|
Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili,
kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI
Ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Kwa
sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo
na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Ninamaanisha JumaMosi)
Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, kweli halisi jionee mwenyewe ambapo tutatijifunza:
MAWE MATANO (5) YA KUMSHINDA GOLIATH THE GIANT!
Imeandaliwa na Pr. Filbert Joseph Mwanga
Mwanadamu
ni kiumbe kidogo katika ya viumbe walioumbwa na Mungu. Lakini ambaye
dunia imemtengenezea silaha kali za nyuklia, mizinga na mabomu, n.k. ili
kumuua na kumfutilia mbali. Silaha zimewekwa angani – zote hizo sio
kuangusha milima- la bali kumuua mwanadamu.
Ndipo swali linakuja kwangu – je watu hawa akili zao ziko sawa? Mtu ambaye anauwawa na mbu tu wa malaria – ‘anopheles’ kuna
haja ya kumtengenezea mabomu yote hayo? Silaha zimewekwa angani yote
hiyo ni mwanadamu. Silaha hizi zinamsaka mtu ambaye halingani wa karne
kama Goliath? Goliath ni nani? THE GIANT! JITU LA MIRABA MINNE!
Goliath
aliongoza kambi ya wafilisti akiwa kama mwanaume wa shoka – mtu wa vita
tu! Soma 1 SAMWELI 17:1 – 2. Wafilisti walijipanga kwa ajili ya vita.
Mbaya zaidi vikawa ndani ya mipaka ya Yuda. Ikiwa kuna vita vibaya
kuliko vyote ni vile ambavyo vinapiganwa NDANI YA KAMBI YAKO! Kisa cha
Amerika na Iraq – Technical Defensive Matching. Mchezo huu ni mbaya hata
kwa timu za mpira wa miguu. Wanapojihami na kurudi nyuma ndipo
wanapofungwa maana mpira unachezewa ndani ya goli lao na hivyo
wamekaribisha wameshambulizi wenyewe!
Wapagani
hawa wamehamishia vita ndani ya mipaka ya Israeli. Kama kuna vita
vibaya vya kiroho ni vile vinavyopiganiwa ndani ya mwili wako. Zipo
dhambi zinazotendwa ndani ya mwili na nyingine nje ya mwili. 1
CORINTHIANS 6:18, 16 – 17.
Paulo
anataja dhambi hizo ZINAA. Ndani ya mwili. Bali uongo ni nje ya mwili.
Uvunjaji wa kanuni za afya ni NDANI YA MWILI. UBINAFSI ndani ya mwili
tena unakula taratibu lakini kwa hakika. Unataka kuhudumia MIMI kwanza!
Mzee wa kanisa au kiongozi wa kwaya anapokuwa mzinzi kanisa, familia,
watoto au kwaya inapoteza mwelekeo. Maana wamekaribisha adui ndani ya
ngome. Kiongozi yeyote anapokuwa MBINAFSI kama ni serikali au kanisa
anatafuta kufanya huduma zote yeye tu, ataanza kung’ang’ania madaraka
yote, na hata akiona wengine wanafanya vizuri hatopendezwa maana anabaki
kuuona MIMI anaguswa. Hivyo vita vyake vitapiganiwa moyoni! Ataanza
kuonyesha hasira, uadui, kisha unaanza kujihoji kuwa umefanya nini –
unajifikiria kuwa kuna tatizo gani? Hakuna lolote makosa anayokutoa na
kashfa anazokupa na mateto – ni sababu ya PIGANO LINALOENDELEA MOYONI
UBINAFSI!
Maumivu
makali ni yale yanayomuumiza mtu kwa ndani. Unaweza ukamuumiza ndugu
yako kwa kumpiga na fimbo au chombo chochote kikali na akabaki na kovu;
lakini KOVU baya ni lile linalobaki moyoni. Waswahili walisema maneno ni
sumu! Kwanini? Maneno ni vita vinavyokwenda kupiganiwa Moyoni – vita ya
ndani! Ndoa nyingi zina watu
wanaojua kutoa maneno mabaya – na hayo ndiyo yanayoleta talaka na wala
sio ngumi pekee! Bali masimango kwa mumeo au mkeo au watoto! Maneno ni
SUMU!
1
SAMWELI 17:3 Majeshi yote wapo katika milima - Israeli na wafilisti.
Milima wakati wote inawakilisha – IBADA. ENEO LA IBADA! Inategemea aina
ya Mungu unayemuabudu. Israeli ni Mungu wa mbinguni. Wafilisti ni mungu
Dagoni. Mungu atakayeshinda vita ndiye mkuu. Tatizo la Israeli wamepanda
kwa Mungu wa kweli – lakini katikati yao kuna bonde la ELLA! Hilo ndiyo
tatizo kwa Israeli. Wafilisti walizoea mabonde – Shinari, Timna, Gaza,
n.k. unaposoma Biblia bondeni inawakilisha MAPOROMOKO YA KIROHO!
Mfalme
wao ambaye ni Sauli – amekuwa na ibada nyingi. Pamoja na kuwa wapo
milimani –wapo kaika pigano ambalo halina Mungu wa Kweli kati yao. Wote
wakapoteza tumaini lao kwa Mungu – wakaona kushindwa mbele yao.
Fungu
4. Hebu tumuelewe GOLIATH – the Giant! Israeli pamoja na kupanda juu ya
Kilima – hawamuoni Mungu wa Kweli – bali GOLIATH – kushindwa! Kwanini?
Goliath ni mtu mrefu wa futi 9. Kizazi chao ni watu wa ajabu. Mwingine
alikuwa na vidole 24. (2 SM. 21:19-22). Kabila lake ni mrefai – the
Giant. Dirii aliyokuwa amevaa ni kg. 50 – mfuko wa sementi! Kichwa cha
mkuki wake ni kg. 7. Unawezaje kupambana na mtu aliyekuzidi urefu, uzito
na hata umri wewe mtu uliyemfupi tu wa futi 4 au sana sana 6.5? Tena
huna uzoefu wowote?!
Lazima kuna siri kuu. DAUDI mwana wa YESE anajua siri hiyo! Soma 1 SAMWELI 17:45. Kumbe ni JINA LAYESU! MWAMINI YESU NA MANABII WAKE NAWE UTATHIBITIKA! 2 NYAKATI 20:20.
Unaweza
ukaona kila kitu mbele yako kuwa ni kitu cha kutisha – hata ukapoteza
mwelekeo. Huenda ni ugonjwa – the giant! Kukosa ajira – the giant!
Kukosa mchumba – the giant! Kutafuta wahubiri ni dhambi inayokusumbua –
the giant! Dhambi – zaka na sadaka – the giant! GOLIATH! Hivyo unakata
tamaa – unalia moyoni. Maumivu ya kiroho – spiritual anguish! Kila siku
ngambo ya pili ukiamka asubuhi unaona Goliath amesimama maneno makali
kama mkuki moyoni au ubavuni mwako! Hakuna amani kanisani, nyumbani,
kazini na majirani! Badala ya kumuona YESU siku ya Sabato – mlimani kwa
Bwana unamuona Goliath! Hutamani kurudi nyumbani unaona ni bonde kubwa
utakalozama na kutobolewa macho kama Samsoni.
Hata ijapokuwa muhubiri anasimama saa tano – wengine ndiyo Goliath – Usingizini anaonekana lakini kwenye masengenyo na mateto macho
yote pima! Hata ijapokuwa YESU ameinuliwa juu ya mlima wa Golgotha –
bado hatuwezi kumuona Yesu bali Goliath – the giant! Huku akinguruma
kiasi ya kuwa unataka kuacha vita vya kiroho na kuvaa silaha za mwili –
giza yaani kutumia UBINADAMU kulikabili TATIZO! Huenda hali ya uchumi
imekuwa ngumu – sasa watoto hawana ‘school fees’ – naacha kukaza mwendo
naogopa na kuvaa silaha za wizi wa zaka na sadaka ili kutatua tatizo!
Kumbuka
Israeli kila siku asubuhi walipojipanga hawamuoni BWANA bali GOLIATH –
kwao ni utisho tu. Fungu 8 – 11. Tangazo limetolewa kuwa anatakiwa mtu
mmoja tu. Atakayesimama na kupambana na adui mmoja. Katika Israeli mtu
aliyekuwa anamkaribia Goliath kwa urefu – the giant ni SAULI sio JESHI
lote! (Mtu mmoja sio KANISA LOTE).
Kumbuka
Sauli tayari ana mapepo. 1 SAMWELI 16:23. Je mtu aliye na pepo la
ubinafsi, uzinzi, anaweza kuongoza jeshi la Bwana? Hapo ndipo taifa lote
limepoteza mwelekeo. Huwezi kumtegemea mtu aliye gizani akuongoze
katika vita vya ulimwengu. Unaumwa na una mapepo unaenda kwa MGANGA wa
kienyeji? Tegemea anguko. Pia kujiongezea mapepo zaidi.
Daudi
mwana wa Yese alijua namna kulikabili JITU! Fungu 40. Usikabiliane na
jitu bila kuendea KISIMA CHA MAJI YA UZIMA! YALE MAWE MATANO yapo pale
kisimani na wala sio bondeni au tambarare, LA! MAWE MATANO LAINI YAPO
PALE YA USHINDI! Baada ya kupata mawe hayo ndipo umwendee Goliath – the
giant! Ushindi ni wa LAZIMA! Leo nitaanza na JIWE la kwanza aliokota
Daudi. Nalo ni KUAMINI JINA LA YESU! ZABURI 20:7 Tatizo la Israeli
waliacha Jina la Yesu wakitumainia Jina la Sauli. MATENDO 4:11-12.
Hakuna Jina lingine isipokuwa Jina la YESU MNAZERETI! KISA CHA CAMPOREE
KENYA – MTOTO NA KAFARA!
Unaposimamisha Jina la Yesu – hakuna mwanadamu au jeshi litakalosimama. Soma CLEAR WORD inasema, Israeli na Sauli “walipoteza ujasiri wao baada kuona the ‘giant’ – Goliath. Huwezi
ukamuona mwana wa Adamu ukawa muoga na kupoteza matumaini. Mitume
walipomuona YESU aliyeangikwa msalabani na sasa YU HAI walikuwa
‘Courageous’ – walitiwa shime kuhubiri Jina la YESU bila woga.
Daudi
alitumia Jiwe LAINI – NIRA LAINI YA YESU! Tumaini la kushinda tatizo
lolote linapatikana kwa YESU anaposema leteni mizigo yenu yote mpate
kupumzika. Kila jambo gumu kuna ushindi uliofichika kwa Yesu. Siri kuu
ni kumtegemea YESU kwa asilimia 100% sio kutegemea Helmet, Dirii, fumo,
n.k. hizo silaha zote hazikumsaidia Sauli. Tambua hili SHETANI hatishiwi
na muda mrefu wa kuishi kanisani. Ikiwa hiyo ndiyo ‘Defensive Mechanism
ya Kiroho’ nataka nikupe pole maana Shetani ni giant! Daudi alijaribu
vyote hivyo akagundua hawezi kumshinda Goliath na mambo hayo! Alikumbuka
Yule Simba wa Kabila la Yuda!
Uzoefu
wa kukaa kanisani au kusoma Biblia na kujua mafungu mengi – hauwezi
kumtisha Shetani. Bali uzoefu katika kutumia silaha ya Jina la Yesu
katika shida zako – ni ushindi usio na mpinzani! Shetani ANALOOGOPA NI
JINA LA YESU – JIWE MOJA! JIWE KUU LA PEMBENI! MWAMBA ULIO IMARA! WIMBO
192! MWAMBA WENYE IMARA KWAKO NITAJIFICHA! IMARA – MADHUBUTI. FUNGU 45.
KISA CHA MTU ALIYEKUFA KWA AJILI YA NG’OMBE! Msimamishe Yesu Mnazereti kwa Jina hili ni USHINDI!
SOURCE: INGIA HAPA
|
DO NOT GIVE UP. THE BIGINNING IS ALWAYS THE H a r D e s t. "NI HERI KUFA KATIKA FIKRA ZINAZOISHI KULIKO KUISHI KATIKA FIKRA ZILIZOKUFA."
Mtayarishaji
Morning Star Radio
Jumamosi, Januari 26, 2013
Majibu Yafanyayo Kazi - MAWE MATANO
Alhamisi, Januari 24, 2013
YASABABISHAYO MSONGO WA MAWAZO FAMILIANI
Family stressors
Kuzidiwa na majukumu
Mmoja kutoyaelewa majukumu yake
Mgongano
katika kuyatimiza majukumu ya kifamilia (rule conflict)
Mapungufu
katika kuyatekeleza majukumu ya mmoja
Ukosefu wa kupeana zawadi au
vichochezi pale mmoja anapofanya vema, (suprises and motivators)
Mahusiano mabovu
Ukosefu wa fedha
Kutotoshelezeshwa katika tendo la
ndoa
Tabia binafsi ambazo zaweza kuchangia katika kuleta msongo wa mawazo
Mmoja kujisikia au kujithamini zaidi ya mwezake
Kiwango cha juu
cha hasira
Mmoja kuchukulia kazi yake kuwa ya muhimu zaidi ya ile ya
mwenzake
Mapungufu katika mbinu za mahusiano, Mfano; mmoja hana tabia
yakusema asante, au kutoa zawadi au hata kusema neno “nakupenda”
Udhaifu katika afya ya mmoja
Dalili za kukuonyesha kuwa misongo ya mawazo ipo ndani ya familia
Mahusiano nje ya ndoa
Muda mwingi kazini hata kama hakuna
kinachofanywa huko
Malumbano kuzidi
Mmoja kutokuwa tayari kumhudumia
mwenzake katika tendo la ndoa “sexual withdrawal”
Kuanza au kuzidi
kwa matumizi ya vilevi
Hali ya mmoja kupooza na kukosa raha wakati
mwingi
Uadui baina ya wanandoa
Matokeo ya kuzidi kwa dalili hizi
Talaka au kutengana
Mmoja kunyanyasika au wote kunyanyasana
Unyanyasaji wa watoto (child abuse) nk.
Visababishi toka nje ya
familia (extrafamily stressors)
Kazi
Mahangaiko ya maisha
Familia
kubwa (extended family)
Kukosa kazi
Mshahara mdogo kazini
Matatizo
ya shule (hasa kwa wale wanaosoma wakiwa ndani ya ndoa)
Kukosa
elimu (kwa wale ambao hawakubahatika kusoma)
Matokeo ya misongo hii kiafya baina ya wanandoa
Kuongazeka kwa matatizo ya shinikizo la damu
Kuongezeka kwa
matatizo ya misuli (muscle tention)
Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
Kuongezeka kwa kasi ya mfumo mzima wa upumuaji (breathing system)
Hali hii inapozidi kwa wanandoa tunategemea yafuatayo
Magonjwa ya moyo
Shinikizo la damu
Vidonda vya tumbo (ulcers)
Maumivu makali na ya mara kwa mara ya kichwa
Maumivu ya mara kwa mara
ya mgongo
Hypertension
Saratani (cancer)
Hofu kubwa katika baadhi
ya vitu ( allergic reaction)
Msongo wa mawazo juu ya masuala ya uzazi wa mpango
Pangeni ninyi wawili kukutana na kuzungumza na mshauri, hili sio
jambo la mmoja wenu bali wote. Fanyeni chaguzi fasaha ni njia ipi ya
uzazi wa mpango mtaiweza na mtaipenda. Tafuteni taarifa Muhimu za kuhusu
uzazi wa mpango toka kwa wataalamu, marafiki, ndugu, vitabu, na
vujarida husika, msitegemee taaria za uzushi zisizoweza kuaminika.
Yamkini njia nyingine zitakingana na imani au misimamo yako binafsi,
basi pata ushauri toka kwa kiongozi wako wa dini. Katika kuyatimiza haya
yote shirikianeni kwa upendo katika kuelekezana na kukumbushana juu ya
ushauri mlioupata.
Msongo wa mawazo unaosababishwa na mzazi mmoja kuwa mbali na familia
Panga kuitembelea familia yako kila upatapo nafasi zaidi ya kwenda
maeneo mengine. Wasiliana nao kwa simu mara kwa mara, hii inaruhusu muda
wa maongezi na kujuliana hali. Njia nyingine isiyo ya gharama sana ni
kutumiana barua, hapa ninatia msisitizo katika barua na sio kadi. Kadi
kama za siku za kuzaliwa na nyingine hazina uzito mkubwa wa mawasiliano
kama ule uliopo katika barua. Lazima familia yako ijue kuwa unatumia
jitihada zako zote katika kuwasiliana nao hii itawajengea haja moyoni ya
kutaka kukujibu.
Misongo ya mawazo inayoletwa na masuala ya fedha
Stress zinazisababishwa na masuala ya fedha ni mbaya sana, zaweza
kuvunja mahusiano baina ya wanafamilia, zaweza kuleta matatizo kiafya
hasa pale matibabu yanapocheleweshwa mpaka mgonjwa azidiwe sana,
kwasababu ya ukosefu wa fedha. Hali hii huwafanya wanafamilia kuwa na
hisia mbaya, kutojithamini, na kutojipenda, hali ya kujitawala kwao
hushuka maana hamna mwenye uhakika na maisha.
Jinsi ya kukabiliana na misongo hii.
Jifunzeni kuwa na bajeti ya mapato na matumizi ya familia, bajeti hii
itawasaidia kupunguza madeni, ambayo kama yasipolipwa huleta stress
zaidi na maranyingine kushitakiwa kisheria. Bajeti pia itawasaidia ninyi
kutawala fedha zenu zaidi ya fedha zenu kuwatawala ninyi. Namna nzuri
ya kuandaa bajeti ni kupiga picha nyuma, nijinsi gani mlitumia fedha
mwakajana, au mwezi uliopita. Angalia vyanzo vyenu vya mapato, vile
vikubwa na vile vidogovidogo. Wakati wote jitahidi sana matumizi yasije
yakawa ya kasi kubwa kuliko kasi ya kuingiza. Fahamu ni vitu vipi
hutumia fedha zenu zaidi, matumizi haya yawe ya lazima na yakishatimizwa
yote ndio mwaweza kufikiria matumizi mengine ya anasa.
Jumatano, Januari 23, 2013
Namba Zenye Athira ya Kisiasa
Tangu mwaka ule swali la takwimu ya kidini Tanzania limejadiliwa sana
inaonekana ni swali lenye uzito wa kisiasa pamoja na upande wake wa
kitaalamu. Kwa miaka mingi makadirio ya kawaida yalikuwa Watanzania ni theluthi 1
wafuasi wa dini za jadi, theluthi 1 Waislamu na theluthi 1 Wakristo
Lakini ni wazi ya kwamba dadi ya wafuasi wa dini za jadi imeendelea
kupungua. Baadhi ya viongozi na wanaelimu-jamii wanakadiria kwamba
jumuia za Kikristo na Kiislamu zipo sawa tu kwa ukubwa, zote huhesabiwa kiasi cha asilimia 30 hadi 40 kwa idadi ya wakazi, na waliosalia ni waumini wa imani zingine, dini za jadi, na wale wasio na dini kabisa.
Lakini wataalamu wengine wanasema uwiano huo unashikiliwa kisiasa kwa
sababu uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu ni jambo la siasa ya taifa
kwa hiyo makadirio yanaelekea kutaja uwiano sawa kati ya pande hizi
mbili
Jumanne, Januari 22, 2013
BAHARI SAYARI YA MARS
Na Leon Bahati
WANASAYANSI wa anga kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta uwezekano wa maisha katika sayari nyingine, mbali na dunia. Kuna imani kuwa kwenye sayari hizo, huenda zikapatikana raslimali nyingi kwa urahisi kuliko duniani ambako binadamu wameishi mamilioni ya miaka hadi sasa.
Wataalamu hao wa anga wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda sasa na moja ya mambo muhimu waliyoangalia ni upatikanaji wa maji. Popote maji yanapopatikana, wanaamini maisha yanawezekana.Moja ya sayari ambayo wamekuwa wakiichunguza kwa miaka mingi sasa ni Mars, ambayo ni ya nne kutoka kwenye jua. Dunia ni ya tatu.
Sababu kuu za kuichagua sayari hii tofauti na zingine ni kwamba, hali ya hewa inatofautiana kidogo sana na ya dunia. Sayari nyingine kama Mercury na Venus, zipo karibu zaidi na jua na hali ya joto iko juu kiasi kwamba hali ya maisha inaweza kuwa taabu. Mars ambayo wanasayansi wanaipa jina la sayari nyekundu, ipo karibu na dunia, hivyo ni rahisi kufika iwapo wanasayansi watathibitisha iwapo maisha yanawezekana huko.
Wanaiita sayari nyekundu kwa sababu eneo kubwa la uso wake ni wa rangi nyekundu, tofauti na nyingine zilizomo kwenye mfumo wetu wa sayari. Hakuna mwanasayansi ambaye amethubutu kusafiri hadi kwenye sayari hiyo kutokana na ugumu wa kupata vyombo vya kuaminika, vinavyoweza kusafirisha watu kutoka duniani hadi Mars na kurudi salama.
Hata hivyo, hilo siyo tatizo kwa sababu wakibaini mazingira mazuri, utengenezaji wa vyombo hivyo hauwezi kuwapa taabu. Kazi ya uchunguzi imekuwa ikifanywa kwa vyombo maalumu ambavyo havina watu lakini, vina uwezo wa kuleta mawasiliano duniani.
Pia wanatumia viona mbali katika mchakato huo kuchunguza hali ilivyo kwenye sayari hii, ambayo kumekuwapo na hisia kwamba huenda waliwahi kuishi viumbe hai mamilioni ya miaka iliyopita lakini baadae mazingira yakabadilika na kuwa mabaya.
Uchunguzi unaonyesha kuwa, sayari hii ina mabonde mengi ambayo yanakila dalili kuwa awali yalikuwa yanatiririsha maji kama ilivyo mito hapa duniani. Kwa muda mrefu, wanasayansi wamekuwa wakiichukulia sayari hiyo kuwa na mazingira ya jangwa yanayotokana na ukame wa muda mrefu.
WAGUNDUA MAJI
Mwezi januari 2009 wanasayansi hao walikuja na maelezo kwamba sayari hiyo
ina kiwango kikubwa cha maji na mengi yapo mita chache kutoka uso wake. Mmoja wa wanasayansi waliochunguza sayari hiyo ni Profesa Jay Melosh wa Chuo Kikuu cha Purdue, nchini Marekani.
Yeye alisema uchunguzi huo umewapa imani kwamba siyo tu kwamba Mars ina maji bali kuna viumbe wadogo, mfano wa jamii ya bacteria ambao wanaendelea kuishi humo hadi leo hii. Ni uchunguzi ambao waliamini una matumaini tofauti na taarifa za uchunguzi ulizopita na kizuri zaidi pia ni kubaini moja ya miezi yake miwili, maji yapo kwa wingi zaidi.
Miezi inayoizunguka sayari ya Mars ni Demos na Phobos. Phobos ndio mwezi uliogundulika kuwa na kiwango kikubwa cha maji na ndio ulio karibu zaidi na sayari hiyo. Kwa sababu hiyo, wanaamini kwamba maisha yakianza kwenye sayari ya Mars, kuna uwezekano pia wengine wakahamia kwenye mwezi huo wa Phobos.
Taarifa za uwepo wa maji kwenye sayari hii zilitolewa kwenye mkutano wa wanasayansi wanaochunguza anga za mbali, uliofanyika Austria Juni mwaka 2009. Moja ya dalili za uwepo wa maji ni vimondo ambavyo vimekuwa vikianguka kwa wingi kwenye uso wa sayari hiyo. Mtaalamu wa Uhandisi na Mambo ya Anga, Profesa Kathleen Howell alisema picha walizopiga maeneo ambayo vimondo vimegonga uso wa Mars, zilionesha dalili kama za mtu aliyetupa jiwe kwenye eneo lenye tope.
“Sehemu kimondo kilipoigonga sayari ya Mars, aina ya kitu kama tope kiliruka na kusambaa pembeni,” anasema Profesa Howell. Hali hiyo wakaitafsiri kuwa maji yaliyokaribu na uso wa sayari hiyo yaliruka pamoja na udongo wakati, kimondo kilipozama ndani na kusambaa pembeni.
HALI IKOJE?
Utafiti huo unaashiria kwamba, sayari hiyo ina bahari kubwa iliyoenea chini kwa chini kwenye miamba mita chache kuingia ndani. Milipuko ya volkano ya miaka mingi iliyopita ni kiashirio kingine kwamba, sayari hii ina maji. Uchunguzi unaonyesha kwamba mlipuko huo uliandamana na maji.
Ripoti ya utafiti huo ambao ulichapishwa pia na jarida la Geology, unaonesha kuwa kiwango cha maji kilichopo Mars kinakadiriwa kuwa sawa au kimezidi kile kilichopo hapa Duniani. “Kimsingi, kiwango cha maji tunayoyazungumzia kinalingana ama ni zaidi ya kile kilichopo kwenye uso wa dunia,” Alisema Kiongozi wa Jopo la Wanasayansi hao, Profesa Francis McCubbin, ambaye pia ni Mtaalamu wa Anga Chuo Kikuu cha Mexico.
“Si jambo la kushangaza kwamba, kwenye sayari hii waliwahi kuishi viumbe hai miaka iliyopita,” alisema Profesa Howell na kuongeza: “Tatizo tutakalokabiliana nalo ni iwapo tayari muda umepita sana kiasi cha kutotambua vyema hali hiyo. “Lakini, hata kama hautapatikana uthibitisho wa kisayansi wa viumbe kuwahi kuishi miaka iliyopita, jambo muhimu ni uwezekano wa kiumbe kuweza kuishi kwa sasa.”
HATARI KWENYE MARS!
Hatari iliyopo ni kwamba, ni moja ya sayari ambayo imekuwa ikigongwa mara kwa mara na vimondo vinavyoanguka. Ni vimondo vichache sana ambavyo viliwahi kutua kwenye uso wa dunia. Vinapoanguka kuelekea uso wa dunia hukabiliwa na safari ndefu na kutokana na mwendo mkali wa mwanguko, hujikuta vinapata msuguano mkali na hewa, ambao husababisha joto kali linaloimomonyoa udongo hadi inakwisha.
Sayari hii ambayo ipo karibu na ukanda wa vimondo, uso wake una makovu mengi yanayoashiria athari za vimondo vyenye ukubwa tofauti vilivyotua. Vimondo hivi ndivyo vimeweka wazi dalili za kuwapo kwa maji kwenye sayari hii ambayo uso wake unaonekana kama vile jangwa, kwa kutokuwa na miti na ishara ya ukame wa muda mrefu.
DALILI ZAONYESHA KUNA VIUMBE HAI
JE, NI HATUA NZURI YA UWEZEKANO WA BINADAMU KWENDA KUISHI?
Lamu Kisiwa Ambacho Kimedumu Bila Kubadilika
UPEPO mwanana wenye chumvi
ulipiga matanga ya turubai, na kusukuma mbele meli ndogo ya mbao. Juu
kwenye sitaha, akishikilia mlingoti, mlinzi alitazama hadi upeo wa macho
ili aone nchi kavu, akikaza macho yake kutazama tu Bahari ya Hindi.
Ilikuwa karne ya 15 W.K., na mabaharia hawa walikuwa wanatafuta kisiwa
cha Lamu.
Dhahabu, pembe za tembo,
vikolezo, na watumwa—Afrika ilikuwa na vyote. Wakivutiwa na hazina za
Afrika na hamu ya kuvumbua, wanaume jasiri walisafiri kwa mashua hadi
kwenye pwani ya Afrika Mashariki kutoka nchi za mbali. Mabaharia
walivumilia bahari zilizochafuka na pepo za ghafula wakitafuta hazina.
Walifunga safari ndefu, wakiwa wamesongamana ndani ya meli za mbao.
Mabaharia hao pamoja na meli zao
dhaifu walipata bandari yenye kina iliyokingwa na mwamba-tumbawe
walipofika juu katikati ya pwani ya Afrika Mashariki, palipo na kikundi
kidogo cha visiwa, jamii-visiwa ya Lamu. Walipofika hapa mabaharia hao
waliweza kupakia upya merikebu zao maji safi na chakula.
Kufikia karne ya 15, kisiwa cha
Lamu kilikuwa kituo cha kibiashara chenye mafanikio. Mabaharia Wareno
waliofika katika karne ya 16 walikuta wafanya-biashara matajiri
waliovalia vilemba vya hariri na kanzu kubwa-kubwa. Wanawake waliokuwa
wakitembea-tembea kwenye barabara nyembamba walijiremba kwa bangili za
dhahabu mikononi na kwenye vifundo na kujipaka marashi. Kandokando ya
maegesho, meli za matanga zikiwa matanga yake ya pembe tatu yamekunjwa
zilielea majini, huku zimejazwa pomoni bidhaa za kupelekwa nchi za
kigeni. Watumwa waliofungwa pamoja na kuwekwa katika vikundi, walingoja
kuingizwa kwenye majahazi.
Wavumbuzi wa mapema wa Ulaya
walishangaa kupata usafi wa kiafya wa hali ya juu na usanifu-majengo
katika Lamu. Nyumba za mjini zinazokabili bahari zilijengwa kwa matufali
ya matumbawe yaliyochongwa kwa mkono katika machimbo ya mawe ya karibu,
na milango mizito ya mbao, iliyochongwa kwa uangalifu mwingi, ililinda
njia zao za mwingilio. Nyumba zilipangwa vizuri katika safu
zilizokusudiwa kupitisha upepo mwanana wa baharini kwenye barabara
nyembamba na kutuliza watu kutokana na joto kali.
Nyumba za watu waliokuwa matajiri
zaidi zilikuwa kubwa na zenye nafasi ya kutosha. Bafu zilikuwa na maji
safi ya mfereji yaliyopitishwa kwa mifumo ya kale ya mabomba. Vilevile
mfumo wa kuondoa takataka ulikuwa wenye kuvutia na wa hali ya juu kuliko
wa nchi nyingi za Ulaya wakati huo. Mifereji mikubwa iliyochongwa
kutoka kwa mawe, iliteremka kuelekea baharini na kubeba maji machafu
hadi kwenye mashimo yaliyochimbwa mchangani yaliyokuwa mbali na vyanzo
vya maji safi. Matangi ya maji yaliyotengenezwa kwa mawe yaliyokuwa na
maji safi ya kutumiwa nyumbani yalikuwa na samaki wadogo waliokula mabuu
ya mbu, na hivyo kupunguza idadi ya wadudu hao wanaouma.
Kufikia karne ya 19, majahazi ya
baharini yalipata pembe za tembo, mafuta, mbegu, ngozi za wanyama, kaka
la kobe, meno ya kiboko, na watumwa wengi kutoka Lamu. Hata hivyo, baada
ya muda, ufanisi wa Lamu ulianza kudidimia. Tauni, kushambuliwa na
makabila jirani yenye uhasama, na vikwazo kwa biashara ya utumwa
vilifanya Lamu ididimie kibiashara.
Kuchunguza Wakati Uliopita
Kusafiri kwa mashua hadi kwenye bandari ya Lamu leo ni sawa na kuchunguza wakati uliopita.
Upepo huvuma bila kukoma kutoka Bahari ya Hindi iliyo kubwa ya rangi ya
samawati. Mawimbi mepesi ya feruzi huosha fuko zenye mchanga mweupe.
Majahazi ya mbao ya muundo wa kale hunyiririka kandokando ya pwani, huku
matanga yake yenye umbo la pembetatu na ya rangi nyeupe yakifanana na
vipepeo wanaopuruka. Yakiwa yamepakiwa samaki, matunda, nazi, ng’ombe,
kuku, na abiria, yaelekea kwenye bandari ya Lamu.
Gatini, michikichi inayovuma
kwenye upepo mwanana wenye joto hutokeza kivuli kidogo kwa wanaume
wanaopakua shehena kutoka kwenye meli za mbao. Soko limejaa pilikapilika
za watu wenye kelele wanaofanya biashara ya kubadilishana bidhaa.
Wafanya-biashara hao hawatafuti dhahabu, pembe za tembo, au watumwa,
bali ndizi, nazi, samaki, na vikapu.
Chini ya kivuli cha mwembe
mkubwa, wanaume wanasokota kamba ndefu za makonge na kushona matanga ya
vitambaa yanayoendesha majahazi yao ya mbao. Barabara ni nyembamba na
zimejaa watu wanaoelekea kila upande. Wafanya-biashara waliovalia kanzu
ndefu kubwa-kubwa waita watu kutoka kwenye maduka yao yasiyo na
mpangilio, wakiashiria wateja waje na kujionea bidhaa zao. Punda,
anayejikaza kuvuta mkokoteni wa mbao uliojaa magunia mazito ya nafaka,
apita katikati ya watu wengi. Wakazi wa Lamu waelekea kutoka upande
mmoja wa kisiwa hadi mwingine kwa miguu, kwa kuwa hakuna magari ya
kusafiria kisiwani. Njia pekee ya kufika kisiwani ni kwa kutumia mashua.
Jua lifikiapo upeo katikati ya
mchana, wakati huonekana kuwa umesimama. Katika joto kali, ni watu
wachache ambao hutembea, na hata punda husimama bila kusonga wakiwa wamefunga macho yao kabisa ili kujituliza na joto hilo.
Jua lianzapo kushuka na halijoto
kupungua, kisiwa hicho chenye utulivu hujaa utendaji. Wafanya-biashara
hufungua wazi milango yao mizito iliyochongwa kwa mbao ili kuanza
biashara, na taa zao zitaendelea kuwaka hadi usiku wa manane. Wanawake
huosha watoto wao na kuwasugua kwa mafuta ya nazi mpaka ngozi zao
zinaanza kung’aa. Wanawake huanza kutayarisha chakula wakiwa wamekalia
mikeka iliyofumwa kwa makuti ya nazi. Hapa wanawake bado hupika kwa
kutumia mafiga, wakitayarisha vyakula vyenye ladha tamu vya samaki
waliokolezwa vikolezo vyenye kunukia vizuri na wali uliopikwa kwa tui.
Watu ni wenye urafiki, wakarimu, na wapole.
Ijapokuwa Lamu haina fahari kama
zamani, utamaduni wa Kiafrika wa zamani uliokuwako kabla ya karne ya 20
ungali unasitawi hapa. Chini ya jua la kitropiki, maisha yanaendelea
kama yalivyokuwa karne nyingi zilizopita. Ukiwa hapa unaweza kuona mambo
ya kale na ya wakati wa sasa pia. Kwa kweli, Lamu imeokoka enzi
iliyopita kwa njia ya kipekee, ni kisiwa ambacho kimedumu bila
kubadilika.
Ziara Yetu LAMU
Hivi karibuni, tulizuru Lamu
tukiwa kikundi, lakini hatukuwa tumeenda kununua au kuuza vitu. Tulienda
kuwatembelea akina ndugu na dada zetu Wakristo, Mashahidi wa Yehova
wenzetu. Ndege yetu ndogo ilisafiri kuelekea kaskazini juu ya pwani ya
Kenya yenye mawemawe. Chini kabisa, kulikuwa na mawimbi shwari kwenye
pwani iliyo na misitu mingi ya kitropiki yenye ukingo wa mchanga mweupe.
Kisha, kwa ghafula, tuliona jamii-visiwa ya Lamu ikimetameta kama vito
kwenye bahari ya feruzi. Kama tai mkubwa wa Afrika, tulizunguka visiwa
hivyo kisha tukatua kwenye barabara ya ndege katika bara. Tulishuka,
tukatembea kwenye ukingo wa maji, na kupanda jahazi la mbao ili
kutusafirisha hadi Lamu.
Ilikuwa siku nzuri yenye jua,
na upepo wa bahari ulikuwa na joto na uliburudisha. Tulipokaribia kisiwa
hicho, tuliona kwamba gati ilikuwa imejaa watu furifuri. Wanaume wenye
nguvu waliinua mizigo mizito kutoka kwenye mashua, na wanawake walibeba
mizigo yao kwa kuisawazisha barabara vichwani. Tukiwa tumebeba mizigo
yetu, tulipenya katikati ya umati wa watu na kusimama chini ya kivuli
cha mchikichi. Baada ya dakika chache, ndugu zetu Wakristo walituona, na
tulikaribishwa kwa uchangamfu kwenye makao yao yaliyo kisiwani.
Tuliamka vyema asubuhi kabla
ya jua kuchomoza ili kukutana na akina ndugu na dada ufuoni. Safari ya
kuhudhuria mikutano ya kutaniko ilikuwa ndefu na ingechukua muda wa saa
kadhaa. Tulikuwa tumejitayarishia maji ya kunywa, kofia pana, na viatu
vinavyofaa kwa safari. Kulipoelekea kupambazuka, tulifunga safari hadi
bara, ambapo mikutano ilifanyiwa.
Akina ndugu walichukua fursa ya
kuhubiria watu waliokuwa mashuani, na hadi tulipofika, tulifurahia
mazungumzo fulani ya Biblia na kuangusha magazeti kadhaa. Barabara
isiyokuwa na watu ilikuwa na joto na vumbi. Tulipokuwa tunatembea
kichakani, tulishauriwa kuwa macho kwa sababu ya wanyama wa mwituni,
kutia ndani tembo waliovuka barabara pindi kwa pindi. Akina ndugu
walikuwa na furaha na uchangamfu huku tukitembea polepole mahali
tulipokuwa tunaenda.
Punde si punde, tuliwasili
kwenye kijiji kidogo ambapo tulikutana na wengine wa kutaniko waliokuwa
wametembea kutoka mbali. Kwa sababu ya umbali, mikutano minne ya
kutaniko ingefanywa siku hii moja.
Mikutano ilifanywa katika
shule ndogo iliyojengwa kwa mawe yasiyo laini, bila milango au madirisha
yaliyokamilishwa kwa ustadi. Ndani ya darasa moja, 15 kati yetu
tuliketi kwenye benchi nyembamba na kufurahia programu nzuri
inayotegemea Biblia, iliyokuwa yenye kutia moyo na kufundisha. Hakuna
aliyebabaishwa na joto kali lililokuwa likitoka kwenye paa ya mabati juu
ya vichwa vyetu. Wote walifurahi kuwa pamoja. Baada ya saa nne za
mikutano, tuliagana kisha kila mtu akaenda zake. Kufikia wakati
tuliporudi Lamu, jua lenye rangi ya kidhahabu lilikuwa likitua kwenye
upeo wa macho.
Jioni hiyo, kwenye baridi ya
usiku, tulifurahia mlo sahili pamoja na familia za Mashahidi wanaoishi
Lamu. Katika siku zilizofuata tulitembea pamoja nao katikati ya barabara
nyembamba zenye kujipinda, tukihubiri na kutafuta watu walio na njaa ya
kweli ya Biblia. Tulitiwa moyo na bidii na ujasiri wa ndugu na dada hao
wachache.
Hatimaye siku ilifika ambapo
tulihitaji kuondoka. Akina ndugu walitupeleka ufuoni, na tukaagana kwa
huzuni. Walituambia kwamba walitiwa moyo na ziara yetu. Tulijiuliza
ikiwa walijua jinsi walivyokuwa wametutia moyo! Tuliporudi bara, punde
si punde tulipanda ndege yetu ndogo. Tulipopaa juu kabisa angani,
tulitazama chini na kuona kisiwa maridadi cha Lamu. Tulifikiri juu ya
imani yenye nguvu ya akina ndugu wanaoishi huko, umbali wanaosafiri ili
kuhudhuria mikutano, na bidii na upendo walio nao kwa ajili ya kweli.
Zamani za kale unabii ulirekodiwa katika Zaburi 97:1: “BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie, visiwa vingi na vifurahi.”
(Italiki ni zetu.) Kwa kweli, hata kwenye kisiwa cha mbali cha Lamu,
watu wanapewa fursa ya kushangilia katika tumaini kubwa zaidi la
paradiso ya wakati ujao chini ya Ufalme wa Mungu.—Imechangwa.
SOURCE: CLICK HAPA
Jumanne, Januari 01, 2013
Asili na hatma ya mwisho wa ulimwengu
Ingawa mfano wa Mlipuko Mkubwa ulipambana na mashaka mengi
ulipozinduliwa kwa mara ya kwanza, shaka iliyochangiwa na uhusiano na
dhana ya dini ya uumbaji, imekuja kuungwa mkono na uchunguzi kadhaa wa kujitegemea. Hata hivyo, fizikia ya sasa inaweza kuelezea tu ulimwengu wa mapema kutoka sekunde 10_"43
baada yaMlipuko Mkubwa (ambapo muda sufuri unawiana na kipimo joto
kinafikia idadi isiyopimika), nadharia fulani ya mvuto wa kikwontamu
huenda ikahitajika kurudi nyakati zazaidi.
Hata hivyo wanafizikia wengi
wamedadisi kuhusu nini kinachoweza kuwa kimetangulia kikomo hiki, na
jinsi ulimwengu ulivyoanza.
Baadhi ya wanafizikia hudhani kuwa Mlipuko Mkubwa ulitokea kiajali, na
wakati kanuni ya kianthropiki inapozingatiwa, mara nyingi hutafsiriwa
kama kuashiria kuwepo kwa ulimwengu maridhawa.
Hata hivyo, haijalishi jinsi ulimwengu ulikuja kuwepo, hatma ya
binadamu katika ulimwengu huu ni maangamizi kwani - hata kama ubinadamu
utaishi muda huo wote - maisha ya kibaiolojia hatimaye yatashindwa
kujiendeleza, iwe kupitia Kuthelujika Kukubwa, Kuraruka Kukubwa au
Kupasuka Kukubw]. Ni bayana kuwa njia pekee ya kuishi milele itakuwa
kuuongoza mtiririko wa nishati kwenye Kiasi cha Kikosimki na
kuibadilisha hatma ya ulimwengu.
Jumapili, Desemba 23, 2012
ASILI NA HALI YA MAISHA YA KIBAIOLOJIA
| Photo Credit By: http://www.smithsonianmag.com |
Kufanya kazi kwa abayojenesisi hakueleweki kwa ufasaha: nadharia mashuhuri ni pamoja na nadharia ya dunia ya RNA (vitoaji aina sawa katika makao ya RNA) na nadhari ya dunia ya chuma-sulfuri (umetaboli bila Jenitiki). Nadharia ya mabadiliko ya viumbe haijaribu kuelezea asili ya maisha bali utaratibu ambao viumbe tofauti vimepitia katika kipindi chote cha historia kupitia mabadiliko ya ghafla ya kijenitiki na uteuzi wa kiasili.
Wakati wa mwisho wa karne ya 20, kwa kuzingatia ufahamu kutoka mtazamo wa mbadiliko wa viumbe unaotegemea jeni haswa, wanabaiolojia George C. Williams, Richard Dawkins, David Haig, miongoni mwa wengine, wanahitimisha kwamba ikiwa kuna kazi msingi ya maisha, ni kujinakilisha kwa DNA na kuendelea kuwa hai kwa jeni za mtu.
Hata hivyo, ingawa wanasayansi wameyachunguza maisha vilivyo Duniani, kuyafafanua maisha kibayana bado ni changamoto. Kimwili, mtu anaweza kusema kwamba maisha "hula entirofi hasi" ambayo inahusu utaratibu ambao waliohai wanapunguza entirofi yao ya kindani kwa gharama ya aina fulani ya nishati inayochukuliwa ndani kutoka mazingira.
Wanabiolojia kiujumla wanakubaliana kwamba viumbe mbalimbali ni mifumo inayojipanga yenyewe inayosimamia mazingira ya ndani ili kudumisha hali hii ya mpango, shughuli za kimetaboliki hutumika kutoa nishati, na uzazi unaruhusu maisha kuendelea kwa vizazi vingi. Kawaida, maumbile huwa sikivu kwa uchochezi na habari za kijenitiki huelekea kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi ili kuruhusu marekebisho kupitia mabadiliko ya kimwili, hizi sifa huongeza nafasi ya kuishi ya kiumbe binafsi na wazao wake kwa mtiririko huo.
Viwakala visivyokuwa vya seli vinavyozaana, hasa virusi, kwa ujumla si havitazamwi kama viumbe kwa sababu haviwezi kuzaana kwa "kujitegemea" au kuendeza shughuli za kimetaboliki. Pambano hili ni tatizo, ingawa, baadhi ya vimelea na visimbayonti vya ndani ya mwili pia vinaweza kuishi maisha ya kujitegemea. Astrobaiolojia inajihusisha na masomo ya uwezekano wa kuwa na aina tofauti ya viumbe vyenye uhai katika ulimwengu mwingine, kama vile miundo ya kujinakilisha kutoka vifaa vingine visivyo DNA.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)










