Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Novemba 11, 2013

Je unamfahamu Ludwig van Beethoven? 
Alizaliwa 16 Desemba 1770 na kufariki 26 Machi 1827. Alikuwa mtungaji wa muziki na mpiga piano kutoka nchi ya Ujerumani.
Alizaliwa mjini Bonn akiwa mtoto wa mwanamuziki aliyemfundisha kinanda tangu utoto. 1787 akiwa kijana alisafiri Vienna iliyokuwa mji mkuu wa Dola Takatifu la Kiroma kwa matumaini ya kukutana na Wolfgang Amadeus Mozart akarudi 1792 alipopata mafunzo kuoka Joseph Haydn.

Tangu 1793 alikuwa maarufu mjini Vienna kama mpiga kinanda akaendelea kutunga muziki yake. Alipata usaidizi na wateja kati ya makabaila wa makao makuu ya Kaisari.

Tangu miaka ya 1796 alianza kupoteza uwezo wake wa kusikia wake akaendelea kuwa kiziwi lakini aliamua kuendelea na muziki yake. Kuna hadithi ya kwamba alioongoza simfonia ya tisa na mwishowe watu walimgeuza aangalie wasikilizaji kwa sababu hakusikia jinsi walivyopiga makofi.

Aliweza kuendelea kutunga na kuongoza musiki na kupiga piano. Alifunga fimbo kwenye kinanda akaishika kwa meno na kusikia tetemeko la piano kupitia fimbo na meno yake.

Aliaga dunia alipokuwa na umri wa miaka 57.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni