Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Septemba 19, 2012

KONGAMANO LA MAISHA BORALile  kongamano la maisha bora, lililoandaliwa na Kanisa la Waadiventista Wasabato USHINDI kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kukabiliana na changamoto za maisha limeshaanza na hivi unavyosoma haya maandishi linaendelea.

Kanisa linatambua wajibu wake kwa jamii na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ili kukabiliana na changamoto hizo, kanisa limeandaa kongamano ambalo litachukua siku kumi kuanzia Septemba 17 hadi 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Kanisa la Waadventista kama sehemu ya jamii, tunatambua changamoto zinazoikabili nchi yetu, ingawa jitihada kubwa zinafanywa na Serikali, mashirika ya dini pamoja na asasi mbalimbali.

 “Leo kuna watoto wanaoitwa wa mtaani ama idadi ya wanaolelewa na mzazi mmoja inaongezeka kutokana na kuongezeka kwa talaka na ndoa zisizo na furaha na hali hii huathiri malezi ya watoto, elimu yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.”

Kongamano hilo la maisha bora limelenga katika kupanua uelewa ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa, ikiwamo ukimwi, maadili kwa jamii, uhuru wa dini, ujasiriamali, mazingira, athari za imani za uchawi na namna ya kudumisha amani katika nchi yetu.

KARIBU WATER FRONT GHOROFA YA 8 KILA SIKU KUANZIA SAA 10 JIONI KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni