye kituo cha kutibu wenda wazimu matibabu ya mapema huashiria matokeo mazuri ya baadaye.

Mtu akipata tiba ibayostahili anaweza kuishi vizuri kama mtu wa kawaida. Hali hii hutibiwa kwa dawa na kufanyishwa mazoezi, pamoja kupewa nasaha bora, ukijihusisha na vikundi vya kujisaidia na vituo pia.

Jumamosi, Mei 12, 2012

PETE YA NDOA WALA HAINA CHIMBUKO LA KIDINI

“Fuatana nami katika historia hii fupi na yenye ukweli juu ya chanzo cha Pete ya ndoa”.
Historia 

Kumekuwa na maswali mengi juu ya chanzo hasa cha pete hiyo inayotumiwa katika harakati za ndoa’.
Wale walio na matazamo hasi juu ya matumizi ya pete, wamekuwa na sababu mbalimbali za kutetea msimamo huo hasa ni ile sababu kuwa “pete inafanya wazo la upendo kuwa la kinadharia” na ushahidi wa nje kuliko kuwa na chimbuko halisi la upendo wa ndani ya moyo. Lakini katika makala hii tutaona kwa kina juu ya historia halisi pete.

Pete ya ndoa ilianzishwa na watu wa Farao” Firauni” nchini Misri.
Historia inaonyesha kuwa karne ya 14, BC (kabla ya kristo), katika nchi hiyo ya Misri iliyo kaskazini mwa Afrika, watu wanchi hiyo chini ya mfalme wao Farao’ walianzisha utamaduni wa kuwekeana viapo vya uaminifu katika mahusiano yao ya kimapenzi na ndoa kwa kutumia pete.
Wananchi walilazimika kwenda kwenye ukingo wa Mto Nile ambapo huko walifanya matambiko ya kipagani na kuwekeana viapo vya uaminifu. Sherehe hiyo iliambatana na kuvalishana pete yenye umbo la duara baina ya mke na mume kwenye vidole vyao vya mkono wa kushoto.

Lengo, Maana yake’
Kwa kufanya hivyo wapagani wa Misri waliamini kuwa wameweka kiapo na ahadi ya kuto salitiana ambapo pia ilifuatiwa na kumvalisha mwanamke mkufu wa fedha na dhahabu au chuma kiunoni.
Umbo la duara la pete liliundwa hivyo kuashiria kuwa kifungo hicho cha ndoa ni cha milele kwa maisha yote.

Umbo la duara la pete na upagani’
Umbo hilo la duara la pete liliashiria imani kuwa viapo hivyo vilishuhudiwa na miungu miwili ya wamisri yaani mungu Jua’ na Mwezi ambao alama zake zilikuwa ni umbo hilo la duara la pete.
Pia uwazi huo wa pete “duara ya kati” ilimaanisha kuwa ndiyo mlango wa kuingilia katika maisha ya ndoa” na yakuwa ndoa hiyo na familia ijayo vinalindwa na miungu hiyo Jua’ na Mwezi daima.

Eneo la kuvaa pete na chimbuko lake’
Uamuzi wa kuvaa pete kwenye “kidole” kinachoitwa cha “Pete” ulifanyika kutokana na ushauri wa watalamu wa Sanyansi ya maumbile ya mwanadamu.
Wataalamu hao waliamini kuwa mshipa mkuu wa damu unaogawa damu mwilini toka moyoni (vein) unaunganika moja kwa moja na kidole hicho, hivyo pamoja na elimu ya kinajimu iliyotawala wakati huo bado ilishauriwa kuwa pete hiyo ivaliwe katika kidole hicho.

Kuenea kwa tendo hilo la uvaaji pete
Utamaduni huu wa kuvaa pete ulianza kuenea duniani baada mfalme Alexander, kuvamia nchi ya Misri, ambapo mambo yalovutia utawala huo ni pete ya ndoa.
Baadae Wagiriki walichukua utamaduni huo na kuubadilisha kidogo huku wakiwa na hofu ya kuwaudhi miungu hao Jua na Mwezi.

Miongoni mwa mambo yalofanywa kuhamasisha matumizi ya pete hiyo ni tendo la kuibadilisha jina na kuiita pete hiyo jina la kigiriki “evena amoris” yaani mshipa wa penzi” na kuruhusu itengenezwe kwa matirio tofauti kama pembe za ndovu, mifupa ya miguu, ngozi za wanyama nk.

SWALI:
Leo hii watoto wa Mungu wamechukua ibada hiyo’ na kuiweka katika maisha yao??????

“Unapovaa pete’ fanya ukijua kuwa haina chimbuko takatifu’