Tunauafiki mswaada mzuri kuhusiana na somo hili ulioandaliwa na kuwasilishwa na mchungaji Rei Kesis – Chaplensia wa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki (EUAB), akishirikiana na Idara ya Tiolojia ya UEAB, chini ya usimamizi wa mwenyekiti waIdara – Dr. Lameck Miyayo. Ilikuwa ni kazi njema na tuliyahimiza makanisa yetu yote kunufaika nayo. Unaweza kuupata kwenye ufunguo wa waraka huu.
Katika sehemu hii tutajielekeza kwenye uelewa wa Kanisa la Waadventista Wasabato, kuhusiana na nafasi na usimamizi wa muziki kwenye huduma za ibada. Tutaiangalia Kanuni ya Kanisa, ambacho ni kitabu cha msingi cha sera chenye viwango na kawaida za kanisa zinazotumika kusimamia makanisa yote mawili; lile la mahalia na yale ya ngazi za juu.
Kanuni hizi zilizopo kwenye kanuni za kanisa, zilizojengwa kwenye Biblia na zilizojikita kwa Kristo zinawakilisha uelewa wa kanisa wa wakati huu, kuhusiana na maswala mbalimbali ya kanisa yanayoathiri mahusiano yetu, kama mwili wa waumini, na kama mtu mmoja mmoja. Tunawasihi watumiaji wote wa muziki na viongozi wa kanisa kuwa na hamasa kubwa ya kuelewa kanuni hizi na kuzisimamia kama walinzi waaminifu wa kuta za Zayuni.
Kile Kanuni ya Kanisa inachosema kuhusu Muziki
Angalizo: Nukuu
imechukuliwa kutoka “Kanuni ya Kanisa la Waadventista Wasabato ya 2010,
toleo la Kiingereza. Kupigiwa mistari, kukolezwa kwa wino na mlalo wa
maandishi vimeongezwa. Maoni ni mapendekezo na maelekezo yetu ya
uongozi.
“Muziki ni mojawapo ya sanaa ya kiwango cha juu sana. Muziki mzuri si tu unatupatia maburudisho bali pia huyainua mawazo yetu na kukuza viwango vyetu bora. Mungu mara nyingi ametumia nyimbo za kiroho kugusa mioyo ya wadhambi na kuwaongoza kwenye toba. Kinyume chake, muziki duni unashusha hali ya kiroho na kutupeleka mbali na mahusiano yetu na Mungu.” – (CM, 143)
“Ni lazima tutumie uangalifu mkubwa katika uchaguzi wa nyimbo majumbani mwetu, kwenye mikusanyiko ya kijamii, mashuleni, na makanisani. Mrindimo wowote wenye vionjo vya jazz, rock, au mtindo uliochanganya hayo, au lugha yoyote inayooonesha hisia za kipumbavu au zisizo na maana itaepukwa.” – (Angalia CM, pp. 92, 96, 143.)
MAONI:
- “Kuimba, kama sehemu ya huduma ya kidini, ni tendo la ibada kama lilivyo ombi.” Patriachs and Prophets Uk. 594. Maombi hukuza tabia kwa sababu kupitia maombi tunauona uso wa Yesu, na kwa kumwangali tunabadilishwa na kufanana naye. Muziki mzuri ni wakala wa ujenzi wa tabia. (2 Wakorintho 3:18).
- Muziki wa Jazz, Rock au mtindo uliochanganya hayo mawili haipaswi kuruhusiwa makanisani.
- Angalia kwa makini tuni, mwafaka, na mrindimo; haya yote hayapaswi kufuata muziki wa kidunia.
MAONI
- Mwongozaji wa nyimbo ongoza vema. Epuke makosa ya kawaida.
- Mwongozaji anahitaji kuwa na yafuatayo: Kitabu cha nyimbo chenye alama za muziki za tonic sol-fa au staff notation, chombo cha kuchagulia key kiitwacho Pitch pipe, na kipande cha fimbo kwa kuongozea kunakoonekana na wote.
- Matumizi ya ala za muziki yameruhusiwa. Matumizi mabaya yamekatazwa. Ni afadhali kutotumia ala kabisa kuliko kutumia vibaya na kuwa mtego na laana kwenye ibada kwako mwenyewe na waabuduo wengine.
MAONI
- Huduma zetu za ibada hazipaswi kuongozwa au kuhudumiwa na waimbaji wasiomwabudu Mungu wa kweli katika njia ya kweli.
- Muda mwingi unahitaji kutumika kwa uimbaji wa wote, na muda mchache unapaswa kutumika kwa kwaya na vikundi vya uimbaji. Kila Sabato kabla ya vipindi vya Shule ya Sabato, hebu kuwe na angalau dakika za kuimba na kujifunza nyimbo mpya. Dakika 15 zingine zinapaswa kuwa baada ya Shule ya Sabato na kabla ya huduma kuu. Hebu dakika 15 zitengwe baada ya shule ya sabato na kabla ya ibada kuu kwa ajili ya uimbaji wa pamoja. Ratiba ya kwaya na vikundi vya nyimbo iendelezwe ili kuzipa kwaya fursa ya kuimba pamoja na nyimbo nyingine zilizoandaliwa. Ratiba ihusishe ibada za maombi ya katikati ya juma na ufunguzi wa Sabato. Kwaya zinapokuwa nyingi, usiendekeze maombi mengi ya kutaka nyimbo zilizoimbwa au zile zinazopendwa sana zirudiwe. Hii itumike kunapokuwa na kwaya nyingi zinazosubiri zamu yao ya kuimba.
Shule ya Sabato:
“Baraza linaweza kumteua Mkurugenzi wa Muziki wa Shue ya Sabato kwa kushauriana na viongozi wa vitengo. Kama namna ya kuonyesha ibada, muziki unapaswa kumtukuza Mungu. Waimbaji na wanamuziki wengine wanapaswa kuchaguliwa kwa uangalifu kama viongozi wa maeneo mengine ya huduma za Shule ya Sabato na wanapaswa kupimwa kwa viwango vilevile. (Angalia uk. 92, 144). Baraza pia linaweza kumteua mpiga kinanda wa vitengo vingine”. (CM, uk. 96)
Vijana Waadventista:
Maafisa wa AYS – “Kanisa huwachagua maafisa hawa wa AYS: Kiongozi wa Vijana, msaidizi wa kiongozi wa vijana, Katibu-mtunza hazina, msaidizi wa Katibu-mtunza hazina, mwongozaji wa nyimbo, mpiga kinanda, na mdhamini (ambaye anaweza kuwa mzee). Kwa kuwa muziki unachukua nafasi muhimu katika kuunda tabia za vijana, waimbaji hawana budi wachaguliwe kwa uangalifu kama maafisa wengine wa AYS”. (Angalia uk. 92, 96.) (CM, 102)
Kuchagua Waratibu wa Muziki – “Kanisa ni lazima lichukue uangalifu mkubwa katika kuwachagua viongozi wa kwaya, ikiwachagua wale tu waliojitoa kabisa na wanaotoa nyimbo sahihi kwa huduma zote za ibada za kanisa na mikutano. Muziki wa kidunia au ule wenye asili iletayo maswali, kamwe usiingizwe kwenye huduma zetu.” (CM, 92).
“Viongozi wa nyimbo ni lazima wafanye kazi kwa ukaribu sana na wachungaji na wazee wa makanisa ili kwamba uchaguzi wa nyimbo uoane na wazo kuu la hubiri. Kiongozi huyu wa nyimbo yupo chini ya usimamizi wa mchungaji au wazee wa kanisa na hafanyi kazi kwa kujitegemea. Kiongozi wa nyimbo anapaswa kushauriana nao kuhusu nyimbo zitakazoimbwa na uteuzi wa waimbaji na wanamuziki.” – (CM, uk. 92)
Idara na Huduma zinatakiwa kuteua Wakurugenzi wa muziki, na kulitaarifu baraza la kanisa ili liwapitishe wale waliochaguliwa. Uchaguzi wa viongozi wa muziki wa idara za Shule ya Sabato na Vijana umefafanuliwa na kusisitizwa.
Uangalifu mkubwa utumike katika kuchagua viongozi wa muziki makanisani. Baraza la kanisa ni lazima libatilishe/liidhinishe viongozi wote wa vikundi/kwaya zote ambazo kanisa limevisajili. Kila idara ichague kiongozi wake na kupeleka kwenye baraza la Kanisa ili kubatilisha au kuidhinisha..
Kanisa linaweza kuwa na viongozi kadhaa wa muziki wanaoongoza nyimbo kwenye idara zao, huduma, au makundi. Lakini kanisa ni lazima lichague mkurugenzi mmoja wa muziki, msaidizi/wasaidizi, kutegemeana na mahitaji ya kanisa, watakaoratibu viongozi wengine wote wa muziki kutoka idara mbalimbali za kanisa, huduma au vikundi. (CM, 171).
Mratibu wa muziki ni mjumbe wa baraza la kanisa. – (CM, 125). Huchaguliwa na kibaraza cha uchaguzi. (CM, uk. 171)
Mkurugenzi/Mratibu/Kiongozi (Mratibu Mkuu) wa muziki wa kanisa):
- Ni mjumbe wa baraza la kanisa.
- Ni lazima apimwe na kiwango kile kile cha juu kilichotumika kuwachagua viongozi wengine wa kanisa.
- Ni kiongozi muhimu asaidiaye maandalizi ya ibada. Hufanya kazi chini ya “Msimamizi wa Mimbari/Ibada”. – (Wachungaji na Wazee wa Kanisa)
- Ndiye anayepaswa kuchagua nyimbo na waimbaji watakaoendana na wazo kuu la hubiri la siku hiyo.
- Ndiye atakayeandaa ratiba ya Kwaya (waimbaji)/Vikundi vya Waimbaji, Waimbishaji, na Ala za muziki ikiwa zitakuwepo.
- Ndiye atakayehamasisha na kusimamia filosofia ya Biblia/Kanisa kuhusu muziki.
- Makanisa yaweza kuunda Kamati ya Muziki itakazoongozwa na Mratibu wa Muziki wa Kanisa itakayosimamia huduma za muziki kanisani. Wajumbe wa baraza hili wanaweza kuwa wasaidizi wa Mratibu mkuu (anaweza pia kutumika kama katibu wa kamati), waratibu wa muziki kutoka kwenye maidara, na viongozi wakuu wa kwaya. Wajumbe wengine wanaweza kuwa viongozi wa Chama cha Vijana, Mkurugenzi wa Huduma za Watoto, na Mkurugenzi wa Huma za Washiriki. Mzee wa kanisa na mchungaji ni maafisa wa kamati hii.
- Ukubwa wa kamati utategemea ukubwa na mahitaji ya kanisa. Kamati itafanya vizuri kazi yake kama itakutana walau mara moja kwa mwezi. Baraza la kanisa linaweza kukasimu baadhi ya mambo mepesi yahusianayo na muziki kwa kamati hii.
Makanisa yanaweza kuwa na kwaya nyingi. Kuwa na kwaya ya watoto ni njia ya kuwasaidia kuwalea kiroho, kuwaunganisha na familia ya kanisa, na kuwashirikisha kwenye ushuhudiaji. (CM, uk. 92)
MAONI
- Waimbaji ni lazima wachaguliwe na kanisa
- Kanisa ni lazima lisajili kwaya/vikundi vya uimbaji kwa kuwachagua waimbaji na kuwabatilisha/kuwaidhinisha viongozi.
- Kwa kuwa waimbaji ni wahubiri, ni lazima wawe kielelezo, hasa katika mwonekano na mavazi.
- Waimbaji ni lazima wawe waongofu wa kweli. Kwaya na Vikundi vingi vya uimbaji ni maskani ya Mwovu. Vimejaa wivu, majivuno, migogoro, mashindano, uzinzi, uasherati, ubinafsi n.k.
- Hebu na wajiundie sheria na kanuni zao wenyewe. Kanisa lijiepusha kutunga na kusimamia sheria kwa waimbaji. Kanuni ya kanisa imetoa viwango vya kutosha, hebu kanisa livitumie hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni