Ili
watokezeshe gari lenye nguvu, lisilotumia nishati nyingi, na lisiloharibu
mazingira, wanasayansi walichunguza eneo ambalo wengi hawakutarajia,
chini ya bahari! Samaki anayeitwa boxfish
anayepatikana kwenye matumbawe yaliyo kwenye bahari za tropiki ana
muundo unaofaa kutengeneza gari jepesi, linaloenda kwa kasi na kutumia
nishati kidogo.
Fikiria hili:
Samaki huyo anaweza kuogelea kwa kasi akisonga umbali unaolingana na
mara sita ya urefu wa mwili wake kwa sekunde. Lakini hatumii nguvu ili
asonge kasi hivyo. Umbo lake humwezesha kusonga kwa kasi bila kutumia
nishati nyingi. Wahandisi walitengeneza gari lenye muundo wa samaki huyo
na kulijaribu kwenye barabara yenye upepo mkali iliyo chini ya ardhi na
wakagundua kwamba gari hilo hukata upepo kwa njia bora zaidi kuliko
magari mengine.
Samaki huyo ana ngozi ya nje yenye mifupa ambayo
humfanya asonge kwa nguvu lakini bado awe mwepesi. Maji yanayozunguka
kwa kasi kando ya samaki huyo humfanya asiyumbeyumbe bahari
inapochafuka. Kwa hiyo, samaki huyo ana uwezo mkubwa wa kudhibiti mwili
wake hata anaposonga kwa kasi na anakingwa asiumie.
Wahandisi
wanaamini kwamba samaki huyo atawasaidia kutokeza gari salama, jepesi,
na lisilotumia mafuta mengi. Dakt. Thomas Weber, mtafiti na mbuni
anasema hivi: “Kusema kweli tulishangazwa kwamba kati ya viumbe wote,
samaki huyo anayeonekana mzembe ndiye angechaguliwa kutokeza muundo wa
gari linaloenda kwa kasi na kutumia nishati kidogo.”
Una maoni gani? Je, samaki huyo anayetumia nishati yake vizuri alijitokeza mwenyewe? Au alibuniwa?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni