John Shabani akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake wa sauti
(SIFA NA MBINU ZA KUWA MWIMBAJI BORA)
SINGING COURSE
Jinsi ya kuponya na kutunza Sauti yako
Weka
sauti yako katika afya nzuri ili uweze kuendelea kuimba!
Kila mtu anaweza kutumia sauti yake, lakini
si kila mtu anajua jinsi ya kutunza afya ya sauti yake, au nini cha kufanya kunapotokea tatizo katika sauti. Makala hii itasaidia kila mtu kujifunza jinsi ya kuponya
sauti zao na pia kutoa ushauri wa jinsi ya kutunza afya yake na kuwa nguvu ile ile
kwa ajili ya siku zijazo.
Mambo unayo hitaji au ya kuzingatia kama mwimbaji
- maji kwa uwingi
- ngumu pipi, mints, nk
- mvuke (moto oga)
- Koo kanzu chai
- asali
- limao
Maelekezo
o
1 Kama sauti yako imejeruhiwa, jambo muhimu zaidi la kufanya hivi sasa ni
kuacha kutumia kwa muda. Sauti inahitaji kupumzika pia. Punguza mazungumzo yako na hasa kupayuka na kupaza sauti,
kujifunza kuzungumza zaidi kwa ufupi, na kutumia zaidi kidogo muda katika
ukimya.
o 2 Jambo jingine kubwa
ambalo husaidia sauti iliojeruhiwa ni chai ya moto pamoja na limau kidogo na asali. chai nzuri ni ile iliyo shauriwa ki afya na si kila chai ni bora. Unaweza kupata na dawa za mitishamba katika duka
la dawa, ambazo ni maalumu kwa ajili ya
sauti, Kunywa angalau kikombe asubuhi na kikombe wakati wa usiku.
MAFUNZO YA SAUTI
By John Shabani
Mobile: 0716560094, 0754818767
Facebook: John Shabani
Mambo ya msingi yanayofunzishwa katika program hii:
Ø
Historia
ya uimbaji
Ø
Tofauti
ya mwimbaji na mwanamuziki
Ø
Vyakula
na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa
Ø
Sifa
na mbinu za kuwa mwimbaji bora
Ø
Jinsi
ya kuitunza na kuiponya sauti yako
Ø
Amri
10 za sauti
Ø
Matumizi
ya kipaza sauti (Microphone technique)
Ø
Utunzi
wa nyimbo
Ø
Mazoezi
ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
Ø
Ushauri
kwa wanaotaka kurekodi nyimbo
Kuimba
ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia twaweza kusema ni kutamka
maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya muziki,
tuni) au ghani
Kama vile tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye
pia anazo ala mbili muhimu:
·
Mdomo wenye uwezo wa kutoa sauti ya
uimbaji
·
Mwili
Kumbuka
moja ya vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy) “As you sing
higher, you must need more energy, as you sing lower, you must useless”.
Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa na nguvu za kimwili unahitaji maji
ya kutosha, chakula kizuri pamoja na mazoezi ya viungo.
MAZOEZI NA FAIDA ZAKE
Pamoja na faida nyingi za
mazoezi lakini pia mazoezi huchangamsha mwili, hulainisha koo, husaidia kuwa na
pumzi ya kutosha, hukuhepusha au kupunguza baadhi ya magonjwa kama kisukari,
presha n.k, hung’arisha ngozi, na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu, MAZOEZI HUSAIDIA
KATIKA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA KUWA MZURI , KUKUPA NGUVU NA KUWEZA KUFANYA
KAZI KWA NGUVU ZAKO BILA KUJISKIA UMECHOKA NA MWISHO WA SIKU HUPUNGUZA MAFUTA
MWILINI, HUPUNGUZA UZITO, KUNYOOSHA NA
KUIMARISHA MISULI YA MWILI, HUSAIDIA MAPIGO MAZURI YA MOYO KWA KUONGEZA KASI YA
MAPIGO YAKE WAKATI WA MAZOEZI, UNGUZA MRUNDIKO WA DAMU KWENYE MISHIPA, HII NI
MUHIMU KWA SABABU MGANDO WA DAMU HUSABABISHA MAGONJWA YA MOYO PAMOJA NA
KUPOTEZA FAHAMU, MAZOEZI HUIMARISHA MIFUPA YA MWILI, HUBORESHA USINGIZI.
Fikiria mwenyewe kama mwanamichezo au mtu wa fani fulani na
jifunze kuwa mtu wa kula na kunywa kulingana na fani yako: Aina ya chakula na
kinywaji na muda wa kutumia ni jambo la
kuzingatia sana. Kula na kunywa ni muhimu lakini Jiepushe na ulafi kwani huleta
uchovu, mfumo wa kupumua kuathirika na wakati mwingine kusababisha magonjwa.
Kuna
misimu fulani kama msimu wa vumbi au baridi kali au alegi au matatizo mengine
kibao, wakati mwingine aina fulani ya dawa kwa ajili ya ugonjwa fulani, Wakati
mwingine husababisha mafua au kutokwa na kamasi mara kwa mara au kukausha koo
kabisa, hivyo husumbua sana na kuathiri mfumo wako wa kuimba. Wakati mwingine
mazingira ya shughuli au kazi tuzifanyazo au pia mazingira ya makazi huweza
kuathiri sauti zetu. Hivyo masomo ya utunzaji wa sauti ni ya muhimu sana.
Vilaji na vinywaji visivyofaa Kabla ya kuimba
Vilaji na vinywaji visivyofaa Kabla ya kuimba
Kuhusu chakula, ni muhimu ili kuepuka kuimba tumbo likuwatupu kabisa. Kuimba ni kama
riadha, inahitajika nguvu kwa ajili ya utendaji wako. Hata hivyo, ni muhimu pia
kuepuka kuimba tumbo likiwa limeshiba sana. Yapo madhara mengi yanayotokana na
shibe. Unaweza ukawasiliana na mwalimu wa sauti ili kujua madhara hayo. Kumbuka
kuimba ni kazi ngumu, unahitaji mafuta (you need fuel), hivyo inashauriwa kuwa
na mlo wa kawaida wa saa moja au mbili kabla ya uimbaji ni bora zaidi.
Kulingana na mazoea yetu vipo vyakula na vinywaji ambavyo ni
vigumu kuachana navyo ghafla, mengine huchukua muda. Lakini hata hivyo kwa
ajili ya kutunza koo (Mashine inayozalisha sauti) pamoja na kujihepusha na
madhara yanayoweza kujitokeza unapokuwa na shughuli nzito ya uimbaji, ni muhimu
ujihepushe navyo. Nitakuambia kwa ufupi kuhusu vyakula visivyofaha unapokuwa na
shughuli za uimbaji. Kwasababu za msingi si rahisi kukutajia kwa undani madhara
ya baadhi ya vyakula au vinywaji, wasiliana na mwalimu kwa wakati wako.
Baadhi ya vyakula na vinywaji vya kuepuka kabla ya kuimba ni
kama vile:
- Vinavyoleta mwasho au kukera koo (throat irritants): vyakula au vinywaji vinavyochangamsha, kusisimua au kulewesha (Overly spicy foods) , kama vile kahawa na pilipili, vinywaji baridi sana, sukari iliyosafishwa, chocolate.
- Jamii ya vitu vyenye alkoholi, Sigara, tumbako, bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya
·
Vyakula vinavyoongeza mucous (sehemu
ya kiwambo cha seli inayozunguka mfereji wa chakula): maziwa, koni,
malai/maziwa yenye ubarafu (ice cream), maziwa mgando na aina nyingine ya
maziwa (dairy products)
- Vyakula vinavyofanya koo kuwa kavu: matunda jamii ya machungwa, pombe
- Soda na aina ya vinywaji vinavyochemsha au vinavyojaza gesi au hewa katika tumbo
- Vyenye ubaridi sana au barafu: husababisha koo kubana, kuminywa au kunyongwa.
·
Vyakula vinywaji
vyenye ubarafu na pombe (ikiwa ni pamoja na mvinyo na bia). Kuna baadhi ya watu
pia huwa na alegi (kwa mfano, baadhi ya waimbaji wana shida na matunda jamii ya
machungwa, ngano, karanga, samakigamba au soya).
·
Vyakula vyenye mafuta mengi
Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na
katika uimbaji wako zingatia :
·
Punguza matumizi mengi ya sukari, ongeza matumizi ya
matunda
·
Punguza kula
nyama nyekundu, ongeza matumizi ya mbogamboga
·
Punguza matumizi
ya soda, ongeza matumizi ya maji
·
Punguza
kuendesha, ongeza kutembea kwa miguu
·
Punguza
kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa wakati
·
Punguza msongo
wa mawazo, ongeza kupumzika
Zingatia :
·
Maji ya moto au
aina ya chai mitishamba (herbal tea) ni bora, Mwimbaji mzuri hutumia class 8 za maji kwa siku,
wapo ambao hutumia hadi lita 4 pia yapo maji ya ziada kutoka katika vyakula.
·
Kupasha sauti kwa kukohowa kohowa
sio njia ya kukusaidia kuimba vizuri, badala yake
hukata sauti
·
Pamoja na umuhimu wa maji, lakini acha
matumizi ya maji mengi saa moja au mbili kabla ya kuanza uimbaji badala yake
asali ni bora zaidi. Lakini pia sauti ikipatwa na tatito unaruhusiwa kupata
maji ya moto pamoja na asali
·
Angalizo kuhusu mazoezi: Mazoezi huwa yana ugumu
wake hasa pale unapokuwa unaanza, usikate tamaa wala usikubali uvivu au maumivu
yakakurudisha nyuma. Jitengee muda maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi na
usianze kwa kufanya mazoezi magumu bali anza na mepesi mepesi ili kuupa mwili
nafasi ya ku-adopt mabadiliko
koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa na:
Aina fulani ya pipi, asali, mvuke,
chai fulani ya mitishamba au mchaichai, kusafisha koo kwa maji chumvi, baadhi
ya dawa kwa ushauri wa daktari n.k
Jinsi ya kulinda na kuiponya Sauti yako
Kila mtu anawezakuitumia sauti yake, lakini si
kila mtu anajua jinsi ya kuitunza au kuiponya inapopatwa na tatizo. afya yake,
au nini cha kufanya wakati si tu kufanya kazi haki. Makala hii itasaidia kila mtu kujifunza jinsi ya kuponya
sauti na pia kutoa ushauri wa jinsi ya
kuitunza na kuifanya kuwa na afya na nguvu kwa ajili ya siku zijazo
Masomo
haya yanawafaha walimu, wainjilisti, wanasiasa, wazazi, wanasheria, madaktari,
na waimbaji, na kila mtu ambaye shughuli zake hulazimi kakuongea sana.
·
Kama sauti yako imejeruhiwa
vibaya, basi jambo muhimu zaidi la kufanya sasa hivi ni kuacha kutumia hiyo
Sauti, ipumzishe. Punguza pia kuzungumza kwa muda mrefu na hasa kwa
kupaza sauti kubwa na kutumia muda kidogo zaidi katika
ukimya.
·
Jambo jingine kubwa ambayo husaidia sauti iliyojeruhiwa ni chai ya moto
(Kama vile coat tea). Unaweza kupata pia
dawa za mitishamba zilizohifadhiwa kitaalam katika maduka ya dawa,
lakini ikiwa dini yako au tamaduni yako haina shida katika hili. Kunywa angalau kikombe asubuhi na kikombe wakati wa usiku.
·
kama kuna kitu ambacho kinaweza kusaidia kuponya sauti yako na pia
inaweza kutumika kulinda kwa haraka ni
unywaji wa maji ya kila siku. Maji husaidia na sauti yako katika afya nzuri