Mhandisi wa TCRA,Andrew Kisaka akiwasilisha Mada kuhusu maadili ya Uandishi na Utangazaji wa Habari |
Serikali
imewataka wamiliki na waandishi wa blog nchini kuzingatia maadili ya taaluma ya
uandishi wa habari wakati wa mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali
za mitaa mwezi ujao na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Wamiliki wa blog mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo |
Akizungumza
jijini Dar es salaam hii leo wakati wa ufungaji wa mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) na Wamiliki wa blog mbalimbali nchini Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Tanzania Assah Mwambene amesema
serikali inatambua blog zinafanya kazi ya kutoa habari sawa na vyombo vingine
vya habari lakini vinapaswa kuzingatia uandishi wa mambo ya msingi kwa kufuata
maadili ya uandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo nchini Tanzania Assah Mwambene |
Mwambene
ambaye pia ni Msemaji wa serikali ameeleza kuwa lazima wamiliki na waandishi wa
blog wajue wamechukua wajibu mkubwa unaoendana na wajibu wa kuwajibika kwa
wananchi wanaowandikia habari wa kuzingatia
maadili.
Kamati ya muda ya wamiliki wa blog iliyochaguliwa leo |
Awali
akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Habbi Gunze
amesema waandishi na wamiliki wa blog wananafasi ya kusaidia umma kuweza
kuelewa masuala mbalimbali ya uchaguzi pasipo upendeleo wowote wala uchochezi.
Mwenyekiti wa Kamati ya wamiliki wa blog Joachim Mushi |
Kumekua na
malalamiko toka kwa wananchi kutokana na
habari mbalimbali zinazoandikwa kwenye baadhi ya blog kwa
kutozingatia maadili ya uandishi wa habari na utamaduni wa mtanzania jambo ambalo
ni changamoto kwa serikali kutokana na uhuru uliopo kwa wamiliki wa blogi hizo
na ukosefu wa sheria zinazowaongoza.
Chanzo: Maisha Na Teknohama
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni