Kila mtu ana siku yake ambayo niya pekee sana na mpya katika maisha aliyonayo. Hivyo ndivyo ilivyo na kwangu leo hii. Kiukweli, mara nyingi huwa ni siku inayoashiria kuanza kwa mwaka mwingine mpya kwa mhusika tena ni mwaka ambao unaoanzisha mzunguko mwingine uliyo na mikosi ama Neema katika maisha ya mwanadamu. NI SIKU YA KUZALIWA PEKEE yake ndio NINAYOIZUNGUMZIA HAPA. Naaa.. ukitafakari; kwa kadri na namna maisha yalivyo ni zaidi ya idahaniwayo kuwa ni shule kama sio chuo kikuu chochote hapa Duniani.
Tukiachilia mbali ndugu, jamaa, marafiki, majirani! hata ka sio kila mara nina amini huwa unawatolea WAZAZI wako wote shukrani kwa uwepo wao kwako wewe msomaji. Utakubaliana na mimi kuwa umejifunza mengi kutoka kwa maadui na marafiki uliowahi kuwa nao. Kwa kuwa husemwa palipo na msafara wa mamba kenge hakosi nina uhakika kupitia hao na hayo yote kila mmoja amejifunza mengi yaliyo mabaya na hata mazuri yakiambatana.
Unaweza usinitambue mimi kwa sababu ya changamoto ulizozipata lakini kuna mtu mahali fulani huwa unamkumbuka kutokana na mchango wake kwako. Ninashukuru kwa UMOJA uliopo Kwa Baba na Mama yangu. Baba na Mama, Wajomba, Mashangazi, Mabinamu, ndugu wote wa hiari na marafiki na wewe msomaji, kiukweli ninawapenda sana.
KWA UFUPI.
Ilikuwa ni SEPTEMBER 7TH SAA 9:30 ALASIRI SIKU YA IJUMAA ndipo nilipozaliwa katika hospitali kuu iliyopo Wilayani Tarime mkoa wa Mara katika familia ya kiadventista. Awali mama alikuwa ni nesi lakini aliamua kubalisha fani na kuingia katika ualimu wa shule. Hivyo basi Mama yangu ni MWALIMU na Baba yangu ni MCHUNGAJI japo alisha staafu.
Baada ya siku saba, yaani ilipofika Septemba 14 baada ya mimi kuzaliwa nikapewa jina CHACHA na bibi yangu.
Jina hili lina maana tatu kama sio nne.
Maana ya kwanza ya kiasili:
“Iching’ombe chichele.” yaani
kwa tafsri rahisi ni kwamba NG’OMBE ZIMEKUJA. Hii inatokana na ule wakati binti
anapoposwa sasa mahari inapoletwa na kwa kawaida mahari yenyewe huwa ni ngombe
hivyo mtoto akizaliwa huitwa hilo jina.
Lakini kwangu haikuwa hivyo ila ipo katika maana ya pili na kuendelea, soma hapo chini.
Maana ya Pili: Ni wa uzao wa kwanza. Maana ya
tatu: Ni jina la Babu wa tatu wa baba mzazi wa Chacha aitwaye Daniel Mcharia. Maana nyinge CHACHA NI MTU JASIRI.
Ilipofika Desember 22 nilipelekwa kanisani kuombewa, wanasema kwa lugha nyingine kuwekwa WAKFU KWA MUNGU. Ilikuwa ni siku
ya JUMAMSOI tena ya SABATO ya mtaa. Pr Jackson Magai ambaye kwa sasa ni marehemu, ndiye
aliyefanya hiyo huduma ya kuniweka wakfu. Sadaka ya shukrani kwa ajili yangu iliyotolewa na wazazi wangu kwa MUNGU ilikuwa ni shilingi
50. Kwa miaka 1979 kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni kingi sana.
Katika kukua kwangu; jina Yusuph lilitokana na Baba yangu mdogo ambaye kwa wakati fulani alikuwa akija nyumbani hasa nyakati za likizo, niliona alivyokuwa akipenda kucheza na mimi hatimaye nikaamua kulitumia rasmi hili jina ila maana na yeye alikuwa akiitwa hivyo, nilizidi kupata hamasa na kulipenda mara baada ya kuwa nimesikia simulizi mbalimbali kuhusu YUSUFU WA KWENYE BIBLIA.
JINA YUSUFU Linatokana na jina la kilatini lililotokana na jina la kiyunani (LOSEPHOS), lililotokana na jina la Kiebrania (YOSEF) likiwa na maana ya: “ATAZIDISHA au ATAONGEZA”.
Katika agano la kale Biblia takatifu inaeleza Yusufu na Joseph ni mwana wa kumi na moja wa Yakobo (Israel). Kwa sababu ya kupendwa sana na baba yake Yusufu alionewa wivu na ndugu zake, wakamchukia, wakamuuza akapelekwa Misri kisha wakaenda kumweleza baba yao uongo kwamba alikuwa amekufa.
Lakini huko Misri Yusufu aliongezewa neema ya Mungu akapandishwa cheo na kuwa Mshauri mkuu wa Farao. Jina hili pia limetumiwa na watu wengine wawili ndani ya biblia takatifu waliocheza nafasi muhimu sana ya kiroho na kimaandiko ambao ni Yusufu mume wa Bikira Mariam na Yusufu tajiri wa Arimathaya aliyenunua kaburi la kifahari akalitumia kuhifadhi mwili wa Bwana Yesu Kristo baada ya kufa msalabani.
Nililojifunza katika maisha haya ni kwamba KILA MMOJA WETU ANA FUNZO, SHULE NA KILA MTU NI MUHIMU KWA MWENZIE. Hata kama shule hiyo ni kukufunza usichotakiwa kufanya. NINawapenda, ninawathamini na ninawaheshimu sana mno.
NIWE MUWAZI
Maisha ya sasa yasingekuwa yalivyo bila msaada mkubwa wa MUNGU ALIEYEZIUMBA MBINGU NA NCHI NA VYOTE VILIVYOMO.
******************************************
No one can go back and change a bad beggining,
but anyone can start now and create a successful ending.
******************************************