Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Septemba 04, 2012

UJENZI WA MIJI MIKUBWA

PHOTO BY: Projects cambodia

Ilianza katika kingo za mito. Miji ya kwanza ilijengwa India na Iraq Jiji la kale na maarufu lilikuwa Babeli. Tukizungumzia neno 'ustaarabu' tukumbuke kwamba ni tafsiri ya neno linalotokana na lugha ya Kiingereza ambalo maana yake ni 'kuishi katika miji mikubwa'.

Kabla ya watu hawajaanza kuishi katika vikundi, kila mtu ilimlazimu kujikaza katika kuongezeka mifugo au mavuno ili yeye mwenyewe pamoja na jamaa zake wasife kwa njaa. Lakini baadae binadamu walipojifunza kuishi pamoja kwa wingi, walipata kuendelea vema katika ufundi na ujuzi wa namna mbali mbali katika maisha yao. Kwa maana hiyo kila mtu aliweza kujizoeza kutenda kazi yake maalum na kapata kuifanya vema. Kufuatia hali hiyo kukaibuka wajenzi, wafanyakazi, wahunzi, washoni viatu, wavuvi, wachimba migodi, maserema, askari na wengine wengi.


Kwa hali hiyo kulikuwa na nyumba bora, viatu na vyombo madhubuti na watu wengi walikuwa katika hali iliyo njema zaidi, kwani waliweza kuishi maisha ya raha, walikuwa na mavazi bora ya kuvaa na ya kutumia tofauti na zama zilizokuwa za ukulima tu. Maeneo ya Afrika na nchi nyingine nyingi za mbali pia binadamu na mataifa walitengwa kwa sababu ya milima na bahari nao hawakupata kujifunza kujenga miji na kukaa pamoja, hivyo watu walidumu kukaa katika hali ile ile ya kutopata 'ustaarabu'. Hivi sasa duniani kuna miji mingi mikubwa tunayoishi ambayo kutokana na ukubwa wake mingine imefikia kuitwa au kupewa hadi ya kuwa majiji.


Lakini hata hivyo wakati watu wengi hivi sasa wanaishi ama kutembelea katika miji hiyo kama vile Jiji la Dar es Salaam, Nairobi, Kampala, Harare, Cairo, Lagos, New York, London, Moscow na mingineyo, bado hawafahamu nini hasa chimbuko la kukua kwa miji hiyo na msongamano wa watu na maisha ndani yake.


Kulingana na watafiti wa mambo ya historia na mazingira duniani, imethibitika kwamba miji mingi ambayo sasa ni majiji ilianzia katika kingo za mito mikubwa au kando ya bahari. Katika nchi ya India ambako leo hii kuna miji mingi mikubwa, imeonekana kuwa hapo kale kulikuwa na ustaarabu mwingi hasa kando ya kingo za mto Ganges (unaotamkwa Ganjiz) ambapo wenyeji wa huko walikuwa wakitengeneza vyombo na silaha zao kwa shaba nyeusi katika eneo hilo.


Hata hivyo katika utafiti huo hakukuwa na habari zaidi juu ya miji hiyo vile wakati huo binadamu walikuwa hawakuhifadhi kumbu kumbu ya maandishi ya mambo yao. Katika nchi ya Uchina ambako leo hii kuna idadi kubwa ya watu katika miji yake yote kuliko nchi nyingine dunani majiji yake yote mashuhuri ya sasa yalianzia kando ya kingo za mto mashuhuri unaoitwa Yang Tse Kiang.


Miji mingine mikuu ya zamani iliyokuwa maarufu ilikuwa katika nchi ya 'Mito Miwili' (Mesopotamia) ambayo sasa inaitwa Iraq na pia katika kingo za mto Nile huko Misri. Ni rahisi kufikiri kwamba kwa nini miji mikubwa iliyojengwa kando ya kingo za mito ilistawi haraka haraka. Mito hiyo mikubwa siku zote ilikuwa ikileta tope kwa wingi zilizofanya nchi kuneemeka zaidi hata ikawezesha mazao kumea kwa kurahisi. Tope hizo pia ziliweza kutengenezwa matofali kwa urahisi na kuanikwa juani, hivyo watu waliweza kujenga nyumba nzuri upesi.


Miji mikubwa ya dunia ambayo inatamba kwa uruzi na ukubwa hivi leo ni Beijing, Paris, Mexico City, New York, Berlin, Buenos Aires, New Delhi, Cairo, Mosco na Hong Kong, lakini mji mkubwa wa kale kabisa uliokuwa ukitamba ni Babeli. Katika mji huo ulikuwa akiishi mfalme maarufu aliyekuwa akiitwa Hammurabi ambaye baada ya kuujenga alikuwa akitoa sheria nyingi na kali kwa wakazi wa mji huo kuuenzi na kuuheshimu mji wao. Inaeleza kuwa mfalme huyo hakutaka watu wajenge holela kama ambavyo leo hii tunashuhudia katika Jiji letu pekee la Dar es Salaam.


Mfalme huyo aliyepata kutawala mji huo alimjengea bustani malkia wake ambaye aliona huzuni kwa sababu ya kukaa mabli na nchi yake, hivyo alijengewa bustani hizo kufurahisha. Inaelezwa katika vitabu kwamba bustani hizo zikawa na sifa katika dunia nzima ya kale ambapo pia fahari ama sifa nyingine katika mji huo wa kale ulikuwa na mkataba kubwa ya kusomea mfalme na wakazi wake, lakini vitabu vyake havikuwa vya karatasi, bali vyote vilikuwa vya mbao na undogo uliochomwa hata ukawa ngumu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni