Kwa
mwaka uliopita, tumeanzisha vipengele na vidhibiti vipya ili kukusaidia
kupata mengi kutoka kwa Facebook, na tumewasikiliza watu ambao
wametuomba tufafanue zaidi tunavyopata na kutumia maelezo.
Sasa, ukiwa na Misingi ya Faragha, utapata vidokezo na mwongozo wa jinsi ya kufanya kwa kushughulikia uzoefu wako kwenye Facebook. Pia tunasasisha masharti, sera ya data na sera yetu ya vidakuzi ili kuonyesha vipengele vipya ambavyo tumekuwa tukivishughulikia na kuvirahisisha kueleweka. Na tunazindua maboresho kwenye matangazo kulingana na programu na tovuti unazotumia nje ya Facebook (matangazo ya kitabia za mtandaoni) na kukudhibiti.
Visasisho hivi vinaanza kutumika Januari, 1, 2015. Kama kawaida, tunakaribisha maoniyako kuhusu sera zetu.
Misingi ya Faragha
Misingi
ya Faragha hutoa mwongozo ingiliani wa kujibu maswali mengi
yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu jinsi unavyoweza kudhibiti maelezo
yako kwenye Facebook. Kwa mfano, unaweza kujifunza kuhusu kuondoa
utambulisho, kuondoa urafiki, kuzuia na jinsi ya kuchagua hadhirira kwa
kila chapisho lako. Maelezo haya yanapatikana kwa lugha 36.
Pamoja na ukaguzi wetu wa sera, ukumbusho kwa watu wanaochapisha kwa umma na wateuzi wa hadhira rahisi, Misingi ya Faragha ni hatua ya sasa tuliyoichukua ili kukusaidia kuhakikisha kuwa unashiriki na watu unaotaka.
Kukusaidia kupata mengi kutoka kwa Facebook
Kila
siku, watu hutumia programu na huduma zetu kuunganika na watu, maeneo
na vitu wanavyovijali. Visasisho kwa sera zetu vinaonyesha bidhaa mpya
tulivyokuwa tukivishughulikia ili kuboesha uzoefu wako wa Facebook. Pia
vinaelezea jinsi ambavyo huduma zetu hufanya kazi kwa njia rahisi ya
kuelewa. Hapa kuna baadhi ya viangazio:
- Gundua kinachoendelea karibu na wewe:Tunasasisha sera zetu ili kufafanua jinsi tunavyopata maelezo ya eneo kulingana na vipengele unavyotumia kutumia. Mamilioni ya watu huingia katika maeneo wanayopenda na kutumia vipengele vya hiari kama Marafiki wa Karibu (inapatikana tu katika baadhi ya maeneo). Tunashughulikia njia za kukuonyesha maelezo yanayofaa zaidi kulingana na mahali ulipo na yale marafiki wako wanayafanya. Kwa mfano, baadaye, ukiamua kushiriki uko wapi, unaweza kuona menyu kutoka kwa mikahawa iliyo karibu au visasisho kutoka kwa marafiki katika eneo.
- Kufanya ununuzi kuwa rahisi zaidi:Katika baadhi ya maeneo, tunajaribu kitufe cha Nunua ambacho huwasaidia watu kugundua na kununua bidhaa kutoka kwa makampuni mengine bila kuondoka kwa Facebook. Pia tunashughulikia nia mpya za kufanya miamala hata kwa urahisi zaidi.
- Pata maelezo kuhusu faragha kwenye Facebook wakati unahitaji.Ili kuvifanya kupatika zaidi, tulihamisha vidokezo na mapendekezo kwa Misingi ya Faragha. Serea yetu ya data ni fupi na wazi zaidi, kwa hivyo kuifanya iwe rahisi zaidi kusoma.
- Fahamu jinsi tunavyotumia maelezo tunayoyapokea.Kwa mfano, kufahamu nguvu ya betri na mawimbi husaidia kuhakikisha programu zetu zinafanya kazi vizuri kwenye kifaa chako. Tunaomba idhini ili kutumia eneo lako la simu tunapotoa vipengele vya hiari kama kuingia au kuongeza eneo lako la machapisho.
- Jua familia ya kampuni na programu za Facebook zinazofanya kazi pamoja.Kwa miaka michache iliyopita, Facebook imekua na tunataka kuhakikisha unajua kuhusu familia yetu ya makampuni, programu na huduma. Tunatumia maelezo tunayokusanya kuboresha uzoefu wako. Kwa mfano, ikiwa umefungiwa nje ya akaunti yako ya Instagram, unaweza kutumia maelezo yako ya Facebook kupata nenosiri lako. Hakuna chochote katika visasisho vyetu hubadilisha ahadi ambayo Instragram, WahatsApp na makampuni mengine imetoa ili kulinda maelezo yako na faragha yako.
- Maelezo yako na utangazaji:Wakati mwingine watu huuliza jinsi maelezo yao husambazwa kwa watangazaji. Hakuna jambo linalobadilika kwa visasishi hivi—tunawasaidia watangazaji kufikia watu kwa matangazo muhimu bila kuwaambia wewe ni nani.
Kukupata udhibiti zaidi wa matangazo
Tumesikia
kutoka kwa baadhi yenu kwamba inawezakuwa vigumu kudhibiti aina za
matangazo unazoona ukitumia vifaa na vivinjari tofauti. Hapo awali,
ikiwa ungechagua kutoka kwenye aina fulani za matangazo kwenye kompyuta
yako ndogo, chaguo hilo huenda halikutekelezwa kwenye simu yako. Tunajua
kuwa watu wengi wanatumia zaidi ya simu moja, kompyuta ndogo au
kivinjari ili kufikia Facebook, kwa hivyo inafaa kuwa rahisi kwako
kufanya chaguo moja linalotekelezwa kwenye vifaa vyako vyote.
Hiyo ndiyo maana Facebook uheshimu chaguo unalofanya kuhusu matangazo unayoona, kwenye kila kifaa. Unaweza kuchagua kutoka kuona matangazo kwenye Facebook kulingana na programu na tovuti unazotumia kupitia Muungano wa Matangazo ya Dijitali.
Unaweza pia kuchagua kutoka kwa kutumia vidhibiti kwenye iOS na
Android. Unapotueleza hutaki kuona matangazo ya aina hii, uamuzi wako
hutumika kiotomatiki kwa kila kifaa unachokitumia kufikia Facebook. Pia,
sasa tunatengeneza mapendeleo ya matangazo yapatikane katika nchi zaidi, kuanzia Australia, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Ayalandi na Uingereza.
Tunatumaini
visasisho hivi vitaboresha matumizi yako. Kulinda maelezo ya watu na
kutoa vidhibiti maalum vya ufaragha tunavipa kipaumbele, na tunaamini
matangazo haya ni hatua muhimu.
Chanzo: INGIA HAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni